Quantcast
Channel: MTAA KWA MTAA BLOG
Viewing all 39098 articles
Browse latest View live

WAZIRI MHAGAMA ATEMBELEA IDARA YA MPIGA CHAPA MKUU WA SERIKALI

$
0
0

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista J. Mhagama.(kulia) akimsikiliza Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali Bw.George Lugome wakati akielezea kuhusu kazi ya mtambo wa kukata karatasi mara baada ya kufanya ziara kutembelea Idara ya Mpiga Chapa wa Serikali leo Septemba 14,2023 Jijini Dar es Salaam.Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista J. Mhagama.(kulia) akimsikiliza Mpiga Chapa Msaidizi Mkuu Bw.Ophin Malley mara baada ya kufanya ziara kutembelea Idara ya Mpiga Chapa wa Serikali leo Septemba 14,2023 Jijini Dar es Salaam.Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista J. Mhagama akiwa pamoja na Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali Bw.George Lugome akichukua maelezo kuhusu Mashine ya kuprint maandishi kutoka kwenye kompyuta kwenda kwenye bati (CTP) mara baada ya kufanya ziara kutembelea Idara ya Mpiga Chapa wa Serikali leo Septemba 14,2023 Jijini Dar es Salaam.Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista J. Mhagama akioneshwa nyaraka iliyochapwa na moja ya mashine katika kiwanda mara baada ya kufanya ziara kutembelea Idara ya Mpiga Chapa wa Serikali leo Septemba 14,2023 Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista J. Mhagama akitazama nyaraka za Serikali zilizochapwa na moja ya mashine katika kiwanda mara baada ya kufanya ziara kutembelea Idara ya Mpiga Chapa wa Serikali leo Septemba 14,2023 Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista J. Mhagama akitazama nyaraka za Serikali zilizochapwa na moja ya mashine katika kiwanda mara baada ya kufanya ziara kutembelea Idara ya Mpiga Chapa wa Serikali leo Septemba 14,2023 Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista J. Mhagama akimsikiliza Fundi wa Mashine za utengenezaji wa mihuri Bw.Mohammed Ally mara baada ya kufanya ziara kutembelea Idara ya Mpiga Chapa wa Serikali leo Septemba 14,2023 Jijini Dar es Salaam.

Mpiga Chapa Msaidizi Bw.Mosses Sampa akimuonesha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista J. Mhagama gazeti la Serikali la Kwanza kuchapishwa mwaka 1961 mara baada ya kufanya ziara kutembelea Idara ya Mpiga Chapa wa Serikali leo Septemba 14,2023 Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista J. Mhagama akitazama baadhi ya vitabu katika maktaba ya Idara ya Mpiga Chapa wa Serikali mara baada ya kufanya ziara kutembelea Idara ya Mpiga Chapa wa Serikali leo Septemba 14,2023 Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista J. Mhagama (kulia) akizungumza na Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali Bw.George Lugome kwenye maktaba ya Idara ya Mpiga Chapa wa Serikali mara baada ya kufanya ziara kutembelea Idara ya Mpiga Chapa wa Serikali leo Septemba 14,2023 Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista J. Mhagama (kulia) akimsikiliza Mpiga Chapa Msaidizi Bw.Pater Kikuli mara baada ya kufanya ziara kutembelea Idara ya Mpiga Chapa wa Serikali leo Septemba 14,2023 Jijini Dar es Salaam.


(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)


Ramani: Revolutionizing the FMCG Sector in Tanzania

$
0
0

 

 By Our Reporter

Dar es Salaam. Financial technology start-up Ramani has attained remarkable success after disbursing over $100 million (Sh250.5 billion) in loans to micro-distribution centers.

Speaking on behalf of , Ramani’s CEO, Mr. Iain Usiri, said that success has been attained in the two and a half years to July this year and that he hopes to increase efficiency by providing services in modern ways with a high level of professionalism.

 "What we have done is build software that micro-distribution centres can use to manage their operations. This means a distributor can keep track of where their salespeople are going, who they are selling to, how much they are selling, how much inventory you still have in your warehouse, and much more. The app then helps you track all that data in real time," said Usiri.

 He said the tremendous growth is a testament to the operational excellence of Ramani's model, fulfilling a significant demand in the market for both technological solutions and flexible financing.

 "With the strong backing of Y-Combinator and a foothold in the Tanzanian market, Ramani's future looks promising. The impact of Ramani extends beyond the confines of the fast-moving consumer goods (FMCG) sector. It offers a blueprint for how thoughtful technology integration and inventive financing can dismantle traditional barriers to growth and unlock potential across various industries," he said.

 He said as they continue to expand and refine their offerings, they promise to remain at the forefront of the digital revolution, catalyzing a new era of growth and opportunity for Tanzanian entrepreneurs and beyond.

 "In a world where technology is increasingly becoming the great equalizer, Ramani stands out as a beacon of innovation, proving that with the right tools and vision, even the most traditional markets can be transformed. Our success serves as an inspiring example of how technological innovation can drive economic growth and empower local businesses in emerging markets," he said.

 He explained that in the bustling markets of Tanzania, a technological revolution is taking shape, transforming the way FMCG resellers operate.

 "Ramani, a Y-Combinator-backed start-up and Series A, is leading this charge with a unique blend of software solutions and inventory financing that is rapidly reshaping the FMCG landscape."

 Founded with the aim of automating and digitizing the fragmented operations of the FMCG sector, Ramani provides resellers with proprietary financial technology software to streamline their operations. Their integrated platform covers every aspect of the business, from procurement to warehousing and point-of-sale (POS) services, ensuring a smooth and efficient workflow.

This innovative solution offers an unprecedented level of control and visibility into the day-to-day activities of resellers, allowing them to make informed decisions and optimize their strategies.

 "One of Ramani’s standout features is the provision of inventory financing. By financing inventory purchases on behalf of resellers, Ramani enables businesses to bypass traditional financial barriers and focus on what they do best: sales and growth," he said.

 Resellers are able to purchase unlimited inventory through Ramani's inventory financing system, a feature that liberates them from the financial constraints that typically hamper growth in the industry. This fresh approach to funding has led to a seismic shift in market dynamics, enabling small and medium-sized businesses to compete on an even playing field with larger corporations.






MKURUGENZI TET ASHIRIKI MKUTANO WA KIMATAIFA WA ELIMU NA MAENDELEO NCHINI UINGEREZA

$
0
0
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania Dkt. Aneth Komba ameshiriki katika Mkutano wa Kimataifa wa Elimu na Maendeleo unaofanyika nchini Uingereza kuanzia tarehe 12 - 14 Septemba, 2023.

Mkutano huu unajulikana kama UKFIET International Conference on Education and Development.

Katika Mkutano huo Dkt. Komba ameshirikiana na Bi. Joan Minja kuwasilisha juu ya utekelezaji wa Mradi wa Lipa Kulingana na Matokeo katika maeneo ya msawazo wa walimu na usambazaji wa vitabu vya Kiada na vifaa vingine vya kufundishia na kujifunzia.

Aidha, mkutano huo umehudhuriwa pia na Dkt. Charles Msonde Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI, Bwana .Kayode Sanni Kiongozi wa Timu Mradi wa Shule Bora na Bwana.Benjamini Oganga,Kiongozi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Elimu(System Strengthening Lead)











TBS KANDA YA MASHARIKI YATOA ELIMU YA VIWANGO

$
0
0
Wajasiriamali nchini wahimizwa kuzalisha bidhaa zenye ubora ili kuweza kuhimili ushindani katika soko la ndani na kimataifa.

Haya yamesemwa na Bw. Issa Dadi, Afisa Udhibiti Ubora (TBS Kanda ya Mashariki) wakati akiwatembelea washishiriki wa maonesho ya Wajasiriamali mkoa wa Dar es Salaam yaliyoandaliwa na iMBEJU CRDB ya yaliyofanyika viwanja vya mnazi mmoja.

