Quantcast
Channel: MTAA KWA MTAA BLOG
Viewing all 40137 articles
Browse latest View live

MRADI WA NYUMBA WA DEGE ECO- VILLAGE WAANZA, WANANCHI WACHANGAMKIA FURSA

$
0
0
Mradi wa nyumba unaosimamiwa na kampuni ya Hifadhi inayoitwa Dege Eco-Village umeshiriki maonyesho ya nyumba yaliyofanyika jijini Dar es Salaam inategemea umeanza hivi karibuni.
Akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam,  Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo Bw. Azhar Malik wa Dege eco-Village alisema “Kwa sasa ujenzi unaendelea na karibu aina ya nyumba apartment 3000 zitakuwa tayari ifikapo Januari 2015. 
Aliongezea kusema kwamba kupitia mradi huu waTanzania watanufaika kwa kupata ajira na pia kuwa na huduma kama hospitali, shule, maduka eneo la Kigamboni. 
Mradi huu unajengwa kwenye eneo takriban eka 300 na kampuni hiyo imewekeza zaidi ya dola milioni 350. Kwa ujumla nyumba aina ya villa ziko 300 na apartment ziko 7400. Mradi huu utakamilika mwaka 2018. Apartment zitakamilika mwaka 2017 na villa mwaka 2018. 
Ndani ya mji huu wa Dege Eco-Village wa kazi hawatahitaji kwenda popote kwasababu kila kitu kitakuwepo kama shule za watoto, kituo cha polisi, hospitali, supermarket, na kadhalika.
Wafanyakazi wa Dege Eco - Village wakiwahudumia wateja wao waliofika katika banda lao.
Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo Bw. Azhar Malik wa Dege eco-Village akibadilishana mawazo na mfanyakazi mwenzake.
Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo Bw. Azhar Malik wa Dege Eco-Village akiongea na mteja ambaye alikuwa akiweka kumbukumbu katika daftari la wageni waliofika banda la Dege Eco - Village ndani ya Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo Bw. Azhar Malik wa Dege Eco-Village akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
Wafanyakazi wa Dege Eco-Village wakiwa katika picha ya pamoja.
Wananchi wakionyeshwa mpangilio wa nyumba utakavyokuwa.
Muonekano wa banda la Dege Eco-Village.
Meneja Masoko na Mauzo wa Kampuni ya Dege Eco -Village Bw. Adam akiongea na waandishi wa habari kufafanua jambo. 
Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo Bw. Azhar Malik wa Dege Eco-Village akibadilishana mawazo na wateja waliofika katika banda lao.

MAKAMU WA RAIS AKUTANA NA MABALOZI WA NORWAY NA RWANDA

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Mohammed Gharib Bilal leo amekutana na mabalozi wa Norway na Balozi mteule wa Tanzania nchini Rwanda na kufanya nao mazungumzo ofisini kwake ikulu jijini Dar es Salaam.

Balozi wa Norway nchini Tanzania mheshimiwa Hanne Marie Kaarstad ndiye alikuwa wa kwanza kufanya mazungumzo na mheshimiwa Makamu wa Rais ambapo licha ya kufika kujitambulisha alimueleza mheshimiwa Makamu wa Rais kuwa atajitahidi kuimarisha uhusiano baina ya nchi hizi mbili katika kipindi chake kama Balozi na kwamba Tanzania ni nchi rafiki kwa Norway na akasisitiza kuzidi kuimarisha uhusiano hasa katika masuala ya utunzaji wa mazingira.

Kwa upande wake mheshimiwa Makamu wa Rais alimuelezea Balozi Hanne kuwa, Tanzania inajivunia uhusiano wake na Norway na kwamba uhusiano huo kwa sasa unazidi kuimarika na tena Tanzania inategemea kujifunza mengi toka Norway kutokana na nchi hiyo kuwa miongoni mwa nchi zenye teknolojia ya juu katika masuala ya gesi na mafuta.

Balozi Hanne ambaye aliwahi kufanya kazi nchini Tanzania pia alionesha kufurahishwa kwake na maendeleo ambayo Tanzania inapiga na akafafanua kuwa mji wa Dar es Salaam ni kiashiria kimojawapo kinachoonesha wazi kuwa Tanzania inakuwa kwa kasi.

Pia, Mheshimiwa Makamu wa Rais alimpokea Balozi Ali Said Siwa aliyepangiwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Rwanda na akamtaka Balozi huyo kuhakikisha anasaidia mahusiano baina ya nchi zetui kuzidi kuimarika huku akimsisitizia kuhusu uhusiano wetu kama majirani na pia wananchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Balozi Siwa alitumia nafasi hiyo kumshukuru Mheshimiwa Makamu wa Rais kwa uteuzi wake na akaahidi kuiwakilisha vema Tanzania nchini Rwanda.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Balozi wa Norway nchini Tanzania, Hanne Marie Kaarstad, wakati alipofika ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Septemba 22, 2014 kwa mazungumzo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Norway nchini Tanzania, Hanne Marie Kaarstad, (wa pili kulia) na ujumbe wake baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Septemba 22, 2014.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkaribisha Balozi wa Tanzania, nchini Rwanda, Mhe. Ali Said Siwa, wakati alipofika ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Septemba 22, 2014.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Balozi wa Tanzania, nchini Rwanda, Mhe. Ali Said Siwa, leo Septemba 22, 2014. Picha na OMR.

MSAMA AWASAIDIA WATOTO YATIMA JIJINI DAR

$
0
0
 Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions Ltd, Alex Msama akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla fupi ya kukabidhi misaada kwa vituo vya yatima jijini Dar es Salaam.
Watoto wa kituo cha Mwandaliwa cha Mbweni wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Kituo hicho, Halima Ramadhan wa tatu kulia.
 Watoto wa kituo cha Maunga cha Kinondoni wakiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu wa Kituo hicho, Rashid Mpinda (mwenye kofia).
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama (lushoto), akimkabidhi sehemu ya msaada wa vyakula Katibu Mkuu wa Kituo cha kulelea watoto wanaoishi katika mazingira magumu cha Maunga Center cha Kinondoni jijini Dar es Salaam, Rashid Mpinda.  Msaada huo wenye thamani ya sh. milioni 7 unatokana na mapato yaliyopatikana katika  tamasha la Pasaka na Krismasi. (Picha na Francis Dande) 
Mkurugenzi wa Kituo cha kulelea watoto wanaoishi katika mazingira magumu cha Mwandaliwa cha Mbweni nje Kidogo ya jijini la Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Kituo cha kulelea watoto wanaoishi katika mazingira magumu cha Mwandaliwa cha Mbweni nje Kidogo ya jijini la Dar es Salaam.
Msama akiwa amembeba mtoto anayelelewa katika kituo cha Tovichodo cha Temeke.
 Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama (lushoto), akimkabidhi sehemu ya msaada wa vyakula Katibu Mkuu wa Kituo cha kulelea watoto wanaoishi katika mazingira magumu cha Maunga Center cha Kinondoni jijini Dar es Salaam, Rashid Mpinda.  Msaada huo wenye thamani ya sh. milioni 7 unatokana na mapato yaliyopatikana katika  tamasha la Pasaka na Krismasi.

