Na Chalila Kibuda, Michuzi TV
Shirika la Uwakala wa Meli (TASAC) limesema kuwa michezo kwao ni sehemu ya kipaombele kutokana na kuweka mshikamano na ushirikiano wa kufanya kazi kwa timu wakiwa kazini.
Hayo ameyasema Kaimu Mkurugenzi Mkuu Nahson Sigalla wakati wa Bonaza la Wafanyakazi lililofanyika viwanja vya TCC Gwambina Jijini Dar es Salaam.
Sigalla amesema kuwa wafanyakazi hawapendi kufanya mazoezi lakini kutokana na kushiriki mabonaza ni fursa kwao kuanza kufanya mazoezi ya aina mbalimbali wakiwa majumbani.
Aidha amesema viongozi wakitaifa wanaelekeza juu ya ya umhimu mazoezi hivyo kinachifanyika ni kutekeleza maelekezo hayo kwani yanasaidia afya na pamoja na kujiepupusha na magojwa yasioambukiza ikiwemo shinikizo la damu (BP) pamoja na sukari.
Amesema kuwa katika kushiriki mazoezi kwa wafanyakazi imejenga ari ya mtu mmoja kufanya mazoezi ambapo katika mashindano ya michezo TASAC imekuwa na timu imara.
Hata hivyo amesema kuwa katika Bonaza hilo limekuwa na uboreshaji wa kuongeza michezo ambayo yote ni kutaka kila mmoja kuonyesha uwezo wake wa ushiriki ikiwa ni tofauti na miaka mingine.
Michezo iliyofanyika katika Bonaza hilo ni Mpira wa Pete, Mpira wa Miguu kwa Wanaume , Kufukuza Kuku, Kukimbia na Yai kwenye kijiko, Bao, Kuruka Kamba, Kukimbia Mita 1O0.
Nae Mkurugenzi wa Huduma za Shirika wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Rajab Mabamba amesema kuwa michezo kwao ni moja ya kupima utendaji wa kazi katika kufanya kazi kwa timu katika kuhudumia wananchi.
Amesema kuwa kufanya kazi kwa ushirikiano kwenye michezo ndio unahitajika kufanyika sehemu za kazi na kupata matokeo chanya ya kufanya Shirika kuendelea kufanya kazi katika utoaji huduma bora kwa wateja.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Nahson Sigalla akizungumza wakati wa Bonaza la Michezo la Shirika lililofanyika Viwanja vya TCC Gwambina Jijini Dar es Salaam.![]()

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Nahson Sigalla akipiga mpira wa kutenga (Penalt) kuashiria kufungua Bonaza la Michezo la Shirika lililofanyika Viwanja vya TCC Gwambina Jijini Dar es Salaam.![]()
.jpeg)
Mchezo wa kuvuta kamba
Picha mbalimbali za Mkurugenzi wa Huduma za Shirika wa TASAC Rajab Mabamba akitoa medali na picha za pamoja za makundi mbalimbali kwenye bonaza hilo