Quantcast
Channel: MTAA KWA MTAA BLOG
Viewing all 39112 articles
Browse latest View live

WATAFITI WASISITIZWA USHIRIKI JOPO LA KIMATAIFA LA SAYANSI YA MABADILIKO YA HALI YA HEWA NA TABIA NCHI

$
0
0

 

Kaimu Mkurugenzi mkuu wa TMA na Makamu Mwenyekiti wa Jopo la Kimataifa la Sayansi ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa na Tabianchi, Dkt. Ladislaus Chang’a akitoa hamasa kwa watafiti mbalimbali kutumia fursa zilizopo kwenye jopo la kimataifa kupitia mkutano wa elimu ya uelewa juu ya shughuli zinazofanywa na IPCC na UNFCCC uliofanyika katika ukumbi wa IRA, UDSM jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Tathmini Rasilimali UDSM, Prof. Joel Kirway akitoa shukurani kwa Dkt. Chang’a kwa kuitikia mwaliko wa kukutana na watumishi wa UDSM ili kupata elimu ya uelewa wa Shughuli zinazofanywa na IPCC na UNFCCC kupitia mkutano uliofanyika katika ukumbi wa IRA, UDSM, jijini Dar es Salaam
Washiriki wa mkutano wakichangia mada baada ya kupata uelewa juu ya fursa zilizopo kwenye jopo la kimataifa kupitia mkutano wa elimu ya uelewa juu ya shughuli zinazofanywa na IPCC na UNFCCC uliofanyika katika ukumbi wa IRA, UDSM,  jijini Dar es Salaam.
Mratibu wa Kituo cha Taaluma za Mabadiliko ya Tabianchi-UDSM, Dkt. Edmund Mabhuye akishukuru kwa kupata uelewa juu ya fursa zilizopo kwenye jopo la kimataifa kupitia mkutano wa elimu ya uelewa juu ya shughuli zinazofanywa na IPCC na UNFCCC uliofanyika katika ukumbi wa IRA, UDSM jijini Dar es Salaam.





KAIMU Mkurugenzi Mkuu, Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) na Makamu Mwenyekiti wa Jopo la Kimataifa la Sayansi ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa na Tabianchi, Dkt. Ladislaus Chang’a amewasisitiza watafiti mbalimbali nchini kutumia fursa zilizopo katika Jopo hilo kwa kushiriki kikamilifu na kutoa mchango wa sayansi ya mabadiliko ya hali ya hewa ngazi ya nchi.

Dkt. Chang’a ameyasema hayo hivi karibuni wakati akizungumza na wanasayansi, watafiti, viongozi na watumishi kutoka Idara mbalimbali za Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) ikiwa ni moja ya mkakati wa kuhimiza na kuongeza mchango wa nchi za Afrika kwenye ripoti mbalimbali zinazotolewa na Jopo hilo la Kimataifa.

“Huu ni mkutano wangu wa kwanza kama Makamu Mwenyekiti wa IPCC nikiwa na jukumu la kuhamasisha ushiriki wa Afrika katika mchakato na kazi za IPCC, ikiwemo maandalizi ya Ripoti ya Saba.

Viongozi wa sasa wa IPCC kutoka Afrika tumejipa jukumu la kuhamasisha na kuhakikisha ongezeko la ushiriki wa watafiti kutoka Afrika katika Jopo la IPCC. Aidha, niwajulishe kuwa mchakato wa ripoti hiyo, unatarajiwa kuanza hivi karibuni”. Alisema Dkt. Chang’a.

Naye, Mkurugenzi wa Taasisi ya Tathmini Rasilimali, UDSM Prof. Joel Kirway amempongeza Dkt. Chang’a kwa kuchaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa IPCC na kuitikia mwaliko wa kukutana na watumishi mbalimbali wa UDSM ili kuwasilisha mada ya fursa zilizopo katika Jopo la IPCC kwa Chuo cha Dar es Salaam ambacho kina Kituo cha Taaluma za Mabadiliko ya Tabianchi, kwa kutambua mchango katika maendeleo ya nchi na Afrika kwa ujumla.

Aidha, baada ya majadiliano ya kina, Prof. ameahidi kutoa ushirikiano kwa kushirikisha idadi kubwa ya watumishi na wanachuo ili kuleta mabadiliko chanya katika machapisho mbalimbali ya IPCC.

TBS YASHIRIKI MAONESHO YA 20 YA WAHANDISI

$
0
0
Shirika la Viwango Tanzania (TBS ) limeshiriki katika maonesho ya 20 ya Wahandisi Jijini Dar es salaam, katika maonesho haya Shirika limepata nafasi ya kutoa elimu kwa wajasiriamali,wazalishaji wa bidhaa na Wahandisi.

Akizungumza katika maonesho haya Afisa Masoko TBS, Bi. Rhoda Mayungu ametoa wito kwa wahandisi kushiriki katika mchakato wa uandaaji wa viwango katika sekta mbalimbali kwa kutoa maoni na mapendekezo pale kiwango kinapowasilishwa kwa umma ili kupata maoni kabla ya kuhitimishwa, kwani wahandisi ni wadau muhimu.

"Shirika linapoandaa Viwango kabla ya kuhitimishwa hupelekwa kwa umma ili kupata maoni na mapendekezo endapo wahandisi watashirki kikamilifu katika hatua hii itasaidia wananchi kwani wao ni wadau muhimu sana” Alisema

Mmoja wa Wahandisi kutoka shirika hilo Bi. Christina John,amesema"Tupo hapa kwa ajili ya kuwaasa Wahandisi wenzetu ambao wana miradi ya kihandisi, Wahandisi wa majengo, mitambo,kemikali na wengine wote kwa ujumla wanapokua wanafanya miradi wahakikishe vifaa wanavyo tumia vimehakikiwa kwa ubora kwa ajili ya ubora wa miradi hiyo"Alisema

"Tunawaomba Wahandisi wanapotumia vifaa kwenye miradi yao wahakikishe wanatumia vifaa vilivyo thibitishwa na TBS,amewaomba wale ambao hawatumii vifaa vilivyothibitishwa,kulingana na sheria za Viwango wale wanao kiuka taratibu za ubora sheria zitatumika".Alisema






NAIBU WAZIRI WA MAJI MHANDISI MARYPRISCA ASHIRIKI MAADHIMISHO YA 12 YA MTO MARA.

$
0
0
Naibu Waziri wa Maji, Mhe.Mhandisi Maryprisca Mahundi kwa niaba ya Waziri wa Maji ameshiriki Maadhimisho ya 12 ya Siku ya Mto Mara, hafla hiyo imefanyika Mkoani Mara kwenye Viwanja vya Mugumu/Serengeti

Wakati wa Hafla hiyo Mhe. Mahundi amesema kuwa Maadhimisho ya Bonde la Mto Mara ni njia muhimu ya kudumisha umoja wetu na ujirani mwema sisi wana Afrika Mashariki.

Muitikio huu ni dhahiri kuwa sisi ni ndugu wenye nia moja ya kuhifadhi na kusimamia vyema rasilimali za maji za Bonde la Mto Mara ambao ni kiunganishi cha umoja wetu, ustawi wa jamii na mataifa yetu; pamoja na mustakabali wa kizazi cha sasa na kizazi kijacho "amesema"

Aidha amesema kuwa Mto Mara unafaida nyingi sana ikiwemo Hifadhi ya Taifa ya Serengeti kwa upande wa Tanzania pamoja na pori la akiba la Hifadhi ya Taifa ya Maasai-Mara kwa upande wa Kenya ambapo Hifadhi hizi mbili ni kielelezo cha utalii duniani na uchumi wa mataifa yetu.

Hivyo, uhifadhi wake ni wa lazima na unadhihirisha maana ya maadhimisho ya siku ya Bonde la Mto Mara. Juhudi hizi ni uungaji wa dhamira njema ya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika agenda yake ya kukuza utalii kupitia jitihada mbalimbali kama vile filamu ya The Royal Tour.

Naye, Mkuu wa Msafara kutoka Jamhuri ya Kenya Mheshimiwa Tamalinye Koech amesema kuwa Bonde la Mto Mara ni eneo muhimu kwa maendeleo ya kiuchumi kutokana na baionual zilizopo. Pia, ameendelea kusisitiza kuwa hizi Nchi mbili ( Tanzania na Kenya) ziendelee kutoa elimu juu ya umuhimu wa uhifadhi mazingira ya Bonde la Mto Mara.









TPA YATOA MSAADA WA SHILINGI MILIONI 10 HOSPITALI YA WILAYA KIGAMBONI

$
0
0
Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania- TPA imetoa msaada wa Shilingi Milioni 10 kusaidia ujenzi wa uzio katika Hospitali ya Wilaya ya Kigamboni jijini Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 18 ya Mamlaka hiyo.

Akikabidhi Msaada huo ulioambatana na zoezi la Upandaji miche ya matunda zaidi ya 200 na kufanya usafi wa mazingira hospitalini hapo umekabidhiwa kwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Kigamboni Bi. Pendo Mahalu aliyemuwakilisha Mkuu wa wilaya ya Kigamboni na Mkurugenzi wa Bandari ya Dar es Salaam Bw. Mrisho S. Mrisho kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TPA Bw. Plasduce Mkeli Mbossa

Mrisho amesema, TPA itaendelea kusaidia jamii inayozunguka kwa lengo la kuboresha huduma za kijamii katika maeneo ya Elimu , Afya , Maendeleo ya Jamii na Majanga kulinga na Sera ya Uwajibikaji kwa Jamii (CSR )pamoja na kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuboresha huduma kwa jamii.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Bi. Pendo Mahalu ameishukuru TPA kwa kuguswa na kutoa kwa jamii kwa lengo la kusaidia kuboresha huduma za kijamii hasa katika Afya na Elimu. Kadhalika ametumia fursa hiyo kuzirai Taasisi zingine kuiga mfano wa TPA kutoa sehemu ya faida ya Taasisi zao ili kuunga mkono Juhudi za Serikali katika kuboresha huduma za Jamii.

