Quantcast
Channel: MTAA KWA MTAA BLOG
Viewing all 39066 articles
Browse latest View live

KAMPUNI YA SUKARI KILOMBERO SASA KUUZA PAKETI NDOGO ZA SUKARI, BEI NAFUU

$
0
0
Na Mwandishi Wetu. 

Kampuni ya Sukari ya Kilombero (KSC) imezindua paketi ndogo za sukari yake ijulikanayo kama ‘Bwana Sukari’, ikiwa ni jitihada za kuhakikisha watanzania wengi zaidi wanamudu kununua sukari hiyo kutokana na unafuu wake wa bei.

 Paketi mpya za sukari chapa ya ‘Bwana Sukari’ zinapatikana kwa ujazo wa gramu 350 maarufu kama ‘Robo Plus’ na paketi za gramu 160 maarufu kama ‘Booster’. Paketi za ‘Robo Plus’ zitauzwa shilingi 1,000/ kwa kila paketi, na paketi za ‘Booster’ zitauzwa kwa shilingi 500/-kwa kila paketi. 

Uzinduzi wa paketi mpya za ‘Bwana Sukari’ uliofanyika maeneo ya Mbagala jijini Dar es Salaam ni sehemu ya mkakati wa kampuni ya KSC kuhakikisha sukari yake inawafikia watanzania wa hali mbalimbali za kiuchumi. 

Uzinduzi huo ulihudhuriwa na wawakilishi kutoka Bodi ya Sukari Tanzania (SBT), Chama cha Wazalishaji wa Sukari Tanzania (TSPA), viongozi na wafanyakazi wa KSC. 

Akiongea wakati wa hafla ya uzinduzi, Mkurugenzi wa Biashara wa KSC, Fimbo Butallah alisema kampuni ya sukari ya Kilombero imekua ikipanga mikakati ya kuhakikisha bidhaa ya ‘Bwana Sukari’ inawafikia watanzania wengi zaidi hapa nchini. 

“Sukari ni moja ya bidhaa muhimu kwa matumizi ya kila siku ya nyumbani na sukari ya Bwana Sukari ni moja ya sukari inayopendwa zaidi na watumiaji wengi, tunawashukuru wateja wetu kwa kuikubali bidhaa yetu na kuifanya ifanye vizuri sokoni, kuonyesha shukrani zetu tumeamua kuwaletea paketi hizi ndogo ili wateja wetu wawe na uhuru wa kuchagua ujazo upi utawafaa kwa matumizi yao,” alisema Fimbo. 

 Akiongeza kuwa, paketi mpya za ‘Bwana Sukari’ zitakidhi mahitaji ya watumiaji wengi zaidi, “kwa mfano paketi za ‘Booster’ ambazo zitauzwa kwa shilingi 500/-zitawafaa zaidi wale wanaohitaji sukari lakini kwa wakati huo hawana uwezo wa kumudu kununua paketi kubwa au kwa wale wenye familia ndogo.” “Kwa ufupi, kupitia paketi hizi ndogo za Bwana Sukari tunawapa wateja wetu uhuru wa kununua sukari ya ujazo mdogo lakini iliyofungwa kwa hali ya usafi na usalama kabisa na kwa bei nafuu.” 

 Kwa kuanzia, paketi mpya za ‘Bwana Sukari ’zitapatikana katika maduka yote ya rejareja mkoani Dar es Salaam na wilayani Kilombero mkoani Morogoro wakati KSC inaendelea kufanya mikakati kuhakikisha bidhaa hii inasambaa nchini kote siku za usoni.
 Mkurugenzi wa Biashara wa kampuni ya sukari ya Kilombero Sugar, Fimbo Butallah akizungumza na wananchi wa Mbagala siku ya uzinduzi wa paketi ndogo za sukari ya 'Bwana Sukari' inayozalishwa na kiwanda hicho. Paketi hizo zitauzwa kwa shillingi 500/- na shillingi 1000/-.
 Mkurugenzi wa Biashara wa kampuni ya sukari ya Kilombero Sugar, Fimbo Butallah akimkabidhi paketi mpya za Bwana Sukari mkazi wa Mbagala Zena Athumani siku ya uzinduzi wa bidhaa hiyo uliofanyika viwanja vya Mabagala Zakeem hivi karibuni.
Mkurugenzi wa Biashara wa kampuni ya Sukari ya Kilombero Sugar, Fimbo Butallah akizungumza na waandishi wa habari siku ya uzinduzi wa paketi ndogo za sukari ya Bwana Sukari itakayouzwa kwa shillings 500/- and shillingi 1000/-

WAZIRI WA ARIDHI AFANYA KIKAO NA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA SHERIA NDOGO

$
0
0
 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa William Lukuvi akiiongoza Wizara yake kutoa majibu ya hoja za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo katika kikao cha Kamati hiyo kilichofanyika leo Jijini Dodoma.
 Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Sheria Ndogo wakimsikiliza Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa William Lukuvi alipokuwa akitoa majibu ya hoja za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo katika kikao cha Kamati hiyo kilichofanyika leo Jijini Dodoma.

MSAJILI NGOs AWAHIMIZA WADAU WA MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI KUTILIA MKAZO UTEKELEZAJI WA SERA ZA MAENDELEO

$
0
0
Na WAMJW Dodoma
Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Bw. Marcel Katemba ameyataka wadau wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kutilia mkazo katika kutekeleza Sera za Maendeleo zilizopo katika Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto(Idara Kuu Maendeleo ya Jamii) ili kufanikisha juhudi za Serikali katika kuletea wananchi Maendeleo.

Ameyasema hayo wakati akifungua kikao cha ushirikiano baina ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na Mashirika Yasiyo ya Kiserikali yanayotekeleza Sera zinazosimamiwa na kuratibiwa na chini ya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii leo Jijini Dodoma.

Bw. Katemba amesisitiza kuwa Mashirika hayo yanapaswa kuwasilisha mipango yao kwa Msajili ili kuweza kuwa na Mpango mkakati mmoja wa kuwezesha kufanya kazi kwa ufanisi.

Ameongeza kuwa suala la Maendeleo ni mtambuka na linapaswa kutekelezwa kwa ushirikiano baina ya Serikali, Wadau na wananchi ili kufanya shughuli za Maendeleo kuwa endelevu.

Kwa upande wao wadau kutoka Mashirika Yasiyo ya Kiserikali wakiwakilishwa na Mwakilishi wa Shirika la Care International Bi. Zenais Matemu amesema kuwa wadau ni wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ni muhimu katika Maendeleo hivyo kuiomba Serikali kuendelea kushirikiana ili kufanikisha utekelezaji wa miradi mbalimbali ya Maendeleo.

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto chini ya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii imepanga kukutana na wadau wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali mara moja kila baada ya miezi mitatu kujadiliana masuala mbalimbali ya utekelezaji wa Miradi mbalimbali ya Maendeleo nchini.


 Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Bw. Marcel Katemba akizungumza na wadau wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Jijini Dodoma katika kikao cha ushirikiano baina ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na Mashirika Yasiyo ya Kiserikali yanayotekeleza Sera zinazosimamiwa na kuratibiwa na chini ya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii.
Watendaji wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kutoka Idara Kuu Maendeleo ya Jamii pamoja na wadau kutoka Mashirika Yasiyo ya Kiserikali wakisikiliza mada zilizokuwa zikiwasilishwa kuhusu ushirikiano kati ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali na Serikali katika kikao cha ushirikiano baina ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na Mashirika Yasiyo ya Kiserikali yanayotekeleza Sera zinazosimamiwa na kuratibiwa na chini ya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii. Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW

MARAFIKI WA NMF WAIPA SURA MPYA WODI YA WATOTO YA HOSPITALI YA HALMASHAURI YA NANYUMBU, MTWARA

$
0
0
 Marafiki wa Wafanye Watabasamu, kutoka kushoto, Karim Mchaka, Athuman Said, Nathan Mpangala na Ndalo Kalua wakijadiliana jambo wakati wa zoezi la usafi wa jumla katika wodi ya watoto ya Halmashauri ya Nanyumbu, Mtwara hivi karibuni.
 Wanawafanye Watabasamu, kutoka kushoto, Athuman Said, ndilo Kalua na Winny Majuva wakihamisha vitanda kutoka katoka wodi ya watoto ili kupisha uchoraji hivi karibuni.
 Marafiki wa Wafanye Watabasamu, kutoka kushoto, George Nyandiche, Nathan Mpangala na Winny Majuva wakifanya yao kwenye wodi ya watoto ya Hospitali ya Halmashauri ya Nanyumbu, Mtwara hivi karibuni.
 Kutoka kushoto, George Nyandiche, Neema Loth, Asteria Malinzi na Masoud Kibwana wakiendelea na uchoraji katika wodi ya watoto ya Halmashauri ya Nanyumbu, Mtwara hivi karibuni.
 Wazazi wakiwa na watoto wao katika wodi ya watoto ya Hospitali ya Halmashauri ya Nanyumbu, Mtwara mara baada ya Marafiki wa Wafanye Watabasamu kumaliza kupamba wodi hiyo kwa michoro hivi karibuni.
 Wazazi pamoja na watoto wao wakifurahia muonekano mpya wa wodi ya watoto ya Hospitali ya  Halmashauri ya Nanyumbu, Mtwara hivi karibuni.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya hiyo, Hamis Dambaya (mwenye shati mikono mirefu) akiwa katika picha ya pamoja na Wanawafanye Watabasamu na baadhi ya viongozi mara baada ya kukamilika kwa uchoraji katika wodi ya watoto Hospitali ya Halmashauri ya Nanyumbu, Mtwara. (Picha zote na NMF)

Taasisi isiyokuwa ya kiserikali ya The Nathan Mpangala Foundation (NMF), kupitia programu yake ya Wafanye Watabasamu, hivi karibuni ilishirikisha marafiki wa programu hiyo kubadilisha mwonekano wa wodi ya watoto na chumba cha daktari wa watoto katika Hospitali ya Halmashauri ya Nanyumbu, Mtwara toka kuta nyeupe na kuwa zenye michoro mbalimbali.

Mwenyekitio wa taasisi hiyo, Nathan Mpangala alisema lengo la kazi hiyo ya siku tano mbali na kuichukulia kama ibada pia ililenga kuunga mkono jitihada za Serikali kwa kuipa wodi ya watoto ya hospitali hiyo mazingira rafiki kupitia sanaa ya uchoraji, kurudisha kidogo walichonacho kwa jamii na kuhamasisha umuhimu wa matumizi ya sanaa ya uchoraji kwenye maeneo yanayotoa huduma ya afya.

“Zahanati, vituo vha afya na mahospitali uhudumia wagonjwa. Mara nyingi huwa na maumivu, uchovu, upweke na msongo wa mawazo. Sehemu hizo zinapokosa michoro ukutani ambayo ingeweza kuwasahaulisha maumivu, hali huwa ngumu zaidi kwao. Sanaa si kwa ajili ya wagojwa tu, ni muhimu pia madaktari, wauguzi na wote wanaohusika na huduma ya afya. Kama maofisini, kumbini, sebuleni, hotelini tunaning’iniza sanaa iweje zinakosekana sehemu nyeti kama mahospitalini?”  alihoji Mpangala.

Mpangala anaishukuru Toyota Tz, Shule ya Msingi ya Catton Grove ya Uingereza na marafiki mbalimbali wa NMF kwa kuwezesha tukio hilo  na kwamba ametoa wito kwa wadau na wananchi kujitokeza kushirikiana na taasisi yake. “NMF ina mtandao mkubwa wa wachora nchini na wako tayari kujitolea kwa kushirikiana na wananchi au vikundi vilivyo tayari kujitolea.

Wakati huo huo, Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya hiyo, Hamis Dambaya akizungumza wakati wa zoezi hilo alisema, michoro kwenye wodi za watoto ni muhimu kwani huwaondolea uwoga hivyo kuna umuhimu wakazingatia hilo wakati wa kutengeneza na bajeti zetu.

Aidha, Mganga Mkuu wa hospitali hiyo, Dkt. Furaha Mwakafwila, ameishukuru NMF kwa kuchagua hospitali yake. “Hospitali ziko nyingi nchini, lakini mmeamua kuja kwetu. Tumefurahishwa na moyo wenu wa kujitolea. Karibuni tena siku nyingine,” alisema.

FLYOVER YA TAZARA IMEKAMILIKA KWA ASILIMIA 98-MAJALIWA

$
0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi, Isack Kamwelwe kuhusu barabara ya  juu ya TAZARA wakati alipokagua hatua za mwisho za ujenzi wa barabara hiyo jijini Dar es salaam Agosti  29, 2018. Kulia ni Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua  hatua za mwisho za ujenzi wa barabara ya juu ya eneo la TAZARA wakati alipokagua  ujenzi wa barabara hiyo  jijini Dar es salaam Agosti 29, 2018. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa   Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS), Mhandisi Patrick Mfugale kuhusu ujenzi wa barabara ya  juu ya eneo la TAZARA wakati alipokagua hatua za mwisho za ujenzi wa barabara hiyo jijini Dar es salaam Agosti 29, 2018. Watatu kushoto ni Waziri wa Ujenzi , Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi, Isack Kamwelwe na watatu kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaaam, Paul Makonda.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waandishi wa Habari baada ya kukagua hatua za mwisho za ujenzi wa barabara  ya juu katika eneo la  TAZARA jijini Dar es salaam Agosti 29, 2018.
 Waziri  Mkuu, Kassim Majaliwa alikagua ujenzi wa barabara za juu katika  eneo la Ubungo jijini Dar es salaam Agosti 29, 2018. Watatu kushoto ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi, Isack Kamwelwe na kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es slaam, Paul Makonda.

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesemaujenzi wa barabara ya juu katika eneo la Tazara umekamilika kwa asilimia 98 na itafunguliwa Oktoba mwaka huu na Rais Dkt. John Magufuli.

Mradi wa barabara ya juu (Mfugale flyover) chini ya ufadhili wa Serikali ya Japani, unalengo la kupunguza msongamano wa magari katika makutano ya barabara ya Mandela na Nyerere.

Ameyasema hayo leo (Jumatano, Agosti 29 ,2018) baada ya kukagua ujenzi wa mradi huowa barabara ya juu katika eneo la Tazara jijini Dar Es Salaam.

Waziri Mkuu amesema ameridhishwa kazi ya umaliziaji wa mradi huo inayoendelea kwenye hilo.

“Mradi utapunguza muda wa usafiri katika barabara ya Nyerere hususani  kwa wananchi wanaotoka katikati ya jiji kwenda uwanja wa ndege na wanaotoka Buguruni, Temeke.”

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amewaagiza viongozi Mkoa wa Dar Es Salaam watafute eneo kwa ajili ya  wafanyabiashara ndogondogo ili waweze kuondoka kandokando ya barabara hizo za juu zinazojengwa.

Waziri Mkuu ameyasema hayo baada ya kukagua ujenzi wa barabara za juu (interchange) eneo la Ubungo, katika makutano ya barabara za Morogoro, Mandela na Sam Nujoma, eneo la Ubungo jijini Dar Es Salaam.

Amesema ni vema wafanyabiashara hao wakaondolewa na kutafutiwa eneo lingine ili kulinda usalama wao kutokana na kazi za ujenzi zinazoendelea kwenye maeneo hayo. Pia amewataka viongozi hao wawaelekeze wananchi maeneo watakapowahamishia wafanyabiashara hao ili waweze kwenda kununua bidhaa.

Kadhalika, Waziri Mkuu amesema mradi huo nao unalengo la kupunguza msongamano wa magari kwa kutenganisha njia za barabara za Morogoro, Mandela na Sam Nujoma ili kuwa na ngazi mbili juu ya barabara za sasa.

