Quantcast
Channel: MTAA KWA MTAA BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 39146

Wateja wa Airtel na wasanii wakaribishwa kwenye uzinduzi wa Airtel Trace Music Star,coco beach kesho

$
0
0
Kampuni ya simu za mkononi Airtel inawatangazia wateja wake, wasanii na wanamuziki kuwa yale mashindano yanayotoa fulsa kwa wenye vipaji ya Airtel Trace yanazinduliwa rasmi kesho katika viwanja vya Coco beach jijini Dar es saalam kuanzia saa 12 jioni.

Uzinduzi huu utawashirikisha wasanii Wakali nchini akiwemo Ommy Dimples pamoja na kundi zima la ya YAMOTO BAND kwa burudani kabambe kwa umati utakao jitokeza hapo kesho katika viwanja hivyo.

Akitoa maelezo kuhusu uzinduzi huo, Meneja Masoko wa Airtel,Aneth Muga alisema "tunawakaribisha wateja wetu, wapenzi wa muziki na watanzania kwa ujumla katika viwanja vya coco beach kesho jumatano ili kushiriki pamoja nasi katika kusherehekea uzinduzi huu rasmi na kuanza safari ya kumtafuta mshindi wa Airtel Trace Tanzania.

Airtel kupitia Trace Music Star inatoa nafasi kwa wapenzi wa muziki na waimbaji chipukizi kupata dili poa kabisa kwa kurekodi akapela zao kupitia simu zao za mkononi kwa kipaga na kuimba kaktika namba 0901002233 na hatimae kupata nafasi ya kujishindia zawadi mbalimbali ikiwemo kuingia katika kinyanganyiro cha kuwa super star na mshindi wa Airtel Trace wa Afrika.

Sambamba na hilo tunapenda kuwatangazia watanzani kuwa namba yetu ya kukuwezesha kuwa mshindi ya 0901002233 sasa iko wazi, hivyo wanaweza kurekodi na kutuma nyimbo zao sasa . kwa maelezo zaidi tembelea tovuti yawww.tracemusicstar.com
Meneja Masoko wa Airtel Tanzania,Anethy Muga akitangaza namba itakayotumika katika mashindano ya Airtel Trace Music kuwa ni 0901002233 PIGA, IMBA , SHINDA na AIRTEL
Kikundi cha yamoto Band wakipasha kwaajili ya kutoa burudani kesho katika viwanja vya COCO beach kuanzia saa 12 jioni wakati wa Uzinduzi wa Airtel Trace Music Stars, Kiingilio ni BURE

Viewing all articles
Browse latest Browse all 39146

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>