Quantcast
Channel: MTAA KWA MTAA BLOG
Viewing all 39995 articles
Browse latest View live

PROFESA ANNA TIBAIJUKA AKUTANA NA WADAU WA MJI MPYA WA KIGAMBONI DAR ES SALAAM

$
0
0
Waziri Tibaijuka akifunga majadiliano juu ya mradi huo.
Waziri Tibaijuka akiwa ameshikana mikono na mbunge was Kigamboni Faustine Ndungulie na baadhi ya madiwani na viongozi wengine kuonyesha maridhiano namna mradi utakavyotekelezwa.
Kaimu Mkurugenzi Msaidizi, Usanifu Miji na Uendelezaji Hellenic Mpetuta akitoa mada namna mji mpya utakavyopangiliwa katika mkutano huo uliofanyika Chuo Kikuu cha Kivukoni Dar es Salaam leo.
Baadhi ya wadau wakifuatilia mawasilisho ya mada mbalimbali juu ya mradi huo.
Baadhi ya wadau wakifuatilia mawasilisho ya mada mbalimbali juu ya mradi huo.
Wadau wakipata picha ya pamoja na waziri Tibaijuka (katikati) mara baada ya majadiliano juu ya mradi huo.Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com.

RIDHIWANI KIKWETE AZINDUA MRADI WA MAJI JIMBONI KWAKE CHALINZE

$
0
0
Mbunge wa Jimbo la Chalinze,Mh. Ridhiwani Kikwete akizindua mradi wa maji kwenye kijiji cha Mbala kata ya Vigwaza.kushoto ni askofu mkuu wa Jimbo la Mashariki ya kanisa la Waadventista wasabato,Askofu Mark Malekana.
Mbunge wa Jimbo la Chalinze,Mh. Ridhiwani Kikwete akifungua maji kwenye bomba mara baada ya kuzindua mradi wa maji kwenye kijiji cha Mbala kata ya Vigwaza.
Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete akizindua mradi wa maji kwenye Kijiji cha Mbala hapa anaonekana akifungua maji kwa ajili ya kunyweshea mifugo.
Mbunge wa Jimbo la Chalinze,Mh. Ridhiwani Kikwete akimtwisha ndoo ya maji mmoja wa akinamama wa jamii ya kimasai baada ya kuzindua mradi wa maji kwenye kijiji cha Mbala kata ya Vigwaza wilayani bagamoyo.

Na John Gagarini, Bagamoyo

IMEELEZWA kuwa maendeleo ya Tanzania yataletwa na Watanzania wenyewe na si kutegemea misaada mbalimbali toka kwa wafadhili wa kutoka nje ya nchi kama baadhi ya watu wanavyofikiri.

Hayo yalisemwa jana kwenye Kijiji cha Mbala wilayani Bagamoyo mkoani Pwani na askofu mkuu wa kanisa la waadventista wa Sabato Kanda ya Mashariki, Mark Malekana wakati wa uzinduzi wa mradi wa kisima cha maji kilichojengwa na wamuni wa kanisa hilo wa Manzese Jijini Dare s Salaam.

Askofu Malekana alisema kuwa Watanzania wanapaswa kuhakikisha wanaanzisha miradi ya maendeleo kwa ustawi wananchi na si kutegemea kila kitu kutoka kwa wafadhili.

“Ustawi wa nchi untegemea wananchi wenyewe kwani siyo kila jambo kuwategemea wafadhili hasa wale wan je lakini tukifanya wenyewe inaonyesha uzalendo na watu kuipenda nchi yao lazima tubadili mtazamo na kuanza kufadhili miradi sisi wenyewe,” alisema Askofu Malekana.

Aidha alisema kuwa kanisa hilo mbali ya kutoa huduma za kiroho pia imekuwa ikitoa huduma za kijamii ikiwa ni pamoja na miradi ya maji, elimu na afya ambapo kanisa hapa nchini linamiliki vituo vya afya 34, shule za msingi 11, sekondari 15 na Chuo Kikuu kimoja.

Kwa upande wake mgeni rasmi katika uzinduzi wa kisima hicho cha maji pamoja na sehemu ya kunyweshea mifugo, Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete changamoto ya maji ni kubwa na ailikuwa ikisababisha migogoro.

Ridhiwani alisema kuwa migogoro hiyo inatokana na pande mbili baina ya wafugaji na wakulima ambapo maji wanayokunywa watu yamekuwa yakinyweshewa mifugo hali ambayo inasababisha migogoro baina ya pande mbili hizo.

“Tunawapongeza waumini hawa wa Manzese kwa kuona umuhimu wa kuchimba kisima hicho ambacho kitasaidia kukabiliana na changamoto hiyo ya upatikanaji wa maji kwenye Kijiji hicho na vijiji jirani,” alisema Ridhiwani.

Alisema kuwa mbali ya changamoto hiyo pia wafugaji wanakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa majosho pamoja na madawa ya mifugo hali ambayo inasababisha vifo vya mifugo hiyo ambayo ni tegemeo kwa wafugaji katika kuendeshea maisha yao.

Akisoma risala kuhusiana na mradi huo mkaguzi wa mali za kanisa hilo William Gomera alisema kuwa mradi huo mara utakapokamilika utasaidia kupunguza tatizo la maji kwenye eneo hilo la kijiji hicho na umegharimu kiasi cha shilingi milioni 76 na ulianza mwaka 2009. Mradi huo mbali ya kujengwa na waumini hao pia mradi wa maendeleo wa umoja wa mataifa (UNDP) hapa nchini, Taasisi ya Third Millenium Peace Initiative Foundation (TMPIF), Renewable Energy Development Company of Tanzania Ltd (REDCOT)

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA KONGAMANO LA KIMATAIFA LA WANASAYANSI VIJANA JIJINI DAR LEO

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake ya ufunguzi wakati akifungua Kongamano la siku tatu la Kimataifa la Wanasayansi Vijana, linalojadili masuala mbalimbali yanayohusu Sekta ya Madini, linaloendelea kwenye Ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere, jijini Dar es Salaam, ambapo Tanzania imeteuliwa kuwa mwenyeji wa Kongamano hilo la tatu la Kimataifa la Mtandao wa Wanasayansi Vijana Duniani (YES). Aidha Kongamano hilo lililoshirikisha jumla ya wajumbe zaidi ya 300 kutoka ndani na nje ya nchi pia, litajadili usimamizi wa Rasilimali mbalimbali zikiwemo Mafuta na Gesi.
Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin William Mkapa, akizungumza katika Kongamano hilo kabla ya mgeni rasmi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo, akizungumza katika Kongamano hilo kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kufungua kongamano hilo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea zawadi ya sanamu la mnyama kutoka kwa Rais wa wa Mtandao wa Wanasayansi Vijana Duniani (YES), Meng Wang, baada ya kufungua rasmi Kongamano hilo, la siku tatu la Kimataifa la Wanasayansi Vijana, linalojadili masuala mbalimbali yanayohusu Sekta ya Madini, linaloendelea kwenye Ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere, jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo.
Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin William Mkapa, akipokea zawadi ya picha ya mnyama kutoka kwa Rais wa wa Mtandao wa Wanasayansi Vijana Duniani (YES), Meng Wang, wakati wa ufunguzi rasmi wa Kongamano hilo, la siku tatu la Kimataifa la Wanasayansi Vijana, linalojadili masuala mbalimbali yanayohusu Sekta ya Madini, linaloendelea kwenye Ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere, jijini Dar es Salaam. Katikati ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal (kushoto) ni Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi zawadi ya ramani ya Afrika, Rais wa wa Mtandao wa Wanasayansi Vijana Duniani (YES), Meng Wang, baada ya kufungua rasmi Kongamano hilo, la siku tatu la Kimataifa la Wanasayansi Vijana, linalojadili masuala mbalimbali yanayohusu Sekta ya Madini, linaloendelea kwenye Ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere, jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa Kongamano hilo, baada ya ufunguzi. Picha na OMR

