Quantcast
Channel: MTAA KWA MTAA BLOG
Viewing all 39044 articles
Browse latest View live

WAFANYAKAZI TAA KUNYANG'ANYWA VIWANJA WALIVYOJIGAWIA

$
0
0

 Naibu Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi, Mhandisi Atashasta Nditiye akiteta jambo na  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA),Richard Mayongela. 

Na Avila Kakingo,Globu ya Jamii
NAIBU Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi, Mhandisi Atashasta Nditiye, ameagiza wafanyakazi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) ambao walijigawia viwanja katika viwanja vya fidia za wananchi wanyang'anywe na kufikishwa mahakamani ili sheria ifuate mkondo wake.

Ameyasema hayo wakati alipofanya kikao na wawakilishi wa mkuu wa mkoa pamoja na wawakilishi wa kampuni ya Tanzania Remic centre jijini Dar es Salaam leo Agosti 30,2018.ambapo alieleza wasiwasi wake kuwa kampuni iliyopewa kandarasi ya kuwatafutia viwanja wananchi hao haijatekeleza wajibu wake ipasavyo licha ya kuwa tayari imelipwa kiasi cha shilingi bilioni 3.7.

Nditiye pia ameagiza Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), kwa kushirikiana na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, wakakague viwanja 537 vilivyotengwa maeneo ya Msongola, kwa ajili ya waliokuwa wakazi wa eneo la Kipawa jijini Dar es Salaam Jumanne wiki ijayo ili kujiridhisha kama viwanja hivyo vipo na  vinafaa. 

“Nakuagiza Mkurugenzi wa TAA, kwa kushirikiana na Mkurugenzi wa Wilaya Jumanne ijayo muende mkakague eno hilo la viwanja 537 muone kama vipo kwa sababu kumekuwa na shida sana na hawa wenzetu wa Tanzania Remix Centre  nyinyi wenyewe mnajua, kuna shida ya miundombinu, sasa lazime mjue eneo hilo linafikika, na viwanja hivyo vinajengeka.” Amesema.

Amesema Wananchi wako tayari kushirikiana na serikali katika kuhakikisha upanuzi wa uwanja unakwenda vizuri. Kampuni ya Tanzania Remix Centre ilipendekezwa na Manispaa ya  Ilala na kupewa kandarasi ya kutafuta viwanja kwa ajili ya makazi mapya ya wananchi waliokuwa wakiishi eneo la Kipawa jijini Dar es Salaam.

Hata hivyo kulikuwepo na mivutano kati ya Mamlaka na Wananchi ambapo baadhi yao walipeleka shauri hilo mahakamani na hivyo kufanya zoezi hilo la kuwahamisha wananchi hao kwenye eneo hilo jipya kusuasua.

“Mradi huu ulihusisha upatikanaji wa viwanja 1,600 kwa mujibu wa mkataba wa awali ambapo fidia yake ilipaswa kufanywa kwa awamu mbili ya watu 800, hata hivyo kwa mujibu wa sheria kipinde kile ilitaka mwananchi apewe eneo lakini alipwe fidia pia.” Amefafanua.
Naibu Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi, Mhandisi Atashasta Nditiye akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa kikao kati ya wawakilishi wa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam na Kampuni ya Tanzania Remix Centre katika ukumbi wa VIP terminal II uliopo Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere.
 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA),Richard Mayongela akizungmza wakati wa kikao na  Naibu Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi, Mhandisi Atashasta Nditiye kulia leo jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi wa kampuni ya Tanzania Remix centre akizungumza wakati wa kikao kilichofanyika leo katika ukumbi wa VIP terminal II uliopo katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere kulia ni  Naibu Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi, Mhandisi Atashasta Nditiye.

RAIS MAGUFULI MGENI RASMI KWENYE UZINDUZI WA TAMASHA LA URITHI FESTIVAL JIJINI DODOMA

$
0
0
NA. LUSUNGU HELELA-DODOMA
RAIS wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Mhe. John Pombe Magufuli, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye Tamasha la Mwezi wa Urithi linalotambulika kama Urithi Festival, Celebrating Our Heritage litakalozinduliwa rasmi  kitaifa katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma Septemba 15, 2018.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dodoma,  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga amesema lengo la Tamasha  hilo  ni kuenzi, kudumisha, kuburudisha na kujifunza masuala muhimu yanayohusu Urithi wa Mtanzania hususani tamaduni zetu, historia, malikale na maliasili.

Aidha, Amesema kwa kutambua hazina kubwa ya malikale na utamaduni wa makabila zaidi ya 128 yaliyopo nchini, tamasha hilo litaongeza wigo wa mazao ya utalii kwa kukuza utalii wa utamaduni wa malikale hatua ambayo itaongeza ushindani wa Tanzania kama kituo bora cha utalii kwenye masoko mbalimbali duniani.

Ameongeza kuwa Urithi  Festival itasadia kukuza utalii wa ndani kwa kuongeza muda wa watalii wa kimataifa kukaa nchini kwa vile Tamasha hilo lifanyika katika kipindi ambacho watalii wengi wanatembelea Tanzania.

Naibu Waziri huyo amesema kutokana na watalii kuongeza muda wa kukaa nchini kutaleta faida kwa wananchi na uchumi wa nchi kwa ujumla

Aidha, Naibu Waziri huyo ametaja mikoa  sita pamoja na  tarehe zake  ambayo Tamasha hilo  linafanyika kitaifa wa upande wa  jiji la Dodoma tamasha hilo litafanyika Septemba 15 hadi tarehe 22 na kwa Zanziba litafanyika Septemba 23 hadi 29.

Pia, kwa upande wa  Dar es Salaa na Mwanza tamasha hilo litafanyika Septemba 29 hadi Oktoba 6.
Aidha, kwa upande  wa Wilayani Karatu tamasha hilo litafanyika Oktoba 8 hadi  12, huku Jijini Arusha tamasha hilo linatarajiwa  kutafanyika Oktoba 8 hadi 13 mwaka huu. 

Amesema tamasha hilo kutakuwa na shughuli mbalimbali kama vile sherehe za uzinduzi na kilele, kuenzi lugha adhimu ya Kiswahili na kutoa tuzo kwa wasanii na wadau wa Urithi.

Ameongeza kuwa Tamasha hilo litapambwa na shamrashamra za carnival ya mirindimo ya urithi, burudani za ngoma za asilil, muziki na kwaya pamoja n asana na maonesho ya bidhaa ya wadau.

Katika hatua nyingine, Naibu Waziri huyo amesema kuwa Tamasha hilo litahusisha makongamano ya wataalamu, usiku wa urithi, ziara ya kutembelea vivutio vya utalii pamoja na kunadi urithi katika mitandao ya kijamii na vyombo vya habari kupitia themes za Mvalishe, Misosi ya Kwetu na Michongo ya Urithi.

Tamasha la Urithi Festival litakuwa linafanyika kila mwezi Septemba ya kila mwaka kuanzia mwaka huu.  
Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya   Urithi Festival walioshiriki kwenye mkutano wa Waandishi wa Habari uliofanyika leo jijini Dodoma. Tamasha hilo linalotarajiwa kuzinduliwa Septemba 15, 2018 na  kuenzi, kudumisha, kuburudisha na kujifunza masuala muhimu yanayohusu Urithi wa Mtanzania hususani tamaduni zetu, historia, malikale na maliasili.

 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga akizungumza na Waandishi wa Habari leo jijini Dodoma kuwa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli, anatarajia kuwa mgeni rasmi kwenye Tamasha la Mwezi wa Urithi linalotambulika kama ‘’Urithi Festival, Celebrating Our Heritage’’ litakalozinduliwa rasmi  kitaifa katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma Septemba 15, 2018.

Baadhi ya Wajumbe wakiangalia  nembo ya Urithi Festival inakayotumika kwenye Tamasha hilo.

  (Picha zote  na Lusungu Helela-WMU)

WAZAZI NA WALEZA SERENGETI WATAKIWA KUWA NA MGAWANYO SAWA WA MAJUKUMU YA KAZI KWA WATOTO WAO.

$
0
0
 Picha 1 ni Wanafunzi wa shule ya msingi Nyiberekera pamoja na shule ya msingi Nyamisingisi wakiwa katika maandamano kwa lengo la kufikisha ujumbe kupitia mabango mabalimbali waliyobeba kabla ya kuanza kwa Tamasha hilo.
 Wanafunzi wa shule ya msingi Nyamisingisi wakiimba wimbo ulibeaba ujumbe wa kupiga vita ukatili kwa watoto.
 Leah Kimaro ambaye ni mwezeshaji kutika shirika la RIGHT TO PLAY akitoa elimu juu ya madhara ya ukatili wa kijinsia katika Tamasha hilo.
  Wanafunzi wa shule ya msingi Nyamisingisi wakiimba Shairi lenye ujumbe wa kupiga vita Ukatili.
 Wanafunzi wakionyesha Mchezo unaohusu stadi za maisha katika Tamasha hilo.
 Afisa Elimu kata ya Isenye Neema Fanuel akitoa msisitizo kwa wazazi na walezi kuendelea kutoa magawanyo sawa wa kazi katika familia.



Na Frankius Cleophace Serengeti.
WAZAZI na walezi Wilayani Serengeti mkoani mara wametakiwa kuachana na suala la ubaguzi katika mgawanyo wa majukumu ya kazi majumbani ili kuleta usawa wa kijinsia huku mtoto wa kike akilimbikiziwa kazi nyingi kuliko mtoto wa kiume majumbani. 

Hayo yamebainishwa na wanafunzi katika tamasha la kutoa elimu juu ya masuala ya kupinga Mila na desturi zilizopitwa nawakati ukiwemo Ukeketaji, Ndoa za Utotoni pamoja na mimba za utoto tamasha lililoandaliwa na Shirika la RIGTH TO PLAY nakushirikisha shule za Msingi Nyamisingisi,Nyiberekera kata ya Isenye Wilayani Serengeti Mkoani Mara.

Elizabert Kirinda ni mwanafunzi wa shule ya msingi Nyamisingisi amesema kuwa majumbani watoto wa kike wamekuwa wakipewa kazi nyingi za kufanya kuliko watoto wa kiume jambo amabalo linachangia kukosa muda mwingi wa kijisomea wao kama mabinti hivyo wameomba wazazi na walezi kutoa mgawanyo sawa wa kazi ili kuondoa ubaguzi wa jinsia.

