Quantcast
Channel: MTAA KWA MTAA BLOG
Viewing all 40051 articles
Browse latest View live

WASIFU WA MZEE ALIYEFARIKI DUNIA AKITAFUTA NGUVU ZA KIUME ‘UNATISHA’

$
0
0
MZEE Joseph Sahani (60) ambaye amefariki duniani akiwa kwa mganga wa kienyeji akifanyiwa dawa ya kuongeza nguvu za kiume, imebainika kwamba alikuwa na wake wawili, watoto zaidi ya 10 na ameacha utajiri wa ng’ombe zaidi ya 50.
Mwili wa Mzee Sahani aliyefariki dunia Jumapili jioni umezikwa katika Kijiji cha Ipango jirani na Kijiji cha Nzoza mahali alipozaliwa katika Kata ya Salawe Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga mkoani Shinyanga. Alifariki dunia akiwa anapatiwa matibabu kwa mganga wa kienyeji, Robert Mkoma ambaye anaishi wilayani Kwimba mkoani Mwanza.
Baadhi ya wakazi wa Kijiji cha Nzoza, Shija Kulwa na Mariamu Kuhenge walimueleza mwandishi wa habari hizi kuwa mganga huyo siyo mkazi wa kijiji hicho, bali hutembelea maeneo mbalimbali kwa madhumuni ya kutafuta wateja na kuwapatia huduma ya matibabu.
Kulwa alisema Sahani alipewa taarifa na rafiki yake, Pastori Sitta ambaye alimkaribisha mganga huyo ili afanye matibabu kwa wenye matatizo ya kuishiwa nguvu za kiume na siyo mara yake ya kwanza kufika katika kijiji hicho.
“Mganga huyu siyo mara yake ya kwanza kufika katika kijiji hiki kwani alikwisha kuja na kumtibu mwanaume mmoja aliyeishiwa nguvu za kiume na kuanza kujisifia mitaani kuwa amepona, ndio Mzee Sita alipomfuata Mzee Sahani baada ya kuwa alimueleza naye ana tatizo la kukosa nguvu za kiume na kumhakikishia mganga huyo anaweza kumtibu vizuri tatizo lake,” alidai mkazi huyo wa Nzoza.
Kaimu Mwenyekiti wa Kijiji cha Nzoza, Masalu Msalaba alisema alipewa taarifa na baadhi ya wananchi kuhusu kifo cha Mzee Sahani, kwamba alikuwa akipatiwa matibabu kwa mganga wa kienyeji ndipo alipochukua hatua ya kuwapigia askari Polisi wa Kituo cha Salawe.
Diwani wa Kata ya Salawe, Joseph Buyugu alisema mganga huyo alifika kwa mara ya kwanza kwenye familia ya Mzee Sitta na kumtibu mwanawe aliyekuwa akidaiwa ana tatizo la kukosa nguvu za kiume na alimtibu huku watu wakiamini alimponyesha baada ya yeye na mkewe kukaa miaka mingi bila kupata mtoto na hatimaye akapata mtoto.
“Mganga huyo ameonekana kuaminika na baadhi ya wananchi wa vijiji vya kata hii baada ya kusikia amerudi tena katika familia hiyo akitokea kwenye mji wake Kwimba mkoani Mwanza kwa lengo la kudai deni lake la uponyaji baadhi ya watu walielezana kuwa mganga yupo na huyo mzee kujitokeza kwa kushawishika kuwa atapona matokeo yake kupoteza maisha,” alieleza diwani Buyugu. Mzee Sahani alifariki kwa mganga wa kienyeji Mkoma wakati akipatiwa matibabu ya kupata nguvu za kiume kwa kuwekewa dawa aina ya unga sehemu za siri iliyoingizwa kwa kutumia pampu ya baiskeli.

Chanzo: Habari Leo

MKUU WA MAJESHI TANZANIA AWAONYA WATU WANAOTUMIA JINA LA JESHI HILO KUDANGANYA UMMA KWAMBA WANATOA AJIRA ZA JESHI

$
0
0
Mkuu wa Majeshi ya ulinzi Tanzania,Generali Venance Mabeyo amekemea na kutoa onyo kali kwa baadhi ya watu wanaotumia mwanvuli wa wastaafu wa jeshi,askari wa jeshi au nafasi ya vyeo vyao ndani na nje ya jeshi la wananchi Tanzania kwa kulaghai umma kwamba watoe fedha ili wawasaidie kupata ajira ndani ya jeshi hilo.

Mkuu wa Majeshi ya ulinzi Tanzania,Generali Venance Mabeyo alifika katika kituo cha ITV na kupokelewa na mkurugenzi wa ITV/Radio One Joyce Mhavile pamoja na viongozi wengine na kusaini kitabu cha wageni mashuhuri katika kituo hicho na kisha kutembelea katika maeneo vyumba mbalimbali vya kurushia habari. 

Akizungumza katika kipindi cha dakika 45 kinachorushwa na kituo cha ITV na Radio one kila jumatatu saa 3 usiku na marudio ni jumatano saa 7 kamili mchana,mkuu wa Majeshi ya ulinzi Tanzania,Generali Venance Mabeyo amesema jeshi lake haliwezi kuvumilia baadhi ya watu wenye nia mbaya ya kuchafua jeshi hilo kwa tabia yao mbaya ya kuchukua pesa ndani ya jamii kwa kujifanya watasaidia watu kupata ajira jeshini wakati jeshi la wananchi tanzania halina utaratibu wa kuajiri watu kwa kutumia njia hiyo na hivyo waache tabia hiyo mara moja.

Kwa undani wa mazungumzo na mkuu wa majeshi ya ulinzi nchini Generali Venance Mabeyo,usikose kuangalia kipindi cha dakika 45 jumatatu saa 3 usiku kupitia kituo chako bora cha ITV au kupitia Radio one Stereo.

AHUKUMIWA JELA MIEZI 12 KWA KUMKASHIFU RAIS

$
0
0
MHASIBU wa Shule ya Sekondari ya St Joseph Cathedral, Elizabeth Asenga amehukumiwa kulipa faini ya Sh milioni tano au kwenda jela miezi 12 baada ya kukutwa na hatia ya kutumia lugha ya matusi dhidi ya Rais John Magufuli kuwa kilaza kupitia mtandao wa ‘WhatsApp’.
Hata hivyo, mshitakiwa huyo alilipa faini na kukwepa kwenda jela miezi 12. Akisoma hukumu hiyo jana, Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi alisema mahakama ilisikiliza ushahidi wa pande zote mbili na kumwona mshitakiwa ana hatia. Alisema upande wa mashitaka uliita mashahidi saba, kuthibitisha mashitaka hayo dhidi ya mshitakiwa. “Mahakama inakutia hatiani kwa makosa uliyoshitakiwa nayo, hivyo utatakiwa kulipa faini ya Sh milioni tano au kutumikia kifungo cha miezi 12 jela,” alisema Hakimu Shaidi.
Kabla ya kutolewa adhabu, mshitakiwa aliomba mahakama impunguzie adhabu, kwa kuwa mama yake mzazi ni mzee anamtegemea na ana watoto wanaomtegemea. Katika kesi ya msingi, inadaiwa Agosti 6, mwaka jana aliwasilisha maneno kinyume cha sheria kupitia mtandao wa WhatsApp katika group la wafanyakazi la STJ kwa nia ya kumtusi Rais. Mshtakiwa alinukuliwa kuwa , “Habari za asubuhi humu hakuna rais kilaza kama huyu wetu duniani angalia anavyompa Lissu umashuhuri, fala yule picha yake ukiweka ofisini nuksi tupu ukiamka asubuhi ukikutana na picha yake kwanza siku inakuwa ya mkosi mwanzo mwisho.”

Chanzo: Habari leo

VIDEO: NG’OMBE PORI AZALIWA NA VICHWA VIWILI NCHINI PAKISTANI

$
0
0
Tumezoea kusikia binadamu wanazaliwa wakiwa wameungana vichwa au muda mwingine mapacha wawili kuungana tumbo, lakini hii ya ng’ombe pori kuzaliwa akiwa na vichwa viwili imekuwa ya tofauti na ya kipekee duniani.

