Quantcast
Channel: MTAA KWA MTAA BLOG
Viewing all 40096 articles
Browse latest View live

Tigo yasherekea wiki ya huduma kwa Mteja katika duka la Mlimani City

$
0
0

Meneja Mawasiliano wa Tigo Tanzania, Woinde Chisel akijadiliana jambo na Meneja huduma kwa wateja kutoka kampuni ya simu za mkononi ya Tigo Mwangaza Matotola na msimamizi wa duka la Tigo Mlimani City Joseph Umoti (katikati mapema jana katika duka la Mlimani city.
Meneja huduma kwa wateja kutoka kampuni ya simu za mkononi ya Tigo Mwangaza Matotola (kushoto) akisaidiana na msimamizi wa duka la Tigo Mlimani City Joseph Umoti kutoa huduma kwa Happiness Muthali wakati wa kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja. Maadhimisho hayo yameanza jana.

Meneja huduma kwa wateja kutoka kampuni ya simu za mkononi ya Tigo Mwangaza Matotola (kushoto) na msimamizi wa duka la Tigo Mlimani City Joseph Umoti wakifurahi jambo na mteja wakati wa kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja. Maadhimisho hayo yameanza jana.
Meneja huduma kwa wateja kutoka kampuni ya simu za mkononi ya Tigo Mwangaza Matotola (kushoto) akitoa huduma kwa Happiness Muthali wakati wa kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja. Maadhimisho hayo yamefanyika jana katika duka la Tigo Mlimani City jijini Dar.

wateja wakiendelea kupata huduma.

IDADI YA VIFO KATIKA SHAMBULIZI LA RISASI LAS VEGAS YAFIKIA 59, MUHUSIKA WA TUKIO AMEKUTWA AMEKUFA HOTELINI.

$
0
0
Idadi ya vifo katika shambulizi la risasi katika hoteli ya Mandalay Bay mjini Las Vegas yafikia 59 na waliojeruhiwa 500.muhusika wa tukio amekutwa amekufa.
Polisi wamemtaja muhusika wa shambulio hilo Stephen Paddock mwenye miaka 64 aliyekuwa anafyatulia risasi katika umati wa watu waliokusanyika katika Tamasha la mziki linalokadiliwa kuwa na watu zaidi ya 22,000  walioshiriki.

Muda mfupi baadaye Paddock alikutwa amekufa katika chumba chake hotelini .Polisi wathibitisha.

Eric Paddock, kaaka yake na  Stephen amesema kuwa kaka yake hajawahi kuwa na tatizo lolote la akili wala msukumo wowote wa kisiasa.

TSA yahitaji Sh milioni 66 kwa ajili ya mashindano ya Cana kanda ya tatu

$
0
0
Wakati mashindano ya kuogelea ya kanda  ya tatu ya Afrika (Cana zone 3) yamebakiza takribani wiki mbili kufanyika, Chama Cha kuogelea nchini (TSA) bado kinasaka kiasi cha fedha taslimu shilling milioni 66 ili kufanikisha mashindano hayo. Mpaka sasa, jumla ya nchi nane  zimethibitisha kushiriki katika mashindano hayo ambayo yanafanyika Tanzania kwa mara ya kwanza katika hisoria ya Tanzania. Mashindano hayo yamepangwa kuanza Oktoba 19 mpaka 21 kwenye bwawa la kuogelea la Hopac la jijini.

Katibu Mkuu wa TSA, Ramadhan Namkoveka alisema kuwa pamoja na maandalizi kuendelea vizuri chini ya mwenyekiti wa  Kamati ya mashindano,  Leena Kapadia, bado hawajatimiza lengo lao kukusanya fedha kwa ajili ya mashindano  hayo. Namkoveka alisema kuwa awali walikuwa wanahitaji Sh milioni 100, hata hivyo kiasi hicho cha fedha kimepungua kutokana na wadhamini mbalimbali kujitokeza kuchangia. Wadhamini hao ni pamoja na kampuni ya simu ya Vodacom Tanzania, Swissair, JCDecaux, , Label Promotions , Print Galore na Slipway Hotel.
“ Kamati  imeweza  kutafuta fedha kwa  makampuni 34 na bado tuna imani kati yao watajitokeza kusaidia gharama za maandalizi. Tunatoa wito kwa kampuni zilizopo ndani na nje ya nchi kudhamini mashindano haya ikiamini kuwa licha ya kujitangaza kwa biashara zao itasaidia kwa kiasi kikubwa ukuaji wa mchezo wa kuogelea katika kanda ya Afrika ya Mashariki na Kati,” alisema Namkoveka.

Alifafanua kuwa viwango vya waogeleaji wa timu ya Taifa vinaendelea kuhimarika hasa kwa kutambua kuwa mashindano kwani  ni sehemu ya kujiandaa kwa mashindano ya Jumuiya Ya Madola yatakayofanyika Huko Australia Mwakani, Olimpiki ya Vijana ya Mwezi Oktoba, na Kufanyika Nchini Argentina.

Alisema kuwa mashindano haya ni sehemu ya maandalizi ya mashindano yatakatotumika kwa ajili kushiriki mashindano ya CANA kanda ya nne yatakayofanyika nchini Malawi. Wakati huo huo; Shirikisho la Mchezo wa Kuogelea la Dunia (FINA) watatoa dola za kimarekani 10,000 kusaidia gharama za maandalizi.

Namkoveka alitoa  shukrani kwa  Fina  kwa kusaidia kukua kwa mchezo huu hapa Duniani na hakika wanafanya kazi kubwa ya kusaidia mchezo huu kukua. Mchango wao huu utaleta ufanisi katika mashindano haya. Nchi zilizothibitisha kushiriki mashindano hayo ni nchi za Afrika ya Kusini, Zambia, Kenya, Uganda, Rwanda, Sudan ya Kusini, Djibout, na mwenyeji na  bingwa mtetezi nchi ya Tanzania.
Wakati huohuo, Chama Cha Kuogelea kimeamua kuimarisha usimamizi wa Timu ya Tanzania kwa kuteua Meneja wawili watakaoshughulikia timu ya Tanzania. Chama kimeamua kuteua mameneja wawili kwa kuwa nchi ya Tanzania kwa kuwa ni mwenyeji inaruhusiwa kuwa na timu mbili. Mameneja walioteuliwa ni Priscilla Zengeni na Jones Gouw. Waogeleaji wa Tanzania wapo chini ya makocha Alexander Mwaipasi na Michael Livingstone na baadhi ya wachezaji walioko mikoani wapo chini ya makocha wao wa Klabu au shule.

Alisema kuwa kuna changamoto ya kuweka kambi ya pamoja kwa kuwa wachezaji wanaounda timu hii wengine wanatoka Morogoro, Zanzibar, Arusha, Mwanza na Kilimanjaro na pia ni wachezaji ambao wako mashuleni wanakosoma.