Kiasi hiko cha milioni 10 kilichotolewa na TPA ni kwaajili ya kusaidia ujenzi wa uzio katika hospital hiyo Kwa lengo la kulinda usalama wa watendaji wa afya na wagonjwa.





TANZANIA YAPONGEZWA UTEKELEZAJI MRADI WA HAKIMILIKI NCHINI

$
0
0

Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah (kushoto) amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia kulinda hakimiliki za Ubunifu duniani -WIPO Bw. Daren Tang ( Kulia) makao makuu ya Shirika hilo Mjini Geneva, Uswisi, tarehe 13 Septemba,2023. 

Mazungumzo yao yalilenga kuimarisha ulinzi wa haki miliki za ubunifu na ushirikiano wa kimataifa, ambapo Dkt. Abdallah amemshukuru Bw. Tang kwa ushirikiano Mkubwa ambao WIPO imekuwa ikiutoa, ikiwemo ushauri wa kitaalamu kuhusu uanzishwaji wa Sera ya Taifa ya haki miliki na ubunifu Tanzania bara, kuanzishwa kwa sera ya haki miliki na ubunifu Zanzibar na kuanzishwa kwa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji nchini Tanzania. 

Bw. Tang ameipongeza Tanzania kwa mafanikio makubwa katika utekelezaji wa mradi wa hakimiliki nchini.








RAIS SAMIA AFURAHISHWA UTENDAJI KAZI BANDARI YA MTWARA,AAHIDI KUONGEZA BAJETI KUBORESHA MIUNDOMBINU

$
0
0

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amefurahishwa na ufanisi wa kiutendaji katika Bandari ya Mtwara hasa baada ya maboresho makubwa yanayoendelea kufanyika katika Bandari hiyo.

Akizungumza baada ya kukagua maendeleo ya Mradi wa Maboresho wa Bandari hiyo, Rais Dkt. Samia amesema Maboresho makubwa yaliofanyika Bandarini hapo yameleta ufanisi zaidi na kuufungua Kiuchumi Mkoa wa Mtwara na Mikoa ya Kusini mwa Tanzania.

Ameongeza kuwa Serikali yake itaendelea kuongeza Bajeti ya kuboresha miundombinu ya Bandari ili kuvutia zaidi Wateja, Wadau Wafanyabiashara wa Usafirishaji kuzitumia Bandari zetu.

Vilevile, Rais Dkt. Samia amesema Serikali yake imejiandaa kusafirisha korosho kupitia Bandari ya Mtwara, hivyo ametoa wito kwa Wananchi kujiandaa kuiunga mkono Serikali kwa kuongeza mapato yatokanayo na shughuli za Bandari.

Rais Dkt. Samia pia ametoa rai kwa Watumishi wa Bandari ya Mtwara kufanya kazi kwa bidii na weledi mkubwa ili Bandari hiyo ifikie kiwango cha Bandari ya Dar es Salaam.

Miradi iliyotekelezwa kama sehemu ya maboresho ya utendaji kazi wa Bandari ya Mtwara ni pamoja na ujenzi wa Gati moja la nyongeza lenye urefu ww mita 300, ujenzi wa mita ya kupimia mafuta ili kuhakikisha mafuta yanayoshushwa katika Bandari ya Mtwara yanapimwa, ujenzi wa sehemu ya kuhifadhi Makasha na ukarabati wa ghala na vifaa vya kuhudumia mizigo Bandarini.

Katika mwaka wa Fedha wa 2022/2023 TPA kupitia Bandari zake zote Nchini imehudumia Jumla ya Shehena Tani Milioni 24.899 ambapo Bandari ya Dar es Salaam ni Kinara kwa kuhudumia Shehena Tani Milioni 21.461 ikifuatiwa na Bandari ya Mtwara iliyohudumia Shehena Tani Milioni 1.62.

📍Bandari ya Mtwara

🗓️ 15 Septemba,2023




 

ETE WASHIRIKI SIKU YA USAFI DUNIANI

$
0
0

Katika maadhimisho ya siku ya usafi duniani ETE wamshiriki kusafisha ufukwe wa Kawe katika Bahari ya Hindi Dar es Salaam tuko lilio andaliwa na Haika Chao kutoka Student For Liberty Tanzania.


ETE pamoja na kushiriki kufanya usafi katika eneo hilo  wanatumia Dijitali kuyasemea mazingira  ambayo hayawezi kujisemea yenyewe, kupitia mitandao ya kijamii na majukwaa mbalimbali ya mtandaoni kwa lengo la kufikisha ujumbe wa kukumbusha jamii kuendelea kutunza mazingira na kuyapenda ili yaendelee kuwa faida ya kizazi cha sasa na vizazi vijavyo 

Picha zote na Fredy Njeje




KUSANYA MAOKOTO NA MERIDIANBET KASINO!!

$
0
0

 

LEO nakupasha kuhusu mchezo wa kasino ya mtandaoni wa Meridianbet wenye kuvutia ambapo, shangwe la bonasi za kasino ya mtandaoni linakusubiri. Ili kunogesha mchezo na kuufanya bora zaidi, bonasi zitakuwa zikinyesha kutoka angani. Mvua ya pesa itakunyeshea, shughuli ya kuzikokota noti hizi ni ya kwako.

Rainin Money ni mchezo wa sloti ya kasino ya mtandaoni uliotengenezwa na Iron Dog. Pamoja na kadi zenye nguvu za Wild, mizunguko ya bure, na bonasi maalum iliyopewa jina la mchezo inakusubiri. Pia kuna Ante Bet ambapo alama za scattter hutokea mara kwa mara.

Taarifa za msingi

Rainin Money ni mchezo wa sloti wa Meridianbet wenye nguzo tano zilizopangwa katika safu tatu na una mistari 20 ya malipo iliyowekwa. Ili kupata ushindi wowote, ni lazima upate alama tatu au zaidi zinazofanana kwenye mstari wa malipo.

Mchanganyiko wote wa ushindi huhesabiwa kutoka kushoto kwenda kulia kuanzia na nguzo ya kwanza kushoto.

Unaweza kupata ushindi mmoja kwa kila mstari wa malipo. Ikiwa una mchanganyiko wa kushinda zaidi kwenye mstari mmoja wa malipo, utalipwa mchanganyiko wenye thamani kubwa zaidi.

Jumla ya ushindi inawezekana ikiwa unazishikiza kwenye mistari kadhaa wakati huo huo.

Kubonyeza kitufe chenye picha ya sarafu kwenye kasino ya mtandaoni hii, hufungua menyu ambapo utaona vitufe viwili vya plus na viwili vya minus. Jozi moja ni kwa kuweka dau, wakati nyingine imetengwa kwa kuweka dau la chini na dau la juu.

Pia kuna chaguo la Automatic unachoweza kuamsha unapopenda. Kupitia chaguo hili unaweza kuweka hadi mizunguko 99.

Ikiwa unapenda mchezo wa haraka zaidi, unaweza kuamsha Njia ya Mzunguko wa Haraka katika mipangilio ya mchezo.

Alama za mchezo wa Rainin Money

Linapokuja suala la alama za mchezo huu, malipo ya chini kabisa ni alama za kadi za kawaida: 10, J, Q, K, na A. Zimegawanywa katika vikundi viwili, hivyo Q, K, na A vina thamani ndogo zaidi kuliko nyingine.

Alama nyingine zote zinawakilishwa na noti za benki. Utaona noti zenye namba, 10, 20, 50, na 100. Kwa mantiki, noti yenye namba 100 ina thamani kubwa zaidi.

Kwenye mchezo huu wa kasino ya mtandaoni Alama ya Joka linawakilishwa na alama ya Wild, na badala ya herufi I utaona umeme. Inachukua nafasi ya alama zote, isipokuwa kupandikiza, na kuwasaidia kuunda mchanganyiko wa kushinda.

Hii ni alama mojawapo yenye thamani kubwa katika mchezo huu wa kasino ya mtandaoni. Wild watano katika mchanganyiko wa ushindi utakuletea mara 500 ya dau lako la sarafu.

Bonasi za pekee

Sloti hii ya kasino mtandaoni pia ina chaguo la Ante Bet unaloweza kuanzisha wakati wowote. Ikiwa utaamsha, dau lako huongezeka moja kwa moja, lakini kupandikiza hutokea mara nyingi zaidi.

Scatters zinawakilishwa na birika la fedha la fedha na nyekundu na huonekana kwenye nguzo ya kwanza, ya tatu, na ya tano.

Birika la fedha la fedha ni pandikiza la kawaida na huonekana kwenye nguzo zote tatu katika mchezo wa msingi. Birika la fedha nyekundu ni pandikiza la super na kwenye mchezo wa msingi huonekana kwenye nguzo ya tano.

Kwa msaada wa pandikiza la super, unachochea bonasi ya Rain’s Money kulingana na sheria zifuatazo:

· Alama ya Scatter moja ya super hukupa chaguzi tano

· Alama ya Scatter moja ya super na Alama ya Scatter moja ya kawaida huleta chaguzi 10

· Scatter moja ya super na scatter mbili za kawaida huleta chaguzi 15

Unapochochea bonasi hii, sarafu zitanyesha kutoka angani na utachagua baadhi yao ambazo zitakuletea malipo ya pesa papo hapo au idadi ya chaguzi ziada.

Scatter tatu za aina yoyote kwenye nguzo zitakupa mizunguko ya bure. Ikiwa utapata pandikiza la super kati yao, pia utashinda Bonasi ya Rain’s Money.

Super scatter huonekana kwenye nguzo ya kwanza, ya tatu, na ya tano wakati wa mizunguko ya bure.

NB: Meridianbet inakuletea promosheni mpya ya “Jichukulie Maokoto na Halopesa” unapofanya miamala ya kuongeza salio kwenye akaunti yako ya Meridianbet. Zawadi kabambe ikiwemo Simujanja na Bodaboda mpya kugawiwa kwa washindi.

