Waziri Mkuu Mstaafu, Mh. Edward Lowassa akiusalimia umati wa wanaCCM pamoja na wananchi wa Mji wa Kigoma, wakati alipowasili kwenye ofisi za CCM Mkoa wa Kigoma, kusaka wadhamini wa kumsainia fomu za kupata ridhaa za Chama kuwania Urais wa Tanzania. Mh. Lowassa amedhaminiwa na wanaCCM 11,250 wa Mkoa wa Kigoma, leo Juni 13, 2015.
Umati wa WanaCCM pamoja na wananchi wa Mji wa Kigoma, ukiwa umefurika kwenye Uwanja wa Ofisi Kuu ya CCM Mkoa wa Kigoma, kuja kumuona Mh. Edward Lowassa (anaeonekana kule mbele) wakati alipofika kuomba udhamini wa wanachama wa CCM, ili aweze kupata ridhaa ya Chama kuwania Urais wa Tanzania kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015. Mh. Lowassa amepata udhaminiwa na wanaCCM 11,250 wa Mkoa wa Kigoma, leo Juni 13, 2015.
Katibu wa CCM Wilaya ya Kigoma Mjini, Noverty Kibaji akizungumza wakati akimuelezea Mh. Lowassa, idadi ya wanaCCM waliomdhani ili apate ridhaa ya Chama kuwania Urais wa Tanzania kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015.
Katibu wa CCM Wilaya ya Kigoma Mjini, Noverty Kibaji (kushoto) akimkabidhi, Mh. Edward Lowassa, majina ya wanaCCM wa Kigoma Mjini waliomdhani ili apate ridhaa ya Chama Cha Mapinduzi kuwania Urais wa Tanzania kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015.
Waziri Mkuu Mstaafu, Mh. Edward Lowassa akiteta jambo na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kigoma, Dkt. Aman Kaborou, muda mfupi kabla ya kupokea idadi ya majina ya wanaCCM waliomdhani ili apate ridhaa ya Chama Cha Mapinduzi kuwania Urais wa Tanzania kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015. Mh. Lowassa amedhaminiwa na wanaCCM 11,250 Mkoani Kigoma, leo Juni 13, 2015.