PPF YATOA MSAADA WA VIFAA VYA MAABARA

$
0
0
 Mkurugenzi Mkuu wa PPF, William Erio akikabidhi moja ya Vifaa vya maabara kwa mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Canossa Mhandisi Magayane Machibya wakati wa mahafali ya tisa ya ka kidato cha nne Jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki.
 Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio (Kulia) akimkabidhi cheti Joyce Msumari (Kushoto) mhitimu wa kidato cha Nne katika shule ya Sekondari ya Wasichana ya Canossa iliyopo jijini Dar es Salaam.  Joyce Msumari ni mmoja wa wanufaika wa Fao la Elimu linalotolewa na PPF kwa watoto wa wananchama wanaofariki wakiwa katika Ajira.  
 Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Canossa, Mhandisi Magayane Machibya (Kushoto) na Mkuu wa Shule hiyo Sista Irene Natumanya wakifurahia kupokea vifaa vya maabara kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa PPF William Erio (hayupo pichani) 
 Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Canossa Sista Irene Natumanya (Kulia) akimpa mkono wa shukrani Mkurugenzi Mkuu wa PPF Bwana William Erio (Katikati) baada ya kukabidhiwa vifaa vya maabara na Mfuko wa PPF mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Mkurugenzi wa Bodi ya Shule hiyo Mhandisi Machibya Magayane.
 Wahitimu wa Kidato cha nne wa shule ya Sekondari ya Canossa wakitumbuiza katika mahafali ya 9 yaliofanyika Shuleni hapo mwishoni mwa wiki.
Vifaa vya maabara vilivyotolewa na Mfuko wa Pensheni wa PPF wakati wa mahafali ya 9 ya shule ya Sekondari ya Wasichana Canossa mwishoni mwa wiki.

MFUKO wa Pensheni wa PPF umetoa msaada wa vifaa vya maabara vyenye thamani ya zaidi ya shillingi milioni 6.7 kwa shule ya Sekondari ya Wasichana ya Canossa iliyopo Tegeta jijini Dar es Salaam.

Akikabidhi vifaa hivyo katika mahafali ya tisa ya kidato cha nne shuleni mwishoni mwa wiki,Mkurugenzi Mkuu wa PPF Bw.William Erio amesema Mfuko umeamua kutoa vifaa hivyo ili kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya tano katika kutengeneza uchumi wa viwanda.

Bw.Erio ambaye pia alikuwa mgeni rasmi kwenye mahafali hayo, amebainisha kuwa Mfuko wa Pensheni wa PPF utaendelea kushirikiana na taasisi za elimu nchini katika jitihada za kuelekea uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.

Pia Bw.Erio amesema ushirikiano mzuri uliopo kati ya shule ya Canossa na PPF pia ni moja ya sababu kupeleka vifaa hivyo shuleni hapo..

“Shule ya Canossa imekuwa miongoni mwa waajiri wanaowasilisha michango ya wafanyakazi wao kwa wakati bila kuchelewesha,na idadi kubwa ya wafanyakazi wake ni wanachama wa Mfuko wetu,” amefafanua Mkurugenzi Mkuu.

Sanjari na hilo, Mkurugenzi huyo wa PPF amesema katika shule hiyo Mfuko umeshasomesha wanafunzi 6 ambao wamenufaika na fao la elimu baada ya wazazi wao ambao walikuwa wanachama wa PPF kufariki wakiwa katika ajira.

“Mfuko pia unabeba jukumu la mzazi, kwa mwaka wa fedha ulioishia Juni 2017, tumesomesha wanafunzi 1403 nchi nzima na zaidi ya shilingi 1.4 bilioni zimetumika katika kugharamia masomo yao’’. 

Mmoja wa wahitimu ambaye pia ni miongoni mwa wanafunzi wanaosomeshwa na Mfuko wa PPF, Joyce Msumari ameshukuru PPF kwa kumlipia masomo yake tangu mzazi wake alipofariki  akiwa darasa la tano, miaka 7 iliyopita.

“Naishukuru PPF kwa kunifikisha hapa,na wazazi wengine wanaweza kujifunza kupitia kwangu maana hakuna anayeijua kesho yake hivyo unapojiunga na Mfuko huu utakuwa na uhakika wa masomo kwa mwanao pale ambapo Mungu ataamua kukuchukua na kuwaacha watoto wako wakiwa wanahitaji,” alisema mwanafunzi huyo.

SPIKA NDUGAI AKUTANA NA WABUNGE WA BUNGE LA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI KUTOKA TANZANIA

$
0
0
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kulia) akimsikiliza Mheshimiwa Abdullah Makame (katikati) ambae ni kiongozi wa msafara wa Wabunge wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki kutoka Tanzania walipomtembelea leo Ofisini kwake Mjini Dodoma.
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (katikati) akizungumza na Wabunge wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki kutoka Tanzania walipomtembelea leo Ofisini kwake Mjini Dodoma.
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (katikati) akizungumza na Wabunge wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki kutoka Tanzania walipomtembelea leo Ofisini kwake Mjini Dodoma.

WAZIRI KAIRUKI AZINDUA BODI YA MISHAHARA NA MASILAHI KATIKA UTUMISHI WA UMMA

$
0
0
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Laurean Ndumbaro akimkaribisha Mgeni Rasmi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angellah Kairuki kuzungumza na wajumbe wa Bodi ya Pili ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma wakati wa uzinduzi wa bodi hiyo mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Mgeni Rasmi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angellah Kairuki akisisitiza jambo kwa wajumbe wa Bodi ya Pili ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma wakati wa uzinduzi wa bodi hiyo mapema hii leo jijini Dar es Salaam, kulia ni Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Laurean Ndumbaro na kushoto ni Kaimu Katibu Mtendaji wa bodi hiyo Bi. Mariam Mwanilwa.
Wajumbe wa Bodi ya Pili ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma pamoja na Sekretarieti ya bodi hiyo wakimsikiliza Mgeni Rasmi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angellah wakati wa uzinduzi wa bodi hiyo mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya Pili ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma, Kamishna wa Uhamiaji Mstaafu Donald Ndagula (aliyesimama) akitoa neno la shukrani mara baada ya kuzinduliwa kwa bodi hiyo mapema hii leo jijini Dar es Salaam, kushoto ni Mgeni Rasmi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angellah Kairuki
Mgeni Rasmi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angellah Kairuki (kushoto) akimkabidhi Mwenyekiti wa Bodi ya Pili ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma, Kamishna wa Uhamiaji Mstaafu Donald Ndagula vitendea kazi mara baada ya kuzindua bodi hiyo mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Mgeni Rasmi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angellah Kairuki (wa pili kulia) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe na sekretarieti ya Bodi ya Pili ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma mapema hii leo jijini Dar es Salaam.Picha na Eliphace Marwa – Maelezo



Eliphace Marwa-MAELEZO.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angellah Kairuki amezindua bodi mpya ya mishahara na masilahi katika utumishi wa umma mapema jijini Dar es Salaam leo.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo waziri Kairuki ameitaka bodi hiyo kuzingatia misingi iliyopo kwenye hati maalum ya Rais ambayo inawataka kuzingatia vigezo ambavyo ni pamoja na malipo ya mishahara na masilahi kwa watumishi wa Umma yanapatikana na kuwa endelevu.