MKUU WA JKT NCHINI AUPONGEZA MKOA WA RUVUMA KWA KUONGOZA UZALISHAJI WA CHAKULA NCHINI

$
0
0

 

Na Albano Midelo,Songea

MKUU wa Jeshi la Kujenga Taifa JKT Meja Jenerali Rajabu Mabele
ameupongeza Mkoa wa Ruvuma kwa kuongoza kwa uzalishaji wa mazao
ya nafaka nchini hivyo kuchangia pato la Mkoa kwa asilimia 75.

Meja Jenarali Mabele ametoa pongezi hizo wakati anazungumza na Mkuu
wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas alipomtembelea ofisini kwake
mjini Songea katika ziara ya kikazi mkoani humo.

“Niwapongeza Mkoa wa Ruvuma mimi nilikuwa Mbeya wakati
mnakabidhiwa na Mheshimiwa Rais Tuzo ya mzalishaji wa kwanza wa
mazao ya nafaka nchini,katika mikoa yote ninyi mlionekana mmefanya
vizuri zaidi kwenye kilimo’’,allisisitiza.

Hata hivyo alisema anaamini Jeshi la Kujenga Taifa kambi ya Mlale
wilayani Songea ,ni sehemu ya wazalishaji wa mazao ya nafaka hivyo
katika tuzo iliyotolewa JKT Mlale pia wametoa mchango.

Amempongeza Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma kwa kutoa ushirikiano mkubwa
katika kambi ya JKT Mlale ambapo amemuomba Mkuu huyo wa Mkoa
kuendelea kuwatumia vijana wa JKT katika shughuli mbalimbali.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas
amesema katika msimu wa mwaka 2022/2023 Mkoa wa Ruvuma
umezalishaji tani 1,598,163 za mazao ya chakula hali iliyosababisha Mkoa
kuwa na ziada ya chakula tani 1,043,525.

Hata hivyo amesema kati ya tani hizo zao la mahindi pekee zimezalishwa
tani 1,043,324 na kwamba wananchi 1,848,794 waliopo mkoani Ruvuma
wanahitaji chakula tani 554,638 hivyo Mkoa kuwa na ziada kubwa ya
chakula.

Asilimia 87 ya wakazi wa Mkoa wa Ruvuma wanategemea kilimo.Kwa
mwaka wanne mfululizo Mkoa wa Ruvuma unaongoza kwa uzalishaji wa mazao ya nafaka nchini.
Mkuu wa JKT nchini Meja Jenerali Rajabu Mabele akiwa na maafisa wengine walipowasili ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas mjini Songea.Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa JKT Meja Jenerali Rajabu Mabele akipokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas mwenye suti ya bluu kwenye ofisi ya Mkuu wa Mkoa mjini Songea.

SHIRIKA LA OMUKA HUB NA NDI WAANDAA MAJADILIANO YA JUKWAA LA WANAWAKE KATIKA SIASA

$
0
0
Shirika la Omuka Hub ambalo limeanzishwa na Mhe Mbunge Neema Lugangira kwa kushirikiana na Shirika la Kimataifa la Marekani National Democratic Institute - NDI wameandaa Majadiliano ya Jukwaa la Wanawake katika Siasa kwa lengo la kujadili Mapendekezo ya Kikosi Kazi na Maazimio ya Mkutano Maalum wa Baraza la Vyama Vya Siasa yaliyotangazwa siku ya Jumatano tarehe 13 Septemba 2023.

Mjadala juu ya Ushiriki wa Wanawake katika Siasa katika ngazi zote kuanzia Kitongoji hadi Taifa umefanyika Bukoba, Mjini na umehudhuriwa na washiriki 100 kutoka makundi mbalimbali ya jamii ikiwemo Viongozi wa Dini, wakina Mama Viongozi , Wakuu wa Mashirika/NGOs, Viongozi wa Kisiasa kutoka Vyama Vya Siasa mbalimbali.

Maazimio ya Mjadala huu yanakwenda kuwa chachu katika utekelezaji wa maono ya Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Kuimarisha Uwakilishi wa Wanawake katika Siasa.

Aidha, Maazimio haya yatawasilishwa kwa Mhe Sisty Nyahoza, Msajili Msaidizi wa Vyama Vya Siasa ambae ndio Mgeni Rasmi wa Semina hii.

Washiriki wa Semina hii wamempongeza Mheshimiwa Rais kwa hotuba nzuri aliyotoa wakati anafungua Mkutano Maalum wa Baraza la Vyama Vya Siasa kwani hotuba ile inaeleza uhalisia na inatoa dira jinsi ambavyo shughuli za siasa zinapaswa kufanyika nchini ili kudumisha amani, utulivu na umoja wa kitaifa.

Mhe Rais alipongezwa pia kwa Serikali anayoiongoza kwa kutekeleza sehemu kubwa ya Mapendekezo ya Kikosi Kazi na walipongeza Wajumbe wa Mkutano Maalum wa Baraza la Vyama Vya Siasa kwa kufikia Maazimio yanayokuza demokrasia nchini ikiwemo kuimarisha Ushiriki wa Wanawake katika siasa, na hapa Washiriki wote wameunga mkono Mapendekezo yote ya Kikosi Kazi yaliyo katika eneo la Ushiriki wa Wanawake.

Aidha, Ndg. Sisty Nyahoza, Msajili Msaidizi wa Vyama Vya Siasa ambae ndio Mgeni Rasmi wa Semina amempongeza sana Mbunge Lugangira kwa ubunifu wake mkubwa wa kuandaa Majadiliano ya Jukwaa la Wanawake katika Siasa kwa lengo la kujadili Utekelezaji wa Mapendekezo ya Kikosi Kazi na Maazimio ya Mkutano Maalum wa Baraza la Vyama Vya Siasa (trh 11-13/ Sept. 2023) katika ngazi ya jamii.

Ndg. Nyahoza amewapongeza sana washiriki kwa mjadala mzuri sana na amechukua maoni yao ambayo yatafanyiwa kazi. Kikubwa zaidi amefurahia jinsi ambavyo amekutana washiriki kutoka ngazi ya jamii wa makundi mbalimbali wana uelewa mkubwa na masuala ya Ushiriki wa Wanawake katika Siasa.

Hii imempelekea kuwaomba Shirika la National Democratic Institute - NDI kuwa Majadiliano haya ya Jukwaa la Wanawake katika Siasa aliyoanzisha Mhe Mbunge Neema Lugangira ifanyike katika ngazi ya Kata na pia Wilaya zingine, na Mikoa mingine.






NCBA Golf Series ya mwaka 2023 Inakuja Tanzania: Jiandae Kuwa Sehemu ya Historia

$
0
0
Uko tayari kushiriki kwenye NCBA Golf Series ya mwaka 2023? Basi muda wa kufanya hivyo umefika kwani tayari mashindano haya makubwa yamefika Tanzania. Ikiwa yamepangwa kufanyika siku ya Jumamosi, tarehe 30/09/2023 mashindano haya yanatarajiwa kuwa yenye msisimko wa hali ya juu kwa wapenzi wa mchezo huu nchini Tanzania. 

Mashindano haya yatajumuisha wachezaji kutoka maeneo mabalimbali nchini Tanzania walioalikwa na Benki ya NCBA. Wachezaji hawa watakuwa wakiwania nafasi tatu za kwenda kushiriki fainali ya mashindano haya Nairobi, Kenya.  

Safari ya mashindano haya mwaka huu imepita katika nchi za Kenya, Uganda, Rwanda na sasa Tanzania kisha fainali ya mwisho itafanyika Nairobi, Kenya kuwapata washindi wa jumla wa mashindano haya makubwa. 

 Kinachofanya mashindano haya kuwa ya kipekee zaidi ni nafasi inayowapatia washindi. Kutakuwa na makundi matatu ya mabingwa: mshindi wa jumla, mshindi wa jumla kwa wanaume, na mshindi wa jumla kwa wanawake. Safari ya mabingwa hawa haitaishia kwenye viwanja vya Gymkhana Club badala yake watasafiri kwenda Nairobi, Kenya kuungana na mabingwa wengine kwa ajili ya kuwapata mabingwa wa jumla wa NCBA Golf Series ya mwaka 2023.  

Safari hii ya kuelekea Nairobi italipiwa kila kitu na Benki ya NCBA hivyo kufanya ushindi kwa mabingwa wa Tanzania kuwa na ladha zaidi. Nchini Kenya, wataungana na washindi wengine kutoka maeneo mbalimbali katika mchuano wa mwisho kubaini washindi wa jumla wa mashindano yote ambapo washindi watatu, mmoja kutoka kila kundi, watapokea KSH 100,000. 

 NCBA Golf Series si tu kuhusu ushindani; ni juu ya kuimarisha hisia za urafiki na upendo kwa mchezo huu miongoni mwa wadau wake katika eneo la Afrika Mashariki. Mashindano haya yanakutanisha wachezaji wa golf na mashabiki, yakiumba nyakati za kumbukumbu ambazo zinaimarisha uhusiano kati ya Benki ya NCBA na wateja wetu wenye thamani. 

 Hivyo basi, weka katika kumbukumbu zako Jumamosi, Septemba 30, 2023, na jitayarishe kuona vipaji vikubwa vya golf vikionyeshwa pale Gymkhana Golf Club.

BENKI YA LETSHEGO FAIDIKA YAZINDUA KAMPENI YA “KOPA TUKUBUSTI''

$
0
0

Na Mwandishi wetu

Dar es Salaam. Benki ya Letshego Faidika imezindua kampeni mpya ijulikanayo kwa jina la KOPA TUKUBUSTI yenye lengo la kuwafaidisha wateja wao kwa kushinda zawadi mbalimbali ikiwa pamoja na fedha taslimu. Kupitia kampeni hiyo, mteja anaweza kushinda hadi asilimia 50 ya fedha alizokopa katika benki hiyo.

Mtendaji Mkuu wa Benki ya Letshego Faidika Bank, Bw Baraka Munisi alisema kuwa “lengo kubwa ya kampeni hiyo ni kuwafaidisha wateja wao. Alisema kuwa ubunifu walioufanya utawawezesha kuinua vipato vya wateja na kumudu gharama mbalimbali za maisha.”