Bw. Issa alitumia fursa hii kutoa elimu kuhusu masuala ya viwango, namna bora ya uzalishaji wa bidhaa kwa ukizingatia namna bora ya usafi lengo likiwa ni kuzalisha bidhaa bora na salama kwa watumiaji wa mwisho.

Pia alipata nafasi za kuwaeleza namna wanavyoweza kupata alama ya ubora kwa kutumia huduma ya uthibishaji ubora wa bidhaa bila gharama yoyote kwa wajasiriamali kwani serikali kila mwaka hutengenga fedha ili wajasiriamali wadogo na wa kati wathibitishe ubora wa bidhaa zao ili waweze kufikia makoso makubwa ndani na nje ya nchi.

Kwa upande wake Afisa Masoko (TBS), Bi. Rhoda Mayugu amesema, TBS ilitumia maonesho hayo kuwaelimisha wananchi kuhusu faida na umuhimu wa kununua bidhaa zilizothibitishwa ubora wake pamoja na umuhimu wa kuangalia muda wa watumizi wa bidhaa husika kabla ya kununua bidhaa hizo kwani kwa kufanya hivyo hulinda usalama wa afya zao, na kuepuka hasara za kiuchumi zinazoweza kujitokeza

TBS inawaasa wananchi kutokununua bidhaa hafifu na kutoa taarifa wanapokutana na bidhaa hafifu ama zile zilizozuiliwa kutumika ni hakika Tanzania haitokuwa na bidhaa hafifu na haitokuwa jalala la bidhaa hafifu.






SERIKALI INASISITIZA DHAMIRA YAKE YA KUFANYA TANZANIA KUWA ENEO KUU LA UWEKEZAJI

$
0
0

 

SERIKALI imeendelea kusisitiza dhamira yake ya kuendelea kupitia upya sera na mfumo wa udhibiti unaoongoza mazingira ya biashara nchini, katika jitihada zake za kufanya Tanzania kuwa eneo kuu la uwekezaji wa ndani na nje ya nchi.

Akizungumza leo katika kikao na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Serengeti Breweries Limited (SBL), Obinna Anyalebechi, Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk. Ashatu Kijaji, pia alisema serikali iko tayari kufanya mazungumzo na sekta binafsi kama njia ya kutatua changamoto zinazokabili wafanyabiashara.

"Sekta binafsi ni mdau muhimu katika ujenzi wa taifa. Tunathamini jukumu la sekta hii katika maendeleo ya kiuchumi ya nchi, mchango wake katika kutengeneza ajira, ukusanyaji wa mapato ya serikali, na misaada kwa jamii," Dk. Kijaji alisema.

Katika ziara ya heshima iliyofanyika Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa SBL alimshukuru Waziri kwa msaada wake kwa sekta binafsi, jambo ambalo alisema limeongeza hamu na ujasiri wa wawekezaji nchini Tanzania.

Kama matokeo, Obinna alisema SBL imewekeza zaidi ya TZS bilioni 165 katika miaka mitatu iliyopita kwa lengo la kuongeza uzalishaji wa bia na vileo, jambo ambalo limeleta ajira mpya na kuongeza fursa kwa wazalishaji wa ndani kwa kampuni hiyo.

"Upanuzi huu umesababisha kuongezeka kwa uzalishaji na kwa hiyo kuongeza ukusanyaji wa mapato kwa serikali kutoka kwa biashara yetu wakati unaimarisha uwezo wa kampuni kufadhili programu za kusaidia jamii zaidi," alisema Mkurugenzi Mtendaji huyo.

Programu za kusaidia jamii za SBL, kulingana na Obinna, zinajumuisha utunzaji wa maji, upandaji wa miti, na mafunzo ya stadi za maisha kwa vijana, wanawake, na makundi yanayotengwa. Kampuni hiyo pia inaendesha programu ya kilimo inayosaidia zaidi ya wakulima wa ndani 400 wanaolima shayiri, mahindi, mtama, na nafaka nyingine ambazo kampuni inanunua na kutumia kama malighafi kwa uzalishaji wa bia.

KAMATI YA BUNGE YA KUDUMU YA AFYA NA MASUALA YA UKIMWI YATEMBELEA NIMR, YAACHA MAAGIZO

$
0
0

 Mkurugenzi Mkuu wa NIMR, Profesa Said Aboud wa akimkabidhi zawadi Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Afya na Masuala ya Ukimwi Stansalus Nyongo wakati wa ziara ya wabunge hao katika Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa magonjwa ya Binadamu (NIMR) anayeshudia hi Kaimu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Faustine Ndungulile. Ziara hiyo imefanyika  leo Septemba 14, Mabibo jijini Dar es Salaam.


Mkurugenzi Mkuu wa NIMR, Profesa Said Aboud aliyesimama  akizungumza na wabunge pamoja na wadau mbali mbali wa afya wakati wa ziara ya wabunge hao katika Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa magonjwa ya Binadamu (NIMR) iliyofanyika leo Septemba 14, Mabibo jijini Dar es Salaam



Mkurugenzi Mkuu wa NIMR, Profesa Said Aboud akizungumza na wabunge pamoja na wadau mbali mbali wa afya wakati wa ziara ya wabunge hao katika Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa magonjwa ya Binadamu (NIMR) iliyofanyika leo Septemba 14, Mabibo jijini Dar es Salaam
Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya Ukimwi,  Stanslaus Nyongo (katikati)  akizungumza na wabunge pamoja na wadau mbali mbali wa afya wakati wa ziara ya wabunge hao katika Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa magonjwa ya Binadamu (NIMR) iliyofanyika leo Septemba 14, Mabibo jijini Dar es Salaam.

Na Karama Kenyunko, Michuzi TV
KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Afya na masuala ya Ukimwi, imeelekeza Wizara ya Afya na Baraza la Tiba za asili kuhakikisha wanaweka mkazo katika sheria ya tiba asili ili mtu anayeuza dawa hizo ziwe na ubora na usalama kwa mtumiaji.

Akizungumza Leo Dar es Salaam katika Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) Mwenyekiti wa kamati hiyo, Stanslaus Nyongo amesema lengo la ziara hiyo ni kutembelea kitengo cha utafiti wa tiba asili kwani Tanzania ina miti mingi na serikali ina jukumu la kuhakikisha tiba asili inachukua nafasi yake.

Amesema kuwa kwa kiasi kikubwa wameridhishwa na juhudi zinazofanywa na serikali katika kuona usalama wa dawa za asili ili Watanzania watumie wakiwa na uhakika kuwa dawa hizo ni salama.

"Ni muhimu kujua usalama wa dawa za asili ili kuepusha Watanzania kununua dawa bila kujua kama dawa husika ni salama na haina viambata vya sumu na wakati mwingine zipo feki na huharibu figo na viungo vingine vya mwili," amesema Nyongo.

Ameeleza kuwa ni muhimu kufanyika utafiti kwa dawa za asili ili kujua usalama wake na matumizi salama ya dawa hizo.

"Hapa kuna kama kiwanda ambacho serikali hukusanya dawa kutoka maeneo mbalimbali na kuna wadau mmoja mmoja ambao huleta dawa zao ili kufanyiwa utafiti hivyo pia inawezesha uzalishaji wa dawa za asili kwa ajili ya matumizi salama ya binadamu," amesema.

Amefafanua kuwa jukumu lao ni kuishauri serikali hususan kutenga bajeti kuhakikisha juhudi hizo zinafanikiwa na mipango iliyopangwa inatekelezeka.

Pia amesema baraza la tiba asilia linapaswa kuhakikisha dawa zote zinazotumika zimekidhi vigezo ili kuondoa watu wasio na wanaouza dawa mtaani kwa kile wanachodai hutibu magonjwa mbalimbali.

"Tumeambiwa na wataalamu wapo watu ambao wanauza dawa za asili ambazo wanadai zinatibu nguvu za kiume kumbe ndani yake zimewekwa Viagra hivyo mtu akitumia vibaya zinaweza kumsababishia madhara,"

Nyongo amesema: "Tunataka kama dawa ya asili inayouzwa inatibu ugonjwa fulani kama vile ugonjwa wa moyo, sukari na nguvu za kiume basi iwe kweli na chombo hiki ndio kinatakiwa kuhakikisha ubora huo kabla ya kusajili dawa," ameongeza.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa NIMR, Profesa Said Aboud amesema wana jukumu lakufanya utafiti kuangalia usalama, usahihi na ubora wa dawa zote ikiwemo za asili.

