Quantcast
Channel: MTAA KWA MTAA BLOG
Viewing all 39964 articles
Browse latest View live

MTOTO UMLEAVYO NDIVYO AKUAVYO...


TASWIRA KUTOKA DIMBWII TOPE MTAANI KWETU..

CHANGAMOTO YA BIASHARA PALE MZIGO AUJATOKA...

KUKATISHA HAPO UJUE KUKWEPA MAWE..

$
0
0
Madogo wa Mtaani kwetu ambao ni Wadunguaji mahiri wa Matunda Mtini wakiwa katika udunguaji wa Matunda juu ya Fensi wao na Mawe yao ambayo huwa yakikosa muelekeo hudondokea kwenye Njia ambayo inatumika na wana Mtaa kukatisha hapo.
#Kamerayamtaakwamtaablog.

BIASHARA MATANGAZO KAZI ZA WATU WACHACHE HIZI...

SHEREHE ZA MAULID KITAIFA: WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AWATAKA WAUMINI WA DINI YA KIISLAMU KUFUATA MAADILI MEMA

$
0
0

Waziri Mkuu, Kassim Majliwa na Rais Mstaafu, Ali Hassn Mwinyi wakisikiliza Kasida katika Baraza la Iddi lililohutubiwa na Waziri Mkuu kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam Desemba 24, 2015. Wapili kulshoto ni Sheikh Mkuu wa Tanzania Kufti Abubakari Zubri na kushoto ni Kadhi Mkuu wa Tanzania Alhaji Mnyasi.
Baadhi ya washiri wa Baraza la Maulid wakimsikilza Waziri Mkuu, Kassim Majliwa wakati alipohutubia Baraza hilo kwenye ukumbi wa Karimjee jijiniDar es salaam Desemba 24, 2015.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Shinyanga, Hamisi Mgeja na baadhi ya washiriki wa baraza hilo baada ya kuhutubia Baraza la Idd kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam Desemba 24, 2015.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri Mkuu Mstaafu, Dkt. Salim Ahmed Salim katika baraza la idd alilolihutubia kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam Desemba 24, 2015. ,Kushoto ni Bw. Azim Dewji na wapili kulia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku na kulia nii Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi, Ramadhani Kailima.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Serikali yapiga marufuku matangazo yote yanayohusu tiba asili na tiba mbadala kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii

MAENDELEO NI KWA VITENDO SIO MANENO: PROFESA MUHONGO

$
0
0
Mbunge wa jimbo la Musoma Vijijini ambaye pia ni Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo ameanza kwa kishindo kutekeleza ahadi zake kwa wananchi wa jimbo hilo na huku akiahidi maendeleo kwa kasi zaidi.

Profesa Muhongo alidhihirisha hayo juzi katika kijiji cha Murangi, Mkoani Mara katika kikao chake na baadhi ya wananchi wa jimbo hilo, watendaji wa Halmashauri ya Musoma Vijijini na madiwani huku lengo la kikao likiwa ni kujadili mipango na miradi ya uchumi na maendeleo ya jimbo hilo.

Katika kikao hicho, iliazimiwa kuanzishwe Mfuko wa Elimu wa Jimbo ambapo Profesa Muhongo aliahidi kutoa kiasi cha Shilingi Milioni mia moja ambazo atakopeshwa na Bunge kwa ajili ya kununulia gari.

Alisema badala ya kununulia gari, fedha hiyo ataiingiza kwenye Mfuko huo ili kuleta maendeleo kwenye jimbo hilo. “Dhamira yangu ni kuhakikisha jimbo letu linasongo mbele kiuchumi na kimaendeleo na siyo maneno bila mipango madhubuti,” alisema.
Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo akizungumza jambo wakati wa kikao chake na wananchi wa jimbo hilo pamoja na wadau wa maendeleo.

Katika maelezo yake ya mikakati ya maendeleo kwa jimbo hilo, Profesa Muhongo alisema kufikia Mwezi Januari mwanzoni, ataanzisha Ofisi tano za Mbunge jimboni humo ili kufikisha huduma kwa wananchi kiurahisi.

Alisema Ofisi hizo zitakuwa na mtumishi mmoja ambaye ataajiriwa na Mbunge na atapatiwa vitendea kazi vya kuanzia ambavyo ni pikipiki ili kumuwezesha kuwafikia wananchi kirahisi na kompyuta mpakato (laptop) kwa ajili ya kutunza taarifa na mawasiliano.

Profesa Muhongo alitaja maeneo ambayo ofisi hizo zitaanzishwa kuwa ni kijiji cha Murangi ambapo ndio patakua makao makuu, Busekela, Sangana, Mugango na  Nyegine na alitoa wito kwa vijana wa maeneo hayo kuomba kazi kwa nafasi husika na kwamba watakaofaulu watatakiwa kuwepo maeneo hayo ili kila watakapohitajika waweze kupatikana kiurahisi.
Baadhi ya wananchi waliohudhuria Kikao cha Profesa Muhongo (hayupo pichani).