Kwa upande wake, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe amesema ujenzi wa mradi wa barabara ya juu katika eneo la Tanzara (Mfugale flyover) unagharimu sh. bilioni 100.52 na unajengwa na kampuni  ya Sumitomo Mitsui ya nchini Japan.

Amesema mradi huo umezingatia jinsi ya kuwezesha muunganiko wa mfumo wa usafiri jijini Dar Es Salaam na ule wa mabasi yaendayo haraka awamu ya pili, tatu na ya nne. “Tumeacha eneo la mita 12 katikati ya barabara kwa ajili ya ujenzi wa mradi huo.”

Bandari ya Mtwara kupokea mafuta tani 8000 mwezi Septemba

$
0
0
Na Nuru Mwasampeta, Dodoma
Imeelezwa kuwa Bandari ya Mtwara itapokea mafuta tani za ujazo 8000 (lita milioni 9.6) ifikapo mwezi Septemba mwaka huu ikiwa ni mara ya Pili kupokea shehena hiyo ya mafuta kutoka yaliposhushwa kwa mara ya kwanza mwezi Juni mwaka huu.

Hayo yamebainishwa leo tarehe 29 Agosti, 2018 na Kaimu Mkurugenzi wa Wakala wa Uagizaji Mafuta kwa Pamoja (PBPA), Mjiolojia Erasto Simon, alipokuwa akiwasilisha ripoti ya Wizara ya Nishati kuhusu uanzishwaji wa gati la kupokelea mafuta katika bandari ya Mtwara kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini  jijini Dodoma.

Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu na Katibu Mkuu wa Wizara, Dkt. Hamisi Mwinyimvua waliwaongoza Watendaji mbalimbali wa Wizara na Taasisi zake katika utoaji wa taarifa na ufafanuzi wa masuala mbalimbali yaliyojitokeza.

“ Kiasi cha tani za ujazo 8,000 kinatarajiwa kushushwa katika Bandari ya Mtwara ifikapo mwezi Septemba ambapo tani 5,000 kati ya hizo zitakuwa ni mafuta ya dizeli na tani 3,000 zitakuwa ni petroli,” alisema Simon.

Ameongeza kuwa, Serikali iliamua kutumia rasmi Bandari ya Mtwara kupokea mafuta ili kupunguza msongamano wa magari ya kusafirisha mafuta kwenda mikoa ya Kusini na nchi jirani.

Amebainisha kuwa, kwa mara ya kwanza mafuta yalipokelewa katika bandari ya Mtwara tarehe 28 Juni, 2018 ambapo kiasi cha tani 8,339 kilishushwa bandarini hapo na kupokelewa kwenye maghala ya kuhifadhi mafuta yanayomilikiwa na kampuni za GM & Company /Oryx na Oilcom Tanzania.

Amesema kuwa,  kiasi hicho cha mafuta kilichoshushwa mwezi Juni, tani 5,139 zilikuwa ni mafuta ya dizeli na mafuta ya petroli yalikuwa na ujazo wa tani 3,200.

Akizungumzia manufaa yatakayopatikana kupitia kufunguliwa kwa gati hilo la Mtwara, Simon alisema kuwa ni kupokea mafuta yote yanayokwenda nchi jirani za Malawi, Zambia na Msumbiji na hivyo kupunguza msongamano wa meli zinazoshusha mafuta katika Bandari ya Dar es Salaam.

Ameongeza kuwa, manufaa mengine ni kuchangia katika kukuza uchumi wa mikoa ya Kusini pamoja na kupunguza bei ya mafuta katika mikoa hiyo kutokana na bei hizo kupangwa kuanzia Mtwara tofauti na ilivyokuwa awali ambapo kulikuwa na ongezeko la gharama za usafirishaji  mafuta kutoka Dar es Salaam hadi kufika mikoa ya Kusini.

“Mathalan, kwa mafuta yaliyoshushwa mwishoni mwa mwezi Juni 2018 bei elekezi iliyotolewa na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) ilikuwa ni shilingi 2,329 kwa lita ya dizeli mkoani Mtwara wakati Dar es Salaam ilikuwa ni shilingi 2,360 kwa lita,” alisema Simon.
 Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini pamoja na ujumbe kutoka Wizara ya Nishati na Taasisi zake ukiongozwa na Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu na Katibu Mkuu wa Wizara, Dkt. Hamisi Mwinyimvua wakiwa katika kikao kilichojadili taarifa mbili za utekelezaji wa majukumu ya  Wakala wa Uagizaji Mafuta kwa Pamoja (PBPA) na Shirika la Taifa la Maendeleo ya Petroli (TPDC) jijini Dodoma.
 Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (wa kwanza kushoto) na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt Hamisi Mwinyimvua (wa Pili kushoto) wakiongoza Ujumbe wa Wizara pamoja na Taaisisi zake katika kikao na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini.

JWTZ KUTIMIZA MIAKA 54 SEPTEMBA 1, LAHIMIZA WANANCHI KUSHIRIKI KUFANYA USAFI WA MAZINGIRA

$
0
0
Na Angess Francis Blogu ya Jamii

WATANZANIA wametakiwa kujitokeza na kushiriki kwa wingi katika kufanya shughuli za usafi wakati maadhimisho ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ) kutimiza miaka 54 tangu kuanzishwa kwake.

JWTZ linatarajia kufikisha miaka 54 ifikapo Septemba 1 mwaka huu.Jeshi hilo lolianzishwa mwaka 1964.
Akizungumzia sherehe hizo Mkurugenzi wa Habari na Uhusiano  wa JWTZ Kanali Ramadhani Dogoli amesema katika maadhimisho hayo ya mwaka huu jeshi limeanza kufanya  shughuli mbalimbali za kijamii  pamoja na kujishughulisha katika michezo.

“Itakumbukwa kila mwaka  inapofika tarehe hiyo bada ya kubadilishwa  jina kutoka Tanganyika Rifle (TR)  kuwa Jeshi la Ulinzi  la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).

"Na sherehe hizo kila mwaka tumekuwa tukifanya shughuli za kijamii kwa kufanya usafi  kwenye maeneo ya kambi zote za jeshi na kushiriki katika michezo,”amesema.
Amefafanua michezo inayoendelea kuchezwa ni mpira wa miguu,Pete,wavu, golf na mingine na kwamba timu za jeshi na za uraiani ndizo zinashiriki michezo hiyo.
Kanali Dogoli amefafanua shughuli hizo zilianza kufanyika  Agosti 27  mwaka huu na kwamba zitaendelea hadi siku kilele cha sherehe hizo.

Hivyo limesisitiza umuhimu wa watanzania wote wenye mapenzi mema kungana kuadhimisha siku  hiyo kwa kujitokeza kufanya usafi katika maeneo yao wanayoishi na  kuyaweka katika hali ya usafi.

