↧
MZIGO WA JIWEE...
↧
OFISI BUBUZZ...MTAANI KWETUU..
↧
↧
LOWASSA AHUDHURIA MKUTANO WA BARAZA KUU LA CHAMA CHA WANANCHI CUF, JIJINI DAR LEO

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akiwapungua Wanachama na Wafuasi wa Vyama UKAWA waliofurika kwenye Makao Makuu ya CUF.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akikumbatiana na Mgombea Urais wa Zanzibar wa UKAWA kupitia Chama cha Wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, kabla ya kuelekea kwenye Makao Makuu Chama cha Wananchi CUF, Buguruni jijini Dar es salaam leo August 9, 2015, kulikofanyika Mkutano wa Baraza Kuu la Chama cha Wananchi CUF.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa na Mgombea Urais wa Zanzibar wa UKAWA kupitia Chama cha Wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad na Wenyeviti wenza wa UKAWA, Mh. James Mbatia na Dkt. Emmanuel Makaidi wakitembelea kuelekea Makao Makuu Chama cha Wananchi CUF, Buguruni jijini Dar es salaam leo August 9, 2015, kulikofanyika Mkutano wa Baraza Kuu la Chama cha Wananchi CUF.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa na Mgombea Urais wa Zanzibar wa UKAWA kupitia Chama cha Wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, wakiwapungia wafuasi wa Vyama vinavyounda UKAWA wakati wakielekea kwenye Makao Makuu Chama cha Wananchi CUF, Buguruni jijini Dar es salaam leo August 9, 2015, kulikofanyika Mkutano wa Baraza Kuu la Chama cha Wananchi CUF. Wengine walioambatana nao ni Wenyeviti wenza wa UKAWA, Mh. James Mbatia na Dkt. Emmanuel Makaidi.
Sehemu ya Wafuasi na Wanachama wa Chama cha Wananchi CUF, wakiwa wamejipanga Barabarani tayari kwa kumlaki, Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, alipokuwa akielekea Makao Makuu Chama cha Wananchi CUF, Buguruni jijini Dar es salaam leo August 9, 2015, kulikofanyika Mkutano wa Baraza Kuu la Chama cha Wananchi CUF. PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI.
Sehemu ya Viongozi wakuu wanaounda UKAWA, wakiongozwa na Mgombea Urais wa Zanzibar wa UKAWA kupitia Chama cha Wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, Mwenyekiti wa Chama cha NCCR - Mageuzi, Mh. James Mbatia, Mwenyekiti wa Chama cha NLD, Dkt. Emmanuel Makaidi, wakimsuburia Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa.

Umati wa Watu ukiwapokea Viongozi wao.
Umati nje ya Makao Makuu ya CUF.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akiwapungia mkono wafuasi wa Vyama vinavyounda UKAWA wakati wakielekea kwenye Makao Makuu Chama cha Wananchi CUF, Buguruni jijini Dar es salaam leo August 9, 2015, kulikofanyika Mkutano wa Baraza Kuu la Chama cha Wananchi CUF.
Mgombea Mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt. Juma Haji Duni akiwasili kwenye Makao Mkuu ya CUF.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akisalimiana na Mgombea Mwenza wake, Dkt. Juma Haji Duni.
Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF na Mgombea Urais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad akiwahutumbia maelfu ya wanachama na wafuasi wa Vyama vinavyounda UKAWA, nje ya jengo la Makao Makuu Chama cha Wananchi CUF, Buguruni jijini Dar es salaam leo August 9, 2015, kabla ya kufanyika Mkutano wa Baraza Kuu la Chama cha Wananchi CUF.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Freeman Mbowe akiwahutumbia maelfu ya wanachama na wafuasi wa Vyama vinavyounda UKAWA, nje ya jengo la Makao Makuu Chama cha Wananchi CUF, Buguruni jijini Dar es salaam leo August 9, 2015, kabla ya kufanyika Mkutano wa Baraza Kuu la Chama cha Wananchi CUF.
Mwenyekiti wa Chama cha NCCR - Mageuzi,Mh. James Mbatia akiwahutumbia maelfu ya wanachama na wafuasi wa Vyama vinavyounda UKAWA, nje ya jengo la Makao Makuu Chama cha Wananchi CUF, Buguruni jijini Dar es salaam leo August 9, 2015, kabla ya kufanyika Mkutano wa Baraza Kuu la Chama cha Wananchi CUF.
Mgombea Mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt. Juma Haji Duni akiwahutumbia maelfu ya wanachama na wafuasi wa Vyama vinavyounda UKAWA, nje ya jengo la Makao Makuu Chama cha Wananchi CUF, Buguruni jijini Dar es salaam leo August 9, 2015, kabla ya kufanyika Mkutano wa Baraza Kuu la Chama cha Wananchi CUF.
Mwanasheria wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Tundu Lissu akiwahutumbia maelfu ya wanachama na wafuasi wa Vyama vinavyounda UKAWA, nje ya jengo la Makao Makuu Chama cha Wananchi CUF, Buguruni jijini Dar es salaam leo August 9, 2015, kabla ya kufanyika Mkutano wa Baraza Kuu la Chama cha Wananchi CUF.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akiwahutumbia maelfu ya wanachama na wafuasi wa Vyama vinavyounda UKAWA, nje ya jengo la Makao Makuu Chama cha Wananchi CUF, Buguruni jijini Dar es salaam leo August 9, 2015, kabla ya kufanyika Mkutano wa Baraza Kuu la Chama cha Wananchi CUF.
Mwenyekiti wa Chama cha NLD, Dkt. Emmanuel Makaidi akimpongeza Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa mara baada ya kuhutubia.
Wakielekea kwenye Mkutano wa Baraza Kuu la Chama cha Wananchi CUF.
Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF na Mgombea Urais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, akiwa pamoja na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Freeman Mbowe, Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, Mgombea Mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt. Juma Haji Duni pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Mh. Magdalena Sakaya wakati wa Mkutano wa Baraza Kuu la Chama hicho, uliofanyika August 9, 2015, kwenye Makao Makuu Chama cha Wananchi CUF, Buguruni jijini Dar es salaam.
Sehemu ya Wajumbe wa Mkutano wa Baraza Kuu la Chama cha Wananchi CUF.
↧
RAIS KIKWETE AZINDUZA KIVUKO CHA MV MAFANIKO NA KUZINDUA MRADI WA NYUMBA ZA NHC MKOANI MTWARA LEO
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa,Ndugu Nehemia Mchechu akizungumza jambo na Rais Dkt Jakaya Kikwete mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa nyumba 30za makazi zinazojengwa na NHC Shangani mkoani Mtwara zenye thamani ya shilingi bilioni 4.4,Kulia ni Waziri wa Ujenzi na Mgombea Urais mteule wa chama cha CCM,Dkt John Pombe Magufuli wakiondoka eneo la tukio mapema leo mchana
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa,Ndugu Nehemia Mchechu akizungumza jambo na Rais Dkt Jakaya Kikwete mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa nyumba 30za makazi zinazojengwa na NHC Shangani mkoani Mtwara zenye thamani ya shilingi bilioni 4.4,Kulia ni Waziri wa Ujenzi na Mgombea Urais mteule wa chama cha CCM,Dkt John Pombe Magufuli wakiondoka eneo la tukio mapema leo mchana.