Alisema usaili wa kuwapata watumishi hao utafanyika tarehe 26 na 27 mwezi huu na watakaofaulu wataanza kazi tarehe 1 Januari, 2016 kwa uangalizi wa kipindi cha miezi mitatu (probation period) na alitaja vigezo vitakavyotumika kwenye kuwapata kuwa  ni elimu kuanzia kidato cha nne na ujuzi wa kompyuta.


Mbali na hilo, katika kuimarisha elimu jimboni humo, Profesa Muhongo ametoa vitabu vya kujifunzia vipatavyo 20,000 (elfu ishirini) katika shule mbalimbali na huku kipaumbele kwa wakati huu ni kwa shule zilizofanya vibaya kwenye matokeo ya mwaka huu.

Alisema tayari ameagiza vitabu vingine 22,000 kutoka nchini Marekani na vitakapoingia nchini ameagiza Madiwani kuvisambaza kwenye shule ambazo hazina vitabu vya kutosha.

Mbunge huyo alisema kwa kutumia Mfuko huo wa Elimu wa Jimbo, pamoja na fedha za Halmashauri, kila shule itapatiwa huduma ya umeme, maji pamoja na kujenga na kukarabati shule hizo pamoja na nyumba za walimu.

Akizungumzia suala la miundombinu ya barabara, Mbunge huyo aliahidi kusimamia ujenzi wake ambapo alisema barabara kutoka Musoma mjini hadi makao makuu ya jimbo itajengwa kwa kiwango cha lami na alisema tayari tathmini imeanza na itakamilika mwishoni mwa mwezi huu.

Mbali na hilo, kwa barabara zilizo chini ya Halmashauri, Profesa Muhongo aliagiza madiwani wakae na kupitisha bajeti kwa ajili ya kukarabati barabara hizo na aliagiza kikao hicho kifanyike kabla mwezi huu haujamalizika.

Kuhusu suala la Afya, Profesa Muhongo alisema tayari ameagiza gari la wagonjwa ambalo linatarajiwa kuingia nchini ndani ya wiki mbili zijazo.

Kikao hicho cha maendeleo ya jimbo la Musoma vijijini kilihudhuriwa na wadau mbalimbali wa maendeleo kutoka ndani na nje ya nchi miongoni mwao kukiwa na wazawa wa jimboni humo ambao kwa sasa wanaishi nje ya jimbo hilo na wageni kutoka Ujerumani.

NENO LA LEO MTAANI....

SHEREHE YA MAULIDI MAKUU YA MTUME MUHAMMAD(S.A.W) ILIVYOFANA VISIWANI ZANZIBAR

$
0
0
Wanamadrasa wakipiga dufu kukaribisha wageni na Viongozi wakati wa sherehe za Maulidi Makuu ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W) yaliyofanyika jana katika uwanja wa Maisara Suleiman Mjini Unguja ambayo hufanyika kila mwaka.
Makamo wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Dkt.Mohammed Gharib Bilali akisalimiana na Sheikh Kassim Haidar Jabir mjumbe wa Kamati ya Maandalizi alipowasili katika sherehe za Maulidi Makuu ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W) yaliyofanyika jana katika uwanja wa Maisara Suleiman Mjini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na viongozi mbali mbali alipowasili katika sherehe za Maulidi Makuu ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W) yaliyofanyika jana katika uwanja wa Maisara Suleiman Mjini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Mwanasheria Mkuu Zanzibar Sheikh Said Hassan Said pamoja na viongozi mbali mbali alipowasili katika sherehe za Maulidi Makuu ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W) yaliyofanyika jana katika uwanja wa Maisara Suleiman Mjini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad alipowasili katika sherehe za Maulidi Makuu ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W) yaliyofanyika jana katika uwanja wa Maisara Suleiman Mjini Unguja
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohamed Gharib Bilal alipowasili katika sherehe za Maulidi Makuu ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W) yaliyofanyika jana katika uwanja wa Maisara Suleiman Mjini Unguja
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kulia) Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji Khamis, Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad (kushoto) na Naibu Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Hassan Othman Ngwali wakiwa katika sherehe za Maulidi Makuu ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W) yaliyofanyika jana katika uwanja wa Maisara Suleiman Mjini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kulia) Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji Khamis, Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad (kushoto) na Naibu Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Hassan Othman Ngwali pamoja na Viongozi wengine wakiwa katika sherehe za Maulidi Makuu ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W) yaliyofanyika jana katika uwanja wa Maisara Suleiman Mjini Unguja.
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein (katikati) akiangalia ratiba ya Maulidi ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W) yaliyofanyika jana katika Viwanja vya Maisara Suleiman Mjini Unguja akiwa Viongozi mbali mbali na wananchi.
Baadhi ya Akina Mama wa Kiisalmu wakiwa katika sherehe za Maulidi Makuu ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W) yaliyofanyika jana katika uwanja wa Maisara Suleiman Mjini Unguja ambayo hufanyika kila mwaka.
Wanafunzi wa Madrasa mbali mbali za Zanzibar wakiwa katika sherehe za Maulidi Makuu ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W) yaliyofanyika jana katika uwanja wa Maisara Suleiman Mjini Unguja,ambapo mgeni rasmi alikuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein.
Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji Khamis alipokuwa akitoa historia fupi wakati wa ufunguzi wa sherehe za Maulidi Makuu ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W) yaliyofanyika jana katika uwanja wa Maisara Suleiman Mjini Unguja,ambapo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kulia) akiwa ndio mgeni rasmi katika sherehe hiyo.
Ustadh Juma Seif Said Hamad kutoka Mkoa wa Kaskazini Unguja akisoama Qur'aan Tukufu Surah Luqman Aya 33hadi 34 za ufunguzi wa Maulidi Makuu ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W) yaliyofanyika jana katika uwanja wa Maisara Suleiman Mjini Unguja.