“Ni vema kuhakikisha utumishi wa Umma unavutia na kubakiza taaluma zinazohitajika katika kuendesha shughuli zake ili kuweza kuleta tija kwa kuzingatia uwazi, usawa na haki mahala pa kazi”, alisema Waziri Kairuki.Aliongeza kuwa endapo bodi itazingatia vigezo hivyo, ushauri watakaoutoa utakuwa na manufaa makubwa kwa Taifa na hivyo kujenga imani kwa watumishi wa Umma na wadau wengine.

Waziri Kairuki aliahidi kutoa ushirikiano wa dhati kwa bodi hiyo na kusema kuwa Serikali iko pamoja nayo katika kuhakikisha masiilahi ya watumishi wa Umma yanaboreshwa ili kuongeza tija kwa kuwabakiza wataalam katika Utumishi wa Umma.Naye Mwenyekiti mpya wa bodi hiyo Kamishna wa Uhamiaji Mstaafu Donald Ndagula ameahidi kufanya kazi kwa kushirikiana na Serikali ili kuweza kutatua changamoto mbalimbali zitakazojitokeza kwa kwa kufanya tafiti.


“Napenda kusema kuwa pamoja na changamoto zilizopo katika bodi tutashirikiana na Serikali katika kuboresha hali ya utendaji katika utumishi wa Umma kwa kufanya tafiti kwa lengo la kuishauri Serikali ili iweze kuwapatia maisha ya staha Watumishi wa Umma”, alisema Ndagula.

Waziri Kairuki aliwataja wajumbe wa bodi hiyo kuwa ni Mwenyekiti, Donald Ndagula,Makamu Mwenyekiti, Balozi Charles Mutalemwa ,Wajumbe George Mlawa na Bi Gaudentia Kabaka.Wengine ni Jaji Mstaafu Regina Rweyemamu, Meja Jenerali Mstaafu Zawadi Madawili na Kamishna Mwandamizi wa Polisi Mstaafu Jamal Rwambow.

Waziri Kairuki iliitaka bodi hiyo kuhakikisha kuwa wanatekeleza jukumu lao la kuboresha masilahi ya watumishi ili wahamasike na waongeze tija katika utendaji kazi kwani,Serikali haiwezi kufanya maamuzi sahihi bila ya ushauri wa kitaalamu unaotokana na tafiti kuhusu maboresho ya masilahi ya watumishi wa Umma.

TUNASUBIRI MASAA 48 TUJUE MAENDELEO YA NGOMA- DAKTARI

$
0
0

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

Baada ya kuumia katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mtibwa mshambuliaji wa Yanga Donald Ngoma na kushindwa kufanya mazoezi jana pamoja na kikosi kutokana na maumivu ya misuli siku ya Jumamosi.

Ngoma baada ya kuumia hakuweza kurejea tena uwanjani na nafasi yake kuchukuliwa na Juma Mahadhi, siku ya  jana hakufanya mazoezi pamoja na wachezaji wenginena kupewa mapumziko na daktari wa timu Hussein Bavu.

Ngoma alipewa saa 24 hadi 48 za uangalizi chini ya daktari wa Yanga ili kuona maendeleo kabla ya kutoa majibu kama anaweza kurudi uwanjani mapema au vinginevyo.

Dakatri wa timu hiyo Bavu amesema kuwa baada ya masaa 24 hadi 48 ndipo wanaweza kutoa majibu sahihi kwani kwa sasa wamempa mapumziko Ngoma ili aweze kurejea katika hali ya kawaida na kuangalia maendeleo yake.

Kwa sasa maendeleo ya Ngoma yanaendelea vizuri na anatembea vizuri ukilinganisha na ilivyokuwa mwanzo, anaweza kufanya mazoezi binafsi ikiwa ni tiba ya jeraha lake

Yanga inakabiliwa na mchezo wa raundi ya sita ya ligi kuu VPL dhidi ya Kagera Sugar October 14, 2017 kwenye uwanja wa Kaitaba, mkoani Kagera.


VIJANA KATA YA BUZA WAUNGANA KUPAZA SAUTI KATIKA KULETA MAAENDELEO HAPA

$
0
0
Na Agness Francis, Blogu ya Jamii
Vijana wa kata ya Buza katika  mtaa wa Kidagaa wamejitokeza kwenye semina ya mafunzo  ya kujiunga na taasisi ya sauti ya vijana (MYIDC) Temeke  ili kuepukana na changamoto za kukaa mitaani bila kazi maalumu ya kufanya .

Nae Mwenyekiti Mtendaji  MYIDC,  Ismae  Mnikite amesema hayo  katika semina hiyo iliyofanyika mtaa wa Kidagaa  kata ya Buza  halmashauri ya Temeke  amesema kuwa lego la mafunzo hayo ni kutaka kuwafanya vijana waweze kuunda jukwaa la vijana na  baada ya hapo watapatiwa mafunzo kuhusu dira ya vijana na pia lengo likiwa ni kupaza sauti zao katika kuleta maendeleo.

Naye mkazi wa Buza kata ya Kidagaa Fatma Ramadhani  amesema kuwa amepata mwamko huo wa kijiunga  na taasisi hii ya sauti ya vijana (MYIDC) ili kuepukana na changamoto ya kukaa  tu mitaani ameona ni vizuri kutumia fursa zinazotolewa kama kujiunga katika vikundi vya ujasiliamani ili kujikwamua kiuchumi hapa Nchini.

Mkazi mwingine naye Rajabu Charz amesema kuwa  katika mafunzo hayo amejifunza  namna ya kutafuta na kuweka mtaji kwa ajili ya kuanzisha biashara na kuondoa woga wa   kuthubutu katika kafanya jambo la kuleta mafanikio.
 Mwenyekiti Mtendaji  MYIDC,  Ismae  Mnikite akizungumza na waandishi wa habari pamoja na vijana wa mtaa wa Kidagaa kuhusu umuhimu wa mradi wa Sauti ya Vijana (MYID) katika kata ya Buza mtaa wa Kidagaa Halmashauri ya wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam.
 Muwakilishi wa Diwani kata ya Buza, Mahmoud Rashidi akizungumza na waandishi wa habari  kuhusu changamoto  zinazowakabili vijana na kujitahidi kujitokeza kwenye shuhuli kama hizi  kutokana na  kuwa na utayari, pia amewapongeza vijana wa kata hiyo kwa kujitokeza  kuhudhuria mafunzo hayo katika kata ya Buza mta wa Kidagaa Halmashauri ya wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam.
 Mkazi wa  Buza  kata ya Kidagaa, Fatma Ramadhani akizungumza na waandishi wa habari kususu kuchangamkia fursa na kutoa pongezi za dhati kwa sauti ya vijana  MDYDC kwa kuona umuhimu wao kama vijana Taifa la kesho katika kata ya Buza mta wa Kidagaa Halmashauri ya wilaya ya Temeke jijini Dar Es Salaam.
 Mkazi wa kata ya Buza mtaa wa Kidagaa, Rajabu Charz akizungumza na waandishi wa habari katika kata ya Buza mta wa Kidagaa Halmashauri ya wilaya ya Temeke akitoa wito kwa vijana wenzake kutumia fursa mbalimbali zinazojitokeza  hapa Nchini.
Wakazi wa kata ya Buza mtaa wa Kidagaa waliojitokeza kuhudhuria semina ya mafunzo yaliyotolewa na Mradi wa sauti ya vijana MYIDC ikiwa lengo ni kupata sauti ta vijana pale inapotakiwa kufika ili kuleta maendeleo hapa Nchini.Picha na Agness Francis, Blogu ya Jamii