Kampuni ya Mafuta na Gesi ya Swala yakaribishwa rasmi Soko la Hisa la Dar

$
0
0
Rais mstaafu wa awamu ya pili wa Jamhuri ya Muungano Tanzania Mh.Alhaj Ali HAssan Mwinyi akigonga kengele kuashiria kuingia rasmi kwa kampuni ya Mafuta na Gesi ya Swala kwenye Soko la Hisa la Dar es salaam.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Mafuta na Gesi ya Swala Bw. David Mestres akiongea na waandishi wa habari(hawapo pichani) wakati wa sherehe za kukaribishwa rasmi kwa kampuni ya Swala kwenye soko la Hisa la Dar Es Salaam.
Mwenyekiti wa Kampuni ya Mafuta na Gesi ya Swala Bw. Ernest Massawe akiongea na waandishi wa habari(hawapo pichani) wakati wa sherehe za kukaribishwa rasmi kwa kampuni ya Swala kwenye soko la Hisa la Dar Es Salaam.
Rais mstaafu wa awamu ya pili wa Jamhuri ya Muungano Tanzania Mh.Alhaji Ali HAssan Mwinyi akipozi kwenye picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Kampuni ya Mafuta na Gesi ya Swala Bw. Ernest Massawe(kushoto) na Mkurungenzi wa Swala Bw.Abdullah Mwinyi kwenye sherehe za kukaribishwa rasmi kampuni ya Swala kwenye soko la Hisa la Dar es salaam.
Mwenyekiti mtendaji wa makampuni ya IPP Dk. Reginald Mengi na Mh.Joseph Mungai wakimsikiliza Rais Mstaafu Mh.Alhaj Ali Hassan Mwinyi (hayupo pichani) wakati wa kukaribishwa kwa kampuni ya Swala kwenye Soko la Hisa la Dar es Salaam.

BBC yazindua studio zake nchini,kipindi cha asubuhi cha Amka na BBC kuruka moja kwa moja kutokea dar

$
0
0
Mkuu wa Habari wa BBC Idhaa ya Ulimwengu,Bi. Nikki Clarke akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Kituo cha kurushia Matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya BBC jijini Dar es Salaam,katika Jengo lao lililopo Mikocheni.Kushoto ni Mkuu wa Idhaa ya Kiswahili ya BBC, Ali Saleh.
Mkuu wa Idhaa ya Kiswahili ya BBC, Ali Saleh (wa tatu kulia) akiwapatia maelekezo Waziri Mkuu Mstaafu,Mh. Dkt. Salim Ahmed Salim na Mwenyekiti wa CUF,Prof. Ibrahim Lipumba ya namna Idhaa hiyo inavyoandaa vipindi yake na inavyopeleka hewani wakati wa hafla ya Uzinduzi rasmi wa Kituo cha kurushia Matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya BBC,jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Habari wa BBC Idhaa ya Ulimwengu,Bi. Nikki Clarke akibadilishana mawazo na aliewahi kuwa Mkuu wa Idhaa ya Kiswahili ya BBC,Bw. Tiddo Mhando wakati wa hafla hiyo.
Mkuu wa Idhaa ya Kiswahili ya BBC jijini Dar es Salaam,Hassan Mhelela (kushoto) akizungumza katika hafla hiyo pamoja na kuitambulisha timu yake.
Baadhi ya Wageni waalikwa wakiwa kwenye picha ya pamoja na Viongozi wakuu wa BBC waliokuwepo kwenye hafla hiyo,jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa zamani wa Idhaa ya Kiswahili ya BBC,Bw. Tiddo Mhando (kulia) akiwa katika mazungumzo na Mkuu wa Idhaa ya Kiswahili ya BBC,Bw. Ali Saleh pamoja na Mtangazaji Sussani Mongi.
Taswira za Studio za BBC jijini Dar.
Chumba cha Habari cha BBC jijini Dar.
Wadau Salim Kikeke na Nicolas wakipitia habari kabla ya kuipeleka hewani.












BBC Idhaa ya Ulimwengu, imezindua ofisi zake jijini Dar es Salaam. Ofisi za Dar es Salaam zina studio ambazo zinatumika kuandaa matangazo maarufu ya redio ya asubuhi, Amka na BBC, na pia kuendesha tovuti ya bbcswahili.com.

Katika kuadhimisha uzinduzi huo, vipindi vingine viwili vya BBC Idhaa ya Kiswahili, Dira ya Dunia ya redio na ya TV vitaandaliwa kutoka Dar es Salaam katika siku hiyo ya Jumatatu Agosti 11.

Ufunguzi wa ofisi za Dar es Salaam ni matokeo ya mikakati ya BBC Idhaa ya Ulimwengu ya kuhamisha uandaaji wa vipindi vya redio na tovuti kutoka London kwenda Afrika Mashariki.

Ofisi mpya ina vifaa vya kisasa vinavyoweza kutayarisha vipindi vya redio, TV na huduma za habari kwa njia ya simu za mkononi. Amka na BBC, kipindi cha nusu saa ambacho hutangazwa Jumatatu hadi Ijumaa humulika matukio na taarifa zitakazojiri katika siku, sasa kitaandaliwa Dar es Salaam na watayarishaji na watangazaji 15.

Ofisi mpya pia zina watayarishaji wanaoandaa taarifa mbalimbali za kanda ya Afrika Mashariki na Kati kwa ajili ya vipindi vya TV vya Focus on Africa na Dira ya Dunia. Mkuu wa Habari wa BBC Idhaa ya Ulimwengu Nikki Clarke amesema:

 "Uzinduzi wa ofisi zetu za Dar es Salaam ni hatua kubwa katika safari yetu iliyoanza muda mrefu kidogo, katika kuwapa wanachotaka wasikilizaji katika nchi zinazozungumza Kiswahili, na ambao husikiliza BBC wanapotaka kupata taarifa wanazoziamini na zenye uhakika. Takriban watu milioni 12.4 - ambao ni kama nusu ya idadi ya watu wazima nchini Tanzania, husikiliza matangazo ya redio ya BBC kila wiki.

Na sasa moja ya kipindi maarufu cha BBC, Amka na BBC, kimekuja karibu zaidi na wasikilizaji." Ofisi ya Dar es Salaam, ina studio mbili za redio ambazo zinaweza kutumika na hadi watu sita kwa wakati mmoja, na hivyo ni muafaka kabisa kwa kipindi kichangamfu cha Amka na BBC kwa ajili ya mijadala na mahojiano ya kuvutia.

Mkuu wa Idhaa ya Kiswahili ya BBC, Ali Saleh anasema : "Ofisi mpya zinatoa nafasi bora kabisa kwa watayarishaji wa BBC nchini Tanzania kuimarisha ukusanyaji wa habari na kutoa taarifa kutoka katika eneo la Afrika Mashariki na Kati.

Amka na BBC itakuwa na uwezo mkubwa zaidi kutoa taarifa na habari mchanganyiko, za Afrika Mashariki na pia za dunia, pamoja na mahojiano ya moja kwa moja na watu mbalimbali, lakini pia makala na habari za kijamii." Idhaa ya Kiswahili ya BBC imekuwa kitovu cha hatua ya BBC Idhaa ya Ulimwengu ya kuimarisha kuwepo kwake katika sekta ya habari barani Afrika.

Baada ya ufunguzi wa ofisi ya Nairobi mwaka 1998, BBC Idhaa ya Ulimwengu ilikuwa shirika la kwanza la habari la kimataifa kuwa na kituo cha uandaaji habari barani Afrika. Mwaka 2006 Amka na BBC ilihamishwa kutoka London kwenda Nairobi, na BBC Idhaa ya Ulimwengu, kwa mara nyingine tena ikawa shirika la kwanza la kimataifa la habari kuandaa na kutangaza vipindi kutoka barani Afrika. 

