Quantcast
Channel: MTAA KWA MTAA BLOG
Viewing all 39073 articles
Browse latest View live

VIWANDA VYA SARUJI VYATAKIWA KUZALISHA SARUJI YA KUTOSHA PAMOJA NA KUSIMAMIA BEI YA SOKONI

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
SERIKALI imesema kuwa wenye viwanda vya saruji wazalishe saruji ya kutosheleza mahitaji ya ndani pamoja na kusimamia bei ya bidhaa hiyo mpaka kwa mlaji wa mwisho.

Hayo ameyasema Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charle’s Mwijage wakati alipotembelea viwanda vya Saruji vya Camel na Twiga , amesema amekosa hivi usingizi kwa kuadimika kwa saruji nchini na kuwataka viwanda hivyo vizalishe saruji ya kukidhi mahitaji ya ndani kutokana na kuwepo miradi mbalimbali ya ujenzi.

Mwijage amesema kuwa hivi karibuni kulikuwa kuadimika kwa saruji iliyotokana na baadhi ya viwanda kuwa katika matengenezo pamoja na makaa ya mawe kuzalishwa kwa kiwango kidogo.

Amesema kuwa katika kusimamia wizara hiyo kwa mzalishaji ambaye hatakwenda na kasi ya uzalishaji wa saruji anatomlaka ya kuifuta leseni hivyo wenye viwanda lazima wakidhi mahitaji ya saruji.

Aidha amesema kuwa kwa mwaka tani milioni 10.5 zinalishwa hivyo lazima kila kiwanda kiongeze uzalishaji na kuweza kuuza hata masoko ya nje ya nchi kwa kupata fedha za kigeni zinazotokana na saruji.


Amesema kuwa kuna viwanda vitatu vya saruji vinajengwa nchini ambavyo vitaongeza uzalishaji wa wa saruji hiyo.

Mwijage amesema kuwa viwanda vikizasha saruji na kuweza kuuza katika masoko ya nje kuna uwezekano wa bidhaa ya saruji ikwa inachangia uchumi wa nchi na kuongoza katika uchangiaji huo kwa pato la taifa.

Meneja wa Masoko wa kiwanda cha Saruji cha Twiga , Danford Semwenda amesema kuwa kwa sasa wanazalisha tani 6000 kutoka tani 300O kwa siku 15 zilizopita iliyotokana na matengenezo ya mtambo.
Waziri Mwijage leo Augusti 27,2018 ametembelea viwanda vya kutengeneza Saruji kuanzia cha Camel kilichopo Mbagala rangi Tatu na cha Twiga kilichopo Tegeta jijini Dar es Salaam.




 Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage akizungumza na viongozi wa kiwanda cha saruji cha Camel kilichopo Mbagala rangi tatu jijini Dar es Salaam.
 Mkurugezi Mtendaji wa Kiwanda cha Camel akitoa baadhi ya taarifa kwa 
 Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage kuhusiana na uzalishaji wa kiwanda hicho na jinsi wanavyokidhi soko jijini Dar es Salaam.

 Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage akitembelea kiwanda cha Camel kilichopo Mbagala jijini Dar es Salaam kwaajili ya kuangalia utendaji kazi wa kiwanda hicho kutokana na kukosekana kwa saruji hapa nchini.
 Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage akipewa maelezo na Mkurugenzi mtendajiwa kiwanda cha kuzalisha Saruji cha Camel, Gharibu Hamis jijini Dar es Salaam leo Augusti 27,2018 mara baada ya waziri huyo kutembelea kiwanda hicho.

 Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage akioneshwa baadhi ya maeneo ya kiwanda cha Camel kilichopo Mbagala jijini Dar es Salaam.

  Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage akitembelea kiwanda cha kutengeneza Saruji cha Camel kilichopo Mbagala jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage akipewa maelezo ya mchanga wa kutengenezea saruji katika kiwanda cha kutengeneza Saruji cha Camel jijini Dar es Salaam leo na Mkurugezi Mtendaji, Gharibu Salum wa Kiwanda cha Camel kilichopo Mbagala jijini Dar es Salaam leo, Augusti27,2018.
 Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa kiwanda cha Twiga,Alphonso Velez leo Augusti 27,2018 mara baada ya waziri huyo kutembelea kiwanda hicho.



  Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage akitembelea kiwanda cha Twiga kilichopo Tegeta jijini Dar es Salaam na kushoto ni Mkurugenzi Mkuuwa Kiwanda cha Twiga, Alphonso Velez


  Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage akionyesha baadhi ya mtambo wa Kiwanda cha Twiga Tegeta jijini Dar es Salam na kupata maelezo ya mtambo huo kutoka kwa Mkurugezi Mkuu wa kiwanda cha Twiga Tegeta,Alphonso Velez.



 Baadhi ya mitambo ya kiwanda cha Twiga Tegeta jijini Dar es Salaam.
 Mchanga wa kutengeneza Saruji katika kiwanda cha Saruji cha Twiga Tegeta jijini Dar es Salaam.
  Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage akizungumza jijini Dar es Salaam leo alipotembelea kiwanda cha Twiga Tegeta jijini Dar es Salaam.
Meneja wa Masoko wa kiwanda cha Saruji cha Twiga , Danford Semwenda akijibu swali kutoka kwa  Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage alipotembelea kiwanda cha Twiga kilichopo Tegeta jijini Dar es Salaam.Kulia ni Mkurugenzi Mkuuwa kiwanda cha Twiga kilichopo Tegeta jijini Dar es Salaa, Alfonso Velez.

LUGOLA AMSWEKA NDANI MKUU WA KITUO KIKUU POLISI MTWARA KWA KUSHINDWA KUWAWEKA MAHABUSU WATUHUMIWA

$
0
0
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kulia) akimuuliza maswali Mkuu wa Kituo cha Polisi Mtwara mjini, Ibrahim Mhando (kushoto) baada ya kushindwa kuwaweka mahabusu watuhumiwa wanne akiwemo Mhandisi Mshauri wa Kampuni ya Y&P Architects ambaye ni mshauri mkuu wa ujenzi wa Ofisi Kuu ya Uhamiaji Mkoani Mtwara. Katikati ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali, Jacob Kingu. Wapili kulia ni Kamanda wa Polisi Mkoa huo, Lucas Mkondya. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 

  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akitoka Kituo cha Polisi cha Kati mjini Mtwara mara baada ya kumsweka ndani Mkuu wa Kituo cha Polisi hicho ambaye aliwaweka watuhumiwa chumba cha upelelezi badala ya mahabusu kituoni hapo. Nyuma ya Waziri ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali, Jacob Kingu. Kulia ni Kamanda wa Polisi Mkoa huo, Lucas Mkondya. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kulia) akimuangalia Mkurugenzi wa Ufundi wa Kampuni ya Ujenzi ya Lucas, ambaye pia kandarasi aliyejenga Jengo la Uhamiaji Mkoa wa Mtwara, Theophilius Kessy, wakati alipokua anambana maswali ya kutaka kujua kwanini Jengo la Uhamiaji Mkoa wa Mtwara limejengwa chini ya kiwango. Aliyeshika kitabu ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali, Jacob Kingu. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.   
                                                                                                                         
Na Mwandishi Wetu, Mtwara
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amemweka ndani Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Kati mjini Mtwara (OCS), Ibrahim Mhando, kwa kushindwa kuwaweka mahabusu watuhumiwa wanne akiwemo Mhandisi Mshauri wa Kampuni ya Y&P Architects ambaye alitoa taarifa ya uongo kwa Waziri huyo kuhusu ujenzi wa Makao Makuu ya Uhamiaji Mkoani humo.

Tukio hilo lilitokea saa 12:46 asubuhi Agosti 27 leo Jumatatu, wakati Waziri Lugola na Katibu Mkuu wa Wizara yake, Meja Jenerali, Jacob Kingu walipofika Kituo hicho kikuu cha mkoa kwa kushtukiza wakati alipokua anakwenda Uwanja wa Ndege kwa ajili ya kurudi jijini Dar es Salaam, ndipo Waziri huyo alitaka kuthibitisha kama mtuhumiwa ambaye alielekeza jana usiku akamatwe awekwe mahabusu endapo Polisi walitekeleza agizo lake.

Hata hivyo, Waziri Lugola alimkuta mtuhumiwa huyo, Benjamin Kasiga akiwa chumba cha upelelezi badala ya kuwekwa mahabusu ya polisi hiyo, ndipo akamuuliza Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo, Lucas Mkondya, kwanini agizo lake halijatekelezwa.

“Hivi ndivyo polisi mnafanya hivi, haya ndio madudu mnayoyafanya? Tabia hii siku zote tunaipinga ikichafua Jeshi la Polisi, na hii ndiyo tabia yenu, najua ndio mana nimekuja ghafla, mnafahamu maadili ya Jeshi? RPC hawa polisi wako wanafanya nini, OCS njoo hapa, kwanini umeweka hawa watuhumiwa chumba cha upepelezi badala ya mahabusu, nawe unaingia ndani kwa kushindwa kuwaweka ndani hawa watuhumiwa, RPC muweke ndani sasa hivi huyu,” alisema Lugola akiwa amekasirika. 

Hata hivyo, Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo (RPC), Mkondya alimweleza Waziri Lugola kituoni hapo kuwa, Polisi wake walifanya makosa kwa kutowaweka mahabusu watuhumiwa hao.
Kwa upande wake mkuu wa kituo huyo, Mhando kabla ya kuwekwa mahabusu pamoja na wale watuhumiwa ambao alishindwa kuwaweka mahabusu, alisema sababu kuu yakutowaweka mahabusu watuhumiwa hao ni kwasababu mahabusu ilijaa na wanafanya hivyo mara chache inapotokea mahabusu wamekuwa wengi kituoni hapo. 

Waziri Lugola aliipinga kauli ya OCD huyo kuhusu mahabusu hiyo kujaa wakati nafasi ya kukaa watuhumiwa hao ilikuwepo ndani ya mahabusu hiyo, na watuhumiwa wangeweza kukaa bila tatizo lolote.

“Mbona nafasi ipo pale mahabusu, ile pale nafasi naiona, siwezi kukubaliana na uzembe huu, na hii ni tabia yenu huwa amnakamata watuhumiwa lakini baadhi hamuwaweki mahabusu, unanidanganya kuwa mahabusu imejaa, hii haikubaliki,” alisema Lugola. 
Lugola ambaye alikua katika ziara ya dharura katika Mkoa wa Mtwara na Lindi, baada ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ulinzi na Usalama kugundua majengo ya uhamiaji mikoa hiyo pamoja na Gereza Ruangwa yamejengwa chini ya kiwango. 
Aidha, akiwa wilayani Ruangwa, Lugola aliwataka wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama vilivyopo ndani ya Wizara yake kuwaondoa mara moja wananchi wote waliovamia katika maeneo ya majeshi nchini.

Lugola alisema hayo baada ya kulikagua Gereza jipya la Wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi linalojengwa ambalo lina ekari 100 lakini ekari 20 limevamiwa kwa kujengwa kiwanda cha kukamua mafuta ya alizeti, ufuta na korosho katika eneo hilo la Jeshi la Magereza. 
Akizungumza baada ya kulikagua Gereza hilo, mjini Ruangwa, Lugola alisema kuanzia sasa viongozi wa vyombo vyake wahakikishe hawaruhusu mwananchi yeyote kuingia katika maeneo ya jeshi na atakua mkali kulifuatilia suala hilo.

Lugola ambaye pia aliikataa kuipokea taarifa ya ujenzi wa gereza hilo ambayo ilikua inasomwa na Mkuu wa Magereza Mkoa wa Lindi, Rajabu Nyange, alisema taarifa hiyo ina upungufu mkubwa na hawezi kuipokea licha ya kua imeeleza kuhusu ardhi ya jeshi hilo kuvamiwa. 
“Mimi huwa nashangaa sana inakuaje wananchi wanavamia ardhi ya jeshi tena bila woga, halafu jeshi linakaa kimya linabaki kunung’unika, hii haijakaa sawa kabisa na kamwe sikubaliani nalo,” alisema Lugola.