Wanafunzi wa Madrasat Nurul Islamia ya Jang'ombe -Mkoa wa Mjini wakisoma Qasweeda baada ya mlango wa kwanza wa sherehe za Maulidi Makuu ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W) yaliyofanyika jana katika uwanja wa Maisara Suleiman Mjini Unguja.
Ustadh Rashid Hamadi Bakari kutoka Muungoni Wilaya ya Kusini Mkoa wa Kusini Unguja akisoma mlango wa kwanza wa Maulidi Makuu ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W) yaliyofanyika jana katika uwanja wa Maisara Suleiman Mjini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) pamoja na Viongozi mbali mbali wakisiamama kumswalia Mtume wakati wa Maulidi Makuu ya kuzaliwa kwake Mtume Muhammad (S.A.W) yaliyofanyika jana katika uwanja wa Maisara Suleiman Mjini Unguja.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akitiliwa marashi pamoja na Viongozi mbali mbali wakati wa kumswalia Mtume katika sherehe za Maulidi Makuu ya kuzaliwa kwake Mtume Muhammad (S.A.W) yaliyofanyika jana katika uwanja wa Maisara Suleiman Mjini Unguja.
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein (katikati) pamoja na Wake wa Viongozimbali mbali wakisimama kumswalia Mtume wakati wa Maulidi Makuu ya kuzaliwa kwake Mtume Muhammad (S.A.W) yaliyofanyika jana katika viwanja wa Maisara Suleiman Mjini Unguja.Picha na Ikulu, Zanzibar.

Mambo yalivyonoga Soko la Mapinduzi Mwananyamala, kuelekea sikukuu za Krismasi na Mwaka Mpya

$
0
0
Wakazi wa maeneo mbali mbali ya Jiji la Dar es salaam wakiwa katika Soko la Mapinduzi Mwananyamala, kufanya shopingi ya mahitaji mbali mbali ikiwa ni sehemu ya maandalinzi ya kusherehea vyema Sikukuuu ya Krismass na Mwaka mpya, kama walivyonaswa na Kamera yetu ya Mtaa kwa Mtaa Blog. Picha na Emmanuel Massaka.
Wafanyabiashara katika Soko la Mapinduzi Mwananyamala wakichangamkia wateja wao waliofika kununua bidhaa mbali mbali sokoni hapo.
Mdau akimtumia meseji mteja kumtaarifu kuwa mali mpya imewasili Sokoni hapo.

RAIS MAGUFULI ASHIRIKI MISA YA KRISMASI KATIKA KANISA LA MTAKATIFU PETER JIJINI DAR ES SALAAM LEO

$
0
0
Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiwasili kushiriki Ibada ya Krismas misa ya kwanza katika Kanisa la Mtakatifu Peter jijini Dar es salaam leo Desemba 25, 2015.
Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli, mkewe Mama Janeth Magufuli na Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa wakishiriki Ibada ya Krismas katika Kanisa la Mtakatifu Peter jijini Dar es salaam leo Desemba 25, 2015
Sehemu ya waumini katika Ibada ya Krismas misa ya kwanza katika Kanisa la Mtakatifu Peter jijini Dar es salaam leo Desemba 25, 2015.
Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli, mkewe Mama Janeth Magufuli na Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa wakishiriki Ibada ya Krismas katika Kanisa la Mtakatifu Peter jijini Dar es salaam leo Desemba 25, 2015
Muadhama Askofu Mkuu Polycarp Kardinali Pengo wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, akiongoza misa ya Ibara ya Krismas mapema leo asubuhi.
Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli, mkewe Mama Janeth Magufuli na Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa wakishiriki Ibada ya Krismas katika Kanisa la Mtakatifu Peter jijini Dar es salaam leo Desemba 25, 2015
Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Muadhama Askofu Mkuu Polycarp Kardinali Pengo wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam aliyemkaribisha kusalimia wananchi bada ya kumalizika kwa Ibada ya Krismas misa ya kwanza katika Kanisa la Mtakatifu Peter jijini Dar es salaam leo Desemba 25, 2015.




Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akitoa salamu zake za heri ya Krismasi mara baada ya kumalizika Ibada ya Krismas misa ya kwanza katika Kanisa la Mtakatifu Peter jijini Dar es salaam leo Desemba 25, 2015.







