Quantcast
Channel: MTAA KWA MTAA BLOG
Viewing all 40001 articles
Browse latest View live

WAZIRI NAPE NNAUYE AWATAKA WATANZANIA KUENDELEA KUMUOMBEA RAIS DK JOHN POMBE MAGUFULI, KAZI YA KUTUMBUA MAJIPU NI NGUMU NA INA VIKWAZO VINGI

$
0
0
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Ndugu Nape Nnauye aliyekuwa mgeni rasmi akimuwakilisha Makamu wa Rais Mh. Mama Samia Suluhu Hassan akizindua rasmi albam mbili za kwaya ya Wakorintho wa Pili kwenye tamasha la Krismas lililofanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee leo, ambapo mwimbaji wa muziki wa injili kutoka nchini Afrika ya Kusini Rebecca Malope amefanya onesho kubwa lililovuta hisia za mashabiki wengi waliohudhuria katika tamasha hili akishirikiana na waimbaji mbalimbali wa hapa nyu mbani na nchi jirani ya Kenya.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Nape Nnauye amewaomba watanzania kuzidi kumuombea Rais Dk . John Pombe Magufuli kwa kazi ya kutumbua majipu ambayo amekwishaianza kwani kazi hiyo ni ngumu na ina vikwazo vingi, lakini pia amewataka watanzania na waumini wa madhehebu mbalimbali kuwaombea wasaidizi wake ili waweze kuwa bega kwa bega na Mh. Rais Dk. John Pombe Magufuli ili kutekeleza kazi hii kwa ufanisi na kisha watanzania wafaidi matunda na rasilimali zao wenyewe.

Waimbaji kutoka Kenya walikuwa ni Faustine Munishi na Sara K na Solomon Mukubwa kutoka jiji la Nairobi huku waimbaji wa hapa nyumbani wakiwa ni Rose Muhandom Upendo Nkone, Christine Shusho, Edson Mwasabwite, Joshua Mlelwa na wengine wengi, Tamasha hilo pia lilikuwa na lengo la kumshukuru mungu kwa nchi yetu ya Tanzania kufanya uchaguzi kwa amani, Kulia ni Akex Msama Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion ambayo ndiyo imeandaa tamasha hilo.(PICHA NA JOHN BUKUKU- FULLSHANGWEBLOG-DAR ES SALAAM)
Akex Msama Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion ambayo ndiyo imeandaa tamasha hilo. akimkaribisha Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Ndugu Nape Nnauye ili kuzungumza na wananchi katika tamasha hilo kushoto ni Mbunge Martha Mlata na MC Mwakipesile mshereheshaji wa Tamasha hilo.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Ndugu Nape Nnauye akiwahutubia wananchi na mashabiki waliohudhuria katika tamasha hilo katikati ni Akex Msama Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion ambayo ndiyo imeandaa tamasha hilo na kushoto ni MC Mwakipesile.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Ndugu Nape Nnauye akiimba moja ya mapambio na kuitikiwa na mashabiki wa nyimbo za injili waliohudhuria katika tamasha hilo.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Ndugu Nape Nnauye pamoja na maaskofu na viongozi mbalimbali wakishiriki katika sala maalum ya maombi iliyofanyika katika tamasha hilo,
Wamumini na mashabiki mbalimbali wa muziki wa injili wakishiriki katika maombi maalum ya kumshukuru mungu yaliyofanyika kwenye tamasha hilo.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Ndugu Nape Nnauye na mkewe Mrs Rhobi Nape Nnauye wakicheza pamoja na mwimbaji Upendo Nkone kutoka kulia ni Mbunge Martha Mlata na Alex Msama wakishiriki kucheza.
 
Mwimbaji Rebecca Malope akiimba katika tamasha hilo.
Waimbaji wa mwimbaji Rebecca Malope akiimba katika tamasha hilo.
Mwimbaji Rebecca Malope akiimba kwa hisia huku meza kuu pamoja na mashabiki wake wakiwa wamesimama.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Ndugu Nape Nnauye na mkewe Mrs Rhobi Nape Nnauye akicheza na mwimbaji Rebecca Malope wakati wa tamasha hilo. 
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Ndugu Nape Nnauye na mkewe Mrs Rhobi Nape Nnauye akicheza na mwimbaji Rebecca Malope wakati wa tamasha hilo kulia ni mbunge wa viti maalum mkoa wa mbeya Mary Majelwa na kulia ni Mbunge Martha Mlata.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Ndugu Nape Nnauye na mkewe Mrs Rhobi Nape Nnauye pamoja na maaskofu mbalimbali wakiwa wamesimama wakati mwimbaji Rebecca Malope akifanya vitu vyake katika tamasha hilo.
Mwimbaji Christine Shusho na Mbunge Martha Mlata wakiimba pamoja wakati wa Tamasha hilo.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Ndugu Nape Nnauye na mkewe Mrs Rhobi Nape Nnauye,Alex Msama na Mkewe na baadhi ya wabunge kulia ni Martha Mlata na kushoto ni Mary Majelwa wakiwa katika picha ya pamoja.
Mwimbaji Faustine Munishi kutoka nchini Kenya akiiimba katika tamasha hilo.
Wanakwaya wa Wakorintho wa pili wakiimba wimbo wao mara baada ya kuzinduliwa kwa albam zao katika tamasha hilo.
Mwimbaji kutoka nchini Kenya Solomon Mukubwa akiimba na mwimbaji mwenzake kutoka kushoto Sara K. huku mbunge Martha Mlata akishiriki kuimba nao.
Mwimbaji Joshua Mlelwa naye amefanya mambo makubwa jukwaani katika tamasha hilo.

Mwimbaji Rose Muhando pamoja na waimbaji wake wakifanya vuti vyao jukwaani.

Funga Mwaka Concert na Diamond Ndani ya Dar Live.....

$
0
0
IMG_7348Diamond Platnumz akisema na mashabiki wake waliofurika Dar Live usiku wa kuamkia leoIMG_7989Diamond akicheza na mashabiki wake waliofurika Dar Live.
IMG_7359Akicheza na wacheza shoo wake wa kike.IMG_1416Nyomi ya kufa mtu ndani ya Dar Live wakiendelea kumshangilia Diamond.IMG_7371Wacheza shoo wa kike wa Diamond wakifanya yao.IMG_7324Diamond akiwachombeza mashabiki.
IMG_7325Diamond akicheza na wacheza shoo wake wa kiume.IMG_7344Akiongea na mashabiki.IMG_7377
IMG_7379IMG_7383Diamond akifanya yake na wacheza shoo wake.IMG_7390Diamond baada ya kuwakonga nyoyo mashabiki wake waliofurika Dar Live na wao kuridhika aliamua kupozi nao kwa picha hii.IMG_7432Nyomi ya kutisha ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live.IMG_7455
IMG_7973Diamond akizidi kuwapa raha mashabiki wake wa Dar Live.IMG_7927Mashabiki baada ya kupagawa na shoo. IMG_7975...Akiongea na mashabiki wake.IMG_7991Akiwasalimia mashabiki.
(PICHA: MUSA MATEJA, RICHARD BUKOS/GPL)

hapa vipi tena????