Amesema suala la utafiti kuchukua muda mrefu ni jambo la kawaida kutegemea na aina ya utafiti unaofanyika kwani kama unahusu magonjwa ya binadamu ni lazima wapitie hatua mbalimbali ili kupata matokeo na ni hatari kuharakisha.

Kuhusu tozo, Profesa Aboud amesema wanapata fedha kutoka serikalini kwa ajili ya utafiti na kutokana na maelekezo yaliyotolewa wataangalia namna bora ya kutoza watu ada wanaotaka kufanyiwa tafiti zao.

Amesema baraza la tiba asili kuna ada ambayo inawatoza watu wenye kliniki za tiba asili na wanaotoa tiba asili wakitaka kusajiliwa.

Amesema kuwa waganga wa tiba asili kupitia vyama vyao 28, wanahamasishwa kushirikisha NIMR kufanya tafiti kwenye dawa zao za tiba asili wanazogundua na kwamba hakuna watu watakaowanyang'anya.

Amesema lengo la kufanya utafiti ni kuangalia ubora, ufanisi na usalama wa dawa hizo ili mtumiaji asipate madhara pale ambapo ataitumia.

"Tunaendelea kuhamasisha wadau wa tiba asili kuona umuhimu wa kuleta dawa wanazogundua ili tuzifanyie utafiti na mwisho wa siku tuone ubora na usalama wao," amesema.

Kuhusu utafiti wa Ukimwi, Mkurugenzi huyo amesema Kituo cha NIMR Mbeya inashiriki katika utafiti unaohusisha nchi tatu za Afrika kupitia taasisi nne.

Amesema katika utafiti huo, unajumuisha utolewaji wa chanjo na dawa kinga na kwamba utafiti huo ni wa awamu ya pili.

"Utafiti huu unashirikisha washiriki waliokwenye hatari ya kupata maambukizi ya Ukimwi hivyo tunaangalia kama chanjo na dawa kinga hizi zitaweza kumkinga kupata maambukizi mapya. Utafiti huu ulianza mwaka 2018 na unatagemea kuhitimishwa Juni 2024 na watatoa matokeo," amesisitiza Profesa Aboud.

MERIDIANBET YAZINDUA DUKA LA KUBETIA MBAGALA RANGI 3

$
0
0

 


KAMPUNI kubwa ya kubashiri nchini Tanzania, Meridianbet wamzindua duka linguine jipya la kubetia maeneo ya Mbagala Rangi 3 ambalo ni Max 99 huku nia na madhumuni ilikiwa ni ile ile kuwafikia wateja wao kwa ukaribu zaidi wale ambao hupenda kubeti madukani.

Uzinduzi wa duka hilo ni mwanzo wa endelezo la ufunguzi wa maduka mengine kibao ambao utafanywa na Meridianbet huku wakikusudia kulete mashine nyingi za sloti ambazo watu watazitumia wakati wa kucheza michezo mbalimbali ikiwemo Poker, Aviator na mingine kibao.

Uzinduzi wa duka hilo huko Mbagala liliongozwa na Mhariri mkuu wa Meridiabet Nancy Ingram ambaye alifika eneo la tukio na timu yake nzima na kuanza rasmi kuzindua duka hilo. Pia ujio wao ulipokelewa vizuri na wakazi wa eneo hilo wakifurahia duka hilo mwanzo wa msimu huu wa ligi mbalimbali Duniani.

"Kwenye duka hili ukiachana na kubeti mpira na kucheza keno, lakini pia wateja wetu watapata faida ya kucheza michezo ya sloti safi huhitaji kwenda kasino kila kitu unamalizia humu humu." Nancy Ingram.

NB: Bado Jakpoti inaendelea ndani ya Meridianbet ambapo kwa dau la shilingi 1000/= unaweza kubashiri mechi zako 13 na ukajipigia mkwanja wa shilingi 85,000,000. Ingia Meridianbet na ucheze sasa.

Duka ambalo limezinduliwa Mbagala Rangi 3 ni moja ya maduka ambayo ni makubwa ambayo kila ambacho utataka kitakuwepo, vilevile unaweza ukabashiri mubashara yani mechi zikiwa zinaendelea wewe weka dau lako suka jamvi na sikilizia maokoto baadae. Pia kuna michezo mingi sana kama Keno, Sloti mashine kama American Poker n.k tembelea tovuti ya meridianbet kubashiri michezo mingi www.meridianbet.co.tz

Wakazi wa Mbagala wamefurahia sana kuletewa mchezo wa “kindege” ambao unajulikana kama Aviator ambao umekuwa pendwa sana kwenye michezo ya kasino ya mtandaoni kutokana na kuwa rahisi kueleweka.

Meridianbet, Msimu Mpya Mzigo wa Kutosha
Odds kubwa kasino ya mtandaoni na michezo ya sloti ni vitu vinavyoweza kubadilisha maisha yako kwa kukupatia pesa nyingi. Ingia mchezoni hapa.

Endelea kutumia kampuni yako pendwa ya Meridianbet kufanya ubashiri wa mechi mbalimbali ambapo baada ya mapumziko ya kimataifa wiki hii ligi mbalimbali zinarejea pale EPL mitanange ipo kibao. LALIGA napo hapatoshi, yaani ukisogea ple BUNDESLIGA ndio hatari, kunako LIGUE 1 noma sana halafu malizia pale SERIE A.

TGNP YATOA MAFUNZO KWA WAJUMBE WA KAMATI ZA SERIKALI ZA MTAA

$
0
0
MTANDAO wa Kijinsia Tanzania TGNP imeendesha Mafunzo kwa Wajumbe wa Kamati za Serikali za Mitaa katika kuwajengea uwezo juu ya masuala ya uwezeshaji wa Wanawake katika nafasi za uongozi.

Akizungumza katika Mafunzo hayo, Mwezeshaji Bi.Mary Msemwa amesema kupitia mafunzo hayo tutegemee ushiriki wa wanawake katika ngazi ya maamuzi wataimarika.

Aidha amesema wanawake waliopo kwenye ngazi za maamuzi ni wachache hivyo kupitia mafunzo hayo yatawajengea uwezo na uthubutu kugombea nafasi za uingozi kwenye uchaguzi ujao.

Kwa upande wa washiriki wamesema kuwa katika Kamati zao kumekuwa na changamoto ya usawa wa kijinsia hsa kwneye kamati za ulinzi na usalama ambapo wanaume wengi wapo kwenye kamati hiyo kuliko wanawake kutokana wengi kuamini ya kuwa kazi hiyo hufanywa na wanaume tu.

Nae Mjumbe wa Kamati ya Serikali ya Mtaa wa Kivule Bw.Erick Anderson amesema kupitia Mafunzo hayo wanakwenda kuboresha zaidi kwenye kamati zao ili waweze kupata maendeleo endelevu.

Amesema watatumia Mafunzo hayo kwenda kutoa elimu ya usawa wa kijinsia katika Kamati zao katika kuhakikisha jamii inafanya maendeleo makubwa hasa kutokana na uwepo wa usawa wa kijinsia.

Amesema mafunzo hayo yatakwenda kusaidia kufanya maboresho zaidi katika Kamati zao ili waweze kupata Maendeleo endelevu.













Mtandao wa Bloggers Tanzania (TBN) Wakutana na Maafisa Ubalozi wa Marekani na kuahidiana ushirikiano katika kukuza taaluma

$
0
0

Mtandao wa Bloggers Tanzania (TBN) leo umefanya mkutano usio rasmi na chakula cha mchana na Bi. Jeanne Clark Afisa wa Masuala ya Umma na Kalisha Holmes Afisa Habari kutoka Ubalozi wa Marekani kwa mtiririko huo

katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.


