Mwili wa mwandishi wa habari za michezo wa gazeti la uhuru na mzalendo Amina Athuman ukisafirishwa asubuhi hii na boti ya kilimanjaro kuelekea Dar es Salaam na kusafirishwa hadi kijijini kwao Lushoto kwa mazishi yanayotarajiwa kufanyika siku ya jumanne mchana. Marehemu alikuwa Zanzibar kikazi akiripoti habari za michezo kombe la Mapinduzi na kumkuta mauti hayo baada ya kujifungua mtoto wa kiume, kwa bahati mbaya mtoto akafariki baada ya kuzaliwa na yeye kupata kifafa cha uzazi na kufariki jana asubuhi. Mwenyenzi mungu ampe kauli thabiti na amsamehe madhambi yake-Ameen
↧
MWILI WA MAREHEMU AMINA ATHUMAN KUWASILI JIJINI DAR ASUBUHI HII NA BAADAE KUSAFIRISHWA KIJIJINI KWAO LUSHOTO KWA MAZISHI
↧
Mwenyekiti wa NEC akagua mwenendo wa Uchaguzi Mdogo kata ya Ngh'ambi
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji (R) Semistocles Kaijage (kushoto) akisalimiana na Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Mpwapwa Bw. Mohamed Maje baada ya kuwasili wilayani Mpwapwa kutembelea kata ya Ngh’ambi inayotarajia kufanya uchaguzi mdogo Januari 22 mwaka huu.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji (R) Semistocles Kaijage (kushoto) akisalimiana na Mkuu wa Polisi wilaya ya Mpwapwa OCD Hussein Mdoe baada ya kuwasili wilayani Mpwapwa kutembelea kata ya Ngh’ambi inayotarajia kufanya uchaguzi mdogo Januari 22 mwaka huu.Katikati ni Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Mpwapwa Bw. Mohamed Maje.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji (R) Semistocles Kaijage (katikati) akiongoza kikao cha kupokea taarifa kuhusu mwenendo wa uchaguzi mdogo wa Kata ya Ngh’ambi unaotarajiwa kufanyika Januari 22 mwaka huu.Kulia kwake ni Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Mpwapwa Bw. Mohamed Maje, Mkuu wa Polisi wilaya ya Mpwapwa OCD Hussein Mdoe na kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Huduma za Kisheria wa NEC Bw. Emmanuel Kawishe, Mkuu wa Kanda ya Kati ya Uchaguzi Bi. Saada Kangeta na Afisa Utumishi wa Tume Athumani Masesa.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji (R) Semistocles Kaijage (katikati) akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Jabir Shekimweri wakati alipomtembelea ofisini kwake kabla ya kutembelea Kata ya Ngh’ambi.Kulia ni Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Mpwapwa Bw. Mohamed Maje.
Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Mpwapwa Bw. Mohamed Maje (aliyesimama) akitoa maelezo ya kumkaribisha Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji (R) Semistocles Kaijage (kulia kwake) baada ya kuwasili kwenye Kata ya Ngh’ambi kufuatilia mwenendo wa uchaguzi mdogo wa diwani wa kata hiyo unaotarajiwa kufanyika Januari 22 mwaka huu.
Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi Kata ya Ngh’ambi James Mkinga (wa pili kulia) akimueleza Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji (R) Semistocles Kaijage (wa pili kushoto aliyekaa) kuhusu mwenendo wa Uchaguzi Mdogo wa Kata hiyo unaotarajiwa kufanyika tarehe 22 Januari mwaka huu.Kushoto ni Mkurugenzi wa Huduma za Kisheria wa NEC Bw. Emmanuel Kawishe, Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Mpwapwa Bw. Mohamed Maje (katikati) na kulia ni Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi wa Kata hiyo Clemence Fugusa.
Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi Kata ya Ngh’ambi James Mkinga (aliyesimama) akitoa taarifa ya mwenendo wa Uchaguzi Mdogo wa kata hiyo.
Mkurugenzi wa Huduma za Kisheria wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw. Emmanuel Kawishe (kushoto) akifafanua jambo kwenye kikao cha kupokea taarifa ya mwenendo wa Uchaguzi Mdogo wa Kata ya Ngh’ambi unaotarajiwa kufanyika Januari 22 mwaka huu.
Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Mpwapwa Bw. Mohamed Maje (kulia) akimueleza jambo Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji (R) Semistocles Kaijage (katikati) na Mkurugenzi wa Huduma za Kisheria wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw. Emmanuel Kawishe baada ya kikao cha kupokea taarifa ya mwenendo wa Uchaguzi Mdogo wa Kata ya Ngh’ambi.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji (R) Semistocles Kaijage (kushoto) akikagua daftari la kudumu la wapiga kura kwenye kituo cha kupigia kura cha Kata ya Ngh’ambi kilichopo kwenye Zahanati ya Ngh’ambi. Kushoto kwake aliyevaa miwani ni Afisa Uchaguzi halmashauri ya wilaya ya Mpwapwa Bi. Martina Batholomeu.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji (R) Semistocles Kaijage (aliyevaa kofia nyeusi) akipokea maelezo kuhusu mabango ya Uchaguzi kutoka kwa Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi Kata ya Ngh’ambi James Mkinga (wa tatu kushoto) wakati alipokuwa akikagua mabango hayo nje ya kituo cha kupigia kura cha Kata ya Ngh’ambi kilichopo kwenye Zahanati ya Ngh’ambi.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji (R) Semistocles Kaijage (kulia) akieleza jambo baada ya kukagua mabango ya Uchaguzi kwenye kituo cha kupigia kura cha kata ya Ngh’ambi.Katikati ni Mkurugenzi wa Huduma za Kisheria wa NEC Bw. Emmanuel Kawishe na kushoto ni Afisa Uchaguzi halmashauri ya wilaya ya Mpwapwa Bi. Martina Batholomeu. Picha na Hussein Makame, NEC.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Mhe. Jaji (R) Semistocles Kaijage amesema kila kitu kiko sawa tayari kwa uchaguzi mdogo wa kumpata diwani wa kata ya Ngh’ambi iliyoko katika halmashauri ya wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma.
Mhe. Jaji (R) Kaijage ameyasema hayo kutokana na kuridhishwa na maandalizi ya uchaguzi mdogo wa kata ya Ngah’ambi baada ya kutembelea na kufuatilia mwenendo wa uchaguzi wa kata hiyo unaotarajiwa kufanyika tarehe 22 Januari mwaka huu.
Akitoa taarifa fupi ya mwenendo wa uchaguzi mdogo wa kata hiyo, Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Mpwapwa Bw. Mohamed Maje alisema karibu vifaa vyote kwa ajili ya uchaguzi huo vimepokelewa na kampeni za uchaguzi huo zinaendelea kwa amani na utulivu.
Alisema baada ya uteuzi wa wagombea kufanyika Desemba 22 mwaka 2016 wagombea wanne kutoka vyama vya ADC, CCM, CHADEMA na CUF waliteuliwa ambao ni David Mazengo, Richard Kaleme, Leornard Majenda na Hassan Kiuka, mtawalia.
Kwa upande wa pingamizi kwa wagombea, Bw. Maje alisema walipokea pingamizi kutoka vyama vya CHADEMA na CCM ambapo mgombea wa CHADEMA alipinga uteuzi wa mgombea wa CCM kwa madai kuwa si mkazi wa halmashauri husika.
“Pingamizi hili lilitolewa uamuzi na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya kata kwa kutupilia mbali madai hayo baada ya uthibitisho kuwa mgombea wa CCM ni mkazi halali wa halmashauri husika.Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo pia alikubaliana na uamuzi wa wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya kata.” alisema Bw. Maje na kuongeza kuwa:
“Mgombea wa chama cha CCM alipinga uteuzi wa mgombea wa chama cha CHADEMA kuwa fomu ya uteuzi namba 8 C sehemu C na D imesainiwa na mtu ambaye si Katibu wa chama husika wa mkoa au Wilaya”
“Pingamizi hili pia lilitolewa uamuzi na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya kata kwa kutupilia mbali madai hayo baada ya uthibitisho wa maandishi kuwa aliyesaini ndiye Katibu wa chama husika wilaya ya Mpwapwa.Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo alikubaliana na uamuzi huo”
Aliongeza kuwa kamati za maadili kwa ngazi ya jimbo na kata zinafanya kazi na kwamba hadi kufukia Januria 13 kamati hazikupokea malalamiko yoyote kutoka kwenye vyama vinavyoshiriki uchaguzi mdogo kata hiyo.
Alisema wanatarajia kutoa mafunzo kwa makarani waongozaji na wasimamizi wa vituo vya kupigia kura tarehe 18 na 19 Januari na wameshaandaa vituo 12 vya kupigia kura vyenye wapiga kura 4123.
Kwa upande wa Mkuu wa Jeshi la Polisi wilaya ya Mpwapwa OCD Hussein Mdoe alisema hadi sasa kampeni zinafanyika kwa kuzingatia taratibu za nchi na taratibu za uchaguzi na hakuna vurugu zozote zilizojitokeza.
Hata hivyo aliwakumbusha wananchi kuwa jukumu la ulinzi na usalama ni la kila mwananchi na anaamini wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi wa kata na kamati za maadili zitawakumbusha wananchi jukumu hilo.