“Sisi wasichana majumbani tunapewa kazi nyingi kupika, kuchota maji kulea watoto na wavula hawafanyi kazi zozote na wakati mwingine tunachunga mifugo hatuna muda wa kusoma tukiwa nyumbani tunaomba wazazi waweze kugawanya sawa majukumu ya kazi majumbani” alisema Elizabert.

Leah Kimaro ambaye ni mwezeshaji kutoka shirika la RIGHT TO PLAY Wilayani Serengeti Mkoani Mara amezidi kuhimiza suala la jamii kutoa taarifa kwa wakati pale wanapoona watoto wanafanyiwa ukatili wa kijinsia na siyo kusubiri tukio kubwa kutokea.

Kimaro amesema kuwa shirikla hilo limekuwa likitoa elimu ya kupinga Mila a desturi ambazo zimepitwa na wakati kupitia michezo mbalimbali yakiwemo maigizo, ngonjera, nyimbo, shairi, maigizo pamoja na vichekesho lengo ni kufikisha ujumbe uliobeba masuala ya kupinga Mila na desturi zilizopitwa na waka tikatik jamii.

“Michezo hii tunafanya kwa kushirikisha wanafunzi pia watoto ambao wako nje ya shule pia kuna makocha ambao wanasaidia kuandaa watoto hawa ikiwemo suala la kutoa elimu ya kupiga vita ukatili wa kijnsia kwa watoto” alisema Kimaro.

Neena Fanuel ni Afisa elimu kata ya Isenye na Afisa Mtendaji wa kata ya hiyo Vicenti Kamuga wanazidi kusisitiza wazazi na walezi kuzingatia usawa katika mgawanyo wa kazi majumbani huku wakitaja baadhai ya ukatili ambao unafanyika katika jamii kuwa bado suala la ukeketaji linazidi kukumbatiwa na jamii licha ya jitiada za mashirika likiwemo shiria la RIGHT TO PLAY kuendekea kutoa elimu japo jamii inazidi kubadilikwa na kutoa taarifa pale wanapoona ukatili ukitendeka.

Shirika la RIGHT TO PLAY wamekuwa wakizunguka katika shule za misingi kwa kushirikisha watoto wa shule za msingi na sekondari pamoja ja jamii kwa ujumla na kutoa elimu ya kupiga vita ukatili kupitia michezo mablimba ili kubadili mitazamo hasi ya jamii katika wilaya ya Serengeti na kata kwenye baadhi ya kata.

TFDA YAWATAKA WALISHAJI HAPA NCHINI (CATERING) KUJISAJILI

$
0
0
Na Agness Francis,blogu ya Jamii.
MAMLAKA ya chakula na dawa (TFDA) imesema utoaji wa huduma katika Mikusanyiko lazima uzingatie sheria pamoja kanuni ili kwepusha mad hara kwa walaji wa chakula katika mikusanyiko.

Mkutano huo ulilenga watoa huduma ya chakula kwenye mikusanyiko hapa nchini na kuwataka kujisajili katika mamlaka hiyo na kufuata sheria ya utoaji wa huduma hiyo ikiwemo na mazingira ya uandaji wa Chakula na kufahamu matakwa ya sheria kuhususiana na utoaji huduma hizo kuboresha mifumo ya biashara wa huduma hiyo pamoja na usalama wa chakula kinachotolewa katika mikusanyiko na hivyo kulinda afya ya walaji.

Hayo aliyasema Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Agnes Kijo wakati wa ufunguzi wa mkutano wa wadau wa utoaji wa huduma ya chakula katika Mikusanyiko, amesema kuwa kutokana na mabadiliko ya mtindo wa maisha kumekuwa na ongezeko la uhitaji wa huduma ya chakula katika Misiba, Mikutano,MaofisiHarusi.

Kijo amesema ni muhimu kutambua kuwa utoaji wa huduma ya chakula unapaswa kuzingatia Sheria na kanuni bora za usafiri ili kuhakikisha kuwa chakula kinachoandaliwa ni salama ili kulinda afya ya jamii.

"Uandaaji wa chakuka pasipo kuzingatia matakwa ya sheria na kanuni husababisha uchafuzi wa vimelea vya maradhi na hivyo kuweza kusababisha madhara ya kiafya Kama vile Kuhara,Kuhara Damu,Homa ya Matumbo,pamoja na Kipindupindu"amesema Kijo.

Aidha amesema wadau wamejitokeza kutumia fursa hiyo kutoa huduma ya hiyo ya kulisha kama njia ya kujipatia kipato bila kufata taratibu zozote lakini sasa sheria lazima zifuatwe.

Hata hivyo amesema uchafuzi wa vimelea vya maradhi katika chakula imeendelea kuwa tatizo kwa afya ya jamii hasa katika nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania. 

Amesema mfumo kwa mujibu wa taarifa za shirika la AF ya Duniani (WHO) za mean 2015,inakadiriwa kuwa milioni 600 duniani (sawa na mtu mmoja Kati ya watu 10) huugua kila mwaka kutokana na kula chakula kisicho salama na kati ya hao watu 420,000 hufariki dunia.

Mmoja wa Wadau wa Utoaji Huduma ya Chakula katika Mikusanyiko wa kampuni ya Love Michael Lee amesema kuwa watafuata sheria za TFDA katika kuwaweka huru katika kufanya biashara hiyo.

Amesema kuna uwepo watoa huduma ya vyakula bila kuwa na ujuzi wala kuwa na vibali maalumu.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu Agnes Kijo akizungumza wakati akifungua mkutano wa wadau wa watoa huduma ya Chakula Katika Mikusanyiko uliofanyika Jijini Dar es Salaam. 
(Picha na Emmanuel Massaka Globu ya jamii)
Kaimu Mkurugenzi wa Usalama wa Chakula wa TFDA Justin Makisi akizungumza kuhusiana na madhumuni ya wadau utoaji huduma katika mkusanyiko ,jijini Dar es Salaam. 

Baadhi ya wadau wa watoa huduma ya Chakula katika Mikusanyiko.

Maofisa Habari Wasisitizwa Mawasiliano Kupitia Mitandao ya Kijamii

$
0
0

Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri akizungumza katika kikao baina yake na viongozi wa Chama cha Maafisa Habari na Mawasiliano Seriikalini (TAGCO) na Idara ya Habari –MAELEZO wakati wa ziara ya kutembelea Maafisa Habari wa Mikoa na Halmashauri za Kanda ya Kati leo Mkoani Tabora. Kutoka kulia ni Mjumbe wa Kamati Tendaji wa TAGCO, Inocent Byarugaba, Afisa Tehama wa Mkoa wa Tabora, Frank Lema, Makamu Mwenyekiti wa TAGCO, Bi. Sarah Kibonde Msika na Mweka Hazina Msaidizi wa TAGCO, Gerald Chami. Kutoka kulia ni Mjumbe wa TAGCO, Innocent Byarugaba,Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari –MAELEZO, Bi. Zamaradi Kawawa, Makamu Mwenyekiti wa TAGCO, Bi. Sarah Kibonde Msika, Mweka Hazina Msaidizi wa TAGCO, Gerald Chami na Kaimu Mkuuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano Mkoa wa Tabora, Frank Lema. Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari –MAELEZO,Bi. Zamaradi Kawawa akielezea jambo walipokutana na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Frank Lema katika ziara ziara ya kutembelea Maafisa Habari wa Mikoa na Halmashauri za Kanda ya Kati leo Mkoani Tabora. Kutoka kulia ni Mjumbe wa Kamati Tendaji wa TAGCO, Inocent Byarugaba, Kaimu Mkuuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano Mkoa wa Tabora, Frank Lema, Makamu Mwenyekiti wa TAGCO, Bi. Sarah Kibonde Msika na Mweka Hazina Msaidizi wa TAGCO, Gerald Chami. Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Maafisa Mawasiliano Serikalini (TAGCO), Bi. Sarah Kibonde Msika akifafanua jambo katika kikao baina ya viongozi wa Chama cha Maafisa Mawasiliano Serikalini (TAGCO) na Idara ya Habari – MAELEZO na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Frank Lema wakati wa ziara ya kutembelea Maafisa Habari wa Mikoa na Halmashauri za Kanda ya Kati leo Mkoani Tabora. Kutoka kulia ni Mjumbe Afisa Tehama wa Mkoa wa Tabora, Frank Lema na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari –MAELEZO, Bi. Zamaradi Kawawa(katikati). Mweka Hazina Msaidizi wa Chama cha Maafisa Mawasiliano Serikalini (TAGCO), Gerald Chami akielezea jambo katika kikao baina ya viongozi wa Chama cha Maafisa Mawasiliano Serikalini (TAGCO), Idara ya Habari – MAELEZO na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Frank Lema(wapili kulia) wakati wa ziara ya kutembelea Maafisa Habari wa Mikoa na Halmashauri za Kanda ya Kati leo Mkoani Tabora. Kutoka kulia ni Mjumbe wa TAGCO, Innocent Byarugaba,Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari –MAELEZO, Bi. Zamaradi Kawawa, na Makamu Mwenyekiti wa TAGCO, Bi. Sarah Kibonde Msika . Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Tabora, Ignas Mjwahuzi(kulia)akielezea jambo mara baada ya kikao baina yake na viongozi wa Chama cha Maafisa Mawasiliano Serikalini (TAGCO) na Idara ya Habari – MAELEZO wakati wa ziara ya kutembelea Maafisa Habari wa Mikoa na Halmashauri za Kanda ya Kati leo Mkoani Tabora. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari –MAELEZO, Bi. Zamaradi Kawawa, Mjumbe wa Kamati Tendaji ya TAGCO, Innocent Byarugaba,Mweka Hazina Msaidizi wa TAGCO, Gerald Chami, Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Frank Lema na Makamu Mwenyekiti wa TAGCO, Bi. Sarah Kibonde Msika . Mjumbe wa Chama cha Maafisa Mawasiliano Serikalini (TAGCO), Innocent Byarugaba akisisitiza jambo katika kikao baina ya viongozi wa Chama hicho, Idara ya Habari – MAELEZO na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Frank Lema (katikati) wakati wa ziara ya kutembelea Maafisa Habari wa Mikoa na Halmashauri za Kanda ya Kati leo Mkoani Tabora. Kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari –MAELEZO, Bi. Zamaradi Kawawa, na Makamu Mwenyekiti wa TAGCO, Bi. Sarah Kibonde Msika . Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Chama cha Maafisa Habari na Mawasiliano wa Serikali (TAGCO) na Idara ya Habari – MAELEZO, wakati wa ziara ya kutembelea Maafisa Habari na Mawasiliano katika mikoa ya Kanda ya Kati jana mkoaniTabora. (Picha zote na: Frank Shija- MAELEZO, Tabora)

MTUHUMIWA WA UHUJUMU UCHUMI SINGH SETHI AIAMBIA MAHAKAMA HAJAONANA NA MKEWE KWA MIEZI SITA SASA

$
0
0

Na Karama Kenyunko,Globu ya jamii

MSHITAKIWA  Harbinder Singh Sethi  anayekabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa ana miezi sita sasa hajawahi kuonana na mke wake.

