Mkurugenzi wa CAMFED Tanzania, Bi. Lydia Wilbard akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa mwisho wa mwaka wa watoto wasichana waliosomeshwa kwa msaada na Shirika la CAMFED, ambapo mkutano huo umeipongeza Serikali kwa kitendo cha kuwarejesha shuleni wanafunzi wote waliokatiza masomo kutokana na sababu mbalimbali wakiwemo wanafunzi waliopata ujauzito wakiwa shuleni.
Mkurugenzi wa CAMFED Tanzania, Bi. Lydia Wilbard akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa mwisho wa mwaka wa watoto wasichana waliosomeshwa kwa msaada na Shirika la CAMFED, ambapo mkutano huo umeipongeza Serikali kwa kitendo cha kuwarejesha shuleni wanafunzi wote waliokatiza masomo kutokana na sababu mbalimbali wakiwemo wanafunzi waliopata ujauzito wakiwa shuleni
CAMFED YAUNGA MKONO SERIKALI KUWAREJESHA WANAFUNZI SHULENI
WAKULIMA ARUSHA WAPEWA ELIMU YA USAJILI WA VYAMA VYA UMWAGILIAJI NA UCHANGIAJI WA ADA NA TOZO
Na Mwandishi wetu – Arusha
Wakulima katika skimu za kilimo cha umwagiliaji Mkoani Arusha, wamepewa elimu kuhusiana na namna ya kusajili vyama vya umwagiliaji na utoaji wa ada na tozo na kupewa utaratibu wa kulipia ada hizo zitakazosaidia kuboresha na kurekebisha miundombinu ya kilimo cha umwagiliaji pale itakapokumbwa na madhara yatokananyo na athari za mabadiliko ya tabianchi au uchakavu.
Bi Fatuma Mwera Afisa Kilimo kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji akizungumza na baadhi ya viongozi wa skimu za kilimo cha umwagiliaji katika Halmashauri ya Arusha katika kata ya Ilikiding’a alibainisha kuwa, usajili wa vyama vya umwagiliaji utasaidia skimu kutambulika na kupata fursa zinazojitokeza ikiwa ni pamoja na kupelekewa miradi ya ujenzi wa miundombinu ya umwagiliaji.
Aidha aliwaasa viongozi hao kuwa vinara katika swala zima la usimamizi na utunzaji wa mazingira hususan vyanzo vya maji ikiwa ni pamoja na kutokufanya shughuli za kibinadamu katika vyanzo hivyo.
Aliendelea kusema kuwa, skimu zote za kilimo cha umwagiliaji zitafanyiwa maboresho kwa awamu lakini , skimu ambazo zimesajiliwa ndizo zitakazopewa kipaombele kwanza wakati wa maboresho hayo. “ Ni vizuri kusajili wote kwa pamoja ili tupange mipango ya kazi kirahisi na kuzifikia skimu kwa awamu, Alisisitiza.”
Picha ikionesha wataalam kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji katika kikao cha pamoja na Afisa Kilimo Umwagiliaji na Ushirika wa Wilaya ya Arusha,hayupo pichani wakijadili kwa pamoja maswala ya tozo za Umwagiliaji.
SHULE YA BILIONEA LAIZER NA O'BRIEN ZAANZISHA USHIRIKIANO
BAADHI YA WAISLAMU WAMEASWA KUACHA KULALAMIKA
MERIDIAN GAMING GROUP KUSHIRIKI MAONESHO YA BRAZIL iGAMING SUMMIT

Meridian Gaming Group ambao ni kampuni kubwa ya michezo ya kubashiri duniani na waasisi wa soko la America Kusini, watashiri kwenye maonesho ya Brazil iGaming Summit (BiS) 2021, maonesho makubwa zaidi kufanyika Sao Paolo, Disemba 1-2.
Ukizungumzia michezo ya kubashiri, Meridian Gaming inavitu vingi vipya kwenye soko la Brazili na Amerika Kusini, kubwa zaidi ni Tiketi ya Malipo kwenye akaunti za mtandaoni na sifa ya nafasi tatu. Kampuni hii ni miongoni mwa kampuni za mwanzo kuanza kufanya kazi kisheria kwenye ukanda huu na, ubobezi wake utachangia sana kwenye majadiliano ya kiuchumi na namna bora ya usimamizi kwenye hili soko.