SALAMU ZA X- MAS NA MWAKA MPYA 2016 KUTOKA KWA KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA

$
0
0
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA, KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED ZAHORO MSANGI - SACP, ANAWATAKIA WAANDISHI WOTE WA HABARI "HERI YA KRISMAS NA MWAKA MPYA, 2016"

KAULI MBIU: "ULINZI UNAANZA NA MIMI, WEWE NA SISI SOTE"
KUMBUKA: WHEN YOU SEE SOMETHING, SAY SOMETHING.
TUSHEREHEKEE KWA AMANI NA UTULIVU SIKUKUU YA KRISMAS NA MWAKA MPYA, 2016.

AHSANTENI!!!!

Mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard Kasesela Afungua mafunzo ya ulengaji Shabaha

$
0
0

Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mjini, Richard Kasesela akiongea na wana Mgambo na kuwaasa kuwa waaminifu kwani wao ndio walinzi namba moja katika nchi na wako karibu sana na wananchi. pia Mkuu wa wilaya alisistiza suala la usafi kama nguzo moja wapo ya uadilifu.
Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mjini, Richard Kasesela akizindua mafunzo ya shabaha. alifanikiwa kulenga 10 kati ya 30 zilienda kwenye shabaha.
Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mjini, Richard Kasesela akipokea maelezo toka kwa Mshauri wa Mgambo wa Mkoa Luteni Kanali J. Kitita.
Mkufunzi wa mafunzo akihesabu shabaha.
Mkuu wa wilaya akionyesha jinsi ya kutumia SMG

ZOEZI LA KUTOA ELIMU KWA MADEREVA NA ABIRIA LAZIDI KUPAMBA MOTO CHINI YA VODACOM TANZANIA

$
0
0
  Maofisa wa Jeshi la polisi kitengo cha Usalama barabarani pamoja na Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu(wapili toka kushoto)wakimshuhudia dereva Frank Masawe wa basi lenye Namba za usajili T 798 DCT linalofanya safari za mikoa ya Dar es Salaam na Mtwara akisoma karatasi yenye majibu baada ya kupimwa kilevi,wakati wa zoezi lilioendeshwa na Jeshi la polisi kitengo hicho kwa kushirikiana na Vodacom Tanzania kupitia kampeni ya”Wait to send”inayotoa elimu kwa madereva kutokutumia simu na kilevi wakati wote wakitumia vyombo vya moto ikiwa ni mwendelezo wa kampeni hiyo iliyofanyika jana katika Vituo vya mabasi ya kwenda mikoani cha Ubungo na Mbagala jijini.
 Askari wa Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani mkoa wa Dar es Salaam, SGT. John Jonas(kushoto)akimpima kiwango cha pombe mwilini dereva wa basi lenye namba za usajili T 798 DCT la Dar es Salaa na Mtwara ,Frank Masawe ikiwa ni mwendelezo wa kampeni ya”Wait to Send” inayotoa elimu kwa madereva kutokutumia simu na kilevi wakati wote wakitumia vyombo vya moto ikiwa ni mwendelezo wa kampeni hiyo iliyofanyika jana katika Vituo vya mabasi ya kwenda mikoani cha Ubungo na Mbagala jijini,katikati katika picha ni Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu ambao ni wadhamini wakuu wa kampeni hiyo.
 Baadhi ya Madereva wa Mabasi yanayoenda mikoani na wadalala wa jijini Dar es Salaam,wakimsikiliza Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu(kulia)akitoa elimu kuhusiana na pete ya kidoleni yenye ujumbe maalumu wa “Wait to send” wakati wa zoezi la kukagua magari na kutoa elimu kwa madereva hao kuhusiana na kutokutumia simu na kilevi wakati wote wakitumia vyombo vya moto ikiwa ni mwendelezo wa kampeni hiyo iliyofanyika jana katika Vituo vya mabasi ya kwenda mikoani cha Ubungo na Mbagala jijini.
 Mkuu wa kitengo cha elimu kwa Umma kitengo cha Usalama barabarani makao makuu ya Polisi ASP,Abel Swai(katikati) akifafanua jambo kwa Madereva wa mabasi ya endayo mikoani na daladala za jijini Dar es Salaam pamoja na Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania, matina Nkurlu(kulia) wakati wa zoezi lililofanyika Stendi kuu ya Ubungo na Mbagala ya kutoa elimu kwa madereva kutokutumia simu na kilevi wakati wote wakitumia vyombo vya moto ikiwa ni mwendelezo wa kampeni ya”Wait to Send”inayoendeshwa na Vodacom Tanzania kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi kitengo cha Usalama Barabarani.

Baadhi ya abiria wa Mabasi yaendayo mikoani wakimsikiliza Mkuu wa kitengo cha elimu kwa Umma kitengo cha Usalama barabarani makao makuu ya Polisi ASP,Abel Swai,wakati alipokuwa anawaelimisha abiria hao ndani ya basi linalofanya safari zake mikoa ya Dar es Salaam na Mtwara ikiwa ni sehemu ya mwendelezo wa kampeni ya”Wait to Send”inayotoa elimu kwa madereva kutokutumia simu na kilevi wakati wote wakitumia vyombo vya moto.Kampeni hiyo inaendeshwa na Vodacom Tanzania kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi kitengo hicho ilifanyika jana katika Stendi kuu ya Ubungo na Mbagala jijini.

