Quantcast
Channel: MTAA KWA MTAA BLOG
Viewing all 39995 articles
Browse latest View live

MECHI ZA LIGI KUU ENGLAND WIKIEND HII

$
0
0

JUMAMOSI

Tottenham Vs Wes Brom 

Hull City v Bournemouth

Sunderland v Stoke City

Swansea City v Arsenal

Watford v Middlesbrough

West Ham United v Crystal Palace

Leicester City v Chelsea


JUMAPILI

Everton v Manchester City

Manchester United v Liverpool

BAADHI YA VITUO VYA MAFUTA HAVINA MAZINGIRA BORA-KAIMU RC, HAPI

$
0
0


Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
KAIMU Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Ally Hapi amesema kuwa baadhi ya vituo vya mafuta havina ubora wa mazingira licha ya kuwa na majina makubwa.
Hapi ameyasema hayo leo wakati uzinduzi wa maboresho ya kituo cha mafuta cha Total kilichopo maeneo ya Sokota barabara ya Mandela jijini Dar es Salaam, amesema vituo vya mafuta vinahitaji kuwa mazingira bora kutokana na huduma wanayoitoa.
Amesema Total imejikita katika uhifadhi wa mazingira kwa kutengeneza vituo bora vya mafuta tofauti vituo vingine ambavyo havisadifu na majina ya kampuni na kuwaasa kuboresha vituo vyao ili kuendana na mazingira ya kisasa.
Hapi amesema kuwa vilanishi vinavyopatikana katika kituo hicho kujenga kiwanda nchini kutokana na kuwepo kwa magari mengi na yatazidi kuongezeka kutokana na viwanda vinavyojengwa nchini.
Katika uzinduzi huo ameomba mafuta lita 10,000 kwa kampuni ya Total kwa ajili ya kutumia katika uchongaji wa barabara za manispaa ya Kinondoni ambapo alikubaliwa kupewa lita hizo.
Amesema kuwa kuna kampuni imejitolea kutoa mitambo ya kufanya kazi hiyo lakini waliomba mafuta nijitegemee kwa kupata mafuta kwa hayo kazi itafanyika.
Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Total, Tarik Moufaddal amesema kituo cha mafuta kuboreshwa kuendana na wakati wa sasa kutokana na huduma wanayoitoa.

Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alli Hapi pamoja na Mwenyekiti wa Total Afrika Mashariki na Kati, Jean Christian Bergeron(wa pili kutoka kushoto) wakikata utepe kuashiria uzinduzi cha Total kilichofanyiwa maboresho kilichopo maeneo ya Sokota jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alli Hapi akipeana mkono na Mwenyekiti wa Total Afrika Mashariki na Kati, Jean Christian Bergeron kuashiria uzinduzi cha Total kilichofanyiwa maboresho kilichopo maeneo ya Sokota jijini Dar es Salaam.

Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alli Hapi akizungumza wakati uzinduzi wa kituo cha Total kilichofanyiwa maboresho kilichopo maeneo ya Sokota jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mafuta ya Total, Tarik Moufaddal(kulia) akizungumza katika uzinduzi wa ya kituo hicho.


Sehemu ya wafanyakazi wa kituo cha mafuta Total wakimsikiliza mgeni rasmi (hayupo pichani) wakati wa uzinduzi cha Total kilichofanyiwa maboresho kilichopo maeneo ya Sokota jijini Dar es Salaam.

SHEREHE ZA HARUSI ZA KIFAHALI ZAPIGWA PINI HUKO SOMALIA

$
0
0
Mji mmoja huko nchini Somalia umepiga marufuku harusi za gharama ya juu ili kuwashinikiza vijana zaidi wa nchi hiyo kuoa pindi wapatato wenza wao.

Kamishna wa wilaya ya Bula Hawa karibu na mpaka wa Kenya, Mohamud Hayd Osman amenukuliwa akisema kwamba ni idadi ya mbuzi wasiozidi watatu ndio wanaofaa kuchinjwa pekee ili kuwalisha wageni na kwamba sherehe katika hoteli hazitaruhusiwa.

Amesema kuwa mahari itakuwa chini ya dola 150 pekee. Uamuzi huo umefikiwa baada ya maafisa wa Serikali ya nchi hiyo kubaini kwamba takriban watoto 150 walizaliwa nje ya ndoa hivi karibuni.

Kamishna huyo ameongezea kwamba gharama ya harusi, ukosefu wa ajira na kiangazi ndio maswala yanayowafanya watu kulihama eneo hilo.

Waandishi wanasema sio kawaida kwa familia ya bwana harusi kutumia takriban dola 5000 katika harusi nchini Somalia.

"Mafunzo ya kiislamu yanasema kuwa ndoa inafaa kuwa ya gharama ya chini, alisema Osman.