Katika kikao hicho wanachama waandamizi wa TBN waliohudhuria walijadili mambo kadhaa na maofisa hao ikiwemo mipango ya sasa na ya baadaye ya chama.


"Tulishiriki  kwa kutoa maoni yetu ya namna kukiendeleza zaidi chama ili kukuza kazi muhimu inayofanywa na wanachama wetu tangu kuanzishwa kwake mapema 2015," mmoja wa wanachama mwanzilishi wa TBN Josephat Lukaza alisema.


"Tulifurahishwa kujua kwamba  Ubalozi wa Marekani inafuatilia kwa karibu kazi za waandishi wa habari mtandaoni na kuonesha nia ya kushirikiana na TBN", alisema John Bukuku, mwanablogu mwingine mkongwe.


Wajumbe hao wa TBN waliushukuru Ubalozi wa Marekani kwa kuonyesha nia ya kutoa fursa za mafunzo ili kuimarisha taaluma na kuzingatia maadili ya uandishi wa habari, wakisema kuwa hatua hiyo inatia moyo kwa kweli.


Mwanablogu mwanzilishi Muhidin Issa Michuzi alisema kuwa ushirikiano baina ya TBN na watu kama ubalozi wa Marekani unaolenga mafunzo ya weledi wa uandishi na kuzingatia maadili ya taaluma hii utasaidia saną  katika kuinua viwango vya uandishi wa habari mtandaoni nchini Tanzania.


"Kujitolea kwa ubalozi wa Marekani kukuza mazingira ya kuunga mkono na kuwawezesha wanablogu na waandishi wa habari mtandaoni ni jambo la kutia moyo. Tuna imani kwamba ushirikiano huu utachangia kwa kiasi kikubwa ukuaji na maendeleo ya chama chetu, pamoja na sura pana ya vyombo vya habari nchini Tanzania", 


Michuzi aliongeza: “Tunafurahia kuwepo kwa uwezekano wa ushirikiano na Ubalozi wa Marekani wa siku zijazo na matokeo chanya yatakayotokana na Ushirika huo utanufaisha wanachama wetu na jumuiya ya wanablogu wa Tanzania kwa ujumla..”


MKURUGENZI MKUU TCAA AKAGUA MABORESHO YA MRADI WA MNARA WA KUONGOZEA NDEGE UWANJA WA NDEGE MTWARA

$
0
0

 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Bw. Hamza Johari ameongoza timu ya wataalamu kutoka Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) na Wakala wa Majengo (TBA) katika ukaguzi wa mradi wa maboresho ya mnara wa kuongozea ndege unaoendelea katika Uwanja wa ndege Mtwara.

Mradi huo unahusisha vipengele viwili ikiwa ni kujenga mnara wa muda ambapo utaruhusu waongozaji ndege kuendelea na kazi wakati mnara wa sasa ukifanyiwa maboresho unatarajiwa kukamilika kabla ya mwezi Novemba.

Huu ni muendelezo wa uboreshaji wa miundombinu unaofanywa na Serikali ya awamu ya sita katika kuhakikisha wataalamu wanatekeleza majukumu yao katika mazingira mazuri ya kazi.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Bw. Hamza Johari (wa kwanza kushoto) akiongoza timu ya TCAA na Wakala wa Majengo (TBA) katika ukaguzi mradi wa maboresho ya mnara wa kuongozea ndege unaoendelea katika Uwanja wa ndege Mtwara.
Mhandisi Swalehe Nyenye kutoka TCAA akielezea mpango wa maboresho uliopo kwenye ramani ya ujenzi wa mnara huo

Timu ikiendelea kukagua hatua za mnara wa muda unaoendelea kujengwa uwanjani hapo.


Tanzania, Msumbiji Zakubaliana Kuimarisha, Kudumisha Ushirikiano

$
0
0

 

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Stergomena Tax, Mwenyekiti kikao cha tano cha kamati ya pamoja ya ushirikiano wa katika sekta ya ulinzi na Usalama kati ya Tanzania na Msumbiji akizungumza na waandishi wa habari leo Septemba 15, 2023 baada ya kufunga kikao cha tano cha kamati ya pamoja ya ushirikiano wa katika sekta ya ulinzi na Usalama kati ya Tanzania na Msumbiji, katika kikao kilichofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Stergomena Tax, Mwenyekiti kikao cha tano cha kamati ya pamoja ya ushirikiano wa katika sekta ya ulinzi na Usalama kati ya Tanzania na Msumbiji akizungumza na waandishi wa habari leo Septemba 15, 2023 baada ya kufunga kikao cha tano cha kamati ya pamoja ya ushirikiano wa katika sekta ya ulinzi na Usalama kati ya Tanzania na Msumbiji, katika kikao kilichofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. Kulia kwake ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Jumanne Sagini  na Kushoto ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Msumbiji, Pascoal Ronda na mkalimani wake.

Na Avila Kakingo, Michuzi Tv
SERIKALI Tanzania na Serikali ya Msumbiji zimekubaliana kuendeleza na kudumisha ushirikiano katika Ulinzi na Usalama kwa maslahi kwa Masilahi ya raia wan chi hizo mbili.

Mwenyekiti wa Mkutano huo ambaye pia ni Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Stergomena  Tax ameyasema hayo leo Septemba 15, 2023 baada ya kufunga kikao cha tano cha kamati ya pamoja ya ushirikiano wa katika sekta ya ulinzi na Usalama kati ya Tanzania na Msumbiji, katika kikao kilichofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. Amesema kuwa Tanzania iko tayari kufanya kazi kwa karibu na Msumbiji ili kuimarisha zaidi ushirikiano wa ulinzi na usalama.

Amesema kuwa Kwa pamoja, tunaweza kushinda changamoto tunazokabiliana nazo na kujenga mustakabali ulio salama na wenye mafanikio zaidi kwa mataifa hayo mawili kwa watu wake.

Ameeleza kuwa uhusiano wa nchi hizo umejengwa kihistoria tangu wakati wa mapambano ya ukombozi kwa sababu tulipigana pamoja, kushinda pamoja na tunapaswa kubaki na umoja huo.

Akizungumza mara baada ya mkutano uliowakutanisha watendaji wa juu katika Idara mbalimbali za masuala ya ulinzi na usalama kutoka nchi Tanzania na Msumbji Dkt. Tax amesema kuwa mkutano huo ni matunda ya ziara ya Dkt.Rais Samia wa Septemba 27-29, 2022 alipotembelea Msumbiji iliyoendesha majadiliano yaliyowezesha kusainiwa kwa mkataba wa makubaliano ya amani na usalama.

Amesema mkutano huu umetoa fursa nyingine ya kuendeleza kushirikiano hasa katika maeneo ya mashirikiano yaliyomo katika mkataba wa makubaliano.

Kuhusu changamoto za uasi, Waziri wa Mambo ya Nje wa Msumbiji, Pascoal Ronda amesema uhusiano wa nchi hizo umekuwa na manufaa ya kihistoria.

“Juni 15 mwaka huu ikiwa ni baada ya miaka mingi ya mazungumzo magumu, Rais wa Jamhuri ya Msumbiji pamoja na kiongozi wa chama cha Renamo alifunga kambi ya mwisho ya kijeshi ya vikosi vya kukabili vuguvugu la kigaidi huko Vunduzi, Wilaya ya Gorongosa, Mkoa wa Sofala.”

“Hatua hii ya kihistoria inaashiria mwisho wa mchakato wa upokonyaji silaha, uondoaji na urejeshaji Silaha, uliofanyika kutokana na juhudi za ndani na nje ya Msumbiji na jumuiya ya kimataifa ikiwa ni pamoja na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.”

“Hatua hiyo inatoa mwelekeo wa maridhiano na utulivu wa nchi huku tukiwa na changamoto kubwa ya kupambana na ugaidi katika Jimbo la Cabo Delgado, ambako ni mapambano ya bila kupumzika huku tukiendelea na ushirikiano wa pamoja na jirani na ndugu zetu Tanzania.”