Lugola aliongeza kua, “uvamizi wa ardhi mara nyingi unakua kwa jeshi la polisi na magereza, mbona Jeshi la Wananchi silisikii hili, kwanini nyie mnakaa kimya wananchi wakivamia ardhi yenu, sasa nawataka muhakikishe ardhi ya jeshi popote nchini iliyoporwa inarudishwa ndani ya jeshi, na wote waliovmia waondooeni haraka iwezekanavyo.” 

Kwa upande wake Mkuu wa Magereza mkoani humo, alisema licha ya ujenzi wa gereza hilo kuendelea kujengwa lakini ekari 20 ilichukuliwa kimakosa na kujengwa kiwanda cha kukamua mafuta ya alizeti na ufuta pamoja na kubangua korosho vinavyomilikiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa.

“Jitihada za ufuatiliaji urejeshaji wa eneo hilo zimefanyika ambapo Mkurugenzi wa Halmashauri hii ameonyesha nia ya kurejeshwa eneo hlo,” alisema Bakari.
Aliongeza kuwa, ujenzi wa gereza hilo ambalo linatarajiwa kukamilika Septemba mwaka huu, unatarajiwa kumaliza msongamano wa wafungwa  na mahabusu kwenye Gereza la Wilaya ya Nachingwea kutokana na mahabusu wengi kutoka Ruangwa.

Waziri Lugola alifanya ziara ya dharura katika mikoa hiyo, pia aliambatana na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Meja Jenerali, Jacob Kingu kwa kufanya ziara ya kutembelea Jengo lililokwama ujenzi la uhamiaji Mkoa wa Mtwara na Lindi na pia kulitembelea Gereza la mahabusu na wafungwa linalojengwa mjini Ruangwa, mara baada ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama kubaini mapungufu ya ujenzi wa majengo hayo. 

TSN OIL YAIBUKA KIDEDEA TUZO ZA AFRICA LEDERSHIP 2018

$
0
0
TSN Oil imeshinda tuzo ya Africa Leadership Oil and Gas Retail of the Year.

TSN Oil imeshinda tuzo ya Africa Leadership Oil and Gas Retail of the Year.
TSN Oil imeshinda tuzo hiyo ya ‘Oil and Gas Retail of the Year’ ya Africa Leadership Awards 2018, katika hafla iliyofanyika jana (tarehe 26 Agosti 2018) katika ukumbi wa hoteli ya Sandton Sun, Johannesburg Afrika ya kusini.

Tuzo hizo za Africa Leadership zinalenga kutunuku Washikadau mbalimbali na viongozi waliochangia mafanikio makubwa katika kukuza uchumi na uongozi bora. Tuzo hiyo kwa TSN Oil inatambulisha Mchango wake katika sekta ya Mafuta Nchini na pia jitihada zake katika kupeperusha bendera wa ukuwaji wa sekta hiyo hapa Tanzania. 

Tuzo ya TSN Oil ilikabidhiwa na Senator wa Marekani jimbo la Georgia, Michaael Rhett, na kupokelewa na Mkurugenzi wa TSN Group , Bwana Farough Ahmed Baghozah mwenyewe.Mr Farough ametambuliwa kama Mchangiaji Mkubwa katika ukuaji wa sekta na biashara ya Mafuta Nchini kutokana na Mchango wake, Muda wake wa thamani katika kupigania sekta hiyo na kwa nafasi ambayo TSN Oil imecheza hapa nchini.

Mkurugenzi wa TSN Oil kampuni dada ya TSN Group yenye zaidi ya Miaka 10 kwenye sekta ya Mafuta, Farough Ahmed Baghozah akipokea tuzo hiyo amesema “Ushindi huu unamaana kubwa kwetu kama kampuni na kama Nchi kwa ujumla, unatambulisha kukua kwa sekta hii katika uchochezi wa ukuwaji wa sekta ya viwanda hapa nchini inayohamasishwa na Rais wetu Dr. John Pombe Magufuli Unaelezea safari yetu kama kampuni kwa kusimamia ubora na mhimili wa kauli mbiu yetu, Tanzania Sisi Nyumbani. “
“Tunashukuru na kuendela kuwashukuru wateja wetu kama wadau wakuu kwenye utambulisho huu, Tanzania hii ni ya kwenu.”

Kampuni ya TSN Oil yenye makazi yake makuu Dar es salaam na depo ya mafuta iliyopo Kisosora Tanga inamiliki vituo vya mafuta zaidi ya 28 na kushika asilimia 5% ya soko la Mafuta nchini Tanzania, kwa zaidi ya miaka 10 tangu kuanzishwa kwake 14th November, 2006.
Mafanikio ya TSN Oil ambayo ilitokana na Chemoil yanaonekana kwa kuzalisha pia kampuni nyingine dada kama. 
2009 - TSN Supermarket Ltd 
2010 - TSN Logistics Ltd 
2012 - TSN Distribution Ltd

2015 – Prime Brands Distribution Co. Ltd / TSN Media / TSN Foundation

MAPITIO YA MAGAZETI LEO

Viongozi wa zamani wa KCU 1990 Ltd wakosa dhamana

$
0
0
Viongozi wa zamani wa Chama Cha Ushirika Kagera (KCU 1990 Limited) wataendelea kusota rumande baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Bukoba mkoa wa Kagera   kuwanyima dhamana kutokana na kukabiliwa na mashtaka ya kuhujumu uchumi kwa ubadhilifu wa shilingi Milioni 218 wanaodaiwa kuufanya.

Akisoma uamuzi kuhusu ombi la washitakiwa kutaka wapatiwe dhamana jana Agosti 27, 2018 hakimu mkazi mfawidhi, John Kapokolo alisema mahakama hiyo haina uwezo wa kusikiliza kesi za uhujumu uchumi na kutaka maombi yao yapelekwe kwenye mahakama sahihi.

Akizungumza  mara baada Hakimu Kapokoro kutoa uamuzi huo, mwendesha mashaka wa serikali alisema mahakama hiyo haina mamlaka ya kutoa dhamana kwa watuhumiwa hao kwa kuwa baadhi ya tuhuma zinazowakabili zinahusiana masuala ya kuhujumu uchumi.

Kufuatia uamuzi huo wakili anayewatetea watuhumiwa hao, Aron Kabunga alisema mahakama hiyo haikuwatendea haki wateja wake  kwani mahakama hiyo haikuwa na sababu zozote za kuwanyima dhamana hadi kesi hiyo itapotajwa tena Septemba 10, mwaka huu.


Washitakiwa hao John Binunshu aliyekuwa mwenyekiti wa bodi, Vedastus Ngaiza aliyekuwa meneja mkuu na Bestina Rwebangira walifikishwa katika mahakama hiyo wiki iliyopita na kusomewa mashitaka matano.

Mashtaka yaliyosomwa na wakili mwandamizi wa Serikali, Athumani Matuma ni kula njama, matumizi mabaya ya ofisi, matumizi mabaya ya madaraka, kughushi nyaraka na kuhujumu uchumi na kusababisha hasara ya Sh124 milioni.

Wakili wa washitakiwa Aaron Kabunga alipinga hati ya mashitaka kuwa iliunganisha makosa ya uhujumu uchumi na mengine bila kuwa na kibali cha mkurugenzi wa mashitaka na hivyo alitaka hati hiyo itupiliwe mbali na wateja wake wapewe dhamana.

Tayari Serikali Ilishavunja Uongozi huu uliofikishwa mahakamani na kuchagua uongozi mpya unaokiendesha chama hicho cha Ushirika KCU 1990 Ltd.

DKT. MPANGO: AAGIZA MAKONTENA YA MAKONDA YAPIGWE MNADA LICHA YA VITISHO VYAKE

$
0
0
 Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) akiwasili kukagua Kontena  ishirini za Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Paul makonda, zilizo na Samani vikiwemo viti na Meza katika Bandari ya Dar es Salaam.
 Kamishna wa Forodha  wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Benny Usaje (kulia), akimwongoza Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) kukagua Kontena  ishirini za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Paul Makonda, zinazodaiwa kodi ya takribani Sh. Bilioni 1.2, zilizopo katika Bandari ya Dar es Salaam.
 Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) akifunguliwa Kontena Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Paul Makonda, zenye Samani za Viti na Meza ili kushuhudia kilichopo kabla hajaagiza taratibu za mnada ziendelee ili kodi inayodaiwa ya thamani ya Sh. Bilioni 1.2 iweze kupatikana.
 Baadhi ya meza zilizopo katika moja ya Kontena  ambazo  zinadaiwa kodi ya Sh. Bilioni 1.2, wakati Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) alipofanya ziara katika Bandari ya Dar es Salaam na kuagiza Kamishna wa Forodha kuchukua hatua za kisheria ikiwemo kupigwa mnada kwa vifaa hivyo ili kodi ya Serikali ipatikane.
 Afisa Forodha Mfawidhi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bandari ya Dar es Salaam Bw. Stephano Mathias, akitoa maelezo  kwa Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoto) kuhusu bidhaa za samani za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Paul Makonda, zinazodaiwa kodi ya Sh. Bilioni 1.2, huku mmiliki wake akijulikana kwa jina Paul Makonda.
 Baadhi ya viti vilivyopo katika Kontena zinazodaiwa kodi ya Sh. Bilioni 1.2, wakati Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) alipofika kukagua na kujiridhisha kama kuna taratibu za kodi zimekiukwa ili mzigo huo wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Paul Makonda uweze kuendelea kupigwa mnada.
 Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) akitoa maagizo kwa Kamishna wa Forodha  wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Benny Usaje, ya kuendelea kupigwa mnada kwa Kontena ishirini za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Paul Makonda, zinazodaiwa kodi ya Sh. Bilioni 1.2 ili Serikali iweze kupata kodi yake kama kodi kutoka kwa mmiliki wa Kontena hizo hatalipa kodi kwa wakati.
 Kamishna wa Forodha  wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Benny Usaje (katikati) akieleza kuwa amepokea maagizo ya Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) mwenye dhamana ya kodi nchini kuhakikisha kodi ya kiasi cha Sh. Bilioni 1.2 inalipwa kwa mujibu wa sheria kwenye Kontena hizo 20 za RC Paul Makonda. (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Setrikalini Wizara ya Fedha na Mipango).

Benny Mwaipaja, WFM, Dar es Salaam
WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, amefanya ziara ya kushitukiza katika eneo la kuhifadhia makontena-Bandari Kavu Dar es Salaam (DICD), na kukagua makontena 20 yaliyoingizwa nchini na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na kuiagiza Mamlaka ya Mapato Tanzania -TRA kuendelea na mnada wa makontena hayo ili kupata kodi ya Serikali inayokadiriwa kufikia shilingi bilioni 1.2.

Dkt. Mpango amesema kuwa kodi hiyo inadaiwa kwa mujibu wa sheria za nchi baada ya mwenye mali kushindwa kulipa kodi na kwamba amesikitishwa na vitisho vinavyotolewa na Mkuu huyo wa Mkoa na vilivyonukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari nchini  akitumia vifungu vya Biblia kwamba yeyote atakaye nunua mzigo huo atalaaniwa.

"Sheria za nchi hazichagua sura wala cheo cha mtu, na mimi ndicho nilicho apa, kutekeleza sheria za nchi, sheria za kodi, ndiyo dhamana niliyo pewa kwahiyo Kamishna, simamia sheria za kodi bila kuyumba" alisisitiza Dkt. Mpango akitoa maelekezo kwa Kamisha wa Forodha Bw. Ben Usaje.

Alifafanua kuwa mzigo wa Samani ulioagizwa kutoka nje ya nchi hauna msamaha wa kodi na kwamba huyo aliye agiza (RC Paul Makonda) alipe kodi stahidi na asipo lipa kodi hiyo mchakato unaoendelea wa kuyapiga mnada makontena hayo uendelee.

"Napenda niwaombe viongozi wenzangu Serikalini, ni muhimu tukachuja maneno! unasema mtu anayekuja kununua samani atapata laana, tena laana ya Mungu, kwa nini tunamhusisha Mungu kwenye vitu vya namna hii" alieleza kwa masikitiko Dkt. Mpango

Dkt. Mpango alitoa wito kwa watanzania wanaotaka kununua bidhaa hizo ambazo nyingi ni vifaa vinavyoweza kutumika shuleni ama maofisini kama vile viti meza na makabati, kujitokeza bila hofu kununua mali hizo.