 Katibu Mkuu wa Kituo cha kulelea watoto wanaoishi katika mazingira magumu cha Maunga Center cha Kinondoni jijini Dar es Salaam, Rashid Mpinda akimshukuru Mkurugenzi wa Msama Promotions, Alex Msama kwa misaada aliyotoa.
 Msama akiwa amembeba mmoja wa watoto wanaolelewa katika kituo cha Maunga.
Watoto wakimshukuru Msama baada ya kuwapatia msaada wa vyakula mbalimbali.
 Mkurugenzi wa Kituo cha Tovichodo cha Temeke, Honoratha Michael akipokea sehemu ya msaada wa vyakula kutoka kwa Mkurugenzi wa Msama Promotions, Alex Msama.

Na Francis Dande 

KAMPUNI ya Msama Promotions Ltd ya jijini Dar es Salaam chini ya Mkurugenzi wake Alex Msama, juzi ilitoa misaada ya kiutu kwa vituo vitatu vya kulea yatima vya wilayani Kinondoni na Temeke.
Msaada huo ambao ni utekelezaji wa programu ya kampuni hiyo kama moja ya kurejesha sehemu ya faida itokanayo na uratibu wa matamasha ya muziki wa injili kwa jamii.

Msama Promotions Ltd ambayo pia ni waratibu wa tamasha la muziki wa injili la Pasaka na Krismas, si mara ya kwanza kwao kutoa misaada ya aina hiyo kwa vituo vua yatima na watu wengine wenye mahitaji kama wajane na wazee.

Vikundi vilivyonufaika na msaada huo Jumapili, ni kituo cha Kulea Watoto Yatima  cha Mwandaliwa cha Mbweni, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam na Maunga pia cha Kinondoni.

Aidha, misada hiyo imewafariji watoto yatima wa kituo cha Tovichido cha Wilayani Temeke akisema amefanya hivyo baada ya kuguswa na hali halisi inayowakabili.

Msama alitumia fursa hiyo pia kutoa wito kwa watu wenye uwezo, makampuni na taasisi mbalimbali kuona umuhimu wa kusaidia makundi hayo maalumu katika jamii  kwani nao wana haki ya kuishi na kufurahia maisha kama wengine.

Kwa upande wa misaada iliyokabidhiwa kwa vituo hivyo, ni mchele, sukari, unga, mafuta ya kula, chumvi, unga wa ngano na vingine vingi kwa ajili ya matumizi ya kila siku nyumbani, vyote vikiwa na thamani ya shilingi mil 7.

Akizungumza baada ya kupokea msaada huo, Katibu wa Kituo cha  Maunga, Rashid Mpinda   alitoa pongezi kwa Msama kutokana na misaada hiyo na kuwasihi wengine waige mfano huo wa kusaidia makundi maalum.

Akielezea changamoto zilizopo katika kituo hicho, Mpinda alisema ni kukosa uwezo wa kifedha kuwalipia ada watoto wanaosoma hadi kufukuzwa kwa kukosa karo, hivyo kushindwa kupata elimu.

Msama kwa upande wake alisema jukumu la karo za wanafunzi hao analibeba yeye pamoja na sare  kutokana na kuguswa kwake na kilio cha watoto hao.

WIKI YA NENDA KWA USALAMA BARABARANI YAZINDULIWA KITAIFA JIJINI ARUSHA LEO.

$
0
0
Washiriki wa maonesho, wananchi mbalimbali wakiwa katika maandamano ya kuadhimisha Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani iliyozinduliwa katika Kiwanja cha Mpira wa Amri Abeid jijini Arusha leo. Mgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mrongo aliyazindua maonesho hayo huku akiwataka madereva nchini wawe makini kwa kufuatia sheria za barabarani ili kuepuka ajali. Kauli mbiu ya Maadhimisho ya mwaka huu ni “Maamuzi yako Barabarani Hatma Yetu-Fikiri Kwanza”.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima (kushoto) akimpa zawadi ya ngao Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mrongo baada ya mgeni rasmi huyo kuyafungua Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani ambapo kwa mwaka huu maadhimisho hayo kitaifa yanafanya jijini Arusha. Kauli mbiu ya Maadhimisho ya mwaka huu ni “Maamuzi yako Barabarani Hatma Yetu-Fikiri Kwanza”.
Waendesha pikipiki (bodaboda) pia walishiriki kikamilifu katika uzinduzi wa maonesho hayo yaliyofanyika katika Kiwanja cha Mpira cha Amri Abeid, jijini Arusha leo. Kauli mbiu ya Maadhimisho ya mwaka huu ni “Maamuzi yako Barabarani Hatma Yetu-Fikiri Kwanza”.
Trafiki Makao Makuu jijini Dar es salaam, Mkaguzi Msaidizi, Yohana Mjema (kulia), akitoa maelezo kwa mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mrongo (watatu kushoto), namna ajali barabarani zinavyoweza kuepukika endapo watumiaji barabara watakuwa waangalifu kwa kufuata sheria za barabarani. Mkuu wa Mkoa aliyazindua maonesho hayo ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani katika Kiwanja cha Mpira Amri Abeid jijini Arusha leo. Wapili kushoto ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima, na kushoto ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Kamishna Msaidizi Mohamedi Mpinga.
Sajenti wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Damian Muheya (kulia) akiwaelimisha wananchi wa jijini Arusha jinsi mtungi mdogo wa kuzimia moto unavyotumika wakati moto unapotokea. Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani imezindulia leo na Mkuu wa Mkoa wa Arusha (Magesa Mrongo katika Kiwanja cha Mpira cha Amri Abeid jijini humo. Kauli mbiu ya Maadhimisho ya mwaka huu ni “Maamuzi yako Barabarani Hatma Yetu-Fikiri Kwanza”.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mrongo (katikati waliokaa), Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima (wanne kutoka kushoto-waliokaa) wakiwa na wajumbe wa usalama barabarani katika picha ya pamoja baada ya uzinduzi wa maonesho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani ambayo Kitaifa mwaka huu yanafanyika jiijini Arusha leo. Kauli mbiu ya Maadhimisho ya mwaka huu ni “Maamuzi yako Barabarani Hatma Yetu-Fikiri Kwanza”. Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

WENYEVITI WA BODI ZA TAASISI ZILIZO CHINI YA WIZARA MAWASILIANO WATIA SAINI MKATABA WA UTENDAJI NA WAZIRI MBARAWA

$
0
0
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia,Prof. Makame Mbarawa ameongoza zoezi la utiaji Saini Mkataba wa Utendaji baina yake na Wenyeviti wa Bodi za Taasisi zilizo chini ya Wizara kwa ajili ya utekelezaji wa majukumu ya Taasisi zao kwa mwaka wa fedha wa 2014/2015.