Sethi ameeleza hayo leo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Huruma Shaidi wakati kesi yao ilipokuja kwa kutajwa.

Ameeleza hayo, baada ya Wakili wa Serikali Mwanaamina Kombakono kuieleza Mahakama kuwa kesi ilipangwa kwa ajili ya kutajwa, upelelezi bado haujakamilika na akaomba ipangiwe tarehe nyingine.

Kutokana na maelezo hayo kutoka kwa Kombakono Wakili anayemtetea Sethi,  Dorah Mallaba alidai kuwa bado hawajapata kibali kwa  ajili ya mshtakiwa Sethi kuonwa na mkewe.

Kutokana na hayo, aliiomba Mahakama iruhusu japo kwa dakika tano Sethi aonane na mkewe.

"Naomba Mahakama itumie busara kwa kuwa make wake yupo hapa mahakamani," amesema.

Wakili Kombakono alipinga hoja hiyo ya wakili Mallaba na kueeleza  kuwa  taratibu za kuwaona mahabusu zifuatwe.

Hata hivyo, Hakimu Shahidi amewaeleza upande wa utetezi kuwa taratibu za kuwaona na kuwatunza mahabusu ipo chini ya Magareza hivyo, kama kuna jambo lolote mahususi walete mahakani.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Septemba 13 mwaka huu kwa ajili ya kutajwa.

Katika kesi hiyo Sethi  anashtakiwa pamoja na James   Rugemarila, ambapo  wanakabiliwa na mashtaka  12 ya  uhujumu uchumi  kwa kula njama, kujihusisha mtandao wa uhalifu , kighushi,  kutoa nyaraka za kughushi, kujipatia fedha kwa njia za udanganyifu,  kutakatisha fedha  na kuisababisha hasara ya USD 22, 198,544.60 na Sh 309,461,300,158.

RAIS DKT. MAGUFULI AZUNGUMZA NA MADIWANI PAMOJA NA WATUMISHI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA CHATO MKOANI GEITA

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Madiwani, Viongozi mbalimbali pamoja na Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato katika mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato mkoani Geita. Wengine katika picha ni Mkuu wa Wilaya ya Chato Eng. Mtemi Msafiri Semeon(kushoto) na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Chato Eliud Mwaiteleke(kulia).
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato mara baada ya kumaliza mkutano huo na Madiwani, Viongozi mbalimbali pamoja na Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato. Wengine katika picha ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato Christian Manunga wapili kutoka (kulia) mstari wa kwanza mbele, Mkuu wa Wilaya ya Chato Eng. Mtemi Msafiri Semeon watatu kutoka (kulia), Waziri wa Nishati na Madini Dkt. Medard Kalemani, wanne kutoka (kushoto) pamoja na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Chato Eliud Mwaiteleke.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Baadhi ya Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato mara baada ya mkutano huo uliofanyika katika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato mkoani Geita. Wengine katika picha mstari wa mbele ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato Christian Manunga wakwanza kutoka (kulia) mstari wa kwanza mbele, Mkuu wa Wilaya ya Chato Eng. Mtemi Msafiri Semeon wapili kutoka (kulia), Waziri wa Nishati na Madini Dkt. Medard Kalemani wapili kutoka kushoto pamoja na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Chato Eliud Mwaiteleke.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono Madiwani pamoja na Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato wakatika akiondoka katika Ofisi za Halmashauri hiyo Chato mkoani Geita.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwasili katika ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Chato kwa ajili ya mkutano na Madiwani, Viongozi mbalimbali pamoja na Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato mkoani Geita.
Baadhi ya Watumishi wa halmashauri ya Wilaya ya Chato wakifatilia kwa makini wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli alipokuwa akizungumza masuala mbalimbali katika ukumbi wa Halmashauri hiyo Chato mkoani Geita. 
PICHA NA IKULU

16 WANAODAIWA KUKWAPUA FEDHA ZA USHIRIKA WILAYANI HAI ,WAWEKWA NDANI KWA AMRI YA DC SABAYA

$
0
0

 
Mkuu wa wilaya ya Hai,Lengai Ole Sabaya akizungumza wakati wa mkutano wa utoaji wa taarifa ya uchunguzi wa kamati iliyoundwa na mkuu huyo kuchunguza ubadhilifu wa fedha za Ushirika wa watumia maji katika kijiji cha Mijongweni.
Mkuu wa wilaya ya Hai,Lengai Ole Sabaya akiwahoji baadhi ya wajumbe wa serikali ya kijiji cha Mijongweni kuhusiana na ubadhilifu uliofanyika katika Ushirika huo.
Mkuu wa wilaya ya Hai,Lengai Ole Sabaya ,akizungumza juu ya maamuzi yaliyochukuliwa mara baada ya kamati aliyoiunda kuwasilisha taarifa yake.
Baadhi ya wananchi wakisikiliza kwa makini juu ya maamuzi yaliyochukuliwa na Mkuu huyo wa wilaya.
Baadhi ya wananchi wakionesha mabango yenye ujumbe mbalimbali wakati wa mkutano huo.
Katibu tawala wa wilaya ya Hai,Upendo Wera akizungumza katika mkutano huo.
Mmoja wa wakazi wa kijiji cha Mijongweni ,Omary Mohamed akizungumza kwa niaba ya wananchi wengine katika mkutano huo.

Mkuu wa wilaya ya Hai,Lengai Ole Sabaya akitizama baadhi ya mashine zilizotolewa kwa Ushirika huo ambazo zinatajwa kutumika huku mapato yake hayajulikani yalipo.
Moja ya Mashine hizo ikiwa tayari imeharibika baada ya kuondolewa Roller inayotumika kwa ajili ya kutembelea.
Mashine mpya ya Ushirika huo ambayo haijaanza kutumika bado.

Baadhi ya watuhumiwa wa ubadhilifu wa fedha za Mradi wa Ushirika huo wakiwa kwenye gari la Polisi mara baada ya kukamatwa wakiwa eneo la mkutano.



Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini.
-WADAIWA KUFANYA UBADHILIFU WA ZAIDI YA MIL 200.
-WENGINE WAUZA VIPURI VYA MASHINE.

WATU 16 wakiwemo viongozi wa Bodi ya Ushirika wa Umoja wa watumia maji katika kijiji cha Mijongweni (UWAMI) wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa amri ya mkuu wa wilaya ya Hai,Lengai Ole Sabaya wakituhumiwa kuhusika na ubadhilifu wa fedha za mradi zaidi ya Sh Mil 200.

Mbali na Viongozi wa Bodi ya ushirika huo wakiongozwa na Mwenyekiti wake ,Nuru Ndoma pia wamo baadhi ya wajumbe wa serikali ya kijiji, Viongozi wa kamati ya mpito ya kusimamia mradi huo ikiongozwa na Alex Mkwizu.

Kukamatwa kwa Viongozi hao kunatokana na taarifa ya uchunguzi uliofanywa na kamati iliyoundwa na Mkuu huyo wa wilaya kuchunguza madai ya ubadhilifu wa fedha baada ya kukataa taarifa yaawali ya kamati kama hiyo iliyoundwa na aliyekuwa mkuu wa wilaya hiyo Gelasius Byakanwa.

Tuhuma zinazowakabili watu hao zimetajwa kuwa ni pamoja na kuuzwa kinyemela kwa Mashine ya kulimia (Power tiller ) aina ya Kubota iliyotolewa na Wizara ya Kilimo kwa kijiji cha Mijongweni ambayo inatajwa kuuzwa kwa mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la Yusuph Losindilo.

Baadhi ya viongozi hao pia wanatajwa kutakatisha fedha za malipo ya ukodishwaji wa mashine ya kuvunia Mpunga kwa kuziingiza katika akaunti ya kijiji na kasha kuzitoa wakati huo huo na kuzipangia matumizi yasiyokuwa na maelezo ya kutoshereza.

Aidha watu hao pia wanadaiwa kuuza baadhi ya vipuri vya Mashine hizo na baadae kuonesha kuwa wamenunua vipuri kwa ajili ya matengenezo ya mashine hizo huku ikionyesha vipuri vinavyodaiwa kununuliwa ni vile vilivyoletwa pamoja na mashine.

Katika taarifa yake ,Mwenyekiti wa kamati hiyo maalumu ya uchunguzi ,Valeria Banda alisema wizara ya Kilimo ,chakula na Ushirika kupitia Halmashauri ya wilaya ya Hai ilipeleka mashine tano za kuvuna na moja ya kupura mpinga kwa lengo la kupunguza adha ya wananchi kuvuna na kupura mpunga kwa kutumia mikono.

“Lengo jingine la kutolewa kwa mashine hizi ilikuwa ni kuongeza chanzo cha mapato kwa wananchi wa kijiji cha Mijongweni ,mashine tatu zenye thamani ya Sh Mil 222.5 zilikuwa ni Combine Harvester aina ya Kubota , mbili aina ya Daedong na moja ya Kupura mpunga (Paddy thresher) zenye thamani ya Sh Mil 152.8”alisema Valeria.

Alisema katika kuendeleza ubadhilifu watu hao wanadaiwa kushindwa kusimamia matumizi ya mashine hizo ambapo inadaiwa wajumbe wa bodi walipangiana zamu ya kusimamia mashine izo wakati wa zoezi la uvunaji kwa maslahi yao binafsi huku wengine wakivuna nyakati za usiku bila kuwasilisha hesabu za mavuno hayo kwa uongozi.