Kwa upande wa Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi Kata ya Ngh’ambi Bw. James Mkinga alisema maandalizi yote ya uchaguzi yamekamilika na wameshabandika daftari la kudumu la wapiga kura kwenye vituo vya kupigia kura.
Mkurugenzi wa Huduma za Kisheria wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw. Emmanuel Kawishe aliwakumbusha wasimamizi wasaidizi kuhakikisha Sheria, kanuni na taratibu zote za Uchaguzi zinazingatiwa.
Aliwataka wawakumbushe wananchi kufika kwenye vituo vya kupigia kura kwa wakati ili kuepuka kukosa haki ya kupiga kura kwa sababu ya kuchelewa kufika kituoni.
“Hakikisha mnavikumbusha vyama vyote kuondoa mabango ya kampeni yaliyopo kituoni siku ya kupiga kura na kama hawawezi kuyaondoa uwafahamishe kwamba utayaondoa kwa sababu sheria inakataza” alisema Bw. Kawishe na kuongeza kuwa:
“Wakumbusheni wasimamizi wa vituo kufuata Sheria, kanuni na taratibu na yeyote atakayekiuka Sheria Tume ya Taifa ya Uchaguzi haitasita kumchukulia hatua za Kisheria”
Aliwakumbusha kuhakikisha kuwa mawakala wa vyama wanafuata taratibu zote inapotokea chama kinataka kumbadilisha wakala kwenye kituo cha kupigia kura.
Naye Mkuu wa Kanda ya Kati ya Uchaguzi kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bi. Saada Kangeta aliwakumbusha wasimamizi wasaidizi kuwa iwapo litajitokeza jambo linaloweza kuchelewesha matokeo kama kufanya uamuzi ya kura za mgogoro wawafahamishe wananchi ili kuepuka vurugu.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Mhe. Jaji (R) Semistocles Kaijage amesema kila kitu kiko sawa tayari kwa uchaguzi mdogo wa kumpata diwani wa kata ya Ngh’ambi iliyoko katika halmashauri ya wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma.
Mhe. Jaji (R) Kaijage ameyasema hayo kutokana na kuridhishwa na maandalizi ya uchaguzi mdogo wa kata ya Ngah’ambi baada ya kutembelea na kufuatilia mwenendo wa uchaguzi wa kata hiyo unaotarajiwa kufanyika tarehe 22 Januari mwaka huu.
Akitoa taarifa fupi ya mwenendo wa uchaguzi mdogo wa kata hiyo, Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Mpwapwa Bw. Mohamed Maje alisema karibu vifaa vyote kwa ajili ya uchaguzi huo vimepokelewa na kampeni za uchaguzi huo zinaendelea kwa amani na utulivu.
Alisema baada ya uteuzi wa wagombea kufanyika Desemba 22 mwaka 2016 wagombea wanne kutoka vyama vya ADC, CCM, CHADEMA na CUF waliteuliwa ambao ni David Mazengo, Richard Kaleme, Leornard Majenda na Hassan Kiuka, mtawalia.
Kwa upande wa pingamizi kwa wagombea, Bw. Maje alisema walipokea pingamizi kutoka vyama vya CHADEMA na CCM ambapo mgombea wa CHADEMA alipinga uteuzi wa mgombea wa CCM kwa madai kuwa si mkazi wa halmashauri husika.
“Pingamizi hili lilitolewa uamuzi na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya kata kwa kutupilia mbali madai hayo baada ya uthibitisho kuwa mgombea wa CCM ni mkazi halali wa halmashauri husika.Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo pia alikubaliana na uamuzi wa wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya kata.” alisema Bw. Maje na kuongeza kuwa:
“Mgombea wa chama cha CCM alipinga uteuzi wa mgombea wa chama cha CHADEMA kuwa fomu ya uteuzi namba 8 C sehemu C na D imesainiwa na mtu ambaye si Katibu wa chama husika wa mkoa au Wilaya”
“Pingamizi hili pia lilitolewa uamuzi na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya kata kwa kutupilia mbali madai hayo baada ya uthibitisho wa maandishi kuwa aliyesaini ndiye Katibu wa chama husika wilaya ya Mpwapwa.Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo alikubaliana na uamuzi huo”
Aliongeza kuwa kamati za maadili kwa ngazi ya jimbo na kata zinafanya kazi na kwamba hadi kufukia Januria 13 kamati hazikupokea malalamiko yoyote kutoka kwenye vyama vinavyoshiriki uchaguzi mdogo kata hiyo.
Alisema wanatarajia kutoa mafunzo kwa makarani waongozaji na wasimamizi wa vituo vya kupigia kura tarehe 18 na 19 Januari na wameshaandaa vituo 12 vya kupigia kura vyenye wapiga kura 4123.
Kwa upande wa Mkuu wa Jeshi la Polisi wilaya ya Mpwapwa OCD Hussein Mdoe alisema hadi sasa kampeni zinafanyika kwa kuzingatia taratibu za nchi na taratibu za uchaguzi na hakuna vurugu zozote zilizojitokeza.
Hata hivyo aliwakumbusha wananchi kuwa jukumu la ulinzi na usalama ni la kila mwananchi na anaamini wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi wa kata na kamati za maadili zitawakumbusha wananchi jukumu hilo.
Kwa upande wa Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi Kata ya Ngh’ambi Bw. James Mkinga alisema maandalizi yote ya uchaguzi yamekamilika na wameshabandika daftari la kudumu la wapiga kura kwenye vituo vya kupigia kura.
Mkurugenzi wa Huduma za Kisheria wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw. Emmanuel Kawishe aliwakumbusha wasimamizi wasaidizi kuhakikisha Sheria, kanuni na taratibu zote za Uchaguzi zinazingatiwa.
Aliwataka wawakumbushe wananchi kufika kwenye vituo vya kupigia kura kwa wakati ili kuepuka kukosa haki ya kupiga kura kwa sababu ya kuchelewa kufika kituoni.
“Hakikisha mnavikumbusha vyama vyote kuondoa mabango ya kampeni yaliyopo kituoni siku ya kupiga kura na kama hawawezi kuyaondoa uwafahamishe kwamba utayaondoa kwa sababu sheria inakataza” alisema Bw. Kawishe na kuongeza kuwa:
“Wakumbusheni wasimamizi wa vituo kufuata Sheria, kanuni na taratibu na yeyote atakayekiuka Sheria Tume ya Taifa ya Uchaguzi haitasita kumchukulia hatua za Kisheria”
Aliwakumbusha kuhakikisha kuwa mawakala wa vyama wanafuata taratibu zote inapotokea chama kinataka kumbadilisha wakala kwenye kituo cha kupigia kura.
Naye Mkuu wa Kanda ya Kati ya Uchaguzi kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bi. Saada Kangeta aliwakumbusha wasimamizi wasaidizi kuwa iwapo litajitokeza jambo linaloweza kuchelewesha matokeo kama kufanya uamuzi ya kura za mgogoro wawafahamishe wananchi ili kuepuka vurugu.
↧
↧
SENEGAL YAWA TIMU YA KWANZA KUPATA USHINDI MICHUANO YA AFCON 2017
Na Bakari Issa Madjeshi
Timu ya Taifa ya Senegal maarufu kama Simba wa Teranga hatimaye imekuwa timu ya kwanza kupata ushindi katika mfululizo wa mechi za hatua ya makundi ya michuano ya Mataifa ya Afrika kwa mwaka 2017.
Senegal inayoshiriki michuano hiyo inayoendelea nchini Gabon imefanikiwa kupata ushindi wa bao 2-0 dhidi ya Tunisia ikiwa ni mchezo wa kundi B ambapo kabla yake kulitanguliwa kwa mchezo wa kundi hilo baina ya Algeria dhidi ya Zimbabwe ambao walitoka sare ya bao 2-2.
Katika mchezo huo,Senegal ilifanikiwa kupata bao la kuongoza dakika ya 10 kupitia mkwaju wa penalti uliokwamishwa wavuni na Mshambuliaji anaeichezea Liverpool ya Uingereza,Sadio Mane baada ya Kiungo wake,Cheikhou Kouyate kuangushwa katika eneo la hatari.
Dakika 30 ya mchezo,Simba wa Teranga walipachika bao la pili kupitia kwa Mlinzi wake,Kara Mbodji baada yakumalizia mpira uliokufa uliopigwa na .
Licha ya mabao hayo kupatikana katika Kipindi cha kwanza,Tunisia walionekana kuja juu zaidi kipindi cha pili kutaka kusawazisha mabao hayo lakini mbinu zao hazikiwezekana.
Hata hivyo mpaka dakika 90 za mchezo zinamalizika,Senegal waliweza kutoka kifua mbele kwa mabao yake 2-0 dhidi ya Waarabu hao.
Tangu kufunguliwa kwa michuano hiyo Januari 14 michezo ya kundi A ilifanyika kwa wenyeji,Gabon kulazimishwa sare ya bao 1-1 na Guinea Bissau kabla ya Cameroon kwenda sare ya 1-1 pia na Bukina Faso 'Wabukinabe'
↧
VIDEO YA NGOMA MPYA MTAANI: Roma FT Moni - Usimsahau Mchizi (Official Video)
↧
MAGARI YA SERIKALI YENYE MAKOSA KUTOZWA FAINI
Kamanda wa Polisi Kikosi cha usalama Barabarani, Mohamed Mpinga amesema kumekuwepo na malalamiko mengi kuwa magari ya serikali yanapendelewa hivyo kutawekwa kamera katika barabara kuu ili kupiga picha magari yote yenye makosa na kuadhibiwa.