Lengo la Mhe. Waziri kuwekeana saini Mkataba wa Utendaji na Wenyeviti wa Bodi ni kufuatilia kwa karibu utekelezaji wa majukumu ya Wenyeviti wa Bodi hizo ili kuleta ufanisi na tija kwenye Sekta ya TEHAMA, Sayansi na Teknolojia ili iweze kuendelea kuchangia ukuaji wa uchumi na mchango wa sekta kwenye pato la Taifa.

Aidha, Mhe. Mbarawa alisema kuwa mapitio ya utekelezaji wa mkataba huo utafanyika kila baada ya miezi mitatu ili kufuatilia namna unavyotekelezwa na kubaini changamoto zinazowakabili wenyeviti wa Bodi za Taasisi zilizo chini ya Wizara kabla ya mwisho wa mwaka wa fedha wa 2014/2015.

Taasisi zilizo chini ya Wizara ni pamoja na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia, Kampuni ya Simu Tanzania, Shirika la Posta Tanzania, Taasisi ya Sayansi na Teknolojia, Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya, Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela, Tume ya Nguvu za Atomii Tanzania na Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote.
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia,Prof. Makame Mbarawa akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa Utiaji Saini Mkataba wa Utendaji baina yake na Wenyeviti wa Bodi za Taasisi zilizo chini ya Wizara kwa ajili ya utekelezaji wa majukumu ya Taasisi zao kwa mwaka wa fedha wa 2014/2015.
Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote,Prof. John Nkoma akiweka saini mkataba wa utendaji baina yake na Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia,Mhe. Prof. Makame Mbarawa kwa ajili ya utekelezaji wa majukumu ya Taasisi kwa mwaka wa fedha wa 2014/2015
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia,Mhe. Prof. Makame Mbarawa akipeana mkono na Prof. Nkoma baada ya kuwekeana saini mkataba.








Mradi wa TEDAP kutatua changamoto za upatikanaji wa umeme Jijini Dar

$
0
0
Meneja wa Miradi, Usambazaji na Usafirishaji kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Emmanuel Manderabona akiwaonesha waandishi wa habari mfumo wa usambazaji umeme kwenye Moja kituo cha Mradi “Tanzania Energy Development and Access Program (TEDAP)” unaofadhiliwa na Benki ya Dunia, kilichopo Mbagala kitakachozalisha megawatt 100 za umeme, kituo hiki kinatarajiwa kuanza kutoa huduma za umeme wa uhakika kwa wakazi wa maeneo ya Kurasini, Kigamboni, Mbagala na Maeneo ya Mkuranga kuanzia Mwezi Agosti, 2015.
Meneja wa Miradi, Usambazaji na Usafirishaji kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Emmanuel Manderabona akiwaonesha waandishi wa habari (hawapo pichani) moja ya Transfoma iliyopo katika eneo la Mradi Mbagala lenye MVA (MEGAVOLT-AMPERE) 50. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mhandisi Felchesmi Mramba.
Baadhi ya mafundi wakiedelea na kazi ya kusuka Transfoma iliyopo katika eneo la Mradi Mbagala lenye MVA (MEGAVOLT-AMPERE) 50.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mhandisi Felchesmi Mramba akiwaeleza waandishi wa Mikakati inayowekwa na shirika hilo ikiwemo kutekeleza miradi mbalimbali ya kuzalisha, kusafirisha na kusambaza Umeme ili kuhakikisha wanakabiliana na Tatizo la Umeme Nchini,wakati wa Ziara kwenye Mradi wa “Tanzania Energy Development and Access Program (TEDAP)” unaotekelezwa katika maeneo ya Mbagala, Gongo la Mboto na Kinyerezi, Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Assah Mwambene akiwaeleza waandishi wa habari kufurahishwa kwake na ziara hii iliyoratibiwa Wizara ya Habari, Vijana , Utamaduni na Michezo kwa kushirikiana na Shirika la umeme Tanzania (TANESCO) yenye lengo la kuona nini Shirika hilo linatekeleza katika jitihada za kukabiliana na Tatizo la Umeme Nchini.Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mhandisi Felchesmi Mramba.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Assah Mwambene akimweleza jambo Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mhandisi Felchesmi Mramba (kushoto) wakati wa ziara kwenye Miradi ya umeme Katika Eneo la Mbagala, Gongo la Mboto na Kinyerezi Jijini Dar es Salaam.
Afisa Uhusiano wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Bi. Neema Mbuja akiwaeleza jambo wahandisi Emmanuel Manderabona(Kushoto kwake) na Saimon Jilima, wakati wa ziara kwenye Miradi ya umeme Katika Eneo la Mbagala, Gongo la Mboto na Kinyerezi Jijini Dar es Salaam.
Meneja wa Miradi, Usambazaji na Usafirishaji kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Emmanuel Manderabona akiwaonesha waandishi wa habari mtambo wa kuongoza umeme uliopo katika eneo la Gongo la Mboto uliowekwa mfumo wa Sakiti Mzunguko (Ring Circuit) kwenda Mbagala, Sakiti Mzunguko ni Mzunguko mkubwa utakaotoa fursa ya upatikanaji wa umeme kwa muda wote kwani umeme ukikosekana eneo moja ni rahisi kuunganisha kwa kupitia upande wa pili na umeme ukaendelea kupatikana.
Mitambo Miwili iliyofungwa katika kituo cha KINYEREZI ONE yenye uwezo wa kuzalisha Megawatt 150 za umeme utakaogawanywa katika sehemu mbili kuingia katika gridi ya Taifa, ikiwa ni kujenga msongo wa kilovolt 220 kwenda Kimara na kujenga laini ya msongo wa kilovolt 132 kwenda Gongo la Mboto, Kituo hiki kitagharimu Dola za Kimarekani Milioni 183. (PICHA NA HASSAN SILAYO-MAELEZO)

TUNDA MAN ASINDIKIZA SHOW YA VIPAJI WAREMBO MISS TANZANIA BABATI MKOANI MANYARA

$
0
0
 Warembo 15 kati ya 30 wanaoshiriki shindano la Redds Miss Tanzania 2014 wakisindikizwa na mkali wa Bongo Fleva kutoka Jijini Dar es Salaam, Tunda Man, wametoa burudani kali wakati wa shindano dogo la awali la kumtafuta mrembo mwenye kipaji lililofanyika Babati Mkoani Manyara. Pichani juu ni washindi wa tano waliofanikiwa kuingia fainali ya shindano hilo la vipaji litakalofanyika jijini Dar es Salaam baada ya wengine 15 kufanyika Arusha mjini. 
 Msanii wa Bongo Fleva  Tunda Man akitoa burudani kwa wadau wa urembo Babati.
 Tunda Man aliburudisha vilivyo ukumbini hapo.
 Warembo hao walishindana vikali katika kucheza na kuimba miziki ya aina mbalimbali.Na Father Kidevu Blog.
 Jopo la majaji likifuatilia kwa makini shindano hilo
 Kila aina ya stile za uchezaji zilioneshwa na warembo hao jukwaani...
 Warembo wenzao waliobakia wakishangilia burudani ya vipaji kutoka kwa washiriki wenzao.
 wadau wa sanaa ya Urembo Babati wakifuatilia shindano hilo.
Mkuu wa Wilaya ya Hanang, Christina Mndeme aliye mwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Manyara, akiwa na waratibu wa show hiyo, Mzee Ally Sumaye (kushoto) na Mfanyabiashara Mohamad Bajwa.
 Ilikuwa ni shwangwe kwa warembo hao ambao wapo Mikoa yua Kaskazini kwa ziara ya kimafunzo katika hifadhi za Taifa.