“Mfano Mayunga Mathayo anatuhumiwa kuvuna nyakati za usiku na kutowasilisha hesabu za fedha alizokuwa anapata ,hali iliyosababisha afukuzwe kuwa mjumbe wa bodi.Mayunga pia aliuza Hydrolic pump (Orignal) aina ya Kubota yenye thamani ya sht Mil 5 ya mashine namba tisa ya kuvuna mpunga na kufunga pump isiyo na ubora kwenye mashine hiyo ambayo kwa sasa imeharibika.”alisema Valeria.

Valeria alisema fedha zilizokuwa zinapatikana shambani zaidi ya asilimia 50 zilifanyiwa matumizi shambani na wakati mwingine fedha zote zilitumika huko huko shambani bila kufikishwa ofisini na hata zilizofikishwa bado zilipangiwa tena matumizi.

“Baada ya fedha kufanyiwa matumizi zilizobaki zilipelekwa SACCOS ya jitegemee na kutolew wakati huo huo kwa matumizi mengine yasiyo na kibali wala vithibitisho vyovyote ,mfano Oktoba 18 ,2016 kiasi cha sh 810,000 ziliingizwa kwenye akaunti na tarehe hiyo hiyo Sh 800,000 zikatolewa ,katibu wa Bodi Severa Kimati aliyehusika kuziweka na kuzitoa hakuwa na maelezo ya kutosha zaidi ya kusema alitumwa na mwenyekiti wa Bodi Nuru Ndoma”alisema Valeria.

Alisema fedha ambazo zingetakiwa kuwekwa katika akaunti ya kijiji toka Machi,2016 wakati mashine hizo zikianza kufanya kazi hadi kufikia Juni ,2018 kipindi ambachowalifanya kazi wajumbe wawili kutoka kwenye jamii zilipaswa kuwa Sh Mil 285.6 lakini kiasi kilichopo ni Sh Mil 10.9 ambazo zilipatikana baada ya afisa mtendaji na afisa ugani kuamua kusimamia mashine moja katika kipindi cha mwezi mmoja.

Akizungumza baada ya kutolewa kwa taarifa hiyo ,Mkuu wa wilaya ya Hai,Lenga Ole Sabaya alimuagiza Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Hai,Lwelwe Mpina kumkamata aliyekuwa Mkuu wa idara ya Ushirika wa wilaya hiyo , Raphael Mbwambo ambaye alitajwa pia kuhusika katikaubadhirfu huo.

Alisema viongozi wa Bodi, ya Ushirika huo hawakuwa na uhalali kutokana na kwamba hakuna wanahisa wala wanachama waliokaa na kuwachagua na kwamba waliteuana kwa maslahi yao binafsi huku akitaka fedha zote zilizopotea kurejeshwa.


“HAwa viongozi wa Bodi kwa kushirikiana na wajumbe wa serikali ya kijiji warudishe fedha walizoiba za wananchi wanyonge wa kijiji cha Mijongweni ,Nimeelekeza wasiingie kwenye ofisi yoyote ya umma,hawa ni waharifu kama waharifu wengine hadi itakapothibitika vinginevyo.”alisema Ole Sabaya.

Wanaoshikiliwa ni pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya ushirika huo ,Nuru Ndomba na Katibu wake wake Severa Kimati pamoja na wajumbe wengine, Salama Amani,Sadiki Msangi, Abuu Musa na D eogratius Bruno,.

Wengine ni Alex Mkwizu, Mashati Amani, Bakari Malola, Adamu Mdaki,Mayunga Mathayo ,Abdalah Dhamiri,Richard Msele,Ramadhan Miraji ,Miraji Araba na Koswai Mrisho.

WATAKIWA KUACHA KUTUMIA MAGARI YAO YA DHARURA VIBAYA

$
0
0
 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Ramadhani Ng’anzi akizungumza wakati akiwakaribisha ofisini kwake  Viongozi wapya wa Makampuni ya Ulinzi Mkoa wa Arusha waliochaguliwa tarehe 11 Agosti,2018 katika Ukumbi wa Maofisa wa Polisi Arusha.
  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Ramadhani Ng’anzi akiwa katika picha ya pamojamara baada ya kuwakaribisha ofisini kwake  Viongozi wapya wa Makampuni ya Ulinzi Mkoa wa Arusha waliochaguliwa tarehe 11 Agosti,2018.

Na Gasto Kwirini wa Polisi Arusha
JESHI la Polisi Mkoani hapa limeyaonya baadhi ya Makampuni ya Ulinzi kuacha tabia ya kutumia magari yao ya dharura vibaya kinyume na utaratibu pindi wawapo barabarani.

Hayo yamesemwa leo na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Ramadhani Ng’anzi wakati akiwakaribisha ofisini kwake  Viongozi wapya wa Makampuni ya Ulinzi Mkoa wa Arusha waliochaguliwa tarehe 11 Agosti mwaka huu katika Ukumbi wa Maofisa wa Polisi Arusha.

“Kuna baadhi ya Magari ya Makampuni ya Ulinzi yanatumiwa vibaya kwa kigezo cha kuwahi dharura japokuwa wakati mwingine huko waendako hakuna hiyo dharura inayowataka wafanye hivyo. Lakini pia pale kwenye ulazima msitumie magari hayo ya  dharura kwa kubeba vitu haramu  kama vile bhangi”. Alionya kamanda Ng’anzi.

Aidha aliwahakikishia kufuatilia na kuzifanyia kazi changamoto zao hasa za ucheleweshwaji wa utolewaji wa vibali vya umiliki wa silaha, ucheleweshwaji wa utolewaji wa matokeo ya alama za Vidole kwa Askari wapya wanaoajiriwa. Ameyataka Makampuni yenye changamoto hizo kuorodhesha majina yao kupitia viongozi hao, na kuyapeleka ofisini kwake ili aweze kuyafanyia kazi kwa kushirikiana na idara husika na matokeo ya Alama hizo na Vibali hivyo viweze kutolewa haraka na kwa wakati.

Pia amewahaidi kuwasiliana na Ofisi ya Mshauri wa Mgambo Mkoa wa Arusha ili Askari ambao hawakupata mafunzo wayapate kwa awamu huku wakiendelea na majukumu yao. Amewataka Viongozi hao kuorodhesha majina ya Askari hao na kuyapeleka Ofisini kwake.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Makampuni ya Ulinzi Mkoa wa Arusha Bwana Daudi Mungi kwa niaba ya Viongozi wenzake, alitoa shukrani kwa Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha kwa ushirikiano wa mara kwa mara wanaondelea kuupata na kuhaidi kuendelea kutoa ushirikiano kwa Jeshi hilo wakati wote.

Awali akiwakaribisha Viongozi hao, Mkuu wa Operesheni wa Polisi Mkoa wa Arusha Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) Elias Tabana Mwita alisema kwamba ataendeleza ushirikiano uliopo kwa Makampuni ya ulinzi hasa ikizingatia kuwa mchango wa Makampuni hayo ni mkubwa katika kuimarisha ulinzi na usalama katika Mkoa huu. Pia aliwataka kufanya kazi kwa kufuata Sheria na taratibu zinazowaongoza.

Mwenyekiti wa Makampuni ya Ulinzi aliambatana na Viongozi wenzake ambao ni Makamu Mwenyekiti Bwana James Rugangila, Bi. Malima Macha ambaye ni  Katibu, Naibu katibu Bwana James Babu na Mjumbe mmoja Bwana Rashid Mtungi.

Picha 1. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Ramadhani Ng’anzi akiwa akiwa katika kikao na Viongozi wa Makampuni ya Ulinzi Mkoa wa Arusha waliofika Ofisini kwake kwa ajili ya kujitambulisha

Picha 2. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha akiwa katika Picha ya pamoja na viongozi wa Makampuni ya ulinzi Mkoa wa Arusha pamoja na Baadhi ya Maofisa wa Polisi mkoani 

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuomgoza ujumbe wa Tanzania kwenye Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya Afrika na China (FOCAC) mjini Beijing

$
0
0
Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya Afrika na China (FOCAC) utafanyika Beijing kuanzia tarehe 01 hadi 04 Septemba, 2018.

Ujumbe wa Tanzania kwenye mkutano huo utaongozwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa. Viongozi wengine watakaoshiriki Mkutano huo ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga; Mhe. Khalid Salum Mohamed, Waziri wa Fedha na Mipango wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Mhe. Rashid Ali Juma, Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, na Viongozi wengine Waandamizi.

Mkutano huo utafunguliwa na Rais wa China, Mhe. Xi Jinping ambaye pia ni Mwenyekiti wa jukwaa hilo, kwa kushirikiana na Mwenyekiti Mwenza, Rais wa Afrika Kusini, Mhe. Matamela Cyril Ramaphosa, utahudhuriwa pia na Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika ambaye pia ni Rais wa Rwanda, Mhe. Paul Kagame, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Mhe. Antonio Guterres na Mwenyekiti wa Kamisheni ya Afrika ambaye pia ni Rais wa Chad, Mhe. Moussa Faki Mahamat. Mkutano huo pia utashuhudia uchaguzi wa Mwenyekiti Mwenza mpya kutoka Afrika.

Kaulimbiu ya Mkutano wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika kwa mwaka 2018 ni “China na Afrika: Kuelekea Jumuiya Imara kwa mustakabali wa wote kupitia ushirikiano kwa manufaa ya wote” (China and Africa: Toward an Even Stronger Community with a Shared Future through Win-Win Co-operation).

Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali utatanguliwa na kikao cha Makatibu Wakuu kitakachofanyika tarehe 01 Septemba, 2018. Kikao hicho pamoja na mambo mengine kitapitia agenda za mkutano huo na kuziwasilisha kwenye kikao cha Mawaziri kitakachofanyika tarehe 02 Septemba, 2018.

Mkutano wa Jukwaa la Ushirikiano kati Afrika na China pamoja na mambo mengine utajadili namna ya kuimarisha ushirikiano kati ya Afrika na China na kufanya mapitio ya mikakati ya pamoja ya maendeleo iliyopo kati ya Afrika na China. Jukwaa hilo ambalo lilianzishwa mwaka 2000 huwaleta pamoja viongozi wa Afrika na China kujadili masuala ya ushirikiano na maendeleo na kutathmini utekelezaji wa makubaliano mbalimbali yanayofikiwa kati yao.