Waraghabishi wakoleza kasi ya mabadiliko wilayani Kishapu

$
0
0
Watendaji wa Kituo cha Maendeleo cha Jamii ya Uchunga wilayani Kishapu wakiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi mbele ya jengo la kituo hicho likiwa limekamilika kutokana na michango yao ya fedha na nguvu kazi. 

Na Krantz Mwantepele ,Kishapu 

Mabadiliko katika jamii yoyote kwa kiasi kikubwa huchangiwa na ongezeo la mahitaji ya binadamu katika mambo mbalimbali. Kwamba, kadri dunia inavyopitia mabadiliko, kadiri ile ile changamoto, mahitaji na huduma katika jamii husika huongezeka.

Ili kufikia malengo yanayotokana na misukumo na mageuzi yasiyokwepeka, binadamu amelazimika kubuni mikakati mbalimbali ya maendeleo. Si hivyo tu, mabadiliko haya yamemfungulia binadamu fursa ya uthubutu wa kujaribu mambo mbalimbali, siyo tu kwa faida yake, bali jamii nzima inayomzunguka.

"Sikutegemea kama siku moja katika maisha yangu nitapata wazo ambalo lingebadili na kushawishi watu kuchukua hatua kwa mustakabali wa jamii.” 

Baadhi ya wananchi na wajumbe wa Kituo cha Maendeleo cha Uchunga wakiwa mbele ya kituo kabla hakijaezekwa na mabati.
Hiyo ni kauli ya mraghbishi Revocatus Richard ambaye pia, kitaaluma ni mwalimu katika shule ya msingi Uchunga. Richard alitoa kauli hiyo baada ya kupitia mafunzo ya uraghbishi na mwalimu mwenzake, Restusta Katobesi, ambao baadaye kwa pamoja, walianzisha Kituo cha KIMAJU (Kituo cha Maendeleo cha Jamii ya Uchunga) kwa kushirikiana na uongozi wa kijiji na wananchi. Na hilo ndiyo lilifanya achaguliwe kuwa Mkurugenzi wa kituo hicho. 

Walimu hao walikuwa miongoni mwa waraghbishi 30 walioshiriki mafunzo ya uraghbishi yaliyotolewa mwezi Machi, mwaka 2012 wilayani Kishapu katika mkoa wa Shinyanga. Kutokana na faida na maarifa waliyoyapata kwenye mafunzo hayo, walimu hao waliamua kuunda umoja uliokuwa chachu ya kuanzishwa kituo hicho cha maendeleo.
Mwanazuoni Sarah Earl, aliwahi kusema: "Maendeleo ni watu na mazingira yao. Kwamba, kusingekuwa na maana iwapo barabara, hospitali, shule na miradi mingine ya maendeleo inayojengwa kwa ajili ya watu isingetumika." 

Kwa mantiki hiyo, miradi yote ya maendeleo, ikiwamo Chukua Hatua ni kwa ajili ya ustawi wa maisha ya watu. Kwa kuwa kiini cha maendeleo ni watu. Shabaha kubwa ya mradi huu wa Chukua Hatua ni kuhakikisha wananchi (waraghbishi) wanajielewa na kujitambua katika kutimiza majukumu yao na kupata haki zao zikiwamo huduma bora za kijamii na kuhakikisha wananufaika na rasilimali zao. Pia unawasaidia kuwawajibisha viongozi wao ili watimize majukumu yao ya kuhamasisha maendeleo na kutatua shida za wananchi.

Mraghbishi ni mwananchi anayeleta uhai mpya ndani ya jamii kwa kutambua matatizo na kupendekeza njia sahihi za kuyatatua.Katika kipindi cha miaka mitano ya mradi, zaidi ya waraghbishi 380 wameleta uhai katika jamii zao, hususani kwenye vijiji vya mikoa ya Shinyanga, Simiyu, Geita na Arusha hasa katika wilaya ya Ngorongoro.

Tafsiri ya uhai huu ni pamoja na kuwachukulia hatua viongozi wabadhirifu, watendaji wabovu, kuandaa midahalo, kudai huduma bora za kijamii, kuibua na kufuatilia matatizo mbalimbali katika vijiji vyao kama ambavyo waraghbishaji Richard na Katobesi wamefanya.

Uraghbishi Kijiji cha Uchunga 

Baada ya kupatiwa mafunzo ya uraghbishi, walimu hawa walirudi kijijini kwao wakiwa na jukumu moja la kutambua changamoto zinazoikabili jamii yao na kupendekeza nini kifanyike wakitumia nafasi na uwezo walio nao.

Kikubwa walichoangalia ni mustakabali wa mtoto wa Kijiji cha Uchunga, kwa maana ya nafasi ya mtoto, ikiwamo ya kufahamu huduma anazopata.Katika kufikiria sehemu ya kuanzia na ili kumpa mtoto wa kike nafasi katika jamii, hasa ya kuongoza, walianza na wanafunzi wa shule wanayofundisha, Uchunga.

“Nimepata bahati ya kuwa mwalimu mkuu msaidizi mara kadhaa na nimetumia fursa hiyo kuleta mabadiliko, nikianzia kubadilisha utaratibu wa kuchagua viongozi wa wanafunzi katika shule yetu," alisema Richard na kuongeza:

"Kwanza tulibadilisha wazo la Kaka Mkuu na badala yake tukasema tutakuwa na Kiranja Mkuu, ili kutoa fursa kwa wanafunzi wa kike kushika nafasi za uongozi wa wanafunzi."

Hadi sasa chaguzi mbili za kidemokrasia za kuchagua viongozi wa wanafunzi zimefanyika shuleni Uchunga Julai 2012 na Mei 2013. 

Katika kuhakikisha wanaendeleza mawazo hayo, waraghbishi hao walikuja na wazo la kujenga kituo cha kujisomea. Walianza kuwatembelea wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Kata ya Uchunga wanaoishi katika kijijini hapo. 

Ili kufikia malengo yao, waliomba ushirikiano, siyo tu kwa walengwa ambao ni wanafunzi, bali kutoka kada zingine ndani ya jamii.

Akielezea jinsi walivyoanza, mraghbishi Katobesi alisema:

“Tulikutana na wanafunzi na kuunda umoja wa kikundi wa Wanafunzi wa Sekondari Uchunga (UWASU). Kikundi hiki kiliamsha hamasa kwa wanafunzi waliokukubali kujitolea kufanya kazi.” 