Hatua hiyo ya kupunguza matumizi katika sherehe za harusi za kifahari ni pamoja na matumizi mengine baada ya maafisa kugundua kwamba ni kwa nini watoto 150 walizaliwa nje ya ndoa mjini humo.

Wasichana walikuwa wanakataa kuolewa hadi pale kitita cha pesa kitakapotumika kwa dhahabu pamoja na fanicha, alisema.

POLISI WAFANYA UKAGUZI KATIKA KUTUO KIKUU CHA MABASI UBUNGO

$
0
0
 Mkaguzi wa Magari wa Jeshi Polisi , Ibrahim Samwix akikagua basi la leo yenye namba za T 735 DFX usajili katika kituo kikuu cha mabasi Ubungo jijini Dar es Salaam.
 Mkaguzi wa magari wa Polisi Sajeti , Elisante Bulla akikagua basi la kampuni ya Imo yenye namba za usajili T 773 CVX ambapo alibaini kukosa mikanda na kuirudisha ndani ya kituo cha mabasi Ubungo leo jijini Dar es Salaam.
Mkaguzi wa magari wa Polisi Sajeti , Elisante Bulla akikagua basi la kampuni ya Islam na kubaini kukosa langi katika mgongo wa basi hilo na kung’o namba za usajili ili wakapake rangi katika kituo kikuu cha mabasi Ubungo leo jijini Dar es Salaam.
 06.Sehemu ya mabasi yakisubiri abiria wa mikoa mbalimbali leo katika kituo kikuu cha mabasi Ubungo leo jijini Dar es Salaam.
 Mkaguzi wa Magari wa Jeshi Polisi , Ibrahim Samwix akimuonyesha mwaandishi wa blog hii vifaa ambavyo vilikuwa vibovu katika mabasi ambavyo walileta baina kubaini makosa hayo leo jijini Dar es Salaam.

 Mkaguzi wa magari wa Jeshi la Polisi, Jackson Mafuru akifanya ukaguzi wa basi katika kituo kikuu cha mabasi Ubungo leo jijini Dar es Salaam. Picha na Emmanel Massaka,Globu ya Jamii.

MAMA SAMIA AFUNGUA MAFUNZO YA VIONGOZI NA WATENDAJI WA CCM MKOA WA KASKAZINI UNGUJA

$
0
0
Mlezi wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Kaskazini na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakazi wa mkoa wa Kaskazini A, Unguja wakati wa Kufungua Mafunzo maalum ya Viongozi na watendaji wa Chama Cha Mapinduzi na Jumuiya zake wa ngazi ya Matawi, Wadi na Majimbo.
Wana CCM wa Kaskazini A wakiwa wamejitokeza kwa wingi kwenye mafunzo ya Uongozi yaliofunguliwa na Mlezi wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Kaskazini na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan. 
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kaskazini A Unguja, Ndugu Juma Haji akihutubia kabla ya kumkaribisha Mlezi wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Kaskazini na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kufungua mafunzo maalum ya Uongozi yaliofanyika Mkokotoni Unguja kwenye Chuo cha Amali.

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa ambaye pia Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewataka viongozi wa CCM katika Mkoa Kaskazini (A) Unguja kuwachukulia hatua stahiki wanachama ambao wanakisaliti na kuhujumu shughuli katika hatua ya kujenga CCM mpya.


Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduz i(CCM) Taifa SAMIA SULUHU HASSAN ametoa kauli hiyo wakati anafungua mafunzo maalum ya viongozi na watendaji wa CCM na Jumuiya zake wapatao 556 katika ngazi ya matawi, wadi/tarafa na majimbo katika Mkoa wa Kaskazini (A) Unguja.

Samia Suluhu Hassan amesema kuwa hatua hiyo itasaidia chama kuimarisha shughuli zake kwa sababu chama kitakuwa na watu waadilifu na wenye nia ya kukisaidia CCM kusonga mbele na kupata ushindi mkubwa katika chaguzi zijazo.

Amesisitiza wanachama na viongozi wa CCM kote nchini waendelee kuweka mipango na mikakati imara itakayowezesha chama kuendelea kupata ushindi mkubwa na kushika dola.

Mjumbe huyo ambaye pia ni Mlezi wa CCM katika mkoa wa Kaskazini A Unguja amesema Umoja na Mshikamano miongoni mwa wananchama na viongozi ndio silaha madhubuti itakayowezesha chama hicho kuimarisha shughuli zake na kuongeza maradufu idadi ya wanachama nchini.

Amesema kwa sasa Viongozi watakiwa kujielekeza katika kufufua na kuimarisha jumuiya za chama ambazo katika baadhi ya maeneo hazifanyi kazi vizuri ili zianze kutekeleza majukumu yake kwa kuzingatia kanuni na taratibu za chama.