 Aliwaomba walimu na wanafunzi wasiwe na wasiwasi na kwamba Serikali ya Awamu ya Tano imejipambanua na kuwekeza kwenye elimu kwa kutenga zaidi ya shilingi bilioni 20 kila mwezi kulipa ada ya wanafunzi ili wasome bila kulipa ada na ina mpango madhubuti wa kuboresha miundombinu ya elimu nchi nzima ikiwemo ujenzi wa madarasa na ofisi za walimu.

"Tunawapenda na kuwathamini sana walimu wetu, asitokee mtu yeyote  akaanza kuwaambia hadithi kama vile Serikali hii inawapuuza! si kweli hata kidogo" Aliongeza Dkt. Mpango

Kwa upande wake, Kamishna wa Forodha wa Mamlaka ya Mapato Tanzania-TRA, Ben Usaje, alimweleza Dkt. Philip Mpango kwamba Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Paul Makonda, aliwasilisha maombi ya kutaka kupewa msamaha wa kodi wa makontena 36 yenye samani kutoka Diapora nchini Marekani.

Alisema kuwa kati ya makontena hayo, yaliyoingia nchini ni makontena 20 ambayo yanadaiwa kodi ya shilingi bilioni 1.2 na kwamba utaratibu kwa kumtaka Paul Makonda alipe kodi hiyo ili aruhusiwe kuyachukua makontena hayo ulifanyika kwa mujibu wa sheria na kwamba mpaka sasa hajayachukua ndio maana yanapigwa mnada.

Naye aliwatahadharisha watu wanao tumia masuala ya siasa na uongozi Serikalini kutaka kukwepa kulipa kodi a kwamba suala la kodi za samani zinaonekana ziko juu kwa sababu Bunge lilitunga sheria hiyo ili kulinda soko la ndani la samani na kuweka sheria ya kutokuwepo kwa msamaha wowote wa kodi kwenye bidhaa kama hizo.

Dkt.KIJAJI AFUNGUA MKUTANO 41 WA BIMA KUTOKA NCHI 39 MASHARIKI NA KUSINI MWA AFRIKA(OESAI)

$
0
0

Naibu Waziri wa Fedha Dkt. Ashantu Kijaji akizungumza katika mkutano wa 41 wa umoja wa kikanda wa makampuni ya Bima kutoka nchi 39 za Mashariki na Kusini mwa Afrika (OESAI) Picha na Vero Ignatus.
Kamishna wa Mamlaka ya Usimamizi wa BIMA nchini (TIRA) Dk, Baghayo Saqware akifafanua jambo kwa waandishi wa habari leo Jijini Arusha. Picha na Vero Ignatus

Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya mkutano huo,Khamis Suleiman akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Arusha.
Wapili kutoka kushoto ni Naibu waziri wa Fedha Dkt. Ashantu Kijaji, aliyepo kulia kwake ni Kamishna wa Mamlaka ya Usimamizi wa BIMA nchini (TIRA) Dk, Baghayo Saqware, akifuatiwa na Rukia Adam Mjumbe kutoka (TIRA) wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe kutoka baadhi ya matataifa 39 Duniani. Picha na Vero Ignatus.

Na.Vero Ignatus.Arusha
Mkutano wa 41 wa umoja wa kikanda wa makampuni ya Bima kutoka nchi 39 za Mashariki na Kusini mwa Afrika (OESAI) umefunguliwa leo rasmi mkoani Arusha.

Mkutano huo umefunguliwa na Naibu waziri wa fedha Dkt. Ashatu Kijaji ambapo ameyataka makampuni ya Bima kutoa huduma za Bima kwa wakulima ili kufikia uchumi wa kati.

Dk, Kijaji amesema asilimia 75 ya Watanzania ni wakulima ambao bado hawana elimu kuhusu bima ikiwemo kupata mikopo ya bei nafuu kwaajili ya kutatua changamoto za kilimo na kufikia katika uchumi wa kati.

Ameyataka makampuni ya bima nchini kuangalia kundi hilo la wakulima ili nao waweze kunufaika na bidhaa wanazozalisha kwakuwa kundi hilo ni kubwa na ni fursa kwa makampuni ya bima nchini kuongeza idadi ya watumiaji wa bima.

Amesema watanzania wanaotumia bima hapa nchini ni chini ya asilimia moja idadi ambayo hairidhishi kabisa kwakuwa watanzania wapo zaidi ya milioni 45 kwa mujibu wa ofisi ya Takwimu za Taifa.

Kamishna wa Mamlaka ya Usimamizi wa BIMA nchini (TIRA) Dk, Baghayo Saqware amesema mkutano huo wa 41 unatoa fursa kwa kampuni za bima zilizopo hapa nchini kujifunza jinsi kampuni za nje za bima zinavyofanya kazi kwa ufanisi.

Aidha amesema kampuni hizo zitapata fursa ya kujifunza uboreshaji wa huduma kwa kutumia mfumo wa Tehama unaoleta mageuzi katika utoaji wa huduma bora zako bima, rasilimali watu na kuongeza wigo wa kutafuta watu mbalimbali kwaajili ya kulipia bima ya maisha.

Hata hivyo Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya mkutano huo,Khamis Suleiman amesema lengo la mkutano huo ni kuhakikisha ifikapo mwaka 2020 asilimia 50 ya watanzania wawe na aina yoyote ya bima kwani kwa sasa Tanzania ipo kwenye nafasi ya pili kwa nchi za Afrika Mashariki kwa kutoa huduma za bima

CHANGAMOTO ZA USAFIRI HAZIKWAMISHI USAMBAZAJI DAWA VISIWANI MULEBA

$
0
0
 Mkazi wa Kata ya Katunguru, Robert Lomwadi, akipakia moja ya boksi la dawa, katika Boti namba BKT 00098 MV BMU Mulumo tayari kupelekwa Zahanati ya Kisiwa cha Mazinga, wilayani Muleba mkoani Kagera leo hii.
 Mganga Mkuu wa Wilaya ya Muleba, Dkt. Modest Burchard, akizungumza na waandishi wa habari kuhusu masuala mbalimbali ya afya na upokeaji wa dawa kutoka MSD.
 Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Kisiwa cha Mazinga, Johanes Sweetbert (kulia), akizungumza na waandishi wa habari kuhusu jinsi wanavyopokea dawa kutoka MSD na changamoto zilizopo.
 Afisa Huduma kwa Wateja wa MSD Kanda ya Mwanza, Cornelia Mwillawi (kushoto), akizungumza na Wajumbe wa Kamati ya Afya wa Kisiwa cha Mazinga wakati wa kukabidhi dawa.
 Afisa Huduma kwa Wateja wa MSD Kanda ya Mwanza, Cornelia Mwillawi (kushoto), akiwakabidhi mifuko ya vifaa vya mama vya kujifungulia.
 Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Kisiwa cha Mazinga, Johanes Sweetbert (wa pili kulia), akisaini fomu maalumu baada ya kukabidhiwa vifaa hivyo. Wendine ni wajumbe wa kamati ya afya wa Kisiwa cha Mazinga.
 Mkazi wa Kata ya Katunguru, Robert Lomwadi, akibeba boksi la dawa kuzipeleka tayari kwenda kwenye boti kabla ya kuziingiza kwenye boti.
 Mjumbe wa Kamati ya Afya ya Kisiwa cha Mazinga, Winfrida Itaganisa, akizungumzia jinsi wanavyo pokea dawa kutoka MSD.
Wananchi wa Kata ya Katunguru walioshuhudia makabidhiano ya dawa hizo.

Na Dotto Mwaibale, Muleba Kagera.  

MGANGA Mkuu wa Wilaya ya Muleba, Dkt. Modest Burchard amesema licha ya changamoto za kusafirisha dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara kwenda visiwani, Bohari ya Dawa (MSD) imekuwa ikitoa ushirikiano mkubwa kuhakikisha dawa zinafika kwenye vituo vya kutolea huduma za afya kwa wakati kwenye visiwa 26 vilivyopo katika wilaya hiyo.

Dkt. Burchard ameyasema hayo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari ambao wapo ziarani mkoani Kagera kuangalia taratibu za usambazaji dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara pamoja na kuzungumza na wateja wa MSD.

"Tunaishukuru sana MSD kwa kazi kubwa ya kufikisha dawa katika maeneo yote ya visiwa licha ya kuwepo kwa changamoto ya usafiri majini, hasa vipindi vya hali mbaya ya hewa kwenye ziwa victoria".

Alisema katika mkoa wa Kagera, wilaya ya Muleba ndiyo ina visiwa vingi lakini serikali kwa kushirikiana na MSD wamefanikiwa kufikisha dawa katika visiwa hivyo kwa ushirikiano mkubwa wa wananchi.

Aliongeza kuwa Halmshauri ya Wilaya ya Muleba ina boti mbili kwa ajili ya kusafirisha wananchi kutoka mwaloni katika Kijiji cha Katunguru kwenda kisiwa cha Mazinga, ambapo pia ina mpango wa kununua boti jingine kwa ajili ya kuongeza nguvu ya usafirishaji.

Akizungumzia kuhusu upatikanaji wa dawa muhimu wilayani humo, alisema hivi sasa hali ni nzuri kwani upatikanaji wake ni kati ya asilimia 90 hadi 98  na kuwa hali hiyo imetokana na ushirikiano uliopo baina ya Serikali na MSD.

"Kuhusu upatikanaji wa dawa kwa kweli hivi sasa hakuna mtu anayelalamika kwani serikali imeongeza fedha katika bajeti yake  karibia mara 10 kutoka sh.bilioni 30 mwaka 2015/16 hadi kufikia sh.bilioni 260 kwa mwaka wa fedha 2018/2019 ambapo kwa wilaya yetu tunatumia zaidi ya milioni 600 kwa ununuzi wa dawa" alisema Burchard.

Alisema wilaya hiyo ina kata 43, wakazi 750,000 wanaotoka kwenye visiwa ishirini na sita, huku ikiwa na vituo vya afya vitano, zahanati 27 na Hospitali teule moja ya Rubya.

Naye Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Kisiwa cha Mazinga, Johanes Sweetbert alisema licha ya usafiri wa majini kuwa na changamoto zake lakini dawa zote muhimu zimekuwa zikipatika na kuwa zahanati hiyo inahudumia vijiji viwili vya Iramba na Rubili ambavyo vina visiwa tisa ambavyo ni Rubili, Iramba, Mjunwa, Runenke, Magege, Garinzila, Kino, Mazinga na Buyonzi.

Alisema mawasiliano mazuri kati ya MSD na serikali yamewezesha dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara kufika kwa wakati ambapo hutumia boti kusafirisha dawa hizo pamoja na wagonjwa waliopewa rufaa kwenda hospitali ya wilaya.

Mmoja wa wajumbe wa Kamati ya Afya wa Kisiwa cha Mazinga Winfrida Itaganisa amesema kamati ya afya imekuwa ikivuka kwenda Muleba kwa ajili ya kupokea dawa wanazokuwa wameomba na kufanya makabidhiano kabla ya kuvushwa.


WASIMAMIZI WA UCHAGUZI MDOGO WATAKIWA KUZINGATIA SHERIA, KANUNI NA TARATIBU.

$
0
0
  Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji (Rufaa), Semistocles Kaijage akifungua mafunzo kwa Wasimamizi wa Uchaguzi na Wasimamizi Wasaidizi Uchaguzi mdogo wa Ubunge na Udiwani utakaofanyika Septemba 16 mwaka huu katika Majimbo ya Ukonga, Korogwe Vijijini, Monduli na kwenye Kata 23 za Tanzania jijini Dodoma.
 Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Dkt. Athumani Kihamia akiwasilisha Mada wakati wa mafunzo kwa Wasimamizi wa Uchaguzi na Wasimamizi Wasaidizi Uchaguzi mdogo wa Ubunge na Udiwani utakaofanyika Septemba 16 mwaka huu katika Majimbo ya Ukonga, Korogwe Vijijini, Monduli na kwenye Kata 23 za Tanzania jijini Dodoma.
Baadhi ya Wasimamizi wa Uchaguzi na Wasimamizi Wasaidizi Uchaguzi mdogo wa Ubunge na Udiwani utakaofanyika Septemba 16 mwaka huu katika Majimbo ya Ukonga, Korogwe Vijijini, Monduli na kwenye Kata 23 za Tanzania wakifuatilia Mada mbalimbali  jijini Dodoma.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imewataka Wasimamizi wa Uchaguzi mdogo wa Ubunge na Udiwani utakaofanyika Septemba 16 mwaka huu katika Majimbo ya Ukonga na Monduli na kwenye Kata 13 za Tanzania Bara kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia matakwa ya Katiba, Sheria na Kanuni zinazosimamia uchaguzi huo.