Kamanda Mpinga ameyasema hayo katika mahojiano maalumu na Gazeti la Mwananchi na kusema kwa kipindi cha January hadi Disemba mwaka jana makosa yaliyotokea nchini ni milioni 1.9.
“Kamera hizo hazitajali ni gari la waziri, serikali, wala Mpinga na zitapiga picha gari zote kama ilivyo kwa msemo wa kupanga na kuchagua,”amesema Mpinga.
Aidha Mpinga alisema kuwa makosa hayo yalitokana na ulevi, mwendo wa kasi,kupita katika taa nyekundu,kukatisha safari na kutovaa kofia ngumu.
↧
↧
MTANZANIA AIBUKA KIDEDEA KWENYE MARATHON INDIA
Alphonce Simbu
Mtanzania Alphonce Simbu, amefanikiwa kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania kwenye mbio ndefu za Mumbai Marathon ya mwaka huu huku akiwapiku Mkenya Joshua Kipkorir pamoja na wakimbiaji wengine wazoefu kutoka mabara mbalimbali.
Mashindano hayo yajulikanayo kama Standard Chartered Mumbai Marathon hufanyika Jumapili ya tatu ya mwezi Januari katika jiji la Mumbai nchini India na yanaaminika kuwa ni mbio kubwa kabisa barani Asia kwa idadi ya washiriki wanaomaliza mbio.
Mwanariadha huyo ambaye yupo chini ya udhamini wa kampuni ya Multichoice Tanzania, aliibuka mshindi baada ya kutumia muda wa saa 2:09:28 muda ambao ni mzuri kwa mbio za aina hiyo.
Simbu amesema kuwa anaamini ushindi huo umesababishwa na maandalizi aliyoyafanya.
Amesema ushindi huo kwake ni changamoto kwa mashindano mengine makubwa na kwamba huo ni mwanzo tu. Amesema ushindi huo siyo wake peke yake au wathamini wake , bali ni ushindi wa Taifa zima la Tanzania.
Kwa upande wa Serikali, Waziri wa Habari, Utamaduni , Sanaa na Michezo, Mh. Nape Nnauye amempongeza kupitia kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter akisema , “Tumefanikiwa tena, hongera Simbu, hongera RT (Chama cha Riadha Tanzania), asanteni Multichoice Tanzania kwa kumsapoti. Mungu ibariki Tanzania.”
Mkuu wa Mahusiano wa Multichoice Tanzania Johnson Mshana amesema Multichoice imefurahi sana kwa matokeo huku akisisitiza kuendelea kumdhamini Simbu kwa mujibu wa makubaliano yao, ili kuhakikisha anaendelea kufanya vyema na kuliletea taifa sifa kubwa.
“Tulichukua jukumu la kumdhamini Simbu katika mazoezi na maandalizi yake kwa kipindi cha mwaka mzima, kwani tunafahamu fika kuwa mazoezi na maandalizi ndiyo siri kubwa ya mafanikio katika mchezo wowote.
Alisema Mshana na kuongeza “Dhamira yetu kubwa ni kuinua vipaji na kulirejesha taifa letu kwenye ramani ya dunia katika ulingo wa michezo na burudani”
Alphonce anatarajiwa kurejea Tanzania Jumatatu hii.
↧
MWIJAGE AZINDUA FURSA ZA WANAWAKE KUWEKEZA SEKTA YA KILIMO
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage,akizungumza na viongozi wa Asasi isiyo ya Kiserikali ya Wasaa-Tanzania Chapter inayojishulisha na bidhaa za kilimo kusini mwa jangwa la sahara, wakati wa ufunguzi wa semina ya kuwajengea uwezo wanawake katika fursa za uwekezaji wa viwanda iliyofanyika katika ukumbi wa 5s uliyopo eneo la Bahari beach Ununio,Dar es Salaam jana.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage,akiongoza na Rais wa Asasi isiyo ya Kiserikali ya Wasaa-Tanzania Chapter inayojishulisha na bidhaa za kilimo kusini mwa jangwa la sahara, Margaret Chacha, wakati wa ufunguzi wa semina ya kuwajengea uwezo wanawake katika fursa za uwekezaji wa viwanda iliyofanyika katika ukumbi wa 5s uliyopo eneo la Bahari beach Ununio,Dar es Salaam jana.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage, akizungumza katika ufunguzi wa semina ya kuwajengea uwezo wanawake katika fursa za uwekezaji wa viwanda iliyoandaliwa na Asasi isiyo ya Kiserikali ya Wasaa-Tanzania Chapter inayojishulisha na bidhaa za kilimo Kusini mwa Jangwa la Sahara iliyofanyika katika ukumbi wa 5s uliyopo eneo la Bahari beach Ununio,Dar es Salaam jana.
Mjumbe na Mjasiriamali wa Asasi isiyo ya Kiserikali ya Wasaa-Tanzania Chapter Mmiliki wa Ukumbi wa 5s, Salome Kaselwa, akizungumzana waandishi wa habari kuhusu fursa za uwekezaji katika semina ya kuwajengea uwezo wanawake katika uwekezaji wa viwanda.
Mkurungezi wa Idara ya Viwanda na Biashara ndogo wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Dk. Consolatha Ishebabi, akizungumza wakati wa semina ya kuwajengea uwezo wanawake katika fursa za uwekezaji wa viwanda Ununio,Dar es Salaam jana.
Mwanasiasa Mkongwe nchini, Getrude Mongera, akizungumza wakati wa semina ya kuwajengea uwezo wanawake katika fursa za uwekezaji wa viwanda iliyoandaliwa Asasi isiyo ya Kiserikali ya Wasaa-Tanzania Chapter katika ukumbi wa 5s uliyopo eneo la Bahari beach Ununio,Dar es Salaam jana.
Rais wa Asasi isiyo ya Kiserikali ya Wasaa-Tanzania inayojishulisha na bidhaa za kilimo Kusini mwa Jangwa la Sahara Chapter, Margret Chacha, akizungumza wakati wa semina ya kuwajengea uwezo wanawake katika fursa za uwekezaji wa viwanda iliyoandaliwa iliyofanyika katika ukumbi wa 5s uliyopo eneo la Bahari beach Ununio,Dar es Salaam jana.
Mwenyekiti wa Asasi isiyo ya Kiserikali ya Wasaa-Tanzania Chapter inayojishulisha na bidhaa za kilimo Kusini mwa Jangwa la Sahara , Dk. Fatma Mrisho, akizungumza katika semina ya kuwajengea uwezo wanawake katika fursa za uwekezaji wa viwanda iliyoandaliwa iliyofanyika katika ukumbi wa 5s uliyopo eneo la Bahari beach Ununio,Dar es Salaam jana.
↧
WAZIRI MKUU MAJALIWA AZINDUA SAFARI ZA NDEGE ZA ATCL KATI YA DAR NA DODOMA
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea mfano wa Boarding Pass kutoka kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mahandisi Edwin Ngonyani kabla ya kusafiri kwa ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) kutoka uwanja wa ndege wa Julius Kambarage Nyerere, Dar es salaam kwenda Dodoma Januari 16, 2017. Alikuwa akizindua safari za ndege za shirika hilo kati ya viwanja viwili hivyo.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na wafanyakazi wa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) kabla ya kupanda ndege ya Shirika hilo kwenye uwanja wa Ngege wa Julius Kambarage Nyerere kwenda Dodoma ikiwa ni uzinduzi wa safari za ndege za ATCL kati ya viwanja viwili hivyo, Januari 16, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisafiri kwa ndege ya Bombardier Q400 ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) kutoka uwanja wa ndege wa Julius Kambarage Nyerere kwenda Dodoma Januari 16, 2017. Alikuwa akizindua safari za ndege za ATCL katika viwanja viwili hivyo. Kushoto kwake ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Leonard Chamuriho.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia viongozi na wananchi wa Dodoma baada ya kutua kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma akitoka uwanja wa ndege wa Julius Kambarage Nyerere jijini Dar es salaam Januari 16, 2017 ikiwa ni uzinduzi wa Safari za ndege za Shirika hilo kati ya viwanja viwili hivi.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma akitoka uwanja wa ndege wa Julius Kambarage Nyerere jijini Dar es salaam ikiwa ni uzinduzi wa safari za ndege za Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) Januari 16, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma akitoka uwanja wa ndege wa Julius Kambarage Nyerere jijini Dar es salaam ikiwa ni uzinduzi wa safari za ndege za Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) kati ya viwanja viwili hivyo, Januari 16, 2016. Wapili kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijan, Ajira na Watu Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mtendaji Mkuu wa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL), Kapteni Richard Shaidi baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma akitoka uwanja wa ndege wa Julius Kambarage Nyerere jijini Dar es salaam ikiwa ni uzinduzi wa safari za ATCL kati ya viwanja viwili hivyo, Januari 16, 2017. Kulia kwake ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Leonard Chamuriho. Wapili kushoto ni Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Anthony Mavunde na kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Dodoma, Christina Mndeme.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na wafanyakazi wa Shirika la Ngege ya Tanzania (ATCL) baada ya kutua kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma akitoka uwanja wa ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam ikiwa ni uzinduzi wa safari za ndege za ATCL kati aya viwanja viwili hivyo, Januari 16, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri Mkuu Mstaafu, John Malecela baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma akitoka uwanja wa ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam ikiwa ni uzinduzi wa safari za ndege za ATCL kati aya viwanja viwili hivyo, Januari 16, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Spika wa Bunge, Job Ndugai baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma akitoka uwanja wa ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam ikiwa ni uzinduzi wa safari za ndege za ATCL kati aya viwanja viwili hivyo, Januari 16, 2017.