Kutakua na safu tofauti za kasino, sloti ya Meridian Casinoitaonekana kule Sao Paolo. Tayari ni kampuni inayojulikana zaidi duniani kutokana na upekee wa michezo yake na bonasi za aina mbili.
Kwa miezi mingi sasa, Meridian imekuwa ikilipa mamilioni ya ushindi na jakipoti za kasino lakini, ushindi mmoja uliweka rekodi kwenye michezo ya sloti duniani na, pengine itaendelea kubaki kwenye rekodi.
Kwa siku za hivi karibuni, Meridian imelipa jakipoti ya €1,129,692.15 kwenye mchezo wa sloti ya Wild Crusade: Empire Treasures. Haya ni malipo makubwa kwenye soko la Ulaya kwa siku za hivi karibuni.
Mtandao makini michezo na teknolojia ya kubashiri wa B2C na B2B, upo tayari kwa maonesho ya Brazili. Kwa taarifa zaidi na kupata tiketi yako, tuwasiliane kupitia https://meridian.bet/contact.html na info@meridianbet.com
NSSF YATUNIKIWA TUZO KUTHAMINI MCHANGO WAKE KATIKA MAPAMBANO DHIDI YA UKIMWI
Afisa Mwandamizi Utawala, Naphisa Jahazi ambaye pia ni Mwelimishaji rika mahala pa kazi kutoka NSSF, Mkoa wa Temeke akielezea kwa baadhi ya wananchi namna NSSF ilivyojielekeza katika kudhibiti VVU, UKIMWI na magonjwa sugu yasiyoambukizwa mahala pa kazi, wakati wa Maonesho ya Maadhimisho ya siku ya UKIMWI duaniani Kitaifa yanafanyika katika Mkoa wa Mbeya
Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), haujawaacha nyuma makundi yenye mahitaji maalum, Mkalimani wa Lugha ya alama Baraka Bakari (wa kwanza kulia) akiwatafsiria walemavu wa usikivu elimu kuhusu hifadhi ya jamii, walipotembelea banda la NSSF wakati wa Maonesho ya Maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani ambayo Kitaifa yamefanyika Mbeya
WAWEKEZAJI ZAIDI YA 140 KUTOKA ITALIA WAWEKEZA TANZANIA
KICHANGA CHAOKOLEWA KWENYE SHIMO LA CHOO KIKIWA HAI KAGERA
Benki ya CRDB yaahidi Mitaji na Mikopo kwa wafanyabiashara, wawekezaji kutoka Italia

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela wakati wa jukwaa la biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Itali liloandaliwa na ubalozi wa Tanzania lililofanyika Jijini Roma, nchini Italia.
Nsekela amesema Benki ya CRDB ipo tayari kushirikiana na Serikali ya Awamu ya Sita pamoja na wawekezaji katika kuhakikisha kuwa changamoto zinazoendana na huduma za kibenki zinatatuliwa.
“Nawahakikishia kuwa Benki ya CRDB itawawezesha mikopo ya kuwekeza katika sekta mbalimbali hivyo msiwe na wasiwasi kuhusu mitaji ya kuwekeza ipo karibuni sana tuijenge Tanzania,” amesema Nsekela.
Nsekela ameongezea kuwa Benki ya CRDB inafarijika kuona wawekezaji wengi wameonesha nia ya kuwekeza zaidi Tanzania, huku akimpongeza Balozi wa Tanzania nchini Itali, Mhe. Mahmoud Thabiti Kombo kwa kuandaa Jukwaa hilo ambalo limetoa fursa ya kueleza sekta mbalimbali za uwekezaji zinazopatikana Tanzania.
“Benki ya CRDB pamoja na mambo mengine tutahakikisha kuwa sisi kama benki tunawawezesha wawekezaji wanaowekeza nchini na kuwapa mitaji ya biashara pamoja na biashara za kimataifa kati ya nchi moja na nyingine…,” alisisitiza.