Na baadhi ya wanafunzi hao wametembelea shule nyingine na kuhamasisha wenzao kujitolea kusaidia kazi mbalimbali kama kuchota maji na kuokota mawe kwa ajili ya ujenzi wa jengo la kituo hicho cha kujisomea. 

Ndani ya jamii yoyote kuna mamlaka, hivyo ili malengo yao yatimie kuliwalazimu waraghbishaji hao kupata ruhusa kutoka kwa walimu na aliyekuwa mwenyekiti wa kijiji wakati huo, Mahona Punguja.

“Baada ya kutoka kwenye mafunzo yao, walikuja kuzungumza na mimi kuhusiana na mambo waliyojifunza na jinsi watakavyoleta mabadiliko. Nilikubaliana nao na kuweka utaratibu wa kuwashirikisha wazazi kama wadau muhimu na makundi mengine maalumu,” alisema Punguja.

Makundi maalumu ni pamoja na watumishi wa uma, kwa maana ya walimu na mtendaji wa kijiji na kata, wazee maarufu, viongozi wa dini, vijana na wajumbe wa halmashauri ya serikali ya kijiji. Waraghbishi hawa kwa ushirikiano na uliokuwa uongozi wa serikali ya kijiji waliweza kukutana na makundi hayo ili kuwaelimisha kuhusu wazo la kituo cha kujisomea. Baada ya kila kundi kukutana na waraghbishi, uliitishwa mkutano wa pamoja wa kujadili jambo hilo na kamati ikaundwa ya kusimamia mchakato mzima. Kamati hii ilichaguliwa kwa kila kundi kuwa na mwakilishi wake. 

“Njia ya kwanza ilikuwa ni kukusanya fedha, kisha kuwaomba wananchi kuchangia nguvu zao. Kila mmoja kwa nafasi yake alijitolea. Wengine tulisomba mawe na kuchimba msingi. Wanawake walileta vyakula kwa ajili ya mafundi ambao nao walijitolea pia utaalamu wao bure”, anaelezea Michael Butu, Mwenyekiti wa Kituo cha KIMAJU.

Wanajamii waliohamasika waliombwa kuchangia kila mmoja Shilingi 10,000 za Kitanzania, ingawa baadhi walitoa nusu ya mchango huo. Kila kitongoji kiliombwa kuchangia Shilingi 60,000. Michango hii ilikusanywa baada ya kuundwa kwa nguvu ya pamoja na wenyeviti wa vitongoji. Kati ya vitongoji vitatu, viwili vilikamilisha ahadi zao.

Harakati hizi ziliwezesha wanajamii kujenga kituo hadi ngazi ya linta, kabla ya mlezi wa kituo hicho, Charles Dida kutoa shilingi 355,000 kama mkopo kwa ajili ya kununua mabati na mbao. 

“Nilipoona jengo letu linasuasua, niliamua kujitolea kufanikisha ujenzi. Niliamua kumshirikisha mke wangu, ambaye aliunga mkono uamuzi wangu kwa kujua mafanikio yatakayopatikana ni ya jamii nzima,” alisema Charles Dida.

Katika hili tumejifunza mahusiano yaliyopo baina ya baba na mama katika kufanya maamuzi ya pamoja. Ni tofauti na mfumo dume uliozoeleka katika jamiii ya kisukuma. Na mpaka sasa kituo kimeweza kulipa kiasi cha Shilingi 110,000 na hivyo bado kinadaiwa Shilingi 245,000. 

Ili kuhakikisha kituo kinaendelea kutoa huduma kwa watoto wa Uchunga wajumbe wa kamati tendaji wanafanyakazi kwa kujitolea kwa kuwa wao kuwa sehemu ya jamii ya wananchi wa kijiji cha Uchunga. 

“Nilihamasika baada ya kupendezwa na wazo la kuanzishwa kwa kituo hiki. Na siku nilipoombwa kuwa sehemu ya kuleta mafanikio, nilikubali mara moja na kushiriki mikutano na ratiba nyingine,” alifafanua katibu wa vijana, Bahati Juma.

Moja ya majukumu aliyokabidhiwa ni huhakikisha kituo kinafunguliwa saa mbili asubuhi na kufungwa saa 10 jioni. Kwa wastani, kituo kinahudumia wanafunzi 20 kwa siku. 

Mbali na katibu huyo, watendaji wengine ni pamoja na mkurugenzi, katibu, mhasibu, na kamati tendaji chini ya mwenyekiti na mlezi wa Kituo. Nafasi hizi zote zina wasaidizi isipokuwa ya mkurugenzi na mlezi.

Uongozi huu ulipatikana kidemokrasia kwa kuchaguliwa kwenye mkutano mkuu wa kijiji. Baada ya kupata uongozi walitengeneza katiba na kukisajili kituo chao. Kwa mujibu wa katiba ya kituo hicho, uongozi unachaguliwa kila baada ya miaka mitatu. 

“Waasisi wa kituo ndio waliopendekeza mfumo wa uongozi na baada ya hapo wakauwakilisha kwenye mkutano mkuu wa kijiji. Kwa hiyo walioweza walishiriki. Na kila mtu aliyeona anafaa kuwa sehemu ya uongozi wa kituo hicho alipendekeza jina lake ama la mwenzake. Baada ya majina hayo kupatikana ndipo yalipigiwa kura na kupata viongozi,” anafafanua mwenyekiti wa kituo, Michael Butu. 

Tukiachilia suala la uongozi, kuna utaratibu maalumu wa kuendesha kituo hicho. Kuna vijana wanaohusika na kuhakikissha ofisi inafunguliwa ili kutoa huduma za kujisoma bure, ikiwa ni mkakati wa kuhamasisha watu na kukifahamu kituo.

Huduma za KIMAJU

Taasisi hii ya kijamii kwa kiasi kikubwa imelenga kwenye uzalishaji maarifa kwa kutoa huduma ya maktaba, ambayo wanafunzi wanaoishi kijiji cha Uchunga hutumia kusoma na kufanya kazi za nyumbani baada ya masomo shuleni.

Katika ziara za ufuatiliaji na uwezeshaji, wafanyakazi wa shirika mtendaji la TAMASHA katika mradi huo wa Chukua Hatua, walishauri kituo kupanua wigo wa huduma zake, kama anavyoelezea Afisa Mradi Winston Churchill.

“Tuliwashauri kuwalenga pia vijana walio nje ya shule ili kuwawezesha vijana wote kutumia kituo hicho vizuri kijijini hapo.”

Watu wazima pia wanatumia kituo hicho kujisomea magazeti, ambayo huwa ni ya siku nyingi na hii ndio sababu ya umuhimu wa kutafuta redio ili watu wasikilize taarifa za habari. 