Ndama mmoja huko nchini Pakistani amezaliwa na vichwa viwili katika malisho ya Lucky Foods Dairy Farm mjini Karachi.

Zizi la Lucky Foods Dairy Farm ambako ndama huyo wa maajabu amezaliwa.
Ndama huyo ana vichwa viwili, macho manne, masikio manne, midomo miwili amepatwa na hali hiyo ambayo kitaalamu inaitwa (polycephaly) na inatokea kwa wanyama tuu na huenda hii ni mara ya kwanza kwa ng’ombe pori wa namna hiyo kuzaliwa duniani.
Mwaka jana ng’ombe anayefanana na huyo alizaliwa huko nchini Georgia lakini vichwa hivyo vilikuwa vina masikio matatu na tofauti kidogo na ndama huyu.

Ndama huyo aliyezaliwa septemba 27 mwaka huu kwa sasa analishwa maziwa kwa njia ya kawaida kutokana na kushindwa kunyanyua vichwa vyake viwili na kunyonya moja kwa moja kutoka kwa mama yake.Tazama video ya mtoto huyo wa ng’ombe pori (Mbogo) mwenye vichwa viwili

NINI HATMA YA BARCELONA KWENYE LIGI YA HISPANIA?

$
0
0
 Wanachama wa klabu ya Barcelona watalazimika kuamua ni ligi ipi watahitaji kwenda kucheza endapo kama Catalonia itapata uhuru wake kutoka Hispania hayo yamesemwa na rais wa timu hiyo, Josep Maria Bartomeu hapo siku ya Jumatatu.
Klabu hiyo inayotoka katika Jimbo la Catalonia siku ya Jumapili imecheza mchezo wake wa Ligi Kuu nchini Hispania ‘La Liga’ dhidi ya Las Palmas bila ya mashabiki kufuatia vurugu za baadhi ya wakazi kuhitaji kupiga kura ya kujitenga na nchi hiyo wakati Serikali ikizuwia zoezi hilo kwa kutumia askari, Barca ilichomoza na ushindi wa mabao 3-0.
Rais wa klabu ya Barcelona Josep Maria Bartomeu
“Kwa swala la uhuru wa Catalonia klabu na wanachama wake watapaswa kuamua tutapenda kushiriki kucheza,” amesema rais wa klabu ya Barcelona Bartomeu baada ya kikao cha wanachama.
Josep Maria Bartomeu “Tunapitia kipindi kigumu na tutalazimika kuheshimu kile kitakachotokea na kuwa watulivu.”
Waziri wa michezo wa Catalonia, Gerard Figueras wiki iliyopita amesema klabu ya Barcelona inaweza kushiriki Ligi za nchi nyingine kama endapo watapata uhuru kutoka Hispania.
“Kuhusiana na swala la Uhuru timu zote za Catalonia zinazoshiriki La Liga Barcelona, Espanyol na Girona wataamua wapi watapenda kwenda kucheza kama ni hapa Hispania, ama nchi za jirani kama Itali, Ufaransa hata Ligi Kuu ya nchini Uingereza,” amesema waziri wa michezo, Figueras.

RAHCO: Bomoabomoa Moshi, Tanga iko palepale

$
0
0
Kampuni Hodhi ya Rasilimali za Reli (Rahco) imesema bomoabomoa ya nyumba zilizopo katika hifadhi ya reli (mita 30 kila upande) iko palepale tofauti na ilivyoelezwa kwamba kwenye baadhi ya mikoa itakuwa tofauti.
Septemba 29 mwaka huu ofisa habari wa kampuni hiyo, Catherine Moshi aliiambia Mwananchi hili kuwa katika mkoa wa Kilimanjaro, Tanga na Dar es Salaam watalegeza masharti ya umbali kwa majengo yanayopaswa kubomolewa
Leo Jumatano katika tangazo lao lililotolewa katika gazeti la Mwananchi, Rahco imesema itaendelea na zoezi la kuwaondoa wavamizi wote wa hifadhi za reli nchi nzima, waliopewa notisi na kuwekewa alama ya X.
“Rahco inakanusha uzushi unaoenezwa kuwa kuna mabadiliko ya upana katika hifadhi ya reli kwa baadhi ya mikoa,” limeeleza tangazo hilo.

Chanzo: mwananchi

WAAFUNZI WAASWA KUHUSIANA NA SOKO LA AJIRA.

$
0
0
ILI kuondokana na tatizo la ukosefu wa ajili nchini, wanafunzi wametakiwa kuyapenda masomo ya sayansi na hesabu ambayo yatawajengea uwezo wa kupata ajira kupitia kauli mbiu ya Tanzania ya viwanda. 

Mkurugenzi wa shule ya awali na msingi ya Deira English medium ya mjini Babati Mkoani Manyara, mhandisi Nada Narya aliyasema hayo kwenye mahafali ya pili ya darasa la saba na ya nane ya kumalizika elimu ya awali ya shule hiyo. 

Mhandisi Narya alisema shule hiyo imewaanda ipasavyo wanafunzi wa shule hiyo kupenda masomo ya sayansi na hesabu ili kukabiliana na tatizo la ajira kupitia kauli mbiu ya Tanzania ya viwanda hivyo wanafunzi wengine nchini wapende masomo hayo. 

Alisema hivi sasa soko la ajira ni dogo na ili kuondokana na hali hiyo inawapasa wanafunzi kuyapenda masomo sayansi na hesabu kwa lengo la kujiandaa kwa nguvu zote katika kuhakikisha wanajipanga ipasavyo hivi sasa ili baadae wachangamkia fursa ya ajili kupitia Tanzania ya viwanda. 

"Sisi kama Deira tumeanza kuwaandaa wanafunzi wetu wapende masomo ya sayansi na hesabu ili baadaye waweze kuendesha maisha yao kwenye soko la ajira kwani wataalamu mbalimbali watatokea hapa shuleni kwetu," alisema mhandisi Narya. 

Mgeni rasmi wa mahafali hayo, ofisa elimu ya msingi wa halmashauri ya mji wa Babati, Doroth Mwandila alimpongeza mwanafunzi wa darasa la saba wa shule hiyo, Edson Elias kwa kuongoza kwenye mtihani wa moku katika shule 37 za sekondari za halmashauri ya mji huo. 

Mwandila alisema ili kumuandaa kwa ajili ya masomo ya kidato cha kwanza mwakani, anampa mwanafunzi huyo zawadi ya sh20,000 na atamnunulia vitabu, madaftari na kalamu pindi akianza masomo yake kwa lengo la kumpa motisha ya kusoma kwa bidii zaidi. 

Aliwataka wazazi na walezi wa wanafunzi wanaohitimu darasa la saba kwa mwaka huu, kuwafuatilia watoto wao ipasavyo kwenye mienendo yao ya kila siku wakiwa majumbani ili kuhakikisha wanawaanda vizuri kwa ajili ya kuanza elimu ya sekondari mwakani. 

Mwalimu mkuu wa shule hiyo, Daniel Gaitu alisema shule hiyo ilianzishwa rasmi Januari 2010 ikiwa na watoto watano, wavulana wawili na wasichana watatu na hivi sasa ina wanafunzi 253 kati yao wavulana 119 na wasichana 134. 

Gaitu alisema kwa upande wa taaluma, shule hiyo imekuwa ikifanya vizuri kwenye mitihani kwani wanafunzi wa darasa la nne walifanikiwa kushika nafasi ya kwanza kwenye halmashauri ya mji huo katika mtihani wa Taifa wa mwaka 2013, 2014 na nafasi ya pili mwaka 2016. 