Katika hatua ya kuhamisha utayarisaji wa vipindi na taarifa za kwenye tovuti, kipindi maarufu cha jioni cha redio, Dira ya Dunia sasa kinatayarishwa Nairobi. Mwisho// Kwa taarifa zaidi wasiliana na afisa wa idara ya mawasiliano ya BBC Idhaa ya Ulimwengu - Lala Najafova, lala.najafova@bbc.co.uk.

Kwa wahariri: BBC Idhaa ya Ulimwengu ni shirika la utangazaji la kimataifa lenye idhaa nyingi za lugha mbalimbali zinazotoa huduma ya matangazo ya redio, TV, kwenye mtandao wa internet na pia simu za mkononi. BBC Idhaa ya Ulimwengu hutumia njia mbalimbali kuwafikia wasikilizaji wake wapatao milioni 191 duniani kote. BBC huwafikia watu milioni 265 duniani kote kila wiki kwa huduma zake kutoka BBC Idhaa ya Ulimwengu, BBC News TV na bbc.com.

MAGUFULI AKAGUA BARABARA YA MWENGE-TEGETA, MRADI WA MABASI YAENDAYO HARAKA (BRT) PAMOJA MIRADI YA UJENZI WA BARABARA ZA JUU TAZARA FLYOVER NA MAKUTANO YA BARABARA ZA JUU UBUNGO JIJINI DAR

$
0
0
Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli katikati akiwa na Balozi wa Japan Nchini Masaki Okada kulia wakipita juu ya Daraja la Lugalo mara baada ya kulikagua katika ziara ya Ukaguzi wa Barabara ya Mwenge Tegeta jijini Dar es salaam leo.
 Balozi wa Japan nchini Ndugu Masaki Okada akiwa na Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa Said Meck Sadick wakipanda ngazi za daraja la juu la watembea kwa miguu flyover Ubungo katika ukaguzi wa Barabara za kupunguza Msongamano (BRT) Ubungo jijini Dar es Salaam
 Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikagua ujenzi wa kituo cha Mradi wa Mabasi yaendayo haraka (BRT) Morocco jijini Dar Es Salaam
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Mhandisi Mussa Iyombe wakwanza kulia akiwa pamoja na Waziri wa Ujenzi Dkt.John Pombe Magufuli wakikagua moja ya madaraja makubwa katika barabara ya Mwenge-Tegeta jijini Dar es Salaam
 Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akitoka kukagua daraja katika barabara ya Mwenge - Tegeta ambayo ujenzi wake umeshakamilika.
 Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini TANROADS Mhandisi Patrick Mfugale aliyenyoosha mkono akitoa maelezo ya mradi wa ujenzi wa Barabara ya Mwenge-Tegeta ambao umekamilika.
 Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli kushoto akizungumza na Balozi wa Japan Nchini Masaki Okada wakati wa Ukaguzi wa Barabara za Kupunguza msongamano katika eneo la manzese jijini Dar es Salaam
 Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa Said Meck Sadick , Balozi wa Japan Masaki Okada pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Mhandisi Mussa Iyombe wakisikiliza kwa makini maendeleo ya mradi huo.
Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli katikati akipita juu ya daraja la waenda kwa miguu katika eneo la Ubungo jijini Dar es Salaam

MAMA SHUJAA WA CHAKULA 2014 AKABIDHIWA ZAWADI YAKE WILAYANI UKEREWE MWANZA

$
0
0
Mshindi wa Maisha Plus/Mama shujaa wa chakula msimu wa tatu 2014 Bahati Jacob Muriga jana alikabidhiwa zawadi nyumbani kwake  Ukerewe. Zawadi hizo ni vifaa vya kilimo vyenye thamani ya shilingi milioni 20 ambapo Bahati Muriga alichagua kununua shamba lenye ukubwa wa ekari 7, pikipiki yenye miguu mitatu aina ya TOYO, vifaa vya kulimo kama vile mbegu, mbolea, mipira ya kumwagilia, watering cane, water pump, spray pump, koleo na dawa za kuondoa wadudu na ukungu, majembe, mundu, engine oil lita 2  na petroli lita 96.

Shindano la Maisha Plus/Mama Shujaa wa Chakula 2014 lilifikia tamati mnamo  tar. 18 May, 2014 ambapo Bahati Jacob Muriga ndiye  aliyeibuka kidedea  wa shindano hilo. Mama shujaa huyu ni mkulima kutoka Nansio, Ukerewe mkoa wa Mwanza na pia ni mwalimu mkuu shule ya Msingi Mhozya. Ni mjane mwenye watoto watatu na hutumia kilimo kama nguzo ya kuhakikisha mahitaji ya kifamilia yanatimizwa.

Hafla fupi ya kumkabidhi zawadi zake Bahati zilifanyika katika Ukumbi wa Afro Beach ambapo watu na wawakilishi mbali mbali kutoka serikalini na mashirika yasiyo ya kiserikali kama vile Kivulini, EMEDO walihudhuria ili  kushuhudia jinsi anavyokabidhiwa zawadi. 

Bw. Kombo, akimuwakilisha mkuu wa wilaya ya Ukerewe alionesha furaha yake kwa mama shujaa kutoka Ukerewe alisema” Ninayo furaha kubwa na kama kiongozi kijana kuona wilaya yetu imetoa mshindi wa shindano kubwa kama hili na kuiweka ukerewe katika historia na  ramani ya nchi kuwa, kumbe nasi tunaweza, najisikia furaha pia kwa ushindi huu kwani toka anaanza huu mchakato wa kuchukua fomu na kuelekea kijiji cha maisha plus nilikua miongoni mwa niliotoa ushirikiano mkubwa kwa kutoa  ruhusa na araka zangu za yeye kushiriki katika shindano hili kwani ni mwalimu huyu”

 
Mama Shujaa wa Chakula 2014  Bahati Muriga akitoa neno la Shukurani Baada ya Kukabidhiwa zawadi rasmi zawadi zake Wilayani kwake Ukerewe
Eluka Kibona kutoka Oxfam akimkabidhi ufunguo wa Pikipiki Mshindi wa Mama shujaa wa Chakula
 Mama Shujaa wa Chakula 2014 Bahati Muriga akisaini kupokea zawadi zake kutoka OXFAM kupitia Programu ya GROW, Wekeza kwa wakulima wadogo wadogo Inalipa.
Bwana Hamis Kombo muwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe akitoa salamu za pongezi kwa Mama Shujaa wa Chakula 2014 pia kuwashukuru OXFAM kwa kutoa zawadi hizo.
Bahati Muriga akijaribisha kuiwasha Pikipiki yake Mara baada ya Kukabidhiwa
 Bahati Muriga akifurahia zawadi zake

 Kulwa Kizenga wa kwanza kushoto  na Eluka Kibona kutoka OXFAM  wakimkabidhi zawadi Bahati Muriga
 Mkamiti Mgawe wa kwanza kushoto kutoka OXFAM akiwa na Mama shujaa wa Chakulaa
Zawadi alizopokea Mama Shujaa wa Chakula.

BENKI YA CRDB YAZINDUA HUDUMA YA INDIA DESK

$
0
0
Balozi wa India, Shri Debnath Shaw (wa tatu kulia), Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRD, Dk. Charles Kimei (wa pili kushoto), wakizindua kwa pamoja huduma mpya ya India Desk  inayowaunganisha wawekezaji na wafanyabiashara nchini India kufanya huduma za kibenki bila ya kuwa na akaunti nchini. Wa pili kulia ni Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo anayeshughulika na Uendeshaji na Huduma kwa Wateja, Saugata Bandyadhiyay, mjumbe wa bodi ya Wakurugenzi, Ally Laay (kushoto), Celina Mkonyi (kulia). Uzinduzi huo ulifanyika jijini Dar es Salaam.
Balozi wa India, Shri Debnath Shaw (wa tatu kulia), Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRD, Dk. Charles Kimei (wa pili kushoto), Wa pili kulia ni Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo anayeshughulika na Uendeshaji na Huduma kwa Wateja, Saugata Bandyadhiyay, mjumbe wa bodi ya Wakurugenzi, Ally Laay (kushoto), Celina Mkonyi (kulia).
Balozi wa India, Shri Debnath Shaw (wa tatu kulia), Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRD, Dk. Charles Kimei (wa pili kushoto), Wa pili kulia ni Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo anayeshughulika na Uendeshaji na Huduma kwa Wateja, Saugata Bandyadhiyay wakiwa na furaha baada ya kuzindua huduma hiyo.
Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo anayeshughulika na Uendeshaji na Huduma kwa Wateja, Saugata Bandyadhiyay akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma India Desk inayotolewa na Benki ya CRDB.

