Quantcast
Channel: MTAA KWA MTAA BLOG
Viewing all 40096 articles
Browse latest View live

JISAJILI NA MERIDIANBET USHINDE MGAO WAKO WA TZS 3,000,000!

$
0
0

 

Shinda Mpaka TZS 1,000,000 na Meridianbet!

 

Ofa za Meridianbet zinaendelea kutaradadi katika kila kona, ofa baada ya ofa, promosheni baada ya promosheni katika mwezi wenye mambo mengi. Nafasi yako ya kujishindia mgao wako wa bonasi ya TZS 3,000,000 kutoka hapa nyumba ya Odds bomba.

Jisajili, weka pesa katika akaunti yako na cheza sasa uwe mmoja ya washindi wa mgao wa bonasi wa TZS 3,000,000 kwaajili ya kucheza michezo mbalimbali katika tovuti yetu.
 
Jisajili kwenye APP au tovuti ya www.meridianbet.co.tz kuanzia tarehe 01.01.2023 mpaka tarehe 20.01.2023, na uweke angalau TZS 5,000 na ubeti michezo mbalimbali na michezo ya kasino ujiwekee nafasi ya kushinda bonasi ya pesa ya TZS 1,000,000
 
Unavyoweka pesa zaidi, kubeti na kuzungusha – nafasi ya kushinda moja ya zawadi zetu inaongezeka. 
 
Zawadi zitatolewa kama ifuatavyo:
Nafasi ya 1 – TZS 1,000,000 Bonasi ya pesa
Nafasi ya 2 – TZS 500,000 Bonasi ya pesa
Nafasi ya 3 – TZS 300,000 Bonasi ya pesa
Nafasi ya 4 – TZS 200,000 Bonasi ya pesa
Nafasi ya 5 mpaka 24 – TZS 50,000 Bonasi ya pesa
 
Vigezo na Masharti:
 
 Promosheni itadumu kuanzia tarehe 01.01.2023 mpaka tarehe 20.01.2023 saa 5:59 usiku
Washindi watatangazwa tarehe 21.01.2023 Kwa kujisajili na www.meridianbet.co.tz wateja watakuwa wamekubaliana na vigezo na masharti ya promosheni. 
Ofa hii ni kwaajili ya mchezaji mmoja au IP adress mmoja pekee.
  Meridianbet wana haki ya kutotoa zawadi, kusitisha au kubadili sheria za prmosheni wakati wowote.
 




SALAMU ZA PONGEZI

RAIS SAMIA AFANYA UTEUZI VIONGOZI MBALIMBALI

RAIS SAMIA AFANYA UTEUZI

AFISI YA MWANASHERIA MKUU ZANZIBAR IMESHAURIWA KUONGEZA JUHUDI YA UTOAJI WA ELIMU YA KISHERIA KWA JAMII

$
0
0

 

Na Faki Mjaka-AGC,Zanzibar 07.01.2023

Afisi ya Mwanasheria Mkuu Zanzibar imeshauriwa kuongeza juhudi ya utoaji wa elimu ya kisheria kwa jamii ili iweze kufahamu maswala mbalimbali ya kisheria.

Kwa kufanya hivyo Jamii ya wazanzibari itaweza kupata uelewa wa maswala ya kisheria na kuepuka kuingia katika hatia zisizo na ulazima.

Wito huo umetolewa na wananchi tofauti waliotembelea Banda la Maonesho la Afisi hiyo katika Tamasha la tisa la Biashara linaloendelea katika Viwanja vya Maisara mjini Unguja.

Mtumwa S. Kijiba kutoka Chukwani amesema muda umefika sasa kwa afisi hiyo kuvitumia vyombo vya habari kutoa elimu kupitia Wataalam wake waliobobea katika maswala ya kisheria.

“Hapa nimepata elimu iliyonifungua kichwa, natarajia kurudi tena kujifunza mambo mengi ila nivyema sasa mujipange kutufikishia taalumu hiyo kupitia vyombo vya habari ili watu wengi wanufaike” Alisema Kijiba

Kwa upande wake Abdallah S. Kinoo amesema elimu pia inahitajika hasa vijijini kulikosheheni migogoro ya ardhi hivyo ni vyema Afisi ya Mwanasheria Mkuu kuelekeza nguvu maeneo hayo.

Akijibu hoja na maswali kutoka kwa Wananchi hao Wakili wa Serikali kutoka Afisi ya Mwanasheria Mkuu Zanzibar Salum Khamis Salum amesema Afisi hiyo imejiwekea utaratibu wa kutoa elimu ya sheria kwa wananchi (outreaches program) kila baada ya muda hasa katika maeneo ya vijijini ili kuongeza uelewa kwa wananchi.

Amefahamisha kuwa kila inapokaribia siku ya Sheria Afisi hiyo imejipangia utaratibu wa kufika maeneo tofauti ya Unguja na Pemba kutoa elimu kuhusu mambo mbali mbali ya kisheria.

“Pamoja na kuyachukua maoni yenu na kwenda kuyafanyia kazi ila ukweli utaratibu huo wa kutoa elimu upo hasa maeneo ya vijijini, tunafanya hivyo kipindi cha kuelekea maadhimisho ya siku ya sheria” Amesema Wakili Salum.

Akizungumzia kuhusu maendeleo ya Tamasha hilo kwa ujumla wake Wakili Salum amesema watu wengi na rika tofauti huja katika Banda lao kuuliza maswali kuhusu kazi za taasisi na namna Afisi hiyo inavyotekeleza majukumu yake ya kila siku.

Hata hivyo amebainisha kuwa Idadi kubwa ya wananchi wamekuwa wakiulizia kuhusu kesi za migogoro ya ardhi na udhalilishaji jambo ambalo linaashiria kukithiri kwa mambo hayo katika jamii.

Hivyo amesema Afisi inapaswa kufikiria namna ya kutoa msaada na ushauri wa makusudi katika maeneo ya udhalilishaji na Ardhi ili kusaidia kupunguza matatizo hayo nchini.

Afisi ya Mwanasheria Mkuu Zanzibar imeweka Banda lake katika Tamasha la tisa la Biashara linaloendea katika Viwanja vya Maisara mjini Unguja ili kuitumia fursa hiyo kutoa Elimu ya kisheria kwa wanachi wanaofika katika Banda hilo.


 

UNAWEZAJE KUBETI NA KITOCHI MERIDIANBET-USSD

$
0
0

 

Usijali endapo hauna Intaneti Piga *149*10# BURE!

 Ushindi unaendelea ukibeti na Meridianbet USSD Piga *149*10# BURE kutengeneza mkeka wako usipokuwa na Intaneti mahali popote Tanzania. Nafasi nyingine ya kuendelea kufurahia odds nono za soka kiganjani mwako.

 

Jinsi ya Kujiunga na Meridianbet USSD!

 

Ni rahisi sana kujiunga na huduma hii ya USSD, cha kufanya ni kuwa na simu yako ya mkononi, haichagui aina ya simu ukiwa na kitochi inakubali na hata ukiwa na simu janja msisimko unaupata kama kawaida.

 

Kitu cha pili ni kupiga *149*10# kisha utachagua lugha, Kiingereza au Kiswahili, ukishachagua utaona umeletewa vigezo na masharti ya kukubali kubashiri ikiwa una zaidi ya miaka 18+ hairuhusiwi kubashiri ukiwa na chini ya miaka 18.

 

Baada ya hapo utabonyeza 90 kuendelea kwenye hatua inayofuata ambapo itakuletea machaguo ya mechi zilizopo zikiwa na odds kubwa nono kama unataka kujua mechi za masaa 24 zijazo, au mechi kubwa kwenye soka, au kama unataka kumtumia rafiki yako mualiko, kuangalia tiketi zako 5 za mwisho na kuangalia salio la akaunti yako kwenye waleti yako.

 

Tengeneza Mkeka wa Ushindi na Meridianbet USSD!

 

Ukimaliza kujiunga kazi inayobaki ni wewe kuonesha umwamba wako wa kubashiri na kitochi huku ukijipatia odds kubwa za soka

katika kila mechi unayoichagua na kuiweka kwenye mkeka wako.