BARAZA LA KILIMO TANZANIA LAKUTANA KUJADILI USALAMA WA CHAKULA NA MASOKO KWA WAKULIMA

$
0
0
Mkurugenzi wa Sera, Mipango na Utetezi kutoka ACT Bw Timothy Mmbaga akichangia mada kwenye Mkutano wa wadau wa Kilimo uliokuwa ukijadili usalama wa Chakula na Masoko kwa wakulima ulioandaliwa na Baraza la Kilimo chini ya Mradi wake wa Ubia wa Kilimo Tanzania (TAP) uliofanyika jana mjini dodoma. 
Katibu Tawala Msaidizi Sekta za Uchumi na Uzalishaji Mkoa wa Dodoma Bi Aziza Mumba akichangia Mada kuhusu Nafasi ya NFRA na CPB katika kuimarisha Usalama wa Chakula, Bei za vyakula na Masoko kwa wakulima ulioandaliwa na Baraza la Kilimo Tanzania (ACT) chini ya Mradi wake wa Ubia wa Kilimo Tanzania (TAP) uliofanyika jana Mjini Dodoma
Mratibu wa taifa wa ubia wa kilimo Tanzania TAP, Bw. Mark Magila akichangia mada wakati wa mkutano wa wadau wa kilimo uliokuwa ukizungumzia usalama wa chakula na masoko kwa wakulima ulioandaliwa na baraza la kilimo Tanzania chini ya mradi wake wa TAP na kuhudhuliwa na wadau mbalimbali wa kilimo uliofanyika mjini Dodoma jana. 
Sehemu ya washiriki wa warsha ya wadau wa kilimo nchini wakifuatilia kwa ukaribu mjadala wa nafasi ya NFRA na CPB katika kuimarisha usalama wa chakula bei za vyakula na masoko ya wakulima, ulioandaliwa na Baraza la Kilimo Tanzania ACT, Chini ya Mradi wake wa Ubia wa Kilimo Tanzania TAP, uliofanyika jana mjini Dodoma.
Afisa Sera kutoka Baraza la Kilimo Tanzania (ACT), Bi Laetitia Wiliam akisikiliza kwa makini uwasilishwaji wa Mada ya iliyokuwa ikihusu Nafasi ya NFRA na CPB katika kuimarisha Usalama wa Chakula, Bei za vyakula na Masoko kwa wakulima, katika walisha iliyoandaliwa na ACT chini ya Mmradi wake wa Ubia wa Kilimo Tanzania (TAP) uliofanyika jana Mjini Dodoma.
Mkurugenzi wa Sera, Mipango na Utetezi kutoka ACT Bw Timothy Mmbaga akiwa katika Picha ya pamoja na baada ya kumalizika kwa Mkutano wa wadau wa Kilimo uliokuwa ukijadili usalama wa Chakula na Masoko kwa wakulima ulioandaliwa na Baraza la Kilimo chini ya Mradi wake wa Ubia wa Kilimo Tanzania (TAP) uliofanyika jana mjini dodoma.

SIMBACHAWENE AONGOZA KIKAO CHA KAMATI YA BUNGE YA BAJETI

$
0
0
 Mwenyekiti wa Kamati ya Bajeti , Mhe. Goerge Simbachawene akiongoza Kikao cha Kamati hiyo kilichokutana leo  katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma, pembeni ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Mashimba Ndaki . Kamati hiyo ilikuwa ikipitia na kuchambua Muswada wa Sheria ya Ubia baina ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi wa mwaka 2018.
 Kamati ya Bunge ya Bajeti ikiongozwa na Mwenyekiti wake Mhe. George Simbachawene ikiwa katika kikao cha Kamati leo katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma.Kamati hiyo ilikuwa ikipitia na kuchambua Muswada wa Sheria ya Ubia baina ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi wa mwaka 2018.

Kamati ya Bunge ya Bajeti ikiongozwa na Mwenyekiti wake Mhe. George Simbachawene ikiwa katika kikao cha Kamati leo katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma.Kamati hiyo ilikuwa ikipitia na kuchambua Muswada wa Sheria ya Ubia baina ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi wa mwaka 2018

MATUMIZI YA POMBE YANA MADHARA MAKUBWA KWA JAMII

$
0
0
MTANDAO wa Kudhibiti Madhara ya Matumizi ya Pombe (TAAnet) umeeleza kuwa matumizi makubwa ya pombe ni chanzo kikubwa cha matatizo hasa ugomvi na mifarakano katika familia.

Aidha mtandao huo umesema asilimia nne ya vifo vitokeavyo duniani na asilimia nne ya magonjwa yasitoambukizwa usababishwa na matumizi makubwa ya pombe yanayofanika kwa sasa.

Hayo yamebainishwa jijini Dar es Salaam Jana na Mjumbe wa bodi katika mtandao huo, Dk. Mashombo Mkamba wakati wa semina ya siku moja kwa waandishi wa habari kuhusu madhara ya matumizi ya pombe.

Alisema licha ya pombe kusababisha matatizo hayo pia inaelezwa kuwa ni moja ya visababishi vikubwa vya aina mbalimbali ya saratani zinazotesa baadhi ya watu nchini na duniani kwa ujumla.

"Najua ni vigumu kwa baadhi ya watu wanaotumia pombe kuacha Ila upo uwezekano wa kuiacha kama utaamua kwani hakuna faida yoyote inayotokana na unywaji wa pombe," alisema na kuongeza kuwa.

"Licha ya pombe kuwa chanzo kikubwa cha mapato ya serikali duniani kote,lakini usababisha ajali nyingi zinazosababisha vilema  na kupoteza maisha ya watu wengi," alisema.

Aidha alisema inakadiliwa katika kila mwaka lita 2.4 bilioni za pombe za kienyeji utengenezwa na kunywewa hapa nchini na kusema hiyo ni idadi kubwa ya pombe inayonywewa na watu.

Naye Kaimu Mwenyekiti wa TAAnet Sophia Komba alisema yapo magonjwa zaidi ya 120 usababishwa na matumizi ya pombe hivyo ameitaka jamii kubadilika kuacha matumizi ya vilevi kwani havina maendeleo wala faida yoyote.
Waandishi wa habari wakiwa katika semina ya siku moja inayohusu madhara ya matumizi ya pombe.

MWENYEKITI WA NEC AKAGUA MAENDELEO YA UJENZI WA OFISI ZA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI JIJINI DODOMA

$
0
0
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji (Rufaa), Semistocles Kaijage (katikati) akizungumza na baadhi ya Mafundi na  Wahandisi wa Mradi wa Ujenzi wa jengo la Ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi kutoka TBA na Chuo Kikuu Ardhi alipotembelea eneo la mradi wa ujenzi wa Ofisi hizo eneo la Njedengwa leo jijini Dodoma. Wengine ni Wajumbe na Watendaji wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji (Rufaa), Semistocles Kaijage (katikati) akikagua eneo linapojengwa ghala la kuhifadhia vifaa vya uchaguzi akiwa ameambatana Wahandisi wa Mradi wa Ujenzi wa jengo la Ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi kutoka eneo la Njedengwa leo jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji (Rufaa), Semistocles Kaijage (katikati) akizungumza na Wajumbe na Watendaji wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (kulia) mara baada ya kutembelea eneo la mradi la ujenzi wa Ofisi za NEC jijini Dodoma. Wengine (kushoto) ni Mafundi na  Wahandisi wa Mradi wa Ujenzi wa jengo hilo kutoka TBA na Chuo Kikuu Ardhi.
Msimamizi wa Mradi wa Ujenzi wa jengo la Ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi Muhandisi Geofrey Mushanyela akitoa ufafanuzi kuhusu maendeleo ya mradi wa ujenzi wa ofisi hizo kwa wajumbe na watendaji wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi waliotembelea mradi huo leo jijini Dodoma.

Wajumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) wakipita mbele ya jengo la Utawala la Tume ya Taifa ya Uchaguzi wakiongozwa na Wahandisi wanaosimamia mradi huo kutoka TBA na Chuo Kikuu Ardhi. Jengo hilo la Ofisi za NEC linajengwa eneo la Njedengwa jijini Dodoma leo. PICHA/ TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI

MADIWANI WATANO PWANI WAKIMBILIA CCM LEO NI PAMOJA NA RAMADHANI LUTAMBI WA KATA YA MAILMOJA

$
0
0
MADIWANI watano wa vyama vya upinzani ikiwemo Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA, CUF na ACT Mzalendo na viongozi wengine sita wamevikimbia vyama hivyo na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoani Pwani.

Madiwani hao ni pamoja na Ramadhan Lutambi aliyekuwa diwani wa kata ya Mailmoja kupitia Chadema na Ramadhan Kombe aliyekuwa diwani  kata Mbwawa kupitia ACT. 

Wengine ni, Muharami Mkopi Cuf kata ya Ruaruke wilayani Kibiti,Seif Lwambo kupitia Cuf kata ya Beta,Muharami Mketo Cuf Kata ya Lukanga na Mwenyekiti wa Kijiji cha Lukanga.

