Na Chalila Kibuda, Michuzi TV
NCHI za Afrika Mashariki za Tanzania , Kenya pamoja na Uganda zimekubaliana kwenda mbele katika matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) kwenye sekta ya elimu kutokana na majanga yanayotokea ambapo wanafunzi ndio wanakuwa wanaathirika kwa kipindi hicho inayochangiwa na mifumo iliyowekwa kwenye ufundishaji.
Hayo yamesemwa na Wadau wa Elimu wa nchi za Afrika Mashariki wakati wa ufungaji wa Mkutano wa Siku Tatu wa wadau wa Elimu wa wa nchi za Afrika Mashariki ulioandaliwa na Taasisi ya Maendeleo ya Aga Khan katika kuhusisha wadau ambao ni watendaji katika sekta ya elimu kwa kila nchi na kufanyika jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari kwenye mkutano huo Mkuu wa Taasisi ya Maendeleo ya Elimu ya Aga Khan Profesa Jane Rarieye amesema kuwa katika kufundisha Tehama tufikirie kuwekeza kwa walimu na wanafunzi.
Profesa Jane amesema kuwa kwenye kufundisha wanafunzi kunahitaji kuangalia njia za vifaa mawasilino vitakavyotumika kwa wanafunzi kutokana na uwezo kila mzazi kumudu gharama za kununua kifaa cha mawasiliano na bila kuacha ufundsishaji wa ana kwa ana ‘Face to Face’
Mkuu wa Utafiti wa Taasisi ya Maendeleo ya Elimu ya Aga Khan Profesa Fredrick Mtenzi amesema kuwa katika matumizi ya Tehama kwa nchi za Afrika Mashariki kuacha visingizio vya kutotumia kwani Dunia inabadilika kwa majanga kwani wakati wa UVIKO 19 mambo yalivurugika kwenye sekta ya elimu.
Amesema kuwa walimu wote wanavishikwambi hivyo wanatakiwa kutumia katika kufundisha walimu na sio kutumia kupiga picha huku akiongeza kuwa wanafunzi nao wana uwezo wa kutumia vishikwambi wakati mwingine wakawazidi walimu.
Kwa upande wa Mkurugenzi wa Elimu Maalum wa Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia Dk.Magreth Matonya amesema kuwa mkutano huo umeonyesha umuhimu wa Tehama kotokana na kipindi kilichokuwepo cha UVIKO 19 Tanzania imekwenda kwenye uwekezaji wa Tehama ikiwemo kuwa na Studio ya kunakiri vipindi kwa ajili ya kufundishia iliyopo kwenye Taasisi ya Elimu.
Amesema kuwa katika kufundisha wanafunzi basi kusiachwe wanafunzi wenye mahitaji maalum kwa kuwaandalia vitu vitakavyowezesha kusoma kama watoto wenginr.
Dk.Magreth amesema kuwa katika mkutano huo wamekubaliana kwa pamoja kuweka mkazo wa elimu ya awali kwa kuamini kuwa msingi elimu unajengwa kutokana na elimu ya awali na kuongeza kuwa kwenye elimu sasa wanafunzi wanaweza kusoma vitabu vyote kwenye mtandao.
Mkuu wa Taasisi ya Maendeleo ya Elimu ya Aga Khan Profesa Jane Rarieye akizungumza na waandishi habari kuhusiana mikakati waliyopeana katika sekta ya elimu kwa nchi za Afrika katika mkutano ulioandaliwa na Taasisi ya Maendeleo ya Elimu ya Aga Khan, jijini Dar es Salaam.![]()

Mkurugenzi wa Elimu Malum wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dk.Magreth Matonya akzungumza kuhusiana na Tanzania ilivyochukua hatua katika matumizi ya Tehama wakati wa Korona na Baada ya Korona kupungua kwenye Mkutano uliondaliwa na Taasisi ya Maendeleo ya Elimu ya Aga Khan , jijini Dar es Salaam.![]()

Mkuu wa Utafiti wa Taasisi ya Maendeleo ya Elimu ya Aga Khan Profesa Fredrick Mtenzi akizungumza kuhusianq na matumizi ya Tehema wakati wa ufungaji wa Mkutano wa Nchi za Afrika (Mashariiki Kenya, Uganda na Tanzania) ulioandaliwa na Taasisi hiyo jijini Dar es Salaam.![]()

Picha ya pamoja ya Wadau wa Elimu wa Tanzania wa Taasisi za Serikali na Taasisi zisizo za Kiserikali wakati wa Mkutano uliondaliwa na Taasisi ya Maendeleo ya Elimu ya Aga Khan jijini Dar es Salaam.![]()
Mkuu wa Taasisi ya Maendeleo ya Elimu ya Aga Khan Profesa Jane Rarieye akimkabidhi Mfuko ikiwa ni zawadi ya Taasisi ya Maendeleo ya Elimu ya Aga Khan Mkurugenzi wa Elimu Maalum wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dk.Magreth Matonya mara baada ya kufungwa Mkutano uliondaliwa na Taasisi hiyo jijini Dar es Salaam.