 

Wakati huu ushabonyeza code ya ushindi ambayo ni *149*10# sasa utakupeleka kwenye uwanja wa kuonesha ufundi wako wa kubeti, na uwanja huo una machaguo yafuatayo:

 

1. Mechi za saa24 zijazo.

2. Top Football ikiwa ni mechi kubwa siku husika.

3. Kumtumia rafiki yako mualiko wa kujiunga na familia ya mabingwa Meridianbet.

4. Unaweza kuangalia tiketi zako 5 za mwisho 

5. Ni kujua akaunti yako ina kiasi gani.

 

Njia rahisi ya kubashiri na kitochi (USSD)

 

Usisahau kwamba odds kubwa za soka unazipata Meridianbet hata ukiwa hauna bando la internet au ukiwa na kitochi.

 

Unaweza kuweka mkeka wako kwa kubonyeza namba moja ambayo inaonesha mechi za saa 24 zijazo na hapo utazikuta mechi kibao, utachagua timu na mechi unazozitaka wewe kila mechi na timu ina machaguo yake yenye odds kubwa na nono.

 

Ukimaliza unabonyeza 91 kuweka ubashiri au kama unahitaji kuongeza mechi zaidi utabonyeza 92.

 

Ukibonyeza 91 kuweka ubashiri wako utaweka kiwango/dau unalotaka kuweka kwenye beti yako kisha utathibitisha malipo na hapo utakuwa umefikia mwisho unasubiri mkeka wako ucheke.

 

Lakini pia kama umekosea ubashiri wako Meridianbet wanakupata nafasi ya kurudia ikiwa hujaweka dau na kuthibitisha malipo. dau la chini kabisa unaloweza kubeti ni TZS 250/= Ushindi upo kiganjani mwako fanya maamuzi sasa, Meridianbet ndio habari ya mjini hawana ubabaishaji.

 

UKARABATI NA UPANUZI KIWANJA CHA NDEGE SONGEA WAFIKIA ASILIMIA 97,NDEGE KUANZA KUTUA USIKU

$
0
0

 



Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas akizungumza baada ya kukagua mradi wa ukarabati na upanuzi wa kiwanja cha Ndege Songea ambapo serikali ilitoa kiasi cha shilingi bilioni 37 kutekeleza mradi huo



Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas akiwa na Kamati ya ulinzi na Usalama Mkoa pamoja na watumishi wa kiwanja cha Ndege Songea kwenye ukaguzi wa mradi wa ukarabati na upanuzi wa kiwanja cha ndege Songea ambapo utekelezaji wake umefikia asilimia 97

Mnara mpya wa kuongozoea ndege katika kiwanja cha Ndege Songea ambao umekamiilika kwa asilinia 100 na unatarajia kuanza kutumika kuongozea ndege hivi karibuni



baadhi ya abiria katika kiwanja cha ndege cha Songea wakipanda ndege kuelekea jijini Dar es salaam



taa za kuongozea ndege ambazo zinatarajia kutumika kuongozea ndege usiku katika kiwanja cha ndege Songea ambapo sasa ndege zitaweza kutua usiku na mchana

………….

KAZI ya ukarabati na upanuzi wa kiwanja cha Ndege Songea mkoani Ruvuma imefikia asilimia 97 na kiwanja hicho kinatarajia kukabidhiwa serikalini Januari 30 mwaka huu.

Akitoa taarifa ya mradi wa ukarabati na upanuzi wa kiwanja hicho kwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma,Meneja wa TANROADS Mkoa wa Ruvuma Mhandisi Ephatar Mlavi amesema serikali ilitoa zaidi ya shilingi bilioni 37 kwa ajili ya kutekeleza mradi huo.

Amesema mradi huo ulitekelezwa na Mkandarasi Kampuni ya CHICCO toka nchini China kwa miezi 20 kuanzia Septemba 2019 hivyo unatarajiwa kukabidhiwa mwezi huu.

Amezitaja kazi ambazo zimefanyika kuwa ni ukarabati na utanuzi wa njia ya kurukia ndege kutoka urefu wa meta 1625 na upana wa meta 30 hadi kufikia urefu wa meta 1740 na upana wa meta 30.

“Kazi nyingine zilizofanywa ni upanuzi wa maeneo ya usalama wa ndege,ukarabati na upanuzi wa eneo la maegesho ya ndege,ujenzi wa eneo jipya la maegesho ya ndege kwa dharura,jengo jipya la abiria na upakaji wa rangi wa alama za kiwanja’’,alisema Mhandisi Mlavi.

Amezitaja kazi nyingine kuwa ni ujenzi wa mitaro,ujenzi wa uzio wa kuzunguka kiwanja,ujenzi wa barabara ya ndani ya kukagua usalama wa kiwanja,ufungaji wa taa za kuongozea ndege,ufungaji wa vifaa vya mawasiliano ya anga na ujenzi wa jengo la mitambo ya umeme.

Meneja huyo wa TANROADS Mkoa amezitaja kazi zilizoongezeka kuwa ni utanuzi wa njia ya kurukia ndege,ujenzi wa barabara ya nje ya kukagua usalama wa kiwanja,ujenzi wa jengo la muda la mitambo ya mawasiliano na anga na uongozi wa ndege.

Hata hivyo amesema utekelezaji wa mradi kwa ujumla umefikia asilimia 97 na kwamba kazi zilizosalia ni mitambo ya umeme,mitambo ya kusukuma maji ,taa za kuongozea ndege na vifaa vya usambazaji mawasiliano ya anga ambapo amesema kazi zote zinatarajia kukamilika Januari 30,2023.

Akizungumza baada ya kukagua mradi huo,Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas amemshukuru Rais kwa kutoa fedha za ukarabati wa kiwanja cha ndege na miradi mingine mikubwa ya kimkakati kukamilika mkoani Ruvuma.

Kanali Thomas amesema wananchi sasa wanahitaji kuona miradi yote inakamilika kwa asilimia 100 na kwamba wananchi wa Ruvuma wanatamani kuona sasa ndege zinatua usiku katika kiwanja cha Songea.

Ameyataja mahitaji ya abiria wanaotumia ndege katika Mkoa wa Ruvuma ni makubwa ambapo hivi sasa wanahitaji safari za usiku na mchana kwa kutumia ndege za ATCL.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Songea Mheshimiwa Pololet Mgema amesema Mkoa wa Ruvuma umepata uwanja wa kisasa wa ndege ambao utawezesha wasafiri kufika Songea mchana na usiku na kufanya biashara na kurejea Dar es salaam.

Amesema Mkoa wa Ruvuma una vivutio vya utalii na uwekezaji ambavyo sasa unaweza kuvifikia kwa haraka kwa kutumia usafiri wa anga.

Kwa upande wake Meneja wa Uwanja wa Ndege Songea Jordan Mchami amesema kabla serikali kuleta ndege za ATCL,wananchi wenye uwezo walisafiri kwa gharama kubwa Kwenda na kurudi Songea hadi Dar es salaam ilikuwa ni shilingi milioni moja.

Amesema hivi sasa kupitia ndege wa ATCL Kwenda na kurudi Songea hadi Dar es salaam ni kati ya shilingi laki tatu hadi nne kwa safari ya Kwenda na kurudi.

Amesema kiwanja cha Songea kina uwezo wa kutua ndege aina ya Bombadier yenye uwezo wa kubeba abiria 76 ambayo mara nyingi imekuwa inakuja na abiria 76 kwenda na abiria 76.

“Ndege inajaa hivyo tunatoa rai kwa kampuni nyingine za ndege kuanzisha safari na ATCL kuongeza safari za ndege ikiwezekana hata kila siku, tunatarajia kuanza safari za usiku taa zimeshafungwa tunasubiri kufanya majaribio ya kutua usiku ili hatimaye ndege zianze kutua usiku’’,alisema Mchami.

Uwanja wa ndege wa Songea ni miongoni mwa viwanja bora vya ndege Tanzania ambao ulijengwa kati ya mwaka 1974 hadi 1980.


WADAU WA ELIMU WAASWA KUDUMISHA WELEDI ILI KUINUA KIWANGO CHA ELIMU

$
0
0

Sehemu ya Maafisa Elimu Kata mkoa wa Kigoma waliohudhuria na kushuhudia utiaji saini wa Mikataba ya utendaji kazi kati ya Afisa Elimu Mkoa na Maafisa Elimu Wilaya za Mkoa wa Kigoma
Afisa Elimu Mkoa wa Kigoma akimkabidhi Mkataba wa utendaji kazi Afisa Elimu Sekondari wilaya ya Kobondo Julius Katyama
Afisa Elimu Mkoa wa Kigoma Pauline Ndigeza akimlabidhi Mkataba wa Utendaji kazi Afisa Elimu Sekondari Halmashauri ya Kigoma Exavery Ntambala
 
Na. Andrew Mlama-Kigoma

Wadau wa Elimu mkoani Kigoma wametakiwa kuzibadili changamoto kuwa fursa kwa kutanguliza uzalendo na kudumisha weledi katika kutekeleza mikakati mbalimbali inayoandaliwa na Serikali ili kuboresha na kuinua kiwango cha Elimu.