Aidha, masuala ya ushirikiano katika uendelezaji Miundombinu kama Barabara, Reli, Bandari na upatikanaji wa umeme wa uhakika kwa Bara la Afrika yatajadiliwa kwa kina. Agenda nyingine itahusu kilimo cha kisasa ambapo China itatoa uzoefu wake katika kutumia sayansi na ubunifu wa kiteknolojia katika kufikia uzalishaji wenye tija na kuongeza thamani kwa mazao ili kuwa na soko la uhakika.

FOCAC 2018 pia itajadili masuala ya biashara na uwekezaji ambapo kwa kuona umuhimu huo, Mhe. Xi Jinping, Rais wa China atafungua rasmi Mkutano wa Jukwaa la Biashara kati ya China na Afrika utakaofanyika tarehe 03 Septemba, 2018.

Mkutano wa kwanza wa Wakuu wa Nchi wa Jukwaa hili ulifanyika Beijing mwaka 2006 na Mkutano wa Pili ulifanyika nchini nchini Afrika Kusini mwaka 2015.

Wakati wa Mkutano wa pili, China ilitangaza mpango kabambe wa kuhamasisha mapinduzi ya viwanda na kilimo cha kisasa kwa Afrika wenye gharama ya Dola za Marekani bilioni 60 katika utekelezaji wake. Kufuatia ushirikiano kupitia Jukwaa hilo biashara kati ya China na Afrika imeongezeka pamoja na ongezeko la ushirikiano wa kiutamaduni na biashara baina ya watu wa China na Afrika.

Pembezoni mwa Mkutano huo, Tanzania na China zimeandaa Kongamano la Biashara ambalo litafunguliwa rasmi na Mhe. Waziri Mkuu tarehe 02 Septemba, 2018. Kongamano hilo ambalo litajadili kwa kina masuala ya uwekezaji na biashara kati ya Tanzania na China litashirikisha takribani makampuni 80 kutoka nchi hizi mbili.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Dodoma.



30 Agosti 2018

MAKAMU WA RAIS AONGOZA KIKAO CHA BARAZA LA MAWAZIRI JIJINI DODOMA

$
0
0



  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongoza kikao cha Baraza la Mawaziri , kushoto ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, kikao hicho kimefanyika kwenye ukumbi wa TAMISEMI, Mkapa House leo jijini Dodoma
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Kangi Lugola (kushoto) akizungumza na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega kabla ya kuanza kwa kikao cha Baraza la Mwaziri katika ukumbi wa TAMISEMI jijini Dodoma.
 Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Subira Mgalu (kulia) akizungumza na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji muda mfupi kabla ya kuanza kikao cha Baraza la Mawaziri katika ukumbi wa TAMISEMI jijini Dodoma. 

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongoza kikao cha Baraza la Mawaziri katika ukumbi wa TAMISEMI, Mkapa House jijini Dodoma leo.
Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Subira Mgalu (kulia) akizungumza na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji muda mfupi kabla ya kuanza kikao cha Baraza la Mawaziri katika ukumbi wa TAMISEMI jijini Dodoma. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

SHIKAMOO RAIS DK.MAGUFULI…UKIPATA NAFASI NAOMBA USOME NILICHOKUANDIKIA

$
0
0
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
SHIKAMOO Mheshimiwa Rais Dk.John Magufuli.
Pia naomba kutumia nafasi hii kutoa pole nyingi kwako kutokana na msiba wa kuondokewa na dada yako mpendwa Monica Magufuli.

Pole Rais wangu, pole familia ya Rais, ndugu, jamaa na marafiki. Mungu aiweke roho ya mpendwa wetu mahala pema peponi. Amina. 

Baada ya utangulizi huo naomba niseme jambo kidogo. Nilishiriki uchaguzi Mkuu mwaka 2015 na kura yangu ya Urais nilikuchagua wewe.

Nikiri sikukosea kwa uamuzi wa kura yangu kukupa wewe uwe Rais wangu. Sijakosea na nashukuru Mungu alinipa utulivu wa kuchagua Rais sahihi kwa ajili ya maisha ya Watanzania wote.

Rais wangu mpendwa nimekuwa nikifuatilia utendaji wako wa kazi, nimekuwa nikifuatilia maagizo yako kwa walio chini yako.Kubwa zaidi nimekuwa nikifuatilia hotuba zako mbalimbali.

Naomba nikiri Rais wangu hotuba yako ambayo umeizungumza wilayani Chato imenigusa mno. Najua umetoa hotuba kadhaa ukiwa Chato lakini naomba nikukumbushe naizungumzia hii hotuba yako ya  kuhusu makontena ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.

Hotuba yako imethibitisha namna ambavyo unaamini katika kusimamia misingi ya utawala wa sheria.

Najua namna ambavyo umewakosha wengi. Umewakosha si kwa sababu wanamchukia au wanampenda saana Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, bali ni kwa kuonesha unavyosimamia sheria.

Ujue Rais wangu huku mtaani ninakoishi kuna mengi yamekuwa yakizungumzwa. Wapo wanaosema unampenda sana Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na kwa sababu unampenda basi hata akikosea huwezi kumchukulia hatua.

Si mimi ninayesema, ila huku mtaani ndio wanavyosema hivyo. Ukweli ni kwamba mtaani kuna maneno maneno mengi yanazungumzwa hasa tukiwa kwenye vijiwe vya kahawa. Basi bwana watu wanazungumza lakini wakifika kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam utasikia wakisema “Huyooo RC wa Dar anapendwa sana. Hawezi kuchukuliwa hatua.”

Basi watasema maneno mengi na wengine wanakumbusha matukio mengi mengi. Kwa kuwa maneno ya kijiweni huwa yanaishia huko huko kijiweni. Anayezungumza sana ndio anaonekana mshindi. Haya ya mtaani yasikupe tabu tuachie sie wa mtaani ndio maisha yetu.

Binafsi nimekuwa na tabia ya kukaa kimya hasa kwenye mambo yanayohusu viongozi wangu, huwa naogopa kusema maana naweza kuambiwa sina adabu.

Nimekuwa muumini wa kuheshimu, kuthamini na kutambua mamlaka zilizopo pamoja na wale ambao umewapa dhamana ya kutusimamia.

Leo naomba nivunje mwiko wa kuzungumza japo kidogo. Iko hivi, Rais wangu hotuba yako kuhusu makontena ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam nimeisikiliza na kuichambua kwa kina.

Naomba nieleweke nimeichambua kwa kiwango cha uwezo wangu wa kufikiri na kuchambua mambo, usinielewe vibaya huenda nachangia ujinga lakini bora niuseme niwe huru.

Baada ya kukusikiliza cha kwanza ambacho kimenijia akilini nilisema kimoyo moyo hakika huyu ndio Rais ambaye Watanzania tunamuhitaji.

Pia nikasema nimeamini Rais wangu anasimama katika sheria katika kuzungumzia jambo lolote, hili  la makontena umelizungumza kwa misingi ya kisheria.

Wakati naendelea kutafakari kuhusu hotuba yako pia nikabaini huna rafiki wala adui wa kudumu, kwako unaangalia sheria inataka nini katika kuzungumzia jambo. Hongera Rais Magufuli.

Binafsi nimekuwa nikifuatilia kwa karibu suala la makontena ya Makonda ambayo ndani yake yana samani kwa ajili ya walimu wa Mkoa wa Dar es Salaam. Ndivyo tunavyoambiwa.

Kwa bahati mbaya baada ya makontena hayo kutangazwa kuwa yatapigwa mnada Makonda kwa mara kadhaa amezungumza.

Mazungumzo yake kwa sehemu kubwa yalionesha hana shaka, hata kama kuna watu akiwamo Waziri wa Fedha Dk. Philip Mpango wanataka kukwamisha makontena hayo yasitoke atakwambia wewe (Rais).

Sina hakika kama tayari alishakwambia kuhusu kuzuiliwa kwa makontena hayo.

Pia mwishoni mwa wiki iliyopita Makonda akiwa wilayani Ngara mkoani Kagera akiwa kanisani akaamua kuzungumzia tena suala la kuzuiliwa kwa makontena hayo.

Akaenda mbali zaidi kwa kusema kuwa atakayenunua Mungu atamlaani ni kauli ya vitisho ambayo ameitoa kwa Waziri Mpango.

Hata hivyo, Waziri Mpango naye Jumatatu ya wiki hii akaamua kutoa msimamo wake, akasema lazima makontena hayo yalipiwe kodi, kinyume na hapo yapigwe mnada akaenda mbali zaidi kwa kusema  hatakuwa tayari kuona sheria za kodi zinachezewa. Hakusita kutoa la moyoni kuwa iwapo atashindwa kusimamia hilo atajipima.

Sijui Dk. Mpango, alikuwa anamaanisha nini lakini nadhani alikuwa tayari kukaa kando iwapo makontena hayo yataruhusiwa kutoka bandarini bila kulipiwa kodi.

Ahsante Rais Magufuli, kwa sababu umesimama katika kweli, kwa hotuba yako ya jana kuhusu makontena hayo maana yake umefunga rasmi mjadala.

Makonda anatakiwa kulipa kodi ili mambo mengine yaendelee.
Nikiri sina chuki na Mkuu wangu wa Mkoa wa Dar es Salaam, pia nikiri sina urafiki naye, bali nikiri ndio Mkuu wangu wa Mkoa na naheshimu na kuthamini nafasi yake, navutiwa na utendaji wake.

Hata hivyo, kabla ya kusikia kauli yako Rais wangu nilikuwa najiongelesha kimoyo moyo kwamba Makonda hakustahili kutumia nguvu nyingi kupambania makontena hayo yatoke bila kulipiwa kodi.

Nikakumbuka ule usemi unaosema hivi: “Mdomo ulimponza kichwa.” Hata hivyo, sikuwa na mahali pakusemea, ila hotuba yako imenipa nguvu na ndio maana napata uthubutu wa kusema.

Najua niko salama maana si dhambi kutoa maoni yangu.
Nilikuwa nawaza iwapo makontena hayo yataruhusiwa yatoke bila kulipiwa kodi. Itakuwaje ikitokea na wakuu wa mikoa wengine wakaanza kuagiza makontena kwa ajili ya wananchi wao na kisha wakataka yasilipiwe kodi?