Sehemu kivuko hicho kilichozinduliwa Rais Dkt Jakaya Kikwete mapema leo mkoani Mtwara.
Naibu Waziri wa Fedha Mh.Mwigulu Nchemba akiteta jambo na Waziri wa Ujenzi Mh.John Pombe Magufuli kabla ya uzinduzi wa Kivuko cha Mv Mafanikio mkoani Mtwara mapema leo mchana
Waziri wa Ujenzi Dkt John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Rais Jakaya Kikwete kabla ya uzinduzi wa kivuko cha Mv Mafanikio mkoani Mtwara mapema leo mchana,kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mh.Fatma Salum Ali.
Rais Dkt Jakaya Kikwete akizungumza jambo na Naibu Waziri wa Fedha,Mh Mwigulu Nchemba ambaye pia alihudhuria sherehe hizo fupi uzinduzi wa kivuko cha Mv Mafanikio mkoani Mtwara mapema leo mchana
Rais Kikwete akizindua rasmi kivuko cha MV Mafanikio kwenye pwani ya mji wa Mtwara kitachofanya safari kutokea Msemo kuelekea Msangamkuu muda huu mkoani Mtwara.
Rais Dkt.Jakaya Kikwete akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa kivuko cha Mv Mafanikio kwenye pwani ya mji wa Mtwara kitachofanya safari kutokea Msemo kuelekea Msangamkuu muda huu mkoani Mtwara.Kivuko cha MV Mafanikio kina uwezo wa kubeba watu 100 na magari sita,chenye jumla ya thamani ya shilingi bilioni 3.3
Rais Dkt.Jakaya Kikwete akiwa ameambatana Waziri wa Ujenzi Dkt John Pombe Magufuli mara baada kushuka kwenye kivuko cha Mv Mafanikio katika kata ya Msanga Mkuu-Mtwara vijijini mara baada ya kuzinduliwa na Rais Jakaya Kikwete,kivuko hicho kina uwezo wa kubeba watu 100 na magari sita,chenye jumla ya thamani ya shilingi bilioni 3.3
Rais Dkt.Jakaya Kikwete akiwapungia mkono wananchi wa Msanga Mkuu-Mtwara vijijini waliofika kwenye uzinduzi wa kivuko cha MV Mafanikio chenye uwezo wa kubeba watu 100 na magari sita,chenye jumla ya thamani ya shilingi bilioni 3.3
Baadhi ya wananchi wa Msanga Mkuu-Mtwara vijijini wakishangilia jambo mara baada ya kivuko cha MV Mafanikio chenye uwezo wa kubeba watu 100 na magari sita,chenye jumla ya thamani ya shilingi bilioni 3.3 kuzinduliwa na Rais Dkt Jakaya Kikwete mapema leo mchana mkoani Mtwara.
Waziri wa Ujenzi na Mgombea Urais wa chama cha Mapinduzi,Dkt Jonh Pombe Magufuli akizungumza jambo mbele ya wananchi wa Msanga Mkuu-Mtwara vijijini baada ya uzinduzi wa kivuko cha MV Mafanikio chenye uwezo wa kubeba watu 100 na magari sita,chenye jumla ya thamani ya shilingi bilioni 3.3,Dkt Magufuli amesema kuwa Rais Jakaya Kikwete katika utawala wake ndani ya maiaka kumi amefanikiwa kujenga vivuko vipya 15 na vingine 7 vimekwishakarabatiwa na vinafanya kazi mpaka sasa
Rais Dkt.Jakaya Kikwete akizungumza jambo mbele ya wananchi wa Msanga Mkuu-Mtwara vijijini kuzindua kivuko cha MV Mafanikio chenye uwezo wa kubeba watu 100 na magari sita,chenye jumla ya thamani ya shilingi bilioni 3.3
Bango la mradi huo
Mkuruegenzi Mkuu wa NHC,Nehemia Mchechu akizungumza jambo mbele ya mgeni rasmi Rais Dkt Jakaya Kikwete pamoja na viongozi mbalimbali wa serikali na wananchi kwa ujumla katika mradi wa ujenzi wa nyumba 30 za makazi zinazojengwa na NHC Shangani mkoani Mtwara zenye thamani ya shilingi bilioni 4.4,
Rais Jakaya Kikwete akiweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa nyumba 30 za makazi zinazojengwa na NHC Shangani mkoani Mtwara zenye thamani ya shilingi bilioni 4.4,kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa,Ndugu Nehemia Mchechu pamoja na Waziri wa Ujenzi na Mgombea Urais mteule wa chama cha CCM,Dkt John Pombe Magufuli akishuhudia tukio hilo.
PICHA NA MICHUZI JR-MTWARA
↧
SKULI BODA BODA HUKU KWETU NANIHII
↧
↧
TANZIA: MBUNGE AFARIKI DUNIA AJALINI MKOANI MTWARA LEO
Taarifa iliyotufikia hivi punde inaeleza kuwa Aliyekuwa Mbunge wa Viti maalumu kupitia Chama cha Wananchi CUF, Mh. Clara Mwatuka, amefariki dunia jioni ya leo kwa ajali baada ya gari lake alilokuwa akisafiria kupinduka lilipokuwa linashuka eneo la Makonde Plateu kuja Ndanda.
Gari ilikuwa inaendeshwa na dereva wake,ambaye inasemekana ni mwanae.Maiti ipo Hospitali ya Rufaa ya Ndanda, Mkoani Mtwara.
Mwenyezi Mungu aiweke Roho yake mahala pema Peponi
-Amin.
↧
RADIO 5 YASHINDA NAFASI YA KWANZA MAONYESHOA YA NANENANE ARUSHA
Kituo cha Radio 5 kilichopo jijini Arusha kimeshika nafasi ya kwanza katika maonyesho ya nanenane kwa upande wa Radio na wapili katika sekta nzima ya mawasiliano katika kilele cha sherehe za sikukuu ya Wakulima nanenane na maonyesho ya kilimo Kanda ya Kaskazini yaliyofanyika katika uwanja wa maonyeshoThemi Mkoani Arusha
Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa kikombe na mgeni rasmi Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Sera Mahusiano na Uratibu Dkt.Mary Nagu Meneja masoko na mawasiliano Sarah Lazaro Keiya alisema kuwa wanafuraha kubwa kwa kupata ushindi huo
Alisema kuwa Radio 5 imekuwa ikiwapa kipaumbele wakulima ambapo wamekuwa wakiandaa vipindi vya kilimo ambapo katika studio zao huwaalika wataalamu mbalimbali wa kilimo lengo ni kuwapa elimu kuhusu kilimo cha kisasa.
