Quantcast
Channel: MTAA KWA MTAA BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 39146

MZIKI MNENE WA EFM WAPAGAISHA UKONGA

$
0
0
Jumamosi ya tarehe 4 Mwezi wa Oktoba 2014,wakazi wa ukonga walipata fursa ya kupagaishwa na burudani ya mziki mnene inayoandaliwa na kituo cha redio cha EFM kwenye ukumbi wa Ukonga Reaction Centre.

Idadi ya watu wasio hesabika walijitokeza kwa wingi ndani ukumbi huo. Tuliongea na mmoja wa waandaji wa tamasha hili Dickson Ponella,ambae alisema kuwa mziki mnene utazunguka Dar Es Salaam nzima na viunga vyake,kama ratiba inavyo elekeza.

“Haina haja ya watu kugombania kuingia ndani,wakumbuke tamasha hili halina kiingilio,ni kwa watu wote.Tunashukuru kuona baadhi ya watu walio safari kutoka mikoa ya karibu kama vile Morogoro,Tanga na Mtwara kuja kutushika mkono”,alisema.

Kwa upande mwingine meneja uhusiano wa EFM Kanky Mwaigomole,alisema kuwa wasikilizaji wote waendelee kusikiliza matangazo yao ili wajue watakuwa wapi na lini.
“Kwakila tamasha hili tuna kipengele kiitwacho kibunda.Huwa tunawaita watu angalau watatu,na tunawauliza maswali kumi ndani ya dakika moja na mshindi hupewa zawadi mbali mbali,ikiwemo pesa taslimu”,alisema Mwaigomole.

Meneja uhusiano huyo aliendelea na kusema kuwa tamasha hilo la muziki mnene litaendelea tena jumamosi ya tarehe 11 mwezi huu wa Oktoba mwaka 2014,huko Kigamboni Navy Beach,Dar es Salaam.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 39146

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>