Quantcast
Channel: MTAA KWA MTAA BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 39650

BENKI YA POSTA (TPB) YAKABIDHI MADARASA NA OFISI YA SHULE YA MSINGI MAKAMBAKU, MKOANI NJOMBE

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Njombe Dkt Rehema Nchimbi(katikati) na Mwenyekiti wa Bodi ya benki ya posta Profesa .Lettice Rutashobya( kulia) pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Njombe Lucy Msafiri wakizindua madarasa na ofisi ya walimu katika shule ya Msingi Makambaku ambayo yamejengwa kwa ufadhiri wa benki ya Posta Tanzania (TPB) kwa thamani ya shilingi milioni 35.
Mkuu wa Mkoa wa Njombe Dkt Rehema Nchimbi na Mwenyekiti wa Bodi ya benki ya Posta (kushoto ) Profesa .Lettice Rutashobya wakifungua jiwe la msaingi mara baada ya kuzindura rasmi madarasa na ofisi ya walimu katika shule ya Msingi Makambaku ambayo yamejengwa kwa ufadhiri wa benki ya Posta Tanzania (TPB) kwa thamani ya shilingi milioni 35. Walioketi mbele kwenye madawati yaliyotolewa na benki ya Posta Tanzania (TPB) ni Mkuu wa Mkoa wa Njombe Dkt Rehema Nchimbi (katikati) na Mwenyekiti wa Bodi (kushoto ) Profesa .Lettice Rutashobya na mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Makambaku Rehema Msigwa pamoja na viongozi wa benki ya Posta Tanzania (TPB) .
Muonekano wa jengo la madarasa mawili na ofisi moja ya walimu katika shule ya msingi Makambaku ambayo yamejengwa na Benki ya Posta Tanzania (TPB) kwa thamani ya shilingi milioni 35.
Muoekanao wa moja ya Chumba cha darasa kilichojengwa na Benki ya Posta Tanzania (TPB) kwa thamani ya shilingi milioni 35.
Wazazi waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa jengo la shule ya msingi Makambaku yaliyojengwa kwa ufadhiri wa Benki ya Posta Tanzania (TPB) kwa thamani ya shilingi milioni 35.
Mwenyekiti wa Bodi Profesa .Lettice Rutashobya akizungumza katika hfala ya uzinduzi wa jengo la madarasa mawili na ofisi ya walimu katika shule ya msingi Makambaku Mkoani Njombe lililojengwa kwa ufadhiri wa benki ya Posta Tanzania (TPB) kwa thamani ya .shilingi milioni 35.
Mkuu wa Mkoa wa Njombe Dkt Rehema Nchimbi akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa jengo la madarasa mawili na ofisi ya walimu katika shule ya msingi Makambaku Mkoani Njombe lililojengwa kwa ufadhiri wa benki ya Posta Tanzania (TPB) kwa thamani ya .shilingi milioni 35.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania (TPB)Moshingi SabaSaba akizungumza katika hfala ya uzinduzi wa jengo la madarasa mawili na ofisi ya walimu katika shule ya msingi Makambaku Mkoani Njombe lililojengwa kwa ufadhiri wa benki ya Posta Tanzania (TPB) kwa thamani ya shilingi milioni 35.
Mkuu wa Mkoa wa Njombe Dkt Rehema Nchimbi akichenza ngoma na wanafunzi wa shule ya msingi Makambaku mara baada ya kuzindua rasmi jengo la Madarasa mawili na ofisi moja ya wawilimu katika shule ya msingi Makambaku ambayo yamejengwa kwa ufadhiri wa Benki ya Posta Tanzania kwa thamani ya shilingi milioni 35.
Meza kuu katika picha ya pamoja na watumishi na viongozi wa benki ya Posta Tanzania (TPB)


Meza kuu katika picha ya pamoja na wananchi na wateja wa benki ya Posta Tanzania TPB.