RAIS DKT MAGUFULI AFUNGUA MKUTANO MKUU WA 33 WA JUMUIYA YA TAWALA ZA MITAA TANZANIA (ALAT) JIJINI DAR ES SALAAM LEO

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na meza kuu wakipata picha ya kumbukumbu na wadau wa maendeleo na wafadhili wakuu wa Mkutano Mkuu wa 33 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) baada ya kuufungua katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo. 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda akiongea machache wakati wa kuanza kwa hafla ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa 33 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) Bw. Gulma Hafeez Muccadam akisoma risala yao mbele ya Rais Dkt magufuli wakati wa kuanza kwa hafla ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa 33 wa katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo.
Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Suleiman Jaffo mbele ya Rais Dkt magufuli wakati wa kuanza kwa hafla ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa 33 wa katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo.
Waziri Mkuu Mhe Kassim majaliwa akimkaribisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kufungua wa Mkutano Mkuu wa 33 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo.




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akifungua wa Mkutano Mkuu wa 33 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipeana mikono na Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya NMB Bi. Ineke Bussemaker baada ya kufungua Mkutano Mkuu wa 33 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiagana na Makamu Mwenyekiti wa ALAT Bw. Stephen Mhapa baada ya kufungua Mkutano Mkuu wa 33 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiagana na Mstahiki Meya wa Dar es salaam Mhe. Isaya Mwita Baada ya kufungua Mkutano Mkuu wa 33 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akifurahia ngoma ya Kigogo wakati akiwasili kufungua Mkutano Mkuu wa 33 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akitembelea banda la benki ya NMB na mabanda mengine kabla ya kufungua wa Mkutano Mkuu wa 33 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo. PICHA NA IKULU.

MAKAMU WA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN UZINDUZI WA MAKUMBUSHO MPYA YA OLDUVAI - NGORONGORO

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Makumbusho mapya ya mambo ya kale katika bonde la Olduvai ndani ya hifadhi ya Ngorongoro, wengine pichani  ni Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Profesa Jumanne Maghembe (kushoto) pamoja na Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo (kulia). ( Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akipiga makofi pamoja na Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Profesa Jumanne Maghembe (kushoto) pamoja na Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo (kulia) mara baada ya kukata utepe kuashiria uzinduzi wa Makumbusho mapya ya mambo ya kale katika bonde la Olduvai ndani ya hifadhi ya Ngorongoro. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akipata maelezo mbali mbali kuhusu maisha ya binadamu na wanyama wa kale kutoka kwa Mhifadhi wa Mambo ya Kale kutoka Makumbusho ya Taifa Dkt. Agness Gidna mara baada ya kufungua Makumbusho mapya ya mambo ya kale katika bonde la Olduvai ndani ya hifadhi ya Ngorongoro. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiangalia historia kuhusu maisha ya binadamu na wanyama wa kale iliyopo kwenye Makumbusho ya Olduvai mara baada ya kufungua Makumbusho mapya ya mambo ya kale katika bonde la Olduvai ndani ya hifadhi ya Ngorongoro.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiangalia uzinduzi wa tovuti na mtanzao wa bure wa Hifadhi ya Ngorongoro mara baada ya kufungua Makumbusho mapya ya mambo ya kale katika bonde la Olduvai ndani ya hifadhi ya Ngorongoro.
:Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akihutubia mara baada ya kufungua kufungua Makumbusho mapya ya mambo ya kale katika bonde la Olduvai ndani ya hifadhi ya Ngorongoro. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

STARS WAJICHIMBIA NJE YA MJI KUJIANDAA NA WAMALAWI JUMAMOSI UWANJA WA UHURU

$
0
0



Na Zainab Nyamka,Globu ya Jamii.
TIMU ya Taifa Tanzania Taifa Stars wameingia kambini jana kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa kirafiki dhidi ya Malawi unaotarajiwa kufanyika siku ya Jumamosi kuanzia saa 10 alasiri katika dimba la Uhuru.

Stars inakutana na Malawi ikiwa ni mara ya pili kwa mwaka baada ya kuvaana nao June 25 mwaka huu katika michuano ya COSAFA yaliyofanyika nchini Afrika Kusini na kufanikiwa kupata wa ushindi wa goli 2-0.

Timu hiyo chini ya Salum Mayanga inafanya mazoezi katika Uwanja wa Boko Veterani nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam na tayari Nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Ally Samatta tayari ametua nchini kuungana na nyota wengine wa Tanzania katika mazoezi ya pamoja.

Kocha Mayanga mapema wiki iliyoisha aliita kikosi kitakachounda Taifa Stars kwa ajili ya kuvaana na Malawi siku ya Jumamosi na akiwajumuisha nyota mbalimbali na akimrudisha Ibrahim Ajib baada ya kutokumuita kwa muda mrefu sambamba na golikipa Peter Manyika.

Mayanga aliteuliwa Januari 4, mwaka huu ameita nyota watano wanacheza soka nje ya mipaka ya Tanzania akiwamo nahodha wa kikosi hicho, Mbwana Ally Samatta.
Kikosi hicho kina makipa Aishi Manula (Simba SC), Ramadhani Kabwili (Yanga) na Peter Manyika (Singida United).
Mabekii ni Gardiel Michael (Yanga), Boniphace Maganga (Mbao FC), Abdi Banda (Baroka FC/Afrika Kusini), Kelvin Yondani (Yanga), Salim Mbonde (Simba SC), Erasto Nyoni (Simba SC) na Adeyum Ahmed (Kagera Sugar).


Viungo ni Himid Mao ambaye pia ni Nahodha Msaidizi (Azam FC), Hamisi Abdallah (Sony Sugar/Kenya), Muzamil Yassin (Simba SC), Raphael Daud (Yanga), Simon Msuva (Difaa El Jadidah/Morocco), Shiza Kichuya (Simba SC), Abdul Hilal (Tusker/Kenya) na Morel Orgenes (FC Famalicao/Ureno).
Washambuliaji ni Mbwana Samatta (KRC Genk/Ubelgiji), Ibrahim Hajib (Yanga) na Mbaraka Yussuph (Azam FC). 