TAASISI YA MAMA ONGEA NA MWANAO KUANZA KAMPENI YA SAMIA NIVISHE KIATU AWAMU YA PILI MIKOA YA LINDI,MTWARA, RUVUMA

$
0
0

 Na Mwandishi Wetu , Michuzi TV.


TAASISI ya Mama Ongea na Mwanao imesema inatarajia kuanza awamu ya pili ya kampeni ya Samia nivishe kiatu kwa kugawa viatu kwa wanafunzi wa shule zilizopo katika wilaya zote za Mkoa wa Lindi na Mtwara.

Imesisitiza katika kufanikisha kampeni hiyo imejipanga kuhakikisha wanashirikiana vizuri na Serikali ya Awamu ya Sita ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa kumfikia kila Mtanzania wa kijijini na kumpatia kiatu kama sehemu ya kumuongezea hamu ya kupenda shule.

Akizungumza Septemba 14,2023 jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa Taasisi ya Mama Ongea na Mwanao Steve Mengele maarufu Steve Nyerere amesema hakuna sare ngumu kupatikana kwa mwanafunzi kama kiatu, hivyo wao wameamua kubeba jukumu hilo.

“Wanafunzi wa mjini wao wanavaa tu la kuchumpa la kupalama, hivyo tutakwenda katika shule zote na tutahakikisha wanafunzi wanapata viatu, wanapata daftari.Lakini tutakuwa tunazungumza na walimu maana yake tunaweza kuwa tunawapa viatu na kila kitu lakini walimu hawaingii madarasani.

“Kwa hiyo na sisi tutashirikiana kuwambiaa walimu tunataka taifa endelevu lenye amani na utulivu kama Tanzania tukose vijana wenye elimu kutoka mjini na kutoka vijijini.Tunafahamu Elimu yetu ni bure na kama elimu ni bure lazima tuwajenge watoto kisaikolojia.

“Na kinachotakiwa ni kumuwezesha mtoto kupenda shule kwani anaweza akawa na daktari lakini hana kiatu.Katika sare sare ya shule ngumu ni kiatu , bukta unaweza kupata lakini kiatu ndio adimu sana katika shule zetu, unaweza kukuta mtoto hajavaa kiatu ana miaka mitano

“Wewe toto lako kila likirudi shule huku mjini halirudi na kile kiatu linaondoka na kipya.Sasa tunajiuliza tumewaandaliwa mazingira gani ya watoto kupenda shule?Hivyo tunaweza kumuandaa mtoto kwa kitu kidogo tu nacho ni kiatu,”amesema Stive Nyerere.

Amefafanua kuwa miaka ya nyuma kidogo walikuwa wanafunzi wanapewa madaftari bure na kumfanya mtoto kuwa na hamu na shule.

Akifafanua zaidi kuhusu kampeni ya kugawa viatu Stive Nyerere amesema walianza kampeni ya Samia Nivishe Kiatu kwa kwenda shule za vijijini.

“Kule vijijini ndiko tunawakuta watu wa nguvu kazi leo mimi nikiwambia kitu hamuwezi amini watu wanaotoka vijijini ndio wanakuja hapa wanakuwa matajiri wanapata vyeo sisi tupo tupo tu.

”Sisi ndio tunakuwa mdananda wao lakini mtu katoka kijijini ndio anakuwa tajiri, anapata vyeo, sisi ambao tuko mjini ndio tunajichukulia poa kawaida kwasababu hatuna kasi ya kutafuta maisha.

Tunakazi ya kutafuta umbea, tuna kazi ya kutafuta huyu anapata wapi hela, tuna kazi ya kutafuta kunyong’onyesha mtu lakini yule anayetoka kijijini anapata kasi ya kuhangaika na baadae sisi ndio tunaanza kumsalimia na kumuita mheshimiwa.

“Sasa tumewajengea uwezo gani?Tumeona twende tukawavishe watoto viatu na viatu vile humpi mwalimu mkuu .Ukifanya hivyo utakuta familia nzima inabadili tu ,watoto wa mwalimu mkuu anang’aa hatari.”

Amesema hivyo wameamua unapofika shule inapigwa kengelengele pale watoto wanapata viatu na mtoto anaondoka na kiatu chake kwenda nacho nyumbani .

“Hii tafsiri yake nini, inamfanya mtoto awe na hamu na shule .Unajua unaweza kuwa huna akili lakini unahamu na shule unakipenda kile kitu lakini mazingira unayoishi na kukutana nayo, unajua kule kijijini kuna kitu kinaitwa mbigili

“Ukichomwa mbigili sita huwezi kumsikiliza mwalimu ,wee kazi yako unawaza namna gani unatoa miba kwenye miguu. Hivyo Katiba yetu mpya tunakwenda kuvisha watoto viatu na tunapowavisha viatu watakuwa na hamu ya kupenda shule.

“Naa badae tunakwenda kujenga kizazi chenye tija , kizazi kinachopenda elimu , kizazi ambacho kitatuvusha na kulinda heshima ya taifa lao.Hatuwezi tukakubaliana kila mmoja apende , wengine watachukia, wengine watanuna, wengine watabinua midomo lakini sisi tunaenda kuwapa wale wengi viatu.”

Steve Nyerere amesema baada ya hapo watarudi kugawa daftari na huko mbeleni wanaweza kugawa na mabegi .Hivyo kuanzia Jumatatu ya wiki ijayo watakuwa Lindi na baada ya hapo wataenda Mtwara, Ruvuma na kisha Dar es Salaam.

Amefafanua baada ya hapo watakwenda Mwanza,Mara na kurejea tena Dar es Salaam huku taasisi ikieleza tayari imegawa viatu 2000 katika wilaya ya Kibiti mkoani Pwani pamoja na Mkoa wa Tabora katika wilaya zake zote.













AICC yampongeza Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan katika kufungua mipaka

$
0
0

*Ni katika kupata mikutano mikubwa kufanyika katika Vituo vya Mikutano Dar na Arusha

Na Chalila Kibuda, Michuzi Blog

 Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Mikutano Kimataifa  Arusha (AICC) Ephraim Mafuru amesema kuwa kumekuwa na faida kwa kituo hicho kutokana na juhudi zilizifanywa na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kufungua Diplomasia ya uchumi na kufanya kituo hicho kuwa  na mikutano mingi.

Rais Dkt Samia Suluhu Hassan amepongezwa kwa kuonesha Uthubutu katika kuhakikisha Diplomasia ya Uchumi wa Tanzania inaimarika kupitia Diplomasia ya Mikutano ya Kimataifa, ambayo pia inatajwa kufungua nchi kupitia Sekta mbalimbali zilizopo hapa nchini.

Mafuru ameyasema hayo   Jijini Dar Es Salaam ukiwa ni mwendelezo wa Vikao kazi baina ya Taasisi na Mashirika ya Umma Chini ya Uratibu wa Ofisi ya Msajili wa Hazina.

Amesema wageni wanapenda Tanzania kutokana na juhudi zilizoonyeshwa na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ambapo ni kazi kwao kuendelea kukaribisha wageni na taasisi mbalimbali kufanya mikutano nchini.

Amesema kuwa mikutano hiyo ikifanyika nchini inaongeza fedha za ikiwemo dollar pamoja na kuchangia shughuli zingine kwa wageni kufanya huduma mbalimbali.

Mafuru amesema kuwa mpango wake ni kwa kila mfanyakazi katika taasisi hiyo wanakwenda kila mmoja kujipima na ambao hawatafikia malengo wataoandolewa ikiwa ni kutaka kukua katika sekta hiyo.


Amesema Tanzania katika kufanya mikutano imeshika nafasi ya Tano kutoka nafasi 18 ambapo hatua hiyo mafanikio kwao ni ndogo kwa kutaka kujenga majengo mengine ya kuchukua watu zaidi ya 5000 kwa wakati mmoja na michoro tayari.

"Wageni kutoka mataifa mbalimbali wanavutiwa kuja Tanzania kwa hilo ninamshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa ya Kufungua nchi, Ninajua kuna Royal Tour, lakini amekuwa akishiriki mikutano mbalimbali kuitangaza nchi, hatua ambayo imesaidia Tanzania kuwa chaguo muhimu na Kuvutia mikutano mbalimbali ya Kimataifa" amesema Mafuru.