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji (Rufaa), Semistocles Kaijage ameyasema hayo jijini Dodoma wakati akifungua mafunzo kwa Wasimamizi wa Uchaguzi na Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi wa Kata na Majimbo hayo.

Jaji Kaijage amewataka Wasimamizi hao kuzingatia weledi na kuepuka kufanya kazi kwa mazoea ili wapunguze na kuondoa malalamiko yanayojitokeza wakati wa uchaguzi.

Amesema  Uchaguzi ni mchakato unaojumuisha hatua na taratibu mbalimbali zinazopaswa kufuatwa na kuzingatiwa akisisitiza kwamba hatua na taratibu hizo ndiyo msingi wa uchaguzi mzuri wenye ufanisi usio na malalamiko au vurugu.

“ Tunakutana hapa kwa muda wa siku tatu (3) ili kwa pamoja tubadilishane uzoefu, tujadili namna ya kufanikisha zoezi la uchaguzi lakini pia namna ya kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazoweza kujitokeza katika hatua zote za uchaguzi,” Amesema Jaji Kaijage.

Aidha, amewataka Wasimamizi hoa waepuke madhara yanayotokana na ukiukaji wa Sheria, Kanuni na taratibu za Uchaguzi  na akisisitiza kwamba katika kipindi hiki chaguzi  zinafanyika katika mazingira ambayo yana hamasa kubwa ya Kisiasa, kutoaminiana na wakati mwingine hutawaliwa na mihemko ambayo imekuwa chanzo cha uvunjifu wa amani.

Jaji Kaijage amewaeleza Wasimamizi hao kwamba wameaminiwa na kuteuliwa katika nafasi hizo za usimamizi wa Uchaguzi kwa kuwa wana uwezo wa kufanya kazi hiyo hivyo wajiamini na kujitambua.

Amaetoa wito kwa Wasimamizi hao kuhakikisha kuwa wanayaelewa vema maeneo yao ya kazi na kuhakikisha kwamba wanawatumia vizuri wasaidizi walio nao katika maeneo yao kwa matokeo bora.

“Mjue mna jukumu la kuimarisha imani ya wananchi pamoja na wadau wote wa uchaguzi kwa Tume. Hivyo mfanye kazi kwa ufanisi wa hali ya juu, bila kuegemea upande wowote. Kufanya kazi kwa uhuru na kwa uwazi kutasaidia kudumisha amani katika maeneo yenu ya Uchaguzi” Amesisitiza.

Kuhusu kufanyika kwa Uchaguzi huo mdogo Septemba 16 mwaka huu,  Jaji Kaijage amesema kwa kuzingatia matakwa ya kifungu cha 37 (1) (b) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura 343 kikisomwa pamoja na kifungu cha 13(3) cha Sheria ya Serikali za Mitaa, Sura 292, ni jukumu la Tume kusimamia, kuendesha na kuratibu uchaguzi wa kujaza nafasi zilizo wazi.

Amesema kwa nyakati tofauti Tume imepokea taarifa kutoka kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye kwa kuzingatia Kifungu cha 37 (3) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura 343 aliitaarifu Tume uwepo wa nafasi wazi za Ubunge katika Majimbo ya Ukonga, Korogwe Vijijini na Monduli.

Pia amefafanua kuwa Waziri mwenye dhamana ya Serikali za Mitaa, ambaye kwa kuzingatia masharti ya kifungu cha 13(1) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali ya Mitaa, Sura, 292 alitoa taarifa ya uwepo wa nafasi wazi za Madiwani katika Kata 23 kutoka katika Halmashauri 15 zilizopo katika Mikoa 10 ya Tanzania Bara.

Aidha, katika uchaguzi huu mdogo wa Ubunge na Udiwani utakaofanyika Septemba 16 mwaka huu Mgombea Ubunge katika Jimbo la Korogwe Vijijini amepita Bila Kupingwa na jumla ya wa wagombea 10 wa Udiwani katika Kata 10 wamepita bila Kupingwa, hivyo jumla ya Kata zilizobaki zitakazoingia kwenye uchaguzi mdogo ni 13 na Majimbo 2 ya Monduli, Arusha na Ukonga jijini Dar es salaam.

CAF YARIDHISHWA NA MAANDILIZI YA AFCON

$
0
0
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (C)akipokea Bendera ya CAF kutoka kwa Rais wa  Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) Ahmad Ahmad baada ya mazungumzo ya kikazi katika Ofisi ndogo ya Waziri Mkuu Jijini Dar es Salaam Agosti 27/2018.kushoto kwa Waziri Mkuu ni Waziri wa Michezo na Utamaduni Dkt Harisson Mwakembe.
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja Rais wa Shirikisho la Soka Barani Aafrika  (CAF ). Ahmad Ahmad, Waziri Mkuu ni Waziri wa Michezo na Utamaduni Dkt Harisson Mwakembe pamoja na viongozi wa mpira wa Tanzania.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiagana na Rais wa Shirikisho la Soka Barani Aafrika  (CAF ). Ahmad Ahmad . baada ya mazungumzo ya kikazi  katika ofisi ndogo ya Waziri Mkuu Jijini Dar es Salaam  Agosti 27/2018

RAIS wa Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF), Bw. Ahamd Ahmadamesema ameridhishwa na maandalizi ya michuano ya Afrika ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 (AFCON).

Mashindano ya mpira wa miguu kwa Vijana wenye umri wa chini ya  miaka 17 AFCON yanayotarajiwa kufanyika mwaka 2019 nchini Tanzania.

Ameyasema hayo Jumatatu, Agosti 27, 2018 wakati akizungumza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa katika makazi ya Waziri Mkuu, Oysterbay jijini Dar es Salaam.

Pia ameihakikishia Serikali kwamba hakuna mabadiliyo yoyote ya ratiba yatakayofanyika kuhusu wenyeji wa mashindano na kwamba CAF itaendelea kushirikiana na Tanzania katika kufanikisha michuano hiyo.

Rais wa CAF yupo nchini kwa ajili ya kuongoza mkutano maalum wa mabadiliko ya katiba ya Baraza la Vyama vya Soka katika Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati (CECAFA).

Mkutano huo unaofanyika jijini Dar es Salaam, umehudhuriwa na viongozi wa juu wa nchi wanachama wote 12 wa CECAFA wakiwemo marais.

Kwa upande wake,Waziri Mkuu WAZIRI amesema mechi zoteza michuano ya Afrika ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 (AFCON) zitafanyika jijini Dar es Salaam.mashindano

“Tupo katika hatua za mwisho za maandalijzi ya michuano hiyo itakayofanyika jijini Dar Es Salaam katika viwanja vya Taifa, Uhuru, Chamanzi na JK Park utatumika kwa mazoezi.”

Waziri Mkuu amesema ni muhimu kwa nchi kushiriki katika mashindano makubwa kama hayo kwa kuwa yanasaidia kwenye ukuzaji wa vipaji kwa vijana ambao wengi wao ni wanafunzi.

TRA YATAJA WALENGWA WANAOSTAHILI MSAMAHA WA RIBA NA ADHABU YA MALIMBIKIZO YA KODI

$
0
0
Na Veronica Kazimoto, Tabora

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imewataja walengwa wanaostahili kuomba msamaha maalum wa riba na adhabu ya malimbikizo ya madeni ya kodi kwa asilimia 100 ambapo mwisho wa kutuma maombi ya msamaha huo ni tarehe 30 Novemba, 2018.

Akizungumza wakati wa mkutano wa washauri wa walipakodi (Tax consultants)  mkoani Tabora, Afisa Elimu Mkuu kwa Mlipakodi wa mamlaka hiyo Rose Mahendeka amesema Walengwa wa msamaha huu ni makampuni, taasisi na watu binafsi ambao wamewasilisha ritani za kodi lakini bado wanadaiwa kodi yote au sehemu ya kodi zitokanazo na ritani hizo.

"Walengwa wengine ni wale wote ambao hawajawasilisha ritani za kodi, hawajasajiliwa na kupatiwa Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi (TIN) au Namba ya Usajili wa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) na wale walio wasilisha pingamizi au rufaa za kodi ambazo bado zinashughulikiwa katika ofisi za TRA, Bodi ya Rufaa na Mahakama ya Rufani za kodi", alisema Mahendeka.

Aidha, amewataja wasiohusika na msamaha huu kuwa ni pamoja na wale ambao wangestahili kupata msamaha lakini tayari wameshalipa madeni yao, ambao masuala yao ya kikodi yapo katika hatua ya ukaguzi au uchunguzi, wana madeni ya nyuma ya kodi ambayo yanatokana na kesi za jinai za kodi, utakatishaji fedha, usafirishaji wa binadamu au shughuli nyingine haramu kama ilivyothibitika kisheria.

"Wengine ambao hawahusiki na msamaha huu ni taasisi, makampuni na watu binafsi ambao wana madeni ya nyuma ya kodi yanayotokana na adhabu zilizoamuliwa tayari au adhabu za makosa yatokanayo na uzembe wa kukusudia uliobainika kisheria pamoja na wenye riba au faini zilizotokana na kutoa au kutumia risiti za kielektroniki za kughushi," alibainisha Mahendeka.

Kwa upande wake Afisa Elimu kwa Mlipakodi wa TRA Chama Siriwa ametoa wito kwa washauri wa walipakodi mkoani hapa kuendelea kuwaelimisha wafanyabiashara na wale wote wenye taasisi na makampuni mbalimbali yenye malimbikizo ya madeni ya kodi kuwahi kutuma maombi ya msamaha huo kabla muda uliopangwa haujamalizika.

"Mimi napenda tu kusisistiza kuwa mwisho wa kutuma maombi ya msamaha huu ni tarehe 30 Novemba, 2018. Hivyo, natoa wito kwenu washauri wa walipakodi muendelee kuwaelimisha wafanyabiashara na wote wenye taasisi na makampuni kutuma maombi mapema ili waweze kunufaika na msamaha huu," alieleza Siriwa.

Serikali kupitia Mamlaka ya Mapato Tanzania ilitangaza msamaha wa riba na adhabu ya malimbikizo ya madeni ya kodi mwezi Julai, 2018 kwa lengo la kutoa unafuu kwa walipakodi wenye malimbikizo ya madeni ya riba na adhabu kwa kusamehe madeni yao na kuwapa fursa ya kulipa malimbikizo ya madeni ya msingi ya kodi - principal tax mara moja au kwa awamu ndani ya mwaka wa fedha wa 2018/19.