Kwa upande wake Balozi wa Tanzania nchini Italia, Mhe. Mahmoud Thabiti Kombo ameipongeza Benki ya CRDB kwa utayari wake wa kusaidiana Serikali kuboresha mazingira ya uwekezaji nchini kupitia utoaji wa mikopo na mitaji, pamoja na huduma nyengine za kifedha zinazoongeza ufanisi katika uendeshaji wa biashira.
“Benki ya CRDB imeonyesha uzalendo mkubwa kwa kushirikiana na Serikali kuvutia wawekezaji kuja kuwekeza nchini, binafsi sina shaka na uwezo wao kimtaji. Nimefurahi pia wamekwenda mbele zaidi kwa kutoa huduma za ushauri katika uwekezaji, hii inaonyesha ni jinsi gani wamejipanga vizuri,” amesema Balozi Kombo.
Naye, Mwenyekiti wa Chama Wawekezaji katika Hoteli Zanzibar, Bw. Paulo Rosso amewasihi wawekezaji kutoka Italia kuwekeza kwa wingi Tanzania kwa kuwa mazingira ya biashara na uwekezaji ni tulivu na salama.
“Tanzania ni sehemu salama kuwekeza….nawahakikishia mimi nimewekeza Tanzania na ninaona ni sehemu salama ya kuwekeza karibuni sana kuwekeza kwa maendeleo ya Tanzania na Italia,” amesema Bw. Rosso
Jukwa hilo la biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Italia limehudhuriwa na Wafanyabiashara na Wawekezaji takribani 250 kutoka nchi zote mbili. Wafanyabiashara na wawekezaji hao ni wa sekta za utalii, kilimo, madini, na ujenzi.
Pamoja na mambo mengine, jukwaa hilo limewawezesha wafanyabiashara na wawekezaji kujadili fursa, uwezekano wa ubia, changamoto zinazokabili mazingira ya biashara na njia ya kuboresha mahusiano ya kibiashara kati ya nchi hizo mbili.
ELIMU KWA WATOTO WENYE ULEMAVU MKOANI SINGIDA BADO NI CHANGAMOTO
SIMBA YAIFUATA RED ARROWS KWA TAHADHARI
KIKOSI cha Simba kimeondoka leo kuelekea nchini Zambia kwa ajili ya mchezo wa marudiano wa mtoano wa Kombe la Shirikisho la Afrika dhidi ya Red Arrows utakaochezwa Jumapili Desemba 05.
Kocha Mkuu wa Simba Pablo Franco amesema wamejipanga vizuri kwa mchezo wa marudiano japo wanafahamu utakuwa ni mgumu kwao.
Pablo amesema anajua Red Arrows wanataka kupata matokeo katika Uwanja wao wa nyumbani, ila Simba wanamtaji wa mabao hivyo wamejipanga kuhakikisha wanalinda ushindi.
Kauli hiyo ameitoa leo wakati akiwa Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere pamoja na kikosi wakiwa tayari kuelekea Zambia kwa ajili ya mchezo huo.
"Tunajua mchezo utakuwa mgumu Red Arrows watataka kushinda lakini tumejipanga kupambana nao, kikubwa tunahitaji kulinda ushindi wetu tuliopata katika mchezo uliopita"amesema.
" Wachezaji wote wako kwenye hali nzuri na morali ipo juu na tunafahamu kitu gani tunatakiwa kufanya kuelekea mchezo wa jumapili ili kuwapa furaha mashabiki wetu"amesema
Katika mchezo wa awali uliopigwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Simba walipata ushindi wa goli 3-0 na Red Arrows wanatakiwa kushinda goli 4-0 au na zaidi ili kutinga hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho.
Simba walitolewa katika mchezo wa raundi ya kwanza ya Klabu Bingwa Afrika dhidi ya Jwaneng Galaxy na kupangiwa kucheza mchezo wa Play Off dhidi ya Red Arrows.