Aidha viongozi waliojiuzulu kwenye vyama hivyo ni Ayubu Chapile ambae alikuwa katibu kata ya Mkuza (CUF) ,Karimu Kasimu katibu tawi chuo kikuu cha Mwalimu Nyerere (Chadema) ,Selemani Mwinyimkuu mwenyekiti tawi (Cuf),David Mramba Act,Latifa Sangalala mwanachama Chadema Mkoani B na Jumanne Urembo Diwani kivuli ACT kata ya Sofu.

Awali Ramadhani Lutambi alisema ,chama kinachofaa kuongoza nchi daima ni CCM kwani vyama vingine havina uwezo,na havijali  viongozi wa ngazi za chini .

Alifafanua ,ameamua kuondoka Chadema ili kutekeleza yale yanayofanywa na Rais Dk. Magufuli kwa wananchi wanyonge.

Lutambi alikiri kuondoka Chadema kwa hiari yake, kwa akili zake timamu na kudai anajivua vyeo vyote alivyonavyo kuanzia sasa. 

Akiwapokea madiwani na viongozi wa vyama hivyo kwenye ofisi za CCM Mkoa, mwenyekiti wa CCM mkoani Pwani, Ramadhani Maneno alisema ,kutokana na utekelezaji mzuri wa ilani wameona hakuna sababu ya kubaki kwenye vyama vyao.

Alisema kazi kubwa inayofanywa na chama kupitia Rais Dk .John Magufuli ndio sababu kubwa ya madiwani na viongozi hao kukimbilia CCM. 

"Baadhi ya watu wamekuwa wakipotosha kuwa wabunge,madiwani na viongozi wanaohamia CCM wananunuliwa ,suala hili halipo ,ni kwamba wanarudi kutokana na utendaji kazi wa chama chetu," alisema Maneno.

Maneno alieleza, viongozi hao hawanunuliwi wala kuhongwa bali ni mapenzi yao .

"Kuhusu gharama za uchaguzi kuwa ni kubwa hilo ni suala la Tume ya uchaguzi na chama kisilaumiwe kwani kuhama kwao hakuhusiani na kurubuniwa ," alisema Maneno.
 Aliyekuwa diwani wa kata ya Mailmoja, Kibaha Ramadhani Lutambi kupitia Chama Cha Chadema amekimbilia Chama Cha Mapinduzi (CCM)
 Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi  (CCM) mkoani Pwani Ramadhani Maneno akizungumza baada ya kuwapokea madiwani watano kutoka upinzani na viongozi na wanachama wengine wa vyama hivyo wapatao sita.

Aliyekuwa diwani wa kata ya Mailmoja, Kibaha Ramadhani Lutambi kupitia Chama Cha Chadema akiwapungia mkono baadhi ya wananchi na wanachama wa CCM katika ofisi za CCM mkoani Pwani baada ya kuacha chama hicho na kukimbilia Chama Cha Mapinduzi (CCM) (picha na Mwamvua Mwinyi)

ANAYEJENGA FLY OVER TAZARA AWEKA REKODI YA AINA YAKE

$
0
0
 Mwakilishi Mkuu wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan(JICA) Ofisi ya Tanzania Toshio Nagase akizungumza leo jijini Dar es Salaam ya miradi mbalimbali ya maendeleo.
Mhandisi Mkuu wa Shirika la Umeme Tanzania(Tanesco) Ilala, Dastani Ndamugoba  katikati akizungumza na wandishi wa habari jijini Dar ees Salaam leo kuhusu mradi wa umeme uliopo Muhimbili. Kulia ni Meneja wa Tanesco Ilala Mhandisi Sotco Nombo.
 Jinsi barabara ya flyover ilivyo.
Baadhi ya wajumbe kutoka JICA wakifurahia kukamilika kwa ujenzi wa Fly over ya Tazara jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya washiriki wakisikiliza maelezo kutoka kwa mwakilishi wa JICA.

*Atumia saa milioni 2.4 ya kazi bila kupata ajali.
*Mwakilishi JICA ataja vipaumbele miradi ya maendeleo

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
MWAKILISHI Mkuu wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan(JICA) nchini Tanzania Toshio Nagase amesema Mkandarasi wa kijapani amefanikiwa kuweka rekodi ya usalama wakati wa ujenzi Fly over ya Tazara ambapo kwa zaidi ya saa milioni 2.4 ya kazi yamepita bila ajali.

Amesema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati anaelezea namna JICA wamekuwa wakishiriki katika kutoa misaada ya mikopo yenye masharti nafuu kwa ajili ya miradi ya kimaendeleo.

Amefafanua JICA imekuwa inatekeleza miradi mbalimbali hapa nchini tangu mwaka 1963 na kwamba Watanzania 18,000 wamepata mafunzo Japan, wataalam 2,000 wa Japan wamekuja nchini.Pia watalaam wa kujitolea kutoka nchi hiyo 1600 wameletwa Tanzania kwa nyakati tofauti.

Hivyo wakati anazungumzia ujenzi wa Fly over hiyo amesema mkandarasi Japan ameweka rekodi kwani hadi sasa hakuna aliyepata ajali.

“Barabara ya juu ya kwanza yenye urefu wa mita 425 ambayo itakamilika Septemba mwaka huu.Msongamano wa magari kwenye makutano ya barabara yenye magari mengi hapa nchini utapungua kwa kiasi kikubwa.

“Muda wa kusafiri utapungua kwa takribani asilimia 40,”amesema Nagase.

Mbali na ujenzi huo wa Flyover amesema JICA wamefanikiwa kutoa misaada ya fedha kwa ajili ya miradi mbalimbali nchini na kufafanua Tanzania ndio nchi inayoongoza miongoni mwa zile zilizopo Kusini mwa Jangwa la Sahara kwa kupata misaada mingi kutoka Japani.

“Serikali ya Japani na JICA ina mipango tisa chini ya maeneo matatu ya kipaumbele na eneo la kwanza ni kukuza uchumi, kuendeleza kilimo, kuendeleza kilimo cha mpunga na kuendeleza viwanda.

“Eneo la maendeleo ya miundombinu na hasa usafirishaji na mipango ya nishati  na eneo la tatu uimarishaji wa huduma za jamii hasa utawala bora,utawala wa fedha za umma , afya na miradi ya maji,”amesema.

Pia JICA imeelezea mradi wa umeme katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam ambapo kukamilika kwa mradi huo umesaidia kuondoa changamoto mbalimbali zilizopo hospitalini hapo.

Akizungumzia mradi huo wa umeme Mkuu wa Idara ya Ufundi na Matengenezo Mhandisi Leonard Elizeusi amesema kukamilika kwa mradi huo kumeifanya Hospitali ya Muhimbili kuondokana na changamoto ya kukatika umeme.

“Hatuna tatizo la umeme katika hospitali ya Muhimbili.Tunao umeme wa uhakika na mahitaji yetu uniti 4 lakini umeme unaozalishwa hapa ni uniti 12,”amesema.

Amefafanua kabla ya kuwepo kwa kituo hicho cha umeme kulikuwa na changamoto ya kukatika umeme mara mbili kwa wiki na hivyo kwa mwezi kutumia gharama kubwa kununua mafuta kuendesha majenereta.

Pia amesema changamoto ya umeme ilisababisha wakati mwingine huduma kutofanyika na hivyo kusabibisha vifo lakini sasa hakuna matatizo ya umeme na hilo ni jambo la kujivunia.

WACHEZAJI SITA WA SIMBA WAONDOLEWA TIMU YA TAIFA

$
0
0
Kikosi cha Taifa Stars.

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
KOCHA Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania(Taifa Stars) Emmanuel Amunike amewaondoa kikosini wachezaji Sita(6) wa klabu ya Simba na mchezaji mmoja(1) wa klabu ya Yanga kwa kushindwa kuripoti kambini. 

Wachezaji walioitwa kwenye timu ya Taifa walitakiwa kuripoti Jumatatu jioni Agosti 27,2018 isipokuwa wachezaji wa Yanga wanaokabiliwa na mchezo wa Kombe la Shirikisho barani Afrika dhidi ya Rayon Sports ya Rwanda na wale wanaocheza soka nje ya Tanzania.

