Na Chalila Kibuda, Michuzi TV
Bodi ya Bonde la Wami/Ruvu imesema kuwa Wakazi wa Mkoa wa Pwani na Dar es Salaam Milioni 11 wanahitaji maji kila siku hivyo kila mmoja ana nafasi ya kulinda vyanzo vya maji juu ya ardhi na chini Ardhi ili kuwa na uhakika wa kupata maji hayo.
Hayo aliyasema Afisa wa Kidakio cha Pwani wa Bodi ya Bonde la Wami/Ruvu (WRBWB) Halima Faraj wakati wa kikao cha Jukwaa la Kidakio cha Pwani walikutana kwa ajili ya kuangalia na namna ya kuhifadhi maji na kulinda vyanzo vya maji kilichofanyika jijini Dar es Salaam.
Halima amesema Jukwaa ni muhimu katika utekelezaji wa mikakati ya usimamizi wa maji kwenye vyanzo kutokana na wadau wake wanatoka kwa kwenye jamii na kwenda kuwa mabalozi.
Amesema Bodi ya Bonde la Wami/Ruvu imeanzisha majukwaa ili kushirikiana katika usimamizi wa vyanzo vya maji katika kufanya huduma za upatikanaji wa maji zinakuwa endelevu.
Aidha amesema Serikali ya awamu ya Sita chini ya Rais Dk.Samia Suluhu Hassan imekuwa ikisisitiza utunzaji wa mazingira ya vyanzo vya maji ya kutaka wananchi kuacha kuharibu vyanzo vya maji vilivyopo.
Amesema kuwa Mabadiliko ya Tabianchi ni kutokana na uhalibifu wa mazingira ambapo uhalibifu huo ndio kisasi ya kuwepo mabadiliko hayo ya tabianchi.
Amesema kuwa wananchi wakichimba visima bila kupata vibali ambao ni kosa la kisheria kutokana na maji ya chini ardhi kuna vitu vya kitaalamu vinatakiwa kufanyika.
Halima amesema mifugo na na shughuli za kilino kwenye kando kando ya mito ndio changamoto kwenye vyanzo vya maji ndio wakati mwengine kidakio cha cha Pwani kinakosa maji.
Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Temeke Thabit Mohamed akizungumza na wananchi walioko kando kando ya Mto Mzinga mara baada ya kumaliza zoezi la upandaji miti.
Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Temeke Thabit Mohamed akipanda mti kando kando ya Mto Mzinga Buza.
Afisa wa Kidakio cha Pwani Halima Faraji (Mwenye kilemba cha rangi ya Samawari 'Blue') akipanda mti kwenye kando kando ya mto Mzinga , Buza Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam.
Afisa wa Kidakio cha Pwani Halima Faraj akizungumza ma wananchi wa Buza wakati wa zoezi la upandaji miti kando kando ya mto Mzinga jiijini Dar es Salaam.
Meneja wa Mtambo wa Mtoni wa Dawasa Hilder Razalo akizungumza kuhusiana na utunzaji wa mazingira katika vyanzo vya maji wakati zoezi la upandaji mito katika Mto Mzinga.