Bw Baraka Munisi alisema kuwa “benki yao inawajali wateja wao na kuamua kuanzisha kampeni hiyo itakayodumu kwa kipindi cha miezi mitatu (siku 90).”

Kwa upande wake, meneja Masoko na Mauzo wa benki ya Letshego Faidika bw Asupya Nalingigwa alifafanua kuwa watakuwa wanafanya droo ya kutafuta washindi kila baada ya wiki mbili ambapo jumla ya washindi 30 watazawadiwa zawadi mbalimbali.

“Kampeni hii ina lengo la kuwawezesha au kuwafaidisha wateja wetu, ambapo zawadi ya kwanza ni kiwango cha fedha cha asilimia 50 ya fedha ya mkopo ambapo mteja wetu alikopa. Pia tutakuwa na zawadi nyingie za fedha taslimu, pikipiki, fulana na shajara (Diary),” alisema Asupya Nalingigwa.

Kwa mujibu wa Bw Nalingigwa, vigezo mbalimbali vimewekwa kwa washiriki wa kampeni hii ikiwa pamoja na umri kuanzia miaka 18, lazima awe mfanyakazi aliyethibitishwa wa serikali na taasisi binafsi na lazima awe na sifa za kupata mkopo kwa mujibu wa vigezo na masharti.

“Pia mteja ambaye ataingia kwenye kampeni hii lazima ajaze fomu maalum ya kukubali vigezo na masharti yaliyowekwa. Tunawaomba wateja wetu kushiriki kwa wingi katika kampeni hii yenye lengo la kuwafaidisha. Benki yetu inawajali wateja wake na kuanzisha kampeni hii kwa ajili yao,”  alisisitiza Bw Asupya Nalingigwa.

Benki ya Letshego Faidika ni muunganiko wa  taasisi mbili za kifedha za Letshego Tanzania na Faidika na ilianza rasmi shughuli za kibenki mwezi Julai mwaka huu (2023).

Mendaji Mkuu wa Benki ya Letshego Faidika Bank, Bw Baraka Munisi  (kulia) akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Kopa Tukubusti yenye lengo la kuwafaidisha wateja wao. Kushoto ni meneja Masoko na Mauzo wa benki ya Letshego Faidika bw Asupya Nalingigwa.  Kampeni ya Kopa Tukubusti ina  lengo la kuwafaidisha wateja wao kwa kushinda zawadi mbalimbali ikiwa pamoja na fedha taslimu. Kupitia kampeni hiyo, mteja anaweza kushinda hadi asilimia 50 ya fedha alizokopa katika benki hiyo

Mkaguzi wa  Bodi ya Michezo ya Kubahatisha nchini Joram Mtafya (kulia) akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Kopa Tukubusti  ya benki ya Letshego Faidika. Kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa benki ya Leshego Faidika, Baraka Munisi.  Kampeni ya Kopa Tukubusti ina  lengo la kuwafaidisha wateja wao kwa kushinda zawadi mbalimbali ikiwa pamoja na fedha taslimu. Kupitia kampeni hiyo, mteja anaweza kushinda hadi asilimia 50 ya fedha alizokopa katika benki hiyo.

Mkaguzi wa  Bodi ya Michezo ya Kubahatisha nchini Joram Mtafya (katikati) akipozi mara baada ya kuzindua rasmi kampeni ya Kopa Tukubusti  ya benki ya Letshego Faidika. Kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa benki ya Leshego Faidika, Baraka Munisi na kulia ni Afisa Masoko wa benki hiyo, Hindu Juma.Kampeni ya Kopa Tukubusti ina  lengo la kuwafaidisha wateja wao kwa kushinda zawadi mbalimbali ikiwa pamoja na fedha taslimu. Kupitia kampeni hiyo, mteja anaweza kushinda hadi asilimia 50 ya fedha alizokopa katika benki hiyo

Mtendaji Mkuu wa Benki ya Letshego Faidika, Baraka Munisi  (wa tatu kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Afisa Ukaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Joram Mtafya (wa pili kulia) na maofisa mbalimbali wa benki hiyo na wa kampuni ya maarufu ya kuandaa matukio mbalimbali  na masoko, Radian Limited chini ya Afisa mtendaji Mkuu Freddie Manento (wa kwanza kulia). Kampeni ya Kopa Tukubusti ina  lengo la kuwafaidisha wateja wao kwa kushinda zawadi mbalimbali ikiwa pamoja na fedha taslimu. Kupitia kampeni hiyo, mteja anaweza kushinda hadi asilimia 50 ya fedha alizokopa katika benki hiyo.


Wapiga kura 216,282 kupiga kura uchaguzi mdogo wa Mbarali na kata sita

$
0
0

 
Wapiga kura 216,282 walioandikishwa kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura wanatarajiwa kupiga kura kesho tarehe 19 Septemba, 2023 kwenye uchaguzi mdogo wa Jimbo la Mbarali na kata sita za Tanzania Bara.

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Jacobs Mwambegele ameyasema hayo Wilayani Mbarali, Mkoani Mbeya leo tarehe 18 Septemba, 2023 wakati akisoma risala kwa ajili ya uchaguzi huo na kuongeza kwamba uchaguzi utahusisha vituo 580 vya kupigia kura.

“Katika uchaguzi huu kuna jumla ya wapiga kura 216,282 walioandikishwa katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ambao watashiriki kuchagua viongozi wao. Aidha, uchaguzi huu utahusisha vituo 580 vya kupigia kura vilivyobainishwa,” amesema Jaji Mwambegele.

Kata zenye uchaguzi ni; Nala iliyopo Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Mfaranyaki iliyopo Halmashauri ya Manispaa ya Songea, Mwaniko iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi, Old Moshi Magharibi iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Moshi, Marangu Kitowo iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Rombo na Mtyangimbole iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.

Mwenyekiti wa Tume amevikumbusha vyama vya siasa, wagombea, mawakala wa vyama, wapiga kura na wananchi kwa ujumla kuhakikisha kwamba hawapigi kampeni siku ya kupiga kura kwa kuwa kufanya hivyo ni kinyume cha sheria.


“Alama za vyama vya siasa zinazoashiria kampeni kama vile vipeperushi, bendera na mavazi haviruhusiwi kutumika kesho tarehe 19 Septemba, 2023 ambayo ni siku ya uchaguzi,” amesema.Jaji Mwambegele ameongeza kwamba zoezi la kupiga kura katika maeneo yote ya uchaguzi litafanyika katika vituo vile vile vilivyotumika wakati wa Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020.

Ameongeza kwamba vituo vya kupigia kura vitafunguliwa saa moja kamili (1:00) asubuhi na kufungwa saa kumi kamili (10:00) jioni.

“Iwapo, wakati wa kufunga kituo watakuwepo wapiga kura katika mstari ambao wamefika kabla ya saa kumi kamili (10:00) jioni katika mstari na hawajapiga kura, wataruhusiwa kupiga kura. Mtu yeyote hataruhusiwa kujiunga katika mstari wa wapiga kura baada ya saa kumi kamili (10:00) jioni,” amesema.

Jaji Mwambengele amebainisha kwamba watakaoruhusiwa kupiga kura ni wale tu ambao wamo kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwenye kata husika na wana kadi zao za mpiga kura.

Ameongeza kuwa, hata hivyo, Tume kwa kuzingatia masharti ya kifungu cha 61(3) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343 pamoja na kifungu cha 62(1) cha Sheria ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Sura ya 292 imeruhusu wapiga kura ambao wamepoteza kadi zao au kadi kuharibika kutumia vitambulisho mbadala

“Mojawapo ya kitambulisho mbadala ambacho mpiga kura anaweza kutumia ni Pasi ya Kusafiria, Leseni ya Udereva au Kitambulisho cha Taifa kinachotolewa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA),” amesema.


Mwenyeki wa Tume amesisitiza kwamba ili mpiga kura aruhusiwe kutumia kitambulisho mbadala ni sharti awe ameandikishwa kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura na jina lake lipo katika orodha ya wapiga kura katika kituo anachokwenda kupiga kura.


“Katika kituo cha kupigia kura, kipaumbele kitatolewa kwa wagonjwa, watu wenye ulemavu, wazee, wajawazito na akina mama wanaonyonyesha watakaokwenda na watoto kituoni,” amesema.

Kuhusu wapiga kura kurudi nyumbani baada ya kupiga kura, Jaji Mwambegele amesema hilo ni sharti la kisheria na kwamba maadili ya uchaguzi yaliyosainiwa na kuridhiwa na vyama vyote vya siasa, Serikali na Tume yanaelekeza hivyo.

Alisisitiza kwa kusema “wapiga kura watatakiwa kuondoka kituoni mara wanapomaliza kupiga kura ili kuepusha msongamano na vitendo vinavyoweza kuchochea uvunjifu wa amani. Hivyo, Tume inawashauri wananchi kujiepusha na mikusanyiko katika maeneo ya vituo vya kupigia kura”.

Ametoa rai kwa wapiga kura katika Jimbo la Mbarali na kata sita zinazohusika na uchaguzi huu mdogo, kujitokeza kwa wingi kwenye vituo vya kupigia kura, ili kuwachagua viongozi wanaowataka.

Jumla ya vyama 17 vya siasa vinashiriki kwenye uchaguzi huo mdogo, vyama hivyo vinajumuisha AAFP, ACT–WAZALENDO, ADA–TADEA, ADC, CCK, CCM, CUF, Demokrasia Makini, DP, NLD, NRA, SAU, TLP, UDP, UMD, UPDP na NCCR–MAGEUZI.

MKURUGENZI MANISPAA YA TABORA AMPA SIKU TATU MKUU WA KITENGO CHA TAKA NGUMU KUONDOSHA TAKA ZOTE ZILIZOLUNDIKANA MAENEO YA KUKUSANYIA TAKA

$
0
0

 

 

Mkurugenzi wa Manispaa ya Tabora Ndugu Elias M. Kayandabila amemtaka Mkuu wa Kitengo cha Taka Ngumu Ndugu Adamu Baleche kuhakikisha kuwa ndani ya siku tatu awe ameondosha taka zote zilizopo maeneo yote ya kukusanyia taka na kuzipeleka dampo. 