Pia Radio hiyo imekuwa ikiwapatia wakulima msaada wa mbegu,mbole na wamekuwa wakiwatembelea mara kwa mara kujua maendeleo yao katika masuala ya kilimo.
“Vipindi vyetu vya kilimo vimekuwa vikitupa tuzo mbalimbali nah ii leo katika maonyesho haya pia tumepata tuzo”alisema Keiya.
Aidha alisema kuwa wamekuwa wakitoa zawadi kila mwaka kwa mkulima bora atakayechaguliwa na TASO ambapo wametoa pikipiki aina ya powew king yenye thamani ya shilingi milioni mbili,mbole pamoja na mbegu
Hata hivyo alitoa shukrani zake kwa mkurugenzi wa kituo hicho Bw,Robert Francis kwa kuwawezesha wafanyakazi kufanya vizuri katika maonyesho hayo huku akisema kuwa anatimu nzuri inayojituma na yenye uwezo mkubwa kikazi.
Aliwashukuru wadhamini SBs(pepsi),Kishen enterprises limited,Upendo kwa mama foundation,Grandmaster records,Atown records na wote waliojitokeza kushirikiana nao
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Sera Mahusiano na Uratibu Dkt.Mary Nagu akiwa anamkabidhi kikombe Meneja masoko na mawasiliano Sarah Lazaro Keiya mara baada yakituo cha Radio5 kutangazwa washindi wa kwanza kwa upande wa Radio na wapili katika sekta nzima ya mawasiliano katika kilele cha sherehe za sikukuu ya Wakulima nanenane na maonyesho ya kilimo Kanda ya Kaskazini yaliyofanyika katika uwanja wa maonyeshoThemi Mkoani Arusha(Habari Picha na Pamela Mollel wa jamiiblog)
Meneja masoko na mawasiliano Sarah Lazaro Keiya wa Radio 5 akiwa ameshikilia kikombe walichoshinda katika maonyesho ya nanenane
Meneja masoko na mawasiliano Sarah Lazaro Keiya akiwa na timu yake ya ushindi mara baada ya kituo hicho kutangazwa washindi wa kwanza kwa upande wa Radio na wapili katika sekta nzima ya mawasiliano katika kilele cha sherehe za sikukuu ya Wakulima nanenane na maonyesho ya kilimo Kanda ya Kaskazini yaliyofanyika katika uwanja wa maonyeshoThemi Mkoani Arusha
Meneja masoko na mawasiliano Sarah Lazaro Keiya wa Radio 5 akiwa anamkabidhi funguo ya pikipiki kwa Mkuu wa wilaya Monduli Jowika Kasunga zawadi ya mshindi wa kwanza katika kilimo
Kushoto ni Rais wa Taasisi ya upendo kwa mama Eng.Carlos Mkundi akiwa katika banda la Radio 5 na DJ Haazu ambapo Taasisi ya upendo kwa mama wamedhamini maonyesho ya nanenane kupitia kituo cha Radio 5





Wafanyakazi wa Radio 5 katika nyuso za furaha
↧
WASANII WATAKIWA KUWAKUMBUKA WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUM
Na Mwandishi Wetu
Wasanii nchini wametakiwa kurejesha kwa jamii sehemu ya faida wanayoipata kupitia kazi zao za Sanaa kwa kuwakumbuka watoto wenye mahitaji maalum ili kujijengea mtandao wa kudumu wa masoko, uhalali na taswira nzuri kwa jamii.
Wito huo umetolewa mapema wiki hii na mtengeneza filamu wa Tanzania mwenye makazi yake nchini Marekani Bi. Honeymoon Mohamed wakati akiwasilisha mada kuhusu Filamu za Kitanzania na Masoko kwenye programu ya Jukwaa la Sanaa inayoandaliwa na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA).
“Wasanii wanaitegemea jamii kama chanzo cha mapato yao hivyo ni lazima wajenge utamaduni wa kurejesha kile kidogo wanachokivuna kutoka kwa jamii kupitia kusaidia watu wenye uhitaji maalum” alisema Honeymoon ambaye filamu yake ya Daddy’s Wedding imeshinda tuzo kwenye tamasha la kimataifa la filamu la Zanzibar (ZIFF) lililomalizika hivi karibuni eneo la Ngome Kongwe, Zanzibar.
Aliongeza kwamba watoto wenye uhitaji maalum wanapata faraja na kuhisi kupendwa na jamii pale wanapotembelewa mara kwa mara na watu mbalimbali wenye umaarufu na nafasi kubwa katika jamii hivyo wasanii wetu hawana budi kuwa sehemu ya kujenga faraja hii kwa watoto hawa.
Kwa mujibu wa Honeymoon wasanii wa Tanzania wako nyuma katika kuikumbuka jamii hususani kutembelea makazi ya watoto wenye uhitaji maalumu na kuchangia huduma mbalimbali zinazokuwa zinahitajika.
“Watoto wenye utindio wa ubongo wako wengi, kuna wale wenye ulemavu wa ngozi na wengine wanaishi wakiwa yatima kwenye vituo mbalimbali lakini wasanii wetu wamekuwa wazito kuwakumbuka. Wasanii hawana budi kuyakumbuka makundi haya maana wako kwa ajili ya jamii” alisisitiza.
Awali kabla ya uwasilishaji wa mada hiyo, watoto wanaoandaliwa kupitia programu ya BASATA ya ‘Sanaa kwa Watoto’ kutoka Shule ya Msingi wa Msimbazi iliyopo Ilala jijini Dar es Salaam walitoa burudani mbalimbali za Sanaa wakisaidiana na Kikundi cha Sanaa cha Jivunie chenye maskani yake neo la Mbagala Manispaa ya Temeke.
Afisa Habari wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Aristides Kwizela (Kushoto) akifuatilia burudani zilizokuwa zikitolewa na watoto wanaondaliwa na Baraza hilo kupitia programu ya ‘Sanaa kwa Watoto’ wakati wakitumbuiza kwenye Jukwaa la Sanaa la BASATA mapema wiki hii. Watoto hao wanatoka shule ya Msingi ya Msimbazi iliyoko Ilala jijini Dar es Salaam. Katikati ni Msanii wa filamu Honeymoon Mohamed na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utafiti na Stadi za wasanii Bi. Vick Temu.
Sehemu ya watoto wanaoandaliwa na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kupitia programu yake ya Sanaa kwa Watoto wakicheza igizo kwenye programu ya Jukwaa la Sanaa la BASATA mapema wiki hii. Watoto hao wanaosoma Shule ya Msingi Msimbazi walikuwa kivutio kikubwa kwa wadau wa Sanaa.
Wasanii kutoka Kundi la Ngoma za Asili na Maigizo la Jivunie lenye makazi yake eneo la Mbagala jijini Dar es Salaam wakionesha ufundi wao katika kuchenza ngoma za asili kwenye Jukwaa la Sanaa la BASATA mapema wiki hii.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Bw. Godfrey Mngereza akitoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali kwenye Jukwaa la Sanaa la BASATA linalofanyika makao makuu ya Baraza hilo Ilala Sharif Shamba kwa mwezi mara mbili siku za Jumatatu.