Wito huo umetolewa na Kaimu Katibu Tawala Msaidizi upande wa Elimu Mkoa wa Kigoma Paulina Ndigeza, alipokuwa anafungua Kikao kazi cha Utiaji Saini Mkataba wa Utendaji Kazi baina yake na Maafisa hao kilichofanyika wilayani Kasulu Mkoani Kigoma.

Ndigeza amesema kuwa dhamira ya Serikali kupitia mkataba huo ni kuhakikisha yanafanyika maboresho makubwa katika Sekta ya Elimu ili kuimarisha hali ya utendaji kazi katika mazingira ya ufundishaji na ujifunzaji ili kuinua kiwango cha Elimu sambamba na ufaulu nchini.

Serikali inawekeza kiasi kikubwa cha Fedha katika kukabili changamoto na kuboresha miundombinu ya Elimu nchini. Hivyo watendaji wameshauriwa kufanya kazi kwa weledi ili kurejesha thamani ya Fedha ambayo Serikali inaendelea kuwekeza katika Sekta ya Elimu.

Aidha Ndigeza amesisitiza Maafisa Elimu Sekondari kwenda kusimamia vigezo vyote 22 vya upimaji wa utendaji kazi vilivyoainishwa kwenye mikataba waliyoisaini ili kuleta matokeo chanya kwa kuongeza ufaulu katika matokeo ya mitihani ya kuhitimu  Darasa la Saba, Kidato cha Nne na Sita.

Naye Afisa Elimu Sekondari Halmashauri ya Kibondo Julius Kakiama, amesema vigezo vilivyomo kwenye mikataba hiyo vitawaongezea ari  ya utendaji kazi kwani inatoa fursa ya kila mtendaji kujipima na kujitathimini kisha kujua mapungufu yake na hatua za kuchukua ili kutimiza malengo yaliyowekwa.

‘‘Unapokuwa na mwongozo kama huu uliomo kwenye mkataba unarahisisha  kufahamu majukumu unayopaswa kuyatekeleza na kutambua hatua uliyofikia kiutekelezaji hivyo kuruhusu uwezekano mkubwa wa kupata matokeo chanya’’ amesema Julius.

Upande wake Afisa Elimu Kata Ruben Kahuza amesema kupitia kikao hicho wamejifunza namna ya kuzibadili changamoto kuwa Fursa ili kuepuka sababu zozote zitakazosababisha kushindwa kutekelezwa kwa vigezo vya upimaji vilivyomo kwenye mkataba wa utekelezaji.

Pamoja na uwepo wa changamoto ya kutotosheleza kwa ikama ya walimu, umbali kutoka makazi hadi shule zilipo pamoja na uelewa duni wa baadhi ya wazazi kuhusu ushiriki wa masuala mbalimbali ya kielimu. Watendaji tunapaswa kuzibadili na kuzifanya fursa ili kuhakikisha malengo yaliyowekwa na Serikali ili kuinua ufaulu yanafikiwa.

Serikali Kujenga Minara 8 ya Mawasiliano Mlimba

$
0
0

 


Na Immaculate Makilika - WHMTH
HUDUMU za mawasiliano ni za msingi katika maisha ya wananchi kwa vile zinagusa nyanja za kijamii, kiuchumi na kisiasa. Aidha, mawasiliano yanawezesha na kuhimili sekta mbalimbali ikiwemo elimu, afya, kilimo, uwekezaji na biashara, ajira, benki na utalii kwa kuziongezea ufanisi wa kiutendaji na kutoa mchango mkubwa katika uchumi wa moja kwa moja kupitia sekta hizo.

Ili kutimiza azma hiyo, Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa. Dkt. Samia Suluhu Hassan imedhamiria kujenga minara nane ya huduma za mawasiliano katika Jimbo la Mlimba lililopo mkoani Morogoro.

Akizungumza juzi (Januari 9, 2023) katika mkutano wa hadhara na wananchi wa Kijiji cha Kisegese, Kata ya Namwawala, Jimbo la Mlimba mkoani Morogoro, wakati alipokuwa katika ziara yake ya kukagua upatikanaji wa huduma ya mawasiliano na kuzungumza na wananchi. Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mheshimiwa. Mhandisi Kundo Mathew amesema “Mheshimiwa Rais alielekeza kufanya tahmini ya mawasiliano katika jimbo hili ambapo takribani shilingi bilioni 2.4 zitatumika kujenga minara nane ya huduma za mawasiliano katika jimbo hili la Mlimba”.

Ameongeza “Minara nane yote itakayojengwa itakuwa na huduma za intaneti na hivyo mkawe walinzi wa hiyo minara kwa kuwa mawasiliano ni haki ya kila mwananchi na mtanufaika kwa kuinua uchumi kupitia biashara mtandao”.

Mbunge wa Jimbo la Mlimba, Mheshimiwa Godfrey Kunambi amemshukuru Mheshimiwa Rais kwa kutoa fedha za ujenzi wa minara hiyo nane na kusema kuwa mara baada ya minara hiyo kuanza kutoa huduma wananchi wa jimbo hilo watanufaika kwa kutumia fursa mbalimbali za mawasiliano kwa kukuza uchumi wa wananchi wake.

Naye, Mratibu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) Kanda ya Pwani, Mhandisi Mwandamizi Baraka Elieza amesema katika zabuni itakayofunguliwa Januari 31, 2023, UCSAF itahakikisha wazabuni (makampuni ya simu) watakaoshinda wanafikisha mawasiliano katika kata hizi nane ndani ya Jimbo la Mlimba kwa ufanisi.

“Minara hii itawezesha kufikisha mawasiliano katika kata za Ching’anda, Chita, Signal, Kamweni, Kiberege, Masagati, Namwawala na Uchindile na hivyo kusaidia kuwa na mawasiliano ya uhakika”. Amesema Mhandisi Baraka.

Wadau Sekta ya utalii, misitu wapongeza Serikali

$
0
0

 

Na Mwandishi wetu, Arusha
WADAU wa sekta ya utalii na misitu wamezipongeza hatua za serikali ikiwa ni pamoja na kudumisha utamaduni wa kukutanisha wajumbe wa sekta binafsi na sekta ya umma katika kujadili changamoto zinazokabili sekta za utalii na misitu.

Wadua hao walihudhuria mikutano ya utalii and misitu iliyoandaliwa na Baraza la Taifa la Biashara Tanzania (TNBC)

Wakizungumza kwa nyakazi tofauti wadau wamesema Serikali ya Awamu ya sita chini ya Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendeleza utamadini huo na kwamba imeonyesha dhamira ya kutatua na kuondoa vikwazo vyote vinavyokabili sekta hizo .

Mikutano kama hii ya kisekta imekuwa chachu kwani inatukutanisha wadau mbalimbali kujadii changamoto na kutoa mapendekezo ya kukuza sekta hizi, walielezana na pia kumpongeza Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt Pindi Chana, kwa kuhudhuria na kuchangia mawazo katika mikutano hii.

Mwakilishi wa Zanzibar Association of Tour Operators (ZATO), Bw. Hassan Ali Mzee, alipongeza mikutano hiyo inayoandaliwa na TNBC na kusema imewapa wadau uwanja mpana wa kutoa kero zao katika sekta hizo na imechochea ari kuendelea kuwekeza katika sekta hizo.

“TNBC amekuwa akituunganisha na serikali katika kujadili namna tutakavyokuza na kuendeleza sekta za miliasili na utalii. Sekta hizi ni muhimu katika kuinua pato la taifa, kuingiza fedha ya kigeni na kutengeneza ajira kwa vijana,” alisema Bw. Mzee

Bw. Benedict Minja, kutoka Mtandao wa Jamii wa Usimamizi wa Misitu Tanzania (MJUMITA). alipongeza azimio la kuwa na wiki ya maonyesho maalum ya bidhaa za misitu na kusema kwamba maonyesho hayo yatawafanya wananchi kutambua ubora wa bidhaa za mazao ya misitu zinazotengezwa Tanzania.