Benchi la Ufundi la Mayanga linaundwa na yeye mwenyewe ambaye ni Kocha Mkuu, Fulgence Novatus (Kocha Msaidizi), Ame Ninje (Kocha Msaidizi), Patrick Mwangata (Kocha wa Makipa), Danny Msangi (Meneja), Dkt. Richard Yomba (Daktari wa timu), Dkt. Gilbert Kigadye (Daktari wa Viungo) na Ally Ruvu (Mtunza Vifaa).

Shirkisho la mpira wa miguu nchini wamewataka watanzania kwa ujumla kujitokeza kwa wingi kuja kuishangilia timu ya Taifa kwa kujenga dhana ya mchezaji wa 12 uwanjani wakati wale 11 akiwamo Msuva, Ajib, Mbaraka wakileta faraja ya mabao.

DK. KALEMANI : NI MARUFUKU UMEME KUKATIKA JIJINI DSM KWA SASA

$
0
0
Na Zuena Msuya
Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dkt. Medard Kalemani amesema kuanzia sasa ni marufuku nishati ya umeme kukatika katika jiji la Dar es salaam, kwa kuwa Mradi wa kuimarisha miundombinu ya nishati hiyo imekamilika.
Dkt. Kalemani alisema hayo Octoba 2, 2017 wakati wa ziara yake ya kutembelea mradi huo, uliojengwa na Serikali kwa msaada wa Serikali ya Japani kupitia Shirika lake la Maendeleo la  JICA kwa ajili ya kuimarisha huduma ya upatikanaji umeme katika jiji la Dar es salaam, ikiwemo maeneo ya hospitali, biashara, viwanda na makazi ya watu.
Dkt. Kalemani alisema kuwa mradi huyo ulijengwa mahususi kwa mkoa wa Dar es salaam, kwakuwa kwa sasa ni jiji hilo ni  la kibiashara hivyo matumizi ya nishati ya umeme yanaongezeka kwa kasi ikilinganishwa na miaka ya nyuma. 
Aidha aliweka wazi kwamba, ameridhishwa na kufurahishwa na kasi ya ujenzi ya utekelezaji wa mradi huo, uliogharimu kiasi cha shilingi bilioni 66.4 za kitanzania, ambao umejengwa kwa kipindi cha miaka miwili na nusu badala ya mitatu kama  ilivyokuwa imepangwa hapo awali.
Akizungumzia utunzaji wa vituo hivyo, Dkt. Kalemani aliwataka Mameneja na wasimamizi wa vituo hivyo kufanya kazi kwa uadilifu na weledi mkubwa, na kuhakikisha kuwa ukarabati wa mara kwa mara unafanyika ili viweze kutumika kwa muda mrefu zaidi.
Katika ziara hiyo, Dkt. Kalemani alitembelea vituo vitano vya kupooza umeme vilivyojengwa ambavyo ni pamoja na kituo cha Muhimbili, ambapo pamoja na mambo mengine aliagiza kutokukatika kwa umeme katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete,(JKCI) na Chuo Kikuu cha Tiba Muhimbili( MUHASI).
Alitoa agizo hilo kwa kuwa kito hicho kinauwezo wa kutoa umeme wa megwati 12 na mahitaji halisi ya umeme katika maeneo hayo ni megawati 4 tu mpaka sasa.
“Mradi wa kuimarisha huduma ya upatikanaji wa umeme wa uhakika kwa jiji la Dar es salaam, umekamilika kabla ya wakati uliopangwa , hongereni sana, sitarajii kusikia kwamba umeme umekatika katika jiji hili wala katika hospitali zote za Mkoa wa Dar es salaam, na endapo itatokea aliyehusika atawajibika” alisisitiza Dkt. Kalemani
Pia, alitembelea kituo cha kupokea na kupoza umeme cha Ilala ambacho baada ya ukarabati wa miundombinu yake, kwa sasa kinauwezo wa kuhudumia wateja zaidi ya laki moja tofauti na ilivyokuwa awali ambapo kilikuwa kinahudumia wateja 40 Elfu.
Pamoja na kituo hicho, njia mpaya ya umeme wa Kv 132 kutoka Ubungo imejengwa, hivyo kuimarisha upatikanaji wa uhakika na wa kutosha wa umeme katika Hospitali ya Amana , Maeneo ya biashara, na Makazi ya watu.
Sambamba na hilo, Dkt. Kalemani pia alitembelea kituo cha Mwanyamala ambacho kinauwezo wa kutoa umeme wa megawati 12, na mahitaji halisi kwa sasa ni megawati 6 tu. 
Aidha alitembelea vituo vya Jangwani na Masaki ambavyo pia vinauwezo wa kutoa megawati 12 za umeme, hivyo kuagiza kuwa ni marufuku kukatika kwa umeme katika maeneo yote yanayozunguka vituo hivyo zikiwemo hoteli kumbwa na makazi ya watu.
 Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dkt. Medard Kalemani( wa pili kushoto)akikagua kituo cha kupokea na kupooza umeme cha Ilala wakati wa ziara yake ya kukagua Mradi wa kuimarisha miundombinu ya umeme katika Mkoa wa Dar es salaam, kushoto ni Meneja wa Tanesco Mkoa wa Ilala, Mhandisi Atanasius Nangali ambaye ndiye msimamizi wa kituo cha cha Ilala na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania( TANESCO) Mhandisi Titus Mwinuka( kulia).
 Moja ya Transfoma mpya zilizofungwa katika vituo vya Mradi wa Kuimarisha Miundombinu ya umeme kwa mkoa wa Dar es Salaam. 
 Sehemu ya mitambo ya kupokea na kupoza umeme katika vituo vya Mradi wa Kuimarisha Miundombinu ya umeme kwa Mkoa wa Dar es Salaam. 
Sehemu nyaya zilizotandazwa chini ya ardhi zinazotoka na kuingia katika Vituo vya Mradi wa Kuimarisha Miundombinu ya umeme kwa Mkoa wa Dar es Salaam. 

UWT MKOA WA MBEYA WATOA ELIMU YA AFYA YA UZAZI KWA WANAFUNZI WA SEKONDARI KUELEKEA MAHADHIMISHO YA MIAKA 38

$
0
0
Na Mwandishi wa Globu ya Jamii Mbeya

Umoja wa wanawake wa  Chama Cha Mapinduzi Tanzania (UWT) wilaya ya Mbeya mjini  imendesha zoezi la kutoa elimu ya afya ya uzazi na Maendeleo  kwa wanafunzi  wa shule ya kutwa ya Mbeya .

akizungumza na Globu ya Jamii   Katibu wa UWT  Mkoa wa Mbeya , Mary Mwenisongole amesema kuwa kwa kushirikiana na wataalam wa afya na Maendeleo ya jamii,leo tarehe  wameshiriki kutoa elimu ya afya na kujitambua kwa watoto wa kike zaidi ya 500 shule ya sekondari ya kutwa Mbeya ikiwa ni sehemu ya maazimisho ya wiki ya  miaka 39 ya jumuiya ya wanawake.