WANAKIJIJI WA KIJIJI CHA ENGUSEROSAMBU WAFURAHIA MSITU KUREJESHWA MIKONONI MWAO.

$
0
0
Mraghbishi Noorkiyengop Mbaima toka kijiji cha Enguserosambu akisimama mbele ya mifugo iliyokutwa msituni katika eneo lililoruhusiwa la msitu wa jamii wa Enguserosambu

Ilikuwa ni siku ya shangwe na furaha kwa wananchi wa kata ya Enguserosambu wilayani Ngorongoro. Hii ni baada ya serikali kukubali ombi lao la kusimamia rasilimali ya msitu wa Loliondo namba 2 unaopakana na vijiji vinne vinavyokadiriwa kuwa na idadi ya wakazi wapatao 20,000 wanaotegemea mahitaji yao toka katika huo msitu.

Huu ni msitu pekee ambao wananchi kwa kushirikiana na Mkuu wao wa wilaya, na mashirika rafiki, wamefanikiwa kuishawishi serikali kuukabidhi msitu huo kwao. Katika mchakato huo uliochukua miaka kadhaa wanawake toka katika vijiji vya Enguserosambu, Ng’arua, Orkiu na Naan wamekuwa mstari wa mbele katika kufanikisha azma hiyo ya kubakiza msitu wao wa enzi mikononi mwao. Akielezea furaha yake aliposikia msitu wa Loliondo namba 2 umekabidhiwa kwa wananchi, mraghbishi mwanamke Noorkiyengop Mbaima alisema 

“Mimi mwenyewe nimefurahia, kwa sababu sisi akina mama tunategemea sana msitu huu kwa mahitaji yetu. Huu msitu kama ungeondoka katika mikono ya jamii basi tungeathirika sana sisi kina mama.” Umuhimu wa msitu huu kwa kina mama ndio uliowapelekea wao kutunga na kuimba nyimbo za hamasa na kutumbuiza, kushiriki kwa wingi katika vikao mbalimbali vya maamuzi wakati wote wa mchakato huo. 


Kwa kuwa msitu huu ndio tegemeo lao katika kuendesha maisha ya kila siku. Hakuna chochote ambacho kiliamriwa bila ya wao kuchangia na kushirikishwa kuanzia utungaji wa sheria ndogongogo za usimamizi wa msitu hadi kukabidhiwa rasmi msitu huo. “Nikichukulia mfano katika mikutano yote ya vijiji. Kiukweli wanawake wamekuwa wanajitokeza kwa wingi, kuliko makundi mengine yoyote. Hata ile siku ya uzinduzi wa msitu walikuwa wengi zaidi,” anaelezea Jackson Nangiria 

Ushiriki huu wa wanawake unatokana na ukweli kwamba wana uhusiano wa karibu na msitu huo wa enzi wa Enguserosambu.Si kwa ajili yao tu pamoja na watoto wao pia. Ni watoto hawa wa kike wenye majukumu ya kujenga nyumba kwa kutumia miti inayotoka ndani ya msitu huu, ndio wanaotembea na punda wakiwabebesha maguduria ya maji kwa umbali mrefu wakitafuta maji ambayo chanzo chake kipo kwenye msitu huu. Wanapopata watoto wanahitaji dawa za kuwaogeshea na dawa za uzazi ambazo zinatoka kwenye msitu huu. 

Wao ndio wapishi katika familia zao hivyo wanahitaji kuni zinatokana na miti iliyoanguka na kukauka ambayo inapatikana kwenye msitu huu. “Kina mama wanafanya mitambiko ndani ya msitu huu wengine ambao hawakupata watoto wanapatia hapo baada ya kuomba ndani ya msitu huu. Si hivyo tu ndani ya msitu huu kuna dawa mbalimbali za asili kwa mfano mtoto akizaliwadawa ya kumwogesha na kumnawisha hupatikana humo humo na nyingine ni za kunywa kama maziwa na nyingine kwa ajili ya mama,” anaeleza mwanamama mraghbishi Noorkiyengop Mbaima. Uwepo wa wanawake hawa wa Kimasai katika kata ya Enguserosambu kiukweli unatokana na uwepo wa msitu huu. Huu ndio msitu wa enzi ambao serikali ilipendekeza uwe chini ya usimamizi wake kama ulivyokuwa msitnamba moja wa Loliondo. 

Pendekezo hilo lilitolewa kupitia timu mbalimbali toka wizarani, ofisi za kanda na halmshauri ya wilaya, ambazo zilitembelea kijijini hapo kuomba kupatiwa muhtasari wa kikao cha kijiji kitakachopitisha ombi hilo la serikali. 

Ombi hilo linakuja kwa kijiji kwa sababu msitu huo umekuwa chini ya usimamizi wa wananchi wa kata ya Enguserosambu kwa miaka mingi. Ni wananchi hao ndio ambao wameutunza msitu huo pasipo Kuombwa wala Kukabidhiwa na serikali. Na kwa kweli wameweza kuutunza kwa muda wote huo. Miti haijakatwa, wananchi wamejiwekea sheria ndogondogo na pia kuwakamata wale ambao wamekuwa wakiharibu msitu huo. Hivyo wananchi hawa wamewajibika katika kuhakikisha msitu unabaki katika hali yake ya asili pasipo kushurutishwa na mtu yeyote. 