Alisema wanafunzi wa darasa la saba wa mwaka jana walishika nafasi ya kwanza kwa mtihani wa Taifa kwenye halmashauri ya mji huo na darasa la saba wa mwaka huu wameshika nafasi ya kwanza kwenye mtihani wa moku mkoa wa Manyara kwenye shule 37 za halmashauri ya mji wa Babati. 
Ofisa elimu msingi wa Mji wa Babati Mkoani Manyara, Doroth Mwandila akimkabidhi mwanafunzi wa darasa la saba wa shule ya msingi Deira English medium Vannesa Nada, cheti cha kuhitimu elimu ya msingi (kushoto)  ni Mkurugenzi wa shule hiyo mhandisi Nada Narya.
Wanafunzi wa darasa la saba wa shule ya msingi Deira English medium ya mjini Babati Mkoani Manyara, wakionyesha mchezo wa kareti wakati wa mahafali yao yaliyofanyika shuleni kwao.

MISS UNIVERSE YAPONGEZWA NA BASATA

$
0
0

Mkurugenzi wa Ukuzaji Sanaa na Masoko wa Basata, Vivian Shalua (wanne kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na warembo, waandaaji na maofisa wa Basata mara baada ya kumalizika kikao cha pamoja cha kujadili mashindano hayo.
 Mkurugenzi wa Compass Communications ambaye pia ndiye mwandaaji mkuu wa mashindano haya Maria Sarungi Tsehai (Kulia) akisisitiza jambo wakati wa kikao na Baraza la Sanaa Tanzania (Basata).Anayesikiliza Mkurugenzi wa Ukuzaji Sanaa na Masoko wa Basata, Vivian Shalua na Afisa Sanaa, Bona Leon Masenge.
 Mkurugenzi wa Ukuzaji Sanaa na Masoko wa Basata, Vivian Shalua (Katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Miss Univerese mwaka jana, Jihan Dimachk (Kulia) na Miss Earth Tanzania, Lilian Loth.
Na Mwandishi wetu
Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) limeipongeza kampuni ya Compass Communications Tanzania kwa kufanya mashindano bora ya Miss Universe hapa nchini.

Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Ukuzaji Sanaa na Masoko wa Basata, Vivian Shalua wakati wa kufanya tathimini ya mashindano hayo na mashindano ya urembo kwa ujumla.

Mrembo Jihan Dimachk alishinda taji la Miss Universe mwaka jana  huku Lilian Loth akishinda nafasi ya pili katika mashindano hayo.

Shalua alisema Basata wamefarijika sana na jinsi mashindano hayo yanavyoendeshwa na hakuna malalamiko yoyote kuhusiana na zawadi na upendeleo.

Alisema kuwa kutokana na utaratibu mzuri wa mashindano yao, Basata imeridhia waandaaji wa mashindano hayo, kufanya mashindano ya mwaka huu na vile vile kuandaa mashindano ya kutimiza miaka 10 tokea kuanzishwa kwa mashindano hayo mwaka 2007.

“Pamoja na kuwa na shindano moja kwa kushirikisha warembo wa mikoa tofauti, bado Basata imefarijika na jinsi mnavyoendesha na utaratibu unaotumia kuwapata warembo, uendeshaji wa mashindano mpaka kumpata mshindi,” 

“Tunajua kuwa kuna changamoto za wadhamini na kusababisha kufanya mashindano yenye kalenda fupi na kuondoa mlolongo wa matukio, hatua hii ni bora zaidi ili kuondoa malalamiko ya zawadi na mambo mengine, huu ni mfano wa kuigwa,” alisema Shalua.

Mkurugenzi wa Compass Communications ambaye pia ndiye mwandaaji mkuu wa mashindano haya Maria Sarungi Tsehai aliishukuru Basata kwa usimamiaji bora wa mashindano katika sekta ya sanaa nchini na kusema kuwa watajihidi kuongeza wigo ili kuona warembo wengi zaidi kutoka mikoa tofauti wanashiriki katika mashindano yao.

Maria alisema kuwa pamoja na changamoto zote wanazokabiliana nazo, bado wanahitaji msaada kutoka Basata ili kupata wadhamini na kufikia malengo yao katika kuendeleza Sanaa hapa nchini.

“Kwa sasa kuna changamoto kubwa ya wadhamini wa mashindano, kuna haja ya kupata msaada kutoka Basata ambao ni chombo cha serikali, mnaweza kutusaidia kupata wadhamini hata kwa Wizara ya Maliasili na Utalii, sisi tunatangaza jina la nchi na utalii pia, tunaamini kupitia kwenu, tunaweza kupata sapoti kubwa kutoka wizara hiyo, Bodi ya Utalii (TTB) na mamlaka ya zake kama Tanapa,” alisema Maria.

BENKI YA NMB ,TAWI LA NELSON MANDELA MJINI MOSHI YASHEREHEKEA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA.

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Anna Mghwira akiwaongoza wageni wengine wakati wa kupata Chai iliyoandaliwa na Benki ya NMB tawi la Nelson Mandela mjini Moshi ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja .
Baadhi ya Wateja wa Benki ya NMB wakipata Chai katika tawi la Nelson Mandela mjini Moshi.
Meneja wa NMB tawi la Nelson Mandela,Emmanuel Kishosha akimueleza jambo Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira wakati akimkaribisha kuzungumza na Wateja a Benki hiyo waliojumuika katika Chai ya asubuhi ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya Huduma kwa Wateja.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Anna Mghwira akizungumza na Wateja wa Benki ya NMB wakati wa Maadhimisho ya wiki ya Huduma kwa Wateja iliyoanza Oktoba Mosi.
Baadhi ya Wateja wa Benki ya NMB pamoja na viongozi mbalimbali wakifuatilia hotuba ya Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro aliotoa wakati wa Maadhimisho ya wiki ya Huduma kwa wateja katika Benki ya NMB tawi la Nelson Mandela.
Meneja wa Benki ya NMB tawi la Nelson Mandela mjini Moshi ,Emanuel Kishosha akielezea Historia ya Benki hiyo ilipotoka na wapi ilipo sasa kwa Wateja wa Benki hiyo .
Baadhi ya Viongozi wa Benki ya NMB tawi la Nelson Mandela mjini Moshi.
Baadhi ya Wafanyakazi wa NMB tawi la Nelson Mandela mjini Moshi wakifurahia wiki ya Huduma kwa Wateja iliyoanza Oktoba mosi.
Meneja wa NMB tawi la Nelson Mandela akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Anna Mghwira cheti cha kutambua mchango wake wakati wa Maadhimisho ya wiki ya Huduma kwa Wateja.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira akionesha cheti chake alichokabidhiwa na Benki ya NMB.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Anna Mghwira akikabidhi Vyeti kwa Wadu mbalimbali kwa niaba ya Benki ya NMB kwa kutambua mchango wao katika kufanikisha utendaji kazi wa Benki hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira akikata Keki kwa ajili ya kuadhimisha wiki ya Huduma kwa wateja katika Benki ya NMB tawi la Nelson Mandela mjini Moshi.
Meneja wa Benki ya NMB tawi la Nelson Mandela ,Emanuel Kishosha akimlisha keki mkuu wa Mko wa Kilimanjaro ,Ana Mghwira wakati wa maadhimisho hayo.
Meneja wa NMB tawi la Nelson Mandela ,Emanuel Kishosha akimlisha keki Mkuu wa wilaya ya Moshi ,Kippi Warioba katika maadhimisho hayo.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Anna Mghwira akiwa katika picha ya pamoja na Wateja wa Benki hiyo na viongozi mbalmbal waliohudhuria kuanza kwa wiki ya Huduma kwa Wateja.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini.

COCA-COLA YAJA NA PROMOSHENI YA ‘MCHONGO CHINI YA KIZIBO’

$
0
0

Msafara wa magari ya kampuni ya Nyanza Bottlers yakipita mitaani katika mji wa Mwanza wakati wa uzinduzi wa promosheni hiyo.
Mkuu wa Masoko na Mauzo wa kiwanda cha Nyanza Bottlers, Japhet Kisusi (katikati),akiongea na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa promosheni hiyo.Wengine pichani ni Maofisa Waandamizi wa kampuni hiyo
 Kikosi kazi cha timu ya mauzo ya Nyanza Bottlers katika picha ya pamoja wakati wa uzinduzi wa Mchongo chini ya kizibo.