Kwa mtu wa aina yangu huwa tunawaza na kuacha tu mambo yapite. Hata ukisema nani anakusikia? Hata ukishauri nani anakusikiliza? Je baada ya kupaza sauti yako nani ataifanyia kazi?

Basi nikawa najiuliza maswali mengi bila majibu.
Nikwambie Rais wangu Magufuli, umejibu maswali mengi ambayo nilikuwa najiuliza kimya kimya moyoni. Umethibitisha kumbe unaweza kuyajibu hata yale ambayo tumeamua kukaa kimya.

Wewe ni Rais bora kwa Taifa la Tanzania. Wakati wa kampeni zako za kuwania urais nikiri nilipata bahati ya kuzunguka kwenye kampeni zako katika mikoa karibu yote, sikubahatika kuwa katika Mkoa wa Kigoma, Mbeya na Iringa, lakini mikoa mingine yote nilishiriki.

Kupitia kazi yangu ya uandishi wa habari chombo changu cha habari (Jambo Leo) nilichaguliwa kuwa sehemu ya waandishi wa mgombe urais wa CCM (Ni wewe Rais Magufuli).

Nikwambie tu sijuti kuwa sehemu ya waandishi waliokuwa wanaandika kila unachosema na kukifanya wakati wa kampeni zako.

Matunda ya jua, vumbi, mvua, kutokula  mchana, kulala usiku wa manane kwa ajili ya kuhakikisha natimiza majukumu yangu kuhakikisha Watanzania wanakuchagua nilikuwa nafanya kazi sahihi.

Kwa kweli leo umenifurahisha. Si kwa sababu nataka kuona unachukua hatua zaidi kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam. Hapana umenifurahisha kwa sababu umethibitisha kwako sheria ni msumeno na unakata kote kote.

Umetimiza wajibu wako Rais wangu katika kulizungumzia hili la makontena ya Makonda. Nadhani wenye jukumu la kusimamia kodi inapatikana kutoka kwenye makontena hayo wanatekeleza yale ambayo umeyasema. Nadhani wamekusikia.

Najua una mambo mengi ya kufanya na lengo la kuandika maelezo yoote haya marefu ni kutaka uyasome. Najua huenda nimeandika kwa kirefu lakini ujumbe wangu ukawa ni mdogo. Naomba uuchukue Rais wangu na huenda hata ukishindwa kunielewa kwa niliyoeleza basi naomba ushike hata hili la kwamba nakupongeza kwa namna ambavyo umelitolea ufafanuzi suala la makontena ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.

Pia nitoe ushauri kwa Makonda kwamba najua unao marafiki wengi. Nikwambie marafiki wanaokuzunguka baadhi yao wapo kwa ajili ya kukusifu na wengi wanaogopa kukwambia ukweli maana utachukia.

Makonda kwa kuwa marafiki zako wananufaika kwa kuwa karibu yako wanajua wakikwambia ukweli utawaweka kando. Hivyo, hata ukikosea wenyewe wanakusifu.

Sitaki kutaja orodha ya marafiki zako maana unawajua vizuri kuliko mimi. Wengine kwenye hili la makontena waliamua kusimama kidete kutoa maoni yao. Si kwa sababu hajui ukweli bali walikuwa wanafanya hivyo wakiamini wanakufurahisha. Ukweli baadhi ya marafiki zako wamechangia kukufikisha hapo ambapo umefika.

Hili la ushauri kwa Makonda wala halina maana kwa siku ya leo. Uliyesoma nilichoandika baki na kile ambacho nimemwambia Rais wangu. Ahsante Rais. Hata ukishindwa kusoma hiki ambacho nimekiandika naamini wasaidizi wako watakufikishia tu. Hata kwa kusema kuna mtu anaitwa Said Mwishehe amekupongeza.

Ndugu yangu Gerson Msigwa na Dk. Hassan Abbasi mkipata nafasi ya kusoma nilichoandika basi mfikishieni na Rais wangu. Nikisikia amesoma mwenyewe nitafurahi zaidi. Si unajua tena akina sie wenye maisha ya pangu pakavu tia mchuzi ukisema kuna jambo umelisema jema na Rais amelisikia unakenua meno yote 32 nje. Ahsante Rais Magufuli. Ahsante baba. Ahsante mkuu wa nchi. Tanzania ni yangu. Tanzania ni ya kwetu. Tanzania ni ya kila mtanzania.
Napokea maoni kwa 0713 833822.

KITUO CHA SHERIA NA HAKI ZA BINADAMU CHABAINI KUONGEZEKA KWA KASI UKATILI WA KINGONO,UBAKAJI KWA WATOTO

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Glogu ya jamii
KITUO cha Sheria na haki za binadamu (LHRC)  kimezindua ripoti ya nusu mwaka ikionesha hali ya haki za binadamu katika kipindi cha miezi 6 ya mwaka 2018 yaani kuanzia Januari hadi Juni.

Akizungumza na wanahabari katika uzinduzi huo Mkurugenzi Mtendaji wa kituo hicho na Wakili  Anna Henga ameeleza kuwa ripoti hiyo imeandaliwa kwa kutumia vyanzo mbalimbali kama vile jeshi la polisi, ripoti za mashirika mbalimbali pamoja na vyombo vya habari na ripoti hiyo imegawanyika katika makundi matatu ambayo ni haki za kiraia na kisiasa, haki za kijamii na haki za za makundi maalumu.

Henga ameeleza kuwa ripoti hiyo imeibua mambo muhimu ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa kiasi kikubwa kwa ukatili dhidi ya watoto hasa ukatili wa kingono na ubakaji mara tatu zaidi ukilinganisha na kipindi cha mwaka 2017 na hii ni kwa kulinganisha matukio 12 kwa mwaka 2017 kufikia matukio 533 kwa mwaka 2018 na kati ya matukio 6376 ya ukiukwaji wa haki za watoto  matukio 2365 yametokana na ubakaji na matukio 533 ni ulawiti 

Pia ameeleza kuwa ukatili dhidi ya wanawake umeongezeka  hasa wa kingono na mwili ambapo matukio ya ubakaji yaliyoripotiwa  kuanzia mwezi Januari hadi Juni mwaka huu yamefika1218 ikikadiriwa idadi ya wanawake 203 hubakwa kwa mwezi.

Aidha ameeleza kuwa matukio ya mauaji wa kutokana na imani za kishirikina yamepungua kutoka matukio 172 hadi 106, na ajali za barabarani zinazosababisha vifo zimepungua huku hofu kubwa ikiongezeka kwa watu wenye ulemavu wa ngozi wakati nchi ikielekea kwenye uchaguzi 2019/2020.

Pia amesema kuwa haki ya kujieleza imeendelea kuminywa na hii ni baada ya kutungwa kwa kanuni za maudhui mtandaoni na changamoto katika mazingira ya elimu hasa upungufu wa matundu ya vyoo mashuleni akitolea mfano wa shule ya Msingi Ichenjezya mkoani Songwe yenye wanafunzi wapatao 1300 wanaotumia matundu 8 pekee.

Kwa upande Mtafiti anayefanya kazi na kituo hicho bw. Fundikira Wazambi ameeleza kuwa matukio ya ukatili kwa watoto yameongezeka kutoka 4,728 kwa mwaka 2017 hadi kufikia matukio 6,376 mwaka huu na matukio hayo ni pamoja na ubakaji na ulawiti na suala la ndoa za utotoni na ukeketaji bado ni changamoto.

Kwa upande wa wanawake matukio ya ukatili  dhidi ya wanawake yameongezeka hasa kimwili na kingono takimwu zinaonesha kwa nusu mwaka pekee wanawake 203 wamebakwa pia rushwa ya ngono makazini na vyuoni bado ni changamoto kubwa na hii ikihusisha wanahabari wa kike.

Kuhusiana na haki za kiraia na kisiasa yaliyoelezwa na mtafiti huo ni pamoja na mauaji yaliyofanywa na vyombo vya dola, kuminywa kwa uhuru wa kujieleza huku haki ya kuishi ikiimarika kidogo kwa kipindi cha Januari hadi Juni mwaka huu.

Haki za kijamii zimeelezwa kuwa sera ya elimu bure imewezesha watoto wengi zaidi kupata elimu ukilinganisha na miaka ya nyuma licha ya kuwepo na changamoto ikiwemo upungufu wa matundu ya vyoo mashuleni.

Pia imeelezwa kuwa kuna upungufu wa wafanyakazi wa sekta ya afya baada ya zoezi la wenye vyeti feki kupita, pia watu wenye ulemavu wameendelea kukumbwa na changamoto za unyanyapaa kwenye nyanja za elimu, ajira na miundombinu.

NAIBU WAZIRI WA FEDHA AZINDUA DCB DIGITAL MJINI DODOMA

$
0
0
  Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji (wa tatu kushoto), akibonyezxa kitufe cha kompyuta kuashiria uzinduzi rasmi wa huduma za kibenki katika mfumo wa kidigitali za Benki ya Biashara ya DCB jijini Dodoma. Wanaoangalia kutoka kushoto (mstari wa mbele ni; Mkurugenzi Mtendaji wa DCB, Godfrey Ndalahwa, Mwenyekiti wa Bodi ya DCB, Prof. Lucian Msambichaka, Mbunge wa Viti Maalumu, Mama Janeth Masaburi, Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Peter Pinda na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini, Patrobas Katambi. Huduma hizo ni pamoja na DCB Akaunti Kidigitali, Kibubu Kidigitali, Nusu Mshahara Kidigitali na huduma ya kutoa pesa katika ATM bila kadi.
 Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji akizungumza katika uzinduzi huo.
 Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda akizungumza katika hafla hiyo jijini Dodoma juzi.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Biashara ya DCB, Godfrey Ndalahwa akikaribisha wageni mbalimbali waliohudhuria uzinduzi huo jijini Dodoma.
 Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Peter Pinda (katikati), akishikana mikono na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashaitu huku Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Biashara ya DCB, Prof. Lucian Msambichaka akiangaalia mara baada ya uzinduzi huo.
 Mwenyekiti wa Bodi ya DCB, Prof. Lucian Msambichaka (kulia), akikabidhi tuzo kwa Naibu Waziri wa Fedha, Dk. Ashatu Kijaji aliyekuwa mgeni rasmi katika uzinduzi huo jijini Dodoma
Baadhi ya waalikwa waliohudhuria tukio la uzinduzi wa DCB Digital jijini Dodoma.
                            