Kwa mantiki hiyo muhtsari uliokuwa unaombwa na serikali ya halmashauri yan wilaya ulihiitaji baraka za wananchi, ambao hawakuwa tayari kutoa sehemu ya uhai wao unaotegemea msitu huo. Hakuna mwanakijiji aliyekuwa tayari kukubali ombi hilo. Na jibu lilikuwa ni wazi kabisa kwamba ombi hilo lilitishia mustakabali wa jamii zinazozunguka msitu huo ambazo ni vijiji vya Enguserosambu, Ng’arua, Orkiu na Naan. Hivyo wakati serikali ikipendekeza kuusimamia 

msitu huo wananchi kwa upande mwingine wakaanza kuiomba serikali iwaruhusu kuusimamia. Ni kama kichekesho pande zote zinaombana kuusimamia msitu huo. Serikalikupitia halmashauri ya wilaya inasema tunahitaji kuusimamia, na wananchi wanaiomba serikali hiyo hiyo kuusimamia msitu huo. “Kwa kweli sisi kama wananchi wa Enguserosambu tumeona kwamba huu msitu ukiondoka chini ya usimamizi wetu tutaathirika. Kwa sababu msitu huu ni uhai wa wananchi wa hapa. Tukikosa huu msitu, hatupati maji wala mvua, tutakosa chakula. Kwa kifupi tutakosa kitu muhimu cha uhai wa jamii,” anaelezea mraghbishi Noorkiyengop 
Mbaima. 

Ndani ya msitu huu kuna miti ambayo wazee wanaitumia kwa ajili ya shughuli za kimila pamoja na miti ya kiasili ambayo inatumika kwa shughuli mbalimbali. Baadhi ya miti hiyo ni pamoja na Oroilieni ambao unatumika kwenye shughuli za jadi, ujenzi na kiimani. Akifafanua kuhusu mti huo Robert Kamakia anaelezea, “Huwezi kuingia jando bila kuwa na mti Oroilieni. Kwa kuwa unatumika katika kufanya baadhi ya shughuli za kimila. Mti mwingine ni Orikienyi ambao unatumika kama dawa ya kutibia magonjwa ya aina mbalimbali kama homa, kifua, malaria na kadhalika. Mti mwingine ni Ostiani ambao hutumika kwa ajili ya kivuli na kutunza maji.”

 Hivyo msitu huu una maana kubwa sana kwa makundi mbalimbali yakiwemo ya wazee, wanawake na vijana. K wa upande wa vijana kwa mfano, mila na desturi za kimasai zinawataka kujitenga hasa pale wanapoingia ngazi ya Morani. Ambapo hutakiwa kuweka kambi kwa ajili ya kuchinja ng’ombe na kula nyama. Tukio hili huchukua mpaka mwezi mmoja wakati vijana hao, wanapoazimisha sherehe hizo. 

Tukio hili linashirikisha matumizi ya miti mbalimbali kwa mujibu wa taratibu zao. Supu wanazokunywa huchanganywa na baadhi ya majani ya miti hiyo. Ni dhahiri ulaji wa nyama kwa mwezi mzima unahitaji pia matumizi ya dawa za asili. Na ndio maana wamasai hawasumbuliwi sana na magonjwa yanayotokana na ulaji mwingi wa nyamba. Si hivyo tu porini hamna vitanda hivyo baadhi ya majani hutumika kwa ajili ya zoezi hilo.

 “Kiukweli bila msitu vijana hawawezi kufanya chochote. Kwa kuwa kila kitu kinatoka katika huo msitu,” anafafanua Julius Long’oli. Lakini si hivyo tu, wakati wanaingizwa jando pia kuna miti inayotumika. Vivyo hivyo na katika sherehe za kumaliza jando. Hivyo msitu ni sehemu ya mila na utamaduni wa jamii hizi zinaouzunguka. Ni imani yao pia, ambayo kimsingi ni lazima iheshimiwe. Huu ni msitu wao wa enzi na enzi. “Huu ni msitu wa jamii kwa Kimasai unaitwa Elieteti yaani ndani ya jamii kwa maana ya jina hilo ni msitu unaosaidia jamii ya sasa na ya kizazi kijacho. Kwamba huu msitu unategemewa na kizazi cha sasa na kijacho,” anafafanua Yohana Tuluni mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya kusimamia msitu. Mtizamo huu wa wananchi wa kata hii, kwamba wao ndio wausimamie msitu huu, unatokana hali halisi ya msitu namba moja wa Loliondo unaosimamiwa na serikali kupitia halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro kuwa katika hali ya kutoridhisha. Miti mingi imekatwa kwa ajili ya matumizi ya ujenzi na hivyo kutishia uhai wa msitu huo. Kitu ambacho wana Enguserosambu hawakupenda kitokee kwa msitu namba mbili wa Loliondo ambao wanautegemea kwa mustakabali wa maisha yao. Msitu huu umekuwa ukitegemewa na jamii ya hapa kwa miaka mingi. Ni wao ndio ambao wamekuwa wakiutunza na kwa kweli wamefanikiwa kwa njia moja ama nyingine kuufanya uwe mzuri zaidi kuliko hata ule wa Liliondo moja unasimamiwa na serikali. 