Kampuni ya Coca-Cola, imezindua kampeni kubwa ya wiki 10 kwa wateja wake inayojulikana kama ‘Mchongo Chini ya Kizibo’ ambayo itawawezesha wateja wake wa mikoa ya kanda ya ziwa na jirani kujishindia zawadi nono za fedha taslimu zaidi ya milioni 400,bodabado 100,televisheni 60 aina ya SONY LED zenye inchi 32,T-shirts , kofia na soda za bure. 

 Akiongea wakati wa uzinduzi uliofanyika jijini Mwanza, Mkuu wa Masoko na Mauzo wa kiwanda cha Nyanza Bottlers, Japhet Kisusi, alisema lengo la promosheni hii ni kuleta msisimko zaidi kwa wateja wanywaji wa soda zote zinazozalishwa na kampuni ya Coca-Cola waliopo mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Kigoma, na mikoa mingine jirani ya kanda ya ziwa.

 “Kampuni yetu ya Coca-Cola katika kutoa shukrani kwa wateja wetu wanaotuunga mkono tumekuwa tukifanya promosheni mbalimbali zenye lengo la kuleta furaha na kubadilisha maisha yao kupitia Coca-Cola na promosheni ya ‘Mchongo Chini ya Kizibo’ tunayoizindua leo. Kwa kunywa soda aina yoyote inayozalishwa na kampuni ya Coca-Cola wataweza kujishindia zawadi mbalimbali zikiwemo fedha taslimu, bodabado, televisheni aina ya SONY LED zenye inchi 32, T-shirts , kofia na soda za bure.” Alisema Kisusi. Alisema ili mteja kujishindia zawadi atabandua.

Iambatanisho laini kilichopo chini ya kizibo cha soda. Kwa upande wa fedha taslimu kuna zawadi za shilingi 5,000/-, 10,000/- na 100,000 na zaidi ya shilingi milioni 400/- zimetengwa kwa ajili ya kushindaniwa na wateja, ambapo kwa upande wa zawadi ya bodaboda anachotakiwa kufanya mteja ni kukusanya vizibo vitatu vyenye picha zinazokamilisha picha ya bodaboda – kuonyesha upande wa Nyuma, Katikati na Mbele.

 Kisusi aliongeza kuwa pia zawadi nyinginezo za Televisheni, kofia, T-shirt na soda za bure zinapatikana chini ya kiambatanisho laini chini ya kizibo kama zilizvyo zawadi kubwa. “Natoa wito kwa wateja wetu kuchangamkia promosheni hii ili waendelee kuburudika na soda zinazotengenezwa na kampuni ya Coca-Cola sambamba na kunufaika kwa zawadi za kuleta furaha na kuboresha maisha yao, familia zao na wapendwa wao.”

 Kuhusu jinsi ya kupata zawadi alisema kuwa zawadi zote kwa washindi zitatolewa bila urasimu wa aina yoyote kuanzia kwenye maduka ya rejareja, mawakala maalumu wa kusambaza vinywaji vya kampuni ya Coca-Cola na kwenye kiwanda cha Nyanza Bottlers. Soda za kampuni ya Coca-Cola ambazo zitakuwa na zawadi kwenye ganda la vizibo ni Coca-Cola, Fanta, Sprite, Tangawizi, Sparleta na Novida.

RAIS MAGUFULI AMTEUA HAB MKWIZU KUWA MWENYEKITI WA BODI MPYA YA USHAURI YA TSN.

MKURUGENZI WA MASHTAKA AFUNGUA MAFUNZO YA UELIMISHAJI KUHUSU MFUKO WA FIDIA KWA WAFANYAKAZI

$
0
0
 Mkurugenzi wa Bw. Mashtaka Biswalo Mganga akifungua Mafunzo ya Uelimishaji kuhusu Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF)  kwa Mawakii wa Serikali wa Mikoa ya Dar es Saaam, Morogoro, Lindi na Mtwara yaliyofayika mkoani Marogoro jana (Leo).
 Mkurugenzi  Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) Bw. Masha Mshomba akimkaribisha mgeni rasmi ambaye ni Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Biswalo Mganga kwenye Mafunzo ya Uelimishaji kuhusu Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF)  kwa Mawakii wa Serikali wa Mikoa ya Dar es Saaam, Morogoro, Lindi na Mtwara yaliyofayika mkoani Marogoro jana (Leo).
 Mkurugenzi wa Mashtaka Biswalo Mganga (wa nne kutoka kushoto akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa Mafunzo ya Uelimishaji kuhusu Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF)  kwa Mawakii wa Serikali wa Mikoa ya Dar es Saaam, Morogoro, Lindi na Mtwara yaliyofayika mkoani Marogoro jana (Leo).
 Baadhi ya Washiriki wa Mafunzo wakimsikiliza Mkurugenzi wa Mashtaka katika Mafunzo ya Uelimishaji kuhusu Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF)  kwa Mawakii wa Serikali wa Mikoa ya Dar es Saaam, Morogoro, Lindi na Mtwara yaliyofayika mkoani Marogoro jana (Leo). (Picha zote na Mpiga picha wetu)

Na Sebera Fugence – Afisa Uhusiano Mwandamizi (WCF)Morogoro.
IMEELEZWA kuwa waajiri ambao hawajisajii na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi hatua kali zitachukuliwa dhidi yao.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Mashtaka Mhe. Biswalo Mganga katika mafunzo ya uelemishaji wa Mawakili wa Serikali wa Mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Morogoro, Lindi na Mtwara yaliyofanyika Mkoani Morogoro jana. (leo).

Mheshimiwa Mganga alisema   hatua za kisheria zitachukuliwa kwa waajiri watakaobainika kutenda makosa mengine yakiwemo ya kutowasilisha michango katika Mfuko kwa wakati.

Alisema lengo la Serikali ni kuona kila mfanyakazi anayeumia, kuugua ama kufariki kutokana na kazi anapata mafao yake kama ambavyo imeeekezwa katika Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi  Sura 263 ikisomwa pamoja na kanuni zake za mwaka 2016.

“Mafunzo haya yatatoa fursa kwa Ofisi yangu na Maafisa wengine kueleza uzoefu wao kuhusu  namna ya kuendesha Mashauri ya Jinai zikiwemo changamoto wanazokutana nazo na mapendekezo ya utatuzi wa changamoto hizo hasa pale wanaposhughulikia kesi dhidi ya waajiri wanaokiuka sheria.
Alisema Ofisi yake ni mdau muhimu sana katika kuhakikisha kuwa matakwa ya Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi yanatekelezwa kikamilifu na wale wanaoshindwa kutekeleza wajibu wao wanachukuliwa hatua stahiki za kisheria.

Nae Mkurugenzi  Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) nchini  Bw. Masha Mshomba alisema  Ofisi  ya Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali  ipo kwa mujibu wa Sheria ya Ibara ya 59B ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 na moja kati majukumu yake ya msingi ni kufungua, kusimamia  na kuendesha mashauri ya jinai katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 

Alisema Ofisi ya Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali ni mdau muhimu sana katika kuhakikisha malengo ya Mfuko huo yanafikiwa kwani ndio wasimamizi wakuu katika uendeshaji mashauri ya jinai yakiwemo makosa ya jinai yaliyoainishwa kwenye Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi. 

Aliitaja changomoto inayoikabii Mfuko huo kuwa ni  idadi kubwa ya waajiri ambao hawajajisajili na hawachangii kwenye Mfuko na kuongeza kuwa changamoto hiyo isipopatiwa suluhisho la haraka itaathiri uwezo wa  Mfuko kulipa fidia kwa wafanyakazi.

Alisema hadi kufikia juni 30, 2017 Mfuko umelipa fidia ya kiasi cha Shilingi 613,843,555.64 ikiwa ni gharama za matibabu fidia ya ulemavu wa muda mfupi na ulemavu wa kudumu.
Kwa upande wa usajili Bw. Mshomba amesema hadi kufikia juni 30, 2017 mfuko tayari ulikuwa umesajii waajiri 7,857 ambapo hadi kufikia juni 31, 2017 inakadiriwa kuwa  zaidi ya waajiri 13,918 waliopo Tanzania Bara hawajasajiiwa kwenye Mfuko.

Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi ni Taasisi ya Hifadhi ya Jamii iiyoanzishwa chini ya kifungu cha 5 cha Sheria ya Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi Sura 263 marejeo ya mwaka 2015 kwa lengo la kushughuikia masuala ya fidia kwa wafanyakazi wanaoumia ama kuugua ama kufariki wakati wakitekeeza majukumu ya mwajiri kwa mujibu wa mikataba ya ajira zao.

DC MTATURU AAGIZA WATAALAMU WA KILIMO KUWAUNGANISHA WAKULIMA NA MFUMO WA BENKI YA KILIMO

$
0
0
Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Mkoani Singida ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu Akizungumzia katika kikao Cha kazi na wataalamu wa Kilimo, Ufugaji na Mipango miji.
Wataalamu wa Kilimo, Mifugo na Mipango Miji katika Halmashauri ya Itigi na Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni wakimsikiliza kwa makini Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Mkoani Singida ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu wakati wa kikao Cha kazicha namna ya kuboresha kilimo, Ufugaji na Mipango Miji.Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Mkoani Singida ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu Akizungumzia katika kikao Cha kazi na wataalamu wa Kilimo, Ufugaji na Mipango miji.
Wataalamu wa Kilimo, Mifugo na Mipango Miji katika Halmashauri ya Itigi na Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni wakimsikiliza kwa makini Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Mkoani Singida ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu wakati wa kikao Cha kazicha namna ya kuboresha kilimo, Ufugaji na Mipango Miji.


Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Mkoani Singida ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu Akizungumzia katika kikao Cha kazi na wataalamu wa Kilimo, Ufugaji na Mipango miji.

Na Mathias Canal, Singida

Wataalamu wa Kilimo wametakiwa kuwaunganisha wakulima na Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) kwa ajili ya kusaidia upatikanaji wa Masoko ili kuongeza Mapinduzi yenye tija katika Sekta ya Kilimo.

Akizungumzia katika kikao Cha kazi na wataalamu wa Kilimo, Ufugaji na Mipango miji Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Mkoani Singida ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu alisema kuwa pamoja na wananchi kujituma katika uzalishaji wa mazao ya chakula na kilimo lakini changamoto Ni kubwa ya namna ya kuongeza ufanisi katika masoko.

Alisema kuwa endapo wakulima wataunganishwa na Benki ya Kilimo itakuwa Ni njia pekee ya kuchagiza na kusaidia kuwezesha Sekta ya Kilimo kutoka kilimo cha kujikimu kwenda kilimo cha kibiashara ili kukuza uchumi na kupunguza umasikini.

Alisema kuwa Katika kutekeleza majukumu ya wananchi Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania imeanza huduma zake kwa kulenga minyororo michache ya ongezeko la thamani katika kilimo ambapo mikopo ya aina mbalimbali hutolewa kuwezesha wakulima kuongeza tija na uzalishaji katika sekta ya kilimo nchini Tanzania. 

Katika kikao hicho Cha kuwakumbusha majukumu wataalamu hao Mhe Mtaturu amewataka kuandaa mpango kazi wa mazao ya Kilimo hususani mazao ya chakula na Biashara.

"Ili kuwe na kilimo kizuri na tija kwa wananchi, Wataalamu mnapaswa kuzingatia uwepo wa Pembejeo za kilimo na mbegu Bora za kisasa ambazo zinazalisha mazao mengi" 

"Tufanye hivi ili kuwa mfano Bora katika Mnyororo wa thamani ambao Ni sera ya Taifa ya viwanda kuchakata mazao ili kuondoa uuzaji wa malughafi na hivyo kuuza bidhaa" Alisema Mhe Mtaturu

Aliongeza kuwa kupitia Mnyororo wa thamani utapandisha thamani ya Mazao ya Wakulima ikiwa ni pamoja na kujiunga kwenye vyama vya Ushirika Jambo ambalo litaibua chachu ya wananchi kutilia mkazo zaidi katika kujiusisha na kilimo.

Mhe Mtaturu Alimuelekeza Katibu Tawala wa Wilaya ya Manyoni kuandaa kikao na maafisa ugani ili kukumbushana ufanisi na namna Bora ya kuendeleza Kilimo kwa wananchi kuanza kulima mazao ya kipaombele yaliyoelekezwa na Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa ambayo Ni zao la Pamba, Korosho, Chai, Kahawa na Tumbaku.

Alisema pomoja na mazao ya kipaombele pia wananchi wanapaswa kuendelea kuongeza nguvu katika mazao yanayostawi kwa wingi Wilayani humo ikiwa Ni pamoja na zao la Alizeti na zao la Dengu.

Katika upande mwingine Mhe Mtaturu alishauri wataalamu wa Mifugo kutilia msisitizo Ufugaji wa kisasa (Ziro Grazing) kwa kutembelea na kupata utaalamu wa Ufugaji na mbegu Bora za ya Ng'ombe wa kisasa kwa wataalamu katika Rachi ya Taifa ya Kongwa (NARCO) na LITI iliyopo Mpwapwa Mkoani Dodoma.

Naye Afisa Kilimo Umwagiliaji na Ushirika katika Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni Ndg Chimsala Fadhili na Afisa Kilimo Umwagiliaji na ushiriki wa Halmashauri ya Itigi Ndg Renatus Mtatina walimpongeza Mkuu huyo wa Wilaya kwa kutangaza kufanya uzinduzi wa msimu wa Kilimo Wilaya kwani utaongeza chachu na Hamasa kwa wananchi kulima kwa wingi na tija.

Walisema kuwa miongoni mwa mambo Msingi na yenye tija katika Jamii Ni pamoja na viongozi kuwa wabunifu katika utendaji Jambo ambalo llimeonekana kwa Mkuu huyo wa Wilaya.

Uzinduzi wa msimu wa Kilimo Wilayani Manyoni utafanyika hivi karibuni ambapo utaambatana na mashindano ya Kilimo katika kila Kijiji, Kata na Tarafa.

IGP SIRRO AWAKUMBUSHA ASKARI WAJIBU WAO WA KUTENDA HAKI WANAPOTEKELEZA MAJUKUMU YAO

$
0
0
 Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro, akisalimiana na maafisa wa Polisi alipowasili katika mkoa wa Mtwara, leo kwa ziara ya siku moja ya kikazi yenye lengo la kuzumgumza na askari pamoja na kuwakumbusha wajibu wao wa kutenda haki wakati wanapotekeleza majukumu ya kazi za Polisi.
 Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro (kushoto), akimsikiliza Kmamanda wa Polisi mkoa wa Mtwara, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Lucas Mkondya, leo kwa ziara ya kikazi ya siku moja yenye lengo la kuzumgumza na askari pamoja na kuwakumbusha wajibu wao wa kutenda haki wakati wanapotekeleza majukumu ya kazi za Polisi. Picha na Jeshi la Polisi.
 Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro, akizungumza na waandishi wa habari nje ya Makao Makuu ya Polisi mkoa wa Mtwara, akiwa kwenye ziara ya kikazi mkoani humo yenye lengo la kuzumgumza na askari pamoja na kuwakumbusha wajibu wao wa kutenda haki wakati wanapotekeleza majukumu ya kazi za Polisi.
 Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro, akipokea salamu ya heshima ya kijeshi alipowasili mkoa wa Mtwara kwa ziara ya kikazi ya siku moja yenye lengo la kuzumgumza na askari pamoja na kuwakumbusha wajibu wao wa kutenda haki wakati wanapotekeleza majukumu ya kazi za Polisi.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro, akizungumza na askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia mkoa wa Mtwara, mara baada ya kukagua gwaride maalum lililoandaliwa kwa ajili yake. IGP Sirro, yupo mkani humo kwa ziara ya kikazi ya siku moja yenye lengo la kuzumgumza na askari pamoja na kuwakumbusha wajibu wao wa kutenda haki wakati wanapotekeleza majukumu ya kazi za Polisi. Picha na Jeshi la Polisi.