Wachezaji walioondolewa kikosini ni Erasto Nyoni,Shomari Kapombe, Jonas Mkude, Ramadhan Kichuya,John Bocco,Hassan Dilunga wote Simba na Feisal Salum wa Yanga.

Feisal ameondolewa kwa kushindwa kuripoti kambini kwa kuwa hakuongozana na klabu yake ya Yanga kwenda nchini Rwanda kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho kutokana na kutokuwa na leseni ya kucheza mashindano hayo hivyo alitakiwa kuripoti kambini kama alivyotakiwa. 

Wachezaji walioitwa kuziba nafasi hizo ni 
Salum Kimenya(Tz Prisons)Paul Ngalema,(Lipuli),Frank Domayo(Azam FC),Salum Kihimbwa(Mtibwa),Kelvin Sabato(Mtibwa)David Mwantika(Azam FC) na Ally Abdulkarim(Lipuli)

Wachezaji hao wanaungana na wengine walioitwa Taifa Stars kukamilisha kikosi cha wachezaji 25.

Wachezaji wengine walioitwa awali ni 
Aishi Manula(Simba)
Mohamed Abdulrahiman (JKT Tanzania )
Beno Kakolanya (Yanga)
Hassan Kessy (Nkana)
Gadiel Michael (Yanga)
Abdi Banda (Baroka)
Kelvin Yondan (Yanga)
Aggrey Morris Lipuli(Azam FC)
Andrew Vicent (Yanga )
Himid Mao (Petrojet)
Mudathir Yahya (Azam FC)
Simon Msuva (Al Jadida)
Rashid Mandawa (BDF)
Farid Mussa (Tenerife)
Feisal Salum (Yanga)
Mbwana Samatta (Genk)
Thomas Ulimwengu (Al Hilal)
Shabani Chilunda (Tenerife)
Yahya zaydi(Azam FC)

Wachezaji walioingia kambini hotel ya Sea Scape wanaendelea na mazoezi kwenye uwanja wa Boko Veterans chini ya kocha Mkuu Emmanuel Amunike na wasaidizi wake Hemed Morocco na Emeka Amadi. 

Tayari kati ya wachezaji 7 walioitwa kuchukuwa nafasi za walioondolewa wamesharipoti kambini na kuanza mazoezi na wenzao.

Wachezaji walioripoti baada ya kuitwa leo ni Frank Domayo na David Mwantika wote wa Azam FC.

Wakati huohuo viongozi wa klabu ya Simba Kaimu Katibu Hamisi Kisiwa na Meneja wa timu hiyo Richard Robert watafikishwa kwenye kamati ya maadili ya TFF kwa kukiuka maagizo halali ya TFF na kushindwa kuhakikisha wachezaji wao wanaripoti kambini huku wakifahamu taarifa hiyo iliyowafikia kimaandishi.

VIONGOZI WAPYA WA TSA WATALETA MAENDELEO

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
BARAZA la Michezo la Taifa (BMT) limesema kuwa uchaguzi mkuu wa chama cha mchezo wa kuogelea Tanzania (TSA) ulienda vizuri ingawa kulikuwa na changamoto zilizojitokeza hapo awali.

Uchaguzi huo uliofanyika mapema wiki hii, uliweza kuwapata viongozi wapya watakaoongoza kwa kipindi cha miaka minne ambao wameapa tayari kwa ajili ya kuanza kutumikia nafasi zao kwa ajili ya maendeleo ya mchezo huo.

Akizungumzia uchaguzi huo Afisa habari wa BMT Najaha Baklari amesema kuwa uchaguzi huo ulifanyika kwa amani kubwa sana ingawa awali kulitokea changamoto mbalimbali na Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi Juma Ikangaa aliweza kutoa rai kwa wagombea wote walioshinda nafasi zao wakazitumikie kwa ueweledi mkubwa ili kuleta manufaa kwa chama hicho, pia hata wale ambao hawakupata nafasi wae dele kuunga mkono.

Amesema kuwa  uchaguzi ulikuwa na ushindani mkubwa sana hususani katika nafasi za  Makamu Mwenyekiti  na Katibu Mkuu ambapo zilikuwa na wagombea zaidi ya mmoja na nafasi nyingine kuwa na mgombea mmoja mmoja lakini hakukuwa na wakati mgumu sana katika nafasi ya mwenyekiti, Mweka Hazina na Mkugenzi wa Elimu na Maendeleo ambazo  zilikuwa na mgombea mmoja mmoja.

Katika uchaguzi huo, Imani Dominick alishinda kwa kupata kura 21 kati ya 26, Asmah Hilal alishinda  Makamu Mwenyekiti baada ya kumshinda kiongozi mzoefu , Thauriya Diria. Asmah alipata kura 19 na  Diria akipata kura saba (7).  Mgombea mwingine, Mary Mugurusi hakupata kura hata moja  katika nafasi hiyo.

Wakati Diria akishindwa kwa Asmah, Ramadhan Namkoveka ambaye alikuwa katika uongozi wa siku nyingi, mdau huyo wa mchezo wa kuogelea akishindwa kutamba kwa  Inviolata Itatiro alishinda nafasi ya Katibu Mkuu kwa kupata kura 17 huku Namkoveka akipata kura saba tu.

Katika uchaguzi huo Anna Shanalingigwa aliyepata kura 25 kati ya 26 zilizopigwa huku Amina Mfaume akishinda nafasi ya ukurugenzi wa Ufundi kwa kupata kura 19 na kuwashinda Alex Mwaipasi aliyetangaza kujitoa hata hivyo alipigiwa kura (5) na Filex Mosi aliyepata kura moja ambaye naye alitangaza kujitoa pia.

Nafasi ya ukurugenzi wa Elimu na Maendeleo ilichukuliwa na Donald Kweka aliyepata kura 20 kati ya 26. Uongozi huo utakaa madarakani kwa kipindi cha miaka minne.

Viongozi wote waliapishwa kiapo cha utiifu wa uongozi  na Msajili wa Klabu na Vyama Vya Michezo, Ibrahim Mkwawa na kuwataka viongozi hao kuendeleza mchezo  huo.

Mwenyekiti mpya wa TSA, Imani Dominick wadau wa mchezo huo na serikali kwa ujumla kuwa wataleta maendeleo makubwa kwani mpaka kufikia hatua ya kuwania uongozi huo kumetokana na matarajio ya wanachama.

“Lengo ni kuleta maendeleo ya mchezo, nawaomba wanachama kuzingatia Katiba, naomba isomeni na kuifuata,tunaahidi  kuleta maendeleo makubwa,” alisema Dominick.

NCHI ZA AFRIKA WAKUTANA DAR KUTATUA CHANGAMOTO ZA USARISHAJI MIZIGO

$
0
0
 Washiriki kutoka nchi mbalimbali za Afrika wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya semina iliyohusu kubadilishana uzoefu wa usafirishaji wa mizigo barani Afrika.
Kamishna wa Forodha wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)Usaje Asubisye akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo baada ya semina ya kujadili na kubadilishana uzoefu kuhusu usafirishaji wa mizigo kati ya nchi moja na nyingine barani Afrika.

Na Said Mwishehe, Globu ya Jamii
NCHI wanachama wa Umoja wa Afrika (AU) wamekutana Dar es Salaam kujadili na kubadilishana uzoefu wa kutatua changamoto hasa wanazokutana nazo katika usafirishaji mizigo kati ya nchi moja na nyingine.
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Kamishna wa Forodha wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) Usaje Asubisye wakati anafungua semina kwa washiriki wa nchi hizo.

Amefafanua msingi wa kukutana kwao ni kujadili kwa kina kutatua changamoto zilizopo na lengo lao ni kuhakikisha nchi za Afrika zinashiriki kikamilifu katika kujenga uchumi.