'' Sisi kama Jumuiya ya Wanawake wa chama kikongwe hapa nchini tumeona kuwa katika shamra shamra za miaka zaidi ya 38 ya Jumuiya yetu ndani ya chama ni vyema tukaanza kutoa elimu ya afya ya uzazi kwa watoto wa kike waliopo mashuleni kwani wao ndio Viongozi wa UWT ya baadae" amesema .

  Akishukuru kwa niaba ya ya Walimu mwalimu wa nidhamu   Benson John aliishukuru jumuiya kwa jambo walilofanya na kuomba waendelee kwani tatizo la mimba ni kubwa na kwa mwaka huu 2017 kufikia mwezi wa 9 wanafunz 6 wameshindwa kuendelea na masomo yao kutokana na tatizo la ujauzito.

 UWT  mkoa wa Mbeya imewahakikishia walimu kuwa zoezi hili lita kuwa endelea na katibu UWT ameahidi kufika mara nyingi iwezekanavyo kupitia mpango  wa sauti ya shangazi ambayo imepokelewa kwa shangwe, na wanafunzi wameahidi kutoa ushirikiano kwa SHANGAZI.

 Katibu wa UWT mkoa wa Mbeya Mary Mwenisongole   akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Kutwa ya Mbeya katika programu ya Ongea na Shangazi
 Afisa Maendeleo ya Jamii wa Mbeya Mjini Mama Mtani akizungumza na na Wanafunzi wa kike wa Mbeya kutwa.

WANACHAMA WA MTANDAO WA KIJANI KIBICHI TANZANIA WAKAGUA SHAMBA LA UWEKEZAJI MKUBWA WA KILIMO CHA PAPAI RUAHA, IRINGA

$
0
0

Mwenyekiti wa Bodi ya Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania (Mkikita) Mkakati wa Dkt. Kissui Stephen Kissui akielezea malengo ya ziara YA Wakulima wanachama wa mtandao huo walipowasili katika eneo la shamba hilo lililopo Ruaha- Kware, wilayani Kilolo, mkoani Iringa, patakapolimwa zao la kibiashara la Papai. Kushoto kwake ni Mkurugenzi Mtendaji na Mwanzilishi wa mtandao huo, Adam Ngamange, Wa pili kushoto ni Afisa Mtendaji Kilimo na Mifugo wa Ruaha -Kware Wilaya ya Kilolo, John Mchopa, na Mwenyeji wa Shamba hilo na mkulima wa Ruaha, Amani Matinya. 

Dk. Kissui amesema lengo ya ziara hiyo ni kuwaonesha Wakulima wanachama wa Mkikita mashamba wanayotarajia kuanza kulima kwa mkataba pia kuutangaza mtandao huo ili watu waanze kuwaza kijani na kila mtu arudi kwenye kilimo. 

Alisema kama mtu hawezi kulima mwenyewe kuna wataalamu mbao watawekwa shambani kwa gharama nafuu ambao wataweza kuendeza mashamba hayo. 

Pia, Dk. Kissui alisema wanatumia mbegu za kisasa zinazozalisha mara tatu zaidi na mbolea za Organic ambazo hazina madawa na haziharibu ardhi ili kuhakikisha vizazi na vizazi viweze kufurahia. Alisema pia Mkikita husaidia kutafuta masuala ya masoko duniani kabla ya kuanza kulima zao husika. 

"Sisi tunaanza kutafuta masoko ya ndani na nje na baadaye tunawaaunganisha wakulima kwenye masoko" Alisema Kissui.

Wanachama wa Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania (MKIKITA) wakiwasili Ruaha -Kware Wilaya ya Kilolo, Mkoa wa Iringa wakati wa ziara ya kujionea shamba lenye ekari 3000 kwa ajili ya kuwekeza Kilimo cha PAPAI.

Mkurugenzi Mtendaji wa Mkikita, Adam Ngamange akielezea miradi ya kuhamasisha kilimo na ufugaji kibiashara wakati wa ziara ya kutembela shamba kwa ajili ya kuwekeza kilimo cha PAPAI Ruaha -Kware Wilaya ya Kilolo Mkoa wa Iringa. 

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji na Mwanzilishi wa Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania, Adam Ngamange alisema katika mtandao wanafanya miradi ya uhamasishaji kilimo na ufugaji kibiashara. 

Alisema waligundua Watanzania wengi wanalima lakini si kibishara ambapo wameanza na miradi mitano katika maeneo maalum kama Ruaha ambako waendesha kilimo cha Papai kwa kufuata taratibu zote za msingi za kilimo hai. 

Aliongeza kuwa mradi huo utakaoanza na ekari 384 zitakazogawanywa katika mafungu ya ekari 32 na kupandwa katika utaratibu wa kili mwezi mara moja ili waweze kusambaza papai kwenye masoko makubwa.

Wanachama wa Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania wakitembelea na kukagua shamba kwa ajili ya kuwekeza kilimo cha PAPAI.
Mwenyekiti wa Bodi ya Mkikita, Dk. Kissui (katikati) amueleza jambo Mwenyeji wa Shamba hilo na mkulima wa Ruaha, Amani Matinya.
Mwenyeji wa Shamba hilo na mkulima wa Ruaha (alienyosha mkono), Amani Matinya akiwaonesha wanachama wa Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania ukumbwa shamba hilo na mbinu zinazotumika kumwagilia.
Muonekano wa shamba hilo.
Wanachama wa Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania wakielekea kujionea maji yanayotoka Mto Lukosi unaotumika kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji.
Wanachama wa Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania wakiangalia mashine zinazovuta maji kutoka Mto Lukosi kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji.
Muonekano wa Mto Lukosi.
Mmoja wa wakulima wa eneo la Ruaha -Kware Wilaya ya Kilolo Mkoa wa Iringa (kulia) akifafanua jinsi maji yanavyo sambazwa kwa wakulima.
Wanachama wa Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuhitimisha ziara hiyo.
Wanachama wa Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania wakipanda kwenye basi tayari kuanza safari kuelekea jijini Dar es Salaam. HABARI/ PICHA NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG

STARTIMES WASHEREKEA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA KWA KUZINDUA CHANELI MPYA KWA WATEJA WAKE

$
0
0





KATIKA kusherekea wiki ya huduma kwa wateja kampuni inayotoa huduma za ving'amuzi Tanzania Wamezindua chaneli mpya kwa wateja wake.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es aSalaam leo, Mkurugenzi wa uendeshaji wa Startimes, Carter Luoh amesema kuwa kampuni hiyo wameongeza chaneli mpya katika king'amuzi ambapo wanajisogeza karibu na wateja wake.

Pia amesema kuwa Startimes inafuraha kubwa kutoa huduma za kidijitali kwa mikoa 17 kwa kutoa huduma za ving'amuzi ambayo imewafikia wateja wa mikoa zaidi ya 17 hapa nchini kwa kuwafikia wateja kwa kufungua zaidi ya mawakala 300.

Kwaupande wake Meneja uendeshaji wa Startimes, Gaspa Ngowi amesema kuwa katika wiki hii muhimu ya huduma kwa wateja wamezindua chaneli nyingine mpya kwenye king'amuzi cha startimes pamoja na pamoja na chaneli zitakazokuwa kimetafsiliwa kwa kiswahili pamoja na movi za kihindi.