Vodacom yazindua njia ya kipekee ya kuhamisha data kwa kutumia duka la kidijitali

$
0
0
 Mkurugenzi  Mtendaji wa Dar Teknohama Business Incubator (DTBi), Mhandisi Dkt, George Mulamula ( kulia) akikata utepe  wakati wa  uzinduzi wa duka jipya la Vodashop lenye sehemu maalum ya kutengenezea simu (Techzone) na kuhifadhi na kuhamisha kumbukumbu lililopo  makao makuu ya kampuni  hiyo Vodacom Tower Morocco jijini Dar es Salaam.Kushoto  ni Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania Plc,  Rosalynn Mworia.
 Mkurugenzi  Mtendaji wa Dar Teknohama Business Incubator (DTBi), Mhandisi Dkt, George Mulamula ( katikati) na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania Plc,  Rosalynn Mworia (kulia) wakimsikiliza mtaalamu wa Data,   Hendrick  Rupia wakati wa  uzinduzi wa duka jipya la Vodashop lenye sehemu maalum ya kutengenezea simu na kuhifadhi na kuhamisha kumbukumbu lililopo  makao makuu ya kampuni  hiyo Vodacom Tower Morocco jijini Dar es Salaam
 Mkurugenzi  Mtendaji wa Dar Teknohama Business Incubator (DTBi), Mhandisi Dkt, George Mulamula (wa pili kulia)  akiongea   na wafanyakazi wa Vodacom    wakati wa  uzinduzi wa duka jipya la Vodashop lenye sehemu maalum ya kutengenezea simu na kuhifadhi na kuhamisha kumbukumbu  lililopo  makao makuu ya kampuni  hiyo Vodacom Tower, Morocco jijini Dar es Salaa , wapili kushoto ni Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania Plc,  Rosalynn Mworia,  Kushoto ni Mkuu wa Kanda ya Dar es Salaam na Pwani George Lugata na Meneja wa maduka ya Rejareja ya Vodacom Tanzania, Happiness Macha.
 Mkurugenzi  Mtendaji wa Dar Teknohama Business Incubator (DTBi), Mhandisi Dkt, George Mulamula (wa pili kulia)  akikata keki  wakati wa uzinduzi wa duka jipya la Vodashop lenye sehemu maalum ya kutengenezea simu na kuhifadhi na kuhamisha kumbukumbu uliofanyika leo  katika  makao makuu ya kampuni  hiyo Vodacom Tower, Morocco jijini Dar es Salaam, wanaoshuhudia ni Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania Plc,  Rosalynn Mworia,  (wa pili kushoto) na wafanyakazi wa kampuni hiyo.
 Mkurugenzi  Mtendaji wa Dar Teknohama Business Incubator Mhandisi Dkt, George Mulamula  (kulia) na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania Plc,  Rosalynn Mworia wakigongea glasi ya shampeni wakati wa hafla ya uzinduzi wa duka jipya la Vodashop lenye sehemu maalum ya kutengenezea simu na kuhifadhi na kuhamisha kumbukumbu  lililopo Makao Makuu ya kampuni hiyo,Vodacom Tower, Morocco jijini Dar es Salaam.

MADIWANI WANNE WA CHADEMA MOSHI WAUNGANA NA MWENYEKITI WA CCM KUHAMSISHA MAENDELEO

$
0
0
Diwani wa kata ya Shirimatunda katika Manispaa ya Moshi,Fransic Shio (CHADEMA) akizungumza wakati wamkutano wa kata uliolenga kujadili masuala ya maendeleo pamoja na kutambulisha wajumbe wanaounda kamati ya maendeleo ya kata hiyo.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Kilimanjaro,Patrick Boisafi akizungumza katika mkutano  wa kata ya Shiriamtunda ambapo yeye amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa kamati ya maendeleo ya kata hiyo.
Baadhi ya wananchi wakifuatilia kwa makini maelezo yaliyokuwa yakitolewa na viongozi .
Naibu Meya wa Manispaa ya Moshi na Diwani wa kata ya Njoro,Jomba Khoi akizungumza katika mkutano huo ambapo yeye na madiwani wenzake walifika kumuunga mkono Diwani wa kata hiyo katika kuchangia shuhghuli za maendeleo .
Baadhi ya wananchi waishio kata ya Shirimatunda wakiwa katika mkutano huo.
Diwani wa kata ya Kiboriloni,Frank Kagoma ni miongoni mwa madiwani walifika kuhamsisha shghuli za maendeleo katika kata ya Shrikamtunda.
Baadhi ya wawananchi waliofika katika mkutano huo.
Diwani wakata ya Soweto,Collins Tamimu pia ni miongoni mwa Madiwani waliofika katika mkutano huo.
Baadhi ya wananchi waishio katika kata ya Shirimatunda.
Diwani wa kata ya Ng'ambo katika manispaa ya Moshi ,Genesis Kiwhelu akiwa mmoja wa madiwani waliofika kuhamisisha shughuli za maendeleo katika kata hiyo.
Baadhi ya wananchi wakichangia hoja mbalimbali wakati wa mkutano huo ikiwemo ya kuchangisha fedha kwa ajili ya ujenzi wa darasa kwa ajili ya shule ya awali katika kata hiyo.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini
MADIWANI wanne kutoka  Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) katika manispaa ya Moshi  pamoja na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Kilimanjaro Patrick Boisafi wamejitokeza kumuunga mkono Diwani wa kata ya Shirimatunda ,Francis Shio (Chadema) kuhamasisha uchangiaji katika shughuli za maendeleo.
Madiwani waliojitokea katika mkutano maalumu wa Diwani  kata na wananchi wa kata hiyo ,ni pamoja na Diwani wa kata ya Soweto,Collins Tamimu,Diwani wa kata ya Njoro na Naibu Meya wa manispaa ya Moshi,Jomba Khoi ,Diwani wa kata ya Ng’ambo Genesis Kiwhelu na Diwani wa kata ya Kiboriloni ,Frank Kagoma.
Akizungumza wakati wa mkutano huo uliofanyika katika ofisi ya kata ya Shirimatunda  ,Diwani wa kata ya Shirimatunda ,Fransic Shio alisema maendeleo ya wananchi katika maeneo yao yataletwa na wananchi wenyewe na si itikadi za kisiasa kama baadhi ya wanasiasa wanavyoamini.
“Shirimatunda yetu ni ya kwanza kuliko vitu vingine,haya ninayo yasema ni ya uwazi tukikubali kuyaingiza mambo ya kisiasa katika maendeleo ya kata yetu ,yapo mambo mengi sana yatasimama  ,ni lazima kaul yetu ya wana Shirimatunda,umoja ya wana Shirimatunda na amani yetu tuweze kuilinda kwa gharama yoyote”alisema Mh Shio.
Shio aliwataka wakazi wa Shirimatunda kuwaondoa katika misingi ya umoja wa wakazi wa kata ya Shirimatunda huku akiwaomba kupitishwa azimio la kuchangisha fedha kwa kila familia katika kata hiyo kutoa kiasi cha Sh 10000 kwa ajili ya ujenzi wa darasa la wanafunzi wa shule ya awali.
Kwa upande wao ,Madiwani waliofika kumuunga mkono Diwani huyo,walisema ili kushawishi wadau mbalimbali pamoja na serikali kujitokeza kuchangia maendeleo katika kata hiyo wakazi wa eneo hilo wanapaswa kuwa wa kwanza katika kuchangia.
“Mgeni akija nyumbani akakuta wewe mwenyewe hujielewi ,hata kama amekuja na zawadi atarudi nayo ,watu wa Shirimatunda wanaangaliana nani anatoa nini ,endapo kila mkazi wa Shirimatunda akiguswa na hiki tunachokifanya basi angechangia katika eneo hili la elimu”alisema Diwani Kagoma.
Naye Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Kilimanjaro ambaye pia amechaguliwa kuwa mwenyekiti ya maendeleo ya kata hiyo ,Patrick Boisafi alisema kuchangia ujenzi wa Madarasa kwa wanafunzi wa elemu ya awali ni jambo la Kihistoria katika kata hiyo.
“Hakuna mashamba tena hata ya kuwagaiwa watoto wetu ,shamaba lililobaki ni moja na la muhimu sana ambalo ni Elimu,kuna watu ambao wamekuja hapa kutuunga mkono wakasema wafanye jambo ambalo litaacha Historia na ni hili la kuchangia shule ya awali name naunga mkono jambo jema kama hili “alisema Boisafi.
Kwa upande wake ,Naibu Meya wa Manispaa ya Moshi na Diwani wa kata ya Njoro alisema Halmashauri itatoa kipaumbele katika ujenz wa Madarasa hayo kwa kutenga Fungu hasa kutokana na hamasa walioyoionesha wakazi wa kata ya Shirimatunda kw akuanza kuchangia.
 “Niliwaambia nimekuja kujifunza kutoka kwenu na nimeona jinsi mlivyo weza kuanzisha michango na kuonyesha mahitaji yenu kwamba shule ya awali imeonekana kuwa kipaumbele ,ni lazima na mimi kwenye halmashauri yangu tutaipa kipaumbele tutatoa Sh Mil 10 kwa mwaka wa fedha ujao wa 2018/2019.”alisema Khoi.
Katika hatua nyingine wananchi  wa Kata hiyo wameiomba serikali kupitia Wakala wa Barabara vijijini na Mjini  (TARURA) pamoja na Halmashauri ya manispaa ya Moshi kutoa kipaumbele cha barabara kwa kata hiyo ambayo haina kipande hata kimoja cha barabara ya Lami .

Waziri Mwakyembe akutana na Wamiliki wa Televisheni nchini

$
0
0
Na Immaculate Makilika na Bushiri Matenda- MAELEZO
Serikali imesema kuanzia septemba 5, mwaka huu visimbuzi vitaanza kuonesha channeli zote za ndani bila kutoza gharama yoyote kwa mtazamaji.

Akiwaeleza waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam, kuhusu yaliyozungumzwa katika kikao kati ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe na wadau na wamiliki wa televisheni nchini, Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi amesema kuwa serikali imefikia uamuzi huo baada ya visimbuzi vya AZAM, ZUKU na DSTV kutoonesha channeli za ndani, kulingana na aina ya leseni zao.

“Ningependa watanzania wafahamu kwamba kuanzia septemba 5 mwaka huu, visimbuzi vya TIN, Starmedia, Continental na Digtek vitaonesha takribani channeli 34 za ndani bure, ili kutoa fursa ya kila mwananchi kuwa na haki ya kupata taarifa” alisema Dkt. Abbasi

Aidha, alielezea kuwa wadau hao na wamiliki wa televisheni wameonesha kuridhishwa na hatua hiyo ya kwa vile Serikali imetengeneza miundombinu itanayoruhusu channeli zao kuonekana nchi nzima.

Dkt. Abbasi, alisisitiza kuwa “nchi imeandaa mfumo, ambao unaweza kufanyakazi bila kutegemea kampuni kutoka nje ya nchi kwa ajili ya kuonesha channeli za ndani au matangazo, kwa hivyo wadau au wamiliki wa vyombo vya habari wasihofu kuhusu hilo”

Kikao kati ya Waziri Mwakyembe na wadau na wamiliki wa televisheni nchini, kimefanyika kwa lengo la kuwa na majadiliano ya pamoja baina serikali na wadau hao ili kupata muafaka kuhusu kutooneshwa kwa chaneli za ndani katika visimbuzi vilivyokiuka masharti ya leseni zao.

Aidha, kikao hicho pia kilihudhuriwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Injinia James Kilaba, pamoja na wataalamu wake.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe (katikati) akizungumza na wawakilishi wa wamiliki wa televisheni nchini (hawapo pichani) wakati alipokutana nao mapema hii leo jijini Dar es Salaam ili kusikiliza matatizo ya visimbuzi, kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA), Mhandisi James Kilaba na kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dk. Hassan Abbasi.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dk. Hassan Abbasi (kushoto) akizungumza na wawakilishi wa wamiliki wa televisheni nchini (hawapo pichani) wakati Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe (katikati) alipokutana nao mapema hii leo jijini Dar es Salaam ili kusikiliza matatizo ya visimbuzi, kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA), Mhandisi James Kilaba.

Baadhi ya wawakilishi wa wamiliki wa televisheni nchini wakimsikiliza Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe (hayupo pichani) wakati alipokutana nao mapema hii leo jijini Dar es Salaam ili kusikiliza matatizo ya visimbuzi.

KITUO CHA TRENI STESHENI DAR SASA KUHAMISHIWA SHAURIMOYO

$
0
0
 Treni ya Pugu ikipita chini katika njia ya reli ya kati ambapo juu yake itapita reli ya kisasa itakayotumia umeme.
 Mkurugenzi Mtendani wa shirika la reli Tanzania, Masanja Kadogosa akizungumza jijini Dar es Salaam leo Augusti 28,2018 wakati wa ziara ya bodi ya wakurugenzi wa shirika la reli Tanzania(TRC) kufanya ziara kwenye mradi wa reli ya kisasa, (Standard Gauge Railway )ambayo imeanzia Shaurimoyo mpaka kituo cha Soga na kuendelea mpaka Kirosa mjini Morogoro.