Mtendaji Mkuu wa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL), Kapteni Richard Shaidi akizungumza katika uzinduzi wa safari za ndege za ATCL kati ya Uwnja wa Julius Kambarage Nyerere na Dodoma,mjini Dodoma Januari 16, 2017. Uzinduzi huo ulifanywa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana akizungumza katika uzinduzi wa safari za ndege za ATCL kati ya Uwnja wa Julius Kambarage Nyerere na Dodoma,mjini Dodoma Januari 16, 2017. Uzinduzi huo ulifanywa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma .
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama, akizungumza katika uzinduzi wa safari za Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) kati ya uwanja wa ndege wa Julius Kambarage Nyerere na Dodoma Januari 16, 2017.
Waziri Mkuu, Mstaafu John Malecela akizungumza katika uzinduzi wa safari za ndege za ATCL kati ya Uwnja wa Julius Kambarage Nyerere na Dodoma,mjini Dodoma Januari 16, 2017. Uzinduzi huo ulifanywa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipozindua safari za ndege za Shirika la Ndege la Tanzania kati ya uwanja wa Julius Kambarage Nyerere na Dodoma katika hafla iliyofanyika kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma Januari 16, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
↧
NCHI HAIJAKUMBWA NA BAA LA NJAA-MAJALIWA
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema nchi haijakumbwa na baa la njaa na amewataka Watanzania utosikiliza kampeni za upotoshwaji zinazofanywa na baadhi ya wafanyabiasha kuhusu hali ya chakula kwani si za kweli bali ni za uzushi zenye lengo la kupandisha bei za vyakula.
Amesema Serikali ndio yenye jukumu la kutoa taarifa za kuwepo kwa njaa ama kutokuwepo na kwamba taarifa zinazosambazwa za kuwepo kwa baa la njaa nchini hazina ukweli wowote na Serikali inawahakikishia wananchi kuwepo kwa usalama wa chakula.
Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Jumatatu, Januari 16, 2017) wakati akizungumza na waandishi wa habari mkoani hapa mara baada ya kuzindua safari za ndege za Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) kutoka Dar es Salaam kwenda Dodoma, ambapo amesisitiza kwamba hali ya upatikanaji chakula nchini ni tofauti na inavyoelezwa na baadhi ya vyombo vya habari.
Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo baada ya kutolewa kwa taarifa katika vyombo mbalimbali vya habari kuhusu kuwepo kwa baa la njaa nchini jambo ambalo si la kweli. Amewataka wananchi kuwa watulivu na jambo hilo likitokea Serikali itatoa taarifa.
“Mwaka jana nchi ilikuwa na akiba ya chakula cha zaidi ya tani milioni tatu hali iliyopelekea baadhi ya Wabunge na wafanyabiashara kuomba kibali cha kuuza nafaka nje ya nchi, ambapo Serikali ilitoa kibali hicho baada ya kujiridhisha kuwepo kwa akiba ya kutosha ya chakula,” amesema.
Amesema baada ya kutolewa kwa kibali hicho tani milioni 1.5 ziliuzwa nje ya nchi na
Kiasi cha tani milioni 1.5 zilizobaki zilihifadhiwa kama akiba ambapo tayari wameruhusu ziuzwe hapa nchini ili kupunguza kupanda kwa bei za vyakula nchini.
“Naomba wananchi msiwe na wasiwasi juu ya hali ya chakula nchini. Msisikilize kelele zinazopigwa na watu mbalimbali pamoja kwenye baadhi ya vyombo vya habari yakiwemo magazeti kwani taarifa hizo si za kweli. Chakula kipo cha kutosha licha ya mvua kusuasua katika baadhi ya maeneo nchini,” amesema.
Hata hivyo Waziri Mkuu amesema kuwa kwa sasa mvua zimeanza kunyesha katika maeneo mbalimbali nchini, hivyo amewaomba wananchi kuzitumia kwa kulima mazao ya muda mfupi yanayostahimili ukame.
Waziri Mkuu amesema kwamba endapo kutatokea uhaba wa chakula nchini, Serikali itatoa utaratibu wa namna ya upatikanaji wa chakula kwa wananchi wake. Kuhusu kupanda wa bei ya vyakula katika baadhi ya masoko amesema inatokana na kuwepo kwa uhaba wa chakula katika nchi jirani.
Aidha, Waziri Mkuu amesema kwamba Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, itatoa taarifa kuhusiana na hali halisi ya chakula nchini kwa sasa na pia itatoa taarifa kuhusu hali ya mvua ili Watanzania waweze kupata ukweli wa hali ilivyo.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 980,
DODOMA.
JUMATATU, JANUARI 16, 2017.
↧
↧
MWILI WA MAREHEMU AMINA ATHUMANI WAAGWA NYUMBANI JIJINI DAR
Baadhi ya waumini wa dini ya Kiislam wakiusalia mwili wa aliyekuwa mwandishi wa habari wa Kampuni ya Uhuru Publications, marehemu Amina Athumani nyumbani kwao Kipunguni A jijini Dar es Salaam jana, kabla ya kusafirishwa mkoani Tanga kwa mazishi yanayofanyika leo. (Picha na Francis Dande).
Baadhi ya waombolezaji wakiwa wamebeba jeneza lililokuwa na mwili wa aliyekuwa mwandishi wa habari wa Kampuni ya Uhuru Publications kabala ya kusafiriswa mkoani Tanga kwa mazishi.
Meneja wa rasilimali Watu wa Kampuni ya Uhuru Publications akisoma salama za rambiorambi za kampuni hiyo.
Mkwe wa marehemu.
Baadhi ya waombolezaji.
Waombolezaji wakiwa msibani.
Mwili wa marehemu ukitolewa nyumbani kwao Kipunguni A.
↧
WAFAMASIA WAASWA KUFANYA KAZI KWA MAADILI
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Msajili wa Baraza la Famansia nchini, Elizabeth Shekalaghe amesema maduka yote ya famasi yanatakiwa kuwa na mtaalam wa famasia.
Akizungumza katika semina ya utoaji leseni kwa wafamasia pamoja na miongozo, amesema wafamasia wanafanya kazi za maisha ya binadamu hivyo kuwa na duka la famasi bila kuwa fani ya famasia ni kosa kisheria.
Elizabeth amesema wafamasia lazima wafanye kazi kwa maadili yaliyowekwa na watakaokwenda kinyume baraza hilo litachukua hatua.
Elizabeth amesema kwa sasa nchi hii inapoelekea kwenye sera ya Viwanda ni fursa kwa wafamasia kuungana kwa kuwa kiwanda cha kuzalisha dawa.
Aidha amesema sheria inataka kila duka la famasi kuwa na mfamasia mmoja. Amesema soko la wafamasia ni kubwa hivyo wanahumuimu sana serikalini pamoja sekta binafsi. Elizabeth amesema mwaka 2013 walikuwa na wafamasia 350 na kufikia mwaka jana wamefikia wafamasia 1400.
Msajili wa baraza la Famasia, Elizabeth Shekalaghe akizungumza katika semina ya kuwajengea uwezo wafamsia iliyofanyika ukumbi wa. TFDA ,jijini Dar es Salaam.
Wafamasia wakila kiapo
Sehemu ya wafamasia wakiwa katika semina.Picha na Emmanuel Massaka, Globu ya Jamii .
↧
MBUNGE WA TANGA AWAOKOA ASKARI WA JIJI LA TANGA NA KIPIGO KUTOKA KWA WASAFIRISHAJI
Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga,Mhina Mustapha Selebosi mwenye miwani na tisheti akizungumza na wasafirishaji wanaofanya shughuli zao kati ya Mombasa nchini Kenya kuhusu kuwataka kuhamia eneo la stendi mpya ya kange kwa ajili ya kutoa huduma zao kulia mwenye kofia ni Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaj Mussa Mbaruku.
Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga, Mhina Mustapha Selebosi mwenye miwani na tisheti akizungumza na wasafirishaji wanaofanya shughuli zao kati ya Mombasa nchini Kenya kuhusu kuwataka kuhamia eneo la stendi mpya ya kange kwa ajili ya kutoa huduma zao katikati mwenye kofia ni Mbunge wa Jimbo la Tanga,Alhaj Mussa Mbaruku
Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga,Alhaj Mhina Mustapha Selebosiakisisitiza jambo kwa wasafirishaji hao kulia kwenye kofia ni Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaji Mussa Mbaruku
MBUNGE wa Jimbo la Tanga (CUF) alhaj Mussa Mbaruku jana amelazimikakuingilia kati na kuwaokoa askari wa Jiji la Tanga waliotaka kupigwana wafanyabiashara wa magari yaendayo Mombasa nchini Kenya kwa madaiya kukamata magari yanayotakiwa kuhamia stendi ya kange na kuwatoza
faini bila ya kuwa na mashine za EFDs.