 Mkurugenzi wa uendeshaji wa Star Media (T) Ltd, Carter Luoh akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Startimes jijini Dar es Salaam leo wakati wa kuzindua chaneli mpya ya kwenye king'amuzi cha Startimes katika wiki ya huduma kwa wateja.

















 Mkurugenzi wa uendeshaji wa Star Media (T) Ltd, Carter Luoh (katkati) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na Kampuni ya Startimes kuzindua chaneli mpya katika king'amuzi cha Startimes wakati wa kuzindua wiki ya huduma kwa wateja na kujiweka karibu zaidi na wateja wake. Kulia ni Meneja wa Huduma kwa wateja wa Startimes, Henry Ngailo na Kushoto ni Meneja uendeshaji wa Startimes, Gaspa  ngowi.
 Meneja uendeshaji wa Startimes, Gaspa  ngowi akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa kuzindua chaneli mpya ya king'amuzi cha Satrtimes katika kusherekea wiki ya huduma kwa wateja ambayo hufanyika kila wiki ya kwanza ya mwezi Oktoba ikiwa ni kujiweka karibu zaidi na wateja wake. Amesema kuwa sherehe hizi zinaambatana na uongezwaji wa chaneli mpya kama vile ST Bollywood Afrika, ST Bollywood na FOX life. katikati ni Mkurugenzi wa uendeshaji wa Star Media (T) Ltd, Carter Luoh (katkati) na Kulia ni Meneja wa Huduma kwa wateja wa Startimes, Henry Ngailo.
 Mkurugenzi wa uendeshaji wa Star Media (T) Ltd, Carter Luoh akikata keki kwa pamoja na wateja wa king'amuzi cha Startimes kwaajili ya kusherekea wiki ya huduma kwa wateja.
Mkurugenzi wa uendeshaji wa Star Media (T) Ltd, Carter Luoh akiwalisha keki wateja jijiji Dar es Salaam leo mara baada ya kufungua chaneli mpya katika king'amuzi cha startimes katika wiki ya huduma kwa wateja.

 Meneja wa mitambo wa Startimes, Yusuph Baracha akizungumza na wateja wa startimes jijini Dar es Salaam leo mara baada ya kuwatembeza katika chumba cha kurushia matangazo na vipindi mbalimbali vya king'amuzi cha startimes.
 Meneja wa mitambo wa Startimes, Yusuph Baracha akizungumza na wateja wa startimes jijini Dar es Salaam leo mara baada ya kuwatembeza katika chumba cha kurushia matangazo na vipindi mbalimbali vya king'amuzi cha startimes.
  Meneja uendeshaji wa Startimes, Gaspa  ngowi akizungumza na wateja wa startimes jijini Dar es Salaam leo wakati wa wiki ya huduma kwa wateja ambayo huadhimishwa kila wiki ya kwanza ya mwezi Oktoba.
Meneja wa Huduma kwa wateja wa Startimes, Henry Ngailo akizungumza na wateja wa startimes jijini Dar es Salaam leo wakati wa wiki ya huduma kwa wateja ambayo huadhimishwa kila wiki ya kwanza ya mwezi Oktoba.
Picha na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.

TIMU ZA TANZANIA KIKAPU ZAANZA VIBAYA MICHUANO YA KANDA YA TANO AFRIKA

$
0
0


Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
Timu tatu za Tanzania za mpira wa kikapu zimeshindwa kutamba mbele ya timu kutoka nchi zingine katika mashindano ya klabu bingwa kanda ya tano yanayoendelea katika jiji la Kampala nchini Uganda.

Michuano ya Klabu  Bingwa kanda ya tano (Zone 5) yameanza jana huku timu za Tanzania zikionekana kuanza vibaya, wanaume wakianza kwa hatua ya makundi na wanawake wakianza kwa mtoano.

Tanzania imewakilishwa na Savio na  ABC kwa upande wa wanaume na DB Lioness kwa upande wa wanawake. Matokeo ya siku mbili ya michuano ya kanda ya tano yanayoendelea jiji la Kampala.


Day 1

APR 45 (Rwanda ) /KCCA (Uganda) 57 -wanawake


UCU 108 (Uganda) /Horseed 42 (somalia) -wanawake

Equity Bank  70 (Kenya) / DB Lioness 48 (Tanzania) -wanawake

Hawasa  43(Ethiopia)/ Patriot 110 (rwanda) -wanaume


KPA 108 (Kenya) /Gonder city 35 (Ethiopia) -wanaume

City Oilers  93 (Uganda)/ Savio  46 (Tanzania)  -wanaume


Betway Power  87 (Uganda) / ABC 55 (Tanzania)  -wanaume


Day 2
APR 84 (Rwanda ) /DB Lioness 48 74 (Tanzania) - wanawake

KPA 81 (Kenya)  /ABC 77 (Tanzania )  -wanaume

Patriots  77(Rwanda) /Savio  48 (Tanzania ) - wanaume

KCCA 51 (Uganda) /Equiyt Bank 56 (Kenya) - wanawake

UCU 69 (Uganda) /KPA 68  (Kenya)  - wanawake

City Oliers  111 (Uganda) /Hawasa City  41 (Ethiopia) - wanawake

Betway Power 113 (Uganda) /Gonder City  31 (Ethiopia) - wanaume

UTANDIKWAJI WA BOMBA LA MAJI SAFI WAZIDI KULETA FARAJA KWA WAKAZI WA MBEZI

$
0
0
Mmoja wa Vibarua wanaochimba mtaro wa kutandika bomba la maji linaloelekea Mbezi Makabe akiwa anaendelea na kazi ya kuchimba mtaro

Bomba la Maji Safi kutoka Dawasco ambalo limetandikwa ndani ya mtaro kuelekea Mbezi Makabe mpaka Msakuzi kwa ajili ya kupeleka maji safi , Wakazi wa eneo hilo wanapata maji ya Bomba kwa mara ya kwanza katika utawala wa awamu ya tano ya Dk John Pombe Magufuli tangu nchi hii ipate uhuru
Kibarua wa kuchimba mtaro akiendelea na kazi ya kuchimba mtarokwa ajili ya kupitisha bomba la Maji ya Dawasco katika eneo la Mbezi Makabe mpaka Msakuzi
Bomba la Maji likiwa limetandikwa kwenye mtaro tayari kwa ajili ya kufukiwa kwa ajili ya kupeleka maji Mbezi Makabe mpaka Msakuzi . Picha zote Na Humphrey Shao

FILAMU YA BEI KALI KUZINDULIWA RASMI KESHO MLIMANI CITY

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

FILAMU ya Bei Kali inatarajiwa kuzinduliwa kesho katika ukumbi wa Mlimani City Golden Premier huku wasanii wakijinasibu kuwa ni moja kati ya filamu bora ndani ya soko la filamu.