NCHI ZA ME ZAWEKEZA ZAIDI KWENYE MAPAMBANO DHIDI YA UHALIFU MTANDAO

$
0
0
 Ukipitia takwimu za mwaka huu na mwaka jana inaonyesha Nchi za Ulaya na Marekani zimeendelea kuathirika zaidi na uhalifu mtandao, Huku Nchi za mashariki ya kati kuonekana kunyemelewa na wahalifu mtandao. Wakati huo huo takwimu zilitabiria Nchi za Afrika  kuwa katika hali mbaya baadae kutokana na ukuaji wa kasi wa matumizi ya mitandao ambao hauendani sanjari na maandalizi madhubuti ya usalama wa mitandao.

Mengi yalizungumzwa kuhusiana na tishio jipya katika nchi za kiarabu huku kampuni inayojihusisha na ulinzi mtandao ya Kaspersky wakiandika "NCHI YA SAUDI ARABIA" imedhamiriwa zaidi na wahalifu mtandao kauli ambayo iliambatana na "UTAFITI" ukibainisha kampuni za mashariki ya kati zimeendelea kulengwa na wahalifu mtandao.

Hatua hiyo ilisababisha nchi hizo za mashariki ya kati kuwekeza zaidi na kuimarisha jitihada zake za mapambano dhidi ya uhalifu mtandao. "JEDDAH" iliyoko Saudi Arabia ilianzisha kituo kipya kilicho imarishwa maalum kwa ajili ya mapambano dhidi ya uhalifu mtandao na Hivi karibuni "JORDAN" nao wakazindua kituo chao maalum kwa ajili ya kupambana na uhalifu mtandao.

Vile vile nchi nyingine za Mashariki ya kati (ME) zimeendelea kuwekeza na kufungua vituo maalum kwa ajili ya mapambano dhidi ya uhalifu mtandao katika ukanda huo ambapo imeenda sambamba na uboeshwaji wa sharia mitandao.

NINI TUNAJIFUNZA KAMA TAIFA?

Tayari imezoeleka nchi za ulaya na Marekani zimekua vinara kwenye kuwekeza katika mapambano dhidi ya uhalifu mtandao kutokana na athari kubwa ambayo tayari imesha ziona.Na hivi sasa inaonekana Nchi za Mashariki ya kati nazo zikiwekeza katika upande huo. 


Nchi za Afrika pia zimeendelea kujipanga na kkuwekeza kwenye sekta hii ambayo inaonekana kuwa tishiokubwa mapema baadae. Jitihada zilizopo zinapaswa kuendana sambamba na kuweka vizuri sharia mtandao huku itafutwa njia rafiki itakayofungua mipaka kwenye mapambano dhidi ya uhalifu huu mtandao ambao hauna Mipaka.


Maboresho ya mara kwa mara yanahitajika kwenye vituo maalum vya mapambano dhidi ya uhalifu mtandao pamoja na kuwa na mapitio ya sheria mtandao mara kwa mara kutokana na mabadiliko na ukuaji wa teknolojia inayochangia kasi ya uhalifu mtandao kuongezeka. Haya na mengine nimepata kuya ainisha  kwa kina kwenye andiko linaloweza kusomeka "HAPA"

NAIBU WAZIRI SILIMA AFUNGUA MKUTANO MKUU WA BARAZA LA TAIFA LA USALAMA BARABARANI JIJINI ARUSHA LEO

$
0
0
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na Mwenyekiti wa Baraza la Usalama Barabarani, Pereira Ame Silima akizungumza na Wajumbe wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani kutoka mikoa yote nchini katika mkutano wa baraza hilo ambao unajadili masuala mbalimbali ya jinsi ya kupunguza ajali za barabarani nchini. Kulia kwa Mwenyekiti ni Katibu wa Baraza hilo ambaye pia ni Kamanda wa Kikosi cha Polisi Usalama Barabarani nchini, Mohamed Mpinga. Mkutano huo ambao unaenda sambamba na Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani unafanyika katika hoteli ya Golden Rose jijini Arusha leo.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na Mwenyekiti wa Baraza la Usalama Barabarani, Pereira Ame Silima akizungumza na Wajumbe wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani kutoka mikoa yote nchini katika mkutano wa baraza hilo ambao unajadili masuala mbalimbali ya jinsi ya kupunguza ajali za barabarani nchini. Kushoto ni Katibu wa Baraza hilo ambaye pia ni Kamanda wa Kikosi cha Polisi Usalama Barabarani nchini, Mohamed Mpinga. Kulia ni Mwenyekiti wa Mafunzo na Uenezi wa Baraza hilo, Henry Bantu. Mkutano huo ambao unaenda sambamba na Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani unafanyika katika hoteli ya Golden Rose jijini Arusha leo.
Katibu wa Baraza la Usalama Barabarani ambaye pia ni Kamanda wa Kikosi cha Polisi Usalama Barabarani nchini, Mohamed Mpinga akizungumza na Wajumbe wa Baraza hilo kutoka mikoa yote nchini katika mkutano wa baraza hilo ambao unajadili masuala mbalimbali ya jinsi ya kupunguza ajali za barabarani nchini. Katikati ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na Mwenyekiti wa Baraza la Usalama Barabarani nchini, Pereira Ame Silima. Kulia ni Mwenyekiti wa Mafunzo na Uenezi wa Baraza hilo, Henry Bantu. Mkutano huo unaenda sambamba na Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani unafanyika katika hoteli ya Malaika Beach Resort jijini Mwanza leo.
Sehemu ya Wajumbe wa Baraza la Usalama Barabarani kutoka mikoa yote chini wakimsikiliza kwa makini Mwenyekiti wa Baraza hilo, Pereira Ame Silima (hayupo pichani) katika mkutano wa baraza hilo ambao unajadili masuala mbalimbali ya jinsi ya kupunguza ajali za barabarani nchini. Mkutano huo unaenda sambamba na Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani unafanyika katika hoteli ya Golden Rose jijini Arusha leo. Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

MPANGO WA AWAMU YA PILI WA UTEKELEZAJI WA MAENDELEO YA SEKTA YA MAJI WAZINDULIWA TANZANIA

$
0
0
Waziri wa Maji, Prof. Jumanne Maghembe na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia, Philippe Dongier wakikata utepe kuzindua rasmi Mpango wa Awamu ya Pili ya Utekelezaji wa Maendeleo ya Sekta ya Maji.
Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Inj. Mbogo Futakamba, akisoma hotuba katika uzinduzi rasmi wa Mpango wa Awamu ya Pili ya Utekelezaji wa Maendeleo ya Sekta ya Maji, akiwa na Waziri wa Maji, Prof. Jumanne Maghembe na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia, Philippe Dongier.
Waziri wa Maji, Prof. Jumanne Maghembe, akisoma hotuba katika uzinduzi wa Mpango wa Awamu ya Pili ya Utekelezaji wa Maendeleo ya Sekta ya Maji.
Baadhi ya Washirika wa Maendeleo wa Tanzania waliohudhuria hafla hiyo.
Baadhi ya Watumishi wa Wizara ya Maji.