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi(CCM) Taifa pia ameendelea kuonya baadhi ya viongozi waache tabia ya kutengeneza makundi ya ndani ya chama kwa ajili ya kusaka madaraka bali wawe mstari wa mbele katika kujenga umoja na mshikamano ndani ya chama. 

Kuhusu mafunzo, Samia Suluhu Hassan amewahimiza viongozi wanaopata mafunzo hayo kuyatumia vizuri ili kuhakikisha wanaporudi kwenye maeneo yao wanafanya kazi kwa bidii na kwa uaminifu mkubwa. 

Amesema kwa sababu Serikali iliyopo madarakani inatekeleza ilani ya Chama cha Mapinduzi ni muhimu kwa viongozi wa chama katika ngazi zote washirikiane na viongozi wa Serikali katika maeneo husika ili kuhakikisha miradi ya maendeleo ya wananchi inafanyika kwa ubora unaotakiwa kulingana na thamani ya fedha.

DSTV WAUNGANA NA WAANDISHI KUSHUHUDIA UFUNGUZI WA AFCON GABON

$
0
0
Mkurugenzi wa Multichoiuce Tanzania  Maharage Chande akizungumza wakati wa kuwakaribisha waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbaliu nchini wakati wa ufunguzi wa kombe la mataifa Afrika yanayofanyika Gabon
Afisa Masoko wa Multichoice Tanzania Shumbana Walwa akuzngumza wakati wahafla ya waandishi wa habari pamoja na kuangalia ufunguzi wa kombe la mataifa Afrika AFCON kwa oamoja leo Jijini Dar es salaam

baadhi ya waandishi wa habari wakiwa katika hafla hiyo leo Jijini Dar es salamm.


Afisa Masoko wa Multichoice Tanzania Shumbana Walwa (Katikati) akijadiliana jambo na John Bukuku (kulia) wakati wa hafla ya waandishi wa habari pembeni ni Othman Michuzi.

Bendi alikwa wakitumbuiza kwenye hafla ya waanidhi wa habari leo Jijini Dar es salaam.


Mkurugenzi wa Multichoiuce Tanzania  Maharage Chande akiwa pamoja na wafanyakazi wengine wakampuni hiyo wakati wa hafla ya waandishi wa habari iliyofanyika leo Jijini Dar es salaam.
Ahmad Michuzi akisaini katika kitabu cha wageni wakati wa hafla ya waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam.

Waandisi wa habari kwa pamoja na wafanyakazi wa Multichoice Tanzania wakiburudika wka pamoja katika hafla ya waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam.



Waaandishi wa habari wakishuhudia kwa pamoja uzinduzi wa michuano hiyo leo Jijini Dar es salaa.Picha na Emanuel Masaka

SERIKALI KUENDELEZA MAPAMBANO YA DAWA ZA KULEVYA NCHINI

$
0
0
 Waziri  wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (katikati), akihutubia katika Maadhimisho ya Siku ya Familia ya Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni Dar es Salaam leo. Kutoka kushoto ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Kinondoni, Gift Msuya,Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ali Hapi, Kamanda wa Polisi Kinondoni, Suzan Kaganda na Meya wa Manispaa hiyo, Benjamini Sitta.
 Waziri  wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, akimkabidhi zawadi Mkaguzi wa Polisi, David Mabula.
 Ofisa wa Polisi Hamad akikabidhiwa zawadi na Waziri Nchemba.
 Askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani Sajeni, Moses Alphance Sinyagwa akipongezwa baada ya kukabidhiwa zawadi ya pikipiki kutokana na ufanyakazi bora.
 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Ali Hapi akitoa neno la shukurani katika maadhimisho hayo.
 Maofisa wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Kinondoni wakiwa katika shindano ya kumkamata kuku kwenye maadhimisho hayo.
 Maofisa wa jeshi la polisi wakiwa kwenye maadhimisho hayo.
 Waziri Nchemba akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali.
 Waziri Nchemba akiwa katika picha ya pamoja na maofisa wa polisi waliotunukiwa vyeti.
 Hapa Waziri Nchemba akiwa katika picha ya pamoja na wadau 
kutoka akampuni yaliyodhamini maadhimisho hayo.
 Bendi ya Jeshi la Polisi ikitoa burudani.
Askari polisi, jamaa zao na waandishi wa habari  wakiwa kwenye hafla hiyo.

Na Dotto Mwaibale
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba amesema Serikali itaendelea kupambana wa waingizaji na wauzaji wa dawa za kulevya nchini.

Mwigulu alitoa kauli hiyo wakati akihutubia katika Maadhimisho ya Siku ya Familia ya Polisi Mkoa wa Kinondoni jijini Dar es Salaam leo ambapo alikuwa mgeni rasmi.

"Serikali imejipanga  kupambana na dawa za kulevya ambazo zimekuwa janga la kitaifa ambapo vijana wengi wanakuwa waanga wakubwa'' alisema Mwigulu.