Filamu hiyo inayojulikana kwa jina la 'Bei Kali' itazunduliwa rasmi kesho kuanzia saa moja usiku ikiwa mbashara kupitia kituo cha televisheni cha Azam Tv kwenye chaneli ya Sinema zetu na kuanza kuingia mtaani.

Akizungumza na Globu ya Jamii, Daud Michael 'Duma' amesema kuwa filamu hiyo iliyofanywa chini ya Kwetu Studio imeweza kuchukua waigizaji wakubwa akiwemo Irene Uwoya, Hemed Suleiman, Patcho Mwamba na Kaptu Rado.

Duma amesema kuwa filamu hiyo inayoelezea maisha ya kawaida yenye mahusiano ndani yake yakimuhisha mwanadada aliyetoroshwa na mwanaume mwingine na kuletwa mjini lakini alipofika akajiingiza katika mahusiano mengine tofauti na baadae mumewe akaja kumtafuta mjini.

Ameeleza kuwa, filamu hiyo imejaa uhalisia zaidi na ana imani wapenzi wa filamu za kitanzania wataoendezewa nayo kwani imeweza kugusa maisha hali ya kitanzania hasa katika mahusiano na ndoa.

Filamu hiyo, imesimamiwa na Kaptu Rado sambamba na Rashidi Mrutu ambapo Duma amesema itakuja kuwakamata mtaani kwa ubora mzuri na hata waigizaji wake wameweza kutendea haki sehemu walizopatiwa.

BENKI YA CRDB TAWI LA QUALITY CENTER WAZINDUA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA

$
0
0

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei, akizungumza na wateja wa benki hiyo tawi la Quality Center jijini Dar es Salaam, ikiwa ni maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja Duniani. (Na Mpiga Picha Wetu).
Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Quality Center, Clementine Kinabo, akizungumza na Wateja wa Benki hiyo ikiwa ni maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja iliyofanyika katika tawi hilo Barabara ya Nyerere jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya NN General Supplies, Selina Letara, akimshukuru Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei,wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja iliyofanyika katika tawi Quality Center.
Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Quality Center, Clementine Kinabo, akimshukuru Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei, baada ya kukutana na wateja wa tawi la Quality Center.Meneja wa Wateja wa Mikopo Midogo na ya Kati wa Benki ya CRDB, Mussa Mwinyidaho, akitoa mada.
Meneja Mahusiano Huduma za Biashara, Baraka Eusebio, akitoa mada kuhusu huduma za Biashara.
Ofisa wa Benki ya CRDB Anayehusika na Ubadilishaji Fedha na Masoko ya Mtaji, Olais Tira, akitoa mada kwa wateja wa Benki ya CRDB (hawapo pichani), wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja iliyofanyika katika tawi la Quality Center.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya PMM Estates (2001), Dk. Judith Mhina, akichangia mada katika maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja iliyoandaliwa na Benki ya CRDB tawi la Quality Center.

Ofisa Mikopo wa Benki ya CRDB, Eric Mgonja, akizungumza katika hafla iliyoandaliwa kwa ajili ya wateja wa benki hiyo, wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja.

Maofisa wa Benki ya CRDB wakiwa wameshika keki maalumu wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja iliyofanyika katika tawi la Quality Center Barabara ya Nyerere Dar es Salaam.

Meneja wa Benki ya CRDB, tawi la Quality Center, Clementine Kinabo (kushoto), akimkabidhi tuzo maalumu, Mhasibu Mkuu wa Kampuni ya Master Mind Tobacco, Joseph Dominic, wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja, iliyofanyika iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya PMM, Dk. Judith Mhina, akipokea tuzo maalumu kutoka kwa Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Quality Center, Clementine Kinabo (kushoto), wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja.

Keki.

Wateja wa Benki ya CRDB tawi la Quality Center wakikata keki wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja iliyofanyika katika tawi hilo Barabara ya Nyerere Dar es Salaam.

Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Quality Center, Clementine Kinabo, akimlisha keki Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya NN General Supplies, Selina Letara.

Wateja wakipata keki.

Kufungua Champagne.

Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Quality Center, Clementine Kinabo (katikati), akigonganisha glasi na wateja.

Kunywa kwa afya.

Baadhi ya maofisa wa Benki ya CRDB tawi la Quality Center wakiwa katika picha ya pamoja.

Picha ya pamoja.
Zawadi kwa wateja.
Baadhi ya wateja wakiwa na zawadi zao.
Picha ya pamoja.
Mkurugenzi wa Fedha wa Kampuni ya Easy Connection, Justus Bashara, akiishukuru Benki ya CRDB kwa niaba ya wateja wenzake.

BENKI YA UBA TANZANIA WAZIDI KUNG'ARA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA

$
0
0
 Afisa huduma kwa wateja wa Benki ya UBA Tanzania, Bi Stella Matau akifurahia kumuhudumia mmoja wa wateja wao wakubwa aliyefika katika benki hio huku benki hio ikiendelea kung'ara katika kutoa huduma bora kwa wateja kwa wakati wote
Baadhi ya wafanyakazi wa benki ya UBA Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wateja wao waliofika katika benki hio kwaajili ya kupata huduma za kibenki
Meneja Uendeshaji wa Benki ya UBA Tanzania, Bw Chriss Byaruhanga (wa Kwanza kushoto) akikata keko na baadhi ya wateja wao ikiwa ni ishara ya kuendeleza shamrashamra za wiki ya huduma kwa wateja ambapo wateja hao wameisifu benki hio kwa kutoa huduma bora wakati na sio kwa kipindi cha kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja.
Meneja Uendeshaji wa Benki ya UBA Tanzania, Bw Chriss Byaruhanga akigawa keki kwa baadhi ya wateja na wafanyakazi wa benki hio ikiwa ni ishara ya kuzindua wiki ya huduma kwa wateja.
Mmoja wa wateja wa benki ya UBA Tanzania akipata huduma ya kuweka pesa 
Mkuu wa idara ya masoko wa benki ya UBA Tanzania, Brendasia Kileo akigawa keko kwa mmoja wa wateja waliokuwa wakipata huduma ndani ya benki mapema leo ikiwa ni muendelezo wa wiki ya Huduma kwa wateja
Wiki ya huduma kwa wateja inaendelea huku benki ya uba tanzania ikiendelea kutoa huduma bora na zenye kutimiza malengo ya wateja wao huku kituo chao cha huduma kwa wateja kikiendelea kushika hatamu kwa wateja wao kwa kuwapa huduma bora masaa 24. Uba Bank ambao hivi karibuni walijidhatiti tena kwa kuanzisha kituo cha huduma kwa wateja kwa masaa 24 wamezidi kuwapatia huduma bora wateja wao bila kuangalia kuwa ni wiki ya huduma kwa wateja wao Hutoa huduma bora siku zote.
Uba bank wanafurahi kuwahudumia wateja wao siku zote huku wiki ya huduma kwa wateja ikiendelea kuwa sehemu tu ya kuendeleza kutoa huduma bora kwa wateja.
Viewing all 40096 articles
Browse latest View live
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>