Kamati ya siasa (CCM) yakagua miradi inayojengwa kwa mamilioni ya fedha za Uviko
Wajumbe wa kamati ya siasa wakikagua maendeleo ya ujenzi wa madarasa manne katika shule ya sekondari ya wasichana ya Manyunyu iliyoko Matembwe shule hiyo imetengewa shilingi milioni 80.Na Amiri Kilagalila,Njombe
NI DESEMBA 26, KIDUNDA DHIDI YA KATOMPA UBINGWA WA WBF
Rais Samia azindua Kiwanda cha Raddy Fiber Manufacturing Ltd , Mkuranga Pwani
NAIBU WAZIRI MWANAIDI AIAGIZA TAASISI YA USTAWI WA JAMII KUFANYA UTAFITI HUDUMA ZA USTAWI WA JAMII




WAZIRI SIMBACHAWENE AKAGUA MAENDELEO YA AWALI UJENZI WA JENGO JIPYA LA WIZARA AWAMU YA PILI
WAZIRI SIMBACHAWENE AKAGUA MAENDELEO YA AWALI UJENZI WA JENGO JIPYA LA WIZARA AWAMU YA PILI, MJI WA SERIKALI, JIJINI DODOMA, KUKAMILIKA OKTOBA 2023.
JUKWAA LA KWANZA LA BIASHARA NA UWEKEZAJI LAFANYIKA ITALIA KWA MAFANIKIO MAKUBWA
MAFANIKIO YA MIAKA SITINI YA UHURU KATIKA SEKTA YA KILIMO CHA UMWAGILIAJI
Kuhusu Tume ya Taifa ya Umwagiliaji;
Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Sera ya umwagiliaji ya Taifa ya Mwaka 2010, ilitoa Mwongozo wa kuwepo kwa mambo mahususi kwenye uendelezwaji wa sekta ya Umwagiliaji pamoja na mambo mengine ni kuwa na chombo cha kuboresha na kusimamia sekta ya umwagiliaji nchini.
Kilimo cha umwagiliaji kilianzia mkoani Arusha enzi za ukoloni, na baada ya Uhuru serikali iliendeleza mikakati mbalimbali ndipo mipango mahuhusi ilianzishwa chini ya wizara husika kama Wizara ya maji na kilimo. Ameeleza Bwana Daudi Kaali, Kaimu Mkurugenzi Mkuu Tume ya Taifa ya Umwagiliaji.
Akiongea Ofisini kwake Mwanasheria wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji, Bw. Godwin Mutahangarwa,alisema katika kutekeleza Sera ya Taifa ya Umwagiiaji, ambayo ilitoa muelekeo wa sekta ya umwagiliaji nchini, serikali ilipeleka mapendekezo bungeni ya kuwa na sheria inayoitwa Sheria ya Taifa ya Uanzishwaji wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji. National Irrigation Act ya mwaka 2013.
Imeelezwa kuwa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji imeanza kutekeleza majukumu yake mwaka 2015, ikiwa ni pamoja na uendelezwaji utekelezwaji na kutoa utaalam na kuratibu na kuthibiti shughuli zote za umwagilaji nchini.
Tume imekuwa ikitekeleza sheria na miongozo na kanuni pamoja na kutoa elimu ya sheria hiyo kupitia vyombo mbalimbali vya habari.
Mkurugenzi wa Tume ya taifa ya Umwagiliaji Bw. Daudi Kaali anabainisha kuwa Tume ina mpango wa kuanza kutoa elimu kwa wananchi ya namna bora ya kuvuna maji ya mvua kwa ajili kilimo cha umwagiliaji na matumizi mengine.
Anaongeza kuwa kwa kusema kuwa lengo ni kuwawezesha wakulima watumie teknolojia ambazo zitawezesha matumizi madogo ya maji ikilinganishwa na sasa ambapo bado wakulima wengi wanatumia mbinu za kizamani.
MABADILIKO YA TABIA YA NCHI.
Kuhusu mabadiliko ya tabia ya nchi Mkurugenzi huyo anaeleza kuwa kuna mikakati kabambe, imewekwa ya kuanza kutoa elimu na kuhamasisha wananchi namna ya kuvuna na kutunza maji wakati wa msika ili yaweze kutumika wakati wa kiangazi kwaajili ya kilimo cha umwagiliaji.