Mwigulu alisema serikali ya awamu ya tano haitamfumbia macho mtu yeyote atakaye kwamisha jitihada za kupambana na uhalifu nchini ambao wamepanga kuupunguza kwa asilimia 10 ifikapo mwaka 2019.

Aliongeza kuwa kanuni na sheria zilizowekwa na mkoloni ambazo zinazotumika ndani ya jeshi la polisi zimekuwa na changamoto kubwa kwa askari polisi. 

Akitolea mifano kadhaa alisema askari polisi aliyekosa nyumba ya kuishi ya jeshi hilo anapaswa kupewa fedha za kulipia pango nje ya kambi ya polisi na suala hilo si la kumuonea huruma askari husika bali ni haki yake.

Alisema kwa upande wa askari polisi aliyeumia au kupoteza kiungo wakati wa mapambano dhidi yake na wahalifu askari huyo anapaswa kulipa fidia yake kwa wakati badala ya kuunda tume ya kuchunguza jinsi alivyoumia akiwa katika mapambvano hayo.

"Mambo mengine hayahitaji mpaka uwe na elimu kubwa askari amepambana na majambazi mbele ya watu lakini majambazi hayo yamemjeruhi fidia yake anashindwa kulipwa eti mpaka iundwe tume haya si mambo ya ajabu" alihoji Mwigulu.

Alisema kwa muda mrefu askari anapopangiwa kituo cha kazi amekuwa akijigharamia kwa nauli na fedha za kujikimu kwa zaidi ya miezi mitatu na zaidi bila ya sababu za msingi.

Alisema hali hiyo kama askari husika anakuwa si mzalendo anaweza kujiingiza katika tamaa na kutumia silaha aliyonayokufanya uhalifu hivyo akaomba wahusika kuliangalia jambo hilo kwa karibu kwani mshahara na posho kwa askari hao ni haki yao.

Mwigulu alisema serikali kupitia Rais Dk. John Magufuli imejipanga kuweka mazingira mazuri kwa askari polisi ikiwa ni pamoja na kujengewa nyumba na kuona namna ya kubadilisha sheria ambazo zinaonekana hazina tija kwa wakati huu katika kuliongoza jeshi hilo.

MWANDISHI WA HABARI ZA MICHEZO GAZETI LA UHURU AMINA ATHUMAN AFARIKI DUNIA

$
0
0
Mwandishi wa habari za Michezo wa Gazeti la Uhuru, Amina Athuman (pichani) amefariki Dunia leo asubuhi katika Hosptali ya Mnazi Mmoja mjini Zanziba alikokuwa amelazwa.

Amina alilazwa Hospitalini hapo baada ya kuzidiwa (kushikwa na uchungu) kutokana na ujauzito na kukimbizwa kupata huduma katika hospitali hiyo ambpo alijifungua mtoto wa Kiume (Bahati mbaya) na yeye akaendelea kupatiwa matibabu hadi ulipomkuta umauti asubuhi ya leo.

Amina alikua mjini Zanziba kikazi alipokwenda kuripoti mashindano ya Kombe la Mapinduzi, ambapo alikuwa arejee jijini Dar es Salaam jana.

Mungu ilaze roho ya Marehemu Amina Athuman mahala pema peponi, Amina

JOSEPH MWANUKUZI NA MARIAM WAMEREMETA LEO

$
0
0
 Joseph Mwanukuzi akiwa amepozi na mke wake Mariam wakati wa Ibada ya Ndoa yao iliyofanyika katika Kanisa la St. Peter Oysterbay jijini Dar es Salaam leo.
Joe na mke wake wakielekea kula kiapo cha ndoa.
Joseph akimvisha pete ya ndoa mke wake Mariam.
Mariam akimvisha pete ya ndoa mume wake Joseph.
Jose akimkumbatia mke wake baada ya kuvalishana pete za ndoa.
Josephna Mariam wakioneesha pete zao za ndoa.
Mmeona....
Bwana na Bi. harusi wakiwa katika pozi.
Mapozi.....

Wakiwa na kila aina ya furaha.
Bwana harusi akihakikisha Bi. harusi anakuwa katika hali ya kupendeza muda wote.
Akiweka sawa vazi la Bi. harusi.
Bwana harusi akiweka saini cheti cha ndoa.
Bi, harusi akiweka saini cheti cha ndoa.
Maharusi wakionesha shahada zao za ndoa.
Joseph na Mariam wakitoka kwa furaha baada ya kufunga ndoa takatifu katika kanisa la St. Peter Oysterbay jijini Dar es Salaam leo.
Ndugu na jamaa wakiwapongeza.
Picha ya pamoja.