“Wazo la kutaka kumiliki msitu lilikuwa kama ndoto, ukiangalia na hali halisi ilivyokuwa. Ni maono ya mtu mmoja aliyewashirikisha wenzake. Mwishowe wazo likatolewa Kwa wanakijiji ambao waliungamkono wazo hilo. Na mwishowe tukamwandikia Mkuu wa Wilaya na kwa kweli alituunga mkono sana,” anafafanua mraghbishi na mjumbe wa Bodi ya Wadhamini Jackso Nangiria Mchakato wa kuomba hadi kukabidhiwa usimamizi wa msitu umewezesha wananchi wa Enguserosambu kuongeza ufahamu wa mambo mbalimbali juu ya usimamizi wa misitu lakini pia mahusiano baina ya wananchi na viongozi yameboreka zaidi.

 Umoja ni nguvu utengano ni udhaifu, hivi ndivyo unavyoweza kusema Wanaenguserosambu wamekuwa wamoja zaidi. Mashirika rafiki yamesaidia sana katika kutoa elimu kwa wananchi na viongozi wao ambao maarifa hayo yamewezesha kujiwekea mikakati na hatimaye kufanikisha jamii kumiliki msitu wake wa enzi kwenye mikono yake. Wakati mchakato unaanza palikuwa na kijiji kimoja tu cha Enguserosambu kilichokuwa kinaundwa na vitongoji vinne vya Enguserosambu, Ng’arua, Orkiu na Naan ambavyo sasa vimepata hadhi ya kuwa vijiji. Kwa sasa sauti yao ni kubwa zaidi kuliko pale Mwanzo.
Watendaji wa PALISEP wakiwa pamoja na wanajamii wakishikana mikono kuonesha ushirikiano baina yao. Kuanzia kushoto ni Sarah Saningo, Robert Kamakia, Jackson Nangiria, Norkiyengop Mbaima, Sunde Tutayo na Fredy Samberu 

Hivyo Bodi ya Wadhamini ilichaguliwa na mkutano mkuu wa kijiji, ambacho sasa kina hadhi ya kata. Kwa hiyo usimamizi wa msitu huu kwa sasa umekabidhiwa kwa Kata ya Enguserosambu. Hivyo wananchi kutoka katika kila kijiji walichagua wawakilishi wao waliounda Bodi ya Wadhamini. Wawakilishi hawa jukumu lao kubwa ni kuratibu mchakato wote wa uombaji usimamizi wa msitu wa Loliondo 2. 

Baada ya kuchaguliwa wajumbe walipatiwa mafunzo na shirika la PALISEP ambao pia walisaidia uandikishwaji wa bodi tarehe 12/09/2012. Bodi hiyo imeundwa na wajumbe 10 kati ya hao wanawake ni 4. Bodi hii ilipata mafunzo ya sheria mbalimbali za misitu, usimamizi wa misitu na bodi yenyewe pia kupitia video ya hali ya msitu wa Loliondo 1. Walipata pia ziara za mafunzo kwa kutembelea misitu inayosimamiwa na jamii kwa mfano msitu wa Suledo uliopo Manyara wilaya ya Kiteto. Bila jamii kujitoa kwa hali na mali isingewezekana kufanikiwa kwenye hili. Kwani bodi ya wadhamini imefanya kazi kubwa. Jamii imeshiriki katika kuandika katiba ya bodi na sheria ndogondogo ambazo zimepitishwa katika mikutano ya vijiji. 

“Baada ya kuchaguliwa jukumu letu ilikuwa ni kutembelea msitu ili kujua hali yake. Lakini pia tuliweza kutoa elimu kwa wale waliokuwa wanaishi na kufanya shughuli za kilimo ndani ya msitu. Ili waweze kuondoka. Si kazi rahisi,” mjumbe wa Kamati ya Bodi ya Wadhamini Sunde Tutayo.

Kwa sasa mpango ni kuboresha na kutunza vyanzo vya maji. Kupitia bodi hiyo, wananchi wamejiwekea malengo ya kuuongeza zaidi kwa kupanda miti zaidi. Hili linafanywa kwa uangalifu mkubwa kwa kuwa kuna baadhi ya miti si rafiki mzuri kwa vyanzo vya maji inayakausha. Lakini si hivyo tu Bodi ya Wadhamini inaangalia njia sahii ya kuhakikisha kwamba zinapatika fedha za kununulia miti mipya. Wazo lililopo ni kuwakilisha mtizamo huu kwa wanajamii ili waweze kutaarifiwa na kusikilizwa nini yatakuwa maamuzi yao kwenye uchangishaji huo wa fedha. Changamoto nyingine ni uboreshwaji wa sheria ndogondogo kwa kuwa hakuna mipaka ya majukumu baina ya Bodi ya Wadhamini na Halmashauri ya serikali za vijiji. Kuna umuhimu wa suala hili kuwekewa utaratibu mzuri wa kiuwajibikaji kwa sababu muda mwingine vyombo hivi vinaweza kugongana kimawazo na kiutendaji na nani anawajibika kwa nani. 