Askari wa Jiji la Tanga ambao walinusurika kipigo hicho na kumlazimuMbunge huyo kuwaingilia kati na kuwaondoa eneo hilo ni Timime Makasina Emanuel Lyimo ambao walikuwa tayari wamezingizwa na wafanyabiasharahao wakijiandaa kuwatembezea mkongoto.
Magari hayo yalikuwa yamepakiwa kwenye eneo la barabara 10 karibu naAssad Hotel ambapo kumekuwa kukipakiwa magari yanayoelekea Mombasanchini Kenya ambapo askari hao walidaiwa kukamata moja ya garilinaloelekea mjini Mombasa na kulitaka kulitoza faini.
Baada ya kuwepo na kadhia hiyo ilimlazimu Mbunge huyo ambaye yupomkoani Tanga mapumziko ya mwishoni mwa wiki kabla ya kwenda mkoaniDodoma kuendelea na vikao vya kamati aliamua kufika eneo la tukio nakuwachukua askari hao kwa gari lake na kuwapeleka mpaka kwenye ofisizao zilizopo Kata ya Nguvumali Jijini Tanga.
Akizungumza na wasafirishaji hao,Mbunge huyo aliwataka kuwawatulivu kwani suala hilo linajadilika na huenda likapatiwa ufumbuzikutokana na vikao vya baraza la madiwani ambavyo vinatarajiwa kuketihivi karibuni mjini hapa.
Aidha pia Mbunge huyo alishtusha na kitendo cha askari hao kuchukuaushuru bila ya kutumia mfumo wa kieletroniki jambo ambalo ni kunyumena utaratibu wa serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Magufuli.
Hata hivyo askari, Timime Makasi ambaye ni askari wa Jiji ambayealisema wao wanafanya kazi chini ya Halmashauri ya Jiji hilo nawanatekeleza agizo hilo kama walivyoelekezwa ya kukamata gari zoteambazo zinatakiwa kupaki kwenye stendi kuu ya Kange.
Alisema kufuatia agizo hilo la halmashauri la kuzikamata gari hizo naatakae kwenda kinyume atatakiwa kutozwa faini ya shilingi 50,000 jambolililozua utata baada ya askari hao kuonekana kutokuwa na mashine zakielektroniki.
Aidha pia mmoja wa wamiliki wa magari yanayofanya safari zake za TangaMombasa Mohammed Nassor alisema kuwa swala liliwashitua zaidi nikutokuwepo na mashine hizo za risiti kama Serikali ilivyoelekeza jamboambalo lilitaka kuzua mzozo baina ya wafanyabiashara na askari hao.
Akizungumzia sakata hilo, Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga,Alhaj MustaphaSelebosi alisema halmashauri ina uhaba wa mashine za EFDs nahawaruhusu askari hao wa Jiji kuchukua ushuru bila kuwepo kwa mashinehizo.
Alisema wanachotakiwa kukifanya askari hao ni kulikamata gari nakulipeleka depo ya Halmashauri ambao ndio kunafanyika taratibu zakutozwa faini kwa mfumo wa mashine za EFDs
faini bila ya kuwa na mashine za EFDs.
Askari wa Jiji la Tanga ambao walinusurika kipigo hicho na kumlazimuMbunge huyo kuwaingilia kati na kuwaondoa eneo hilo ni Timime Makasina Emanuel Lyimo ambao walikuwa tayari wamezingizwa na wafanyabiasharahao wakijiandaa kuwatembezea mkongoto.
Magari hayo yalikuwa yamepakiwa kwenye eneo la barabara 10 karibu naAssad Hotel ambapo kumekuwa kukipakiwa magari yanayoelekea Mombasanchini Kenya ambapo askari hao walidaiwa kukamata moja ya garilinaloelekea mjini Mombasa na kulitaka kulitoza faini.
Baada ya kuwepo na kadhia hiyo ilimlazimu Mbunge huyo ambaye yupomkoani Tanga mapumziko ya mwishoni mwa wiki kabla ya kwenda mkoaniDodoma kuendelea na vikao vya kamati aliamua kufika eneo la tukio nakuwachukua askari hao kwa gari lake na kuwapeleka mpaka kwenye ofisizao zilizopo Kata ya Nguvumali Jijini Tanga.
Akizungumza na wasafirishaji hao,Mbunge huyo aliwataka kuwawatulivu kwani suala hilo linajadilika na huenda likapatiwa ufumbuzikutokana na vikao vya baraza la madiwani ambavyo vinatarajiwa kuketihivi karibuni mjini hapa.
Aidha pia Mbunge huyo alishtusha na kitendo cha askari hao kuchukuaushuru bila ya kutumia mfumo wa kieletroniki jambo ambalo ni kunyumena utaratibu wa serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Magufuli.
Hata hivyo askari, Timime Makasi ambaye ni askari wa Jiji ambayealisema wao wanafanya kazi chini ya Halmashauri ya Jiji hilo nawanatekeleza agizo hilo kama walivyoelekezwa ya kukamata gari zoteambazo zinatakiwa kupaki kwenye stendi kuu ya Kange.
Alisema kufuatia agizo hilo la halmashauri la kuzikamata gari hizo naatakae kwenda kinyume atatakiwa kutozwa faini ya shilingi 50,000 jambolililozua utata baada ya askari hao kuonekana kutokuwa na mashine zakielektroniki.
Aidha pia mmoja wa wamiliki wa magari yanayofanya safari zake za TangaMombasa Mohammed Nassor alisema kuwa swala liliwashitua zaidi nikutokuwepo na mashine hizo za risiti kama Serikali ilivyoelekeza jamboambalo lilitaka kuzua mzozo baina ya wafanyabiashara na askari hao.
Akizungumzia sakata hilo, Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga,Alhaj MustaphaSelebosi alisema halmashauri ina uhaba wa mashine za EFDs nahawaruhusu askari hao wa Jiji kuchukua ushuru bila kuwepo kwa mashinehizo.
Alisema wanachotakiwa kukifanya askari hao ni kulikamata gari nakulipeleka depo ya Halmashauri ambao ndio kunafanyika taratibu zakutozwa faini kwa mfumo wa mashine za EFDs
↧
WAZIRI NAPE AFANYA ZIARA TBC
Makamu Mwenyekiti Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) Bw. William Kalaghe Akimueleza jambo Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Nape Nnauye alipofanya ziara na kuongea na watumishi wa Shirika hilo leo Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Taifa (TBC) Dkt. Ayoub Rhioba akimueleza jambo Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Nape Nnauye wakati alipokutana na uongozi wa Shirika hilo wakati wa ziara na kuongea na watumishi wa Shirika hilo leo Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Nape Nnauye akiongea na uongozi wa Shirika la Utangazaji Taifa (TBC) alipofanya ziara ya kuongea na watumishi wa Shirika hilo leo Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Nape Nnauye akitembelea maeneo mbalimbali ya studio za Shirika la Utangazaji Taifa (TBC) wakati wa ziara katika shirika hilo leo Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Nape Nnauye akisaini kitabu cha wageni wakati wa Ziara katika shirika wa Shirika la Utangazaji Taifa (TBC) leo Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Taifa (TBC) Dkt. Ayoub Rhioba akitoa taarifa ya utekelezaji wa shirika hilo kwa Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Nape Nnauye ambapo alimueleza mipango ya shirika hilo katika kuhakikisha linakuwa mfano barani Afrika.
Makamu Mwenyekiti Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) Bw. William Kalaghe akimkaribisha Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Nape Nnauye kuongea na wafanyakazi wa Shirika la Utangazaji Taifa (TBC) alipofanya ziara katika shirika hilo.
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Nape Nnauye akiongea na wafanyakazi wa Shirika la Utangazaji Taifa (TBC).
Baadhi ya Wafanyakazi wa Shirika la Utangazaji Taifa (TBC) wakimueleza Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Nape Nnauye changamoto za kiutendaji zinazolikabili shirika hilo wakati wa ziara katika shirika hilo leo Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Shirika la Utangazaji Taifa (TBC) wakimsikiliza Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Nape Nnauye.
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Nape Nnauye akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa TBC na wafanyakazi wa Shirika hilo.
(PICHA NA IDARA YA HABARI/WHUSM)
Na Shamimu Nyaki-WHUSM
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Nape Moses Nnauye amewataka wafanyakazi wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) kufanya kazi kwa ari ili kuhakikisha linakuwa mfano Barani Afrika katika kuhabarisha umma.
Waziri Nape ameyasema hayo leo alipofanya ziara katika Shirika hilo ili kuona utendaji kazi pamoja na kuona changamoto mbalimbali zinazolikabili Shirika hilo.
“Fanyeni kazi kwa bidii na uadilifu kwa kutoa taarifa za ukweli na zenye uhakika kwa watazamaji puuzeni propaganda zinazoenezwa mtaani kuwa Shirika hili limepoteza Watazamaji na wasikilizaji kwa manufaa ya Taifa letu”.Alisema Waziri Nape.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo Dkt.Ayoub Ryoba ameeleza kuwa Shirika linaendelea kuongeza wasikilizaji na watazamaji ambapo kuanzia mwaka 2012 hadi 2016 limeongeza mitambo kutoka kumi na mbili hadi hadi kumi na tisa iliyofungwa Mtwara,Rombo,Mbambabei na Tarime.