Picha ya pamoja.
Bi. harusi akiwa amepozi kwa picha.
Mapozi.
Wakiwa katika pozi.
Ni furaha tupu.
Busu takatifu....
Maharusi wakitoka kanisani.
Click here to Reply, Reply to all, or Forward

MAMA AUA MTOTO WAKE KISA KUKATAA SHULE

$
0
0
Mkazi wa Nsumba katika Manispaa ya Ilemela jijini Mwanza Joyce Mathayo (33), anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa kosa la kumpiga mtoto wake Mathayo Manisi (12) na kumuua kwa kosa la utoro shuleni.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza Ahmed Msangi akizungumza na wandishi wa habari ofisini kwake jijini hapa jana alisema tukio hilo lilitokea Januari 11, mwaka huu saa 4 asubuhi.
Alisema Mary alikamatwa na polisi baada ya kumpiga fimbo mtoto wake huyo ambaye ni mwanafunzi wa darasa la tatu sehemu mbalimbali za mwili na kumsababishia kifo, kitendo ambacho ni kosa la jinai.
Kamanda Msangi alisema siku ya tukio, mtoto huyo alimkatalia mama yake kwenda shule na kusema hataki shule tena, ndipo mama huyo alipopatwa na hasira na kuanza kumpiga fimbo sehemu mbalimbali za mwili na kumsababishia kifo muda mfupi baadaye.
Alisema baada ya mtoto huyo kufa, wananchi waliamua kutoa taarifa Kituo cha Polisi na polisi walifika mapema kwenye eneo la tukio na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa.
“Mtuhumiwa yupo katika mahojiano na polisi, pindi uchunguzi utakapokamilika atafikishwa mahakamani, mwili wa marehemu umefanyiwa uchunguzi na timu ya madaktari kutoka Hosipitali ya Rufaa ya Mkoa ya Sekou Toure na tayari umekabidhiwa kwa ndugu wa marehemu kwa ajili ya maziko,” alisema.
Kufuatia tukio hilo la kusikitisha, Kamanda Msangi ametoa wito kwa wazazi kuwalea watoto wao katika maadili mema na nidhamu kwa kuwaelimisha mambo mazuri na mabaya ili kuepusha kutoa adhabu za vipigo kwa watoto kwa kujenga familia bora isiyo ya ukatili.
Source: Habari Leo

YALIYOJIRI KWENYE MSIBA WA MAREHEMU AMINA ATHUMANI MWANDISHI WA HABARI ZA MICHEZO GAZETI LA UHURU NA MZALENDO KISIWANI ZANZIBAR.

$
0
0
Katibu wa Kamati ya Kombe la Mapinduzi na Makamo Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Zanzibar Ndg Khamis Said akimfariji Mume wa Marehemu Amina Athumani Ndg Toufik Majaliwa alipofika nyumbani kwa jamaa wa marehemu katika mtaa wa kariakoo unguja leo. kutowa mkono wa pole akiwa na waandishi wa habari za michezo Zanzibar ZASWA.

Kwa taarifa za msemaji wa familia Ndg Nurdin Ramadhani amesema mwili wa marehemu tasafirishwa kesho asubuhi na Boti ya Kampuni ya Azam Marine saa moja asubuhi kwa ajili ya mazishi yatakayofanyika Kijiji kwao Lushoto siku ya Jumanne mchana. 

Mwili wa marehemu utawasili jijini Dar es Salaam saa tatu asubuhi ukitokea Zanzibar baada ya kuwasili katika bandari ya Dar es Salaam utasafirishwa kuelekea kijiji kwao Wilaya ya Lushoto Mkoano Tanga kwa ajili ya mazishi.
 Katibu wa Kamati ya Kombe la Mapinduzi Ndg Khamis Said akimfariji kaka wa marehemu Ndg Nurdin Ramadhani alipofika katika msiba kutowa pole leo asubuhi.
Katibu wa Kamati ya Kombe la Mapinduzi Zanzibar Ndg Khamis Said akimfariji Mume wa Marehemu Amina Athuman Ndg Toufik Majaliwa alipofika nyumbani kwa ndugu wa marehemu katika mtaa wa kariakoo zanzibar leo asubuhi kutowa mkono wa pole kwa wafiwa.


Katibu wa Kamati ya Kombe la Mapinduzi Zanzibar Ndg Khamis Said akizungumza na waandishi wa habari za michezo Zanzibar Zaswa alipofika nyumbani kwa ndugu wa marehemu katika mtaa wa kariakoo zanzibar.
Mwenyekiti wa Chama Cha Waandishi wa  Habari za Michezo Zanzibar Ndg Mwinyimvua Mnzuki akizungumza na waandishi wa habari kwa kupokea kwa masikitiko kifo cha mwandishi mwezao mrehemu amani athuman kilichotokea leo asubuhi katika hopspitali ya mnazi mmoja.
Ndugu wa marehemu wakiwa msibari wakisubiri taratibu za kusafirisha mwili wa marehemu kuelekea Wilayani Lushoto Mkoani Tanga.