Hali hii imehamasisha wanafunzi wa shule za sekondari na msingi kuja kujisomea, kama anavyoelezea mwanafunzi wa darasa la saba Leticia Isaka kutoka Shule ya Msingi Uchunga,
“Kituo kinanisaidia kutambua mambo mbalimbali, kwa mfano kupitia mafunzo ya hapa, napata malezi bora ya kuniandaa niwe mwalimu au daktari. Lakini si hivyo tu, wakati wa mapumziko ya saa sita huwa tunakuja kujisomea hapa baada ya kupatiwa mazoezi na walimu shuleni,” 

Pamoja na sababu nyingine, uwepo wa kituo hiki umechangia kuongezeka kwa kiwango cha ufaulu katika shule ya sekondari ya kata ya Uchunga, ambapo mwaka 2013 jumla ya wanafunzi .... tu ndio waliofaulu katika ngazi ya ... , wakati mwaka uliofuata waliongezeka na kufikia kiasi cha ...

"Mbali na mafanikio haya, kituo kina changamoto kadhaa ikiwamo ukosefu wa meza, viti na makabati ya kuhifadhia vitabu," anasema mkurugenzi wa kituo, Richard na kuongeza:

“Haya mabenchi na meza tumeazima kanisani na tukimaliza tunarudisha sehemu husika. Hatuna vitabu vya mitaala kwa ajili ya wanafunzi wetu, ingawa eneo la kujisomea lipo vizuri, nishati ya umeme nayo ni shida.” 

Kimsingi, wanajamii wa Uchunga kwa kushirikiana na waraghbishi na uongozi kwa kijiji wamefanikiwa kufikia malengo.

Asha Salum ‘Kidoa’ ashinda Shindano la Ijumaa Sexiest Girl 2015

$
0
0
IMG_1255 
Video Queen anayefanya pia filamu, Asha Salum ‘Kidoa’ akiwa na tuzo yake ya Ijumaa Sexiest Girl 2015 baada ya kuwafunika Elizabeth Michael ‘Lulu’ na Vanessa Mdee ‘Vee ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala- Zakhem jijini Dar.

Fainali ya lile Shindano la Ijumaa Sexiest Girl 2015 ilifanyika jana ambapo Video Queen anayefanya pia filamu, Asha Salum ‘Kidoa’ aliibuka kidedea. Kidoa alitangazwa mshindi kufuatia kupigiwa kura nyingi na wasomaji wa Gazeti la Ijumaa hivyo kuwafunika wenzake, Elizabeth Michael ‘Lulu’ na Vanessa Mdee ‘Vee Money’. 
 Akizungumza na Risasi, mratibu wa shindano hilo lililodhaminiwa na kampuni ya uandaaji na usambazaji wa filamu ya Hamadombe Distributor, Amran Kaima alisema kuwa, ushindani ulikuwa mkubwa kwani wasanii wote walioshiriki walikuwa wakali ile mbaya. 
 “Kidoa amefanikiwa kuibuka mshindi baada ya kupigiwa kura nyingi. Atapokea tuzo, cheti pia atapewa ofa ya kutengeneza nywele kwenye saluni ya Bulldozer iliyopo Kigamboni jijini Dar kwa miezi sita pamoja na kufanyiwa shopping ya nguvu,” alisema Amran.
IMG_1250 Kidoa (katikati) akiwasalimia mashabiki baada ya kutangazwa mshindi wa Ijumaa Sexiest Girl 2015.
IMG_1252
...Akilia kwa furaha.IMG_7945Kidoa akikabidhiwa tuzo na Mkurugenzi wa Hamadombe Distributor,Fatuma Makame.IMG_1232rt
...Akibusu tuzo. IMG_1260Akiwa katika picha ya pamoja na mratibu wa shindano hilo lililodhaminiwa na kampuni ya uandaaji na usambazaji wa filamu ya Hamadombe Distributor, Amran Kaima (kulia).
IMG_1266
...Akiwa na tuzo na cheti baada ya kukabidhiwa.
IMG_1232
Amrani Kaima akiongea jambo.
IMG_1311Mshindi wa Ijumaa Sexiest Girl 2015, Kidoa akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Gazeti hilo.


(PICHA NA RICHARD BUKOS NA MUSA MATEJA/GPL)

TOYOTA AVENSIS FOR SALE

$
0
0
TOYOTA AVENSIS 1.9 cc DEISEL ENGINE MODEL 2005 MANUAL THE CAR IS IN DAR ES SALAAM JUST IMPORT FROM U.K LONDON 
PRICE T.SH. 7.5 MILION

CONTACT.
+255 718 030 320
+255774 659 895 

CHEKA KI WIKIENDI NA MDAU ALIEAMUA KUFANYA ZIARA ZA KUSHTUKIZA......

$
0
0
Mimi ni msomaji mzuri wa magazeti, na msikilizaji mzuri wa redio, huwa naangalia luninga mara chache sana kama nikibahatika kupita mahala kuna luninga. Sasa wiki hii nimesikia mengi kuhusu hizi ziara za kushtukiza za viongozi wetu, nikaona hili ni jambo zuri tena linafaa kuigwa na sisi wananchi wapenda maendeleo. Nikaona nijipange na mimi nifanye ziara kadhaa za kushtukiza katika sehemu mbalimbali zinazonihusu.

Nikaona nianze na ziara ya kushtukiza pale shuleni kwa huyu mwanangu, maana kila siku anakunywa chai na kuondoka na daftari zake na mie sijawahi kwenda shuleni kwao toka nilipomuandikisha shule mwezi Januari. Nilifika shuleni na kumuona mwalimu mkuu, ambae alianza kutetemeka nilipomuambia kuwa nimekuja pale kwa ziara ya kustukiza, sijui alidhani mi ni mmoja wa Mawaziri wapya, maana nilimuona jasho linamtiririka ghafla. Akanikaribisha ofisi yake iliyokuwa na vitabu kila kona, na kuita waalimu wote na kunitambulisha kuwa ni kiongozi nimekuja kwenye ziara ya kustukiza.

Nilipojitambulisha kuwa ni mzazi, waalimu wote nikawaona waanza kupumua kwa raha. Nikawaambia kuwa mimi nina mwanafunzi pale na nilikuja ziara ya kustukiza kujua maendeleo yake. Baada ya mwalimu mkuu kusaka jina la mwanangu nae akanambia, “Mzee huyu mtoto hajaja shule mwezi wa tatu sasa, tulijaribu kukutafuta ikashindikana, hatujui yu wapi” Jasho likaanza kunitoka mimi, yule mtoto kila asubuhi nampa nauli anaenda shule, na mara nyingi ananiomba michango kumbe hata shule haji.

Niliondoka bila kuaga presha ikiwa juu. Nikaona niende kwenye genge la mke wangu nae nikamfanyie ziara ya ghafla nimhadithie mambo ya mwanae, nilipofika pale nikakuta kuna mdada mwingine anauza genge. Nikamsalimu, na kumuuliza mwenye genge ntampataje, jibu lake lingeniua kama ningekuwa si mkakamavu, “Mume wake kaja kumchukua na gari wameenda kununua shamba Bagamoyo”.