Wadau wa Benki ya CRDB.

Wadau mbalimbali wa Benki ya CRDB.
 Mkurugenzi wa Masoko Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa (katikati) akiwa na maofisa wa Benki hiyo wakati wa hafla ya uzinduzi wa huduma ya India Deski.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dk. Charles Kimei akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma ya India Deski uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wageni waalikwa wakiwa katika uzinduzi mpya ya India Desk inayotolewa na Benki ya CRDB.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei (kulia) na  Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo anayeshughulika na Uendeshaji na Huduma kwa Wateja, Saugata Bandyadhiyay (kushoto) wakisakata rhumba wakati wa hafla hiyo.


FLAVIANA MATATA FOUNDATION NA PSPF WAKABIDHI VIFAA VYA SHULE LINDI

$
0
0
Mwanamitondo afanyae kazi zake za mitindo nchini Marekani Flaviana Matata, yuko nchini kwa ajili ya kufanya kazi za kijamii kupitia taasisi yake ya Flaviana Matata Foundation. katika mradi wa Back to school project /FMFstationarykit ambao unafadhiliwa na mfuko wa penseni PSPF.

Baada ya mwezi January Flaviana kugawa vifaa shule za msingi za jijini awamu hii ameenda Mtwara na kufanikiwa kugawa shule za Msingi Mtua na Chemchem ziliyopo Nachingwea pamoja nashule za msingi Litingi na Mnengulo ziliyopo Lindi.

bado wanaendelea kugawa vifaa hivyo kwa shule za msingi mikoa mingine "hadi sasa tumeshagawa vifaa kwa watoto 700 na bado kuna kits 800 vitasambazwa Tunduma ,Tunduru na Monduli"
Flaviana alitoa shukran kwa PSPF kwa kudhamini huu mradi na akasisitiza makampuni na mashirika kujaribu kuwezesha elimu kama hali halisi inavyoonekana kwenye picha hadi leo kuna wanafunzi wanasoma chini na mti, na walio madarasani,madarasa ni mabovu na hayana madawati.
2G2A8088 Flaviana Matata ameongozana na Meneja wa Mawasiliano, Masoko na Uenezi wa PSPF, Costantina Martin pamoja na wafanyakazi wa PSPF katika zoezi la kukabidhi vifaa hivyo. Martin2G2A81562G2A81742G2A8196
2G2A82342G2A82482G2A82792G2A8299IMG-20140811-WA0044IMG-20140811-WA0023IMG-20140811-WA0029

SERIKALI WILAYANI NGORONGORO YATAKIWA KUTOA USHIRIKIANO KWA REDIO ZA KIJAMII

$
0
0
DSC_0010
Mkuu wa wilaya ya Ngorongoro, Elias Wawa Lali akiwakaribisha wadau wa maendeleo ofisini kwake Loliondo walioongozwa na Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph (wa tatu kushoto) aliyefuatana na Meneja Mauzo wa Kampuni a Samsung tawi la Tanzania , Bw. Slyvester Nteere (wa pili kushoto) pamoja na mwakilishi wa Ubalozi wa Uswiss nchini, Bw. Eric Kalunga (kushoto) wakiwa na mwenyeji wao Diwani wa kata ya Ololosokwani, Yannick Ndoinyo (kushoto kwa DC).

Na Mwandishi wetu, Ngorongoro

Serikali na halmashauri wilayani Ngorongoro zimetakiwa kutoa ushirikiano kwa redio za kijamii wilayani humo kwa lengo la kuwaletea maendeleo ya haraka wananchi wao.

Hayo yameelezwa na Meneja wa redio ya kijamii ya Loliondo FM, Joseph Munga, wakati wa ziara ya kukagua miradi inayoendeshwa na Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) redio hiyo ikiwa miongoni mwa miradi inayofadhiliwa na UNESCO wilayani hapa wakiambatana na wadau wa maendeleo kutoka kampuni ya Samsung na Ubalozi wa Uswiss hapa nchini.

‘Redio za Jamii ndio chombo pekee kinachoziunganisha serikali na jamii katika suala zima la kujiletea maendeleo’ alisema Joseph Munga.
DSC_0019
Mkuu wa wilaya ya Ngorongoro, Elias Wawa Lali akiwa kwenye mazungumzo na wadau wa maendeleo waliofika wilayani humo kukagua miradi ya maendeleo inayofadhiliwa na Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO).

Munga aliongeza kwa kusema kuwa redio hiyo iliyoanza kurusha matangazo mwezi Oktoba 2013 imekuwa ni kichocheo cha kutoa taarifa mbali mbali kwa jamii wilayani Loliondo na kuibua changamoto mbalimbali zinazoikabili jamii huku akiitaka serikali na halmashauri wilayani humo kuisaidia katika kufikia malengo ya kuitumikia jamii na kuwashukuru wadau mbali mbali wanaoiwezesha redio hiyo ikiwemo kampuni ya simu za mkononi ya Airtel ambayo imetoa mnara wao kurushia Matangazo ya redio Loliondo.

“Suala hapa ni ushirikiano hasa kwa halmashauri kuelewa na kuona umuhimu wa kutumia redio hii katika matukio mbali mbali yanayofanyika kwenye halmshauri vikiwemo vikao vya baraza la madiwani ili wananchi walioshindwa kufika waweze kujua baraza lao limepitisha nini sanjari na huduma kwenye sekta za afya na elimu”, alisema Munga.

Redio Loliondo ni miongoni mwa miradi inayofadhiliwa na UNESCO wilayani humo kupitia asasi isiyokuwa ya kiserikali ya RAMAT kwa kufadhili miradi ya Maktaba,kutoa elimu kwa jamii ya kifugaji yenye malengo ya kuinua uelewa na ufahamu kwa jamii hizo zilizopo pembezoni hasa katika suala zima la kujiletea maendeleo.
 