Ametaja baadhi ya nchi ambazo zimeshiriki semina hiyo ni Rwanda,Afrika Kusini ,Kameruni,Every Coast na nchi nyingine za Afrika Mashariki.

Amesema kuwa pamoja na mambo mengine watajadili namna ya kuboresha utoaji huduma ya kusafirisha mizigo na kwa Tanzania nayo itatoa uzoefu wake na namna ambavyo wamefanikiwa kuondoa changamoto.

“Afrika tunataka liwe bara ambalo litakuwa na uchumi imara na hivyo kwetu sisi kupitia semina hiii tutaangalia nini kifanyike ili tupige hatua,”ameongeza.

Ameeleza pia nchi za Afrika ambazo zinabandari kuweka mkakati sahihi wa kusaidia nchi nyingine katika kusafirisha mizigo.

Pia amesema kuna baadhi ya changamoto ambazo zipo katika nchi moja na nyingine hakuna kutokana na uwepo wa masuala ya sharia, hivyo kupitia semina hiyo wataangalia namna ya kutua baadhi ya kero ili kurahisisha usafirishaji bidhaa katika nchi hizo.

Kuhusu mafanikio Asubisye amesema awali  kwa Tanzania usafirishaji wa mizigo kutokea bandari ya Dar es Salaam hadi nchini Rwanda zilikuwa zinatumika siku 12 lakini kwa sasa ni siku tano.

Akizungumzia zaidi changamoto ambazo wanaendelea kuzitafutia ufumbuzi wake ni kwamba TRA inataka kuona idara na mamlaka za Serikali zinafanya kazi kwa pamoja.

Amefafanua kwa sasa unaweza kukuta TRA wametoa kibali mzigo usafiri lakini anapofika barabarani mzigo unazuliwa kwasababu ya kuzidi au askari wa usalama barabarani nao wanakuwa na mambo yao na hivyo kusababisha usumbufu.

Hivyo katika kushughulikia hilo wanataka wote ambao wanahusika wanafanya kazi kwa pamoja kwani kuzuia mzigo kunasababisha kuongezeka kwa gharama na athari zake zinamkuta mtumiaji wan chi nyingine.

NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI ATEMBELEA KISIWA CHA GANA

$
0
0
 Naibu waziri Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega akiwa ameambatana na Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe,Lucas Boniphace Magembe wakiwa katika  boti ya kizamani, tayari kwa ajili ya safari ya  kwenda katika kisiwa cha Gana 
 katika ziara yake ya  kanda ya ziwa  ya kuwahamasisha wavuvi ufungaji wa samaki kwa vizimba katika ziwa Victoria.
(picha na Emmanuel Massaka Globu ya jamii)
 Naibu Waziri wa Mifugo na  Uvuvi,Abdallah Ulega akizungumza na wananchi wa kisiwa cha Gana wilaya ya  Ukerewe mkoa wa Mwanza ambapo aliwasisitiza polisi pamoja na mgambo wanapoenda kwenye operesheni ya kupambana na  uvuvi haramu wawewanaenda na maafisa uvuvi kwa kuwa wao wanajua zana haramu pamoja samaki wasioruhusiwa kisheria.
 Naibi Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega akipanda boti ya kizamani, tayari kwa ajili ya safari ya kuelekea katika kisiwa cha Gana Wilaya ya Ukerewe  kwaajili ya kuhamasisha ufungaji wa samaki kwa vizimba katika Vctoria.
 Wananchi wa kisiwa cha Gana wilaya ya Ukerewe  wakimsikiliza Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega wapili (kushoto) akiwa ameambatana na Mkuu wa Wilaya ya Sengerema,Lucas Magembe (kushoto) wakiwasili katika kisiwa cha Gana.

HAKI MADINI WAJENGEA UWEZO JAMII WA ARDHI NA MADINI

$
0
0
SHIRIKA la Haki Madini la jijini Arusha, limewajengea uwezo viongozi wa serikalini, wa kimila na baadhi ya wananchi wa mikoa ya kanda ya kaskazini, juu ya utambuzi wa uthamini wa fidia ya ardhi na madini. 

Mwanasheria wa shirika la Haki Madini, Erick Luwogo akizungumza mjini Moshi Mkoani Kilimanjaro,  alisema kupitia mafunzo waliyotoa, elimu ya fidia ya ardhi na madini itaifikia jamii ipasavyo. 

Luwogo alisema wanataka kuona changamoto ya ucheleweshaji wa fidia, isiyo sahihi na kukatazwa kufanya maendelezo zinapatiwa ufumbuzi kwa haraka. 

"Tumekutanisha wadau wengi wakiwemo wanasheria, wenyeviti wa vijiji, watendaji wa vijiji, viongozi wa kimila, jamii na lengo hasa ni kupata majawabu ili serikali inapotoa fidia iwe inafanya kwa wakati," alisema. 

Mkazi wa mji mdogo wa Mirerani, Anthony Mavili alisema miradi mingi mikubwa ya eneo hilo imefanyika lakini wananchi ambao waliathirika kwa namna moja au nyingine hawakufidiwa. 

"Kuna barabara ya lami ya Kia-Mirerani wananchi waliovunjiwa nyumba zao hawakufidiwa na pia ukuta unaozunguka migodi ya madini ya Tanzanite kuna makazi, maboma ya wafugaji na njia za mifugo ilipitiwa ndani ya ukuta lakini jamii haikufidiwa," alisema Mavili. 

Ofisa mtendaji wa kijiji cha Mundarara Wilayani Longido Mkoani Arusha, Yohana Muyase alisema tatizo la muda mrefu wa kulipwa fidia linawatatiza wananchi. 

Muyase alisema fidia ni suala lililopo kisheria hivyo linapaswa kutekelezwa mara baada ya kufanyika kwa tathimini tofauti na ilivyo hivi sasa. 

Ofisa mtendaji wa kijiji cha Naisinyai Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, Godbless Mollel amesema kupitia elimu hiyo ataenda kuwasaidia wananchi juu ya elimu ya fidia. 

Mthamini mkuu wa Halmashauri ya jiji la Arusha, Rosemary Kirenga alisema pamoja na manufaa ya elimu hiyo bado tatizo la kulipwa fidia kwa wakati baada ya kufanyika tathimini ni changamoto na watalifanyia kazi. 

Kirenga alisema ofisi ya mthamini imeona changamoto hizo hivyo wanaendelea kutoa elimu ya fidia ili jamii itambue kuwa serikali ipo pamoja nao katika kuwatekelezea kwa wakati. 

Alisema kupitia sheria mpya ya wathamini iliyopitishwa na bunge ya mwaka 2016 pamoja na kanuni zake zitawawezesha wananchi walipwe fidia zao kwa wakati. 
 Baadhi ya walioshiriki warsha hiyo mwanasheria wa TLS Linda Shamba (kushoto) na mhandisi wa madini Ernest Sanka.
 Baadhi ya viongozi wa serikali, wanasheria na wananchi walioshiriki kwenye warsha ya sheria ya fidia ya ardhi na madini iliyoandaliwa na shirika la Haki Madini, mjini Moshi Mkoani Kilimanjaro. 
 Mmoja kati ya wawezeshaji wa warsha hiyo, mthamini mkuu wa Halmashauri ya jiji la Arusha, Rosemary Kirenga (kushoto) na mwanasheria wa shirika la Haki Madini, Erick Luwogo wakizungumza na washiriki wa warsha hiyo. 
Mkazi wa Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, Anthony Mavili akizungumza juu ya fidia kwenye warsha ya sheria ya fidia ya ardhi na madini iliyoandaliwa na shirika la Haki Madini mjini Moshi Mkoani Kilimanjaro. 

MKUU MPYA WA WILAYA YA BAGAMOYO ZAINABU KAWAWA AFUNGUA RASMI MAFUNZO YA AWALI YA JESHI LA AKIBA KWA VIJANA 183 CHALINZE

$
0
0
VICTOR MASANGU,  CHALINZE
MKUU mpya wa Wilaya ya Bagamoyo Zainabu Kawawa amewataka vijana ambao wanahitimu  mafunzo ya jeshi la akiba  kuhakikisha wanakuwa wazalendo na nchi yao na kuachana kabisa na vitendo vya kujiingiza katika matukio ya kihalifu na badala yake wahakikishe wanazingatia sheria na taratibu zote zilizowekwa  kwa lengo la kuweza kulinda hali ya ulinzi na usalama wa wananchi na mali zao.