NA EMANUEL MADAFA, MAKAMBAKU

BENKI ya Posta Tanzania (TPB) kupitia tawi lake la Makamabko Mkoani Njombe , imejenga madarasa mawili pamoja na ofisi ya walimu katika Shule ya Msingi Makambako ikiwa ni jitihada zake za kukuza elimu nchini.
 
Akikabidhi msaada huo katika Halmashauri ya mji wa Makambaku Mkoani Njombe Mwenyekiti wa bodi ya Benki ya Posta Tanzania (TPB), Prof. Lettice Rutashobya amesema msaada huo wa madarasa utasaidia kupunguza kwa kiasi kikubwa msongomano wa wanafunzi kwenye vyumba vya madarasa, na kuwawezesha watoto kusoma kwenye mazingira bora zaidi na kwenye madawati ambayo nayo yametolewa na benki ya Posta
 
Amesema ujenzi huo wa madarasa pamoja na ofisi ya walimu yaliojengwa kisasa umeigharimu Benki ya Posta Tanzania kiasi cha shilingi milioni 35, hivyo kuwaomba wanafunzi na wananchi wa eneo hilo kuyatunza na kuyatumia vyema ili yaweze kudumu kwa muda mrefu.
 
Amesema benki ya Posta inayo sera madhubuti ya kusaidia jamii (CSR Policy), ambapo kila mwaka hutenga kiasi cha fedha kutokana na faida tunayoipata ili kusaidia jamii inayo tuzunguka.
 
Mwenyekiti huyo wa bodi amefafanua kuwa wanafanya hivyo kwa kutambua kuwa bila jamii kutumia huduma wanazozitoa hawawezi kupata faida, hivyo faida wanayoipata wanairudisha kwa jamii
 
Amesema kwa Mwaka jana benki ya Posta ilitenga kiasi cha shilingi Milioni 150 kwa ajili ya kusaidia shughuli za kijamii, na miongoni mwa miradi tuliyoifanya ni pamoja na kujenga kituo cha Afya huko Ungi Msuka, Pemba, ujenzi wa kisima cha maji safi kwa ajili ya shule ya Sekondari ya Sakasaka
 
Amesema maeneo mengine ambayo yamebahatika kupata msaada huo ni pamoja na Shinyanga, tulichangia mashuka kwa ajili ya hospitali ya rufaa mkoani Singida, tulichangia madawati kwa ajili ya shule ya msingi Gideli Mkoani Mwanza, pamoja na miradi mingine mingi yenye kuigusa jamii kwa namna moja au nyingine.
 
Amesema kwa Mwaka huu Benki imejidhatiti kuchangia miradi mingi zaidi, kwa ajili ya kusaidia shughuli za kijamii, mradi huu ukiwa ni mojawapo ya miradi iliyochaguliwa katika kipindi hiki
 
Pia wameweka mkakati madhubuti wa kuhakikisha kuwa tunaunga mkono tamko la Mheshimiwa Rais wa awamu ya tano Mhe. John Magufuli, wa kuhakikisha kuwa hakuna mwanafunzi atakae kaa chini, kwa kuchangia madawati kwenye shule mbalimbali nchini, shule ya Makambako ikiwa ni mojawapo ya shule zilizofaidika.
 
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Njombe Dkt Rehema Nchimbi akipokea msaada huo wa majengo aliishukuru Benki ya Posta Tanzania kwa moyo wao wa ukarimu na upendo waliouonesha kwa wanamakambako pamoja na Mkoa wa Njombe kwa ujumla.

Aidha Mkuu huyo wa Mkoaa ametumia fursa hiyo kuwataka wazazi na walezi kuwasimamia vyema watoto pamoja na kujali maendeleo ya watoto wao.

Shule hiyo bado inakabiliwa na changamoto kubwa ya ukusefu wa vyumba vya madarasa kutokana na kuwepo kwa idadi kubwa ya wanafunzi hali inayolazimisha wanafunzi kusoma kwa awamu hivyo bado wanauhitaji wa vyumba 24 vya madarasa.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 39650


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>