DSC_0049
Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph (kushoto) ambaye pia ndio mkuu wa msafara huo akifafanua jambo mbele ya Mkuu wa wilaya ya Ngorongoro, Elias Wawa Lali wakati wa mazungumzo hayo. Kulia ni Meneja Mauzo wa Kampuni a Samsung tawi la Tanzania, Bw. Slyvester Nteere.
Nae Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph, alisema kuwa misingi ya redio hiyo inalenga kuikomboa jamii ya Loliondo kwa kutoa elimu ya kifugaji na elimu kwa wananchi wilayani humo ambao hapo awali hawakupata fursa ya kupata taarifa na matukio mbalimbali yanayoendelea wilayani humo.
Akifafanua faida za redio hiyo kwa jamii ni kupata taarifa mbali mbali zinazoendana na shughuli zao za ufugaji hususan taarifa za chanjo ya mifugo na madawa na kupata taarifa nyingine kuhusiana na masuala mbali mbali ya kijamii ndani na nje ya wilaya hiyo ambayo hapo awali yalikuwa vigumu kupatikana kwa wakati kutokana na jiografia ya wilaya hiyo.
“Pamoja na kwamba malengo ya mradi huu yameanza kuonekana dhahiri machoni petu,wafadhili kutoka UNESCO pamoja na kampuni ya simu za mikononi ya Airtel ambayo mnara wake umekuwa ukitumika kurusha matangazo ya redio hii, tunataka kuhakikisha kwamba mnaweza kujiendesha wenyewe hapo baadae ili mradi kama huu uweze kuwanufaisha na wenzenu sehemu zingine”, alisema Al Amin.
DSC_0156 Diwani wa kata ya Ololosokwani ambaye pia ni Mkurugenzi wa Shirika lisiolo la kiserikali la RAMAT, Bw. Yannick Ndoinyo akitoa maelezo juu mradi waliobuni wa kituo cha utamaduni wa Kimasai ambao uko mbioni kuanza ujenzi wake wakati wa ziara ya UNESCO kukagua miradi mbalimbali inayofadhiliwa na shirika hilo.
Akizungumzia miradi inayoletwa na wafadhili wilayani humo Mkuu wa wilaya ya Ngorongoro, Elias Wawa Lali alisema kuwa imechangia kwa kiasi kikubwa kuwahamasisha vijana ambao wana shauku ya kuishi mijini kurudi nyumbani na kuendeleza jamii hali ambayo imetafsiriwa kutoa uelewa kwa wanajamii na hivyo ni faraja kubwa kwa wananchi wilayani Loliondo.
Ameyataka mashirika na taasisi za kiserikali na zisizo za kiserikali kuingalia Ngorongoro kwa ukaribu na kuwa wadau wazuri wa kuiletea maendeleo wilaya hiyo kwani miradi iliyopo itachochea ukuaji wa uchumi na kusaidia uelewa wa wakazi wilayani Loliondo katika dhana nzima ya kujileta maendeleo na kukuza uelewa wa wananchi wa kupata taarifa mbalimbali kwa wakati.
DSC_0179 
Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph (wa pili lulia) akitoa ushauri kuhusu kituo hicho kuwa kitakuwa na manufaa ya kiuchumi kwa jamii hiyo ya kifugaji pindi kitapokamilika huku akisisitiza kuwa mipango iliyopangwa kama walivyopewa maelezo iendane na wakati.
DSC_0310
Mmoja wa wadau wa maendeleo kutoka Ubalozi wa Uswiss nchini, Bw. Erick Kalunga akisoma moja ya vitabu ndani ya maktaba hiyo inayofadhiliwa na UNESCO, Maktaba hiyo inayotumiwa na wanafunzi wa shule ya sekondari Ololosokwani na vijana wa kata hiyo.
DSC_0361
Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph (kulia) ambaye pia ni mkuu wa msafara huo wa kukagua miradi inayofadhiliwa na UNESCO akiteta jambo na Meneja Mauzo wa Samsung tawi la Tanzania, Bw. Sylvester Nteere ndani ya maktaba hiyo. Anayefuatilia mazungumzo hayo kwa karibu ni Afisa Mradi wa uchumi wa kijani ndani ya hifadhi hai (GEBR) Kitengo cha Sayansi kutoka UNESCO na mwakilishi wa KOICA, Myoung Su Ko (katikati).
DSC_0294
Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph (wa pili kulia) akitoa maelezo baada ya kutembelea Maktaba inayofadhiliwa na UNESCO nje ya maktaba hiyo.
DSC_0392
Kikundi cha ngoma ya Kimasai kilichowatumbuiza wageni waliotembelea mradi wa redio ya Loliondo FM inayofadhiliwa na UNESCO wakitumbuiza wakati wa ziara hiyo.
DSC_0412
Afisa Miradi wa kitengo cha Sayansi kutoka UNESCO, Myoung Su Ko, akijumuika na kinamama wa kikundi cha ngoma za kimasai kutoka kata ya Ololosokwani wilayani Ngorongoro mkoani Arusha.
DSC_0432
Diwani wa kata ya Ololosokwani ambaye pia ni Mkurugenzi wa Shirika lisiolo la kiserikali la RAMAT inayomiliki Redio Loliondo FM, Bw. Yannick Ndoinyo akitoa maelezo kuhusu maendeleo ya miradi mbalimbali ikiwemo maktaba, redio na ugawaji wa vitabu vya masomo ya Sayansi na hesabu vinavyoafadhiliwa na UNESCO kwenye kata hiyo.
DSC_0441
Meneja Mauzo wa Samsung tawi la Tanzania, Bw. Sylvester Nteere akitoa pongezi kwa redio Loliondo FM kwa kuweza kuihamasisha jamii inayoizunguka kwa kuburudisha, kutoa elimu na habari kwa ujumla hiyo sio kazi nyepesi kutokana na uchanga wenu wa redio yenu.
DSC_0476
Meneja Mauzo wa Samsung tawi la Tanzania, Bw. Sylvester Nteere akikabidhi zawadi kwa kikundi cha ngoma cha kinamama wakati wa ziara hiyo ya ukaguzi wa miradi inayofadhiliwa na UNESCO kwenye kata ya Ololosokwani.
DSC_0478
Wanakikundi cha ngoma na wakazi wa kata ya Ololosokwani wakiangalia taarifa mbalimbali za mitandao kwenye “Tablet” inayotengenezwa na kampuni ya Samsung wakati wa ziara hiyo.
DSC_0488
Mmoja wa wanakikundi akitumia Tablet kupiga picha wanakikundi wenzake pamoja na wadau wa maendeleo (hawapo pichani).
DSC_0509
Wanakikundi cha ngoma za kimasai wakiwa kwenye picha ya pamoja na ugeni huo huku wakionyesha furaha baada ya kupokea zawadi ya fulana kutoka kampuni ya Samsung.
IMG-20140807-WA0024
Meneja wa redio jamii ya Loliondo FM, Joseph Munga akiwa kwenye studio za redio hiyo wakati wa ziara ya UNESCO kukagua miradi inayoifadhili.
DSC_0516
Meneja mauzo wa Samsung tawi la Tanzania, Bw. Sylvester Nteere (aliyeketi) akiwa na Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph ndani ya studio za kurushia matangazo za redio ya Loliondo FM inayorusha matangazo yake kwenye mnara wa Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel na kuifika jamii kubwa kwenye maeneo hayo.

OMO FASTACTION YAZINDULIWA RASMI LEO JIJINI DAR

$
0
0
 Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mama Asha Bilal akitoa hotuba yake wakati alipokuwa Mgeni Rasmi kwenye hafla ya Uzinduzi wa Sabuni ya kufulia ya OMO FastAction uliofanyika rasmi leo kwenye hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam.
Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Unilever kwa Afrika Mashariki,Marc Engel akitoa hotuba yake wakati wa hafla ya Uzinduzi wa Sabuni ya kufulia ya OMO FastAction uliofanyika rasmi leo kwenye hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam.
Meneja Masoko na Huduma kwa Wateja wa Kampuni ya Unilever Tanzania,Teresia Kamweru akitoa shukrani zake kwa Mgeni Rasmi na Wadau mbali mbai walioshiriki kwenye hafla hiyo ya Uzinduzi wa Sabuni ya kufulia ya OMO FastAction uliofanyika rasmi leo kwenye hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam.
Meya wa Manispaa ya Ilala,Jerry Silaa akizungumza machache wakati akimkaribisha mgeni rasmi kuja kuzindua Sabuni ya kufulia ya OMO FastAction uliofanyika rasmi leo kwenye hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam.
Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mama Asha Bilal akipokea zawadi ya picha ya mchoro kutoka kwa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Unilever kwa Afrika Mashariki,Marc Engel mara baada ya Uzinduzi wa Sabuni ya kufulia ya OMO FastAction uliofanyika rasmi leo kwenye hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam.  
MC Taji Liundi a.k.a Master T akiongoza hafla hiyo.
Warembo wakiwa na mfano wa Sabuni ya OMO FastAction wakati wa Uzinduzi wa Sabuni ya kufulia ya OMO FastAction uliofanyika rasmi leo kwenye hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam.
Meza Kuu.
Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Unilever kwa Afrika Mashariki,Marc Engel akiteta jambo na Meneja Masoko na Huduma kwa Wateja wa Kampuni ya Unilever Tanzania,Teresia Kamweru .
Mtaalam wa Bidhaa kutoka Kampuni ya Unilever,Gideon Rono (wa pili kulia) akifanya Demo ya Sabauni hiyo ya OMO FastAction wakati wa Uzinduzi wake uliofanyika rasmi leo kwenye hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Kampuni ya Unilever Tanzania wakiwa kwenye hafla hiyo.
kikundi cha Ngoma cha Safi Kidds Dancers kikitoa burudani.
Mama OMO akiwa na mwanae aliechafuka kupindukia.