Waziri wa Maji, Prof. Jumanne Maghembe,jana amezindua Mpango wa Awamu ya Pili wa Utekelezaji wa Maendeleo ya Sekta ya Maji, kwa kipindi kingine cha miaka 5 kuanzia Julai Mosi, 2014 mpaka Juni 30, 2019 katika Makao Makuu ya Wizara ya Maji, Ubungo baada ya kukamilika kwa Mpango wa Awamu ya Kwanza wa Utekelezaji wa Maendeleo ya Sekta ya Maji.

Uzinduzi huo ulihudhuriwa na Washirika wa Maendeleo, Watumishi kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI), Watumishi wa Wizara ya Maji na Taasisi zake.

“Tunapozindua Awamu ya Pili ya Programu hii, tunajivunia mafanikio ya Awamu ya Kwanza katika kuboresha usimamizi na uendelezaji wa rasilimali za maji kwa kuanzisha Bodi ya Taifa ya Maji na Bodi za Maji za Mabonde yote 9 nchini zenye wajumbe kutoka sekta mbalimbali.

Na pia, kuzijengea uwezo bodi hizo kwa kuzipatia watumishi pamoja na vitendea kazi katika kuhakikisha zinatekeleza majukumu yake ipasavyo”, alisema Waziri wa Maji, Prof. Jumanne Maghembe.

Aidha, Prof. Maghembe alisema kwamba ili kukabiliana na uharibifu wa vyanzo vya maji unaosababishwa na shughuli za kibinadamu, tumeandaa Programu Maalum ya Miaka 5 ya utunzaji na uhifadhi wa vyanzo vya maji kwa kushirikiana na wadau mbalimbali utakaoanza 2014/15.

Pia, Prof. Maghembe alisema kwamba katika kutekeleza Awamu ya Pili ya Maendeleo ya Sekta ya Maji chini ya utaratibu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Wizara imedhamiria kujenga miundombinu ya huduma bora za maji, usafi wa mazingira na vyoo kwenye maeneo yenye mikusanyiko ya watu wengi na kuendelea kutoa mafunzo na ushauri kwenye taasisi za umma na kaya zote za mijini na vijijini zijenge vyoo bora na kuzingatia usafi binafsi na mazingira.

Prof. Maghembe aliagiza kwamba zipewe kipaumbele kazi za usimamizi wa miradi inayotekelezwa, ikamilike ndani ya muda uliopangwa kwa mujibu wa mikataba na kuhakikisha kuwa miradi hiyo inalingana na thamani ya fedha iliyotumika.

Naye Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia, Philippe Dongier aliipongeza Wizara ya Maji kwa kutekeleza Awamu ya Kwanza ya Programu hii kubwa na kuridhishwa na maendeleo yake mazuri. Pia, alisema kwamba kwa niaba ya Washirika wenzake wa Maendeleo wanapendelea baadhi ya vipaumbele ikiwemo kuweka mpango maalum wa kuhakikisha vyanzo vya maji vinatunzwa ili kukabiliana na changamoto za uharibifu wa rasilimali za maji kwa ajili ya kupata maji ya kutosha.

Mpango wa Awamu ya Kwanza umefanikiwa kuongeza vituo vya kuchotea maji vijijini, kutoka vituo 44,738 vilivyokuwa vikifanya kazi mwaka 2007 hadi vituo 77,584 mwezi Juni, 2014 ambalo ni ongezeko la asilimia 78 ukilinganisha na lengo la awamu hii, ambalo lilikuwa ni kujenga vituo 41,900.

Vile vile, ongezeko la wateja wapya 236,541 waishio mjini, wenye makazi yenye jumla ya watu 2,700,000 sawa na asilimia 90 kwa kulinganisha na wateja 287,200 waliokuwa wamelengwa, wenye makazi yenye watu 3,000,000.

Mpango wa Utekelezaji wa Maendeleo ya Sekta ya Maji, ni mpango wa miaka 20 unaotekelezwa kwa awamu na ulizinduliwa rasmi na Rais wa Tanzania, Mh. Jakaya Kikwete, Julai Mosi, 2007 na unategemewa kukamilika ifikapo Juni, 2025.

Madhumuni makuu ya Programu hii ni kuhakikisha kuwa Sekta ya Maji inayafikia malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo ifikapo mwaka 2025, yenye dhima ya kuwapatia wakazi wote wa mijini huduma za maji safi na salama na kuwapatia huduma hizo wakazi wa vijijini kwa asilimia 90.

Awamu ya Pili ya Programu hii inakadiriwa kugharimu Dola za Marekani Trilioni 3.34, ambazo zitatokana na Bajeti ya Serikali kwa kuchangiwa na Washirika wa Maendeleo.

ZEE LA NYETI NA USHAURI MWANANA WA WASANII

$
0
0
Wasanii wamesisitizwa juu ya matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii kwani waandaaji wa matamasha na matukio mbalimbali ya kisanaa sehemu mbalimbali duniani wamekuwa wakiitumia katika kuwapa kazi.

Akizungumza kwenye Jukwaa la Sanaa lililofanyika mapema wiki hii kwenye Ukumbi wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) ulioko Ilala Sharif Shamba jijini Dar es Salaam, mdau wa Sanaa Henry Mdimu a.k.a Zee la Nyeti alisema kuwa ni jambo la kushangaza kuona wasanii wakitumia kurasa zao kuonesha mambo binafsi kama ya mapenzi na matusi wakati zinapaswa kutumika kwa ajili ya kazi zao za Sanaa na kuwasiliana na mashabiki wao.

Alisisitiza kwamba si kila kitu kinapaswa kuwekwa kwenye kurasa za kijamii za wasanii na kwamba lazima wasanii wajifunze kutenganisha maslahi au masuala yao binafsi dhidi ya yale ya wapenzi wao na kwamba Sanaa iko kwa ajili ya walaji na si wasanii pekee.

“Wasanii hawana budi kuelewa kuwa hawatengenezi sanaa au kurasa za mitandao ya kijamii kwa ajili yao. Wanaitengeneza ili kuwasiliana na mashabiki wao kuhusu kazi wazifanyazo na kutafuta fursa za masoko na kazi nje. Lazima waelewe mapromota wa kimataifa hutumia sana kurasa hizi katika kutoa fursa” alisisitiza Mdimu.