Kanyandabila ameyatoa maelekezo hayo leo Septemba 18, 2023 wakati wa Ziara fupi ya Timu ya Menejimenti ya Halmashauri (CMT) ya kukagua hali ya usafi katika viunga vya Manispaa ya Tabora.

Aidha Ndugu Kayandabila ameunda timu ndogo itakayoshirikiana na Kitengo cha Taka Ngumu katika kuratibu na kusimamia kazi zote za usafi mjini hapo, lengo kubwa ikiwa ni kuongeza ufanisi wa shughuli za usafi katika Manispaa yetu.

Wajumbe wa CMT nao baada ya kujionea hali mbaya katika maeneo ya kukusanyia taka, wameafiki kwa pamoja umuhimu wa timu hiyo ndogo ambayo itaongeza nguvu kwenye kitengo cha taka ngumu.


 

KONGAMANO LA 10 LA THS KUFANYIKA OKTOBA, MDH KUENDELEA KUTOA HUDUMA ZA UKIMWI

$
0
0

 Rais wa Kongamano la Afya Tanzania (Tanzania Tanzania Health Summit,(THS) Omary Chillo katikati akizungumza na waandishi wa habari leo Septemba 18, 2023 kuhusu kongamano la 10 la Kitaifa la Afya linalotarajiwa kufanyika kuanzia Oktoba 3-5, 2023 katika Kituo Cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Meneja wa Tathmini Afya ya Jamii kutoka Shirika la MDH, Dk Wilhelmuss Mauka akizungumza na Michuzi Tv leo Septemba 18, 2023 kuhusu kongamano la 10 la Kitaifa la Afya linalotarajiwa kufanyika kuanzia Oktoba 3-5, 2023 katika Kituo Cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

KONGAMANO la 10 la Afya Tanzania (THS), litakalofanyika Oktoba 3 hadi 5 mwaka huu,  linatarajia  kujadili mfumo wa afya, upatikanaji wa huduma za afya kwa wote na huduma za afya ya msingi.

Aidha, katika kongamano hilo, Shirika la MDH litaeleza namna lilivyohakikisha upatikanaji wa huduma za Ukimwi zinaendelea kutolewa licha ya mlipuko wa ugonjwa wa Marburg huko mkoani Kagera .

Akizungumza na waandishi wa habari leo Dar es Salaam, Meneja wa Tathmini Afya ya Jamii kutoka Shirika la MDH, Dk Wilhelmuss Mauka amesema katika kongamano hilo watazungumzia afya ya pamoja na namna walivyotekeleza utoaji wa huduma kwa wenye Ukimwi wakati wa mlipuko wa ugonjwa wa Marburg.

Lengo ni kutaka kuelezea namna walivyokabiliana nalo na kushirikiana na wadau, serikali na wagonjwa kupata huduma kama kawaida huku wakiendelea na utekelezaji wa huduma hizo Mkoa wa Kagera.

Ameeleza kuwa Afrika Mashariki na Afrika imekuwa ikikabiliwa na ugonjwa huo wa Marburg na Tanzania wamepata uzoefu ambao hawakuwahi kuwa nao awali kutokana na kuambukiza kwa kugusa.

"Wakati tunatoa huduma kwa wagonjwa wa Ukimwi watu wanakuwa wengi na wamejazana hivyo MDH kwa kushirikiana na serikali walitafuta namna ya kuzuia maambukizi wakati wakiendelea kutoa huduma hizo," 

Amesema kama shirika lisilo la kiserikali watazungumza namna walivyoshirikiana na serikali kutoa huduma za afya huku wakipambana na ugonjwa huo kuanzia Machi hadi Mei.

Akizungumzia takwimu za ugonjwa wa Ukimwi, Dk Mauka alisema asilimia 95 ya Watanzania wanajua hali zao, asilimia 95 wameanza kutumia dawa na wengine wanaendelea na huduma za dawa.

"Malengo ya dunia ni kufikia mwaka 2030 kutokuwa na maambukizi mapya ya Ukimwi na vifo," alisema Dk Mauka.

Alishauri wadau kutoa elimu kwa Watanzania wote ili waweze kupata huduma ya kupima na dawa ili kuepuka maambukizi mapya ya Ukimwi.

Kuhusu bima, alisema serikali inatoa muongozo kuhusu masuala ya bima, hivyo kama wadau wanatakiwa kujipanga na kuwa mstari wa mbele kuhakikisha huduma zinapatikana.

Alisema kama shirika wataangalia maeneo mengine ambayo wanaweza kuisaidia serikali ili watu wote wapate huduma za afya bure.

Dk Dunstan Mshana  Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), amesema mikutano ya nyuma ilikuwa na mafanikio na kwamba kuongeza kwa wadau katika mkutano huo utainua sekta ya afya.

Amesema wao ni watekelezaji wa sera kuwezesha ufanisi wa  zahanati, vituo vya afya na hospitali za Wilaya 

Ameeleza kuwa wanaweka utekelezaji mzuri wa Mfuko wa afya ya pamoja kwani kuna vituo vya afya zaidi ya 1,800 vimejengwa kwa miaka mitano hususan katika sehemu ambazo hazikuwa na huduma.

Amesema wamekuwa wakiajiri kujenga mazingira rafiki na kufikia wananchi katika huduma za afya na kuhakikisha kwamba ngazi za chini za huduma zinakuwa mali ya wananchi.

"Tunahakikisha tunaweka mazingira mazuri ya kuhakikisha huduma nzuri za afya zinatolewa kwa ngazi zote na wananchi wafurahie," amesisitiza Dk Mshana.

Ameongeza kuwa wataendelea kuwawezesha na kuwasaidia wadau wote wa afya kutekeleza majukumu yao ya  vizuri.

Mkuu wa Divisheni ya Utafiti Wizara ya Afya Zanzibar, Rashid Maulid Rashid amesema kuwa sera ya kuboresha huduma za afya kwa kuzingatia ngazi za chini inawagusa na kwamba wanashirikiana na wadau kuhakikisha huduma za msingi zinaanzia chini.

Amesema kila kilometa tano kuna vituo vya afya kuhakikisha huduma za afya karibu na kwamba hivi sasa wana wana hospitali kwa kila Wilaya.

"Kuhusu Mfuko wa bima ya Afya wananchi kupata huduma za afya bila kikwazo na kwamba wananchi wote wa Zanzibar watapata huduma za afya za uhakika hata wenye kipato cha chini kwa kupata matibabu bure," amesitiza Rashid.

Joseph Mhagama Meneja Utawala Aphta amesema kuwa wameshiriki kongamano hilo tangu linaanza na kuelezea kuwa moja ya maeneo muhimu katika utoaji wa huduma za afya ni katika ngazi za chini.

Ameongeza ili kuhakikisha afya kwa wote ni lazima kuhakikisha ubora wa huduma za afya na katika kongamano hilo, watazungumzia ubora.

Katika kongamano hilo, wajumbe 1,000 kutoka mashirika ya ndani na kimataifa wanatarajia kushiriki na litazikutanisha taasisi 50 ambazo zimethibitisha ushiriki wao, wawekezaji katika huduma za afya, wabunifu, wataalamu, viongozi wa Serikali na viongozi wa sekta binafsi ili kujadili mwenendo na maendeleo ya  huduma za afya nchini Tanzania.

Kaulimbiu ya mwaka huu ni Kuimarisha Mifumo ya Afya kwa ajili ya Huduma za afya kwa wote UHC, ikilenga Huduma ya Afya ya Msingi(PHC). 

Taasisi zinazoratibu mkutano huo ni Wizara ya Afya (MoH), Wizara ya Afya-Zanzibar, Baraza la Kiislamu Tanzania (BAKWATA), Tume ya Kikristo ya Huduma za Jamii (CSSC), Muungano wa Vituo vya Afya Binafsi Tanzania (APHFTA) na TMHS Tanzania.

Mkuu wa divisheni ya utafiti Wizara ya Afya Zanzibar, Rashid Maulid Rashid akizungumza na waandishi wa habari leo Septemba 18, 2023 kuhusu kongamano la 10 la Kitaifa la Afya linalotarajiwa kufanyika kuanzia Oktoba 3-5, 2023 katika Kituo Cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.




TAASISI YA OMUKA HUB YAFUNGUA MKUTANO KUANGAZIA SUALA UKATILI WA KIJINSIA MTANDAONI KWA WANAWAKE KATIKA SIASA

$
0
0
Taasisi ya OMUKA HUB ambayo imejikita katika masuala ya maendeleo na ujumuishi wa kidijitali ikiwemo kuhamasisha matumizi ya mtandao kwa wanawake katika siasa, imefungua mkutano wake jijini Dar es Salaam wenye lengo la kuangazia suala la ukatili wa kijinsia mtandaoni kwa wanawake katika siasa.

Akizungumza katika hafla hiyo leo Septemba 18,2023 Jijini Dar es Salaam, Mwanzilishi wa Taasisi hiyo Mhe.Neema Lugangila amesema ukatili wa kijinsia katika siasa una shabiana na ukatili wa wanawake katika habari.

"Tumekuwa na majidiliano mazuri ya namna gani tunaweza kuimarisha uwakilishi na ushiriki wa wanawake katika siasa za mtandaoni na tumekubalina tutaandaa kamati ambayo itaenda kudadavua suala hili ili tuje na mpango kazi ambao tutakapo kwenda kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu wanawake wataweza kushirik katika mitandao ya kijamii kunadi sera zao bila bughudha". Amesema.