“Hapo nje kuna mikaratusi tumeikamata sisi kama Bodi ya Wadhamini. Mtu ameangusha mti mbichi ambao haujakauka. Na ameiyangusha bila idhini. Tumefanya hivi kwa kushirikiana na Mheshimiwa Diwani. Tunachosubili tukae na serikali ya kijiji ili tujue tunafanya nini,” anafafanua mraghbishi na Kaimu Katibu wa Bodi ya Wadhamini Jackson Nangiria. Kwenye kukabidhiwa msitu mgeni rasmi alikuwa ni Mkuu wa Wilaya na Diwani wa Kata ya Enguserosambu walikuwepo wakati wa kukabidhiwa kwa msitu huo pamoja na wenyeviti wa vijiji vyote vinavyounda kata ya Enguserosambu. Kwa hakika wenzetu wa Enguserosambu wameweza kujipanga na kuhakikisha kwamba msitu wao wa enzi unabaki mikononi mwao.

MR.BLUE APAGAWISHA MASHABIKI WA MBEYA KATIKA SHOO YA XMASS ILIYO ANDALIWA NA RADIO 91.3 DREAM FM MBEYA.

$
0
0
 Mwanamuziki wakizazi kipya kipenzi cha wengi afaamikae kwa Jina la Mr.Blue apagawisha mashabiki wa muziki wa kizazi kipya Jijini Mbeya katika Shoo ya Xmass iliyo andaliwa na Radio Dream Fm 91.3 Mbeya na kusapotiwa na Cocacola, Paradise In Hotel, Wasanii wa Muziki kutoka Mbeya na Michuzi Media Group, Shoo Nzima ilifanyika katika ukumbi wa wazi Paradise In Soweto                                                                     Jijini Mbeya.
 Kutoka Shoto ni Meneja wa Radio Dream Fm Mzee wa Masauti Tom Chilala akiwa Sanjari na Mwanamuziki wa muziki wa Kizazi kipya Mwana Dada Petronia katika Picha. 
Mwana Daa Petronia akitumbuiza baadhi ya Nyimbo zake katika Shoo ya Xmass iliyo andaliwa na                                                          Radio Dream Fm mbeya.
                                  PICHA ZOTE NA MR.PENGO MBEYA.
                                           PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

neno la leo mtaani

WAZIRI MKUU KESHO KUANZA ZIARA YA KIKAZI MKOANI KIGOMA

$
0
0
Na Editha Karlo wa blog ya jamii,Kigoma
WAZIRI Mkuu Kassimu M Majaliwa(MB) (Pichani) kesho ataanza ziara ya kikazi ya siku mbili Mkoani Kigoma.

Akizungumza na waandishi wa habari juu ya ziara hiyo Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Kanali Mstaafu Issa Machibya alisema kuwa Waziri Mkuu atawasili Mkoani hapa kesho majira ya saa tatu asubuhi.

Alisema kuwa atapokelewa na viongozi mbalimbali wa serikali ya Mkoa na kisha atasomewa taarifa ya Mkoa.

Baada ya hapo ataelekea katika kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu iliyopo Wilayani Kasulu pamoja na kambi ya wakimbizi ya Nduta iliyopo Wilayani Kibondo.


Na siku ya jumatatu atafungua mwalo wa kibirizi na kufanya majumuisho ya ziara yake katika ukumbi wa NSSF na kisha kurejea Dar es salaam

HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI DAR ES SALAAM WANAWAKE 12 WAPATA WATOTO MKESHA WA KRISMAS

$
0
0
Afisa Muuguzi Msaidizi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es Salaam Mwanne Satara akimsaidia kumuelekeza Lulu Mohamed namna ya kumfunika nguo Mtoto aliyezaliwa usiku wa kuamkia Krismas Dar es Salaam ambapo akinamama 12 walipata watoto na Mmoja wa akinamama hao alipata mapacha 2 na kufanya watoto wa kiume kufikia 6 na wakike 7, kati yao akinamama waliofanyiwa upasuaji ni akinamama 10 na kati ya hao watoto njiti 2 na Hospitali ya Temeke akina mama waliojifungua hospitalini hapo kufikia idadi ya watoto 12, wakiume 4 na wakike 8 .
(PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA).
Afisa Muuguzi wa Zamu wa Hospita ya Mkoa Amana Florensia Ndumbaro akizungumza na waandishi wa Habari (pichani hawapo), Hospitali tumepokea idadi ya watoto waliozaliwa mkesha wa Krismas ni 33 kati yao 15 ni wakike na 18 ni wakiume na wote wapo katika hali nzuri na wananyonya vizuri pia mama zao wanaendelea vizuri.
Viewing all 39964 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>