“Wiki hii ya maonyesho maalum itakayofanyika kila mwaka tunatarajia itaonyesha bidhaa bora na kuonyesha ustadi wa Watanzania katika kutengeneza bidhaa zinazotokana na misitu. Inaelekea Watanzania bado tuna kasumba ya kuthamini mno bidhaa kutoka nje,” alisema Bw. Minja. Maonyesho hayo yanatarajiwa kufanyika Jijini Dodoma.



Akifunga mkutano huo mwishoni mwa juma hapa Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt Pindi Chana, alisema Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan amezifungulia fursa sekta za maliasili na utalii kupitia Filamu ya Royal Tour, Filamu hiyo imeongeza idadi ya wawekezaji katika sekta ya utalii nchini, alisema waziri.



Alisema kuna haja ya kuangalia upya namna yakuongeza uwekezaji katika huduma za malazi kama vile hoteli na kambi za kitalii, migahawa, usafirishaji watalii, na uwindaji wa kitalii.



Aidha alitoa wito kwa wadau wote katika biashara za utalii nchini kuendelea kuzingatia sheria, kanuni na taratibu zinazosimamia biashara za utalii nchini ili utoaji huduma kwa watalii uwe bora, salama na wakuvutia.

Katibu Mtendaji waTNBC, Dkt. Godwill Wanga, alisema moja kati ya maazimio ya mikutano hiyo linahimiza ujoaji wa mafunzo kwa wadau wote wanaohudumia watalii wakiwemo wapagazi, waongozaji na watoa huduma na wahifadhi wa milima. Azimio lingine linahusu kuinua ujuzi katika uzimaji wa moto ili kuondoa misukasuko endapo janga la moto litatokea katika mbuga na hifadhi za utalii, alisema Dkt. Wanga

FURAHIA ODDS NONO KUTOKA MERIDIANBET WIKII NI EFL, COPPA ITALIA NA SUPER CUP

$
0
0

  

WIKI hii mechi nyingi ni za EFL, Coppa Italia, Spanish Super Cup lakini pia Ligue 1 itaendelea na michezo kadhaa ya EPL pia ikitimua vumbi, Usipange kukosa kubetia mechi hizi kila moja ina Odds kubwa kutoka Meridianbet.


Huko Hispania ukiachana na LaLiga, Spanish Super Cup ni moja ya mashindano pendwa sana, mchezo mkali ni kati ya Real Madrid watakuwa wenyeji wa Valencia, furahia kubashiri Meridianbet ukiwa na odds kubwa.

Wakiwa na msimu mzuri vijana wa Xavi FC Barcelona watakuwa nje ya dimba la Nou Camp kukipiga na Betis, ukiachana na aina ya soka la pasi nyingi na kasi kwa Barca upande wa Betis wana aina yao ya uchezaji wakishambulia pamoja na kukaba pamoja, mbinu za kocha gani kumpiku mwenzake. Odds kubwa za soka unazipata Meridianbet, tembelea maduka ya kubashiri kuonesha umwamba.

Wametoka kumchakaza Chelsea bao 4 kwenye FA, Jeshi la Pep litawafuata Southampton kwenye mchezo mwingine wa EFL ukiachana na aina ya mpira wanaocheza City, Soton unadhani wanaweza kumdhuia Pep? Bashiri huku ukifurahia odds nono kwa mechi hii, hivi unaanzaje kuziacha odds 10.78 za Soton. Bonyeza hapa kuona machaguo mengi Zaidi 1000+

Baada ya kuanza kwa kusuasua kupata matokeo PSG watakuwa uwanjani tena kwenye mchezo wa raundi 18 dhidi ya Angers, huku Troyes akiwakaribisha Marseille uhondo wote wa kubeti unaupata Meridianbet, kila mechi imepewa odds kibao.

Mechi kalii za Coppa Italia wiki hii ni kati ya Milan dhidi ya Torino ni vita kati ya Milan aliyepo nafasi ya 3 huku Torino akiwa nafasi ya 10 kwenye msimamo. Milan ana 1.59 huku Torino akiwa na 4.90. Meridianbet wanakupa nafasi ya kubashiri mubashara aukuturbo mkeka wako.

AC Roma inayonolewa na Jose Mourinho watakuwa na kibarua kingine cha kusaka ushindi mbele ya Genoa, hapa napo una nafasi ya kuonesha ujuzi wako kwenye kubashiri machaguo yapo kibao yanasindikizwa na Odds kubwa.

N.B Meridianbet wanakupa nafasi ya kushinda mkwanja mrefu sana ukicheza michezo ya Kasino ya Mtandaoni, michezo kama Aviator, TiTAN Dice, Roulette, Fruit Parts, Poker na Mingine mingi. Kingine kikubwa Ukipakua APP ya Meridianbet kisha ukajiunga kwenye APP na Tovuti kisha ukaweka salio unapewa Bonasi ya Ukaribisho. Upewe nini kingine, Jiunge na Meridianbet Ushindi Kiganjani mwako

BIASHARA YA MAKAA YA MAWE ILIVYOSHAMIRI RUVUMA,ZAIDI YA TANI MILIONI MOJA ZAUZWA NJE KWA MIEZI SITA

$
0
0

Waziri Mkuu Mheshmiwa Kassim Majaliwa  alipotembelea na kukagua kampuni ya Jitegemee Holding inayochimba makaa ya mawe katika kijiji cha Ntunduwaro Kata ya Ruanda wilayani Mbinga na kuridhishwa na kushamiri kwa biashara ya makaa ya mawe mkoani Ruvuma
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas akizungumza na wafanyakazi wa Kampuni ya Jitegemee katika  eneo la mauzo ya makaa ya mawe bandari ya nchi kavu kijiji cha  Paradiso wilaya ya Mbinga


mgodi wa makaa ya mawe wa Kampuni ya Jitegemee Holding katika kijiji cha Ntunduwaro  wilayani Mbinga 

DKT MABULA ATAKA WANA CCM KUTUMIA FURSA YA MIKUTANO YA HADHARA KUJIBU HOJA

$
0
0

 

Na Mwandishi Maalum, MWANZA

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi ambaye ni Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula amewataka wanachama wa Chama cha Mapinduzi nchini kutumia fursa ya kuruhusiwa mikutano ya hadhara kama njia ya kujibu hoja kwa kuelezea mafanikio ya yaliyofanywa na chama hicho.

Dkt Mabula amesema hayo tarehe 11 Januari 2023 katika ofisi ya Chama cha Mapinduzi mkoa wa Mwanza wakati wa mapokezi ya wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa waliochaguliwa hivi karibuni kwenye mkutano mkuu wa 10 wa CCM.

Amesema, wana CCM wasiangalie sasa ambapo mikutano imeruhusiwa na kuanza kubishana huku wakiacha kuangalia utekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi na kuifanya kasuasua.

Kwa mujibu wa Dkt Mabula, Chama cha Mapinduzi kinayo matawi, Mashina pamoja na Kamati zake zake za siasa katika ngazi zote na kinachotakiwa ni kurudi kwa wanachama na kuhamasisha maendeleo huku wakikagua utekelezaji wa ilani ya CCM.

‘’Lazima kwenda kila ngazi kwa kukagua na kuangalia kama ilani inatekelezwa lakini siyo kwa kunyanyasa watumishi, hoja ya msingi hatutakiwi kuzifanya hoja zinazokuja kama kero za kujibishana na kila changamoto itakoyokuja igeuzwe kama fursa ya kusonga mbele.

Aidha, alimsifu na kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan na kueleza kuwa kama kuna mtu ambaye watanzania watamkumbuka basi ni yeye kutokana na hekima na busara zake hasa kwa serikali yake ya awamu ya sita kuwa kiungo kizuri cha kuendeleza yale mazuri yote ya serikali ya awamu yaliyopita

‘’kikubwa anachokifanya kama mama ni hekima, busara na maamuzi yake ni furaha kwa watanzania suala la mariasdhiano lililofanyika ninachotaka kuwaomba wana ccm wenzangu maridhaino ni mchakato, hoja ya msingi hapa tusizifanya hoja zinazoibuliwa katika mikutano kama hoja za kubishana bali ziwe za kutoa majibu kwa yale yaliyofanyika’’ alisema Dkt Mabula

Mjumbe huyo wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi Taifa alieleza kuwa, wanachotakiwa wana CCM kufanya ni kuisimamia serikali kwa kujibu hoja na kuangalia yale yote yaliyoelekezwa na chama kama yanafanyika kama ilivyopangwa.