“Kuna teknolojia za kisasa ambazo zinatuwezesha kufanya kilimo cha umwagiliaji pale tu ambapo mmea unahitaji maji, pamoja na umwagiliaji wa kutumia matone ili maji machache yanayopatikana yatumike kuzalisha chakula hapa nchini,”anaeleza Kaali.
Baadhi ya Mafanikio katika sekta ya kilimo cha Umwagiliaji katika kipindi cha miaka 60 ya Uhuru.
Kufikia miaka ya 2000 imelezwa kuwa, Serikali imekuwa ikiendelea kuwekeza katika miundombinu ya kilimo cha umwagiliaji na eneo linalotumika kwa kilimo cha umwagiliaji kwa sasa ni zaidi ya hekta laki sita, (600,000) na kwa kutekeleza ilani ya chama cha mapinduzi (CCM) Tume ya Taifa ya Umwagiliaji, inaendelea kupanua eneo la umwagiliaji kufikia hekta 1,200,000 ifikapo mwaka 2025.
Aidha Serikali, imeendelea kuingiza progam mbalimbali katika sekta ya Umwagiliaji kama vile utengenezaji wa mitambo na maboresho ya Miundombinu ya umwagiliaji, kwa kutumia vyanzo vyake vya fedha vya ndani.
Wakulima nchini walikuwa wakilima kwa kutumia njia za asili,Tume ya Taifa ya Umwagiliaji imeendelea kujenga na kuboresha Miundombinu ya kilimo hicho na wakulima wameweza kujiunga katika skimu kupitia vyama vya umwagilia vinavyosajiliwa na Tume ya taifa ya Umwagiliaji hali ambayo inawapa fursa ya wao kulima katika skimu hizo nchini.
Serikali kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji imetambulisha Ada na Tozo kwa wakulima wa kilimo cha umwagiliaji ili kuendeleza ukarabati wa skimu za umwagiliaji na kuzipatia matunzo, na wakulima wameendelea kupata mafunzo mbalimbali ya kilimo cha umwagiliaji kupitia Technolojia mbalimbali za kisasa zinazotumia maji kidogo,ili kuruhusu maji yaende katika shughuli nyingine za maendeleo na ujenzi wa Taifa,kutoka na mabadiliko ya tabianchi yanayosababisha hali ya ukame na ukosefu wa mvua za uhakika.
Ili kuweza kuhimili na kukabiliana na janga hili,Tume ya Taifa ya Umwagiliaji imekuwa na mikakati ya kuwa na vyanzo vya uhakika vya maji kama vile teknolojia ya uvunaji wa maji ya mvua kwa kuchimba mabwawa yatakayo tumika katika kilimo cha umwagiliaji wakati wa kipindi cha kiangazi.
Bwana Daudi Kaali, Ameeleza kuwa matumizi ya teknolojia ya sensa yaani vifaa vinavyotumika katika kilimo cha umwagiliaji ambapo mkulima atatumia maji kidogo kwa wakati sahihi, teknolojia ambayo imefanyiwa majaribio katika skimu za kilimo cha umwagiliaji mkoani Iringa, imenufaisha wakulima.
Katika ipindi hiki cha miaka 60 ya Uhuru, Idara ya Usanifu na Utafiti; imeweza kuwa kwenye nafasi kubwa ya kusanifu miradi mbalimbali kwa kutumia wataalam wake wa ndani, tofauti na huko nyuma ambapo Tume ya taifa ya umwagiliaji ilikuwa ikitumia wakandarasi washauri kufanya kazi hizo.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara hiyo, Mhandisi Gregory Chigwiye, amesema Idara kwa kutumia wataalam wake wa ndani inaanda na kusanifu miradi kumi, na kuweza kuokoa kiasi cha fedha cha shilingi bilioni moja za kitanzania kama ingetumia mtaalam mshauri kutoka nje.
Mhandisi Chigwiye alisema kuwa, upembuzi yakinifu umekuwa na faida nyingi katika sekta ya kilimo cha umwagiliaji kwani, kabla ya kuanzisha miradi katika sekta ya kilimo cha umwagiliaji, upembuzi yanikinifu unasaidia kufahamu kama mradi unaoenda kutekelezwa unatekelezeka na utakuwa na manufaa kwa jamii.