Kauli hiyo aliitoa wakati wa sherehe za ufunguzi rasmi wa mafunzo  ya awali ya  jeshi la akiba ambayo yamefanyika katika kata ya Bwilingu  na kuwajumusiha vipana wapatao 183 kutoka  katika halmashauri ya Chalinze Wilayani Bagamoyo Mkoa wa Pwani.

Mkuu huyo pia aliwahimiza vijana hao kuhakikisha wanakuwa na nidhamu ya hali ya juu katika kipindi chote cha mafunzo hayo ya kijeshi na kuzingatia maelekezo ambayo wanapatiwa na walimu wao kwa lengo la kuweza kujifunza   mbinu mbali mbali ambazo zitaweza kuwa ni mkombozi mkubwa katika kulilinda Taifa la Tanzania na kuweza kukabiliana na wimbi la matukio ya uhalifu.

“Napenda kuchukua fursa hii  kuwapongeza vijana ambao mmeweza kujitokeza katika mafunzo haya ya jeshi la akiba,lakini kitu kikukbwa ninawaomba muwe wazalendo na nchi yenu kwa kuhakikisha mnazingatia sheria na taratibu za nchi ikiwa ni sambamba na kuyatumia vizuri mafunzo mliyopatiwa kwa maslahi ya nchi na sio vinginevyo,”alisema

Kwa upande wake Mshauri wa jeshi la akiba  Wilayani Bagamoyo Maj Chinguku alibainisha kuwa  mafunzo hayo yatakuwa ya miezi minne na nusu ambapo vijana hao  wataweza kujifunza mbinu mbali mbali za kivita ambazo zitaweza kuwa ni mkombozi mkubwa kwa maslahi ya Taifa.

“Katika mafunzo haya vijana ambao walijitokeza hapo awali walikuwa ni 211 lakini baadhi yao wameshindwa kuendelea kutokana na sababu mbali mbali hivyo ambao wanaendelea kwa sasa na  ni vijana wapatao 183 ambao wametokea katika kata ya bwilingu, ambapo wataweza kupata mafunzo mbali mbali ya kijenzi kwa kipindi cha muda wa wiki 18 alisema Chinguku”

Naye Diwani wa  kata ya Bwilingu Lucas Lufundo alisema  kwamba mafunzo hayo yataweza kuwasaidia vijana kwa kiasi kikubwa kudumisha hali ya ulinzi na usalama katika maeneo mbali mbali  na kwamba kutaweza kupunguza wimbi la vijana wengi  ambao walikuwa wanakaa  vijiweni bila ya kujishughulisha na kazi pamoja na kupunguza na changamoto ya wimbi la  uhalifu.

VIJANA hao wapatao 183 kutoka halmashauri ya Chalinze katika mafunzo hato ya wiki 18 wataweza kupta fursa ya  kujifunza masomo mabli mbali  ya kivita  na yale ya kawaida ikiwemo ujanja wa porini,usomaji wa ramani, huduma ya kwanza usalama wa raia,utimamu wa mwili, uhamiaji,pamoja na vitendo katika medani pamona na kujifunza mapambano dhidi ya rushwa.
  Mkuu mpya wa Wilaya ya Bagamoyo Zainabu Kawawa wa kati kati akirukaruka mara baada ya kufungua mafunzo rasmi ya jeshi la akiba kwa vijana wapatao 183 hawapo pichani  kutoka kata ya  Bwilingu katika halmashauri ya Chalinze pembeni yake kulia ni Mshauri wa jeshi la akiba Wilayani Bagamoyo Maj Chinguku.
Mkuu mpya wa Wilaya ya Bagamoyo Zainabu Kawawa wa kati kati akirukaruka mara baada ya kufungua mafunzo rasmi ya jeshi la akiba kwa vijana wapatao 183 hawapo pichani  kutoka kata ya  Bwilingu katika halmashauri ya Chalinze pembeni yake kulia ni Mshauri wa jeshi la akiba Wilayani Bagamoyo Maj Chinguku.
Mkuu mpya wa Wilaya ya Bagamoyo Zainabu Rashid Kawawa kulia akiwa na  Mshauri wa jeshi la akiba wilayani humo wa kushoto Maj Chinguku wakati wa sherehe za ufunguzi rasmi wa mafunzo wa jeshi la akiba kwa vijana wapatao 183  ambayo yamefanyika katika  kata ya Bwilingu halmashauri ya Chalinze.

DC SOPHIA MFAUME ATEMBELEA SEKONDARI YA NASULI, AWAFUNDA WANAFUNZI WA KIKE, AELEZA MIKAKATI

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma Sophia Mfaume  akiwa katika picha ya pamoja na walimu wa shule ya sekondari Nasuli iliyopo wilaya ya Namtumbo Mkoani Ruvuma leo Agosti 30,2018.

Wanafunzi wa shule ya sekondari ya Nasuli iliyopo Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvumawakimsikiliza MKUU wa Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma Sophia Mfaume katika wilaya hiyo leo Agosti 30,2018.
 Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma Sophia Mfaume akimsikiliza mwanafunzi wa shule ya sekondari ya Nasuli leo. 
Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma Sophia Mfaume akikabidhiwa taarifa ya shule ya sekondari Nasuli na mkuu wa shule hiyo. 

Na Ripota Wetu, Globu ya jamii
MKUU wa Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma Sophia Mfaume ametembelea Sekondari ya Nasuli yenye kidato cha kwanza hadi cha sita iliyokuwa kwanza kimkoa katika matokeo ya Baraza la Mitihani la Taifa(NECTA) mwaka jana.

Akiwa shuleni ametumia nafasi hiyo pia kueleza kuwa malengo yao ni kuhakikisha shule hiyo inashika nafasi ya kwanza kitaifa huku akitoa ushauri kwa wanafunzi wahakikishe wanasoma kwa bidii na kuachana na mambo ambayo hayana uhusiano na masomo.

Akizungumza leo na Michuzi Blog, DC Mfaume amesema ametumia nafasi hiyo kuwakumbusha wanafunzi kwamba kitu chochote kikikaa eneo lisilo sahihi kinakua uchafu.

Amewapa mfano kwamba “Karatasi safi nyeupe nikiichukua na kuitupa pale 'smart area' ya shule basi itageuka na kuwa uchafu.... hivyo hata kuchanganya masomo na mambo yasiyohusu inakua ni uchafu.”

Mfaume amewasisitiza wanafunzi wa kike kuzingatia kanuni ya magauni manne ili wafikie ndoto zao.

Amefafanua gauni la kwanza ni sare za shule, gauni la pili ni joho kwa wanaohitimu Chuo Kikuu, gauni la tatu ni la harusi na gauni la nne ni nguo ya kwenda kujifungua.

Hivyo kwa sasa watambue gauni lao ni sare za shule za sekondari na wasikubali kuchanganya na magauni mengine kwani itakuwa ni uchafu na itawaharibia kufikia malengo yao.

Pia amewakumbusha kuzingatia nidhamu, bidii na kutokata tamaa huku akifafanua ni viungo muhimu katika kuhakikisha wanafaulu katika masomo yao na maisha kwa ujumla.

Amewaambia yeye akiwa shuleni alihakikisha anasimama katika kutimiza ndoto zake , hivyo aliweka kando kila aina ya uchafu na hatimaye alifanya vema kwenye masomo kwa kupata ufaulu mzuri.

Pia amesema amepata nafasi ya kuzungumza na walimu kwa kuweka mikakati itakayofanikisha shule hiyo kufanya vema kwenye mtihani wa Taifa kwa kushika nafasi ya kwanza.
Viewing all 39066 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>