Na mwandishi wetu,Globu ya Jamii
BENKI ya Biashara ya DCB imezindua huduma maalum ijulikanayo kama DCB DIGITAL BANKING ambayo ni huduma za kibenki zinazopatikana kwa njia ya simu.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Jijini Dodoma Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dk Ashatu Kijaji alisema sote tumesikia DCB walikua wakwanza kuorodheshwa kwenye soko la hisa na leo DCB inakwenda kidijitali na ni ya kwanza kuzindua bidhaa zake nne muhimu hili ni jambo zuri sana kwa Benki ya DCB na Taifa letu hongereni sana.

Amesema ‘’Napenda pia niwashukuru sana uongozi wa benki hii kwa kutupatia nafasi sisi Wizara ya Fedha na Mipango kuja kua sehemu ya kihistoria katika sekta yetu ya fedha”.

Nikiwa kama kiongozi wa kusimamia maswala ya fedha nimefarijika sana kuwa pamoja nanyi lakini pia nimefarijika zaidi baada ya kuisikia historia ya DCB ikielezwa hapa mbele yetu na viongozi wa benki hio. Kwakweli ni tukio muhimu sana kwetu sekta ya fedha kwasababu kwa kauli mbiu hii ya SIMU YAKO,TAWI LETU inamaana Benki inawafikia watanzania kule walipo.

Kutokana na Ripoti ya Finscope ya mwaka 2017 ilionyesha idadi ya watanzania waliojiunga na mfumo rasmi wa kifedha imeongezeka kwa asilimia 14 kutoka mwaka 2013 chachu ya ongezeko hili ni pamoja na urahisi wa upatikanaji wa huduma za kifedha kupitia simu zetu za mkononi na mashine za kutolea fedha. Lakini kutokana na uzinduzi huu wa leo naamini tutaongeza zaidi ya asilimia 70 kwasababu tutawafikia kule waliko.

Nawaelekeza DCB kuwatembelea wakulima wetu kwa sababu moja ya mpango wa serikali wa maendeleo wa miaka mitano ulioanza kutekelezwa tangu 2016 hadi 2021 umejikita zaidi katika kujenga uchumi wa viwanda, hivyo hakuna Viwanda bila taasisi za kifedha hususan benki zetu na hakuna uchumi wa Viwanda bila wakulima ambao ndio wazalishaji wa malighafi za viwanda. Kupitia huduma kama hizi za kibenki nawahakikishia tutaifikisha Tanzania yetu ya uchumi wa kati wa viwanda kabla ya mwaka 2015.

Ninachoomba elimu ya kifedha ambayo mmeitoa kwa wajasiriamali wa Dar es salaam nendeni mkaitoe kwa wakulima na wafugaji wa Tanzania kwani serikali inakwenda kuhakikisha Mkulima anapata soko la mazao yake.

Ameongeza Serikali yetu ya awamu ya tano ambayo ipo chini ya Muheshimiwa Rais John Pombe Magufuli inatambua wazi mchango wa sekta ya fedha hususan benki zetu katika kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na kufikia malengo ya Taifa letu hivyo endeleeni kuwekeza lakini pia kubuni bidhaa na huduma zinazo lingana na mazingira ya watanzania na serikali kwa upande wetu tutaendela kuhakikisha mazingira ya uwekezaji yanaendelea kuwa bora.

Kuendelea kuboresha huduma za kibenki, mwezi huu wa nane mwaka 2018 Serikali imechukua hatua madhubuti za kiutawala na kisera ambazo ningependa kuisema leo hapa kwa mara ya kwanza ni kushusha riba kutoka asilimia 16 hadi asilimia 8.

Hivyo upatikanaji wa fedha utakua ni rahisi kwa mabenki yetu.Hii yote ni kuhakikisha watanzania wanapata mitaji kwa gharama nafuu, wito wangu kwa mabenki yote ikiwemo Benki yetu ya DCB kuakisi jitihada hizi za serikali yenu ya awamu ya tano.

Dk Kijaji ameongeza “Nimefarijika sana kusikia kuwa DCB ni moja ya benki chache zilizojiunga na mfumo wa serikali ujulikanao kama Government e Payment Gateaway (GePG ) ambao ni mfumo wa serikali unaotumika kufanya malipo mbalimbali hivyo kupanua wigo wa malipo ya serikali”.

Mwenyekiti wa Bodi ya DCB Profesa Lucian Msambichaka ameongeza ‘’ Benki imeendelea kuimarika na Mwezi uliopita Benki imetangaza kupata faida katika kipindi cha nusu ya kwaka kilichoishia mwezi Juni mwaka 2018, mafanikio haya yametokana na ubunifu wa bidhaa zinazokidhi mahitaji ya wateja wetu, uweledi na huduma bora alisema.

Mkurugenzi Mkuu wa DCB Ndugu Godfrey Ndalahwa nae amesema DCB itaendelea kutoa huduma bora na za ubunifu ili kuweza kushindana kwenye soko. Bidhaa zetu ni nzuri sana na zenye ubunifu mkubwa. Kupitia DCB Digital mteja sasa ataweza kufungua akaunti ya muda maalum (Digital FDR) , Akaunti ya malengo (Kibubu Digital Account) ,Digital Salary advance na vilevile sasa anaweza kupata huduma za kutoa pesa kwenye ATM za umoja switch zilizoenea nchi nzima bila kutumia kadi ya benki (Cardless ATM).

Kwa Mawasiliano:
Rahma Ngassa
Mkuu wa kitengo cha Masoko
Simu Namba: +255 22217201

KATIBU MKUU WA CCM DKT BASHIRU ALLY AFUNGUA KIKAO CHA BARAZA KUU LA UVCCM LEO

$
0
0
Katibu Mkuu wa CCM Dkt Bashiru Ally Kakurwa akivalishwa mara baada ya kuwasili katika Ukumbi wa CCM White House Dodoma
Meza kuu ikiimba pamoja na Wajumbe wa Baraza kuu 
Wajumbe wa Baraza kuu la Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi wakiimba Nyimbo mara baada ya Katibu Mkuu wa CCM Dkt Bashiru Ally Kakurwa 
 ambae pia ni Mgeni Rasmi katika Ufunguzi wa Kikao Cha Baraza kuu ala UVCCM Taifa 
Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Mwl Raymond Mwangwala akizungumza Kuwakaribissha wajumbe wa kikao cha Baraza kuu Kilicho fanyika jjini Dodoma Leo
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Ndg.Kheri D James Akizungumza wakati wa Kumkaribisha Mgeni Rasmi Kufungua kikao Cha Baraza kuu la UVCCM Kilichofanyika JIJINI Dodoma Leo
Katibu Mkuu wa CCM Dkt Bashiru Ally Kakurwa akifungua kikao  Cha Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa CCM Kilichofanyika Jijini Dodoma Leo.
Wajumbe wa Baraza kuu wakifuatilia Mkutano 
Wabunge na wawakilishi wa nao tokana na Umoja wa Vijana

Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Bi Tabia Mwita akitoa neno la Shukran Kwa Mgeni rasmi Mara baada ya kikao cha Kufunguliwa na Katibu Mkuu wa CCM
 Mbunge wa Nzega Mhe Hussein Bashe akizungumza kwa Niaba ya Wabunge wa Chama Cha Mapinduzi katika kikao cha Baraza kuu la Uvccm Taifa.
Naibu waziri wa Kazi Vijana na Ajira na Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini akizungumza kwa niaba ya Serikali katika kikao cha Baraza kuu la UVCCM leo jijini dodoma.
(Picha zote na Fahadi Siraji UVCCM)

KILELE CHA MAFANIKIO KWA MWANAMICHEZO NI KUIWAKILISHA NCHI KIMATAIFA: WAZIRI MWAKYEMBE

$
0
0
 Katibu Mkuu  Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bibi. Susan Mlawi   akizungumza leo Jijini Dodoma na wachezaji walioshiriki mashindano ya Jumuiya ya Afrika Mashariki  (hawapo katika picha) ambapo timu ya mpira wa miguu wanawake waliibuka washindi wa kwanza, katikati ni Waziri wa Wizara hiyo Dkt. Harrison Mwakyembe na wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Bw. Yusuph Singo.
 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe  akisisitiza jambo kwa wachezaji walioshiriki mashindano ya Jumuiya ya Afrika Masharik (hawapo katika picha), wakati wa halfa ya kuwapongeza wachezaji hao leo Jijini dodoma, kwanza kushoto ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo Zanzibar Bw.Hamis Alli Mzee,anayefuata ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bibi. Susan Mlawi na  kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Bw. Yusuph Singo.
 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe  akifurahi pamoja na viongozi wengine wa Wizara  leo Jijini Dodoma baada ya  kupokea kombe kutoka kwa Nahodha wa timu ya mpira wa miguu wanawake Bi. Asha Rashidi (hayupo katika picha).
 Baadhi ya wachezaji wa Twiga Stars wakimsikilza Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (hayupo katika picha) wakati wa halfa ya kuipongeza timu hiyo leo Jijini Dodoma.
 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (Katikati) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa timu  zilizoshiriki  mashindano ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ambapo timu ya mpira wa miguu wanawake waliibuka washindi wa kwanza.
 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (Katikati) akiwa katika picha ya pamoja  na wachezaji wa timu ya Karate.

Katibu Mkuu  Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bibi. Suzan Mlawi (katikati)  akifurahi pamoja na wachezaji wa mpira wa pete  leo Jijini Dodoma  baada ya timu hiyo kurejea ikitokea Bujumbura nchini Burundi ilipokuwa ikishiriki mashindano ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ambapo iliibuka mshindi wa pili.
(Picha na Shamimu Nyaki-WHUSM)


Na Shamimu Nyaki –WHUSM
WAZIRI wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe amesema kuwa mwanamichezo anayepaswa kujivunia mafanikio katika michezo ni yule ambaye ameiletea nchi sifa nzuri ya ushindi.