Wanafamilia wa marehemu Amina Athumani wakiwa katika msiba huo katika mtaa wa kariakoo Zanzibar.

Imetayarishwa na Othman Mapara wa
Zanzinews.com.


CHADEMA KUJA NA MKAKATI MPYA WA KUMTOA GODBLESS LEMA GEREZANI

$
0
0
Chadema imeamua kuja na mpango mpya wa kuhakikisha Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema anatolewa mahabusu.

Lema amekuwa mahabusu tangu Novemba mwaka jana, lakini chama hicho kimesema sasa kinataka apate haki ya kisheria na kuwa huru kwa kuwatumia wanansheria katika kesi mbalimbali zinazomkabili.

Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu amesema hayo baada ya yeye, mwenyekiti wake, Freeman Mbowe pamoja na viongozi wengine kumtembelea Lema mahabusu anakoshikiliwa tangu Novemba 2, mwaka jana kwa tuhuma za kutoa lugha za uchochezi dhidi ya Rais John Magufuli.

Lema amekuwa akikwama kupata dhamana kutokana na sarakasi za kisheria zilizosababisha upande wa utetezi uende hadi Mahakama Kuu katika kuhakikisha anapata haki hiyo, lakini hadi sasa bado vita hiyo ya kisheria haijaisha.

Lissu amewaambia waandishi wa habari mjini Arusha kwamba wataongeza nguvu ya mawakili wa Chadema katika kesi hiyo kila itakapokuwa ikitajwa mahakamani.

Pia, watakiandikia Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) barua rasmi kukitaka kitoe tamko kwa namna yoyote ili kiseme katika kesi ya Lema kipo upande upi na kama kikisema hakihusiki, basi hakutakuwa na chama cha wanasheria nchini na wakiona kuna hoja, basi watawataka watoe mawakili waliopo Arusha kusaidia kesi zinazomkabili Lema.

 “Hawa wanasheria wasijidai hamnazo wakati mbunge wao yupo mahabusu. Tutawaambia wawepo mahakamani kwa kuwa wananchi  wa kawaida hawaruhusiwi kuja kusikiliza kesi hiyo, basi wajae wanasheria,” amesema Lissu.

Awali, Mbowe amesema chama na viongozi waliamua kwenda kumuona Lema na familia yake kwa kuwa yupo mahabusu kinyume na haki za binadamu.

“Lema ana moyo mkuu sana na amejifunza mambo mengi kwa mujibu wa maelezo yake. Anasema wapo mahabusu asilimia 70 wenye makosa yanayostahili kupewa dhamana, lakini hawajapewa,” amesema.

Matokeo ya Kidato cha Pili Yatangazwa

$
0
0
Baraza la Mitihani nchini – NECTA limetoa matokeo ya mitihani ya upimaji kwa wanafunzi wa darasa la nne kwa shule zote za msingi nchini pamoja na ule wa kidato cha pili kwa wanafunzi wa shule za sekondari yanayoonesha ufaulu kuongezeka kwa 1.9%.

Katibu Mtendaji wa Baraza lza Mitihani nchini Dkt Charles Msonde ndiye aliyetoa taarifa hiyo leo jijini Dar es Salaam ambapo katika hali isiyo ya kawaida, shule tisa kati ya kumi zilizofanya vibaya katika mtihani wa kidato cha pili nchini, zimetoka mkoani Mtwara kama zinavyoonekana hapa

Amesema ufaulu umeongezeka kwa asilimia 1.9 kutoka 89.12% mwaka 2015 hadi kufikia 91.02% mwaka 2016 ambapo wanafunzi 372,228 wamepata alama zinazowawezesha kuingia kidato cha tatu huku wanafunzi 36,737 wakishindwa kufikisha alama hizo.

Shule ya St. Francis Girls ya Mbeya imeongoza katika shule 10 bora kitaifa katika matokeo ya mtihani wa kidato cha pili mwaka 2016

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, idadi ya watahiniwa waliopata ufaulu mzuri wa madaraja ya I, II, na III ni 178,115 sawa na asilimia 43.55

Kuhusu ufaulu wa masomo, amesema, katika masomo ya Civics, History, Geography, Kiswahili, Phiysics, Chemistry, Chemistry, Biology na Basic Mathematics umepanda ikilinganishwa na mwaka 2015.

Aidha ufaulu kwa somo la English Language pekee ndio ambao umeshuka ikilinganishwa na mwaka 2015.

Somo lililofanyika vizuri zaidi ni Kiswahili ambapo asilimia 90.06 ya wanafunzi wote, wamefaulu na soko lenye ufaulu wa chini zaidi ni Basic Mathematics ambapo asilimia 21.55 wamefaulu.