↧
MENEJIMENTI YA OFISI YA MKUU WA MKOA WA RUKWA YAMPONGEZA MKUU WA MKOA HUO ENG. STELLA MANYANYA KWA USHINDI WA KISHINDO KURA ZA MAONI CCM JIMBO LA MBINGA MAGHARIBI
Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa ambaye pia ni Katibu Tawala Msaidizi Utawala na Rasilimali Watu Ndugu Erasmus Rugarabamu kwa niaba ya Menejimenti ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa akitoa pongezi kwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya ambaye pia ni Mbunge Viti Maalum Mkoa wa Ruvuma kwa ushindi mnono alioupata katika kura za maoni za Chama cha Mapinduzi (CCM) katika kutafuta mgombea wa ubunge Jimbo la Mbinga Magharibi. Eng. Manyanya alishinda kwa kura 13,276 ambapo mshindi wa pili alikua na kura 3,466. Jumla ya wagombea walikua 10 ambapo tisa kati yao walikuwa ni wanaume.
Awali Jimbo hilo lilikuwa nimeshikiliwa na hayati Capt. John Komba. Kwasasa imebaki hatua ya mwisho ya majina ya wagombea kupitishwa na Uongozi wa juu wa Chama kwa ajili ya kupeperusha bendera ya Chama cha Mapinduzi majimboni katika uchaguzi Mkuu mwezi Oktoba mwaka huu 2015. Uongozi na Watumishi wote wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa unamtakia kila la heri Eng. Manyanya katika safari yake hiyo na hatimae aweze kushinda katika Jimbo hilo.
Akitoa shukurani kwa niaba ya watumishi Katibu Tawala Msaidizi Kitengo cha Serikali za Mitaa Ndugu Albinus Mgonya alimpongeza Mkuu huyo wa Mkoa wa Rukwa kwa msukumo mkubwa wa maendeleo aliouweka katika kipindi cha uongozi wake hususani katika sekta ya elimu ambapo alianzisha Azimio la Kasense kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya elimu mashuleni, Kuboresha afya ya mama wajawazito na watoto wachanga, usafi wa mazingira ambapo alianzisha kampeni ya Sumbawanga Ng'ara iliyozinduliwa na Mhe. Makamu wa Rais, Kampeni ya upandaji miti, kuboresha mazingira ya utalii katika maporomoko ya Mto Kalambo, kuboresha hali ya ulinzi na usalama katika Mkoa, Kuwaunganisha watumishi na viongozi katika kufanya kazi kwa pamoja n.k
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya akizungumza na Wakuu wa Idara na Vitengo Sekretarieti ya Mkoa wa Rukwa katika kikao kifupi cha kumpongeza baada ya kushinda katika kura za maoni Jimbo la Nyasa Magharibi kupitia CCM. Mkuu huyo wa Mkoa aliwataka Viongozi hao pamoja na watumishi kusimamia misingi aliyoiweka ya kufanya kazi kwa bidii na kwa uadilifu mkubwa, kufanya kazi kwa pamoja (team work) na kutekeleza majumu yao ya kila siku kwa ufanisi na ubunifu wa hali ya juu. Alisistiza kuwa maendeleo ya taifa la Tanzania hayataletwa tu kwa kutegemea vyama vya siasa bali kwa wananchi na wafanyakazi kutekeleza majukumu na wajibu wao ipasavyo kwa kuweka uzalendo mbele na kufanya kazi kwa bidii na uadilifu uliotukuka.
Katibu Tawala Msaidizi Kitengo cha Serikali za Mitaa Ndugu Albinus Mgonya akitoa Shukrani na Salamu za pongezi kwa niaba ya watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa kwa Mkuu wa Mkoa huo Eng. Stella Manyanya kufuatia ushindi alioupata katika kura za maoni kutafuta mgombea wa CCM Jimbo la Mbinga Magharibi. Kwa sasa Mhe. Eng. Manyanya.
(Na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa
↧
↧
UTEUZI NA UHAMISHO WA MABALOZI
THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
![]() |
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Ndugu Joseph B. Masikitiko kuwa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS). Kabla ya uteuzi huo Ndugu Masikitiko alikuwa Kaimu Mtendaji Mkuu wa Shirika hilo (TBS).
Aidha, Rais Kikwete amefanya uteuzi wa Balozi mmoja na kuwabadilishia vituo vya kazi Mabalozi wawili kama ifuatavyo:
(i) Lt. Gen. Charles L. Makakala, ameteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe. Kabla ya uteuzi huo Lt. Gen. Makakala alikuwa Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi (National Defence College).
(ii)Balozi Wilson Masilingialiyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Uholanzi amehamishwa kwenda kuwa Balozi wa Tanzania nchini Marekani kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Balozi Liberata Mulamula aliyeteuliwa hivi karibuni kuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje ya Nchi na Ushirikiano wa Kimataifa. Atakuwa pia anaiwakilisha Tanzania nchini Mexico.
(iii) Balozi Irene Kasyanjualiyekuwa Mkurugenzi wa Idara ya Sheria, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, ameteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Uholanzi kushika nafasi inayoachwa wazi na Balozi Wilson Masilingi.
Taarifa iliyotolewa leo, Jumanne, Agosti 11, 2015 na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue mjini Dar es Salaam inasema kuwa Uteuzi na uhamisho huu unaanzia tarehe 07 Agosti, 2015.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
11 Agosti, 2015
↧
TAIFA STARS YAANZA MAZOEZI
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI - RELEASE NO. 142
TAREHE 11 AGOSTI 2015
KIKOSI cha Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) kimeanza mazoezi katika uwanja wa Karume kujiandaa na mchezo dhidi ya Nigeria kuwania kufuzu kwa Fainali za Mataifa ya Afrika mwaka 2017 nchini Gabon.
Wachezaji wa Taifa Stars chini ya kocha wake mkuu Charles Mkwasa watakua wakijifua mara mbili kwa siku asubuhi na jioni katika uwanja wa Karume katika kujiweka fit na maandalizi ya mchezo huo.
Kufuatia baadhi ya wachezaji kuwa na majukumu na timu zao kujiandaa na mchezo wa Ngao ya Hisani utakaochezwa Agosti 22, Mkwasa amewaongeza wachezji wengine kumi (10) kutoka katika orodha yake ya akiba.
Lengo la kambi hii ya awali ya siku tano, ni kocha mkuu pamoja na benchi lake la ufundi kupata nafasi ya kuwaona wachezaji katika mazoezi hayo kabla ya safari ya kuelekea nchini Uturuki Agosti 23 mwaka huu kwa kambi ya siku kumi.
Wachezaji walioitwa na kuanza mazoezi leo ni Said Mohamed, Vicent Andrew (Mtibwa Sugar), Mohamed Hussein, Ibrajim Hajibu (Simba SC), Hamis Ali, Juma Mbwana (KMKM), Tumba Sued (Coastal Unioni), Samuel Kamuntu (JKT Ruvu), Ibrahim Hilka (Zimamoto– Zanzibar) na Mohamed Yusuf (Prisons).