Amesema anaelewa kadhia ambayo wanapitia wanawake wanasiasa katika mitandao hivyo wao kama wabunge wanawake wameamua kubeba ajenda hiyo kusemea wanawake katika siasa lwasababu wanatambua umuhimu wa kushiriki katika mitandao

"Sasa kwa kushirikiana na wanawake katika vyombo vya habari tunaamini tunaweza kushirikiana. vzuri na kupaza sauti kubwa ili kuweka mazingira sawia na wezeshi ili wanawake katika siasa waweze kushiriki ipasavyo katika mitandao ya kijamii".Amesema

Kwa upande wake Msemaji Mkuu wa Serikali Mhe.Gerson Msigwa amesema ukatili haukubaliki uwe wa kwenye vyombo vya habari, bungeni au mahali pengine popote hivyo serikali imekuwa ikishiriana na wadau kuhakikisha kwamba kunakua na kampeni mbalimbali za kukabiliana na ukatili dhidi ya wanawake.

Aidha amesema kuwa zipo sheria mbalimbali ambazo vitendo vyote vya ukatili havikubaliki na ni makosa kwa mujibu wa sheria hivyo wanaangalia kama wanaweza kuja na uwanja mpana zaidi wa kisheria wa kukabiliana na hayo majukumu.

Pamoja na hayo amempongeza Rais Samia Suluhu kuwa mstari wa mbele kuhakikisha anaongoza mapambano dhidi ya vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa wanawake katika maeneo mbalimbali na kuwawezesha wanawake wenyewe.

"Rais Samia ameandaa Wizara Maalumu ya kukabiliana na vitendo hivi ambayo ni Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, ambapo moja ya kazi ya Wizara hii ni kutoa Elimu kwa jamii juu ya kutambua vitendo vya ukatili,kuviripoti na kuchukua hatua kwa mujibu wa sheria". Amesema

Wadau walioshiriki mkutano huo ni pamoja na Wabunge wanawake,wawakilishi wa UNESCO Makao Makuu, na UNESCO Dar es salaam wawakilishi kutoka Habari Maelezo, IPU,TAMWA,Wabunge wanawake kutoka Ghana,Kenya,Uganda na Malawi.











NMB YASHINDA TENA TUZO YA KUONGOZA KUWAFADHILI WAJASIRIAMALI - AFRIKA

$
0
0

Benki ya NMB imetunukiwa tena tuzo na jukwaa la kufadhili ujasiriamali duniani (SME Finance Forum) kutokana na huduma zake wezeshi na ufadhili wake wa kuwaendeleza wafanyabiashara wadogo na wa kati nchini wakati wa mkutano wa jukwaa hilo uliofanyika September 14 katika jiji la Mumbai nchini India.

Ushindi iliyoupata Benki hiyo kwenye tuzo za mwaka huu za ufadhili wa ujasiriamali duniani (Global Finance Awards 2023 - GSMEFF 2023), ni wa Mfadhili wa Ujasiriamali wa Mwaka upande wa Afrika uliyoipa tuzo ya fedha (Silver Award).

Kama ilivyokuwa kwa tuzo zingine, tuzo za GSMEFF 2023 zinatambua dhamira na mafanikio ya taasisi za kifedha na kampuni zinazojihusisha na teknolojia za huduma za kifedha (fintech) katika kuwahudumia wateja wao ambao ni wajasiriamali wadogo na wa kati.

Pamoja na mambo mengine, tuzo hii imetambua mchango wa NMB katika kuwawezesha wajasiriamali kukuza biashara zao kwa:Kuwapa mikopo yenye riba nafuu kwa wakati, kuwapa elimu ya fedha kuhusu jinsi gani watazidi kukuza biashara zao kupitia majukwaa yao ya Business Clubs, Business Executive Network na mengine. Pia, kuwawezesha kupokea malipo kidijitali kupitia NMB Lipa Mkononi na njia zingine za kidijitali, kuwawezesha kukopa kidijitali bila kuwa na dhamana yoyote kupitia huduma ya Mshiko Fasta na kuendelea kufurahia huduma za kibenki kwa urahisi kupitia NMB Mkononi na Wakala popote pale wanapokuwa

Heshima hii ni ushahidi mwingine wa juhudi za dhati za benki hiyo za kuziba pengo la kuwafadhili wajasiriamali na uwekezaji inaoufanya katika uvumbuzi wa kidijitali nchini. NMB inazingatia maendeleo ya wafanyabiashara hao kutokana na mchango wao mkubwa katika ujenzi wa Taifa kwa kutengeneza ajira, kuchochea ukuaji wa uchumi na kuimarisha mapato ya wananchi.

Tuzo hizi na heshima iliyopata NMB ni ushahidi wa mwendelezo wa ubora wa huduma na dhamira ya dhati ya ubunifu wake.

Katika pongezi zake kwa washindi, Afisa Mtendaji Mkuu wa jukwaa la kufadhili ujasiriamali duniani (SME Finance Forum), Bw. Matthew Gamser, alisema ushindani wa mwaka huu ulikuwa mkubwa kutokana na washiriki kuwa wengi wakitoka katika nchi nyingi ikilinganishwa na miaka ya nyuma.

SME Finance Forum, inayoratibiwa na Shirika la Fedha la Kimataifa (IFC) la Benki ya Dunia, ilianzishwa mwaka 2012 na nchi 20 tajiri duniani (G20) chini ya mwamvuli wa Ushirikiano wa Kimataifa wa Ujumuishaji wa Kifedha (GPFI).

Majukumu yake makubwa ni pamoja na kusimamia wanachama wake kubadilishana maarifa, kuchochea ubunifu na kukuza ukuaji wa wajasiriamali.

Mkuu  wa Idara ya Biashara wa Benki ya NMB – Bw. Alex Mgeni (pili kulia)  akipokea tuzo ya Mwezeshaji Bora wa Kifedha kwa Biashara Ndogo na za Kati (SMEs) katika bara la Afrika kwa Mwaka 2023 kutoka kwa  Waziri  wa Muungano wa Biashara Ndogo na za Kati wa Serikali ya India - Bw. Narayan Rane, katika hafla ya tuzo za Kimataifa za Mitaji kwa Biashara Ndogo na za Kati (Global SME Awards) iliyofanyika Jijini Mumbai, India mwishoni mwa wiki. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la IFC Bw. Qamar Saleem na Kushoto ni Mkurugenzi wa Benki Kuu ya India - Bw. India Alok Kumar Choudhary.

Mkuu  wa Idara ya Biashara wa Benki ya NMB – Bw. Alex Mgeni ( katikati ) katika picha ya pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la IFC aliemaliza muda wake Bw. Matthew Gamser  pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la IFC Bw. Qamar Saleem, baada ya kupokea tuzo ya Mwezeshaji Bora wa Kifedha kwa Biashara Ndogo na za Kati (SMEs) katika bara la Afrika, kwa niaba ya Benki ya NMB.


Utafiti wa Mradi wa EFLOWS waonesha maji yanapungua kwenye mito

$
0
0

 

Na: Calvin Gwabara – Mbarali.

Matokeo ya Utafiti wa miaka miwili kuangalia Mtiririko wa maji na afya ya Mto Mbarali
Mkoani Mbeya yameonesha kuwa Maji yanapungua na hii ni kutokana na ongezeko la
watu na mahitaji ya matumizi ya maji kuongezeka sambamba na uharibifu wa vyanzo
vya maji vya mto huo.
Hayo yamebainishwa na Prof. Japhet Kashaigili kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha
Kilimo (SUA) ambaye ni Mtafiti Mkuu wa Mradi huo wa miaka miwili wa Utafiti wa
Usimamizi Endelevu wa Madakio ya Maji Kupitia Tathmini ya Kuimarisha Mtiririko wa
Maji kwa Mazingira na Utekelezaji wake katika Kulinda Ukanda wa Magharibi mwa
Bahari ya Hindi na Athari za Shughuli za Kibinadamu Tanzania (EFLOWS) wakati
akiwasilisha matokeo ya utafiti huo kwa wadau wa maji wa mto Mbarali wilayani
humo Mkoani Mbeya.

“Tulichokiona kwenye utafiti ni kwamba wingi wa maji kwenye mto unaendelea
kupungua, wahitaji wa maji wanaongezeka lakini pia mabadiliko ya tabia nchi nayo
yameathiri kwa kiasi kikubwa mtawanyiko wa maji na mvua kwenye maeneo haya na
hivyo kupelekea maji kupungua mtoni na athari zake hasi zikionekana kwenye mifumo
ikolojia ya mto hasa wakati wa kiangazi. Tumeona uwepo wa matumizi makubwa ya
maji bila vibali kwa kutumia pampu, na uzalishaji mkubwa wa mchanga wakati wa
mvua kutokana na shughuli za kibinadamu kwenye maeneo ya vyanzo milimani na
kwenye mashamba” alisema Prof. Kashaigili.

Aliongeza” Shughuli za kibinadamu zinazofanyika Mbarali kwa maana ya makazi,
kilimo, ufugaji, ufyatuaji wa matofali kwenye vyanzo vya maji na mtoni, kilimo cha
vinyungu, moto na shughuli zingine za kibinadamu zimechangia kwa kiasi kikubwa
mtawanyiko wa maji kwenye mto, lakini uchukuaji wa maji kwenye mto ndio
umeonekana kuongoza kwa athari hasi”.

Prof. Kashaigili amesema changamoto hiyo ya matumizi makubwa ya maji imepelekea
mto kukauka kabisa maeneo ya chini wakati maeneo ya juu ya mto na katikati ukifika
unakuta maji mengi yanatiririka ambayo hayafiki mwisho yanaishia njiani kutokana na
watu kuyachepusha na kuyachota kwaajili ya shughuli zao mbalimbali hususani kilimo
ambacho hakizingatii matumizi sahihi ya maji hayo.

“Kwa maana hii ni kwamba Mto Mbarali hauchangii chochote kwenye Mto Ruaha Mkuu
hasa wakati wa kiangazi kwenye maeneo ya uhifadhi na hii maana yake ikolojia ya
mto na uendelevu wake imeathirika na hivyo kushindwa kufikia malengo makubwa ya
Kidunia ya maendeleo endelevu na yale ya kitaifa ya kuifadhi na kuilinda baonuai ya
mto” alifafanua Mtafiti huyo Mkuu Prof. Kashaigili.