Aliongeza kwamba, msanii yeyote anayefanya kazi ya Sanaa kama kazi yake lazima afikirie kutumia mitandao hii ya kijamii kiweledi katika kujitangaza kwani kutokufanya hivyo ni bora kufanya kazi nyingine maana hiyo ndiyo njia kuu kwa sasa ya kujitangaza na kupata fursa za maonesho mbalimbali ya kimataifa kwa gharama nafuu.

Kwa upande wake Afisa Sanaa kutoka BASATA, Augustino Makame alisema kwamba Baraza limekuwa mstari wa mbele kusisitiza matumizi sahihi ya teknolojia za kupashana habari muiongoni mwa wasanii na kwamba sasa ni muda wa wasanii kuona umuhimu wa mitandao hii ya kijamii na kuitumia ipasavyo katika kukuza Sanaa zao.
Mdau wa Sanaa Henry Mdimu (Zee la Nyeti) (Kulia) akisisitiza umuhimu wa kuwa na mitandao ya kijamii kwa wasanii (hawapo pichani) katika Jukwaa la Sanaa la Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA). Kushoto ni Afisa Sanaa wa BASATA, Augustino Makame.
Afisa Habari wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Aristides Kwizela (Kulia) akisisitiza jambo kwa Wasanii (Hawako pichani) wakati wa Jukwaa la Sanaa lililofanyika mapema wiki kwenye Ukumbi wa Baraza hilo ulioko Ilala, Sharif Shamba jijini Dar es Salaam. Katikati ni mdau wa Sanaa Henry Mdimu na Afisa Sanaa wa Baraza hilo Augustino Makame.
Wadau wa Sanaa pamoja na Wasanii wakipata elimu kuhusu Nafasi ya Mitandao ya Kijamii katika Kukuza Sekta ya Sanaa kwenye mapema wiki hii kwenye Jukwaa la Sanaa la BASATA.

Tamasha la 33 la Sanaa Bagamoyo lazinduliwa kwa kishindo

$
0
0
 Mgeni rasmi ambaye pia ni Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki Mhe. Makongoro Nyerere (kushoto) akifuatilia maonyesho mbalimbali yaliyokua yakiendelea wakati wa uzinduzi wa Tamasha la 33 la Sanaa lililofanyika katika Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) jana, katikati ni Mtendaji mkuu TaSUBa Bw. Michael J. Kadinde na kulia ni Mkurugenzi Maendeleo ya Utamaduni Prof. Hermas Mwansoko.
 Mgeni rasmi ambaye pia ni Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki Mhe. Makongoro Nyerere kati akipiga ngoma kama ishara ya uzinduzi wa Tamasha la 33 la Sanaa lililofanyika katika Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) jana.
 Mgeni rasmi ambaye pia ni Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki Mhe. Makongoro Nyerere kulia akipokea zawadi ya picha kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya TaSUBa Bw. Ghonche Materego wakati wa uzinduzi wa Tamasha la 33 la Sanaa lililofanyika katika Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) jana. Picha hii imechorwa sura ya Mhe. Makongoro na msanii aliyefaamika kwa jina la Sunday Richard Kamangu.
Mgeni rasmi ambaye pia ni Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki Mhe. Makongoro Nyerere kushoto akimpa mkono wa pongezi msanii Sunday Richard Kamangu baada ya kupokea zawadi ya picha iliyochorwa na msanii huyo wakati wa uzinduzi wa Tamasha la 33 la Sanaa lililofanyika katika Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) jana.
Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi Joyce Fisoo kushoto, na Mkurugenzi Msaidizi Sanaa Bibi. Leah Kihimbi kulia wakifuatilia matukio mbalimbali yaliyokua yanaendelea wakati wa uzinduzi wa Tamasha la 33 la Sanaa lililofanyika katika Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) jana.
 Wasanii kutoka Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo wakitoa burudani  wakati wa uzinduzi wa Tamasha la 33 la Sanaa lililofanyika katika Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) jana.
Baadhi ya watazamaji wakifurahia mambo yalivyokua wakati wa uzinduzi wa Tamasha la 33 la Sanaa lililofanyika katika Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) jana. Picha zote na: Genofeva Matemu - MAELEZO

HAPA NI KATIKATI YA JIJI LA DAR KUKO HIVI,HUPO PEMBENI KUKOJE??

$
0
0
 Katika pita pita za Kamera ya Mtaa kwa Mtaa,leo imekatiza katika barabara ya India usoni kabisa mwa jengo la Haidary Plaza na kukutana na hali hii kama ionekanavyo pichani.hapa ni katikati kabisa ya mji wa Dar es Salaam ndani ya Halmashauri ya Manispaa ya Ilala.Je ni kweli kwamba hili halionekani??tunaomba kusikia maoni yenu Wadau.

PRESIDENT KIKWETE IN DIFFERENT ACTIVITIES IN NEW YORK

$
0
0
 President Jakaya Mrisho Kikwete greets Senator Chris Coons of Delaware who paid a courtesy call on him in New York in the sidelines of the UN General Assembly 
  President Jakaya Mrisho Kikwete invites  Senator Chris Coons of Delaware and Chairman of  Perdue Farms Mr Jim Perdue who paid a courtesy call on him in New York in the sidelines of the UN General Assembly 
 President Jakaya Mrisho Kikwete in talks with  Senator Chris Coons of Delaware and Chairman of  Perdue Farms Mr Jim Perdue and their delegation who paid a courtesy call on him in New York in the sidelines of the UN General Assembly 
 President Jakaya Mrisho Kikwete bids farewell to Senator Chris Coons of Delaware who paid a courtesy call on him in New York in the sidelines of the UN General Assembly 
 President Jakaya Mrisho Kikwete chats with President Zuma of South Africa and First Lady Bongi Ngema-Zuma during a reception of the occasion of 20 years of Freedom and Democracy of South Africa held at the River Club 447 in New York.