“Tafiti hizi pia zinaweza kusaidia kufahamu kama kunaweza kuwa athari zozote katika mazingira na kuangalia namna ya kuhimili na kukabiliana na hali hiyo.” Alisisitiza.
Mhandisi Naomi Mcharo ni kaimu Mkuu wa Kitengo cha uthibiti Ubora kitengo kinachohusika na uangaliaji wa ubora wa miundombinu inayojengwa pamoja na kazi zinazofanyika katika sekta ya kilimo cha umwagiliaji.
Mhandisi Mcharo alifafanua kuwa, katika miaka 60 ya uhuru Idara imekuwa na jukumu la kuhakiki na kuangalia ubora ya miundombinu ya kilimo cha umwagiliaji kuanzia kwenye mipango ya pamoja ya ujenzi.
Kwa Upande wa TEHAMA ,katika kipindi hiki cha miaka 60 ya Uhuu, Serikali imefanya mambo mengi makubwa kama vile kuanzisha taasisi za serikali kama vile Serikali Mtandao EGa, Mamlaka ya Mawasilino Tanzania (TCRA) hizi zote ni Juhudi za Serikali za kuhakikisha kwamba Teknolojia ya habari na Mawasiliano (TEHAMA) inakuwa nyenzo muhimu kwa maendeleo ya mtanzania.
Tume ya Taifa ya Umwagiliaji imenufaika na kuwepo kwa mfumo wa mtandao Serikalini wenye kasi, usalama na uhakika ili kuweza kufanya shughuli za ofisi kiufanisi zaidi.
Serikali pia imefanikisha kuwepo kwa mkongo wa Taifa,kuwepo kwa barua pepe katika Ofisi za umwagiliaji nchi nzima kwa njia salama iliyorahisishwa.
MIRADI KATIKA SEKTA YA KILIMO CHA UMWAGILIAJI NDANI YA MIAKA 60 YA UHURU
Mhandisi Ntonda Kimasa ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya ujenzi na uendelezwaji wa Miundombinu ya Umwagiliaji Amesema Serikali Kupitia Tume ya Taifa ya umwagiliaji imewekeza katika Miradi Mikubwa ya kilimo cha umwagiliaji kama ile ya SSIDP, iliyokarabati na kujenga miradi mikubwa ya kitaifa kama DAKAWA na Lower Moshi, miradi ya ASDP, ERPP na TANCAID awamu ya kwanza na ya pili.
Kwa kipindi hiki cha miaka 60 ya Uhuru uzalishaji katika sekta ya kilimo cha umwagiliaji kwa upande wa mazao ya chakula hususan zao la mpunga umeongezeka kutoa tani 2 kwa heka kwa hadi tani 8 hivisasa.
Pamoja na mafanikio yote haya, Tume ya Taifa ya umwagiliaji ina endelea kujenga miundombinu ya umwagiliaji kwa kutumia wataalam wa ndani ili kuboresha utaalam katika shughuli za ujenzi kama vile wa mabwawa na miundombinu mingine.Hataivyo tume ya Taifa ya Umwagiliaji inawashirikisha wakandarasi wenye zoefu wa kujenga miradi mikubwa ya Umwagiliaji ili kuharakisha Maendeleo ya sekta ya Umwagiliaji.
KILIMO CHA UMWAGILIAJI KWA SASA KINACHANGIA 24% YA CHAKULA NCHINI NA MALENGO KATIKA JAMBO HILI NI KUCHANGIA 50% IFIKAPO MWAKA 2025.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Bw. Daudi Kaali akizungumza na waandishi wa Habari hawapo pichani, Ofisini kwake jijini Dodoma mapema leo, kuhusu Mafanikio katika sekta ya kilimo cha umwagiliaji ndani ya kipindi cha miaka sitini ya uhuru.
TGNP YAPONGEZWA KWA JITIHADA ZA KUPINGA UNYANYASAJI WA KIJINSIA
Hayo yameelezwa leo na Diwani wa kata ya Saranga Edward Laizer wakati wa mwendelezo wa siku 16 za Uanaharakati wa kupinga ukatili wa kijinsia uliokutanisha Mtandao wa Vituo vya Taarifa na Maarifa vya Kata za Wilaya ya Ubungo hafla iliyofanyika katika viwanja vya TGNP jijini Dar es Salaam.