Nikaondoka nimechanganyikiwa, nikajuwa hapa dawa yangu moja tu, nayo ni Sabrina, mtoto wa Kinyaturu pale ambapo nikipata maudhi huwa naenda kubembelezwa. Nikatwanga mguu kwa Sabrina nae nikamfanyie ziara ya ghafla ili anipoze moyo. Nilipogonga mlango wa chumba chake akatoka mbaba wa miraba minne, akanisalimia kwa upole, “Salama kaka unasemaje?” Jibu likanitoka “Samahani mie nilimkopesha huyu dada wa chumba hiki vitenge, nilikuja kuuliza kama ameshapata hela yangu” Ziara za kushtukiza zinataka moyo wa chuma jamani

MSAADA TUTANI: MZEE NJEMBA ATOWEKA NYUMBANI KWAKE MAGOMENI MAKUTI, DAR, NDUGU WANAMTAFUTA

$
0
0
Ndugu na jamaa wanatarifiwa kwamba Bw. Hemed Mzee Ibrahim "Njemba" (pichani)  ametoweka nyumbani kwake Magomeni Makuti mtaa wa Mchinga namba 22 jijini Dar es salam toka siku ya Alhamisi tarehe 24/12/2015. 
Alionekana mara ya mwisho kwenye msikiti wa Magomeni Makuti muda wa alasiri alipokwenda kuswali, akiwa kavaa balaghashia (kama hiyo pichani), shati la light purple, suruali ya bluu na kandambili za bluu. Baada ya hapo hakurudi nyumbani kwake na hadi sasa hajulikani alipo. Mzee Njemba hupendelea kutembelea Magomeni Makuti.
Wanafamilia wanaomba mwananchi atayebahatika kumuona atoe tarifa kwa mkwewe Yusuf  anayepatikana katika namba 0784 606 262.
Wanatanguliza Shukurani za dhati kwa wote na kumuombea salama mzee wao.



Kampuni ya Ageco Energy & Construction Ltd yafunga mwaka kwa Kufunga Mtambo Mkubwa wa Sola Hospitali ya Mkoa Singida.

$
0
0


 Kampuni Ageco Energy & Construction Ltd ni kampuni ya kitanzania inayotoa huduma mbali mbali za ukandarasi ikiwemo ufungaji wa mitambo ya umeme wa jua (solar power) kwa watu binasfi, taasisi za umma, mashirika ya nje, na wateja wengine toka sekta binasfi.  Hivi majuzi Ageco ilikamilisha mradi wake wa mwisho wa mwaka kwa kufunga mtambo wa umeme wa sola ujulikanao kitaalamu kama solar hybrid backup system katika hospitali ya Mkoa wa Singida. 

 Mtambo huu wenye uwezo wa kuendesha vifaa vyenye jumla ya Kilowatt 15.7 utasaidia kutoa umeme kwa muda wa masaa 24 katika jingo la maabara la hospitali ya mkoa wa Singida hata kama umeme wa gridi ya taifa ukikatika. Mwezi wa Juni 2015, Ageco pia walifunga mtambo mwingine kama huu katika hospitali kuu ya mkoa wa Rukwa iliyoko Sumbawanga. Miradi hii imepewa ufadhili na Shirika la Misaada toka nchini Marekani linaloitwa Abbott Fund ambalo tayari limetoa misaada mingi katika kuimarisha sekta ya afya nchini Tanzania.

Ageco ni kampuni ya kitanzania inayotoa huduma za ufungaji wa mitambo ya umeme wa kawaida, umeme wa jua, umeme unaotokana na mabaki ya takataka (biomass) pamoja na huduma za ukandarasi wa majengo/nyumba na barabara.  Bei zao ni nafuu na wanatoa huduma kwa ustadi na weledi mkubwa. Wanapatikana kwa njia ya simu kupitia namba 0758 733 333 au 062 222 064. Vile vile wanapatikana kwa email kupitia info@agecoenergy.com. Ofisi zao ziko barabara ya Bima, Mikocheni B, jijini Dar es Salaam. Unaweza pia kutembelea tovuti yao www.agecoenergy.com kwa maelezo zaidi kuhusiana na huduma zao.

KAMERA YA MTAA KWA MTAA NDANI YA MICHUZI TV NA TASWIRA ZA GARI LA SODA BAADA YA KUPIGA MWELEKA.....

YANGA YAIBONYEZA MBEYA CITY 3-0

$
0
0
Mshambuliaji wa Yanga, Deus Kaseke akichuana na beki wa Mbeya City, John Kabanda  katika mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Yanga imeshinda 3-0. (Picha na Francis Dande).
 Mshambuliaji wa Yanga, Deus Kaseke akiwatoka mabeki wa Mbeya City.
 Wachezaji wa Mbeya City wakimzonga mwamuzi Jeonesia Rukyaa kutoka Kagera baada ya Yanga kupata bao la kwanza.
 Sio goli.............
 Kocha wa Yanga, Hans Pluijm akitoka wakati wa mapumziko.


Mashabiki wa Mbeya City.
 Polisi wakituliza fujo zilizotokea katika jukwaa la Mbeya City.
 Donald Ngoma wa Yanga akichuana na Haruna Shamte.
 Amis Tambwe wa Yanga akishangilia bao la pili aliloifungia timu yake.
 Thaban Kamusoko (katikati) akishangilia na Deus Kaseke na Simon Msuva.
 Wakishangilia kwa staili ya aina yake.
 Deus Kaseke wa Yanga akiwania mpira na mchezaji wa Mbeya City.
 Hatari....

 Mashabiki wa Mbeya Cuty wakiwa wameduwaa wakishuhudia timu yao ikipata kipigo kutoka kwa Yanga.

Mdau Edwini Mjwahuzi na Hildegarda Mashauri wameremeta leo jijini Dar

$
0
0
 Mdau Edwini Mjwahuzi ambaye ni Mpiga picha wa Magazeti ya Kampuni ya Mwananchi, jioni ya leo ameamua kuvunja kibanda cha Makapera na kukimbilia kwenye Mjengo wa wanandoa, kwa kufunga pingu za maisha na Bi. Hildegarda Mashauri kwenye Kanisa la Mtakatifu Joseph, Jijini Dar es salaam.
  Mdau Edwini Mjwahuzi na Mkewe Bi. Hildegarda Mashauri pamoja na Wasimamizi wao wakiwa kwenye ibada ya ndoa, iliyofanyika jioni ya leo kwenye Kanisa la Mtakatifu Joseph, Jijini Dar es salaam.
Mdau Edwini Mjwahuzi akimvisha pete Mkewe Bi. Hildegarda Mashauri, wakati wa Ibada ya Ndoa yao iliyofanyika kwenye Kanisa la Mtakatifu Joseph, Jijini Dar es salaam leo.
 Mdau Edwini Mjwahuzi na Mkewe Bi. Hildegarda Mashauri wakiwa ni wenye furaha tele mara baada ya kufunga pingu za maisha na kuwa mwili mmoja, kwenye Kanisa la Mtakatifu Joseph, Jijini Dar es salaam leo.

RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA DKT JOHN POMBE MAGUFULI AKUTANA NA RAIS WA ZANZIBAR DKT ALI MOHAMED SHEIN IKULU DAR ES SALAAM LEO

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimlaki Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein  Ikulu jijini Dar es salaam leo Desemba 26, 2015
  Rais Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiwa katika mazungumzo  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein  Ikulu jijini Dar es salaam leo Desemba 26, 2015
RaisRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimsindikiza  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein  baada ya mazungumzo  Ikulu jijini Dar es salaam leo Desemba 26, 2015. PICHA NA IKULU

NENO LA LEO MTAANI...

TANZIA

$
0
0
Ndugu Crammer Chiduo wa tabata dsm anasikitika kutangaza kifo cha kaka yake Dr Elizer Chiduo kilichotokea siku ya jumamosi tar 27/12/15 katika hosp ya muhimbili. 

Misa ya kumuombea marehemu pamoja na heshima za mwisho itafanyika nyumbani kwake chuo kikuu mjini dsm siku ya jumatatu tar 28/12/15 kabla ya kuanza safari ya kuelekea kilosa katika kijiji cha Magubike kwaaajili ya mazishi siku ya jumanne tar 29/12/15. 

 Bwana alitoa na bwana ametwaa jina lake lihimidiwe.

 Amen

Mwana Fa anogesha hafla ya miaka 250 ya Hennessy

$
0
0
MWANAMUZIKI mahiri wa muziki wa Hip Hop nchini, Hamis Mwinjuma maarufu kama Mwana Fa amezikonga nyoyo za mashabiki wake kwenye hafla ya kuadhimisha miaka 250 ya kinywaji cha Hennessy yaliyofanyika katika baa ya Oasis Masaki.

Mwana Fa alianza kuimba majira ya saa nne ambapo alianza kwa kuimba nyimbo zake mbalimbali zilizowahi kutamba kama vile, Mimi na Mabinti pamoja na nyinginezo za zamani.

Baada ya kumaliza nyimbo hizo za miaka ya nyuma akaanza kuimba nyimbo zake za sasa ukiwamo ule wa Mfalme na nyinginezo mpya.

Watu wengi walihudhuria hafla hiyo ya maadhimisho ya kinywaji hicho iliyoenda sambamba na maonesho ya michoro mbalimbali kuhusianana historia ya kinywjai hicho ambacho asili yake ni Ufaransa.

Pia watoa burudani mbalimbali kama vile kundi la Mosaic Collective pamoja na Mac Band walitoa burudani.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kumalizika kwa maadhimisho hayo, mratibu wa maadhimisho hayo ambae pia ni mmiliki wa baa ya Oasis Nuru Mosha alisema kuwa kinywaji hicho kimekuwa karibu zaidi na sanaa ya Tanzania kwa ujumla mbali na kufanya biashara.

Mosha alisema kuwa kwa kuwa mwanzilishi wa kinywaji hicho alikuwa ni mtu mpenda sanaa hasa aiwa anajishughulisha na sanaa ya uchoraji na hivyo wageni wanaotembelea michoro hiyo wanapata kufahamu kiundani zaidi historia ya kinywaji pia.
 

Mwana FA akiimbaKulikuwa na muziki poa kutoka kwa Dj
Madam Ritha Paulsen akiwa na Mwana FA pamoja na Mmiliki wa Oasis Baa, Nuru mosha
Akiendelea kuimba huku akiwa na chupa yake ya Hennessy
Mheshimiwa Zitto pia alikuwapo

Chupa ya Hennessy 250 Collectors blend iliyotengenezwa maalum kusherekea miaka 250 ya kinywaji hicho.
Kwa ndani kulikuwa na eneo lilikowekwa picha mbalimbali kuhusiana na historia ya kinywaji hicho
Wageni waliojumuika pamoja siku hiyo

NENO LA LEO MTAANI

BEN POL AELEZA SABABU ZILIZOPELEKEA AVRIL KUTOONEKANA KWENYE VIDEO YA 'NINGEFANYAJE'

$
0
0
Siku chache baada ya kuachia video ya wimbo wake - ‘NINGEFANYAJE’, muimbaji wa R&B kutoka Tanzania, Bernard Paul  maarufu kama Ben Pol ameeleza sababu zilizopelekea muimbaji  Avril kutoka Kenya aliyeshirikishwa kwenye wimbo huo,  kutoonekana kwenye video hiyo anayoitaja kuwa kubwa kuliko video zote alizowahi kufanya.

Katika video hiyo iliyoongozwa na Justin Campos wa Afrika Kusini, Ben Pol anaonekana akiimba na Rossie M  ambaye pia ameshirikishwa kwenye wimbo huo huku mashabiki wakiisikia sauti ya Avril bila kumuona mwimbaji huyo mrembo.

Ben Pol amewaomba radhi mashabiki wake kwa kuwapa video ambayo haijakamilisha wahusika wote hususan kutokuonekana kwa Avril,  na kwamba sababu zilizopelekea hivyo zilikuwa nje ya uwezo wa pande zote katika utayarishaji wa video hiyo.

​​​Ben amesema kuwa baada ya yeye na Rossie M kuwasili Afrika Kusini ilikoshutiwa video hiyo, zilijitokeza changamoto muda mfupi kabla ya kuanza zoezi hilo. Ben Pol ameeleza kuwa pamoja na kuwa na maandalizi makubwa, video ya ‘Ningefanyaje’ ilikumbwa na changamoto nyingi tangu awali zilizopelekea kuahirishwa mara tatu.

“Kwa kweli hii video tokea mwanzo ilikuwa na changamoto, kwanza tuliisogeza mbele karibu mara tatu tena tukiwa tayari tumeshafika Afrika Kusini mimi na Rossie,” alisema Ben Pol. “Mara ya kwanza ni kutokana na ‘delay’ ya viza upande wa Avril. Si unajua Wakenya wao wanaenda South kwa viza tofauti na sisi Tanzania hatuendi kwa viza so kwetu ni rahisi zaidi muda wowote tu ukiamua fasta unaenda,” aliongeza.

Mkali huyo alieleza kuwa baada ya terehe mpya kupangwa na muongozaji aliyeshuti video hiyo, Justin Campos, siku moja kabla ya kushuti, AVRIL alipata tatizo lingine ambalo lilimzuia kusafiri kwa siku iliyofata kwenda Afrika Kusini.