Aidha, Dkt Ryoba ameongeza kuwa Shirika hilo bado linaendelea kuwa katika historia ya Kuwa Shirika lililohabarisha umma juu ya Jitihada za Serikali ya Tanzania katika Ukombozi wa Bara la Afrika pamoja na kuendelea kukuza lugha ya Kiswahili kupitia kipindi cha malenga wapya.
“Shirika letu linaendelea kutoa habari, elimu na burudani zinazozingatia muktadha wa Utamaduni wa Nchi yetu ambapo kwa kipindi cha mwaka jana tumekuwa tukirusha matukio mubashara kupitia mitandao ambayo yana wafuatiliaji zaidi ya million tano.” Alisema Dkt.Ryoba.
Shirika hilo linaendelea kuwafikia watazamaji na wasikilizaji wengi zaidi ndani na nje ya nchi kwa kuendelea kuweka mikakati ya kuongeza vituo vingi zaidi.
↧
↧
SERIKALI YAWAONDOA HOFU WANANCHI JUU YA HALI YA UPATIKANAJI WA CHAKULA NCHINI.

Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dkt. Charles Tizeba akizungumza na waandishi wa habari kuhusu hali ya upatikanaji wa chakula nchini leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Mhandisi Mathew Mtigumwe.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi akitoa maelekezo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa mkutano wa Waziri wa Wizara hiyo Dkt. Charles Tizeba9hayupo pichani) na waandishi hao kuhusu hali ya upatikanaji wa chakula nchini leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia mkutano baina yao na Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dkt. Charles Tizeba (hayupo pichani) kuhusu hali ya upatikanaji wa chakula nchini, mkutano umefanyika katika ukumbi wa mikutano wa Wizara hiyo leo jijini Dar es Salaam. Picha zote na: Frank Shija – MAELEZO.
Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO.
SERIKALI imesema kuwa hali ya upatikanaji wa chakula nchini ni ya kuridhisha na kuwataka wananchi kupuuza taarifa zinazodai kuwa hali ya chakula ni mbaya.
Hayo yamebainishwa leo jijini Dar es Salaam na Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dkt. Charles Tizeba wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu hali ya upatikanaji na chakula nchini.
“Ndugu waandishi ukweli ni kwamba hali ya upatikanaji wa chakula nchini ni ya kuridhisha sana katika maeneo mengi, hivyo siyo kweli kwamba kuna tatizo la njaa kama baadhi ya watu wanavyojaribu kupotosha,” alisisitiza Dkt. Tizeba.
Aidha Dkt. Tizeba aliongeza kuwa pamoja na kuwepo kwa hali nzuri ya chakula, Serikali kupitia Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) imeendelea kuweka akiba ya chakula kwa kununua jumla ya tani 62,087.997za mahindi ili kuhakikisha nchi inaendelea kuwa na chakula cha kutosha,
Dkt. Tizeba amesema kuwa kwa mwaka wa fedha 2016/2017 Serikali imejipanga kununua jumla ya tani 100,000 za chakula ambapo hadi kufikia Januari 8 mwaka 2017 imenunua jumla ya tani 62,087.997za mahindi sawa na asilimia 62 ya lengo ililojiwekea.
“Kati ya kiasi kilichonunuliwa, tani 38,162.280 zimenunuliwa kupitia vituo vya ununuzi na tani 23,925.717 kupitia vikundi vya wakulima hivyo hadi kufikia tarehe 12 Januari, 2017 Wakala wana akiba ya tani 88,152.443 za mahindi,” alisema Dkt. Tizeba.
Waziri Tizeba ameongeza kuwa hadi kufikia katikati ya mwezi Januari, 2017 hali ya chakula na upatikanaji wake hapa nchini bado ni ya kuridhisha na hasa upatikanaji wa vyakula kama mchele na maharage ikilinganishwa na zao la mahindi.
Aidha, Wizara kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI, FAO, TFNC pamoja na wadau wengine wanaendelea kufanya tathmini ya kina ya hali ya chakula na lishe nchini ambayo inatarajiwa kukamilika Januari 28 mwaka 2017 na itazihusisha Halmashauri 55, tathmini hiyo itaiwezesha Serikali kupata taarifa za uhakika zaidi kuhusu hali ya chakula na lishe nchini.
Amefafanua kuwa kutokana na hali ya mwenendo wa unyeshaji wa mvua za vuli na msimu kutokuridhisha katika maeneo mengi ya nchi, Serikali imewashauri wakulima kutumia mbegu zitakazokomaa mapema na kupanda mazao yanayostahimili ukame pamoja na kutumia kwa uangalifu na kuhifadhi akiba ya chakula cha kutosha kwa matumizi katika kaya.
Aidha, Sekta binafsi zimehamasishwa kuendelea kushiriki katika kutoa masoko ya kununua na kuuza mazao katika maeneo yenye ziada na kuyauza katika maeneo yenye uhaba.
Ufafanuzi huo umetolewa kufuatia kuwepo kwa taarifa za upotoshwaji juu ya hali ya upatikanaji wa chakula hapa nchini ambapo Dkt. Tizeba amesema huo ni upotoshaji wenye lengo la kuwatia hofu wananchi.
↧
TAASISI YA MOYO YA JAKAYA KIKWETE (JKCI) KWA KUSHIRIKIANA NA HOSPITALI YA APOLO, BANGALOLE YA NCHINI INDIA WAWAFANYIA WAGONJWA UPASUAJI WA MOYO
Madaktari Bingwa wa upasuaji wa Moyo kutoka Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) na Madaktari wa Hospitali ya Apolo, Bangalole ya nchini India wakimfanyia mgonjwa upasuaji wa kumuwekea milango miwili ya moyo ya chuma (Aortic na Mitral Valuves) ambayo itamsaidia kupitisha damu vizuri katika moyo. Kutoka kulia ni Dkt. Sathyaki Nambala, akifuatiwa na Dkt. Bashir Nyangasa na kushoto ni Dkt. Lebighe Khan.
Madaktari Bingwa wa upasuaji wa Moyo kutoka Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) na Madaktari wa Hospitali ya Apolo, Bangalole ya nchini India wakiendelea na kazi ya kumfanyia mgonjwa upasuaji wa kumuwekea milango miwili ya moyo ya chuma (Aortic na Mitral Val uves) ambayo itamsaidia kupitisha damu vizuri katika moyo. Mgonjwa huyo milango yake miwili ya moyo haikuwa inafanya kazi vizuri ya kupitisha damu.
Picha na Anna Nkinda - JKCI
↧
WASTAAFU WANAOLIPWA NA HAZINA WAHAKIKIWA KIGOMA
Mkaguzi Mkuu wa Ndani Msaidizi Bw. Stanslaus Mpembe akimhudumia mstaafu wakati wa zoezi la uhakiki wa wastaafu wanaolipwa na Wizara ya Fedha na Mipango, linalofanyika katika Halmashauri ya Mji wa Kigoma, Mkoani Kigoma.
Baadhi ya Wastaafu Mkoani kigoma wakisubiri kuhakiki taarifa zao katika zoezi la kuhakiki taarifa za wastaafu wanaolipwa na Hazina, linaloendelea katika mikoa ya Kigoma na Tabora.
Bibi Lucy Suzereje aliyekuwa mtumishi wa chuo cha maendeleo – Kihinga Mkoani Kigoma, akiwa ameshika kitambulisho chake cha kustaafu akisubiri kuhakiki taarifa zake za kustaafu kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma.
Bw. Jumanne Mtumwa Kiragu (aliyevaa kofia) ambaye alikuwa mtumishi wa Wizara ya Mambo ya ndani ya nchi Idara ya Magereza akitoa taarifa zake za kusataafu kwa Mkaguzi wa ndani wakati wa zoezi la kuhakiki taarifa za wastaafu Mkoani Kigoma.
Mkaguzi wa ndani wa Manispaa ya kigoma vijijini Bw. Filbert Muhamba (kulia) akipata maelezo kutoka kwa mstaafu katika zoezi la uhakiki wa taarifa za wastaafu wanaolipwa na Wizara ya Fedha na Mipango, linalofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma –Ujiji Mkoani Kigoma.
Mwandishi wa Habari wa TBC Mkoani Kigoma Bw. Dotto Elias (Kulia) akisikiliza maelezo kutoka kwa baadhi ya wastaafu Mkoani Kigoma mara baada ya kukamilisha uhakiki wa taarifa zao.
Mkaguzi Mkuu wa Ndani Msaidizi Bw. Stanslaus Mpembe akiongea na wahandishi wa Habari akielezea utaratibu unaotumika katika kuhakiki taarifa za wastaafu katika zoezi la uhakiki unaendelea katika Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma –ujiji.
Mstaafu Bw. Maganga Patric akiongea na wahandishi wa habari kuhusu zoezi la uhakiki linaoendelea Mkoani Kigoma katika Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma –Ujiji.