"Ili kufanikisha zoezi hili lazima mapambano yaanzie katika ngazi ya familia kwa kuhakikisha hakuna mwanajamii anayethubutu kuonesha vitendo hivyo kwa wanawake na mabinti....Lazima tujenge jamii yenye usawa kuanzia ngazi ya familia." Amesema.
Laizer amesema kuwa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP,) umeleta mabadiliko makubwa tangu kuanzishwa kwake hasa katika ngazi ya familia, jamii na katika ngazi ya kutoa maamuzi.
"TGNP imeleta mabadiliko mengi kubwa zaidi ni katika kutoa elimu kwa makundi mbalimbali wakiwemo wanafunzi juu ya njia ya kuripoti matukio yoyote ya unyanyasaji wa kijinsia hasa unyanyasaji wa kingono, Serikali kupitia Halmashauri, Wilaya, Kata na Mitaa tupo nao pamoja katika hili na kila mmoja kwa nafasi yake ashiriki vita hii." Ameeleza.
Aidha Laizer ameshauri mabadiliko ya sheria ya ndoa ya mwaka 1971 ipewe nguvu zaidi ya kuangazia masuala ya usawa katika umiliki wa mali pamoja na kutambulika na kuipa heshima jinsia ya kike.
Kwa upande wake Diwani wa viti maalum Wilaya ya Ubungo Liberata Samson ameipongeza TGNP kwa kushirikiana na Mtandao wa Vituo vya Taarifa na Maarifa katika kutoa elimu ya kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia.
"Vituo hivi ndiyo jamii na vinashuhudia vitendo hivyo, hatua ya TGNP kushirikiana na vituo hivi wanajamiii na waathirika wa matukio haya wanapata ahueni na pahala pa kusemea,....jamii ishiriki katika vita hii na kwa siku hizi 16 za kupinga vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia ulete mabadiliko chanya kuanzia ngazi ya familia zetu." Amesema.
Awali akitoa taarifa vituo hivyo Mwenyekiti wa Mtandao wa Vituo vya Taarifa na Maarifa Wilaya ya Ubungo Neema Mwinyi amesema ndani ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia vituo vyote vilivyopo katika mikoa 15 nchini vitajadili mafanikio, changamoto na mwendelezo wa mpango mkakati wa kukomesha vitendo hivyo.
Amesema, Serikali imeweka sera na mikakati ya kupinga vitendo vyote vya ukatili na nguvu zaidi ni kwa jamii kushiriki kwa ukaribu katika kukemea na kuripoti vitendo hivyo.
"Tumefanikiwa kwa kiasi kikubwa kutoa elimu katika makundi mbalimbali, kutambulika katika Serikali za Mitaa, Polisi na katika madawati wa jinsia ambapo tumekuwa tukitoa elimu juu ya kupinga vitendo hivyo na jamii imekuwa na mwamko jambo ambalo linaleta matumaini ya kukomesha vitendo vya ukatili wa kijinsia ikiwemo ubakaji, ulawiti na vitendo vingine vya udhalilishaji." Amesema.
Amesema licha ya kuwa na changamoto mbalimbali ikiwemo kutoripotiwa kwa vitendo vya rushwa ya ngono vituo hivyo vimedhamiria kuendelea kutoa elimu, kuwa na mshauri katika kila Kata na Mtaa pamoja na kushirikiana kwa ukaribu na Serikali na wadau katika kukomesha vitendo vya ukatili wa kijinsia.
Hafla hiyo iliyowakutanisha wadau wa Mtandao wa Vituo vya Taarifa na Maarifa Wilaya ya Ubungo, Madiwani, wenyeviti wa Mitaa na wanafunzi ni mwendelezo wa siku 16 za uanaharakati wa kupinga vitendo vyote vya ukatili wa kijinsia kwa kauli mbiu ya 'Ewe Mwananchi Umejipangaje Kupinga Ukatili wa Kijinsia, Komesha Sasa.'