  President Jakaya Mrisho Kikwete chats with President Zuma of South Africa and First Lady Bongi Ngema-Zuma during a reception of the occasion of 20 years of Freedom and Democracy of South Africa held at the River Club 447 in New York
 President Jakaya Mrisho Kikwete greets American civil rights activist and Baptist minister  Rev. Jesse Louis Jackson, Sr during a reception of the occasion of 20 years of Freedom and Democracy of South Africa held at the River Club 447 in New York
 President Jakaya Mrisho Kikwete chats with Mama Graca Machel when they met in Washington DC
 President Jakaya Mrisho Kikwete makes his keynote speech for the 3rd Bunengi African First Ladiues Discussion of Science, Technology, engineering and Mathematics (STEM) in New York
 President Jakaya Mrisho Kikwete makes his keynote speech for the 3rd Bunengi African First Ladiues Discussion of Science, Technology, engineering and Mathematics (STEM) in New York.STATE HOUSE PHOTOS

DKT. SHEIN MGENI RASMI KATIKA SHEREHE ZA ELIMU BILA MALIPO AMAAN ZANZIBAR LEO

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na Walimu na Wanafunzi katika Sherehe za Miaka 50 ya Elimu bila malipo zilizofanyika kitaifa katika Uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimkabidhi kombe Msaidizi Afisa Elimu Mkoa wa Kaskazini Unguja Maulid Nafasi Juma wakati wa Sherehe za Miaka 50 ya Elimu bila malipo zilizofanyika kitaifa katika Uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja leo.
Baadhi ya Viongozi waliohudhuria katika sherehe za miaka 50 ya Elimu bila Malipo zilizofanyika katika uwanja wa Amaan Studium na mgeni rasmi alikuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein.
Baadhi ya walimu wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein wakati alipokuwa akizungumza na Walimu, Wazee,Wanafunzi katika sherehe za kilele cha miaka 50 ya Elimu bila Malipo zilizofanyika leo katika Uwanja wa Amaan Studium Mjini Zanzibar.
Wanafunzi wenye ulemavu tofauti wakipita mbele ya mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein kwa maandano wakati wa sherehe za miaka 50 ya Elimu bila Malipo zilizofanyika katika uwanja wa amaan Studium.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiwapungia mkono wanafunzi waliopita mbele ya jukwaa la viongozi katika uwanja wa Amaan Studium Mjini Zanzibar wakati wa sherehe za kilele cha miaka 50 ya Elimu bila Malipo zilizofanyika leo.
Walimu na Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Taifa SUZA wakipita mbele ya mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein wakati wa maandamo ya kusherehekea kilele cha miaka 50 ya Elimu bila malipo ilizofanyika katika uwanja wa amaan Studium.
Wanafunzi wa Chuo cha Ufundi JKU wakipita mbele ya mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akipokea maandamano ya wanafunzi wa skuli mbali mbali za Unguja na Pemba katika sherehe za miaka 50 ya Elimu bila malipo zilizofanyika kitaifa katika uwanja wa Amaan Studium leo.
Wanafunzi wa Skuli ya wanawake ya Al- Ihsaan ya Magogoni Jitmai wakipita mbele ya mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akipokea maandamano ya wanafunzi wa skuli mbali mbali za Unguja na Pemba katika sherehe za miaka 50 ya Elimu bila malipo zilizofanyika kitaifa katika uwanja wa Amaan Studium leo.
Baadhi ya wanafunzi wa Skuli mbli mbli za Sekondari wakiwa katika jukwaa wakati wa sherehe za Miaka 50 ya Elimu bila malipo zilizofanyika kitaifa katika Uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja leo.[Picha na Ramadhan Othman Ikulu.]

FREE WRISTBANDS FOR CLUBS, NIGHT CLUBS AND SOCIAL

Ndovu Special Malt yakabidhi vifaa vitakavyosaidia kukabiliana na Ujangili katika Hifadhi za Wanyama nchini

$
0
0

 Meneja wa Bia ya Ndovu Special Malt,Pamela Kikuli akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya muendelezo wa harakati zake za kusaidia kuimarisha ulinzi wa Wanyama aina ya Tembo ili wasiuwawe hapa nchini,ikiwa ni Bia iliyobeba jina la Mnyama huyo,ambapo wametoa vifaa mbali mbali vya kusaidia ulinzi huo,ikiwa ni pamoja na Darubini kubwa (Binoculars) na trimble GPS ambazo zitasaidia katika harakati za kupambana na ujangili katika mbuga za wanyama nchini.Kulia ni Meneja Mawasiliano wa TANAPA,Pascal Shelutete.
 Meneja Mawasiliano wa TANAPA,Pascal Shelutete akizungumza na waandishi wa habari kwenye Mkutano uliofanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa TBL jijini Dar es Salaam,ikiwa ni pamoja na upokeaji wa vifaa kutoka kwa bia ya Ndovu Special Malt.Kulia ni Meneja wa Bia ya Ndovu,Pamela Kikuli
 Mkuu wa Idara ya Ulinzi katika hifadhi ya Serengeti,Agricola Lihiru akielezea namna ya matumizi ya vifaa hivyo na faida yake katika kupambana na ujangili kwenye hifadhi za wanyama nchini.
Meneja wa bia ya Ndovu Special Malt,Pamela Kikuli akikabidhi baadhi ya vifaa hivyo kwa Meneja Mawasiliano wa TANAPA,Pascal Shelutete na Mkuu wa Idara ya Ulinzi katika hifadhi ya Serengeti,Agricola Lihiru.

DK. TIZEBA ATOA MISAADA KWA WAHANGA WA MOTO JIMBONI KWAKE

$
0
0
SAM_0783
Naibu Waziri wa Uchukuzi ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Buchosa, Dk Charles Tizeba akipanda boti kuelekea kisiwa cha Nyamango kulikotokea ajali ya moto kwa ajili ya kukabidhi misaada.

Na Daniel Makaka, Sengerema
NAIBU Waziri wa Uchukuzi ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Buchosa Dk Charles Tizeba ametoa msaada kwa wahanga wa ajali ya moto na nyumba zilizoezuliwa na mvua ya upepo katika kisiwa cha Nyamango kijiji cha Lushamba kata ya Bulyaheke jimbo la Buchosa wilayani Sengerema mkoa wa Mwanza.

Misaada aliyoitoa kwa wahanga hao ni Blanketi mia tatu na Magunia manne ya Unga wa Mahindi na moja la Maharagwe vyote vyenye thamani ya shilingi million tatu na laki tano ambavyo vimetolewa kwa kaya hamsini na moja ambazo zilikumbwa na janga hilo Septemba 19 na 20 mwaka huu.

Akikabidhi misaada hiyo Dk Tizeba aliwataka viongozi kuhakikisha misaada hiyo inawafikia walengwa na siyo vinginevyo lakini pia aliwaasa wahanga hao hao kutumia misaada kwa lengo la kuwasaidia wakati kamati ya maafa wilaya ya Sengerema ikiwa bado inaendelea kufanya tathimini il iione namna ya kuwasaidia.
SAM_0723
Naibu Waziri wa Uchukuzi ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Buchosa, Dk Charles Tizeba akiwa ndani ya boti kuelekea kukabidhi misaada katika kisiwa cha Nyamango jimboni kwake.

…..Serikali itaendelea kusaidia kadri iwezavyo si kwamba watapewa fidia bali ni misaada tu.

Awali Katibu wa kamati ya maafa wilaya Sengerema Bw. Benard Myatilo akitoa taarifa ya wahanga wa tukio hilo alisema kuwa matukio hayo yalitokea kwa nyakati tofauti ambapo Septemba 19 majira ya saa nane usiku kaya 40 ziliteketea kwa moto na chanzo cha moto huo ni kulipuka kwa Kibatari ndani ya nyumba na tukio la pili kaya 11 kuezuliwa na mvua ilyoambatana na upepo likiwemo jengo la kanisa Katoliki kisiwani humo.