Naye Mjumbe wa Halamshauri Kuu ya Taifa Bi. Elen Makungu Bogoje amesema Chama cha Mapinduzi kimeendelea kuisimamia serikali kila mahala na kusisitiza kuwa ipo haja kwa viongozi wa CCM katika kila ngazi kwenda kuisimamia serikali katika miradi yote iliyopo maeneo yao.

‘’Niwaombe viongozi wa CCM katika kila ngazi kwenda kuisimamia serikali ili wapinzani wakose hoja za kusema katika mikutano ya hadhara na kazi hii ya kuisimamia serikali tumeifanya na tunaendelea kuifanya’’. Alisema Ellen

Wajumbe wawili wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Dkt Angeline Mabula ambaye ni Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Ellen Makungu Bogoje waliwasili kwa mara ya kwanza katika mkoa wa Mwanza ambako ndiko wanakotokea tangu wachaguliwe kuwa wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM katika Mkutano Mkuu wa Cahama cha Mapinduzi uliofanyika mkoani Dodoma hivi karibuni.Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi ambaye ni Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akivishwa Scarf mara baada ya kuwasili ofisi ya CCM mkoa wa Mwanza ilipofanyika sherehe ya kuwakaribisha wajumbe wa NEC Taifa tarehe 11 Januri 2023.

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi ambaye ni Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akizungumza na wanachama wa CCM waliojitokeza katika sherehe za kuwakaribisha wajumbe wa NEC Taifa tarehe 11 Januari 2023 mkoani Mwanza.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa Bi. Ellen Makungu Bogoje akizungumza kwenye sherehe za kuwakaribisha Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa zilizofanyika ofisi ya CCM mkoa wa Mwanza tarehe 11 Januari 2023.
Mkuu wa mkoa wa Mwanza Adam Malima akizungumza katika sherehe za kuwapokea wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa CCM zilizofanyika ofisi ya CCM mkoa wa Mwanza tarehe 11 Januari 2023. 
Baadhi ya wana CCM waliojitokeza katika sherehe za kuwakaribisha wajumbe wa NEC Taifa ambao ni Dkt Angeline Mabula na Ellen Makungu Bogoje tarehe 11 Januari 2023.
Vijana wa hamasa wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Mwanza wakifurahia wakati wa sherehe za kuwapokea wajumbe wa halmashauri Kuu ya CCM Taifa zilizofanyika ofisi ya CCM mkoa wa Mwanza tarehe 11 Januari 2023.

 

SLOTI YA GOD OF COINS IMEJAA BURUDANI, CHEZA NA USHINDE ZAIDI!

$
0
0

 

Meridianbet wakishirikiana na Expanse Studio wanafanya wepesi katika mwezi huu wenye mambo mengi wakikuletea Sloti mpya ya God of Coins unaokufanya upate zaidi ya mara 1000 ya dau lako kirahisi kabisa, chaguo lako ndio ushindi wako leo.

Kasino ya God of Coins inawalenga wapenzi kindakindaki wa historia ya kale, mchezo huu ukiwasafirisha wachezaji wake hadi ulimwengu wa Misri ya kale kupitia picha zake zenye maelezo mengi zikipata chachu kutoka kwenye nyimbo zinazoendana na ari ya enzi hizo.

Ikiwa na mpangilio maalumu wa gridi ya 4x5, God of Coins Sloti ina ishara za alama 8 ikiwa ni pamoja na alama za mwitu. Katika mistari 20 ya malipo unauwezo wakushinda hadi mara 1000 ya thamani ya dau lako katika kila mzunguko mchezo huu unawafanya wachezaji kufurahia na kucheza kwa muda mrefu bila kuchoka. Ingia katika kasino ya mtandaoni ya Meridianbet sasa!

Kwa kuzingatia teknolojia ya kasino ya mtandaoni duniani Meridianbet na Expanse studio wamehakikisha umakini mkubwa katika kila nyanja ya mchezo ikiwemo picha maridhawa, michoro, sauti na ufundi wa uchezaji wa sloti ya God of Coins.

Mashabiki wa historia ya kale na michezo ya zamani ya kasino ya mtandaoni hakika watataka kukosa kujaribu sloti hii. Mahali pekee kufurahia ladha halisi ya kasino ya mtandaoni, mizunguko ya bure na ofa mbalimbali ni Meridianbet.  

Kasino za Meridianbet ndio njia rahisi ya kufurahia sloti na michezo mingine ya kasino mtandaoni ukiwa na nafasi ya kushinda mkwanja mrefu kwenye kila mzunguko huku ukifurahia picha mjongeo na sauti zenye ubora wa hali ya juu. 

BURIANI MCHUNGAJI SABINA LUMWE

$
0
0

 

Adeladius Makwega-Buigiri

Siku hiyo alifika ofisini afisa elimu maalumu anayefahamika kama Stephern Shemdoe na Halmashauri ya Lushoto ilimpa jukumu la kusimamia shule zenye wanafunzi wanaohitaji msaada maalumu ambazo zilikuwa za kuhesabika.

Wakati huo agizo la serikali ya awamu ya tano lilikuwa ni kuweka mikataba maalumu na shule zile zinazomilikiwa na taasisi za binafsi zenye kutoa huduma kwa watoto wenye mahitaji maalumu. Mwalimu Shemdoe alimjulisha mwanakwetu kuwa wilaya nzima ya Lushoto ina shule moja tu yenye sifa hiyo inayomilikiwa na Dayosisi ya Kaskazini Mashariki ambapo kazi ya kuwatafuta watoto wenye mahitaji maalumu ilikuwa ikifanywa kwa ushirika wa dhehebu hilo na serikali ya wilaya. Maana utamaduni uliokuwepo familia nyingi ziliwaficha watoto wa namna hiyo hivyo kuwapata watoto wenye sifa hiyo kwa darasa la kwanza ilikuwa kazi kubwa.

Mikataba hiyo baina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano na taasisi hizo ilisaidia walimu na watumishi wengine wenye ajira ya serikali kupangwa hapo na shule hizo kupata ruzuku ya uendeshaji wake kulingana na idadi ya wanafunzi waliowapokea. Kinyume chake shule hizo zilijiendesha kwa kutegemea wafadhili au sadaka za washirika wao za kila jumapili kanisani ambazo ni chache na hazina uhakika maana mambo ni mengi.

Zoezi hilo lilimkutanisha mwanakwetu na baadhi ya viongozi wa Dayosisi ya Kaskazini Mashariki akiwamo Baba Askofu Stephern Munga, Mchungaji Mwinuka na mwanasheria wao. Mwanakwetu aliwaambia kuwa sintoweza kusaini mkataba na taasisi nisiyoifahamu naomba niitembelee shule hii kwanza.

Hapo Shule ya Msingi Irente mwanakwetu alikaribishwa na watoto wenye mahitaji maalumu wenye albinism, wenye uone hafifu na wengineo na mbele yake hapo wakaimba nyimbo kadhaa ikiwamo Tanzania Tanzania, Mungu Ibariki Tanzania na
nyingine nyingi.

Baadaye mkataba huo ulisainiwa na upande wa Serikali ukiongozwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga wakati huo Bi Zena Said(Sasa ni Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar), mwanakwetu, Afisa Elimu wa Wilaya ya Lushoto wakati huo Mwalimu Adam Shemnga na upande wa Dayosisi hiyo.

Eneo la Irente lilikuwa na miti mingi mkubwa ya asili na ya kupandwa, ngombe kadhaa wa maziwa na wa kufungwa walizunguka katika eneo tambalale na kando ya eneo hilo tambalale palikuwa na kanisa moja dogo ambalo mwanakwetu aliambiwa kuwa ndilo linalotoa huduma za kiroho kwa jamii ya Irente na shule hii.

Ndani ya kanisa hilo mwanakwetu alitambulishwa kwa mchungaji Sabina Lumwe akiwa mama mmoja wa makamu. Hapo mwanakwetu alizungumza mambo kadhaa na baadaye mchungaji Sabina kumuonesha kitabu chake alichokiandika kilichopewa jina “My Marriage Are Not Start Yet.”


Baada ya safari hiyo mwanakwetu walishirikiana na mchungaji huyu katika mambo kadhaa ya kimaendeleo ambapo yapo yaliyokamilika na yapo ambayo hayakukamilika huku nia ya kuyafanya ilikuwapo kwa pande zote mbili.