Mwanafunzi aliyefanya vizuri zaidi ni Teckla Erasmo Haule kutoka Canosa ya Dar es Salaam akifuatiwa na Joseph Fabian Kalabwe wa Kwema Modern ya Shinyanga na Mirable Rayner Matowo wa Canosa ya Dar es Salaam.

Katika wanafunzi 10 bora kitaifa, wanafunzi 9 ni wasichana, na watano kati yao wanatoka Feza Girls.

Matokeo ya wanafunzi 31 yamefutwa baada ya kubainika kuwa walifanya udanganyifu
.


******

SAMAKI WABICHI....

WAKALI WA KITAA WAKIWA MCHEZONI...


MDOGO MDOGO MPAKA MJENGO WA FAMILIA UISHE...

MEZA YA OFISI...

RC MAKALLA AIGIZA WANAFUNZI 214 WALIOKUWA WANASUBIRI MADARASA WANZE MASOMO JUMATATU YA TAREHE 16 MWEZI HUU...

$
0
0
Image may contain: 6 people, people smiling, crowd and outdoor
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mh.Amos Makalla amekagua ukamilishaji wa madarasa kwa wanafunzi 406 waliokuwa wamekwama kuanza masomo kutokana na upungufu wa Madarasa
Kati ya wanafunzi 406 walikosa nafasi kuanza masomo ni 192 madarasa yao yamekamilika na wanafunzi 214 madarasa yao yatakamilika katika siku 14
Hivyo ili wanafunzi 214 wasiendelee kuchelewa ameridhia na kuagiza maabara ambazo zipo na hazijaanza kutumika kwa kukosa Vifaa sasa zitumike kama madarasa kuanzia jumatatu na baada ya madarasa kukamilika tarehe 30 januari wanafunzi hao watatumia madarasa hayo.
Rc.Makalla amezipongeza halmashauri za jiji la Mbeya na Mbeya vijijini kwa kuchangia ukamilishaji madarasa na amewashukuru wananchi na wadau kwa kuchangia ujenzi wa madarasa.

DC HAI AMUACHIA MKURUGENZI WA HALMASHAURI HIYO HATMA YA WATUMISHI WABADHILIFU

$
0
0
 
Na Dixon Busagaga,Hai.

MKUU wa wilaya ya Hai, Gelasius Byakanwa ametoa jukumu kwa mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya hiyo,Yohana Sintoo la kuamua hatma ya watumishi wake watano wanaotajwa katika tuhuma za ubadhilifu wa fedha wakati wa zoezi la utengenezaji wa madawati.

Akiwa ndio mamlaka ya nidhamu kwa watumishi wa halmashauri hiyo,Mkurugenzi Sintoo ndiye mwenye maamuzi ya kuwasimamisha kazi watumishi hao baada ya tume iliyoundwa na mkuu wa wilaya hiyo, Byakanwa kumaliza kazi yake ya uchunguzi dhidi ya watumishi hao na kubaini mapungufu kadhaa.

Akihitimisha taarifa yake wakati wa kikao na watumishi wa halmashauri hiyo,Byakanwa aliagiza taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) kuchunguza na kuchukua hatua dhidi ya watumishi hao akiwemo aliyekuwa kaimu Mkurugenzi ,Mhandisi Kweka.

“Mamlaka ya nidhamu ya watumishi wa Halmashauri ni mkurugenzi pamoja na baraza la madiwani ,lakini mwajiri ni ofisi ya katibu tawala mkoa ,Ofisi hizi mbili ndizo zinazoweza kukaa na kuchukua hatua za kuzuia matukio au vitendo kama hivyo.”alisema Byakanwa.

“Niishauri ofisi ya Katibu tawala mkoa wa Kilimanjaro pamoja na ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Hai ambayo ndio mamlaka ya nidhamu kwa watumishi hao kupima kuhusu hatua za kuchukua dhidi ya watumishi hawa”aliongeza Byakanwa.

Mkuu huyo wa wilaya alisema tuhuma zinazowakabili watumishi hao ,majina yao tumeyahifadhi kwa sasa ni pamoja na kupitisha barua ya malipo bila kujiridhisha kama kuna mkataba wa kutengeneza madawati na kufanya malipo ya fremu za madawati badala ya madawati.

Tuhuma nyingine inaihusu timu ya ukaguzi iliyokiri kukamilika kwa kazi bila ya kuonesha kama walipokea madawati au walienda kukagua kazi ya mzabuni licha ya mzabuni kuomba malipo ya fremu za madawati badala ya Madawati kamili.

Ofisi ya elimu msingi,ofisi ya mkurugenzi,ofisi ya Mhasibu wa Halamshauri na kitengo cha manunuzi pia zinatuhumiwa kushindwa kubaini nyaraka zilizowasilishwa na mzabuni endapo zilikuwa ni kwa ajili ya fremu za Madawati badala ya Madawati kamili.