Wakati huo huo, Campos naye alimueleza Ben Pol kuwa  kwa jinsi ratiba yake ilivyo endapo ataahirisha tena kushuti video hiyo, ratiba yake isingemruhusu kushuti video hiyo hadi Januari au Februari 2016,  kitu ambacho Ben Pol amesema  kisingewezekana kwasababu ingeendelea kumgharimu zaidi kifedha na kuvuruga ‘timing’ yake.

“Kutokana na hali hiyo, sikuwa na jinsi nyingine zaidi ya kukubali matokeo kwasababu  mwisho wa siku si mimi wala Avril wala director aliyekwamisha bali ni ‘situation’ ambayo ilikuwa nje ya uwezo wa kibinadamu.” Ben Pol anaeleza.

Ameongezea kuwa pamoja na kwamba angeweza kuamua kushuti video kwa kutumia version nyingine ya wimbo huo isiyokuwa na sauti ya Avril ili video isionekane na upungufu wake, lakini hakupenda kufanya hivyo kwa kuwa lengo kuu la wimbo lilikuwa kumshirikisha mwimbaji huyo. Pia, mashabiki wangekosa ladha nzuri na kazi nzuri aliyoifanya Avril.  Hivyo, aliamua kufanya video hiyo bila Avril na kukusudia kuwaeleza mashabiki wake kilichosababisha hali hiyo kwa kuwa aliamini mashabiki wataelewa magumu aliyopitia katika kuwapa video hiyo waliyokuwa wakiisubiri.

“Namshukuru sana Avril kwa kukubali kufanya kazi na mimi kwasababu imetimiza moja kati ya malengo yangu ya 2015, ambayo ilikuwa kuanza kufanya kazi na wasanii wa nje ya Tanzania na yeye ndiye alikuwa chaguo langu la kwanza. Ni imani yangu tutafanya tena project nyingine ya pamoja na kuikamilisha kama tulivyoikusudia,” alimaliza Ben Pol na kuwashukuru  mashabiki wake kwa kuupokea kwa mtazamo chanya wimbo na video yake.

KUPATANA WAUAGA MWAKA KWA KUKUTANA PAMOJA NA WADAU WAO

$
0
0
Kupatana.com ni website ya matangazo madogo madogo ya bidhaa mbalimbali kutoka kwa wauzaji hapa Tanzania. Website hii ilianzishwa rasmi mnamo mwaka 2013 ambapo wakati wa kuanzishwa kwake ilikuwa ikitembelewa na watu takriban elfu tatu kila siku.

Dhumuni la website ya Kupatana.com ni kuwezesha upatikanaji wa taarifa za bidhaa ambazo zinauzwa ikiwemo magari, samani, nyumba, vifaa vya umeme pamoja na nguo au bidhaa binafsi. Lengo ni kuwaunganisha wauzaji na wanunuzi wa bidhaa zao. Katika hili, hadi sasa Kupatana.com imefanikiwa kuwa soko kubwa kabisa la bidhaa mtandaoni. 

Hadi sasa, tunatembelewa na watu wanaozidi 67,000 kwa siku. Kwa kutumia mtandao huu, muuzaji anaweza kupata mafanikio Zaidi kwa kufikisha taarifa ya bidhaa alizonazo nje ya eneo alilopo bila gharama yoyote.

Hayo yalisemwa na Meneja Masoko wa mtandao wa Kupatana.com Bwana Makusaro Tesha katika hafla ya chakula cha jioni ambayo ilihudhuriwa na wafanyakazi na baadhi ya wateja wa Kupatana.com … Vilevile katika hafla hiyo Mr. Tesha alitoa wito kwa vijana na wajasiriamali kuchukua fursa na kuutumia vizuri mtandao wa Kupatana kwani hauna gharama na unawafikia wanunuzi wengi. Alisema, “jambo la kwanza ni kupakua (download) application ya kupatana kwa kupitia Google play store. Ukiwa na app ya Kupatana na kuitumia inavyopaswa ni sawa na kuwa na duka lako wakati wote”.


Vilevile baadhi ya wateja waliohudhuria hafla hiyo walisema kuwa wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuongeza mauzo kwa kutumia mtandao huu. Mmojawapo wa wateja hao Bwana Mohammed Waqas wa Jazmak Motors alisema toka waanze kutangaza magari yao kwenye mtandao wa Kupatana wamekuwa wakipata wateja wengi hata kutoka nchi za jirani ikiwemo Malawi na Zambia. 
Makusaro Tesha akizungmza na wadau mbalimbali wa kupatana wa KUPATANA waliojumuika na watumishi katika tafrija ya kuuaga mwaka 2015 na kuukaribisha mwaka mpya. Tafrija hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam hivi karibuni. 

Kupatana.com ni website ya matangazo madogo madogo ya bidhaa mbalimbali kutoka kwa wauzaji hapa Tanzania. Website hii ilianzishwa rasmi mnamo mwaka 2013 ambapo wakati wa kuanzishwa kwake ilikuwa ikitembelewa na watu takriban elfu tatu kila siku.
Makusaro Tesha akizungmza na wadau mbalimbali wa kupatana wa KUPATANA waliojumuika na watumishi katika tafrija ya kuuaga mwaka 2015 na kuukaribisha mwaka mpya. Tafrija hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam hivi karibuni. 
Makusaro Tesha akizungmza na wadau mbalimbali wa kupatana wa KUPATANA waliojumuika na watumishi katika tafrija ya kuuaga mwaka 2015 na kuukaribisha mwaka mpya. Tafrija hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam hivi karibuni. 
 Makusaro Tesha wa Kupatana wakizungumza na wadau wa KUPATANA
 Wafanyakazi wakiwa na furaha ya kuwa pamoja,
 Mama Kupatana akisalimiana na mmoja wa wadau wa KUPATANA.
 Wafanyakazi wa KUPATANA wakiwa katika tafrija hiyo ya kufunga mwaka 2015
 Msimamizi wa shughuli za Kupata, Ezekiel Alex akizungumza kuhusiana na jumuiko hilo. 
 Mkuu wa huduma kwa wateja, Neema Mwakalonge akizungumza.
 Msimamizi wa bidhaa za 'Real Estate' Liberator Wyson akizungumza.
 Msimamizi wa bidhaa mchanganyiko, Jesca Mathew nae akitoa salamu 
 Muda wa maanjumati ulifika na wateja pamoja na wafanyakazi wa Kupatana.com walijumuika katika mlo huo. 
 Wafanyakazi wa Kupatana.com na wateja wao walikula na kunywa
Burudani ya mziki ilikuwepo ya kukata na shoka.
**************

WAWEKEZAJI KATIKA MIGODI TANZANIA WATAKIWA KUSHIRIKIANA NA WAKAZI WAISHIO MAENEO HAYO ILI KUPUNGUZA MIGOGORO

$
0
0
Baadhi ya Washiriki wa Mdahalao huo wakifuatilia mada iliyokuwa ikijadiliwa wakati wa mdahalo.