BENKI YA AZANIA IMEAMUA KWENDA BEGA KWA BEGA KUWATEMBELEA WATEJA WAKE

$
0
0

Na Mwandhishi Wetu
Katika kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja, Benki ya Azania imeanza kuwatembelea wateja wake katika maeneo yao ya kazi ili kusikiliza kwa ukaribu changamoto wanazokutana nazo zinazohusu  huduma za kibenki, ikiwa ni pamoja na kuwashukuru kwa kuwa wateja wake.

Aidha, katika wiki hii ya huduma kwa wateja, Benki ya Azania imemtambulisha Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Azania Bank Limited, Ndugu Charles Jackson Itembe, ambaye pia ameongoza msafara wa kutembelea wateja katika maeneo yao ya kazi, ambapo mteja aliyetembelewa leo na Benki hiyo, Ndugu Augustine Nyato amekabidhiwa hati ya kuthaminiwa pamoja na biashara ya mteja huyo kuwa katika biashara watakazozipa kipaumbele.

Akizungumza na mteja huyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Azania Bank Limited, Charles Jackson Itembe amesema ikiwa Azania Benki inamjali mteja wameamua kuwatembelea wateja wadogo, wa kati na wakubwa ili kuwapa shukrani kwa kuendelea kuwa na wao katika biashara kwa kipindi kirefu na hata kwa kipindi kijacho ili kunafaika na benki hiyo.

Naye Mteja huyo ambaye ni Mkurugenzi wa  Israel Aaron & Company Augustine Nyato ameishukuru benki ya Azania kwa kutambua mchango mkubwa wa wateja wao mpaka wakaamua kumtembelea ili kusikiliza changamoto anazozipata katika benki hiyo pamoja na kuangalia namna ya kushirikiana vyema katika kutoa huduma iliyobora ili kufikia malengo aliyojiwekea.

Wiki ya huduma kwa wateja imeanza rasmi Jumatatu ya Oktoba 2, 2017 na itamalizika baada ya wiki moja. Ni wakati wa taasisi kuwa karibu zaidi na wateja wake. Ni wakati wa kwenda bega kwa bega katika kuleta maendeleo kwa taifa letu.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Azania Bank Limited, Charles Jackson Itembe akizungumza na mteja wa benki ya Azania ambaye ni mfanyabiashara na mkurugenzi wa  Israel Aaron & Company  Augustine Nyato kuhusu benki hiyo ilivyoamua kuwatembelea wateja wake katika kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja.
Mkurugenzi wa  Israel Aaron & Company Augustine Nyato(katikati) akizungumza kuhusu faida anazozipata pamoja na kuishukuru benki ya Azania kwa kuona umuhimu wa kuwatembelea wateja wao kuwa wanawajali kuliko kubaki maofisini wakisubilia wateja. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Azania Bank Limited, Charles Jackson Itembe.
 Meneja Masoko wa Azania Bank, Diana Balyagati (kulia) akizungumza na mteja wa Benki hiyo kuhusu bidhaa walizonazo kwenye benki hiyo na namna wanavyoweza kushirikiana kwa kufanya kazi kwa pamoja ili kuleta maendelea kwa taifa.Kulia ni mteja wa Banki ya Azania, Bwana Augustine Nyato(kushoto).
  Mkurugenzi Mtendaji wa Azania Bank Limited, Charles Jackson Itembe(kushoto) akimkabidhi  hati ya kuthaminiwa mteja wa Benki ya Azania, Bwana Augustine Nyato leo ofisini kwake katika mtaa wa Survey jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Meneja Tawi wa Benki ya Azania  Tawi la Masdo, Benson Msuya.
Mteja wa Banki ya Azania bwana Augustine Nyato( wa pili kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Azania Bank Limited, Charles Jackson Itembe(kushoto), Meneja wa Tawi wa Benki ya Azania  Tawi la Masdo, Benson Msuya(wa pili kutoa kulia) na Meneja Masoko wa Azania Bank, Diana Balyagati (kulia).

WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA 2017: PSPF YATEMBELEA WATEJA MAJUMBANI, NIA NI KUWAJULIA HALI NA KUWAHAKIKI

$
0
0

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bw. Andrew Mkangaa, (kushoto), na Mteja wa PSPF, ambaye ni Mstaafu, Bw. Kassim Salehe Mafanya, (63), wakifurahia jambo wakati kiongozi huyo wa alipomtembelea Mstaafu Mafanya nyumbani kwake Kitunda B, nje kidogo ya jiji Oktoba 4, 2017 wakati Dunia ikiadhimisha Wiki ya Huduma Kwa Wateja.
Bw. Mafanya, (kulia), akipokea fomu hiyo
NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID
Wakati Wiki ya Huduma kwa Wateja ikiendelea kote Duniani, Mfuko wa Pensheni wa PSPF, umeitumia wiki hiyo sio tu kwa kuhudumia wateja ofisini bali pia kutoka nje ya ofisi na kuwatembelea Wanachama na Wastaafu wa Mfuko huo  majumbani kwao.
Mmoja wa waiotembelewa ni Mstaafu Bw. Kassim Salehe Mafanya,(63), anayeishi Kipunguni B, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam kitendo ambacho kilimfurahisha sana.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu, wa PSPF, Bw. Andrew Mkangaa akifuatana na timu yake, Oktoba 4, 2017 alifika nyumbani kwa Bw. Mafanya, na kufanya mazungumzo naye ikiwa ni pamoja na kumpatia fomu ili aijaze kwa nia ya kumuhakiki kama ambavyo sheria inataka.
Kwa mujibu wa Sheria, Mstaafu anatakia kufika kwenye ofisi za PSPF kuhakikiwa kila mwaka ili kujua uwepo wake, anasema Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bw. Andrew Mkangaa
“Kama mnavyofahamu wiki hii ni wiki ya huduma kwa wateja Duniani kote, na sisi PSPF kupitia ofisi zetu nchi nzima tunajitoa na kutembelea wateja wetu ambao ni pamoja na wanachama na wastaafu, na leo tuko hapa eneo la Kipunguni B, tumekuja kumtembelea Bw. Kassim Salehe Mafanya, ambaye ni mstaafu na lengo ni kumjulia hali na kumuhakiki uwepo wake kama ambavyo sheria inataka.” Alisema.
Afisa Uendeshaji wa PSPF ambaye pia alifuatana na Bw. Mkangaa, alimsomea Mstaafu huyo, maelezo yaliyomo kwenye fomu ya uhakiki kabla hajaweka saini kenyefomu hiyo.
Aidha kwa upande wake, Mstaafu huyo Bw. Mafanya aliishukuru PSPF kwa kitendo hicho cha kuwatembelea wateja wao yeye akiemo na kwamba ni kitendo kinachofaa kupongezwa.
“Siku ya leo nimefarijika sana, kwanza sikutegemea kama nigepokea ugeni kama huu kutoka PSPF wa kunitembelea mimi Mstaafu hapa nyumbani kwangu,” Alianza kwa kusema Bw. Mafanya wakati akiwakaribishas viongozi hao wa PSPF.
“Kitendo cha kuwakumbuka wastaafu kama sisi na kuwatembelea majumbani kwao kimenifurahisha sana na niwapongeze kwa tabia hiyo, Alisema.
Bw. Mafanya alimuhakikishia Kaimu Mkurugenzi Mkuu, kuwa amekuwa akipokea pensheni yake kila mwezi na bila matatizo yoyote na amekuwa akipata ushirikiano mzuri kutoka kwa maafisa wa PSPF kila anapokwenda kufuatilia pensheni yake.
“Nashukuru pensheni yangu inaendelea vizuri, huu ni mwaka wa 14 tangu nistaafu, nachukua vizuri tu pensheni ya kila mwezi na uzuri nikwamba inaboreshwa, na ndio maana mpaka hivi sasa tunaonekana tuna afya nzuri na ninaendelea na shughuli zangu mimi na familia yangu.” Alipongeza.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bw. Andrew Mkangaa, (kushoto), na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSPF, Bw. Abdul Njaidi, wakishuhudia Bw. Mafanya akijaza fomu ya uhakiki ya Mstaafu, kutoka PSPF hapo nyumbani kwake.
Bw. Mkangaa, (Kushoto), akipeana mikono na Bw. Mafanya baada ya kumtembela nyumbani kwake.
Bw. Mkangaa akisalimiana na familia ya Bw. Mafanya
Bw. Mkangaa akiwa amembeba mjukuuu wa Bw. Mafanya.
Bw. Mafanya (kushoto), akifurahia jambo na Afisa Uendeshaji kutoka PSPF, Bw.Ernest Massay
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, na timu yake akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanafamilia wa Bw. Mafanya mbele ya nyumba yake.