Mafuru amesema katika tafiti walizofanya wamejiridhisha kuwa Diplomasia ya Mikutano itaendelea kuwa nguzo ya Kuongeza fedha za Kigeni na Kuimarisha Uchumi pamoja na pato la taifa

Aidha amesema  katika kuendelea kuwa na mikutano hiyo kuna baadhi ya Taasisi za Serikali zimekuwa  hazilipi madeni na kutaka walipe ambapo hayo madeni yamefikia bilioni Saba (7)

Hata hivyo amesema kuwa licha kuwa vituo vya mikutano wana Nyumba ambapo wanakwenda kuboresha zaidi huku wakiwa na hospitali ambayo inatoa huduma kwa wananchi katika jiji la Arusha

Amesema baada ya kampeni kubwa ya kufungua mipaka ya nchi katika utoaji wa huduma katika vituo vya mikutano wamekuwa na asilimia 10 ya Market Share kwa Afrika  malengo yao ni kwenda mbali zaidi.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Mikutano Kimataifa Arusha (AICC) Ephraim Mafuru akizungumza na wahariri  na waandishi wa habari hawapo pichani kuhusiana na utendaji na utoaji wa huduma za mikutano, jijini Dar es Salaam.


Afisa Mawasiliano wa Ofisi ya Msajili wa Hazina David Kosuri akitoa maelezo kuhusiana na uratibu wa mikutano kati ya wahariri na Taasisi na Mashirika ya Umma , jijini Dar es Salaam.

 


Baadhi ya matukio katika picha ya wahariri na watumishi AICC na Ofisi ya Msajili wa Hazina

RAIS SAMIA AFANYA UKAGUZI WA MABORESHO YA UWANJA WA NDEGE MTWARA

$
0
0

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akisalimana na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Bw. Hamza Johari wakati akiwasili uwanja wa ndege wa Mtwara alipofika kufanya ukaguzi wa maboresho yanayofanyika uwanjani hapo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akipokea maelezo juu ya maboresho yanayofanyika uwanja wa ndege wa Mtwara alipofika kufanya ukaguzi.

MHE.LUGANGIRA AZINDUA KAMPENI YA "PIKA KWA GESI, TUNZA MAZINGIRA"

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Agri Thamani Mhe. Neema Lugangira amezindua Kampeni ya "Pika kwa Gesi, Tunza Mazingira" inayolenga kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia ambayo ni sehemu ya utekelezaji wa maelekezo aliyotoa Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan wakati wa Kongamano la Nishati Safi ya Kupikia lililofanyika tarehe 1 Novemba 2022, Dar es Salaam.

Kampeni ya Pika kwa Gesi, Tunza Mazingira inaratibiwa na Ofisi ya Mbunge Lugangira kupitia Neema Na Maendeleo na Shirika la Agri Thamani ambalo Mbunge Lugangira ni Mwanzilishi wake. Kampeni hii imeanzia Wilaya ya Bukoba Mjini ikifuatiwa na Wilaya ya Muleba alafu itafika maeneo mengine ndani na nje ya Mkoa wa Kagera kulingana na uwezeshwaji utakaopatikana.

Kupitia Uzinduzi wa Kampeni ya Pika kwa Gesi, Tunza Mazingira; Mhe Neema Lugangira ametoa jumla ya Mitungi 300 ya Gesi kwa Viongozi wa Makundi Mbalimbali, Wajasariamali, Mama Lishe na Watu Mashuhuri katika Wilaya ya Bukoba Mjini

Mhe Neema Lugangira amewashukuru Wizara ya Nishati kwa kuwapa Semina Wabunge kuhusu umuhimu wa kuhamasisha nishati safi ya kupikia na uwezeshwaji uliofanikisha uzinduzi huu.

Aidha, Mhe Lugangira anamshukuru sana Bi. Jamilla Haroub Juma, Mratibu wa REA Bukoba na Bw. Masota Daudi Mafuru, Afisa Masoko Oryx Gas Mkoa wa Kagera & Geita kwa ushirikiano mkubwa waliompatia.

Kwa kuhitimisha, Mhe Neema Lugangira anakaribisha Wadau kumuunga mkono kufanikisha Kampeni ya Pika kwa Gesi, Tunza Mazingira ili kuweza kufikia Makundi mengine mengi kwenye jamii kwa lengo la kulinda afya za wakina mama, kutunza mazingira na kuepusha madhara ya mabadiliko ya tabia nchi, mambo ambayo yatapelekea kuimarisha Lishe Bora.







Dirisha la Ufadhili wa Masomo NMB Nuru Yangu 2023/24 lafunguliwa

$
0
0

NA MWANDISHI WETU

NMB Foundation imefungua rasmi dirisha la pili wa Ufadhili wa Masomo na Usimamizi mwaka 2023/24, kwa wanafunzi wanaojiunga Vyuo Vikuu kupitia Programu ya NMB Nuru Yangu Scholarship and Mentorship, ambako itafadhili wanachuo 65 kwa kiasi cha Sh. Bilioni 1 zinazojumuisha ufadhili wa wateule wa mwaka wa kwanza.

Ufadhili huo unatolewa kupitia Asasi ya Kiraia ya NMB Foundation iliyo chini ya Benki ya NMB. Asasi hiyo imejikita katika kusimamia na kufuatilia kwa karibu maendeleo ya kijamii na kiuchumi katika Sekta za Kilimo, Elimu, Afya, Mazingira na Ujasiriamali, ambapo mwaka jana ilifadhili wanafunzi 65, ambao wanaendelea na masomo katika vyuo vikuu mbalimbali.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa dirisha la maombi linaloanza Septemba 15 hadi Oktoba 8, 2023, Meneja Mkuu wa NMB Foundation, Nelson Karumuna, alitaja sifa za waombaji kuwa ni ufaulu wa Kidato cha Sita wa Daraja la Kwanza pointi 3 hadi Daraja la Kwanza pointi 7, kwa wanafunzi wenye mazingira magumu na wenye changamoto.

“Ufadhili huu ambao unaenda katika maeneo ya ada, nauli, posho, stationary, mafunzo ‘field’ na laptop, unatolewa kwa wanafunzi wanaojiunga chuo katika fani za Hesabu na Takwimu, Biashara, Uchumi, Teknolojia, Habari na Mawasiliano, Uhasibu, Uhandisi, Mafuta na Gesi, Sayansi pamoja na Udaktari.

“Mwaka huu tutafadhili wanafunzi 65, hivyo kuifanya NMB Foundation kuwa na wanafunzi 130 hadi Mwaka wa Masomo wa 2023/24 utakapoanza. Programu hii pia inatoa usimamizi maalum ‘mentorship’ kuwawezesha wateule kupata ushauri, tukitarajia kuibua vipaji na kuwasaidia vijana hao kutimiza ndoto zao kielimu.

“Tunawahamasisha Watanzania wote kufikisha taarifa hizi kwa wanafunzi waliomaliza ‘form six’ mwaka huu, ambao wanajiandaa kujiunga vyuo vikuu, kutembelea tovuti yetu ya www.foundation.nmbbank.co.tz, wajaze fomu kwa usahihi ili kuepuka makosa yanayoweza kuwatoa kwenye mchakato wasomi wenye vigezo,” alisema Karumuna.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya NMB Foundation, Bi. Ruth Zaipuna, aliweka msisitizo kauli ya Meneja Mkuu wake akiwataka waombaji wahakikishe wanajaza fomu zao kwa usahihi, ili kuepuka makosa kama yaliyochangia kutopata wanafunzi 100 waliowahitaji mwaka jana, badala yake wakapata 65 tu.

“Mwaka jana tulitoa nafasi 100, lakini hadi dirisha la usajili linafungwa, tulipata wanafunzi wenye sifa 65 tu, kutokana na wengi kufanya makosa katika ujazaji wa fomu, tukajikuta wapo wanafunzi wenye sifa wameondolewa kwenye mchakato wakati walikuwa wanastahili ufadhili wetu, tunaomba makosa hayo yasijirudie.