(PICHA ZOTE NA Kitengo cha Mawasiliano-Wizara ya Fedha na Mipango-WFM)
↧
MBARAWA AAGIZA TAASISI NCHINI KUJIUNGA NA KITUO CHA KUMBUKUMBU (IDC)
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akisisitiza jambo wakati alipofanya mazungumzo na wafanyakazi ( Hawapo pichani) wa kituo cha Taifa cha kuhifadhia kumbukumbu Data Center kilichopo Kijitonyama jijini Dar es salaam.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (Katikati) akitoa maelekezo kwa Afisa Mkuu wa Ufundi wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Senzige Kisenge (wa kwanza kulia), wakati alipokagua huduma za mkongo wa Taifa katika ofisi za Kampuni hiyo, Jijini Dar es salaam.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (Katikati) akipata maelezo kutoka kwa Afisa Mkuu wa Ufundi wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Senzige Kisenge, namna Mkongo wa Taifa unavyofanya kazi nchini wakati alipokagua huduma za mkongo huo jijini Dar es salaam.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (Kushoto) akizungumza na mmoja wa watoa huduma wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) wakati alipokagua huduma za Kampuni hiyo, Jijini Dar es salaam.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (Kulia) akizungumza na mteja (kushoto) aliyetembelea ofisi za huduma kwa wateja za Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), ili kujipatia huduma zitolewazo ofisini hapo. Katikati ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni hiyo, Waziri Kindamba.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akifafanua jambo kwa mmoja wa wateja waliotembelea kituo cha huduma kwa wateja cha Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) ili kujipatia huduma zitolewazo katika duka hilo.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (Wa pili kulia) akisikiliza maoni kutoka kwa wateja waliotembelea kituo cha huduma kwa wateja cha Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) ili kujipatia huduma zitolewazo katika duka hilo.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa ameziagiza Taasisi zote za Serikali nchini kuhakikisha zinaleta taarifa zao kuhifadhiwa katika kituo cha Taifa cha Kuhifadhi kumbukumbu cha Kijitonyama (IDC) kwani kituo hicho ni salama na kina ubora wa hali ya juu katika Kanda ya Afrika Mashariki na Kati.
Aidha, amezitahadharisha baadhi ya Taasisi zenye mpango wa kujenga na kuanzisha vituo vyao vya kuhifadhi kumbukumbu kuacha mara moja mpango huo, kwani kufanya hivyo ni kuingilia kazi ya kituo hicho na kupoteza fedha za Serikali.
Hayo yamezungumzwa jijini Dar es salaam na Waziri huyo mara baada yakutembelea kituoni hapo na kupokea taarifa ya uendeshaji wa kituo hicho kutoka kwa Mkuu wa Kituo.
“Sioni sababu kwa Taasisi nyingine kutaka kujenga vituo vyao vya kuhifadhi kumbukumbu, Serikali imeshawekeza fedha nyingi kwa ajili ya ujenzi wa kituo hiki, hivyo taasisi zote nchini zinalazimika kutumia kituo hiki”, amesema Profesa Mbarawa.
Sambamba na hilo amezisisitiza kampuni zilizo chini ya Wizara yake kuwa mfano wa kuigwa na taasisi nyingine nchini kwa kuwa wa kwanza kuleta taarifa zao kuhifadhiwa katika kituo hicho.
Kwa upande wake, Mkuu wa Kituo hicho Abdul Mombokaleo, amefanunua kuwa hadi sasa wameshafanikiwa kuunganisha wateja 13 kujiunga na kituo hicho na wengine zaidi ya 40 wapo katika mchakato wa kujiunga.
Katika hatua nyingine, Waziri Mbarawa ametembelea ofisi za Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) na kusema kuwa ameridhishwa na utendaji wa kampuni hiyo kutokana na jitihada zake za kuteka soko la ushindani katika makampuni ya mawasiliano nchini.
“Nimefarijika zaidi kuona sasa TTCL inafanya vizuri katika eneo la masoko kwani nimeshuhudia matangazo mengi barabarani, kwenye luninga, magazetini na katika mitandao ya kijamii, hii inadhihirisha sasa mna mpango wa kuifufua kampuni hii”, amefafanua Profesa Mbarawa.
Ameutaka uongozi wa kampuni hiyo kuwa wabunifu na kufanya kazi kwa uadilifu na ushirikiano ili kuleta mabadiliko chanya yatakayoboresha kampuni hiyo na kuteka zaidi soko la mawasiliano nchini.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
↧
↧
Wanawake wanaoshiriki katika mradi wa WOW wapewa mafunzo ya haki zao

Martin Gabone-Mkurugenzi Mkuu Mradi wa Wanawake Kwenye Usukani (WOW) akimtambulisha WIGAYI KISSANDU-Mwanasheria Kituo cha Msaada wa Sheria kwa Wanawake (WLAC) mkufunzi wa mafunzo hayo yaliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam.
Wanawake wanaoshiriki katika mradi wa Wanawake Kwenye Usukani (WOW) unaoendeshwa na Kampuni ya AFREXA International Ltd, wametakiwa kufahamu haki mbalimbali za binadamu zinamwongoza mwanadamu kushiriki vyema katika shughuli za kimaendeleo.Akizungumza Jijini DSM, wakati wa semina ya siku moja ya wanawake kuelekea katika mafunzo ya kuendesha vyombo vya moto vya biashara, mwanasheria kutoka Kituo cha Msaada wa Sheria kwa Wanawake (WLAC) WIGAYI KISSANDU amesema ni muhimu kwa wanawake kufahamu haki hizo kwa kuwa zinatoa mwongozo kufikia malengo.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu Mradi wa Wanawake Kwenye Usukani (WOW) MARTIN GABONE amesema semina hiyo ni moja ya hatua za mwanzo za mafunzo ya udereva kwa wanawake kwa ajili ya kuendesha vyombo vya moto vya biashara na kusisitiza wanawa wajibu wa kuhakikisha wanawake hao wanaingia rasmi katika sekta ya usafirishaji kwa kuajiriwa au kujiajiri.
Mradi wa Wanawake Kwenye Usukani (WOW) hadi sasa umesajili zaidi ya wanawake 200 kutoka maeneo mbalimbali nchini, ili waweze kuwapatia bure mafunzo ya udereva wa vyombo vya moto vya biashara ambapo baada ya mafunzo hayo watatafutiwa ajira na wengine watawezeshwa ili waweze kujiajiri.
![]()
![]()
![]()
![]()
![]()
![]()
Martin Gabone-Mkurugenzi Mkuu Mradi wa Wanawake Kwenye Usukani (WOW) akifungua semina ya mafunzo ya haki za wanawake wanaoshiriki katika mradi huo iliyofanyika mwishoni mkwa wiki Kinondoni jijini Dar es salaam.

WIGAYI KISSANDU-Mwanasheria Kituo cha Msaada wa Sheria kwa Wanawake (WLAC) akitoa mafunzo katika semina hiyo.


WIGAYI KISSANDU-Mwanasheria Kituo cha Msaada wa Sheria kwa Wanawake (WLAC) akifafanua jambo wakati alipokuwa akitoa mafunzo katika semina hiyo.

Baadhi ya washiriki wakiwa katika semina hiyo.


Martin Gabone-Mkurugenzi Mkuu Mradi wa Wanawake Kwenye Usukani (WOW) na Victor Francis-Meneja Mafunzo wa Mradi wa Wanawake Kwenye Usukani (WOW) wakiwa katika semina hiyo.
↧
Wilaya tatu Mkoani Pwani kuunganishwa katika Gridi ya Taifa
Mbunge wa jimbo la Mkuranga, Abdallah Ulega,( kulia)akimueleza jambo Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt Medard Kalemani( kushoto) wakati wa ziara ya kukagua miradi ya umeme vijijini wilayani Mkuranga katika kijiji cha Njopeka.
Na Zuena Msuya, Pwani
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani amesema Wilaya za Mkuranga, Rufiji pamoja na Kibiti mkoani Pwani zitaunganishwa katika Gridi ya Taifa wakati wa kuanza kwa Awamu ya Tatu ya utekelezaji wa Mradi Umeme Vijijini unaotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwa kushirikiana na Shirika la Umeme Tanzania ( TANESCO).
Dkt. Kalemani alisema hayo wakati wa ziara yake ya siku moja ya kukagua maendeleo na utekelezaji Mradi wa Umeme Vijiji katika Wilaya hizo pamoja na kuzungumza na wananchi.
Alifafanua kuwa ni lazima Wilaya hizo zikaungwanishwa katika Gridi ya Taifa ili waweze kupata umeme mwingi, wa kutosha na wa uhakika ili kuongeza kasi na ufanisi katika shughuli za wananchi za kujipatia maendeleo.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dkt. Medard Kalemani, (aliyesimama), akizungumza na Wakazi wa Rufiji wakati wa ziara ya kukagua Mradi wa Umeme Vijijini unaotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijiji (REA) katika wilaya hiyo.
dkt. kalemani aliweka wazi kuwa wakati wa kutekeleza awamu ya tatu ya mradi wa rea, tanesco itajenga kituo kikubwa cha kupokea na kupoza umeme katika Wilaya ya Mkuranga ili kusambaza katika Wilaya hizo.
" Umeme unaopatikana hapa Mkuranga , Kibiti na Rufiji kwa sasa hautoshelezi mahitaji ya watumiaji,ni mdogo sana na unakatika mara kwa mara,kwa kuwa shughuli za kiuchumi zimeongezeka, sasa suluhu ya tatizo hili ni kuunganisha Wilaya hizi katika Gridi ya Taifa mara tu baada ya REA, Awamu ya Tatu kuanza", alisema Dkt. Kalemani.