MBUNGE CHUMI AZIPIGA TAFU TIMU ZA JIMBONI KWAKE KWA KUZIPA VIFAA VYA MICHEZO NA FEDHA

$
0
0
Mbunge wa jimbo la Mafinga mjini Cosato Chumi akitoa maelezo wakati wa kugawa vifaa vya michezo kwa timu za mafinga mjini pamoja na kuisaidia timu ta Mufindi United kiasi cha shilingi laki Tano.
Mbunge wa jimbo la Mafinga mjini Cosato Chumi akipeana mkono na viongozi wa timu ya Mafinga veterani wakati wa kugawa vifaa vya michezo kwa timu za mafinga mjini pamoja na kuisaidia timu ta Mufindi United kiasi cha shilingi laki Tano
 Na Fredy Mgunda, Mafinga

Mbunge wa jimbo la Mafinga mjini Cosato Chumi amezipiga tafu timu zinazoshiriki ligi daraja la tatu ngazi ya mkoa wa Iringa kwa kuzipatia jozi moja moja ya jezi kwa kila timu lakini pia ameichangia timu ya Mufindi United inayoshiriki lingi daraja la kwanza Tanzania bara kiasi cha shilingi laki tano kwa lengo la kuisaidia katika harakati zake za kupanda daraja.
 
Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa na pesa hizo Chumi alisema kuwa ameguswa kufanya hivyo kwa kuwa anapenda michezo na anacheza mpira wa miguu kufanya hivyo kutaendelea kuzipa morali timu za jimbo la Mafinga Mji kufanya vizuri kwenye mashindano wanayoshiriki.
  

"Leo nimekabidhi jezi kwa timu zinazoshiriki daraja la tatu ngazi ya mkoa na timu hizo ni Bajaji Fc,Mabo Fc (Boda Boda) na Kinyanambo United nimefanya hivyo kuzifanya timu hizi kuzihamasisha kufanya vizuri kwenye ligi hiyo" alisema Chumi


Chumi aliwataka wananchi na wadau wanaoipenda timu ya Mufindi United kuendelea kuisaidia katika haraka za kupanda daraja kwa kuwa kuendesha timu ni gharama kubwa hivyo tuungane kwa pamoja kufanikisha lengo letu ili kupata timu itayokuwa ligi kuu Tanzania Bara msimu ujao.


“Jamani kushiriki ligi daraja la kwanza ni gharama sana na ligi ya mwaka huu ni ngumu hivyo tunahitaji kuwa na pesa nyingi kufanikisha lengo letu la kuwa na timu ya ligi kuu wenzetu wengine wamejipanga sana na wanapesa hivyo timu yetu ikiwa na njaa itatuwia vigumu kuipandisha” alisema Chumi


Aidha Chumi hakusita kuwapongeza viongozi wa timu ya Mufindi United pamoja na mkuu wa wilaya ya Mufindi Jamhuri William kwa kuendelea kuisadia timu kushiriki lingi hivyo kwa michango na mawazo yao.


“Mimi nilijua mwaka huu tunashushwa daraja maana hali ilikuwa ngumu wakati wa usajili lakini viongozi hawa walipigana kufa na kupona wakahakikisha timu inasajili na inacheza ligi hiyo” alisema Chumi



MKUU WA MKOA WA RUKWA, ZELOTE STEVEN APIGA MARUFUKU MALORI KUBEBA ABIRIA MKOANI HUMO

$
0
0

NA RUKWA YETU BLOG
UONGOZI wa Mkoa wa Rukwa chini ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kmaishna Mstaafu Zelote Stephen umeungana na ndugu wa majeruhi 9 na wafiwa wa vifo vya watu 15 vilivyotokea katika ajali ya lori aina ya fuso eneo la Ntembwa, Wilayani Nkasi.
Katika kuhakikihsa tukio hilo halijirudii Mh. Zelote amepiga marufuku ukiukwaji wa sheria ya kupandisha abiria katika magari ya mizigo na kuonya kuwa yeyote atajayefanya hivyo achukuliwe hatua haraka iwezekanavyo.
“Nimekataza binadamu kugeuzwa kuwa ni mifuko ya misumari, ni bora tubakie na wananchi wetu salama, watu wasipande kwenye malori, nimefikiria ni vyema tutumie zile chai maharage kuliko kupanda kwenye malori,” Alisisitiza.
Mh. Zelote alifika katika eneo la tukio mara tu baada ya kupokea habari hiyo ili kuweza kusaidia na kuhakikisha maiti na majeruhi hao wanapatiwa huduma stahiki na kufanikisha zoezi la uokoaji.
Ajali hiyo ilitokea baada ya lori aina ya fuso yenye namba za usajili T 425 BFF kuacha njia na kupinduka ilitokana na mwendo kasi wa dereva uliochangiwa na ugeni wa barabara hiyo.
Lori hiyo mali ya Bakari Ali Kessy iliyokuwa imetokea Kijiji cha Mvimwa kuelekea Kijiji cha Wampembe ilikuwa imepakiwa shehena ya viroba vya mahindi na watu iliacha njia, kupinduka na kusababisha vifo vya watu 15 kati yao wanawake 10 na wanaume 05.
Waliofariki katika ajali hiyo ni

1.     Domona Tenganamba, 41yrs, mfipa mkulima.
2.     Emmanuel Rashid 84yrs, mfipa mkulima, mkazi wa ntemba
3.     Restuta Sunga , 35yrs, mfipa mkazi wa ntemba
4.     Salula Revana 64yrs, mfipa mkazi wa mtapenda isale
5.     Ferisia Tenganamba , miaka 1 – 6/12
6.     Prisca Madeni, 45yrs, mfipa, mkulima, mkazi wa china
7.     Richard Chikwangara, 24yrs, mfipa, mwalimu mkazi wa kalambanzite
8.     Yusta Somambuto, 36yrs, mfipa, mkulima mkazi wa kizumbi
9.     Gilesi Ramadhan, 24yrs, mfipa, mkulima mkazi wa sumbawanga
10. Odetha Madirisha 46yrs, mfipa mkulima wa kizumbi
11. Megi Nalunguli, 52yrs, mfipa, mkulima mkazi wa wampembe
12. Abuu Amani @ mandevu, 37yrs, muha, biashara, mkazi wa liapinda
13. Nyandindi Batrahamu, 35yrs, mfipa, mkulima, mkazi wa sumbawanga
14. Magdalena Mbalamwezi, 50yrs, mfipa, mkulima mkazi wa ntuchi
15. Mtoto mchanga wa wiki mbili, mwanaume ambaye hajapewa jina
Majeruhi wa ajali hiyo ni:-
1.     Dismas Clement, 26yrs, mfipa, mkulima mkazi wa mwinza
2.     Sema Savery 25yrs, mfipa, mkulima mkazi wa wampembe
3.     Ally Haruna, 33yrs, mfipa, mkazi wa namanyere
4.     Yusta Mfundimwa, 50yrs, mkulima mkazi wa izinga
5.     Tenesfory Oscar, 36yrs, mfipa mkazi wa wampembe
6.     Amos Kitambale, 25yrs, mfipa, mkazi wa wampembe
7.     Neema Mwanandenje, 21yrs, mfipa, mkazi wa mlambo
8.     Joseph Sungula, 28yrs, mfipa, mkulima.
9.     Majeruhi mmoja mwanamke ambaye hajafahamika kwa jina yuko icu
Baada ya kusababisha ajali hiyo dereva alitoroka lakini juduhudi za kumtafuta mtuhumiwa zinaendelea kufanyika.