Baadhi ya nondo zilizosukwa kwaajili ya kutengeneza nguzo  kwaajili ya kutengeneza daraja la juu ambalo reli ya kisasa itakuwa ikipita maeneo ya Shaurimoyo Kariakoo jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya nguzo zilizowekwa tayari kwaajili ya kutengeneza reli ya kisasa itakayopita juu ili kupisha shughuli nyingine za chini kuendelea kama kawaida katika eneo la shaurimoyo jijini Dar es Salaam mradi huo wa reli ya kisasa umekaguliwa leo Augusti 28,2018 na wakurugenzi wa bodi ya shirika la reli Tanzania kwaajili ya kujua maendeleo yake.
Picha na Avila Kakingo,lobu ya Jamii.

*Ni kuanzia keshokutwa , Mkurugenzi Mtendaji TRC azungumza
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
SHIRIKA la Reli Tanzania(TRC) limesema kuanzisha keshokutwa treni inayofanya safari zake kati ya Stesheni na Ubungo na ile ya Stesheni Gongolamboto zote zitaishia eneo la Shaurimoyo jijini Dar es Salaam.

Akizungumza leo Mkurugenzi Mtendani wa shirika la reli Tanzania, Masanja Kadogosa amesema hatua hiyo wanaendelea kuboresha eneo la Shauri Moyo na kesho wanatarajia kukamilisha mahitaji yote muhimu na baada ya hapo hapo ndipo itakuwa Shesheni ya treni hizo sambamba na ile ya mkoani.

"Hivyo wananchi wanaotumia usafiri wa treni za Dar es Salaam badala ya kuanzia Stesheni na kuelekea Ubonga au Gongolamboto sasa watakuwa wanapanda au kushuka eneo la Shauri 
moyo,"amefafanua.

Kadogosa amesema sababu za kuhamishia Stesheni hiyo Shauri moyo ni kupisha ujenzi wa Stesheni ya Reli ya Kisasa ambayo ujenzi wake unaendelea kuanzia Dar es Salaam hadi Morogoro ambapo ujenzi umefikia asilimia 22 hadi sasa.

"Kesho tunakamilisha ujenzi wa eneo hili la Shauri Moyo na kesho kutwa treni zetu zitakuwa zikianzia safari zake hapa na kumalizia hapa.Tunaomba wananchi wafahamu kuwa Stesheni tunataka kuanza ujenzi wa Shesheni ya Reli ya Kisasa.

"Ujenzi huo utafanyika kati ya miezi sita hadi nane hivyo wananchi tunaomba tuwasumbue kwa kuwahamisha.Bahati nzuri ni usumbufu wenye neema kwetu sote,"amesema.

Kadogosa amewahakikishia wananchi wanaotumia usafiri huo kwamba usalama upo wa kutosha na kutakuwa na utaratibu mzuri wa kutoa maelekezo yakiwamo ya mageti ya kuingia na kotokea.

Ameongeza kwani wanatambua licha ya kuhamishia Stesheni Shaurimoyo bado kuna ujenzi wa reli ya kisasa unaendelea, hivyo wamechukua tahadhari zote.

Awali Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) Profesa John Kandoro baada ya kuelezwa taarifa hizo za kuhamishwa kwa Stesheni kutoka ilipo na kuhamishiwa Shaurimoyo alitaka kufahamu usalama wa abiria , ambapo amethibitishwa na Kadogosa kwamba usalama utakuwepo.

Profesa Kondoro alifika eneo la Shaurimoyo akiwa ameongozana na wajumbe mbalimbali wa bodi yake ambao walifika hapo kwa ajili ya kuangalia maendeleo ya ujenzi wa mradi wa reli ya kisasa unaondelea.

UKOSEFU WA UADILIFU ULIITIA DOA SEKTA BINAFSI-MAJALIWA

$
0
0
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza kwenye ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa 18 wa Wanachama wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF). umefanyika  leo Agosti 28, 2018 Jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa kwenye picha ya pamoja na washriki wa Mkutano Mkuu wa 18 wa Wanachama wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) leo Agosti 28, 2018 Jijini Dar es Salaam. PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema ukosefu wa uadilifu ni moja ya eneo ambalo lilitia doa utendaji wa sekta binafsi hususan pale ambapo ilishirikiana na Serikali.

Ameyasema hayo leo (Jumanne, Agosti 28, 2018) wakati akifungua Mkutano Mkuu wa 18 wa mwaka wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) kwa niaba ya Rais Dkt. John Magufuli.

Katika mkutano huo uliofanyika kwenye Hoteli ya Serena, jijini Dar Es Salaam, Waziri Mkuu amesema uadilifu ni changamoto kubwa inayopaswa kufanyiwa kazi na Serikali na TPSF.

“Katika kusisitiza suala la uadilifu, nitoe rai kwamba muwe na mfumo wa kujitathmini,kupeana alama chanya na kuhimizanakuenenda katika misingi bora ya uendeshaji wa shughuli zenu.”

Kadhalika, Waziri Mkuu ameitaka TPSF ijifunze kwa wenzao walioendelea kwa kutokuwa na vitendo vya rushwa, kutoa adhabu kwa wanaoenda kinyume na misingi ya uadilifu walijiwekea.

Amesema kwa kufanya hivyo watakuwa wamejiongezea nguvu yao kama taasisi lakini pia kupeleka ujumbe kwa wanachama wao kuwa wanathamini haki na kuchukia rushwa.

Waziri Mkuu ameongeza kuwa shughuli za sekta binafsi zimeendelea kuongoza katika kuchangia pato la Taifa na ukuaji wa uchumi kwa ujumla.

Amesema kwa mujibu wa takwimu sekta ya utalii inachangia asilimia tisa, huduma asilimia 35, kilimo asilimia 26.6, madini asilimia 3.3 na sekta ya viwanda inachangia takribani asilimia 10.

“Jukumu letu sote ni kuchochea uzalishaji na kufanya wepesi  kwa wajasiriamali wetu watoke nje ya mipaka yetu na kwenda kuuza bidhaa zetu nchi jirani. TPSF mtusaidie katika hili.

Waziri Mkuu amesema Serikali kwa upande wake itaendelea kuweka mazingira wezeshi kwa kuboresha miundombinu, kutoa vivutio kwenye kodi, kanuni na sheria ili kukuza sekta binafsi.

Hivyo, Waziri Mkuu amesema sekta binafsi nchini nayo haina budi kutumia vema fursa hiyo ya uwepo wa mazingira wezeshi na rafiki kwa kuwekeza kwenye uchumi wa nchi.

Amesema ni vema wakatambua kwamba wana jukumu kuliletea Taifa maendeleo, hivyo wafanye kazi kwa ukaribu na ubia baina yao ili kuhakikisha nchi inanufaika na fursa zilizopo.

Pia amewasihi waendelee kuwekeza zaidi kwenye uzalishaji wa bidhaa za viwandani na wahakikishe kuwa wanajali maisha ya Watanzania ambao ndio soko na wateja wa bidhaa zao.

TRC WADHIBITI WIZI WA MAFUTA KATIKA UJENZI RELI YA KISASA

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Reli Tanzania(TRC) Masanja Kadogosa akizungumza kabla ya kuanza ziara ya kutembelea mradi wa reli ya kisasa iliyofanyika leo Augusti 28,2018 kuanzia Shaurimoyo  mpaka Kilosa mjini morogoro.
 Meneja Mradi mradi wa reli ya kisasa ya standard gauge, Injinia Maizo Mgedzi akizungumza kabla ya kuanza ziara ya kutembelea maradi wa Reli ya kisasa ambayo itaanzia Dar es Salaam mpaka morogoro na baadae kuanzia Morogoro mpaka Dodoma. Ziara hiyo iliyohusisha wakurugenzi wa bodi ya wakurugenzi wa shirika la reli Tanzania leo Augusti 28,2018.
 Wajumbe wa Bodi ya wakurugenzi wa shirika la Reli Tanzania wakisikiliza maelezo ya mradi kabla ya kuanza ziara ya kutembelea mradi wa Reli ya kisasa.
 Meneja Mradi mradi wa reli ya kisasa ya standard gauge akitoa maelezo ya mradi wa Reli ya kisasa jijini Dar es Salaam leo mara baada ya kuanza ziara ya kutembelea mradi wa reli ya kisasa leo Augusti 28,2018.
 Reli ya kati ambapo reli ya kisasa.
Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi, Profesa John Kondoro akizungumza wakati ziara ikiendelea leo Augusti 28,2018 ya kutembelea ujenzi wa reli ya kisasa.
  Baadhi ya maeneo ambayo reli ya kisasa yatapita chini ya ardhi.
 Ujenzi wa reli ya kisasa ukiendelea

 Mradi mradi wa reli ya kisasa ya standard gauge ulipofikia baadhi ya maeneo.

 Mataaluma yakiwa tayari kwaajili ya kwenda kuwekwa kwenye maeneo ambayo reli ya kisasa itapita.

Maeneo yanayoendelea kujengwa reli ya kisasa eneo la Mlandizi.
Picha na Avila Kakingo, Globu ya jamii.

*Mkurugenzi Mtendaji Kadogosa asema ujenzi umekamilika kwa asilimia 22

*Wajumbe Bodi ya Wakurugenzi washuhudia kasi ya ujenzi kuanzia Dar 

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii.
MKURUGENZI Mtendaji wa Shirika la Reli Tanzania(TRC) Masanja Kadogosa amesema kwa sasa wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa kudhibiti wizi wa mafuta huku akieleza kuna baadhi ya madereva wamefukuzwa kazi kutokana na tuhuma hizo.

Kadogosa amesema hayo leo katika eneo la Soga mkoani Pwani ambapo kuna kambi ya wafanyakazi wanaojenga Reli ya Kisasa ambapo ameelezea namna ambavyo wamedhibiti wizi wa mafuta kwa kuimarisha ulinzi kwa kushirikiana na mamlaka za ulinzi na usalama.

Sababu za kuelezea hayo ni baada ya baadhi ya waandishi waliokuwa kwenye ziara ya Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya TRC  wakiongozwa na Mwenyekiti wao Profesa John Kondoro kutaka kufahamu hali kutokana na kuwepo kwa taarifa za uwepo wa wizi wa mafuta.

"Tumefanikiwa kwa kiasi kikubwa kudhibiti wizi wa mafuta katika mradi huu.Ni tofauti na hapo awali, tumeimarisha ulinzi na sasa tumefanikiwa kudhibiti wizi huo.

"Kuna watu 30 wamekamatwa kwa tuhuma za wizi wa mafuta na tayari wamefunguliwa kesi.Pia katika kukomesha vitendo vya wizi kuna baadhi ya madereva ambao tumewafukuza,"amesema Kadogosa.


VIPI KUHUSU UJENZI WA RELI?
Akizungumzia ujenzi wa reli hiyo ya kisasa ambayo awamu ya kwanza ni kutokea Dar es Salaam hadi Morogoro, Kadogosa amewaeleza wajumbe wa bodi hiyo  kwamba ujenzi umekamilika kwa asilimia 22.

Amesema katika ujenzi wa reli hiyo kuna hatua mbalimbali za ujenzi zinazoendelea na kila eneo kwa asilimia tofauti na eneo jingine lakini kwa ujumla wake ujenzi umefikia asilimia 22 na ujenzi unaendelea kwa kiwango cha kuridhisha.

Ameongeza ujenzi wa madaraja unaendelea na tayari zimeanza kuwekwa , ujenzi wa tuta nao unaendelea na maeneo maeneo mengine wameanza kuweka kokoto kwa ajili ya kuanza kutandika mataluma.

"Kasi ya ujenzi wa reli ya kisasa inakwenda vizuri, ratiba ya ujenzi huu unatakiwa kukamilika Novemba mwaka 2019, hivyo kazi inaendelea na ujenzi unafanyika usiku na mchana na sisi TRC muda wote tumekuwa tukifuatilia tena hatua kwa hatua,"amesema Kadogosa.

Ametumia nafasi hiyo kusisitiza wanafanya kazi kwa saa 24 kwani changamoto ya mvua ilisababisha kutofanyika kazi za ujenzi na hivyo wamemua kufanya kazi usiku na mchana ili kuhakikisha unakamilika kwa wakati.