Baadhi ya Kinamama kutoka vikundi mbali waliohudhulia hafla hiyo.

WAPAKISTANI WALIOKAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA WATOROKA NCHINI

$
0
0
Mtuhumiwa Abdul Ghan Peer Bux.

 Imeelezwa kwamba Wapakistani wawili, Abdul Ghan Peer Bux na Shahbaz Malk (pichani) waliokamatwa  wakiwa  na  Watanzania  wanaotuhumiwa kwa kukutwa  na  madawa ya kulevya wametoroka nchini. 

Watuhumiwa hao walikamatwa Februari 21, 2011wakiwa na madawa ya kulevya yenye thamani ya  shilingi  bilioni 6.2,  Mbezi Beach  maeneo ya  Jogoo  jijini Dar sa Salaam.Habari za uchunguzi ndani ya Mahakama Kuu zinasema kuwa, Jaji Grace Mwakipesile anayesikiliza kesi  hiyo  inayotarajiwa kuendelea kusikilizwa kesho Jumatano, ametoa amri ya kukamatwa  kwa  watuhumiwa  hao. 
Kesi hiyo ambayo ilisikilizwa mahakamani hapo Julai 4, mwaka huu ilidaiwa kuwa Wapakistani hao walikamatwa  na  kikosi  kazi  cha  kuzuia na kupambana na madawa  ya kulevya kisha kudhaminiwa lakini wametoweka bila kuhudhuria mahakamani hata siku moja.

Mtuhumiwa Shahbaz Malk. 

Imeelezwa kuwa, baada ya watuhumiwa hao kudhaminiwa na wadhimini wawili, Julai 4, mwaka mahakama iliambiwa kuwa wadhamini hao wamefariki dunia. Hata hivyo, jaji anayesikiliza kesi hiyo aliwaagiza ndugu waliotoa taarifa hiyo kupeleka cheti halisi cha kifo kesho na watuhumiwa wahudhurie mahakamani  hapo.
Madawa ya kulevya yaliyokamatwa na watuhumiwa
 hao yenye thamani ya  shilingi  bilioni 6.2.

Watanzania waliokamatwa na Wapakistani hao waliachiwa huru baada ya kulipa dhamana ya shilingi 10,000,000 ambapo wadhamini wao ni Raza Hussein Kanji ambaye alipewa stakabadhi namba 3406367 na Nazar Mohamed Nurd alikatiwa yenye namba 3406355.
Kamanda wa Kupambana na Kudhibiti 
Madawa ya Kulevya nchini, Godfrey Nzowa.

 Februari 21, 2011 polisi chini ya kamanda wao, Godfrey Nzowa waliwakamata Wapakistani hao wakiwa na Watanzania wawili, William Chonde na Kambi Zuberi ambao wapo nje kwa dhamana wakituhumiwa kukutwa na madawa ya kulevya yenye thamani ya shilingi bilioni 6.2.

Airtel yazindua huduma mpya ya mitindo kwa njia ya simu kwa kushirikiana na Mbunifu Mahiri Afrika Mustafa hassanali

$
0
0
Kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel inayotoa huduma nafuu na yenye wigo mpana zaidi wa mawasiliano, imeshirikiana na mbunifu wa mitindo Afrika ,Mustafa Hasanali katika kusheherekea miaka 15 ya mafanikio yake makubwa katika sekta ya mitindo.

 Mustafa Hassanali amefanya maonyesho katika miji 27 katika nchi 18, na kugusa maisha ya watu mbali mbali  kwa njia tofauti. Na anaendelea kuwa maarufu katika sekta ya mitindo nchini na Afrika kwa ujumla.

Ushirikiano huo kati ya Airtel na Guru wa mitindo  Tanzania na nje ya Tanzania, utawezesha wateja wa Airtel na washabiki wa mitindo kuwa karibu  zaidi na ulimwengu wa mitindo kwa kupata habari mbali mbali na za kisasa kupitia simu zao za mikononi.

Akiongea kuhusu muungano huo Mkurugenzi wa huduma kwa wateja wa Airtel Tanzania Adriana Lyamba, alisema “mitindo ni moja kati ya vipengele muhimu katika maisha yetu, zikiwemo nguo, vifaa na vyombo mbalimbali. 
Kila mtu anataka kupendeza na kujihusisha na mitindo ya kisasa.

 Ila , hivi sasa upatikanaji wa habari na huduma za mitindo ni mgumu sana. Hivyo Airtel tumekuwa wa kwanza katika kuwapatia wananchi huduma hii kupitia simu zao za mkononi itakayowasaidia kupata habari mbali mbali za mitindo kwa ujumla . Huduma hii inajulikana kwa jina la “Airtel Fasheni”. 

Tunaamini kuwa , huduma hii itawasaidia wateja wetu wote ambao wangependa kupata habari mbali mbali na kuwafikia wabunifu wa mitindo ili kupata ushauri na pia kununua bidhaa zao.”

Mustafa Hassanali, mbunifu mitindo mahiri Afrika alisema , “ Airtel fasheni ni huduma ya kipekee ambayo wateja wa Airtel wanaweza kuipata mahali popote na wakatii wowote kwa kupiga *148*82#. Huduma hii ni Tsh.90 kwa siku.”
Mbunifu nguli wa mitindo Afrika, Mustafa Hassanali akizungumza na wageni waalikwa kuhusiana na huduma mpya ya kuwa karibu naye kwa mashabiki wa mitindo kupata taarifa zake kupitia simu zao za  mkononi za Airtel  kwa kupiga *148*82# na moja kwa moja utakuwa umeunganishwa na huduma hiyo na kutozwa shilingi 90 za kitanzania kwa siku.

MWANALIBENEKE DOTTO KAHINDI NA ELIZABETH NGUMA WAMEREMETA

$
0
0
Baada ya kuwa marafiki kwa zaidi ya miaka minane Dotto Paul Kahindi (Mandolin) na Elizabeth Riziki Morris Nguma, Agosti 9, 2014 Mungu amewajalia kufunga pingu za maisha kwenye kanisa la Katoliki Parokia ya Mt. Francis wa Assis, mjini Biharamulo, Kagera.
Dotto Paul Kahindi (Mandolin) na mkewe Elizabeth Morris Nguma katika pozi muda mfupi baada ya kufunga ndoa kwenye Kanisa Katoliki Parokia ya Mt. Francis wa Asis, Biharamulo, Kagera.
Mr&Mrs Dotto na wapambe wao Mr&Mrs Frank katika pozi muda mfupi baada ya kufunga ndoa kwenye Kanisa Katoliki Parokia ya Mt. Francis wa Asis, Biharamulo, Kagera.
Bibi Harusi akiwa na mpambe wake katika pozi muda mfupi baada ya kufunga ndoa kwenye Kanisa Katoliki Parokia ya Mt. Francis wa Asis, Biharamulo, Kagera
Mr&Mrs Dotto, wapambe wao Mr&Mrs Frank, pamoja na wasimamizi wa ndoa hiyo Mr&Mrs Wema Rusasa katika pozi muda mfupi baada ya kufunga ndoa kwenye Kanisa Katoliki Parokia ya Mt. Francis wa Asis, Biharamulo, Kagera
Bibi Harusi na Mameid
Mr&Mrs Dotto (Mandolin) na wapambe wao Mr&Mrs Frank katika picha ya pamoja na wazazi wa pande zote mbili

Maharusi wakiwa na wapambe wengine
Bwana harusi ni Baunsa sana tu
Mr&Mrs Dotto Paul (katikati) wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya ndugu zao, kutoka kulia ni Mdogo wa bwana harusi Samweli, Kaka wa bibi harusi Deogratius, kaka wa bwana harusi Peter Kulwa na kaka wa bibi harusi Raygan
Bwana Harusi Dotto Paul na Bibi Harusi Elizabeth Riziki wakila kiapo wakati wa misa ya ndoa iliyofanyika kwenye Kanisa Katoliki Parokia ya Mt. Francis wa Asis, Biharamulo, Kagera
Tumepokea vyeti

Mr&Mrs Dotto Paul wanameremeta
Mr&Mrs Dotto Paul katika picha ya pamoja na kamati ya harusi yao iliyofanyika kwenye ukumbi wa Rest mjini, Biharamulo, Kagera
Utambulisho
Wakati wa chakula
Mama wa bwana harusi Mary Charles Kahindi

Wakati wa zawadi

Waliopata Ufadhili wa masomo China waagwa

$
0
0
Serikali ya China kupitia Wizara ya Nishati na Madini imetoa ufadhili wa nafasi kumi (10) za masomo kwa watanzania katika ngazi ya shahada ya uzamili na uzamivu katika fani ya mafuta na gesi.