Wachezaji wengine waliopo kambini ni Said Ndemla, Hassan Isihaka, Abdi Banda(Simba SC), Rashid Mandawa (Mwadui FC), Michael Aidan (Ruvu Shooting), Orgeness Mollel (Aspire Academy) na Abdulhaman Mbambi (Mafunzo).
TWIGA STARS KUIVAA HARAMBEE STARLETS
Timu ya Taifa ya Tanzania ya Wanawake (Twiga Stars) iliyopo kambini kisiwani Zanzibar, inatarajiwa kucheza mchezo wa kirafiki na timu ya taifa ya Wanawake kutoka Kenya (Harambee Starlets) Agosti 23, 2015.
Mchezo huo wa kirafiki utachezwa katika uwanja wa Aman Kisiwani Zanzibar, ikiwa ni sehmu ya maandalizi ya kikosi hicho kujiandaa na fainali za Michezo ya Afrika (All Africa Games) zitakazofayika nchini Congo-Brazzavile kuanzia Septemba 4 – 19, 2015.
Twiga Stars inaendelea na mazoezi kutwa mara mbili katika viwanja vya Aman na Fuoni chini ya kocha wake mkuu Rogasian Kaijage kujiandaa na fainali hizo za michezo ya afrika, wachezaji wote waliopo kambini wapo katika hali nzuri wakiendelea kujifua na michezo ya Afrika.
USAJILI Dirisha la usajili limeongezwa toka tarehe 06 Agosti hadi tarehe 20 Septemba, baada ya muda huo klabu itakayochelewesha kuleta usajili wake itatozwa kiasi cha shilingi laki tano (Tsh 500,000) kwa kila mchezaji itakayemsajili mpaka siku ya tarehe 30 Agosti.
Mwisho wa kufanya uhamisho wa kimataifa wa wachezaji kwa njia ya mtandao TMS ni tarehe 6 Septemba.
Kikao cha kamati ya sheria kitakaa tarehe 28 kwa ajili ya kuupitisha usajili na kitakaa tena tarehe 8/9/2015 kwa ajili ya kupitisha usajili.
Kuanzia tarehe 21 hadi 27 itakuwa ni wiki ya pingamizi, ambapo majina yatabandikwa TFF Karume na kuwekwa kwenye mtandao ili kuwezesha vilabu vyenye pingamizi kuwawekea wachezaji mapingamizi.
Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) inatarajiwa kuanza tarehe 12 Septemba 2015, Daraja la kwanza (FDL) ikitarajiwa kuanza Septemba 17 na Ligi Daraja la pili inatarajiwa kuanza Oktoba 16 mwaka huu.
MICHUANO YA COPA COCA-COLA 2015
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) bado linaendelea na mazungumzo na wadhamini wa michuano hiyo (Coca-Cola). Kutokana na mazungumzo hayo, ratiba ya michuano hiyo itachelewa kutoka.
Hivyo, tunawaomba kuwa na uvumilivu wakati mchakato wa mazungumzo hayo yanayokaribia ukingoni ukiendelea.
UAMUZI WA KAMATI YA RUFAA YA TFF JUU YA RUFAA YA DR. DEVOTA JOHN MARWA,YA MAAMUZI YA KAMATI YA UCHAGUZI WA SOKA LA WANAWAKE (TFF)
Mwomba rufani, Dr. Devota John Marwa, (Mrufani) ni msomi mbobezi katika taaluma ya michezo, akiwa ni mhadhiri katika kitengo kinachojihusisha na taaluma ya michezo katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Akiamini kwamba anakidhi vigezo vilivyowekwa kwa nafasi ya mgombea uenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu wa Wanawake(TWFA), alichukua fomu ya kuomba kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa Chama hicho.
Maombi hayo yalikumbana na pingamizi zilizoletwa na wakereketwa wawili wa soka la Wanawake, Bi. Chichi Mwidege na Bi. Mwajuma Noty, ambao kwa pamoja walimwekea pingamizi Mrufani, kwamba hakidhi matakwa ya kanuni za ugombea wa nafasi ya Mwenyekiti.
Waleta mapingamizi walidai kuwa Mrufani hakuwa na sifa zilizoainishwa katika Kanuni za Uchaguzi za T.F.F. (TFF Electoral Code) Ibara ya 9 (tisa) kipengele cha 3 (tatu), kinachomtaka mgombea awe amejihusisha na uongozi wa mpira wa miguu kwa muda usiopungua miaka mitano.
Aidha Ibara ya 28 (ishirini na nane) kipengele cha 3 (tatu), kinamtaka mgombea awe amejihusisha japo miaka 2 (miwili) katika shughuli za maendeleo ya mpira wa miguu nchini. Kamati ya Uchaguzi iliridhia mapingamizi hayo na kuliondoa jina la Mrufani katika orodha ya wagombea wa nafasi hiyo ya Mwenyekiti. Rufani hii ni matokeo ya uamuzi huo wa Kamati ya Uchaguzi uliotolewa taraehe 22 Julai, 2015.
Kwa ujumla, sababu za kupinga maamuzi ya Kamati ya Uchaguzi zinaweza kuhesabiwa kuwa ni mbili. Moja ni iliyojikita juu ya hitilafu katika kuamua kwamba Mrufani hakuwa na uzoefu katika uongozi wa soka kwa muda ulioainishwa. Sabau nyingine ni kwamba Kamati ya Uchaguzi illibua sababu ambayo haikuwa katika Hati ya pingamizi iliyoletwa na Mleta pingamizi.
Wakati ambapo Mleta pingamizi alijikita katika kipengele cha 28(3), Kamati iliibua kipengele cha 28(8), cha Katiba ya TWFA kinachomtaka mgombea awe ametimiza uzoefu wa uongozi wa miaka mitano, ambacho hakikuwemo katika hoja za pingamizi zilizowasilishwa na mleta pingamizi.
Katika kufikia uamuzi wake, Kamati ya Rufani ilizipitia sababu za Mrufani kama zilivyoletwa, na baada ya kusikiliza maelezo ya Mrufani na hoja za Mwakilishi wa TFF, Wakili Msomi Edward Augustino, na imeamua kama ifuatavyo. Tutaanza na hoja ya mwisho.
Je, Kamati ilikuwa sahihi kuibua kipengele ambacho hakikuletwa katika hati ya mapingamizi? Kamati inaweza kuibua kipengele hicho endapo kwa kufanya hivyo, itakuwa imejielekeza katika nia njema ya maslahi ya suala linalozungumziwa.
Sharti jingine ni kwamba hoja hiyo inyoibuliwa isiwe na athari hasi(prejudicial) kwa mhusika. Kaika suala hili hata hivyo, hoja iliyoletwa na Mleta pingamizi, yaani hoja chini ya kifungu cha 28 (3), imeainisha kipindi kifupi cha uzoefu
(miaka 2), na hoja iliyoibuliwa na Kamati inahitaji uzoefu wa miaka 5.
