Quantcast
Channel: MTAA KWA MTAA BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 39120

MKUTANO WA BARAZA LA WAFANYAKAZI WA OFISI YA RAIS, TUME YA MIPANGO WAFANYIKA MJINI KIBAHA, PWANI

$
0
0
Mgeni Rasmi wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe. Mwantumu Mahiza (aliyesimama) akisisitiza jambo alipokua akifungua kikao cha Baraza hilo.
Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango Bibi Florence Mwanri (aliyesimama) akimkaribisha mgeni rasmi Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Pwani Bibi Mwantumu Mahiza (aliyekaa kaikati). Kulia ni Katibu wa Baraza hilo Bw. Senya Robert.
Wajumbe wa baraza wakiwa katika hali ya utulivu katika kufuatilia na kuchangia mada mbalimbali wakati wa kikao hicho. Walioketi meza ya mbele kutoka kulia ni Bw. Paul Sangawe, Bw. Dunstan Nyeme, Bw. Abdul Nungu na Bi. Catherine Mbilia. Wengine walioketi meza ya nyuma kutoka kulia ni Bw. Saulo Fisoo na Bw. Paul Masibuka.
Wajumbe wa Baraza wakifuatilia kwa makini majadiliano yaliyokua yakiendelea wakati wa baraza hilo.
Wajumbe wa Baraza la wafanyakazi Ofisi ya Rais, Tume ya Mipando kwa pamoja wakiimba wimbo wa Solidarity Forever kuonyesha mshikamano makazini.
Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi, Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango wakionyesha mshikamano kwa kuimba wimbo wa Solidarity forever mara baada ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani kufungua rasmi kikao hicho.
Kabla ya kuanza majadiliano, wajumbe walimchagua Mwenyekiti Msaidizi wa Baraza la Wafanyakazi ambapo Bibi Magreth Simwela (aliyesimama) aliibuka mshindi kati ya wajumbe watatu waliokua wakigombea nafasi hiyo. Hapo Mwenyekiti Msaidizi alikua akiwashukuru wajumbe kwa kumchagua.
Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi, Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango wakiwa katika picha ya pamoja na Mgeni Rasmi Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Pwani Bi. Mwantumu Mahiza (Walioketi wa pili kushoto). Walioketi pamoja nae kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi Bibi Florence Mwanri, Mwenyekiti wa TUGHE Tawi la Mipango, Bw. Steven Katemba na Katibu wa Baraza Bw. Senya Robert.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 39120

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>