Baadaye mwanakwetu aliondoka Lushoto na hata Dayosisi ya Kaskazini Mashariki ikapata Askofu Mpya Baba Askofu Msafiri Mbilu, huku mchungaji Sabina Lumwe aliendelea na kazi yake hiyo katika kanisa hilo lililo umbali mchache na Jengo la Halimashauri ya Wilaya ya Lushoto. Mwaka wa 2023 ulianza vizuri na juma la kwanza kuelekea la pili la mwezi wa Januari mwanakwetu alipewa taarifa ya msiba wa
Mchungaji Sabina Lumwe hiyo ikiwa ni kazi ya Mungu na mara zote haina makosa.

Januari 10, 2023 Baba Askofu Msafiri Mbilu wa Dayosisi ya Kaskazini Mashariki aliongoza Ibada ya mazishi ya Mchungaji Sabina Lumwe huku akibainisha wazi kuwa Mchungaji Sabina ni miongoni mwa Wachungaji watatu wanawake wa mwanzo wa kanisa lao kupewa daraja hilo na huku Mchungaji Sabina akiwa mwanamke wa kwanza kusomea teolojia katika dayosisi yao mwishoni mwa miaka sabini.

“Mchungaji Sabina alikuwa miongoni mwa wachungaji waliojitolea maisha yao kwa ajili ya wengine, alifanya hivyo kwa kuwa hayo ndiyo maisha yake aliyoyachagua kwa ajili ya yatima, wasio jiweza na alikuwa na maono ya kuwaungasha wanawake.” Askofu Mbilu alisisitiza.

Ibada hiyo ya mazishi ambayo mwanakwetu aliifuatilia alishuhudia Baba Askofu Mbilu akizionesha kazi mbalimbali zilizofanywa na mama huyu huku waombolezaji kadhaa wakiwamo wachungaji aliowahi kufanya nao kazi wakishuhudia.

Mchungaji Sabina Lumwe alizaliwa Julai 21, 1960 Kijiji cha Lutindi , Korogwe Mkoa wa Tanga, akiwa mtoto wa pili wa familia ya Baba Mwageni Mtunguja na Mama Julia Mtunguja. Mwezi mmoja baadaye yaani Agosti 1960 alibatiza na miaka 15 baadaye yaani 1975 alipata Kipaimara huko huko Lutindi Parish. Shule ya Msingi alisoma Lutindi hadi la saba na alijiunga na Shule ya Sekondari ya Wasichana na Kibosho na kuhitimu mwaka 1979.

Alipoitimu tu kidato cha nne aliunganisha mafunzo teolojia katika Chuo cha Makumira kwa ngazi ya astashahada na alihitumu mwaka 1983. Alipomaliza masomo yake alipangiwa majukumu katika usharika wa Lushoto na kwa kuwa wakati huo Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania lilikuwa halijaruhusu wanawake wawe wachungaji alifanya kazi kama mchungaji msaidizi. Mchungaji Sabina Lumwe hadi anafariki amemuacha mgane, watoto na wajukuu watatu.

Mwanakwetu anatoa pole kwa Baba Askofu Mbilu kwa kumpoteza Mchungaji wake, pole kwa wana Dayosisi ya Kaskazini Mashariki wote na pole kwa familia nzima ya Mchungaji Lumwe wa Lutindi na Lushoto Mjini.“N’tambo ntana Mchungaji Sabina Lumwe-Buriani Mchungaji Sabina Lumwe.”
Bwana ametoa, Bwana ametwaa, Jina lake lihimidiwe, amina.











RUWASA WAPOKEA MAGARI 10 KWA AJILI YA KUBORESHA UTENDAJI KAZI

$
0
0

 

Na Janeth Raphael

Serikali kupitia Wizara ya Maji imekabidhi magari 10 kwa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) kwa ajili ya kuboresha utendaji kazi.

Magari hayo yatagawiwa katika mikoa ya Dodoma, Ruvuma, Rukwa, Morogoro, Iringa, Shinyanga, Mara , Kagera na mikoa iliyopo pembezoni mwa Nchi.

Akizungumza na wandishi wa habari leo Januari 11,2023 Jijini Dodoma, wakati wa kukabidhi magari hayo, Waziri wa Maji Jumaa Aweso amesema changamoto kubwa ambayo husababisha miradi kusuasua ni kutokana na usimamizi na ufuatiliaji.
IMG-20230111-WA0177

Aweso amesema kuwa Rais Samia alianzisha Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) na ndani ya muda mfupi kulikuwa na miradi kichefuchefu zaidi ya 147 lakini ndani ya muda mfupi wameweza kukwamua na kutatua changamoto katika miradi mingi.

“Uanzishwaji wa RUWASA lazima kuwe na vitendea kazi ili kusaidia kusimamia na kufuatilia miradi, leo tumekabidhi magari zaidi ya 10 na haya ni uwezeshaji wa Rais Dk.Samia na tumeshajielekeza kuwa kazi iendelee na hatuna kisingizio.

Na kusisitiza kuwa “”Magari yatumike kwa ajili ya kusimamia miradi ya maji vijijini ili kufanikisha azma ya Rais Dk.Samia ya kumtua mama ndoo kichwani na kufikia asilimia 85 ya upatikanaji wa maji vijijini ifikapo 2025.

Aweso ameagiza kuwa RUWASA wahakikishe magari hayo yanafanya kazi iliyokusudiwa ya kusimamia miradi ya maji kwa weledi.

“Kuwepo kwa vitendea kazi hivi naamini utendaji kazi utaongezeka na kuleta mageuzi na mabadiliko makubwa kwa taasisi hii changa kuendelea kufanya kazi kubwa ya kuwasaidia wananchi kupata huduma ya maji,”amesema Aweso

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa RUWASA Mhandisi Clement Kivegalo amesema mahitaji ya magari kwa wakala huo ni 398 huku yalipo ni 392 ambayo mengi yakiwa katika hali isiyoridhisha kutokana na kutumika kwa muda mrefu.

Amesema kupitia ofisi ya Waziri Mkuu RUWASA ilipata kibali cha kununua magari 123 ambapo kati ya hayo 38 tayari yamepatikana na yapo katika mikoa mbalimbali yakiendelea kutoa huduma.

“Kibali kingine ambacho tumeshatumia ni magari 25 ambapo hayo tumeshalipia ambayo yamegharimu kiasi cha sh.bilioni 3.8, kati ya magari hayo 10 yenye thamani ya sh.bilini 1.5 ndio tumepokea leo na mengine 15 yatafuata,”amesema Kivegalo

Mhandisi Kivegalo amempongeza Rais Samia kwani katika kipindi kifupi ametatua changamoto ya usafiri kwa RUWASA. 

Mhandisi Kivegalo amedokeza kuwa katika mwaka wa fedha ujao Serikali imeahidi kuwanunulia Magari 92 ili kuendeleza kasi ya kuhakikisha wanawahudumia wananchi katika mikoa 25 wanaosimamiwa na RUWASA ukiiondoa Mkoa wa Dar es salaam.Waziri wa maji Jumaa Aweso akikata utepe wakati wa zoezi la kukabidi magari hayoWaziri wa maji Jumaa Aweso akizungumza na wanahabari wakati wa  kukabidhi magari hayo leo jijini Dodoma

SHILINGI BILIONI 13.5 ZAKUSANYWA MFUKO WA FAIDA FUND, WAWEKEZAJI 3,800 WAJIANDIKISHA

$
0
0

 

Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV

MKURUGENZI Mtendaji wa Watumishi Housing Investmet Dk.Fredy Msemwa amesema wawekezaji 3,800 wamejiandikisha kuwekeza kwenye Mfuko wa FAIDA FUND na hivyo kufanikiwa kukusanya Sh.bilioni  13.5 katika kipindi kifupi.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam Dk.Msemwa amesema pamoja na mambo mengine kiwango cha uwekezaji katika mfuko huo kimeendelea kukua siku hadi siku, hivyo kuongeza mafanikio makubwa ya mfuko huo.

“Mpaka tunafunga  mauzo ya mwanzo Desemba 31,2022 tumefanikiwa  kukusanya kiwango kikubwa na hivyo kuvuka malengo ambayo tulikuwa tumeyaweka.Mafanikio haya yanatokana na watu wengi kutumia teknolojia rahisi na matumizi ya simu, mitandao ya kompyuta ambayo imesaidia kuufikia mfuko huo kwa wepesi na hivyo kufanikisha makusanyo hayo.”