Endapo Mrufani angekuwa na uzoefu wa miaka 3 hadi 4, bado angekwama kutokana na hoja iliyoibuliwa na Kamati. Hii kwa vyovyote ingekuwa ni athari hasi (negative impact) katika harakati za Mrufani. Ni vema
Kamati zinazosikiliza malalamiko zikajikita kwenye malalamiko yaliyoletwa na wahusika wenyewe. Kama pigamizi lingekuwa liko juu ya kipengele hicho tu, tusingesita kukubaliana na sehemu hii ya rufani. Hata hivyo, takwa la uzoefu wa miaka 5 limeainishwa pia katika Ibara ya 9 (3), ambayo ilikuwa ni sehemu ya mapingamizi yaliyokuwepo kwenye hati ya mapingamizi.
Kwa sababu hiyo, Kamati ya Rufani haioni kama hoja hiyo ina mashiko. Haitaitilia maanani. Hoja kuu ndani ya rufaa hii ni je, Kamati ya Uchaguzi ilijielekeza vema kuhusu suala la uzoefu wa uongozi ulioainishwa na Katiba?
Mrufani ameieleza Kamati ya Rufani mlolongo wa shughuli ambazo amekuwa akizifanya, nyingi zikiwa zimejikita zaidi katika taaluma. Miongoni mwa shughuli hizo ni kuandaa Mpango Mkakati wa kuendeleza soka la wanawake. Mpango huu uliridhiwa na kuwasilishwa Makao Makuu ya Shirikisho la Mpira Duniani, yaani FIFA.
Maelezo mengine ni kushiriki katika kuongoza timu mbali mbali kule Chuo Kikuu, zingine zikiwa za watoto wadogo ambao baadhi ya matunda yake ni wachezaji walioibukia kwake kama vile Simon Msuva. Alisema zaidi kuwa alishiriki kuandaa warsha ilizoandaliwa kwa ushirikiano kati ya FIFA na TFF.
Aidha. Alisema kuwa amekuwa kiongozi tangu akiwa bado kwenye vyuo vya ualimu, na baadaye alipohitimu na kufanya kazi kama Mwalimu, kabla ya kujiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam aliko mpaka sasa. Akasema, hata alipokuwa Sweden kwa masomo ya juu pia lijihusisha na programu za maendeleo ya soka la wanawake.
Wakili msomi wa TFF akijibu hoja hizo, alikubaliana na uamuzi wa Kamati ya Uchaguzi kuwa Mrufani hajaonesha popote kwamba amewahi kuongoza soka, akasema Mrufani ni mtaalamu tu kama msomi, jambo linaloweza kufanywa na msomi yoyote. Akamalizia kwa kuiomba Kamati ya Rufani za Uchaguzi kuitupilia mbali rufaa ya Mrufani kwa kukosa mashiko.
Tofauti na Kamati ya Uchaguzi, Kamati ya Rufani imeona kuwa kwa maslahi mapana ya mchezo wa soka katika ujumla wake, ni vema kuweka tafsiri pana (wide interpretation) juu ya sifa zinazozungumzwa, badala ya kuweka tafsiri finyu (restricted/narrow interpretation) kama ilivyofanya Kamati ya Uchaguzi.
Baada ya kufanya hivyo, kuhusiana na Mrufani, Kamati imeona kuwa ana sifa zinazostahili. Kupitia sababu alizozitoa, na vielelezo vyake, Kamati ya Rufani haina wasiwasi kuwa Mrufani ana uzoefu mbali mbali sio katika soka tu, bali pamoja na michezo katika ujumla wake.
Tumeshuhudia katika maelezo yake kwetu kwamba ushiriki wake katika hatua mbali mbali, japo hakuwahi kuchaguliwa, sio ushiriki wa kitaaluma tu, kama msomi mwingine yeyote. Ni ushiriki wenye dhamira ya dhati ya kuleta mabadiliko/maendeleo katika soka la wanawake. Maelezo
yake kuwa aliaandaa programu ya maendeleo ya soka la wanawake, hayakupingwa. Kamati ya Uchaguzi ingeangalia namna ambavyo “visheni” iliyomo katika programu ile ambavyo ingeweza kutekelezwa na mtu aliyeaiandaa. Kwa hiyo, katika hoja hii, Kamati inakubaliana kuwa Mrufani
anazo sifa stahiki, na kukatwa kwa sababu hii, Kamati ya Uchaguzi haikujielekeza vema. Kwa hiyo, Mrufani ameshinda rufaa yake? Kamati ya Rufani inachelea kujibu swali hili moja kwa moja. Utaratibu wa kuwasilisha rufani ulikiukwa, na hapa ndipo rufaa hii inapokwaa kisiki. Chini ya Ibara ya 13 (1) cha Kanuni ya
Uchaguzi (Electoral Code), mgombea ambaye hakuridhika na maamuzi, atawasilisha rufaa yake ndani ya siku 3 (tatu) tangu uamuzi anaoupinga ulipotolewa.
Kipengele cha 3 (tatu) cha ibara hiyo kinasema kwamba Mrufani yoyote atakuwa na uhalali endapo rufaa yake imewasilishwa kwa mujibu wa kanuni hizo. Uamuzi unaolalamikiwa ulitolewa tarehe 22 Julai 2015, sababu za rufaa ziliandaliwa tarehe 27 Julai na sababu hizo za rufaa zililipiwa tarehe 28 Julai, 2015. Ni dhahiri kwamba rufaa ililetwa nje ya muda uliowekwa na kanuni, na kwa hiyo inakosa uhalali kisheria na kikanuni.
Japo katika mwenedo na maamuzi yake Kamati ya Rufani za Uchaguzi haifungwi na taratibu za kimahakama, suala la muda wa kuwasilisha rufani sio miongoni mwa mambo ambayo Kamati inaweza kutoyazingatia. Kwa sababu hiyo, Rufaa hii imetupwa, lakini kwa sababu tofauti na zile za Kamati ya Uchaguzi.
Pamoja na uamuzi huu, Kamati ya Rufani za Uchaguzi inapenda kwa namna ya kipekee kumpongeza Mrufani kwa jitihada alizozionesha kutaka kuitumikia TWFA. Ni matumaini ya Kamati kuwa hatokata tama, na kwamba atakuwa tayari, akitakiwa kufanya hivyo, kupitia taalum yake, kushirikiana na wenzake katika jitihada za kuendeleza soka la akina mama lililo na changamoto lukuki.