Aidha alitumia fursa hiyo kuwaeleza wananchi kuwa huduma ya umeme kwa sasa ni jambo la lazima kwa kila mtanzania ili kurahisisha maendeleo, hivyo ni vyema kila mmoja ajiunganishe na huduma hiyo kupitia Mradi wa REA ambao huduma hiyo hupatikana kwa bei nafuu na Serikali imeugharamia kwa asilimia mia moja kwa ajili wananchi wa vijijini.
Mbunge wa Jimbo la Rufiji, Mohamed Mchengerwa, akizungumza na wakazi wa rufiji (hawapo pichani)wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt Medard Kalemani ya kukagua miradi ya umeme vijijini wilayani Rufiji.
Katika hatua nyingine, aliwagiza wakandarasi wote wanaotekeleza Mradi wa Umeme Vijijini Awamu ya Pili, katika Mkoa wa Pwani,kuwasha umeme katika vijiji vyote ambavyo vimepitiwa na kuunganishwa na mradi wa huo ifikapo mwishoni mwa mwezi huu wa Januari kabla ya kuaza kwa Awamu ya Tatu ya Mradi huo.
Pia alimuagiza Meneja Tanesco wa Mkoa huo kusimamia wakandarasi hao ili kutekeleza agizo hilo, na endapo halitatekelezwa kama alivyoagiza hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.
"Mwishoni mwa mwezi huu nataka kuona vijiji vyote vilivyounganishwa na REA vinawashwa umeme, nawaagiza wakandarasi wote kutekeleza agizo hilo, Meneja Tanesco fuatiliwa na hakikisha jambo hili linatekelezwa kwa wakati, bila kufanya hivyo mtakuwa mmejifukuza kazi mwenyewe, kwa kuwa hakuna sababu ya kutotekeleza hili agizo", alisisitiza Dkt. Kalemani.
Sambamba na hilo aliiagiza Tanesco,kusogeza huduma zao karibu na wateja kwa kuweka madawati ama kujenga vituo vidogo vya huduma kwa wateja katika kila kijiji kwa lengo la kuwafikia wananchi kwa urahisi badala ya wananchi kuwafuata Tanesco maofisini.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dkt. Medard Kalemani, (aliyesimama kushoto), akizungumza na Wakazi wa kijiji cha Mkiu wilayani Mkuranga wakati wa ziara ya kukagua Mradi wa Umeme Vijijini unaotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijiji (REA) katika wilaya hiyo.
Pia alitumia ziara hiyo kuwaeleza wananchi kuwa Serikali kupitia Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco),imetenga zaidi ya shilingi Bilioni 68.5 kwa ajili ya kuwalipa fidia, jumla ya wananchi 2913 waliopisha Mradi wa msongo mkubwa wa umeme kutoka Somanga hadi Kinyerezi katika vijiji vilivyopitiwa na mradi huo.
Vilevile alibainisha kuwa fidia hiyo italipwa kwa ratiba maaalum ili kuondoa usumbufu kwa wananchi, ambapo mpaka sasa zaidi ya shilingi Bilioni 42, zimelipwa kwa wananchi 923, huku zoezi la ulipaji likiendelea kwa mujibu wa ratiba na linatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi Februari mwaka huu.
Awamu ya Tatu ya utekelezaji wa Mradi wa Umeme Vijijini unaotekelezwa na REA kwa kushirikiana na TANESCO unatarajia kuanza mwishoni mwa mwezi huu( Januari)mwaka huu, na utatekelezwa kwa takribani kipindi cha miaka minne.
Wakazi wa Rufiji wakimsikiliza Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dkt. Medard Kalemani (hayupopichani) alipokuwa akizungumza wakati wa ziara ya kukagua Mradi wa Umeme Vijijini unaotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijiji (REA) katika wilaya hiyo.
Wakazi wa Kijiji cha Ikwiriri wakimsikiliza Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani( aliyenyoosha mkono katikati) wakati wa ziara ya kukagua miradi ya umeme vijijini wilayani Rufiji.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dkt. Medard Kalemani, (jukwaani kushoto) na mbunge wa Kibiti, Ally Ungando( kulia) akizungumza na Wakazi wa Kijiji cha Jaribu Mpakani wilayani Kibiti, mkoani Pwani wakati wa ziara yake ya kukagua Mradi wa Umeme Vijijini unaotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijiji (REA) katika wilaya hiyo. Wananchi hao wanadai fidia baada ya kupisha mradi wa kupitisha msongo mkubwa wa umeme kutoka Somanga hadi Kinyerezi jijini Dar es salaam.
↧
MAMLAKA YA BANDARI YASHAURIWA KUFANYA TARATIBU ZA KURASIMISHA BANDARI BUBU NCHINI
Na Adili Mhina, Tanga.
Mamlaka ya Bandari nchini imeshauriwa kuangalia taratibu za kurasimisha bandari bubu ili kudhibiti upotevu wa mapato ya Serikali pamoja na kuhakikisha bidhaa zinazopitishwa katika maeneo hayo zinakubalika kisheria.
Ushauri huo umetolewa hivi karibuni na Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri wakati timu ya ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Tume ya Mipango ilipofanya ziara katika Bandari ya Tanga kwa lengo la kufanya ufuatiliaji na tahmnini ya shughuli zinazotekelezwa bandarini hapo.
Mwanri alieleza umuhimu wa kurasimisha bandari bubu baada ya kupata taarifa kuwa katika Mkoa wa Tanga pekee kuna bandari bubu takriban 42 ambazo zinaendesha shughuli mbalimbali bila ya usimamizi wa Mamlaka ya Bandari.
Mwanri alieleza kuwa kwa sasa Serikali haiwezi kuendelea kufumbia macho suala hilo kwani licha ya Serikali kupoteza mapato yake wapo baadhi ya watu wanaotumia njia hizo nyakati za usiku kuendesha shughuli zinazoenda kinyume na kisheria na taratibu za nchi, hivyo kuchochea uhalifu.
“Kuna umuhimu mkubwa kuangalia shughuli zinazoendelea katika bandari bubu kwa kuwa wakati mwingine wafanya biashara wanaopaswa kulipa kodi wanatumia maeneo hayo kupitisha bidhaa bila kulipa kodi na wengine wanatumia bandari bubu kuendesha biashara haramu. Ni lazima kuanza kufanya utaratibu wa kurasimisha bandari hizo ili kuharakisha maendeleo ya nchi yetu,” alisema Mwanri.
Pamoja na hayo, Mwari alitembelea maeneo ya Bandari ya Tanga na kushuhudia shughuli mbalimbali zikiendelea ikiwa ni pamoja na ujenzi wa gati namba 2 ikiwa ni moja ya malengo katika kuimarisha huduma za upakiaji na upakuaji wa mizigo bandarini hapo.
Awali, Mhandasi wa Bandari hiyo Bw. Saleh Sapi alieleza kuwa Bandari ya Tanga inapokea tani laki mbili za mizigo kwa mwezi ambapo bidhaa kubwa zinazoingizwa kutoka nje ni malighafi ya kutengenezea saruji wakati bidhaa zinazosafirishwa kwenda nje ni kahawa, mkonge, pamoja na mbao ambazo kwa sasa kibali chake kimesitishwa kwa muda.
Mhandisi huyo alieleza kuwa Bandari ya Tanga haina eneo lenye ukubwa wa kutosha kwa ajili ya kutekeleza huduma zake kwa ufanisi huku kina cha maji kikiwa ni mita nne kitu kinachopelekea meli kubwa kushindwa kufika kwenye gati za bandari na badala yake matishari hutumika kubeba mizigo hiyo.
Mhandisi Sapi alifafanua kuwa kutokana na changamoto hiyo nguvu kubwa inaelekezwa katika kuangalia namna ya kujenga bandari kubwa ya kisasa katika eneo la Mwambani ambapo kuna kina cha maji kinatosha kuhudumia meli kubwa na pia kuna eneo la kutosha shughuli mbalimbali za bandarini.
Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri (kulia) akielekea katika Gati namba moja la Bandari ya Tanga kuangalia shughuli mbalimbali zinazoendelea bandarini hapo. Penmbeni yake ni Mhandisi wa Bandari hiyo Bw. Saleh Sapi.
Mhandisi wa Bandari ya Tanga Bw. Saleh Sapi (mwenye t-shirt) akitoa maelezo kwa Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri (koti jekundu) juu ya kina cha maji katika bandari hiyo. Upande wa kulia ni Bw. Jordan Matonya na Bi Anna Kimwela, wachumi kutoka Tume ya Mipango. Upande wa kushoto (mwenye miwani ya jua) ni Afisa Mipango Mwandamizi wa Bandari ya Tanga, Bibi Moshi Mtambalike.
Shughuli za kupakia Magogo ya Umeme zikiendelea katika Bandari ya Tanga.
Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri akikagua ukarabati wa boti katika Bandari ya Tanga.
Mhandisi wa bandari ya Tanga Bw. Saleh Sapi akimueonesha Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri ujenzi unaoendelea (hauonekani pichani) wa gati namba mbili katika Bandari ya Tanga. Pembeni ya Mhandisi Sapi ni Mchumi Mkuu kutoka Tume ya Mipango Bw. Aloyce Shayo na wa kwanza kulia ni Bw. Jordan Matonya Kutoka Tume ya Mipango.
Ujenzi wa gati namba mbili ukiendelea katika Bandari ya Tanga. NA ADILI MHINA, TUME YA MIPANGO.
↧