Ameongeza kwamba watu wengi wameufikia mfuko wa FAIDA FUND na kufanya uwekezaji ambao umewezesha kukusanywa fedha Sh.bilioni 12.95 hadi kufikia Desemba 31,2022 na kwa sasa kiasi hicho kimeongezeka mpaka kufika Januari 11, 2023 wamekusanya Sh.bilioni 13.5 na kuongeza kiasi cha fedha kimeendelea kukua siku hadi siku.

Pia  thamani ya kipande awali ilikuwa 100 na sasa imeongezeka kwa shilingi 100.54 huku akifafanua hayo yamewezekana kutokana na matumizi ya mfumo rahisi wa malipo Serikali ambao umewaletea faida kubwa ikiwemo ya utambuzi wa miamala kufanyika kwa kasi kubwa.

Pia amesema faida nyingine mfuko huo unawezesha fedha zinazowekezwa kuwa salama ambapo tayari fedha hizo zimeingizwa kwenye uwekezaji wa dhamana za Serikali za muda mrefu mwaka  2022/2025. “Wawekezaji pia wamepata faida katika Mfuko huo kutokana na gharama zake kuwa ndogo kwani wanalipa kidogo kwa ajili ya mtandao na zinazobaki zinaingizwa serikalini.”

Mkurugenzi Mtendaji wa Watumishi Housing Investmet Dk. Fredy Msemwa wakati akizugumza na waandishi wa habari (hawapo pichani)juu  mauzo ya hatifungani katika fuko wa FAIDA FUND uliowekezwa na Shirikala Watumishi Housing  Investiment  leo jijini Dar es Salaam Mkuu wa Kitengo cha Kusimaia Uwekezaji kwenye Masoko ya Mitaji na Dhamana Benki ya CRDB,Masumai Hemed akielezea namna wawekeaji walivyochangamkia uwekezaji huo kupitia benki ya CRDB leo jijini Dar es Salaam.Meneja Maendeleo ya Biashara na Masoko Benki CRDB, Mary Mponda  akifafanua jambo kwenye Mkutano hum ulifanyika leo jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya watumishi wa Watumishi Housing Investmet wakiwa kwenye Mkutano huo uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Picha ya pamoja (PICHA NA EMMANUEL MASSAKA WA MICHUZI TV)

HIZI HAPA ODDS NONO-MERIDIANBET WIKIENDI HII! MERIDIANBET - BASHIRI POPOTE, WAKATI WOWOTE!

$
0
0

 

Hii ni wiki ya washindi kama ukiichagua Meridiabet. Odds nono na machaguo kedekede yanapatikana huku! Zaidi ya michezo 1000 kuchezwa wiki hii, ni fursa ya kutengeneza mamilioni ya pesa. Kubwa zaidi, ni muendelezo wa Ligi ya Mbalimbali EPL, La Liga, Serie A, Ligue 1 na nyingine kibao. Mchongo upo hivi;

 

Dabi ya Italia (Il derby d'Italia) inawakutanisha Napoli dhidi ya Juventus katika dimba la Diego Armando Maradona leo Ijumaa. Napoli anaongoza Ligi kuu y aItalia akiwa amepoteza mchezo mmoja pekee msimu huu, wakati Juventus akiwa amepoteza mechi 2 mpaka sasa. Napoli hawajapoteza mchezo wakiwa nyumbani dhidi ya Juventus tangu mwaka 2019. Odds ya 2.01 Napoli kushinda inaweza kuboost mkeka wako!

 

Pale EPL inapigwa Dabi ya Manchester mapema kabisa siku ya Jumamosi, Manchester United watakuwa wenyeji wa Manchester City kwenye dimba la Old Traford. Vita ya mahasimu hawa waliokatika nafasi ya 2 na 4 inazidi kuchochewa na ubora wa timu hizo kwa sasa. Mshambuliaji Marcus Rashford kufunga goli ana Odds ya 3.43 wakati Erling Haaland akiwa na Odds ya 1.69. machaguo zaidi na Odds nono endelea kubeti na meridianbet.  

 

Jumamosi kuna Odds kibao za ushindi, Kule La Liga – Girona (2.45) watavaana na Sevilla (2.89) wakati Real Sociedad (2.45) wakivaana na Athletic Bilbao (2.99). EPL – Brighton (3.23) dhidi ya Liverpool (2.11) katika dimba laAmerican Express Community. Serie A – Lecce (5.68) dhidi ya AC Milan (1.60), Inter Milan (1.27) vs Verona (9.40). Ligue 1 – Marseille (1.39) dhidi ya Loriente (7.25), Lyon (1.60) dhidi ya Strasbourg (5.09). Kwa Odds hizi ushindi ukiwa na meridianbet ushindi kwako ni jambo la kawaida.

 

Siku ya Jumapili, Dabi ya London Tottenham wakiwakaribisha vinara wa EPL Arsenal-Washika Mtutu hawajashinda katika uwanja wa Tottenham katika misimu 3 iliyopita wamepewa Odds ya 2.20 kuibuka na ushindi ugenini dhidi ya vijana wa Conte. 

 

Baada ya kushinda mchezo mmoja kati ya michezo 11 iliyopita, Chelsea watakuwa nyumbani Stamford Bridge dhidi ya Crystal Palace siku ya Jumapili. Je, Potter ataweza kurekebisha makosa. Hii hapa Odds ya 1.67 kwa Chelsea. Hii ndio nyumba ya ushindi, Meridianbet!

 

Mabingwa wa Ufaransa, PSG hawaja shinda ugenini  katika dimba la Roazhon Park dhidi ya Rennes tangu mwaka 2018. Matajiri wa Paris wamepoteza mchezo mmoja pekee msimu huu, wataweza kuvunja uteja dhidi ya Rennes. Odds ya 4.41 mchezo huu kumalizika kwa sare, weka beti yako sasa!

TUNDURU WAFANYA MNADA WA 10 WA KOROSHO

$
0
0

 

Na Muhidin Amri, Tunduru

JUMLA ya kilo 308,774 za korosho  kutoka vyama vya msingi vya ushirika vinavyosimamiwa na Chama Kikuu cha ushirika wilaya ya Tunduru (Tamcu Ltd), zimeuzwa katika mnada wa 10 uliofanyika katika ghala la TAMCU Tunduru mjini.

Meneja wa Chama Kikuu cha Ushirika(Tamcu)wilayani Tunduru Imani Kalembo alisema, katika mnada huo kampuni moja  ya RV Export Ltd ndiyo imejitokeza kuomba kununua ambapo korosho daraja la pili  ziliuzwa kilo 151,440 kwa bei ya sh.1,340 kwa kilo moja na daraja la kwanza zimeuzwa kilo 157,334 kwa sh.1,600.

Alisema,hadi sasa Chama Kikuu kimeshafanya minada 9 na jumla ya tani 14,380 zenye thamani ya Sh.bilioni  25 zimekusanywa na kuuzwa  kwa makampuni mbalimbali.

Hata hivyo alieleza kuwa,kiasi hicho cha korosho zilizozalishwa katika msimu 2022/2023 ni nusu ya uzalishaji msimu wa mwaka 2021/2022 kwani katika msimu uliopita wakulima walifanikiwa kuzalisha na kuuza zaidi ya tani 25,000.

Kalembo,amewaasa wakulima ambao bado wana korosho majumbani,kuhakikisha wanapeleka kwenye vyama vyao vya msingi(Amcos) kwa ajili ya kuuza ili kuwahi mnada wa mwisho utakaofanyika wiki ijayo.

Aidha,amewataka kufanya palizi ya mashamba yao na kutumia fedha wanazopata kununua pembejeo za ruzuku zilizotolewa na serikali ya awamu ya sita,na kuepuka kutumia kwenye mambo ya anasa jambo linaloweza kuwarudisha nyuma kimaendeleo.

Makamu mwenyekiti wa Tamcu James Chipojola alisema,uzalishaji mdogo wa korosho katika msimu wa mwaka huu umeathiriwa sana na mabadiliko ya tabia ya nchi ambapo mvua za masika ziliwahi kunyesha  na hivyo kuathiri sana uzalishaji na kupunguza ubora wa korosho.

Chipojola,amewashauri  wakulima ambao ni wanachama wa Tamcu, kuanza kulima mazao mengine ya biashara kama vile ufuta,mbaazi,soya, na alizeti ili kujiongezea kipato,badala ya kutegemea zao moja tu la korosho ambalo kwa sasa linakabiliwa na changamoto nyingi ikiwamo ya bei.