Imetolewa na,
JULIUS M. LUGAZIYA
Mwenyekiti-Kamati ya Rufani za Uchaguzi
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

↧
FAINALI YA TMT KUFANYIKA TAREHE 22 AUGUST NDANI YA MAKUMBUSHO YA TAIFA JIJINI DAR

Shindano la kuibua na Kusaka Vipaji vya Kuigiza lijulikanalo kama Tanzania Movie Talents (TMT) ambalo limedumu kwa takribani Miezi Minne hatimaye shindano hilo linakaribia kufika tamati mnamo tarehe 22 August 2015 huku Mshindi Mmoja Akiondoka Na Kitita Cha Shilingi Milioni Hamsini Za Kitanzania. Na Washiriki waliofanikiwa kuingia Hatua ya Kumi bora watapata kifuta jasho huku wakiwa na mkataba mnono wa kufanya kazi na Kampuni namba moja ya Kutengeneza na Kusambaza filamu za Kitanzania ambao pia ndio waratibu wa Shindano Hilo la Tanzania Movie Talents (TMT) ya Proin Promotions Ltd.
Shindano la TMT lilianza mapema mwezi wa Nne kwa kutafuta vipaji katika Kanda ya Ziwa ambapo usaili ulifanyika Mkoani Mwanza na kuhitimishwa Kanda ya Pwani Mkoani Dar Es Salaam kwa kupatikana Jumla ya Washindi 20 kutoka Kanda sita za Tanzania.
Washindi wa kanda sita walipata fursa ya kuingia ndani ya mjengo wa TMT huku wakipatiwa mafunzo ya sanaa kutoka kwa Walimu wa Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam huku mchujo ukiendelea na kupelekea kila wiki Washiriki wawili kuaga shindano, takribani wiki tano jumla ya washiriki 10 waliweza kuaga shindano hili ambalo limefikia hatua ya kuwapata washiriki 10 waliofanikiwa kuingia hatua ya Kumi bora huku wakingojea fainali itakayotoa mshindi wa kitita cha shilingi milioni hamsini za kitanzania
Mpaka sasa washiriki waliofanikiwa kuingia hatua ya Kumi bora wanaendelea na kujifua Kwaajili ya fainali ambayo imebaki wiki moja tu kwa fainali hiyo kuliteka jiji la Dar huku hofu na presha zikiwapata Washiriki hao.
Fainali ya TMT itafanyika Siku ya Jumamosi ya tarehe 22 August 2015 katika ukumbi wa makumbusho ya taifa karibu na Chuo cha IFM kwa viingilio vya shilingi Elfu 50 kwa VIP na Elfu 30 kwa viti vya kawaida.
TMT 2015 inapigwa tafu na Precious Air, Cam gas, ITV na Radio One, Global Publishers, I-View Studio, Paisha na Hussein Pamba Kali.
↧
RAIS KIKWETE AONGOZA KIKAO CHA KAMATI KUU DODOMA
↧
↧
WATANZANIA WAMEASWA KUHIFADHI MAZINGIRA.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Sazi Salula akifungua Mkutano wa wadau wa mazingira unaohusu Miradi ya majaribio nchini wa Mkakati wa Kupunguza Uharibifu wa Misitu (MKUHUMI) leo jijini Dar es salaam.
Kiongozi wa wawezeshaji kutoka Asasi isiyo ya kiserikali ya Niras kutoka Finland inayosimamia Miradi ya majaribio nchini wa Mkakati wa Kupunguza Uharibifu wa Misitu (MKUHUMI) Merja Makela akitoa mada wakati wa mkutano wa wadau wa mazingira kuhusu namna bora ya kuhifadhi mazingira na kuboresha usimamizi wa ardhi na kuongeza mapato kutoka kwenye misitu. Mkutano huo ambao umefanyika leo jijini Dar es salaam umeandaliwa na Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Serikali ya Norway.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Sazi Salula (kushoto) akifuatilia mada wakati wa mkutano wa wadau wa mazingira kuhusu namna bora ya kuhifadhi mazingira na kuboresha usimamizi wa ardhi na kuongeza mapato kutoka kwenye misitu. Wa pili kushoto ni Mkurugenzi wa Mazingira kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Julius Ningu.
Baadhi ya washiriki wa Mkutano wa wadau wa mazingira unaohusu Miradi ya majaribio wa Mkakati wa Kupunguza Uharibifu wa Misitu (MKUHUMI) nchini wakifuatilia mada wakati wa mkutano leo jijini Dar es salaam.
Mhadhiri kutoka chuo Kikuu cha Dar es Salaam Prof. Pius Yanda akibadilishana mawazo na Mwakilishi wa Ubalozi wa Ufaransa mara baada ya ufunguzi wa mkutano wa wadau wa mazingira leo jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi wa Mazingira kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Julius Ningu (aliyevaa suti nyeusi) akiongea na baadhi ya waandishi wa habari baada ya ufunguzi wa mkutano wa wadau wa mazingira leo jijini Dar es salaam.
Picha na Eleuteri Mangi-MAELEZO)
Na Jenikisa Ndile-MAELEZO
Watanzania wameaswa kuzingatia namna bora ya kuhifadhi mazingira, upangaji wa matumizi bora ya ardhi na utekelezaji wa mipango ili kuleta tija na maendeleo endelevu nchini.
Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Sazi Salula leo jijini Dar es salaam alipokuwa akifungua Mkutano wa wadau wa mazingira unaohusu utekelezaji wa miradi ya majaribio ya Mkakati wa Kupunguza Uharibifu wa Misitu (MKUHUMI) nchini.
Bw. Sazi alisema kuwa mipango hiyo ya MKUHUMI inalengo la kuondoa umasikini kwa watanzania waishio vijijini ambao wapo karibu na hifadhi za misitu inasimamiwa na kutekelezwa kwa kushirikiana na Serikari ya kijiji ili kuhakikisha mafanikio yanapatikana kwa kuzingatia utekelezaji na usimamizi wa sheria kupitia kamati za vijiji.
Majaribio ya sera ya mazingira yamefadhiliwa na Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Serikali ya Norway ili kuboresha na kushughulikia masuwala ya ardhi, misitu na kupunguza gesi joto kwa kuhimiza jamii kupanda miti kwa shughuli za maendeleo endelevu nchini.
Mipango hiyo inatekelezwa katika wilaya za Sumbawanga, Lindi, Kilwa, Zanzibar, Pemba, Kigoma na Kondoa ambapo sera hiyo imewapa elimu ya kujenga utayari wa shughuli za MKUHUMA na kuwezesha ushiriki mpana wa wadau ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.
Kwa upande wake Kiongozi wa miradi ya majaribio ya MKUHUMI Merja Makela alisema kuwa taasisi yake imefanikiwa kutokana na kusimamia miradi hiyo ambayo imepokelewa na kutekelezwa kama ilivyopangwa katika maeneo husika nchini.
Naye Mkurugenzi wa Mazingira kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Julius Ningu alisema kuwa kwa tathmini iliyofanyika mwaka 2013, asilimia 55 ya ardhi ya Tanzania imefunukwa na misitu ambapo juhudi zinaendelea kufanyika kwa kuwaelimisha watanzania kuendelea kuitunza misitu hiyo kwa manufaa ya sasa na baadaye.
↧
NURU YA MSHUMAA...
↧
NENO LA LEO MTAANI.