 Abate wa Pambu Martin Mkolwe Abasia ya Mvimwa akiongoza ibada fupi ya kuwaombea marehemu wa ajali iliyoua watu 15 na kujeruhi 9 iliyofanyika katika kituo cha afya Mvimwa, Wilayani Nkasi.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen (kaunda Suti ya ugoro) akitoa salamu zake za pole kwa wafiwa, kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Mh. Said Mtanda na kulia kwake ni Abate Pambu Mkolwe wa Abasia ya Mvimwa.​

MSHINDI WA TISA WA MILIONI 60 ZA TATU MZUKA APATIKANA TUNDURU

$
0
0
 Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Mh Juma Homera (Kushoto) akiwa na MWakilishi wa Tatu Mzuka  Bi Kemi Mutahaba, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Kiuma Bw. Joseph Mtuma  Wakimpongeza Mshindi wa 9 wa Tatu Mzuka Jackpot Bw Fulko Hyera, kijijini Kiuma, Tunduru
  Mshindi wa 9 wa Tatu mzuka Jackpot Bw Fulko Hyera, Mwalimu wa shule ya sekondari Kiuma,akifurahia alipo kabithiwa cheki  ya Milioni 60 kutoka Tatu Mzuka kijijini kwake Kiuma, Wilaya ya Tunduru.
 Bw. Fulko Hyera  and Mke wake Sigsberta Haule mbele ya duka lao kijijini Kiuma wakisherekea kipato cha Million 60 kutoka Tatu Mzuka.
Tatu Mzuka walizawadia marafiki wa TATU wa Bw. Fulko Hyera  million 1 moja kutokana na promociona ya Tatu Mzuka ya "Cheza na Washkaji na Shinda na Washkaji".  Robert Mbai na Owne Simwanga

Mshindi wa droo ya tisa ya Tatu Mzuka amepatikana Jumapili hii ya Oktoba 1, 2017. Mshindi huyu amejinyakulia kitita cha shilingi milioni 60 na ni Bwana Fulko Hyera, mkazi wa kiuma, wilayani Tunduru 

Ushindi huu wa Bw.Hyera unaonesha namna Tatu Mzuka inavyobadili maisha ya wananchi wa Tanzania sio tu wa mjini bali na vijijini pia. Bw. Hyera ambaye ni mwalimu wa shule ya sekondari ya Kiuma.

Bw Hyera alisema “Katika muda wangu wote, sikuwaza kuwa na hela hizi. Kama familia zetu nina majukumu mengi yakutimiza na sasa nitakuwa na uwezo wa kusaidia familia. Sasa nimeamua kuanza biashara, niajiri wengine na kuongeza fursa za vijana” 

Kumkabidhi cheki Bw Hyera, Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Mheshimiwa Juma Homera alimkabidhi cheki mshindi kwenye tulio lilio andaliwa na Tatu Zuka kijijini Kiuma, Tunduru.

Mheshimiwa Homera alikuwa ana machache ya kusema licha la kumpongeza Bw. Hyera alimuhusia “ Hizi ni hela nyingi sana. Lazima uwe na malengo kamili and pia hii itakupa fursa nyingine ya kusaidia jamii.” Amewapongeza sana Tatu Mzuka kwa kuchangia kubadili maisha ya watu tena ya mwana Tunduru.

Licha ya ushindi huo, Bw. Hyera alipata pia fursa ya kutaja majina matatu ya rafiki zake ambao pia walijishindia kiasi cha shilingi milioni 1 kwa kila mmoja. Mmoja ya rafiki zake Bi.Marianna Haule ambaye mara nyinji anamuuguza mama yake, ndio alichaguliwa. “Nilimuwaza Marianna ili nijaribu kumpa haueni akiwa anamuuguza mama yake.” Alieleza Bw. Hyera

Tatu Mzuka hadi leo imetoa zaidi ya Billion 2 kwa washindi na wamepata zaidi ya washindi 900,000.  

Wiki hii Jumapili kutakuwa na Million 80M.Namna ya kucheza promosheni ya Tatu Mzuka Unatakiwa kwenda kwenye sehemu ya fedha kwenye simu yako na kuchagua Lipana kwa M-Pesa au mitandao mingine. Kisha unaingiza namba zako 3 za bahati katika sehemu inayoonekana. Kisha weka kiwango chako cha fedha kuanzia shilingi 500/- hadi 30,000/-

Kwa kuanzia kiasi cha shilingi 500,TatuMzuka inatoa fursa ya kushinda hadi  shilingi milioni 6 ndani ya saa 24 kwa siku. Chagua namba tatu za bahati kuanzia 0-9 kisha zitume zikiambatana na pesa ya ushiriki kuanzia shilingi 500/. Ukishinda namba zako zote tatu utajinyakulia fedha mara 200 ya ile uliyocheza huku pia kila shilingi 500 unayocheza inakupa nafasi ya kushiriki droo inayochezwa kila wiki ambayo inakupa fursa ya kushinda hadi shilingi milioni 70.

Ili kupata taarifa zaidi kuhusu washindi wa Tatu Mzuka angalia Televisheni za Clouds na TV1 kila Jumapili kuanzia saa Tatu na Nusu Usiku.

DCB YAHAMASISHA WATEJA KUTUMIA HUDUMA DCB PESA POPOTE.

$
0
0
Moja ya wateja wa mda mrefu wa benki ya DCB Mama Fatma Simba akielezea namna benki hiyo ilivyweza kumsaidia katika shughuli zake za ujasiriamali mpaka alipofikia sasa na kuwataka wanawake waache tamaa pindi wanapochukua mikopo na kusifia pia huduma za DCB Pesa katika urahisishaji wa huduma za kipeki kupitia simu ya mkononi.

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
BENKI ya DCB imesherehea wiki ya huduma kwa wateja kwa kufurahi pamoja na wateja wa benki hiyo huku wakiendelea kuwahamisha kutumia huduma ya DCB Pesa popote nchini.

Katika maadhimisho ya wiki kwa huduma kwa wateja, Afisa Mikopo wa DCB tawi la Magomeni Miriam Migetto amesema kuwa wanayofuraha ya kujumuika pamoja na wateja wa benki hiyo kusherehekea siku hii muhimu kwao pia na kuwasisitiza kuendelea kutumia huduma za kibenki.

Miriam amesema kuwa kwa sasa wanaendelea kuboresha huduma za kibenki ikiwemo kutumia huduma ya DCB Pesa na DCB Jirani ikiwa ni katika kurahisisha huduma za kipesa kwa wateja wa DCB.

Afisa Mikopo wa DCB tawi la Magomeni Miriam Migetto akizungumza na wateja wa benki hiyo wakati wa maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja ma kuwataka kuendelea kutumia huduma za kibenki kwa njia ya simu pamoja na kuendelea kuchukua mikopo ya riba nafuu.


Wafanyakazi wa tawi la benki ya DCB Magomeni wakiwa katika picha ya pamoja na wateja wa benki hiyo waliohudhuria kusherehekea maadhimisho ya wiki huduma kwa wateja Jijini Dar es Salaam leo.

Moja ya wateja wa muda mrefu wa benki hiyo, Mama Fatma  Simba amesema kuwa ameanza kutumia benki hiyo tangu mwaka 2005 na amekuwa akipata huduma za kifedha kwa urahisi zaidi bila usumbufu na hata pia ameweza kupata mkopo wa bei nafuu na riba nafuu.

"Nimekuwa natumia DCB benki kwa zaidi ya miaka 12 na imeweza kunipatia mahitaji yangu kwa wakati ikiwemo mkopo wa bei nafuu na riba nafuu na hata katika utoaji wa huduma za kibenki kupitia DCB Pesa wameweza kutupunguzia wateja wao kwenda benki mara kwa mara, " amesema mama Fatma.

DCB benki wamesherehea wiki ya huduma kwa wateja katika matawi tofauti na kufurahi pamoja na wateja wao na kuahidi kuzidi kuboresha na  kuwapatia huduma wanazostahili na wakati sahihi.

Baadhi wa wafanyakazi wa Benki ya DCB Tawi la Mabibo External wakiwa katika picha ya pamoja  katika kuazimisha wiki ya huduma kwa wateja.
Viewing all 40051 articles
Browse latest View live
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>