Naye Afisa ushirika wa wilaya hiyo George Bisani alisema, katika msimu wa 2022/2023  malengo yalikuwa kuzalisha tani 30,000 lakini hawawezi kufikia kutokana na kushuka kwa uzalishaji wa zao hilo mashambani.

Bisani,amewaomba wakulima kutokata tamaa kutokana na changamoto zilizojitokeza katika msimu huu,bali waendelee kufanya maandalizi ya msimu mpya kwa kupalilia mashamba yao na kufuata ushauri  wa wataalam wa kilimo.
Mmoja wa wakulima  wa zao hilo Issa Lada,ameiomba serikali kusimamia bei ya korosho kwani  wakulima wanatumia gharama kubwa katika uzalishaji,lakini bei zinazotolewa na makampuni yanayonunua korosho ni ndogo na hailingani na gharama za uzalishaji wake.

Alisema,kama serikali itajipanga na  kusimamia vizuri suala ya bei kwa zao la korosho uchumi wa wilaya hiyo utakuwa mkubwa na wakulima watapata fedha nyingi  na kuongeza uzalishaji mashambani.
Sehemu ya korosho zilizokusanywa katika ghala la Chama kikuu cha Ushirika wilayani Tunduru(Tamcu Ltd) 
Makamu mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika wilaya ya Tunduru(Tamcu Ltd) James Chipojola akisoma bei ya zao la korosho zilizotolewa na wanunuzi wa zao hilo kwenye mnada wa 10 uliofanyika jana,kushoto Meneja Mkuu wa chama hicho Iman Kalembo.
Meneja wa Chama Kikuu cha Ushirika wilaya ya Tunduru(Tamcu Ltd)Imani Kalembo akizungumza na wawakilishi wa wakulima na makampuni yanayonunua korosho kwenye mnada wa 10 wa zao hilo,kulia makamu mwenyekiti wa Tamcu James Chipojola.
Baadhi ya wakulima,wafanyakazi wa Tamcu  wakifuatilia mnada wa korosho uliofanyika katia ghala ya Chama kikuu cha Ushirika wilayani Tunduru.
Makamu Mwenyekiti wa Tamcu James Chipojola akifunga mnada wa 10 wa zao la korosho uliofanyika jana ambapo zaidi ya kilo 308,774 zimeuzwa,kushoto meneja wa Tamcu Imani Kalembo.


Waziri Jafo, Benki Ya Exim na Wadau Wa Habari Waadhimisha Mapinduzi Ya Zanzibar Kwa Upandaji wa Miti Dodoma

$
0
0

 

Waziri Jafo, Benki Ya Exim na Wadau Wa Habari Waadhimisha Mapinduzi Ya Zanzibar Kwa Upandaji wa Miti Dodoma.

Dodoma: Januari 11, 2023; Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Selemani Jafo ameungana na Benki ya Exim Tanzania na wadau wa habari mkoani Dodoma katika zoezi la upandaji miti kwenye soko la Machinga Complex jijini humo ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Miaka 59 ya Mapinduzi ya Zanzibar sambamba na kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi.

Mkakati huo wa upandaji miti kwenye soko hilo ambao umedhaminiwa na Benki ya Exim na kuratibiwa na Taasisi ya Habari Development Association ni sehemu ya mpango wa upandaji miti 6000 katika maeneo mbalimbali jijini humo ikiwemo pia eneo la Hospitali ya Mirembe na Shule ya Msingi Uhuru ya jijini humo.

Akizungumza mara tu baada ya kuongoza zoezi la upandaji miti kwenye soko hilo, Waziri Jafo alisema Wizara yake kwa kushirikiana na wadau hao imejipanga kutumia vema Maadhimisho ya Miaka 59 ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuendesha jitihada mbalimbali za utunzaji mazingira hususani kwa kupanda miti katika maeneo mbalimbali nchini.

“Tukiwa kwenye mkakati huu muhimu tunaguswa zaidi kuona kwamba wenzetu Benki ya Exim wameamua kuungana na serikali ili kufanikisha zoezi hili muhimu ambalo ni sehemu ya Maadhimisho ya miaka 59 tangu kufanyika kwa Mapinduzi Zanzibar…tunawashukuru sana Benki ya Exim kwa kuwa ‘wanaupiga mwingi’ katika jitihada mbalimbali za utunzaji mazingira hususani katika jijini hili la Dodoma’’ alisema.

Kwa mujibu wa Waziri Jafo, taifa kwasasa linapitia changamoto nyingi zinazotokana na athari ya mabadiliko ya tabia nchi na hivyo kusababisha upungufu wa mvua kwa karibu nusu ya kiwango kilichozoeleka. Hali hii imesaababisha upungufu wa uzalishaji wa chakula, upatikanaji wa huduma ya maji, ukosefu wa umeme wa uhakika na hivyo kusababisha mporomoko wa uchumi.

“Hata hivyo serikali inaendelea na miradi mbalimbali inayolenga kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi ikiwemo kupunguza uzalishaji wa gesi ya ukaa, kuchimba mabwawa makubwa ya kuhifadhi maji sambamba na mradi wa uzalishaji umeme wa Bwawa la Mwalimu Nyerere, zote hizi zikiwa ni jitihada za kuhakikisha kama taifa hatuathiriki sana na changamoto hii,’’ alisema.

Kwa upande wake Ofisa Mkuu Idara ya Fedha (CFO) Benki ya Exim Shani Kinswaga alisema benki hiyo imekuwa ikiunga mkono juhudi za Serikali za kupambana na mabadiliko ya tabia ya nchi kwa kuja na namna mbalimbali ikiwemo kupitia Program yake ya ‘Exim Go Green Initiative’ kwa kuhamasisha upandaji wa miti na utunzaji mazingira nchini kupitia matawi yake yaliyo katika maeneo mbalimbali hapa nchini.

“Kwa upande wa ukanda huu wa kati, jiji hili la Dodoma limebahatika kuwa chaguo la Benki ya Exim katika kuendesha Programu hii. Zoezi hili la leo ni zoezi la tatu kwa benki ya Exim kushiriki katika kipindi cha miaka mitatu ndani ya mkoa huu wa Dodoma tukiwa tayari tumedhamini upandwaji wa miti zaidi ya zaidi ya 20, 000 katika maeneo mbalimbali,’’ alisema.

Kwa mujibu wa Bw Kinswaga, benki hiyo kama taasisi ya fedha nchini inaguswa pia na chanagmoto za kiuchumi zinazotokana na athari ya mabadiliko ya tabia nchini hivyo imedhamiria kuunga mkono jitihada mbalimbali zinazolenga kukabiliana na changamoto hiyo.

Awali akizungumza kwenye tukio hilo, Katibu Mtendaji wa Taasisi ya Habari Development Association Bernard Mwanawile alisema taasisi yake imejipanga kupanda miti milioni 1 mkoani humo huku akipongeza wadau mbalimbali wanaounga mkono mpango huo ikiwemo benki ya Exim ambayo hadi sasa imeweza kufadhili upandwaji wa miti 16,000 kupitia taasisi hiyo pekee.

Naye Meneja wa Soko la Machinga Complex Bi Veronica Tarimo aliahidi kuhakikisha kwamba soko hilo na wadau wake wote wakiwemo wafanyabiashara wadogo wanaofanya biashara zao kwenye soko hilo wataitunza vema miti hiyo sambamba na kuendelea na mkakati wao wa utunzaji mazingira katika soko hilo.

“Zaidi tu niseme kwamba kwa kuwa Benki ya Exim imeonesha nia ya kushirikiana na wamachinga nasi pia tunaiomba benki hii iweke kambi kwenye soko letu ili itoe elimu ya kifedha kwa wafanyabiashara hawa ili waweze pia kupatiwa mikopo nafuu kutoka benki ya Exim,’’ alisema.Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Mh Selemani Jafo (Kulia) akishuhudia  Ofisa Mkuu Idara ya Fedha (CFO) Benki ya Exim Shani Kinswaga (wa pili kulia), Meneja Masoko na Mawasiliano wa Benki hiyo Bw Stanley Kafu (katikati) na Katibu Mtendaji wa Taasisi ya Habari Development Association Bernard Mwanawile (kushoto) wakipanda miti kwenye soko la Machinga Complex jijini Dodoma mapema hii leo ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Miaka 59 ya Mapinduzi ya Zanzibar sambamba na kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi.  Kupitia mkakati huo, Benki ya Exim imefadhili upandaji wa miti 6000 katika maeneo mbalimbali jijini humo. 

Viewing all 40096 articles
Browse latest View live
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>