Katika shahada ya uzamili wamechaguliwa watanzania 9 kati ya 46 walioomba ufadhili ambapo katika shahada ya uzamivu amechaguliwa mtanzania mmoja kati ya wanne waliowasilisha maombi.

Msaada huu wa masomo umetolewa na Serikali ya China kwa Tanzania kufuatia juhudi za Wizara ya Nishati na Madini kuhakikisha kuwa Serikali inakuwa na rasilimaliwatu ya kutosha katika kusimamia Sekta za Nishati na Madini hasa sekta ndogo ya mafuta na gesi inayokua kwa kasi hapa nchini.

Ufadhili huu ni wa pili kupitia Wizara ya Nishati na Madini ambapo wa kwanza ulitolewa katika mwaka wa fedha 2013/14 kwa nafasi 10 katika ngazi ya shahada ya uzamili kwenye fani za nishati na madini ikiwemo uhandisi migodi, uhandisi wa nishati katika mafuta na gesi. Wanafunzi hao wanatarajia kuingia mwaka wa pili wa masomo mwezi septemba, 2014.

Nafasi hizi zimepatikana kwa ushindani baada ya kutangazwa kwenye vyombo vya habari ambapo vigezo vilivyotumika kupata ufadhili ni aina ya kozi aliyoisoma mwombaji katika Shahada ya kwanza au Uzamili, Chuo alichosoma shahada ya kwanza, kiwango cha ufaulu katika shahada ya kwanza kuanzia GPA 3.0 na Uwiano wa jinsia.

Faida ambazo Tanzania itapata kutokana na ufadhili huu ni kuongeza wataalam katika fani za sekta za nishati na madini na hasa sekta ndogo ya mafuta na gesi, kuongeza fursa za masomo kwa watanzania hasa kwa kuzingatia kuwa wengi hukosa elimu kutokana na kutomudu gharama, na kuzidi kuimarisha ushirikiano kati ya Serikali ya Tanzania na China.
Watanzania waliopata ufadhili wa masomo nchini China katika ngazi ya shahada ya uzamili na uzamivu katika fani ya mafuta na gesi wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (katikati) na Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi (wa nne kutoka kushoto mstari wa nyuma) pamoja na watendaji wengine wa Wizara ya Nishati na Madini mara baada ya kuagwa rasmi katika Makao Makuu ya Wizara ya Nishati na Madini.Wengine katika picha (mstari wa mbele) ni Kamishna Msadizi Nishati anayeshughulikia Umeme, Eng.Innocent Luoga (wa kwanza kulia), Kamishna wa Madini, Eng.Paul Masanja (wa pili kulia), Kaimu Mkurugenzi Utawala - Bi. Caroline Musika (wa kwanza kushoto).
Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi (wa tano kutoka kushoto waliosimama), akiwatambulisha wanafunzi waliopata ufadhili wa masomo nchini China (baadhi hawapo pichani) waliofika Makao Makuu ya Wizara ya Nishati na Madini na kukabidhiwa nyaraka zitakazowawezesha kujiunga na masomo nchini China.Wanaowatazama wanafunzi hao ni Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (katikati), Kaimu Mkurugenzi Idara ya Utawala na Rasilimali Watu, Caroline Musika (wa kwanza kushoto, waliokaa), Mkurugenzi Msaidizi-Rasilimali Watu, Lusius Mwenda (wa kwanza kulia),Kaimu Kamishna Msaidizi,Maendeleo ya Nishati, Eng. Juma Mkobya (wa pili kutoka kulia), Kamishna wa Madini, Eng. Paul Masanja (kushoto kwa Mhe.Waziri).Wengine katika picha ni watumishi kutoka Wizara ya Nishati na Madini na waandishi wa habari.
Bi. Erasma Rutachura, ambaye amepata ufadhili wa masomo nchini China,ngazi ya shahada ya uzamivu katika mafuta na gesi akipokea nyaraka zitakazomwezesha kujiunga na masomo yake mwaka huu.Anayempa nyaraka hizo ni Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (wa pili kutoka kulia).Wa kwanza kulia ni Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi.
Mmoja kati ya wanafunzi 10 waliopata ufadhili wa masomo nchini China katika ngazi ya shahada ya uzamili, fani ya mafuta na gesi, Faustine Matiku akipokea nyaraka mbalimbali zitakazomwezesha kujiunga na Chuo Kikuu cha Hohai cha nchini humo.Wanaomtazama ni Waandishi wa Habari.

NSSF YAPELEKA VETERANI TANGA

$
0
0
Mshambuliaji wa timu ya Kombaini ya Tanga, Kassim Jumaa (kushoto), akitafuta mbinu za kumtoka mchezaji wa Survey veterani, Ahmad Rasuli (katikati), wakati wa mchezo maalum wa kusherehekea Sikukuu ya Wakulima Nanenane uliofanyika kwenye viwanja vya Disuza mjini Tanga. Mchezo huo ulidhaminiwa na NSSF. Kuilia ni Amir Athuman wa Kombaini ya Tanga.

Na Elizabeth Kilindi, Tanga

Timu ya Survey Veterani ya jijini Dar es salamu imeifunga timu ya Kombaini vijana  Veterani ya Jiji la Tanga 2-1 katika mchezo wa kuazimisha sherehe za wakulima nane nane viwanja vya Disuza vilivyopo Mkoani Tanga.

Mchezo huo ambao umedhaminiwa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), ulikuwa na lengo la kukutanisha timu za maveterani ili kujenga mshikamano na kuhamasisha michezo.

Katika mchezo huo wachezaji wa savey Carlos Mdinga alijifunga wakati akijaribu kuokoa mpira uliopigwa na wapinzani hatua ambayo ilisababisha gori hilo Dakika ya pili.

Aidha katika mchezo huo timu ya Savey ilionyesha makali yake ambapo dakika ya 40 walisawazisha goli kutoka kwa kiungo wake  Silyvester Malango.

Hata hivyo bahati nyota ilizidi kungaa kwa timu ya veterani baada ya Dakika ya 70 kupata goli la pili lililotiwa nyavuni namshambuliaji wake David  Emanuel.

Katika mchezo mwengine ni kati ya Timu ya Best point veterani imeibuka na ushindi wa goli mbili dhidi ya  Kombaini ya wazee Veterani ya Jijini
Tanga.

Magoli  ya Best point yalifungwa na Sadiki Salumu dakika ya saba na goli la  pili lilifungwa na Miraji Paulo dakika za lala salama.

Baada yakumalizika kwa mchezo huo kocha Seleman Mgaya ambaye ni Katibu wa Survey Veterani ya Dar es salaam amesema wamefurahishwa ushirikiano unaotolewa namfuko wa hifadhi ya jamii NSSF hasa kwa kuonyesha mchango wao katika michezo.

“Tunaishukuru sana  NSSF kwa moyo wa kutukutanisha pamoja kimichezo hatua ambayo tunajivunia kwaniwao wametambua umuhimu wetu hivyo hatuna budi kutoa ushirikiano”amesema Mgaya.