Mtafiti huyo aliyebobea kwenye tafiti za Masuala ya maji na Mazingira Duniani
amesema pamoja na Utafiti kutoa matokeo hayo kwa wadau hao muhimu pia
wameainisha njia na mikakati ya kufanya ambayo ikifanyika itasaidia kupunguza athari
zilizojitokeza na kusaidia kurejesha afya ya mto na mtiririko wa maji kwenye Mto
Mbarali na mingine nchini kwa kuwa changamoto zinafanana.

Amesema moja kati ya mikakati hiyo ilikuwa kurejesha uoto wa asili kwenye vyanzo
vyote vya maji vilivyoathirika na kingo za mito, ambapo mradi kwa kuanzia umesaidia
kuanzisha vitalu vikubwa viwili vya miti rafiki wa maji kwenye wilaya ya
Wanging’ombe Mkoani Njombe na Mbarali Mkoani Mbeya kwa kutumia elimu asili na
kufanikiwa kupanda miti zaidi ya elfu 45 kwenye vyanzo na kingo za mito pamoja na
kuanzisha ufugaji wa nyuki kwa ajili ya kuongezea kipato cha jumuiya za watumia
maji wanaosimamia madakio pamoja na kuongezea uhifadhi.

Kwa upande wake Mtaalamu wa Sayansi za maji na Viumbe wake kutoka Chuo Kikuu
Huria cha Tanzania Bw. Sherald Mkama ambaye alikuwa anaangalia afya ya mto na
usalama wa maji kupitia mradi huo amesema matokeo yameonesha maji
yanayotiririka kwenye mto huo bado ni salama kwa kuwa baada ya kufanya utafiti
wamekuta viumbe ambao hawawezi kuishi kwenye maji ambayo sio salama.

“Viumbe wadogo wanaoishi majini pamoja na samaki wanauwezo mkubwa wa kutoa
ishara ya ubora wa maji katika eneo na ndio maana pamoja na watafiti wengine
huchukua sampuli za maji na kuzipima, lakini mbinu ya kuangalia viumbe ndio
muhimu zaidi kwa kuwa ndio wanakaa kwa muda mrefu kwenye eneo hilo kuliko
kupima maji maana unaweza kwenda kuchota maji ukakuta wakati huo ni bora kwa
muda huo tu, ila viumbe waishio kwenye maji hawapiti wapo muda wote” alifafanua
Mkama.

Mtafiti huyo amezitaka mamlaka zinazosimamia maji kuhakikisha kunakuwepo na
usimamizi mzuri hasa kwenye maeneo wanayochota maji mengi kwenye skimu ya
Umwagiliaji ya Igomelo ambayo wanatumia viuatilifu na mwisho sehemu ya maji hayo
yanarudi mtoni yakiwa na viambata sumu kama hawatazingatia matumizi salama ya
viuatilifu, mwisho yaweza pelekea kuua viumbe walio mtoni na kuathiri pia jamii
inayotegemea maji ya mto huo kwa matumizi ya nyumbani.

Naye Mtafiti aliyekuwa anaangalia mimea iotayo kandokando ya mito na vyanzo vya
maji Dkt. Emmanuel Mwainunu kutoka Taasisi ya utafiti wa Misitu Tanzania (TAFORI)
amesema mimea hiyo ni muhimu kwa kuwa ndiyo inayosaidia kuwepo kwa uhai wa
mto kwa kutunza maji, kufyonza mbolea na kuyafanya yatiririke kidogokidogo badala
ya kasi pamoja na kuzuia mmomonyoko wa kingo za mito.

“Tunapoangalia hali ya Uoto kwenye mito na afya ya mto huwa tunatumia madaraja A
mpaka F, hivyo tunaposema hali ya ukanda fulani ni A maana yake hakuna uharibufu
katika eneo hilo, lakini ikiwa daraja B ina maana eneo limeanza kupata athari za
awali lakini hazijaanza kuleta madhara, na ikishuka kufikia daraja D ina maana athari
ni kubwa sana na ikifikia daraja F ina maana eneo hilo limeharibika sana, athari ni
kubwa sana na madhara yake ni makubwa sana ambapo si rahisi kurekebishika katika
hali ya kawaida. Tathmini yetu imeonesha kuwa yapo mabadiliko kadhaa ambayo
yametokana na shughuli za kilimo na ufugaji lakini kimsingi uharibifu wake kwenye
uoto wa kandokando za mto sio mkubwa sana na kupelekea kupata daraja B, hata
hivyo ni lazima jitihada zifanyike kusitisha changamoto hii kuendelea” alieleza Dkt.
Immanuel.

Amesema kuwa wamekuta mimea kama vile Msandali ambayo ni mimea yenye
matumizi mengi kama utengenezaji wa Manukato pamoja na mimea mingine rafiki wa

maji lakini inawezekana kutoweka kwa kuwa jamii zinafanya shughuli mbalimbali
kandokando ya mto huo na kuiathiri, hivyo jitihada za makusudi zichukuliwe na
mamlaka za usimamizi wa mito kunusuru mto kuachwa wazi.

Mradi huu wa Utafiti unatekelezwa na Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kwa
kushirikiana na Baraza la Taifa la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) na
kutekelezwa katika Bonde la mto Rufiji ndani ya dakio la mto Mbarali kwa ushirikiano
na Bodi ya Maji ya mto Rufiji, jumuiya za watumia maji, Wakala wa Huduma za Misitu
(TFS), Wilaya ya Mbarali na Wanging`ombe na jamii, kwa ufadhili wa program ya

Mazingira ya Umoja wa Mataifa, UNEP, kupitia michango ya nchi kumi wanachama wa
Azimio la Nairobi ambapo kwa Tanzania ni kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira,
katika kutekeleza Mpango Mkakati wa Kivitendo wa Magharibi mwa Bahari ya Hindi
chini ya uratibu wa Sekretarieti ya Azimio la Nairobi.
Mtaalamu wa Sayansi za maji na Viumbe wake kutoka Chuo Kikuu Huria cha Tanzania Bw. Sherald Mkama akizungumzia matokeo hayo mbee ya Waandishi wa habari nje ya mkutano huo.
Mtafiti aliyekuwa anaangalia mimea iotayo kandokando ya mito na vyanzo vya maji Dkt. Emmanuel Mwainunu kutoka Taasisi ya utafiti wa Misitu Tanzania (TAFORI) akizungumzia eneo la utafiti wake.
Mtafiti Mkuu wa Mradi wa EFLOWS Prof. Japhet Kashaigili kutoka SUA akiwasilisha matokeo ya mradi huo wa utafiti wa miaka miwili mbele ya wadau.



Utafiti wa afya na mtiririko wa maji ya Mto mbarali utasaidia Viongozi kufanya maamuzi sahihi.

$
0
0

 

Na Calvi Gwabara – Mbarali.

Serikali Wilayani Mbarali imekipongeza Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA)
pamoja na Baraza la Taifa la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kwa
jitihada zao za kusaidia kurejesha uoto wa asili kwenye vyanzo vya maji pamoja na
kufanya utafiti na kutoa matokeo ambayo yataisaidia Serikali kufanya maamuzi
sahihi.
 Hayo yameelezwa na Mkuu wa Wilaya ya Mbarali Mhe. Kanali Denis Mwila wakati
akifungua warsha ya kutoa matokeo ya utafiti wa Mradi wa usimamizi endelevu
wa madakio ya maji kupitia tathimini ya kuimarisha mtiririko wa maji kwa
mazingira na utekelezaji wake katika kulinda Ukanda wa Magharibi mwa Bahari ya
Hindi na athari za shughuri za kibinadamu Tanzania (EFLOWS) iliyofanyika
Wilayani humo Mkoani Mbeya.

“Kuna athari kubwa ya kiusalama ambayo inaonekana kuja kwa juu kwa sasa ya
uharibifu wa mazingira lakini ukiangalia kwa makini na kwa mujibu wa vitabu
kadhaa nilivyosoma inaonekana vita ya tatu ya dunia itakuwa ni vita ya maji na hii
imeanza kudhihirika kwenye maeneo mbalimbali na mfano mzuri ni eneo la mto
Nile na hata ninapopita kwenye wilaya yangu kuongea na Wananchi swala la maji
ndio kilio kikubwa” alieleza Mhe. Kanali Mwela.

Amesema matokeo hayo mazuri ya kina na kisayansi ya utafiti ya Mradi wa
EFLOWS watayapitia vizuri na kuyatumia katika kutekeleza mipango mbalimbali ya
uhifadhi kupitia mapendekezo yaliyotolewa ili kusaidia kuhifadhi vyanzo vya maji
na mazingira kwa manufaa mapana na Taifa kwa kuwa vyanzo vya maji vilivyo
nyanda za juu kusini ndivyo vinavyotegemewa kutiririsha maji yake kwenye mto
Ruaha mkuu na hatimae Bwawa la Kidatu na Mwl. Nyerere.

Amesema kuwa kumekuwa na uelewa kidogo wa jamii na baadhi ya viongozi
katika masuala ya uhifadhi wa mazingira na vyanzo vya maji ndio maana Serikali
inapochukua hatua za kuzuia shughuli fulani za kibinadamu kwenye maeneo
muhimu ya vyanzo vya maji na hifadhi huzuka malalamiko mengi ambayo chanzo
chake kikubwa ni ubinafsi wa watu wachache usiojali maslahi ya watu wengi na
Taifa.

“Nyanda za juu wasipotunza vyanzo vya maji na kufuata sheria za uhifadhi wa
mazingira Mradi mkubwa wa kufua umeme wa Bwawa la Mwl Nyerere
hautafanya kazi na hivyo kusababisha nchi kukosa umeme wa kutosha kuendesha
Viwanda, Treni ya Mwendokasi (SGR) na shughuli zingine za jamii zitakwama
maana nishati hii ni muhimu kwa kila mtu” alieleza Kanali Mwela.