UNAZUNGUMZIAJE UJENZI STESHENI YA DAR?
Kadogosa amefafanua kwamba ujenzi wa stesheni ya Dar es Salaam na maeneo mengine ya mradi huo yamezingatia uhalisia wa Mtanzania na kwamba kabla ya kuanza ujenzi huo walimtaka mtalaamu kuonesha ramani ya majengo atakayojenga.

Amesema hata baada ya kuangalia walimtaka ajenge majengo ambayo yataonesha uhalisia wa nchi yetu.Pia amesema maeneo ya Stesheni baada ya kukamilika mbali ya kuwa sehemu ya abiria yatakuwa na maeneo ya mahitaji yote muhimu.

"Kwa Stesheni ya Dar es salaam kutakuwa na eneo kwa ajili ya abiria, kutakuwa na hoteli, kutakuwa na maeneo ya maduka makubwa ya kisasa na na maduka ya kawaida.Kutakuwa na ofisi mbalimbali za watumishi pamoja na kumbi za mikutano.

"Tunataka maeneo ya Stesheheni hata kama kutakuwa hakuna treni basi shughuli nyingine za kiuchumi ziendelee,"amesema Kadogosa na kufafanua katika maeneo mengine ya vituo vya treni kutakuwa na majengo yanayofanana na nyumba za kabila la Wamasai na Wagogo na yote hiyo ni katika kuonesha uhalisia.


MAANDALIZI YAKOJE?
Kuhusu maandalizi, Kadogosa amesema kuna mikakati mbalimbali inayoendelea ikiwamo ya kuandaa watalaam wataokaofanya kazi ya kuendesha treni hiyo baada ya ujenzi wake kukamilika.

Amesema kuna baadhi ya watalaam wa TRC ambao wameanza kupatiwa mafunzo kwa ajili ya kuusimamia mradi huo na baadhi yao watakwenda kujifunza nje ya nchi na hasa katika nchi ambazo wanao uzoefu wa kusimamia treni za aina hiyo.

Pia amesema kuna watalaam ambao watakuja nchini kwa ajili ya kutoa mafunzo kwa watalaam wazawa huku akielezea kuwa kuna vijana 160 kutoka vyuo vikuu hapa nchini wameanza kupewa mafunzo ya nadharia na kisha watapewa mafunzo kwa vitendo.

"Tunataka mradi huu utakapoanza basi tuwe na watalaam wetu ambao watasimamia shughuli mbalimbali .Hivyo tumeedelea kujieandaa na tunakwenda vizuri sana,"amesema Kadogosa.


HALI IKOJE KWA WAZAWA?
Katika hilo Kadogosa amesema kwamba kwa mujibu wa mkataba uliopo unaeleza wazi kwamba katika ujenzi wa reli hiyo ushiriki wa Watanzania ni asilimia 80 na iliyobaki ni ya wageni.

Amesema hadi sasa ujenzi huo ukiwa umekamilika kwa asilimia 22 idadi ya Watanzania ambao wanashiriki katika ujenzi wa reli hiyo ni asilimia 92 na asilimia iliyobakia ni wageni.

"Katika kila eneo la ujenzi wazawa ni wengi kuliko wageni.Hivyo tumevuka lengo ambalo lipo kwenye mkataba wetu.Wazawa wanashiriki kikamilifu,"amesema Kagogosa wakati anatoa maelezo ya ujenzi huo kwa wajumbe wa bodi ya wakurugenzi wa TRC.

TUMESHAWAHI KUJENGA RELI KWA FEDHA ZETU?
Katika hilo Kadogosa amesema kuwa ujenzi wa reli hiyo ya kisasa ni wa kihistoria kwani kama Taifa ndio ujenzi wa reli ambayo unafanywa na Watanzania wenyewe kupitia fedha zao.

"Hii ndio reli yetu ya kwanza kuijenga kwa fedha zetu kama Taifa.Reli ambayo tunatumia ilijengwa na wakoloni miaka ya nyuma lakini hatimaye Taifa la Tanzania limeamua kujenga reli ya kisasa tena kwa fedha zake.Hili ni jambo la kujivunia,"amesema Kadogosa wakati anazungumzia ujenzi wa reli hiyo.


NINI MAONI YA PROF.KONDORO?
Akizungumza baada ya kukagua ujenzi huo kuanzia Shaurimoyo jijini Dar es Salaam hadi Soga mkoani Pwani Profesa Kondoro amemetoa maoni yake kuwa ameridhishwa na kasi ya ujenzi huo.

Amesema kuwa lengo la ziara yao ambayo ni ya kawaida ni kutoaka kuona kwa uhalisia shughuli za ujenzi huo na kwamba inawapa nafasi ya kuangalia ripoti ambazo wanazo kwenye makaratasi na uhalisia wa ujenzi huo.

"Kwetu sisi wajumbe wa bodi tumeridhika na kasi ya ujenzi wa reli hii.Kwa matamanio ambayo tunanayo tunatamani mradi huu ungekabidhiwa jana lakini kwasababu ujenzi ni mambo ya kitalaam basi tunaacha utalaalam uchukue nafasi yake,"amesema Profesa Kondoro.

Ameongeza ujenzi huo upo katika hatua tofauti na kuna baadhi ya maeneo yanachangamoto zake kutokana na reli inakopita lakini wameridhishwa na maelezo ya wataalam wanaosimamia ujenzi wa reli hiyo.

PANITA, ASASI ZA KIRAIA WATOA USHAURI KWA SERIKALI KUHUSU NAMNA BORA KUBORESHA HALI YA LISHE NCHINI

$
0
0
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii.

SERIKALI kupitia Halmashauri imeshauriwa kujenga tabia ya kutenga fedha kupitia mapato yao ya ndani ili kuweka mfumo thabiti na endelevu katika kuboresha hali ya lishe na ambao utajengeka juu ya msingi bora unaowekwa na fedha za wafadhili pindi miradi hii itakapokwisha.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa PANITA Tumaini Mikindo kwa niaba ya Asasi za kiraia ambazo zimejikita katika masuala ya lishe nchini wakati wa kikao kati ya na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Tamisemi) Suleiman Jaffo.

Lengo la kikao hicho kimekutana kwa ajili ya kuifanya tathimini taarifa ya utekelezaji wa mkataba wa lishe baina ya Makamu wa Rais, Wakuu wa Mikoa wa Tanzania Bara na viongozi wengine wa ngazi mbalimbali.

Hivyo Mikindo ameshauri ni vema pia halmashauri ziweke vipaumbele kwenye afua za lishe ambazo zitaleta matokeo chanya kwa haraka. Pia Serikali iongeze bajeti ya lishe kutoka Sh.1,000 ya sasa kwa mtoto hadi kufikia Sh. 23,000 ambayo ni takribani dola 8.5 za kimarekani kwa mwaka kwa kila mtoto chini ya miaka mitano na iwapo wanalenga kufikia maazimio ya Baraza la Afya Duniani (WHA) kuhusu lishe kufikia 2025. 

"Baada ya maneno haya machache namshukuru Waziri Jafo kwa kutushirikisha katika kikao hiki adhimu cha kujadili utekelezaji wa mkataba wa lishe,"amesema Mikindo kupitia taarifa yake kwa vyombo vya habari aliyoitoa leo kuhusu kikao hicho cha tathimini.

Awali wakati anaanza kuzungumza Mikindo amesema asasi za kiraia zinatoa shukrani kwa Waziri Jaffo kwa kuwaalika kwenye mkutano huo na kwao ni fursa ya kutoa maoni yao kuhusu lishe nchini.

"Hii ni uthibitisho tosha Serikali ya Awamu ya tano chini ya Rais Dk.John Magufuli inavyothamini na kutambua mchango wa wadau ikiwemo Asasi za kiraia katika kusukuma gurudumu la maendeleo ya taifa hili kuelekea uchumi wa kati kupitia viwanda ifikapo 2025.Waziri tunaomba utufikishie shukurani zetu za dhati kwa Rais,"amesema. 

Aidha amesema wanamshukuru Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan kwanza kwa kukubali kuwa kinara wa lishe na pili kwa kutimiza ahadi aliyoitoa siku ya uzinduzi wa ripoti ya lishe ya dunia nchini Tanzania Julai 20 mwaka 2016 jijini Dar es Salaam.

"Naomba nirejee baadhi ya maneno aliyoyatamka siku hiyo. Ninanukuu, “…Ni kweli kwamba kwenye “Political will” jambo lolote linaweza likafanyika; kwa hiyo niseme kwamba na hili suala la lishe tutalipa msukumo mkubwa wa kisiasa ili kila mmoja wetu aimbe lishe na kupunguza Utapiamlo,"amesema wakati anatoa nukuu hiyo.

Pia amesema Mama Samia alisema wakati wa uzinduzi huo kuwa viongozi wa Serikali watahakikisha wanatoa ushirikiano stahiki ili kuwezesha lishe kupata msukumo wa kipekee katika ngazi zote za maamuzi.

Mbali ya kumnukuu Makamu wa Rais, Mikindo amesema katika hotuba ya bajeti kuu ya fedha ya Serikali ya mwaka 2018/19 iliyosomwa na Waziri wa Fedha Dk.Philip Mpango kwa mara ya kwanza Serikali imetambua lishe kama moja ya vipaumbele vya kitaifa katika kufikia uchumi wa viwanda na kuhahidi kutoa msukumo wa kipekee katika kuborsha hali ya lishe nchini.

"Baada ya maneno haya kwa moyo dhati kabisa nimpongeze Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan na Rais Dk.Magufuli na Serikali yote kwa ujumla kwa kulisimamia jambo hili kikamilifu.Ndio maana tupo hapa leo katika kikao hiki kupata tathimini ya utekelezaji wa mkataba huu kwa miezi sita ya mwanzo toka uliposainiwa mbele yako mwezi Desemba mwaka 2017,"amesema.

Amefafanua kwa hiyo kikao chao hicho ni muhimu kupitia yaliyotekelezwa na kama kuna mafanikio watapongezana na kama kuna changamoto basi watazitafutia suluhu kwa pamoja ili waweze kufikia malengo tarajiwa ya kuboresha hali ya lishe nchini Tanzania.

Ametumia nafasi hiyo kuelezea mambo machache ambayo ni muhimu katika kuboresha hali ya lishe nchini Tanzania ambapo amesema Serikali imetenga fedha katika bajeti kwa mwaka wa 
2017/18 zipatazo Sh.bilioni 11 katika ngazi za mikoa na wilaya kwa kigezo cha Sh.1000 kwa mtoto mwenye umri chini ya miaka mitano. 

Amesema jambo hilo ni jema na linapaswa kupongezwa. Aidha utekelezaji wa bajeti hiyo unaonesha mambo kadha yakiwamo ya sehemu kubwa ya bajeti hiyo inatoka kwenye Mfuko wa Afya wa Pamoja (Health Basket Fund) ikifuatiwa na ruzuku ya Serikali Kuu kwenda halmashauri na kwa kiwango kidogo toka kwenye mapato ya ndani ya halmashauri. 

"Kwa kiasi kikubwa fedha ambazo zimetumika ni zile zinazotoka kwenye Mfuko wa Afya wa Pamoja (Health Basket Fund) ikifuatiwa na ruzuku ya Serikali kuu kwa kiasi kidogo na pengine zile zilizotengwa toka mapato ya ndani ya halmashauri zisitolewe kabisa,"amesema Mikindo .

Aidha amesema sehemu kubwa ya mipango na bajeti za lishe kwa ngazi ya wilaya haizingatii afua za lishe ambazo zingeweza kuleta matokeo chanya kwa haraka.

Pia mikoa ambayo inapata fedha za wafadhili au wadau wa maendeleo imekuwa haiweki fedha za vyanzo vya ndani katika bajeti za lishe au zikiweka basi ni kwa kiwango kidogo sana. 

"Hii inamaanisha nini? Kwa kipindi cha kati tutapata matokeo chanya kwa sababu fedha za wafadhili zipo. Lakini mafanikio haya hayatakuwa endelevu pindi miradi ya wafadhili itapomaliza muda wake,"amesema.