Full list of finalists for CNN MultiChoice African Journalist of The Year 2014, Tanzanian Dickson Ng’hily is in

$
0
0

CNN MultiChoice African Journalist of The Year 2014 competition which is in its 19th year, shortlisted 28 finalists from 10 countries across the continent.

This year the competition received entries from 38 countries.

Here is the full list of the finalists:
  1. Daniel Biaou Adje, ORTB, Benin
  2. Safia Berkouk, El Watan, Algeria
  3. Vinayak Bhardwaj M&G Centre for Investigative Journalism, Mail & Guardian, South Africa
  4. Tabelo Timse, M&G Centre for Investigative Journalism, Mail & Guardian, South Africa
  5. Romão Brandão, Jornal OPAÍS, Angola
  6. Sean Christie, Freelance for Landbouweekblad and The Mail & Guardian, South Africa
  7. Obinna Emelike, Business Day, Nigeria
  8. Ben Ezeamalu Premium Times, Nigeria
  9. Emmanuel Ogala, Premium Times, Nigeria
  10. Bob Koigi, Farmbizafrica.com, Kenya
  11. Joseph Mathenge, Freelance for The Saturday Nation, Kenya
  12. Anne Mawathe Citizen TV, Kenya
  13. Rashid Ibrahim, Citizen TV, Kenya
  14. Patrick Mayoyo, Daily Nation, Kenya
  15. Christine Muthee Media Development in Africa (MEDEVA), Kenya
  16. Oliver Oscar Ochanda, Media Development in Africa (MEDEVA), Kenya
  17. Dickson Ng’hily, The Guardian, Tanzania
  18. John Muchangi Njiru, The Star Newspaper, Kenya
  19. Olatunji Ololade, The Nation Newspaper, Nigeria
  20. Bayo Olupohunda, Columnist, Punch Newspaper, Nigeria
  21. Ossène Ouattara, Infoduzanzan.com, Côte d’Ivoire
  22. Brito Simango, Televisão de Moçambique, Moçambique
  23. Joy Summers Mnet Carte Blanche, South Africa
  24. Susan Comrie, Mnet Carte Blanche, South Africa
  25. Suy Kahofi, Freelance for West Africa Democracy Radio, Senegal
  26. Paballo Thekiso, Saturday Star, South Africa
  27. Bento Venancio, Jornal Domingo, Moçambique
  28. Evelyn Watta, Sportsnewsarena.com, Kenya
The finalists will enjoy all-expenses paid four day programme of workshops, media forums and networking in Dar es Salaam, Tanzania culminating in a Gala Award Ceremony on Saturday 18 October 2014.

Castle lite Yazindua Promosheni ya Lite up the wekeend jijini dar leo

$
0
0
 Meneja masoko wa bia ya Castle lite Vimal Vaghmaria kushoto mwenye miwani,Meneja wa Castle lite  Geofray makau   katikati na Meneja msaidizi wa Castle lite Tanzania Victoria kimaro wakionyesha chupa ya bia hiyo kwenye uzinduzi wa kampeni ya shindano la kuwapata washindi wa Castle lite VIP Yacht Party ambapo washindi watafanya tamasha kubwa ndani ya Boti katika bahari ya Hindi.
 Meneja masoko wa bia ya Castle lite Vimal Vaghmaria  kushoto mwenye miwani,Meneja wa Castle lite  Geofray makau   katikati na Meneja msaidizi wa Castle lite Tanzania Victoria kimaro wakionyesha chupa ya bia hiyo kwenye uzinduzi wa kampeni ya shindano la kuwapata washindi wa Castle lite VIP Yacht Party ambapo washindi watafanya tamasha kubwa ndani ya Boti katika bahari ya Hindi.
  Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria uzinduzi huo katika Hotel ya Slip way washindi wa Castle lite VIP Yacht Party watafanya tamasha kubwa ndani ya Boti katika bahari ya Hindi.

msaada wa haraka watakiwa kumnusuru bi. Vailet wa Kongwa

$
0
0
Na John Banda,Kongwa.

Bi Vailet Sekwao (40) mkazi wa kijiji cha Mtanana Wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma, anaomba msaada wa kifedha kiasi cha shilingi million mbili (2) ili aweze kufanyiwa upasuaji wa jicho lake ambalo lina uvimbe.

Akizungumza na mwandishi wetu katika kijiji cha Mtanana alisema kuwa anaomba msaada huo ili umwezeshe kugharima gharama za kumfikisha katika Hospitali ya Mhimbili na kufanyiwa upasuaji  wa uvimbe ulioko kwenye jicho.

Sekwao alisema kuwa uvimbe huo ambao ulinza kama kipele pembezoni mwa jicho hilo mwaka 2013,uliazidi kuongezeka na kufikia hatua ya kuvimba na kulifanya jicho hilo kutokuwa na uwezo wa kuona.

Alisema pamoja na juhudi za kwenda hospitali mbalimbali ikiwemo ya Mvumi, hali jicho hilo limezidi kuvimba na waatalam wamenishauri nikafanyiwe upasuaji kwa hatua iliyofikia.

“Kwa kweli ninapata maumivu makali sana hivyo ninawaomba wasamaria wema,taasisi na mashirika kunisaidia kiasi hicho cha fedha ikibidi hata kama kuna uwezekano wa kuweza kunitibu mimi nitakuwa tayari tu ,kwani hivi sasa nimeuza kila kitu ikiwemo nyumba,shamba na kiwanja,kwa ajili ya kupata fedha za kujitibu”alisema.

Bi Sekwao hata hivyo alisema kwa wale wote watakaogunswa na kilio changu kwa lengo la kunisaidia ninawaomba watumie namba zifuatazo za simu 068752216007881077530682400989

MAMA TUNU PINDA ASHIRIKI MKUTANO WA AMANI NA USALAMA DUNIANI,UNAOFANYIKA NCHINI KOREA KUSINI

$
0
0
Mke wa Waziri Mkuu Mama Tunu Pinda akifuatilia matukio kwenye ukumbi wa Mkutano wa Dunia kuhusu Amani na Usalama unaoendelea jijini Seoul, Korea Kusini. Wa pili kulia ni Rais mstaafu wa Mali, Prof. Dioncounda Traore. Wa kwanza kushoto ni Rais wa Samoa, Bw. Tui Atua Tupua Tamasese na mkewe Bibi Filifilia Tamasese.
Mke wa Waziri Mkuu Mama Tunu Pinda (katikati) katika picha ya pamoja na Rais wa Samoa, Bw. Tui Atua Tupua Tamasese (kulia) na mkewe Bibi Filifilia Tamasese (Agosti 12, 2014). Wa pili kushoto ni Katibu Mkuu wa Universal Peace Federation (UPF), Bw. Tageldin Hamad ambao wameandaa mkutano huo.
Mke wa Waziri Mkuu Mama Tunu Pinda (katikati) katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu wa Universal Peace Federation (UPF), Bw. Tageldin Hamad (kushoto) ambao wameandaa mkutano huo. Kulia ni Dk. Amalberga Kasangala kutoka Tanzania ambaye pia anashiriki mkutano huo.
Mke wa Waziri Mkuu Mama Tunu Pinda akiwa na Rais wa Universal Peace Federation (UPF), Dk. Thomas Walsh (kushoto) na wajumbe wengine wanaoshiriki Mkutano wa Dunia kuhusu Amani na Usalama unaoendelea jijini Seoul, Korea Kusini.
Mke wa Waziri Mkuu Mama Tunu Pinda akiwa na wajumbe wengine kutoka Afrika Kusini, Japan na Marekani ambao wanashiriki Mkutano wa Dunia kuhusu Amani na Usalama unaoendelea jijini Seoul, Korea Kusini.
Baadhi ya wajumbe kutoka Kenya, Tanzania na Lesotho ambao wanashiriki Mkutano wa Dunia kuhusu Amani na Usalama unaoendelea jijini Seoul, Korea Kusini. (PICHA NA IRENE BWIRE WA OWM).
Viewing all 39995 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>