Pia alisema kati ya wahanga hao hakuna mtu aliyejeruhiwa katika matukio hayo licha mali zote zlizokuwemo kuteketea ambapo hadi sasa kaya saba hazina mahali pakuishi huku zilizobaki zikihifadhiwa na baadhi ndugu na jamaa wanaoishi katika kisiwa hicho.
SAM_0749
Muonekano wa baadhi ya nyumba zilizoteketea kwa moto katika kisiwa cha Nyamango wilayani Sengerema mkoa wa Mwanza.
SAM_0750
SAM_0753
Kanisa la Roman Katoliki katika kisiwa cha Nyamango lililoezuliwa na upepo ulioambatana na mvua.
SAM_0775
Naibu Waziri wa Uchukuzi ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Buchosa, Dk Charles Tizeba (mwenye suti ya kijivu) akikabidhi misaada ya mablanketi 300 kwa Mwenyekiti wa kijiji cha Lushamba, Deus Bitulo (kulia kwa naibu waziri) huku Mwenyekiti wa CCM tawi la Nyamango, Japhet Kafula akishuhudia tukio hilo.

TMK FAMILY na Mkubwa na Wanawe Yamoto Band watoa Msaada katika wodi ya watoto Hospitali ya Temeke

$
0
0
 Timu nzima ya TMK Family na Mkubwa na Wanawe Yamoyo Band chini ya uongozi wake Said Fella (mwenye shati la draft) wakiwa kwenye picha ya pamoja wakati walipofika kwenye Hospitali ya Temeke jijini Dar es Salaam,kwa lengo la kutoa Msaada wa bidhaa mbali mbali wa watoto wanaotibiwa katika Hospitali hiyo.TMK Family na Mkubwa na Wanawe Yamoyo Band walifanya hivyo ikiwa ni sehemu ya kugawana kile kidogo wanachokipata na jamii inayowazunguka.
 Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya,Mh. Temba akiwa amebeba moja ya mabox ya bidhaa walizozikabidhi hospitalini hapo.
 Kiongozi wa Bendi iliyochipukia hivi karibuni na kufanya vyema katika tasnia ya muzini ifahamikayo kama Yamoto Band,Dogo Asley nae hakuwa nyuma katika zoezi hilo.
 Mh. Temba na mtoto akimpatia mmoja wa watoto waliolazwa hospitalini hako moja ya bidhaa walizokuwa nazo.
 Msanii Chegge pia akifanya hivyo.
 Kiongozi wa TMK Family na Mkubwa na Wanawe Yamoyo Band,Mkubwa Said Fella akikabidhi sehemu ya misaada hiyo kwa Wauguzi wa Hospitali ya Temeke ikiwa ni mchango wao kwa Jamii inayowazunguka.

Airtel yatoa vitabu kwa shule ya sekondari Shibula Mwanza

$
0
0
Wanafunzi wa shule ya sekondari ya Shibula iliyoko Mkoani Mwanza wamefaidika na vitabu kupitia mradi wa Airtel shule yetu ambapo Airtel imetoa msaaada wa vitabu vya sayansi vyenye thamani ya shilingi milioni moja na Laki tano vitakavyowawezesha wanafunzi hao kupata elimu bora.

Kwa zaidi ya miaka 10 sasa mpango huu wa Airtel shule yetu umekuwa ukisaidia shule za sekondari kwa kuwapatia nyenzo muhimu kma vile vitabu, vifaa za kufundishia , madawati, kuboresha majengo ya shule lengo likiwa ni kuboresha ubora katika kutoa elimu nchini.

Akiongea wakati wa hafla ya kikuabithi vitabu Meneja Mauzo wa Airtel kanda ya Ziwa Bwana Raphael Daudi alisema “ Airtel imewekeza kiasi cha kutosha katika kusaidia malengo mkakatika katika sekta ya elimu kwa kushirikiana na serikali katika kutoa elimu bora. Kwa kupitia mradi wa Airtel Shule yetu tumeweza kuzifikia shule zaidi ya 1000 zilizoko katika maeneo mbalimbali nchini kwa kuwapatia vifaa vya kujisomea na kupunguza changamoto za uhaba wa vitabu huku tukifanikiwa kupunguza uwiano wa kitabu kwa mtoto kutoka watoto 6 kwa kitabu kimoja hadi watoto 2 kwa kitabu kimoja.

Leo tunatoa vitabu vya masomo ya sayansi ikiwemo Hisabati Fizikia, Kemia na Baiologia kwa shule ya Shibula sekondari tukiamini utachangia katika kuongeza kiasi cha ufaulu na kuchochea wanafunzi wengi kujiunga na masomo ya sayansi. Tutaendelea na jitihada hizi katika kuboresha sekta ya elimu na kuhakikisha tunazifikia shule nyingi zaidi nchini aliongeza Daudi.

Kwa upande wake Afisa Elimu Sekondari Manispaa ya Ilemema Mkoani Mwanza Juma Kasandiko ameishukuru Airtel kwa msaada wa vitabu kwa shule za sekondari zilizoko mwanza na kuwaasa wanafunzi kutumia muda wao kujisomea na kuacha tabia ya utoro shuleni na kwa kufanya hivyo kutasaidia kuongeza ufaulu wa wanafunzi shuleni hapo na Mwanza kwa ujumla.

Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa shule ya sekondari ya Shibula Bwana James Elias Chitanda alisema” Napenda kuwashukuru Airtel kwa kutoletea msaada huu wa vitabu shule ni hapa, vitabu ni nyenzo muhimu katika kuongeza maarifa na ujuzi hivyo vitabu hivi vitasaidia kuhamasisha wanafunzi wengi kujisomea na kuongeza upeo, vitawasadia walimu kuandaa masomo yao na kuwahamasisha wanafunzi wengi kujiunga na masomo ya sayansi na kuongeza idadi ya wanasayansi kwa ujumla.

Tunatoa wito kwa makampuni mengine kujiunga na kuchangia katika sekta ya elimu kwani ina mahitaji na changamoto nyingi.
Afisa Elimu Sekondari Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza Juma Kasandiko (kulia) akimkabithi vitabu mkuu wa shule ya shule ya Sekondari Shibula James Chisanda vilivyotolewa na Airtel chini ya mpango wake wa Airtel Shule yetu.
Waalimu wa shule ya Sekondari Shibula wakifurahia vitabu mara baada ya kampuni ya simu za mkononi ya Airte kukabithi vitabu hivyo chini ya mpango wake wa Airtel shule yetu ambapo shule hiyo imepokea vitabu vya masomo ya sayansi vyenye thamani ya shilingi millioni moja na Laki tano
Wanafunzi wa shule ya Sekondari Shibula wakifurahia vitabu vya sayansi walivyokabidhiwa na Kampuni ya simu za Mkononi ya Airtel, chini ya mpango wa Airtel shule yetu Airtel ilikabithi vitabuvya sayansi vyenye thamani ya shilingi millioni moja na nusu kwa shule hiyo
Viewing all 40137 articles
Browse latest View live
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>