“Watanzania watusaidie kuzifikisha taarifa hizi kwa vijana wetu, lakini tuwaombe pia wajaze fomu kwa usahihi ili tupate wanafunzi wote 65 tunaohitaji kuwafadhili mwaka huu, isijirudie makosa ya mwaka jana.

“Nia yetu sisi NMB Foundation ni kuendelea kuweka alama kwa jamii inayotuzunguka, ndio maana tunatafuta wadau zaidi wa kuungana nasi katika kufanikisha ufadhili huu kwa idadi kubwa ya wanafunzi na wanachuo wetu. Tunawaomba wadau wajitokeze kutusapoti kuwabeba vijana wetu, kwani mahitaji ni makubwa.

“Nia yetu kubwa ni kuwa chachu ya maendeleo endelevu ya vijana wa Kitanzania na jamii kwa ujumla. Pamoja na ufadhili huu wa masomo tunaowapa, NMB Foundation tutaendelea kuwatafutia wateule wetu nafasi za mafunzo kwa vitendo, sio tu hapa NMB, bali pia kwa taasisi washirika watakaoungana nasi.

“Mwisho kabisa, niwahakikishie vijana watakaoomba na Watanzania kwa ujumla, kwamba mchakato huu utakuwa wa huru, wenye usawa, haki, uwazi na umakini, ili kupata vijana wanaostahili. Tutafanikisha mchakato huu kupitia matawi yetu 230 yaliyoko kote nchini na Serikali za Mitaa,” alibainisha Zaipuna.





DIT YAZINDUA DAWATI LA JINSIA KWA LENGO LA KUZUIA VITENDO VYA UKATILI

$
0
0
TAASISI ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) imezindua Dawati la Jinsia kwa lengo la kuzuia vitendo vya ukatili na kushughulikia matukio yote yanayoripotiwa na wanafunzi, watumishi na wafanyakazi wengine.

Dawati hilo limezinduliwa leo na Mratibu wa Madawati ya Jinsia kwenye taasisi za elimu ya juu na Vyuo vya kati wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Gift Msowoya.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Msowoya alisema matukio ya ukatili wa jinsia yalikuwa yakiendelea vyuoni lakini hakukuwa na sehemu za kutolewa taarifa.

Amesema kuwa kuanzishwa kwa dawati hilo lengo ni kuwa na mfumo rafiki wa kutoa taarifa za ukatili.

"Mnapaswa kuwa na ofisi yenye usiri itakayomfanya mtu yoyote kutoa taarifa za ukatili bila woga, muwe pia na namba ya simu ili kupokea taarifa za ukatili wakati wowote," amesema Msowoya.

Ameongeza kuwa taasisi hiyo inapaswa kuunda klabu za ukatili wa jinsia za wanafunzi ili kusaidia upatikanaji wa taarifa na kutolifabya dawati hilo la watu binafsi.

"Dawati lisiwe kwa ajili ya kuangamiza watumishi, wanafunzi na wafanyakazi wengine bali mfuate sheria na taratibu zilizowekwa lakini pia kila mtumishi afanye kazi yake au masomo kwa kufuata taratibu," amesema.

Ameongeza kuwa : "Utandawazi umekuwa changamoto kubwa kwa wanafunzi wengi wao wanaingiwa tamaa na kujikuta wakifanyiwa vitendo vya ukatili hivyo muwasaidie kubadili mitazamo yao wasione maisha rahisi kwani mwisho wake ni mbaya."

Amesisitiza kuwa dawati hilo linapaswa kusaidia kunyanyua kizazi cha kujitambua na kuiokoa nchi katika kufikia dira ya dunia ya maendeleo ya kutokuendelea kwa vitendo vya ukatili.

Aidha, ameeleza taasisi kutenga bajeti kwa ajili ya madawati hayo na kutoa ripoti kila robo tatu ya mwaka.

Kwa upande wake, Naibu Mkuu wa Taasisi Taaaluma, Utafiti na Ushauri wa Kitaalamu, Profesa Ezekiel Amri amesema uzinduzi wa dawati hilo sambamba na uwepo wa sera utaongeza chachu katika kutekeleza kwa ufanisi sera ya taifa ya kukabiliana na ukatili.

Amesema kupitia dawati hilo wanalenga kutoa elimu ya ukatili wa jinsia kwa wafanyakazi, wanafunzi na watoa huduma wote wa taasisi, kuendesha semina za ukatili wa jinsia kwa wanafunzi na kushirikiana na madawati na taasisi za kuzuia ukatili wa jinsia.

Pia amesema watakuwa na utaratibu kuelimisha masuala ya ukatili, kutoa takwimu kuanisha matatizo hayo na kuweka mazingira rafiki yatakayowezesha usawa wa jinsia kwa wanafunzi na wafanyakazi wote.

Mary Kidima alisema ukatili wa kijinsia una tabia ya kujirudia, hivyo haipaswi kuvumiliwa badala yake wahusika watoe taarifa ili iweze kushughulikiwa kwa wakati.

Alisema kuwa changamoto zinazohafifisha juhudi za taasisi kufikia malengo ya utendaji katika eneo hili ni pamoja na uelewa mdogo wa baadhi ya wanajamii kuhusu dawati la jinsia ambapo wengi wanaamini kuwa linalenga kuwatetea watu wa jinsia ya kike peke yao na limekaa kiuanaharakati.

" Ukatili wa kijinsia unaweza kufanywa na yeyote mwanaume dhidi ya mwanamke au mwanamke dhidi ya mwanaume, ndio maana dawati linashughulika na jinsia zote. Wahanga wengi wa ukatili wa kijinsia ni waoga wa kutoa taarifa na hata ushahidi pale inapohitajika hivyo tatizo linaendelea kukua bila wahusika kuchukuliwa hatua yoyote," amesisitiza Kidima.

Kauli mbiu ya uzinduzi huo ni Vunja Ukimya, Fichua Ukatili wa Kijinsia' ikitoa wito kwa wanajamii wote kutofumbia macho vitendo hivyo..

JIPAKULIE MINYAMA WIKENDI HII UKIWA NA MERIDIANBET

$
0
0

HATIMAYE wikendi ya maokoto imerejea na Meridianbet ipo tayari kukupatia pesa yoyote unayoitaka wewe ukibashiri na mabingwa hao wa michezo ya kubahatisha nchini Tanzania kwa ODDS KUBWA na machaguo zaidi ya 1000 ambayo wanayatoa kila siku.

Ligi pendwa Duniani EPL imekuja kwa kishindo mechi mbalimbali kurindima siku ya Jumamosi na Jumapili ambapo mechi ya mapema hapo kesho itakuwa ni kati ya Wolves ambao watakuwa nyumbani kukiwasha dhidi ya Liverpool ambao wamekuwa wa moto sana. Nafasi kubwa ya ushindi wamepewa Liver wakiwa na ODDS 1.42.

Hapo hapo Uingereza Manchester United watakuwa Old Trafford kucheza dhidi ya Brighton huku mara ya mwisho kukutana Ten Hag alipoteza mechi. Nani kubeba pointi 3 hapo kesho?

Aviator, poker, Roullette, Wild Icy Fruits, Piggy Party na mingine kibao upige pesa na Meridianbet. Ingia www. meridianbet.co.tz.

Wakati huo huo mabingwa watetezi wa Ligi Manchester City watakuwa ugenini dhidi ya vijana wa David Moyes West Ham United ambao hawajapoteza mechi yoyote. Je Guardiola na vijana wake watapata pointi 3 kesho?

Meridianbet na Halopesa wamekuletea promosheni ya kujichotea maokoto endapo utaweka na kubashiri na Meridianbet na utaweza kupata zawadi kama pikipiki, pesa taslimu, simu janja nk. Ingia hapa na ubashiri.