↧
TASWIRA MBALI MALI KUTOKA KWA MDAU KHAMIS MUSSA
Kijana Ephrahim Maksoni akipita juu ya reli kwa baiskeli maeneo ya Nguruka Mkoani Kigona
Abiria wakiteremka toka ndani ya Basi la Saratola likitokea Nguruka kwenye kituo kipya cha mabasi kilichopo Masanga Gungu mkoani kigoma
Wafanya biashara wa chumvi wakiwauzia abiria waliokuwa wakisafiri na basi lililokuwa likitoka Nguruka kuelekea Kigoma
Wakichota maji eneo katika kituo cha mabasi mjini Kaliua mkoani Tabora
Wananchi wakikata tiketi katika kituo kipya cha Stendi ya mabasi ya Mikoani kilichopo Masanga Gungu mkoani kigoma, ambapo kuingia huingia bure na kutoka huwalazimu kutoa sh. 200. Picha na Khamisi Mussa
↧
↧
World Elephant Day: Conserve and protect the Elephant from the numerous threats it faces
The world is presently witnessing brutality & annihilation of one of the most charismatic mammals on earth, the African Elephant at a shocking rate in human history. Poaching, habitat loss and other cruelty are alarming. Tanzania being a treasure of elephants in Africa has recently revealed its catastrophe.
The recent elephant census conducted in the main elephant ecosystems for seven months consecutively from May to November 2014, indicates a significant decline of current elephant population in Tanzania from 2009 to 2014 survey by 60%. At independence in 1961 there were 350,000 elephants and in 2009 were 110,000 and by 2014 the number dwindled to about 43,521.
‘The increase in elephant poaching is highly linked to an increase of ivory prices and illegal markets in the Far East and South East Asia’ Says Dr. Amani Ngusaru, WWF Tanzania Country Director on marking the World Elephant Day, 12th August 2015, in Dar es Salaam. Elephant poaching and trafficking of wildlife has increased dramatically in recent years, threatening the three pillars of life on earth: - sustainable development, peace and human rights.
It is now more urgent and important to come up with interventions that address the root causes of elephant poaching through more and improved international cooperation in source, transit and consumer countries as well as to identify and address any gaps in the current anti-poaching strategies for better protection of wild elephants.
There is also a need for improving enforcement policies to prevent the illegal poaching and trade of ivory, conserving elephant habitats, better treatment for captive elephants and when appropriate, reintroducing captive elephants into natural and protected sanctuaries. These are the goals that elephant conservation organizations are focusing on around the world.
There is also a need for improving enforcement policies to prevent the illegal poaching and trade of ivory, conserving elephant habitats, better treatment for captive elephants and when appropriate, reintroducing captive elephants into natural and protected sanctuaries. These are the goals that elephant conservation organizations are focusing on around the world.
Due to poaching between 1970s and 1980s, the elephant population in Tanzania declined to 55,000 but then the international ban of sale of ivory and other elephant products together with highly effective anti-poaching operations through Operation Uhai in Tanzania resulted in elephant population recovery from 55,000 in 1989 to an estimated 130,000 in 2005 and 110,000 in 2009.However, by 2011 there was an increase in commercial poaching targeting elephants because the price of ivory went up tremendously in the Far East and South East Asian market.
WWF is backing the Government of Tanzania efforts and contribute to combating poaching at the grass root level while working with local communities in implementing government inclusive management policies. The relevant policy approaches include Community Based Natural Resources Management –(CBNRM) through the Wildlife Management Areas (WMA), community based forest management (CBFM), participatory forest management (PFM) and joint forest management (JFM). In some areas, even Beach Management Units (BMUs) as well as the Water Users Associations (WUA) are useful in dealing with anti-poaching activities.
WWF Tanzania’s focus at local levels provides an important opportunity for engaging in protection of elephants and other natural resources by integrating conventional anti-poaching methods (boots on the ground) and community participation in the fight against all forms of illegal natural resources utilization including elephant poaching.
In commemoration of the elephant day, WWF Tanzania calls the nation to wake up and deal effectively with this SHAME!! Elephant poaching and trafficking should now be dealt as a “serious crime’ that needs special national attention. It needs to be addressed through applying the full extent of the criminal laws in conjunction with the wildlife Act and other laws pertaining to TRA (Customs and excise) money - laundering and to categorize illegal wildlife trade as a predicate offense to be investigated with related financial crimes.
It is equally important to strengthen the judiciary sector to ensure that prosecutions for wildlife crimes are conducted effectively and transparently, with the full extent of the law and using the strongest penalties available. Tanzania should also use the available legislative instruments to seize the assets used to commit poaching and illegal wildlife trade and other profit acquired through this trade.
It is also important to take urgent measures to ensure that the Frontline staffs in fighting against poaching are professionally trained and equipped, have access to adequate welfare and support systems and are legally supported to respond to threats to wildlife and themselves. It is of urgency to support the development and implementation of transportation sector protocols and/ or guidelines to strengthen due diligence and other measures to eliminate illegal trade in wildlife.
WWF Tanzania calls for Government led National campaigns that are well researched aimed at behavior change and demand reduction. It is important also to consider increasing the capacity of local communities to pursue sustainable and alternative livelihoods as well as enhancing local communities’ rights and capacity to manage and benefit from wildlife and enables them to live in more equitable socio- economic conditions.
If successfully conducted, the integrated approach will provide network of sympathizers at the grass root level that would feed into the national anti-poaching intelligence network more efficiently and with less investment costs.
↧
TAARIFA YA SERIKALI KUHUSU MGONJWA ANAYEHISIWA KUWA NA UGONJWA WA KUTOKWA DAMU MKOANI KIGOMA
↧
SAMAKI SAMAKI WA HUKU CHANGANYIKENI KWETU WANAZIDI KUTUNUFAISHA NA HARUFU MWANANA ENEO LA DALAJANI JIJINI MBEYA...
Choko choko za Kameramani wa Mtaa Kwa Mtaa Blog kuchokonoa Taswira mbalimbali katika Eneo korofi kwa Uchafuzi wa Mazingira Jijini Mbeya, Kama ambavyo ionekanavyo Taswira hapo juu ya mwana Mama mmoja akiwa katika Biashara yake ya kuuza Machungwa huku nyuma yake akiwa ametawaliwa na Beseni kubwa la Samaki Samaki likimpatia harufu mwanaaaanaa kabisaaa.Picha na Fadhiri Atick Mtaa Kwa Mtaa Mbeya.
Hapo mdau katika Picha akikatiza Kando Kando ya Beseni la Samaki Samaki..
Wanafunzi nao Hawapo Mbali na Beseni hilo la Samaki Samaki Eneo la Dalajani Jijini Mbeya..
Kwa Mbaali Vijana wakiwa katika Mchezo wa Drafti kalibu na Beseni hilo..
Dalaja hilo likimeremeta kwa Uchafu Mwanana...
Beseni linalo aminika kwa Shombo ya Samaki Samaki Eneo la Dalajani Jijini Mbeya likiwa limekidhili kwa utupwaji wa Taka Taka kiholela.
↧