Awali imeepezwa pia mkutano ulioandaliwa na Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa kushirikiana na UNICEF Tanzania ulikuwa na malengo mahususi ambayo ni kuwasilisha utekelezaji wa afua za lishe na viashiria vilivyo kwenye Mkataba wa Makubaliano wa Masuala ya Lishe baada ye Miezi sita ya utekelezaji. 

Pia kujenga uelewa wa pamoja wa utekelezaji wa Viashiria vilivyoko katika Mkataba wa Lishe,kuongeza msukumo wa usimamizi na uelewa wa Masuala ya Lishe ili kupunguza kiwango cha Udumavu na Utapiamlo nchini. 



Na jambo lingine ni kufafanua madhara na hasara ya Udumavu katika uchumi na maendeleo ya nchi.

WILAYA YA MANYONI MKOANI SINGIDA YATENGA ZAIDI YA EKARI 5000 KUPANDA MIKOROSHO MIPYA

$
0
0
Mkuu wa wilaya ya Manyoni Rahabu Mwagisa akizungumza na viongozi wa bodi ya Korosho nchini ambao hawapo pichani wakati wa ziara ya ya kutembelea maeneo mapya yanayolima korosho nchini yaliyofanyiwa utafiti na kubainika yanaweza kustawi zao hilo na hivyo uhamasishaji wa kilimo hicho ukafanyika akielezia mikakati ya wilaya yake kupanda zaidi ya ekari 5000 za mikorosho
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manyoni Charles Fussi kushoto akimsikiliza kwa umakini Afisa Uhusiano wa Bodi ya Korosho nchini Bryson Mshana wakati wa ziara ya viongozi wa bodi kuhamasiha kilimo cha zao la Korosho kwenye maeneo mapya
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manyoni Charles Fussi kushoto akisistiza jambo kwa viongozi wa bodi ya Korosho nchini Afisa Kilimo Frank Mfutakamba kulia na Afisa Uhusiano Bryson Mshana kushoto wakati walipofanya ziara wilaya ya Manyoni kuhamasisha kilimo cha zao hilo.
Afisa Uhusiano wa Bodi ya Korosho nchini Bryson Mshana kulia akisisitiza jambo kwa Afisa Kilimo ,Umwagiliaji na Ushirika wa Halmashauri ya wilaya ya Manyoni Fadhili Chimsala
Mkuu wa wilaya ya Manyoni Rahabu Mwagisa katikati akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa bodi ya Korosho waliotembelea wilaya hiyo kushoto ni Afisa Uhusiano Bryson Mshana kulia ni Afisa Kilimo Frank Mfutakamba
Mkuu wa wilaya ya Manyoni Rahabu Mwagisa kushoto akiagana na Afisa Kilimo wa Bodi ya Korosho Frank Mfutakamba mara baada ya viongozi wa bodi ya korosho kumaliza mazungumzo naye

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manyoni Charles Fussi wa pili kutoka kushoto akisisitiza jambo na viongozi wa bodi ya Korosho mara baada ya kumalizia mazungumzo nayo kushoto ni Afisa Uhusiano wa Bodi ya Korosho Bryson Mshana na kulia ni Afisa Kilimo wa Bodi hiyo Frank Mfutakamba
Afisa Uhusiano wa Bodi ya Korosho Bryson Mshana akitazama moja ya mikorosho mipya iliyopandwa kwenye shamba mfano ambalo walilitembelea ili kuweza kuhamaisha zao hilo liliopo Kijiji cha Masigati
NA MWANDISHI WETU,MANYONI.

WILAYA ya Manyoni mkoani Singida imetenga zaidi ya ekari 5000 kwenye Kijiji cha Masigati kwa ajili ya kupanda mikorosho mipya baada ya wananchi kuhamasisha kupanda zao hilo.

Hayo yalisemwa na Mkuu wa wilaya ya Manyoni Rahabu Mwagisa wakati wa ziara ya viongozi wa bodi ya korosho nchini ya kutembelea maeneo mapya yanayolima korosho nchini ambao yalifanyiwa utafiti na kubainika yanaweza kustawi zao hilo na hivyo uhamasishaji wa kilimo hicho.

Viongozi wa bodi hiyo ambao walifika kwenye shamba la mfano lililopo katika Kijiji cha Masigati kwenye Halmashauri ya Manyoni ambalo lilianza mwaka jana ni Afisa Kilimo wa Bodi hiyo Frank Mfutakamba na Afisa Uhusiano Bryson Mshana wakiwa kwenye uhamasishaji wa kilimo hicho kwenye maeneo mapya.

Mkuu huyo wa wilaya alisema kati ya hizo ekari zilizopandwa ni 1250 kwa msimu uliopita wa kilimo na msimu umekaribia mwezi Desemba mwaka huu wataanza tena kuendelea na upandaji wa mikorosho mipya.

“Pamoja na kwamba tumetenga ekari 5,000 kwa ajili ya kulima kilimo cha Korosho lakini mipango yetu ni kufikia ekari 10,000 alisema pamoja na hayo tutaendelea kufanya uhamasishaji kwa wananchi kuweza kuchangamkia fursa ya zao hili na kupanda mikorosho kwa wingi “Alisema.

Alisema wananchi wake wamehamasika baada ya kuwepo kwa uhamasishaji mkubwa kupitia mikutano mbalimbali huku akiwataka wananchi wa wilaya hiyo kutumia fursa ya kilimo hicho kutokana na kwamba maeneo yote yana uwezo kustawi zao hilo hivyo walipande kwani litawasaidia na kuwa mkombozi wa maisha yao.

“Lakini pia nisema kilimo hiki kimeweza kutoa fursa kwa watu kutoka mikoa mingine wameanza kulima korosho Manyoni hamasa bado inaendelea kwa halmshauri mbili za Manoyoni na Itigi licha kwamba hawajafanya kilimo cha pamoja lakini watu wanalima Korosho”Alisema

Alisema Halmashauri ya Manyoni wamekuwa na mpango wa kilimo cha pamoja kupitia ekari hizo elfu tano jambo ambalo limesaidia wananchi kupata ajira na hivyo kukuza uchumi wao kutokana na shughuli za upandaji zinazofanyika.

Naye kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manyoni Charles Fussi aliishukuru bodi ya korosho kutokana na kwamba wao ndio wamekuwa chachu ya kuzalisha korosho kama zao la mkakati kwenye halamshauri yao limeanza na wao kama bodi walikuwa wa kwanza kuhamasisha wananchi.

Alisema kabla ya kuanza kilimo hicho Utaftiti ulifanyika na baada ya kugundua korosho inaweza kufanya vizuri hivyo bodi ya korosho waliomba ardhi na wazo lao kubwa lilikuwa la kwanza kupitia Halmshauri walifika Kijijini Masigati kuzungyumza na wananchi waliomba ardhi wakapewa eka 2000 wahamasisha vikundi vikaundwa wakaanza kugawa ardhi kwa vikundi.

Alisema kila kikundi kina ekari si chini ya 100 wameanza kusafisha mashamba wanalima korosho lakini wameamua mradi huo upanuliwe kutokana na mwitikio mkubwa wa wananchi huku akiwakaribisha watanzania wengine kuchangamkia fursa hiyo.

NDEGE ILIYOKODISHWA ILISHALIPIWA

$
0
0
Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.
RUBANI wa kampuni ya ndege ya Tanzania, (ATCL), Sadiki Jabez, ameieleza mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa, ATCL ililipia garama za matengenezo ya ndege iliyokodisha licha ya kwamba matengenezo hayo yalifanywa na kampuni iliyowakodisha.

 Jabez ambaye pia ni mkurugenzi muendeshaji wa ATCL na  shahidi wa tisa wa upande mashtaka ameeleza hayo leo Agosti 29 wakati akitoa ushahidi wake dhidi ya kesi ya matumizi mabaya ya madaraka na kuisababishia serikali hasara ya Sh. Bilioni 71, mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Augustino Rwenzile.

Mattaka anadaiwa kusababisha hasara hiyo kutokana na kusaini mkataba wa kukodi ndege bila kufuata Sheria ya manunuzi ya umma pamoja na ushauri wa kiufundi.

Akiongozwa na wakili wa Serikali, Timon Vitalis, amedai, mwenye jukumu la kutengeneza ndege pale inapokuwa inahitaji marekebisho  hujulikana kutokana na jinsi mkataba ulivyoingiwa lakini hakuwahi kuuuona huo mkataba.

Shahidi Jabez amedai mwaka 2007, ATCL ikiwa chini ya mkurugenzi David Mataka ilikuwa na ndege moja, 737 boing.
 Amedai, baadae ATCL waliazimia kukodisha ndege airbus 320 kutoka kampuni ya Wallis.

Amedai, kutokana na nafasi yake ya mkurugenzi muendeshaji, alikuwa akiingia kwenye mikutano ya bodi ya wakurugenzi kama kisaidia na katika mikutano hiyo hakumbuki kama waliwagi kujadiki juu ya kukodisha ndege na kama ilijadiliwa basi yeye hakuwepo.

Shahidi Jabez ameeleza kuwa Octoba 14.2007 alisafiri baada ya kupata maelekezo kutoka kwa Mataka aliyewataka kwenda Elsavaldo nchini Uingereza  kwa ajili ya kwenda kuangalia ndege wanayotaka kukodisha.

"Nilienda na Fidelis Tarimo pamoja na John Lyimo kwani unapotaka kukodisha ndege pande mbili ile ya uwezeshaji na wahandisi lazima iwepo kwa kuwa yeye ndio anakagua nyaraka ndani ya ndege inayowezesha ndege kuruka( cooperate) kwani ni rubani ndie anayejua kama ndege inafanya kazi sawa sawa" ameeleza shahidi Jabez.

Ameeleza kuwa, matokeo ya ukaguzi yalionyesha kuwa, ndege ilikuwa inaweza kutumika ila vitu kama viti vilikuwa vinahitaji  marekebisho na vitu vingine vilikuwa vimebomoka.

"Nilimfahamisha mkurugenzi kuwa ndege hiyo ilikuwa inahitaji matengenezo kabla ATCL haijaikodoshwa na mkurugenzi akawaambia kuwa amwambie mkurugenzi wa uhandisi atengeneze mapungufu yote" ameeleza Shahidi.

Ameendelea kueleza kuwa, mtu ambaye huwa na jukumu la kutengeneza ndege anajulikana na jinsi mkataba ulivyoingiwa Ila yeye hakuwahi kuuona huo mkataba na mpaka anaondoka Elsalvado ndege hiyo ilikuwa bado haijafanyiwa marekebisho.

Ameeleza, malipo yote ya kufanyia marekebisho ndege hiyo yamelipwa na ATCL licha ya kwamba matengenezo yalifanywa na kampuni yab Wallis ambayo ndio iliwakodisha ndege hiyo.

Mbali na Mattaka washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni aliyekuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA), Ramadhani Mlinga pamoja na Mkurugenzi wa Sheria wa mamlaka hiyo, Bertha Soka.

Inadaiwa Oktoba 9, 2007 katika ofisi za ATCL Dar es Salaam, Mattaka akiwa Mkurugenzi wa shirika hilo, alitumia madaraka yake vibaya kwa kusaini makubaliano ya kukodi ndege yenye namba A 320-214, kati ya ATCL na kampuni ya Wallis Trading Inc, bila kufuata sheria ya manunuzi ya umma na taratibu za zabuni.

Aidha anadaiwa kutumia madaraka yake vibaya kwa kusaini makubaliano ya kukodi ndege hiyo bila kufuata ushauri wa kiufundi na kuidhinisha makubaliano hayo, jambo ambalo lilisababisha shirika hilo hasara ya fedha hizo.

Katika mashtaka yanayowakabili, Mlinga na Soka, inadaiwa Machi 19, 2008, katika ofisi za PPRA, Ilala Dar es Salaam, kwa lengo la kufanya udanganyifu, walighushi muhtasari wa kikao cha Machi 19, 2008, kwa lengo la kuonesha siku hiyo, PPRA ilifanya kikao kujadili maombi ya kuruhusu makubaliano ya ATCL kukodi ndege.
Viewing all 39073 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>