Mhe. Kanali Mwela amepongeza kazi hiyo kubwa ya utafiti iliyofanywa na SUA
kwa kushirikiana na NEMC katika kufanya tathimini ya mtiririko wa maji kwenye
mto Mbarali ambao unachangia maji yake kwenye Mto Ruaha mkuu na hatimae
kuelekea Bwawa la Mwl. Nyerere na kwamba matokeo hayo yanasaidia kuonesha
vizuri hali halisi ya vyanzo vya maji na mtiririko wake na nini kifanyike.

Kwa upande wake Mtafiti Mkuu wa Mradi wa EFLOWS kutoka (SUA) Prof. Japhet
Kashaigili amesema katika kipindi cha miaka miwili ya utafiti huo tathimini ya kina
imefanyika kuangalia hali ya vyanzo vya maji vya mto Mbarali, Afya ya Mto,
Maumbile ya mto na uoto wake kupitia wataalamu waliobobea nchini kwenye
nyanja hizo kutoka taasisi mbalimbali nchini na wananchi wa maeneo hayo
hususani Jumuiya za watumia maji.

“Wakati tunakuja kutambulisha mradi tuliitana wadau wote wa maji wa mto
Mbarali na tukawaeleza malengo ya ujio wetu wa utafiti huu na wengi wenu
mlishiriki pia wakati wa utafiti wenyewe katika kipindi chote na baada ya
kukamilisha kuchakata matokeo ya yale tuliyoyaona kisayansi sasa tumeona ni
vyema kurudi tena kwenu kuwapatia mrejesho ili kwa pamoja tujue tunawezaje
kutumia matokeo hayo kwa pamoja kusaidia kulinda vyanzo vya mito yetu na
mazingira kwa faida ya Taifa” alieleza Prof. Kashaigili.

Aliongeza kuwa“ lengo la pili ni kujadili hatua za kuchukua ili kufikia malengo ya
usimamizi na mpango wa utekelezaji na kuainisha wadau, majukumu, mpango na
ushirikiano ili sote kwa pamoja tukubaliane cha kufanya na kushiriki kikamilifu
maana tunategemeana na tunakwenda na usemi uleule kuwa ukitaka kufika mbali
nenda na wenzako ila ukitaka kwenda haraka nenda peke yako na sisi lengo ni
kufika mbali hivyo lazima twende pamoja”.

Prof. Kashaigili amesema takwimu na sampuli zilikusanywa kwenye maeneo
manne waliyoyateua kupitia vigezo mbalimbali na zoezi hilo lilifanyika wakati wa
kiangazi wakati kina cha maji mtoni kiko chini na wakati wa masika kipindi mto
umejaa maji kuanzia mwanzo mwa mto katika eneo la Wilaya ya Wanging’ombe
na Mbarali ambako unaishia na kumwaga maji yake kwenye mto Ruaha mkuu.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Tafiti za Mazingira kutoka (NEMC) Dkt. Menan
Jangu amesema Baraza linajukumu kubwa la kuhakikisha miradi mikubwa
inayoanzishwa inafikia malengo kwa kupata mahitaji yanayohitajika kwa kupitia
utunzaji wa mzingira na vyanzo vya maji.

Amesema ni wazi kuwa Mazingira, Ikolojia, bioanuai na huduma zinazopatikana
zinaendelea kupata changamoto kubwa kutokana na ongezeko la watu, ongezeko
la mahitaji na kwamba changamoto hizo zisipopatiwa ufumbuzi rasiliamali nyingi
zinaweza kutoweka hususani mtiririko wa maji ambao ni uhai wa Wanyamapori,
Binadamu na Miradi mikubwa ya uzalishaji wa nishati nchini.

“Utekelezaji wa utafiti huu ni moja ya malengo ya NEMC katika kuhakikisha
kunakuwepo na tafiti nzuri na za kina ambazo zinafanywa nchini katika eneo la
mazingira ili kupata matokeo na suluhu za kisayansi ambazo zitasaidia kuhifadhi
mazingira na vyanzo vya maji pamoja na mbinu za kurejesha uhalisia kwenye
meneo ambayo yameathiriwa na shughuli za kibinadamu au majanga ya asili”
alieleza Dkt. Jangu.

Mkurugenzi wa Tafiti za Mazingira amesema matokeo ya utafiti huo yanatoa
muelekeo wa hali ilivyo na kujua kama ni bado ni muelekeo sahihi au kuna
maeneo ya kufanyiwa kazi na ndio maana kwenye eneo la utafiti NEMC inafanya
kazi na wadau pamoja na taasisi zingine kama ilivyo kwenye mradi huu kati ya
SUA, NEMC na wadau wengine.

Mradi huu wa Utafiti unatekelezwa na Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA)
kwa kushirikiana na Baraza la Taifa la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC)
na kutekelezwa katika bonde la mto Rufiji ndani ya dakio la mto Mbarali kwa
ushirikiano na Bodi ya Maji ya mto Rufiji, jumuiya za watumia maji, Wakala wa
Huduma za Misitu (TFS), Wilaya ya Mbarali na Wanging`ombe na jamii, kwa
ufadhili wa program ya Mazingira ya Umoja wa Mataifa, UNEP, kupitia michango
ya nchi kumi wanachama wa Azimio la Nairobi ambapo kwa Tanzania ni kupitia
Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira, katika kutekeleza Mpango Mkakati wa
Kivitendo wa Magharibi mwa Bahari ya Hindi chini ya uratibu wa Sekretarieti ya
Azimio la Nairobi.
Dkt. Winfred Mbungu akitoa matokeo ya tathimini ya maji kwa mazingira na mtiririko wake kwenye mto Mbarali


Mbarali Disctrict Commissioner ,Hon.Col. Denis Mwila speking during the opening of the Workishop.
Mkurugenzi wa Tafiti za Mazingira kutoka (NEMC) Dkt. Menan Jangu akitoa salamu za NEMC.
Mtafiti Mkuu wa Mradi wa EFLOWS kutoka (SUA) Prof. Japhet Kashaigili akieleza malengo ya warsha hiyo.
Picha ya pamoja baadhi washiriki wa mkutano huo.

Ecobank Tanzania yashiriki kwenye upandaji wa miti ili kuhifadhi Bonde la Mto Mara

$
0
0


Ecobank Tanzania imeshiriki pamoja na taasisi na mashirika ya Serikali na binfsi kutoka katika nchi za Kenya na Tanzania ambapo kwa mwaka huu katika  Maadhimisho ya 12 ya Mara yaliyokuwa na kauli mbiu isemayo "Hifadhi Mto Mara kwa Ustawi wa Viumbe Hai na Uchumi Endelevu."

Akizungumza wakati wa maadhimisho hayo Naibu Waziri wa Maji, Maryprisca Mahundi amesema Uhifadhi wa bonde la Mto Mara ni wa lazima na kuwataka wadau wote kushirikiana katika kuihifadhi na kulinda rasilimali hiyo muhimu.

Akihitimisha maadhimisho ya siku ya Mara mjini Mugumu wilayani Serengeti, Septemba 15,2023; Mahundi amesema bonde la Mto Mara linakabiliwa na changamoto nyingi ambazo zinatishia uhai na uendelevu wake.

"Uchafuzi wa mazingira unaotokana na shughuli za kibinadamu kama vile ukataji na uchomaji miti, uchimbaji madini kwenye vyanzo vya maji, kilimo kisichozingatia sheria hizi ni baadhi ya changamoto ambazo zinakabili Mto Mara kwa upande wa Kenya na Tanzania," amesema

Amesema kutokana na kuwepo kwa changamoto hizo suala la usimamizi madhubuti wa mazimgira ya bonde la mto huo kwa ujumla unahitajika na kwamba ni jukumu la kila mdau kuhakikisha bonde hilo linakuwa salama muda wote.

 Naye Mkuu wa kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Ecobank Tanzania  Furaha Samalu amesema  benki hiyo imeamua kujikita kwenye utunzaji wa mazingira kwani Bonde la Mto Mara linawanufaisha mabilioni ya watu katika nchi zetu hizi kwenye sekta za biashara, kilimo na utalii hivyo sote kwa umoja wetu kuanzia ngazi ya jamii hadi taifani tuna wajibu wa kutunza mazingira yake,

Pia amesema Ecobank Tanzania wameshiriki maadhimisho hayo miaka 12 ili kuweza kueleza huduma wanazozitoa kwa wadau mbalimbali ili benki hiyo iweze kujipanua na kuendelea kusaidia katika suala zima la utunzaji wa mazingira ya bonde hilo.

Ecobank Tanzania imeweza kutoa elimu kwa jamii ikiwemo mashuleni hasa kwenye shule za Sekondari na msingi za Mugumu na Halmashauri ya Serengeti ili kujenga uelewa wa utunzaji na kuhifadhi mazingira ikienda sambamba na kujua huduma zinazotolewa na banki hiyo.
Naibu Waziri wa Maji, Maryprisca Mahundi(kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Ecobank Tanzania  Furaha Samalu(kulia) kuhusu na mna walivyojikita katika kutunza mazingira pamoja na kazi zinazofanywa na benki hiyo wakati wa maadhimisho ya siku ya Mara yaliyokuwa na kauli mbiu isemayo "Hifadhi Mto Mara kwa Ustawi wa Viumbe Hai na Uchumi Endelevu."
Naibu Waziri wa Maji, Maryprisca Mahundi akiwa kwenye picha ya pamoja na wadau kutoka taasisi na mashirika ya Serikali na binfsi kutoka katika nchi za Kenya na Tanzania ambapo kwa mwaka huu katika  Maadhimisho ya 12 ya Mara yaliyokuwa na kauli mbiu isemayo "Hifadhi Mto Mara kwa Ustawi wa Viumbe Hai na Uchumi Endelevu."
Mkuu wa kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Ecobank Tanzania  Furaha Samalu(kulia) akipanda mti wakati wa Maadhimisho ya 12 ya Mara yaliyokuwa na kauli mbiu isemayo "Hifadhi Mto Mara kwa Ustawi wa Viumbe Hai na Uchumi Endelevu."

Viewing all 39112 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>