Nchi mbalimbali duniani zimekuwa na sera mahususi kwa ajili ya kukaribisha wawekezaji mbalimbali kuja kuwekeza kwenye nchi zao ili kuweza kupata kipato kupitia kodi mbalimbali na faida nyingine kama ajira kwa wenyeji, uboreshwaji wa miundo mbinu n.k. Moja ya nchi hizoni pamoja naTanzania. Tanzania ilibadilisha sera zake za kiuchumi mwanzoni mwa miaka ya 1990, kwa kutoa fursa kwa sekta binafsi kuweza kumiliki uchumi. 

Sera hii ilivutia wawekezaji wengi toka nje na ndani kuwekeza katika sekta mbalimbali, moja ya maeneo ambayo wakezaji wamejikita ni sekta ya madini. Shinyanga ni moja kati ya mikoa yenye utajiri mkubwa wa madini nchini na hivyo kuvutia wawekezaji wakubwa katika sekta hiyo. Mfano mzuri ni kampuni ya Barrick inayomiliki mgodi wa dhahabu wa Buzwagi uliopo wilayani Kahama mkoani humo.

Mgodi huo unazungukwa na vijiji vitatu ambavyo ni Mwendakulima, Mwime na Chapurwa. Lakini kutokana na hali halisi kumekuwa na kelele nyingi za manung’uniko toka kwa jamii zinazoishi karibu na maeneo hayo kuachwa bila maendeleo yoyote wakati wageni wanachukua madini kwa kiwango ambacho hakijulikani.

“Kitu kingine uwepo uwazi waweke uwazi katika haya masuala ya madini mapato wamepata kiasi gani wawekezaji na serikali yenyewe imepata kiasi gani, ikibidi hata kwa wale wananchi wanaozunguka mgodi huu au migodi mingine ya Tanzania. Waweze kuwa wanawabandikia kwamba mwezi huu mgodi umeingiza kipato hiki na serikali imepata hiki angalau kidogo inaweza kupunguza manung’uniko. Kwa watanzania wengine ambao wanaishi sehemu ambapo hapana madini wapeleke hata kwenye magazeti matangazo ya mapato,” anafafanua mkazi wa Mwime.


Haya yamejiri kwenye mda- halo uliondaliwa na waraghabishi wa Chukua Hatua toka kijiji cha Mwime. Ambapo wananchi walipata fursa yakuchangia mawazo kama madini ni laana ama neema. Katika mdahalo huo ambao ulifanyika katika shule ya sekondari ya Mwendakulima washiriki toka kada mbalimbali za kijamii Kama wachungaji, mashekhe, wakulima, walimu, watendaji wa vijiji, wanafunzi na waandishi wa habari walipatafursa ya kuchangia mawazo yao kama madini ni laana ama neema. 

Mwanafunzi wa kike toka katika shule ya sekondari ya Mwendakulima yeye aliona kwamba madini yanaweza yakawa ni janga la mazingira pale aliposema kwamba, “Suluhisho jingine angalau wangebadilisha mfumo wa uchimbaji, kwa sababu mfumo wanaotumia ule yaani kadri siku zinavyokuja kutakuwa na janga kubwa sana, angalia udongo uliofika pale huku chini kuna nini.” Ukiacha changamoto ya mazingira, suala jingine lililojitokeza ni athari zinazoletwa na kemikali mbalimbali ambapo mwalimu mraghabishi.

Paul Chui wa shule ya msingi Mwime alisema, “Kwa kweli kutokana na sera ya elimu, bado tunafundisha elimu kwa kuzingatia sera ya elimu. Hivyo kwa mimi kama mwalimu najitahidi sana kuwaelekeza wanafunzi kuhusu suala zima la athari za kemikali kama vile sunlight pamoja na mekyuri.” Wakati washirki wengine waliojitokeza wao walielezea tatizo la kiungozi na mikataba mibaya. 

Katika kuelezea tatizo hilo walielezea usiri uliopo kwenye mikatabana hivyo kushauri wananchi kuhusisha siasa na mali zao kwa kuhakikisha kwamba wakati wa kupiga kura ni wakati sahihi wa kudhibiti maliasili za umma kwa kuchagua viongozi wanaofaa. Mapungufu katika sera pamoja na sheria za madini ni moja ya sababu zilizotajwa kufanya madini yaonekane laana kwa wananchi wanaozunguka migodi hiyo.

Katika maelezo yake kwa washiriki, George Kingi ambaye ni mtendaji wa kijiji cha Mwime alisema, “Kuna mapungufu kwenye sheria zetu hata ungemweka leo mwingine hata kila siku kama sheria hujaiboreshwa bado unarudi kulekule kwa hiyo suala la sheria lifanyiwe marekebisho. Kingine ni sera. 

Sera kama haisemi Mwime waachiwe asilimia fulani, hata ungemleta mwingine kesho na mwingine atakwamishwa na sera ambayo haisemi wanamwendakulima mbaki na nini.” Katika hili ushauri uliotolewa ni wa kukaa vikao wananchi wanatakiwa kutoogopa na wanapokaa kwenye vikao kweli wasema.

Kwa kuwa kama kuna watu wa kupiga kelele kule juu sheria na sera zibadilishwe na zikabadilishwa basi kila kitu kitakuwa sawa. Kama anavyomalizia George, “Ukishabadilisha sheria na sera hata maji Mwime unayapata hata gari unaletewa si sera inasema uletewe gari kama sera haisemiutaletewa gari?” 

Akitoa majumuisho ya mdahalo huo uliondaliwa na waraghabishi walimu na wakulima Toka kijiji cha Mwime, mwenyekiti Maimuna Said alisema “Madini sio laana lakini viongozi wenyewe ni laana kwa sababu hawatendi haki ipasavyo kulingana na katiba ya jamhuri wa muungano wa Tanzania. Hii ni neema toka kwa Mungu.” 

 Suala jingine ambalo limejitokeza katika mdahalo huo ni wananchi kutokuwa na furaha jinsi ambavyo serikali haiwashirikishi katika kufanya maamuzi muhimu yanayohusu mustakabali wa maeneo yao. Hivyo ili madini yasiwe laana ni muhimu sana kwa serikali kuwashirikisha wananch toka hatua za mwanzo.

Lakini pia suala zima la kutoa elimu ya uraia kwa wananchi. “Kuna haja kubwa ya kutolewa elimu hususani elimu ya uraia. Watu kwanza watambue haki zao, mtu akishatambua haki zake kuna kuwa na uwezekano wa yeye kuzidai, lakini kama watu bado hawatapata elimu hiyo ni kwamba watu watakuwa wananung’unika tu pembeni. Lakni hajui aanzie wapi na hajui aishie wapi,” anafafanua Maalim Daudi Athman Imamu wa Masjid Noor Nyandekwa.
Viewing all 40001 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>