Katika kikao hicho kilichofanyika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo Byakanwa alisema kampuni iliyopewa zabuni ya kutengeneza madawati ni ya Ujenzi na haijawahi kufanya kazi ya kutengeneza madawati, kuwa na karakana wala vifaa vya uselemala .

Byakanwa alisema kwa malipo yaliyofanyika Halmashauri ilipoteza zaidi ya sh Mil 12 huku akishangazwa na hatua ya mmoja wa watumishi wanaotuhumiwa kuomba malipo badala ya mzabuni.

Akionyesha namna watumishi hao walivyokiuka taratibu Byakanwa alisema taarifa ya uchunguzi inaonyesha Halmashauri iliunda timu ya ukaguzi ambayo katika cheti cha ukaguzi na mapokezi ya bidhaa kinaonyesha bidhaa au madawati yalipelekwa ,Julai 16, 2016 ,siku 12 tangu siku ya mkataba na mzabuni.

“Mmoja w wajumbe wa kamati hiyo ya ukaguzi alikuwa ni mjumbe wa kamati ya kuratibu zoezi la Madawati ,alikuwa na jukumu la kusambaza mbao kwa wazabuni na alikuwa anajua kuwa hajapeleka mbao za kutosha kwa mzabuni ,katika maelezo yake mbele ya tume anakiri kuwa mzabuni hajamaliza kazi kwa sababu Halmashauri haijampa mbao.”alisema Byakanwa.

Alisema mzabuni aliieleza tume kuwa anadaiwa madawati 246 na halmashauri na kuwa amekamilisha kutegeneza madawati 154 na ueleza kua alishindwa kukamilisha kutokana na kukosa mbao kutoka halmashauri.

“June 9,2016 malipo ya Sh Mil 19.2 yakalipwa kwa ajili ya fremu za madawati siyo Madawati.Vocha ya malipo ikasainiwa na DT na kuandaliwa na mtumishi mwingine (jina tunalo) ikakamilisha mchezo.”alisema Byakanwa.

Mkuu huyo wa wilaya alisema kufanya hivyo ilikuwa ni kinyume cha taratibu za malipo kwa kuwa wahusika walipaswa kujiridhisha na nyaraka walizokuwa wakitumia ,kwa nini mzabuni aliamua kudanganya Halmashauri.

Byakanwa aliishauri ofisi ya Katibu tawala mkoa wa Kilimanjaro pamoja na ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Hai ambayo ndio mamlaka ya nidhamu kwa watumishi hao kupima kuhusu hatua za kuchukua dhidi ya watumishi hao.

Kwa upande wake mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Hai,Yahana Sintoo alisema licha ya kwamba amefika wakati zoezi la uchunguzi lina kamilika bado atafanyia kazi taarifa hizo kwa umakini mkubwa ili kujiridhisha na utendajji kazi wa watumishi wa halmashauri hiyo.
Mkuu wa wilaya ya Hai ,Gelasius Byakanwa akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Hai kuhusu ubadhilifu uliofanyika wakati wa zoezi la utengenezaji wa madawati.Kushoto ni Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Yahana Sintoo.
Baadhi ya watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Hai wakiwa katika kikao hicho. 

Mkuu wa wilaya ya Hai,Gelasius Byakanwa akionesha sehemu ya nyaraka ambazo zinaonesha namna baadhi ya watumishi walivyoshiriki kufanya ubadhilifu wa fedha za madawati. 

Mkuu wa wilaya ya Hai,Gelasius Byakanawa (katikati) akiwa na katibu tawala wa wilaya hiyo,Upendo Wela (kulia) pamoja na Mkurugenzi wa Halamshauri ya wilaya hiyo Yohana Sintoo (kushoto). 
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Hai,Yohana Sintoo akizungungunza wakati wa kikao hicho . 

Zoezi la kuchagua mshindi wa tuzo ya ALM 2016 lafungwa, MO Dewji aongoza kwa asilimia 60.8

$
0
0
Jarida la African Leadership limefunga zoezi la kupiga kura kuchagua mshindi wa tuzo ya African Leadership Magazine Person Of The Year 2016, tuzo ambazo Mtanzania Mohammed Dewji alikuwa mmoja kati ya watu nane ambao walikuwa wakiwania.

Baada ya kufungwa kwa zoezi hilo, Mohammed Dewji ambaye pia ni Mkurugenzi wa Makampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL Group) ameibuka mshindi baada ya kuongoza kwa asilimia 60.8.

MO Dewji ameongoza kwa kupata kura nyingi na akifuatiwa na Rais Mstaafu wa Ghana, John Mahama ambaye amepata apata asilimia 38.3.

Kwasasa bado Jarida la African Leadership bado hawajatoa taarifa ni lini watakabidhi tuzo kwa mshindi wa wa tuzo ya African Leadership Magazine Person Of The Year 2016.
Viewing all 39995 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>