Tukipaa hadi pale LALIGA mechi za kukupatia pesa nazo ni nyingi kazi inakuwa kwako wewe. Baada ya mechi ya Atletico kuahirishwa, wikendi hii atakuwa ugenini kukipiga dhidi ya Valencia huku mechi hii ikiwa na ODDS za kibabe. Ingia www.meridianbet.co.tz na ubashiri sasa.

Barcelona atamkaribisha Real Betis na mechi za msimu uliopita walipokutana, Xavi na vijana wake walishinda zote. Je Mgeni atalipiza kisasi? Mechi hii imepewa ODDS ya 1.37 kwa 7.44.

Na siku ya Jumapili majira ya saa 4:00 usiku kinara wa ligi Real Madrid atakuwa pale Santiago Bernabeu kuzichabanga dhidi ya Real Sociedad ambaye yupo nafasi ya 8 akiwa na pointi 6. Je Jude ataendeleza kuuwasha?

Meridianbet, Msimu Mpya Mzigo wa Kutosha

SERIE A ni ya kibabe sana wikendi ambapo mechi ya kuvutia ni Derby della madonnina kati ya Inter Milan dhidi ya AC Milan ambao walipokutana mara ya mwisho Inter alishinda. Nafasi kubwa ya kuchukua pointi 3 ndani ya Meridianbet amepewa mwenyeji akiwa na 2.16 kwa 3.28. Wewe unamdhamini nani?

Baada ya mabingwa wa Scudetto Napoli kupoteza mechi iliyopita, wao watawkuwa ugenini dhidi ya Genoa kusaka alama 3. Rudi Garcia anataka ushindi mechi hii ajiweke kwenye nafasi ya kutetea taji. Je mwenyeji anaweza kumzuia?

Odds kubwa kasino ya mtandaoni na michezo ya sloti ni vitu vinavyoweza kubadilisha maisha yako kwa kukupatia pesa nyingi. Ingia mchezoni hapa.

Naye Juventus atakuwa nyumbani kucheza dhidi ya Lazio ambaye alipata ushindi wake wa kwanza mechi iliyopita. Mechi za msimu uliopita waligawana pointi yani kila mmoja alishinda mechi moja. Karata yako unaitupa wapi?

Kule jijini Paris sasa LIGUE 1 nayo itachezwa wikendi hii Lille atakuwa mgeni wa Srade Rennes ndani ya Meridianbet, nafasi kubwa ya kushinda amepewa mwenyeji akiwa na ODDS ya 2.11 na mgenia akiwa na ODDS ya 3.19. Suka jamvi lako na weka mechi hii.

Jumapili moto utawaka katika dimba la Moustoir ambapo Monaco watakuwa wakisaka pointi 3 dhidi ya Lorient. Monaco ana pointi 10 huku mwenyeji akiwa na pointi 5.

Majira ya saa 12:05 Marseile atakipiga dhidi ya Toulouse. Kushinda mwenyeji amepewa ODDS ya 1.47 na mgeni amepewa ODDS ya 5.88.

NB: Bado Jakpoti inaendelea ndani ya Meridianbet ambapo kwa dau la shilingi 1000/= unaweza kubashiri mechi zako 13 na ukajipigia mkwanja wa shilingi 85,000,000. Ingia Meridianbet na ucheze sasa.





SERIKALI YAAHIDI KUTENGENEZA MAZINGIRA WEZESHI KWA SEKTA ZA BIMA

$
0
0

 Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulua Nchemba akimkabidhi tuzo ya kufanya kazi zaidi ya miaka 20 kama Staff wa kampuni ya Bima ya Alliance, Henry Mgalike wakati wa hafla ya kutimiza miaka 25 kwa  kampuni hiyo. Aliyeko nyuma ya Nchemba ni Kva Krishnan Afisa Mtendaji Mkuu wa Alliance na  aliyeko nyuma ya Mgalike ni Shaffin Jamal  Mwenyekiti wa Alliance.  Hafla hiyo imefanyika Septemba 24,2023 jijini Dar es Salaam.

Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya bima ya Alliance KVA Krishna,akizungumza wakati wa hafla ya kutimiza miaka 25 kwa kampuni hiyo jijini Dar es Salaam.


Kamishna wa Bima nchini, Dkt. Baghayo Saqware, akizungumza wakati wa hafla ya kutimiza miaka 25 kwa kampuni ya bima ya Alliance iliyofanyika jijini Dar es Salaam Septemba 14, 2023.
Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba akizungumza wakati wa hafla ya kutimiza miaka 25 kwa kampuni ya bima ya Alliance iliyofanyika jijini Dar es Salaam Septemba 14, 2023.

JICHUKULIE MAOKOTO YA MERIDIANBET KUPITIA HALOPESA

$
0
0

 

MERIDIANBET, kampuni kubwa ya michezo ubashiri mtandaoni, inafuraha kutangaza ushirikiano wake wa kipekee na Halopesa , moja ya mtoa huduma bora zaidi wa malipo kwa mitandaon ya simu hapa nchini, kuzindua Promosheni ya kibabe Zaidi "Meridianbet JICHUKULIE MAOKOTO na HALOPESA". Ikiwa na lengo la kumnufaisha mtumiaji wa Meridianbet na Halopesa wakati wa kufanya malipo.

“MERIDIANBET JICHUKILIE MAOKOTO NA HALOPESA” inawapa wateja wa Meridianbet njia isiyo na vikwazo, salama, na rahisi ya kuweka pesa kwenye akaunti zao za michezo kupitia Halopesa ambayo itawapatia zawadi kibao kabambe kipindi chote cha promosheni.

Ushirikiano huu utaenda kuongeza tija kwa wapenzi wa michezo ya ubashiri kupitia Meridianbet mabingwa namba moja wa michezo ya kasino ya mtandaoni na ubashiri wa soka.

Tunaposema "MERIDIANBET JICHUKILIE MAOKOTO NA HALOPESA” tunamaanisha kuwa mteja mshindi atapokea zawadi tofauti kama vile pikipiki, simu janja, pesa taslimu, bonasi, na Mizunguko ya bure! Yenye kuleta msisimko usio na kifani na zawadi kedekede kwa watumiaji wetu wote waliotukuka!

Tuna furaha kutangaza ujio wa promosheni hii mpya, inayoanza leo Septemba 15 mpaka 15 Novemba 2023 kwa wateja wafanyao miamala ya simu kupitia Halopesa kwenda kwenye akaunti zao za Meridianbet ili waweze kubashiri soka na michezo ya kasino, wataweza kuingia kwenye droo na kushinda pikipiki mpya, smartphone za kijanja , na zawadi nyingine kibao.

Meneja wa malipo kutoka Meridianbet Dora Kinyaiya alieleza furaha juu ya ushirikiano wao na na kampuni ya Halotel na kusema “Tunajitahidi kutoa uzoefu bora kabisa kwa wateja wetu wanaobashiri Meridianbet, na Tunafurahi kushirikiana na Halopesa kuzindua promosheni ya "Meridianbet jichukulie maokoto na Halopesa" ambayo inaanza leo tarehe 15 Septemba 2023 na itaendelea hadi tarehe 15 Novemba 2023, kwa kuwa inalingana kabisa na dhamira yetu ya kutoa huduma za ubashiri wa michezo yenye utulivu na salama kwa wateja wetu wa thamani. Ushirikiano huu unathibitisha hatua muhimu katika tasnia na unathibitisha dhamira yetu ya ubunifu na kuridhika kwa wateja."

Ndugu mteja endelea kubeti na Meridianbet huku ukisubiri mechi za ligi zote kurejea wiki ijayo na kwasasa odds ni kubwa sana, usikose pia Kasino ya mtandaoni ya Meridianbet yenye michezo rahisi ya sloti kama Poker, Aviator, Roulette.

NB: Habari njema kwako, Meridianbet imesikia ombi la wengi imekuja na Jackpot kubwa ya mechi 13 kwa dau dogo la kuanzia 1,000/=TZS mshindi atajinyakulia donge nono la Tsh 85,000,000/= PIGA *149*10#

#MERIDIANBET MSIMU MPYA, MZIGO WA KUTOSHA


Viewing all 39098 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>