
Katika kikao hicho wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji wakiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati Mhe. Dr. Christine Ishengoma wameipongeza Wizara ya Maji inayoongozwa na Waziri Mhe Jumaa Aweso kwa kufanya kazi nzuri katika utekelezaji wa Miradi ya Maji na kuhakikisha hali ya huduma na upatikanaji wa Maji inaimarika maeneo mbalimbali nchini.
Aidha Wajumbe wa Kamati wameishauri Wizara kufanya maboresho na kuongeza jitihada katika maeneo kadha wa kadha ikiwa ni pamoja na Kukamilisha miradi kwa wakati, kusimamia mwendelezo wa miradi baada ya kukamilika, kuongeza nguvu katika usimamizi wa Rasilimali za Maji na kugusia maeneo yanye changamoto kubwa ya Maji nchini na mjadala wa suluhisho lake.
Katika hatua nyingine,Waziri Aweso akijibu hoja za Wabunge amekiri kuwa Wizara ya Maji imepata ushirikiano mkubwa wa kamati hiyo na ndio siri ya mafanikio na kuweka bayana kuwa ushauri na maoni yote yaliyotolewa na Kamati yamepokelewa na yatafanyiwa kazi kikamilifu.