Hayo ameyasema leo Jijini Dodoma katika halfa ya kuzipongeza timu zilizoshiriki mashindano ya Jumuiya ya Afrika Mashariki yaliyofanyika mjini Bujumbura nchini Burundi ambapo timu ya mpira wa miguu ya wanawake waliibuka washindi wa kwanza.
 “Sasa naona wachezaji  wetu mmebadili muelekeo kwa kuweka juhudi na kuhakikisha mnailetea heshima nchi yetu kwa kuja na kombe la ushindi, hiki ndio kilele cha mafanikio kwa wanamichezo” alisema Dkt. Mwakyembe.

Anazidi kueleza kuwa  Serikali itaendelea kuweka juhudi kwa timu za wanawake ambazo zimeonyesha mafanikio makubwa katika michezo kwani zimekuwa zikifanya vizuri  ambapo ndani ya muda  wa miezi miwili zimeleta makombe mawili kutoka katika mashindano ya kimataifa ikiwemo  CECAFA.

Dkt. Harrison Mwakyembe alisisitiza kuwa zama za kupeleka wachezaji kwa mazoea zimepitwa na wakati bali wachezaji watakaokuwa wakishiriki michezo ya nje ya nchi ni wale wenye juhudi na uzalendo kwa taifa lao.

 Naye Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bibi. Suzan Mlawi amezipongeza timu hizo na kueleza kuwa  Wizara imefanikiwa katika kuchagua wachezaji bora ambao wameiwakilisha vyema nchi na kuiletea heshima kubwa.

 “Haya ni mashindano ya kwanza kushiriki katika Jumuiya ya Afrika Mashariki na tumeweza kurejea na kombe tunahitaji pongezi sana, matokeo haya ya yanatokana na kupeleka timu zinazoweza kushindana”.alisema Bibi. Suzan

Awali akitoa mrejesho wa Mashindano hayo Mkuu wa msafara ambaye pia ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maendeleo ya Michezo wa Wizara hiyo Bw. Addo Komba alieleza  kuwa Tanzania imeshiriki michezo minne ambayo ni Mpira wa Miguu wanawake,mpira wa pete,riadha pamoja na karate ambapo mpira wa miguu wanawake waliibuka washindi wa kwanza.





Mashindano hayo yameshirikisha nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki ambazo ni Burundi ambao ndio walikuwa wenyeji,Tazania ,Kenya  Rwanda na Uganda.

SHIRIKA LA POSTA TANZANIA LAELEZA MATARAJIO NA MALENGO YAKE KWA MWAKA 2018/2019

$
0
0
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Elia Madulesi, akizungumza wakati akiwakaribisha waandishi wa habari katika mkutano ambao Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika, Kanali Mstaafu, Dk. Haruni Kondo, alielezea mambo mbalimbali yanayohusu matarajio na malengo ya shirika hilo, kwa mwaka 2018/2019, jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Postamasta Mkuu, Hassan Mwang'ombe na kushoto ni Kaimu Meneja Mkuu Rasilimali za Shirika Macrice Mbodo.
Baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari, wakichukua taarifa iliyokuwa ikitolewa na  Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania, Kanali Mstaafu, Dk. Haruni Kondo. 
Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania (TPC), Kanali Mstaafu, Dk. Haruni Kondo, akizungumza na waandishi wa habari, wakati alipokuwa akielezea masuala mbalimbali yanayohusu matarajio na malengo ya shirika hilo, kwa mwaka 2018/2019. Kushoto ni Postamasta Mkuu wa shirika, Hassan Mwang’ombe.  
Baadhi ya wapiga picha na waandishi wa habari, wakichukua taarifa kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta, Kanali Mstaafu, Dk. Haruni Kondo.
Baadhi ya wapiga waandishi wa habari, wakisikiliza taarifa  iliyokuwa ikitolewa na Mwenyekiti wa Bodi, Kanali Mstaafu, Dk. Haruni Kondo. 
Mwenyekiti wa Bodi, Kanali Mstaafu, Dk. Haruni Kondo (katikati), akizungumza na waandishi katika mkutano huo.  
Postamasta Mkuu, Hassan Mwang'ombe, akizungumza katika mkutano huo, wakati alipoelezea kuhusu duka la Shirika la kwenye mtandao kwamba sasa tayari linafanya kazi na kuwataka wananchi kulitumia kwa kuweka bidhaa zao ili kuweza kuuza ndani na nje ya nchi. Kulia Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika, Kanali Mstaafu, Dk. Haruni Kondo.
Maofisa wa Kitengo cha Mawasiliano cha Shirika la Posta Tanzania (TPC),wakiwa katika mkutano huo, wakimsikiliza Postamasta Mkuu wa shirika hilo, Hassan Mwang'ombe, alipokuwa akizungumza katika mkutano huo, jijini Dar es Salaam leo. 
Postamasta Mkuu, Hassan Mwang'ombe,akizungumza wakati alipokuwa akijibu maswali yaliyokuwa yakiulizwa na waandishi wa habari katika mkutano huo,jijini Dar es Salaam leo.   
Mwenyekiti wa Bodi, Kanali Mstaafu, Dk. Haruni Kondo akijibu maswali yaliyokuwa yakiulizwa na waandishi wa habari katika mkutano huo.   

TANESCO YATUMIA WIKI YA ZIMAMOTO KUTOA ELIMU DODOMA

$
0
0

 Wiki ya Zimamoti na Uokoaji inataraji kumalizika leo katika Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma ambapo wadau mbalimbali wakiongozwa na jeshi la Zima Moto na Ukoaji wameshiriki katika maonesho yaliyoenda sambamba na utoaji elimu ya majanga ya moto na uokoaji.

Shirika la Umeme Nchini TANESCo ni miongoni mwa wadau waliounga mkono maaonesgo hayo yakwanza kuanza kufanyika mwaka huu.

Tanesco imetumia maonesho hayo kutoa elimu kuhusiana na huduma zao wanazotoa lakini kubwa zaidi likiwa ni elimu ya namna ambavyo umeme unaweza kusababisha ajali ya moto na kuteketeza nyumba na majengo.

Mhandisi wa Shirika Hilo anaeshughulika na Afya na Usalama mahali pa kazi, Donart Makingi amesema kuwa yapo mambo ambayo yanaweza kusabnabisha hitilafu katika jengo au nyumba ambavyo ni pamoja na matumizi ya vifaa vya umeme visivyo na ubora, utumiaji mafundi vishoka katika unganishaji umeme, vifaa visivyo na ubora. 

Lakini pia alisema kutumia vitu kama pasi au jiko bila uangalifu na umakini navyo vinaweza kuchangia hitilafu ya umeme na baade nyumba na mali zingine kuteketea. 
Wanafunzi ni miongoni mwa watu waliopatiwa elimu katika Banda la Tanesco.
Maofisa wa Tanesco kutoka idara mbalimbali wapo uwanjani kuhudumia mamia ya wananhi wanao tembelea.
Tanesco inawakumbusha wananchi kufanya ukaguzi wa mara kwa mara wa mifumo ya umeme walau kila baada ya miaka kadhaa ili kujua kama bado ipo sahihi, 

SERIKALI KUTOTOA KAZI YA UJENZI WA BARABARA KWA MKANDARASI ASIYEKUWA NA UWEZO WA KIFEDHA

$
0
0
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe, akitoa maelekezo kwa Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS) mkoa wa Mara, Mhandisi Mlima Ngaile, wakati akikagua ujenzi wa barabara ya Bulamba-Kisorya yenye urefu wa KM 51, Wilayani Bunda, mkoani humo.

Serikali imeeleza kuwa haitatoa kazi za ujenzi wa miundombinu ya barabara hapa nchini kwa kampuni za ujenzi ambazo hazina uwezo wa kifedha wa kufanya kazi hizo. Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Kamwelwe, amesema hayo Wilayani Bunda, Mkoani Mara mara baada ya kukagua ujenzi wa barabara ya Bulamba-Kisorya yenye urefu wa KM 51 na kubaini kuwa kampuni ya ujenzi ya Nyanza Road Works kuwa na uwezo mdogo wa kifedha na hivyo kuchelewesha mradi huo.

Mhandisi Kamwelwe ameeleza changamoto nyingine iliyochelewesha mradi ni kutokana na kampuni ya Inter Consult iliyofanya usanifu wa barabara kukosea michoro ya mradi huo na hivyo kumsababishia mkandarasi kushindwa kufanya kazi yake kikamilifu.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe, (kulia) akifafanua jambo kwa Meneja wa mradi Mhandisi Antener Mehari, wakati akikagua ujenzi wa barabara ya Bulamba-Kisorya yenye urefu wa KM 51, Wilayani Bunda, Mkoani Mara.

"Aliyesanifu mradi huu hakufanya vizuri na hivyo kumsababishia mkandarasi kuongezewa muda wa kazi miezi 35 mingine kutokana na kuongezeka kwa makalvati katika barabara hiyo na ukubwa wa tuta la barabara", alifafanua Waziri Mhandisi Kamwelwe.

Waziri huyo amemtaka Mhandisi Mshauri kutoka kampuni ya DOCH na Mkandarasi kuongeza vifaa na wataalam wengine ili kuhakikisha kasi ya mradi huo inaenda kwa haraka. Aidha, Mhandisi Kamwelwe, ameiagiza Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Mara kumsimamia mkandarasi huyo ili akamilishe mradi huo ifikapo mwezi Juni mwakani badala ya mwezi Desemba 2019.

Kwa upande wake Meneja wa TANROADS, mkoa wa Mara Mhandisi Mlima Ngaile, amemuahidi Waziri Kamwelwe kuwa atamsimamia mkandarasi huyo kikamilifu na kuhakikisha mradi huo unakamilika kwa viwango.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe, (kushoto) akizungumza na Mhandisi Andrew Nantori, kutoka kampuni ya M/S Mbutu JV anayejenga barabara ya Makutano-Sanzate yenye urefu wa KM 50 baada ya kukagua barabara hiyo na kuridhishwa na kasi ya ujenzi wake, mkoani Mara.

Katika hatua nyingine Waziri Mhandisi Kamwelwe amekagua ujenzi wa barabara ya Makutano - Sanzate yenye urefu wa KM 50 na kuridhishwa na kasi ya makandarasi 10 wazawa walioungana kupitia kampuni ya M/S Mbutu JV na kuwaahidi kuwaongeza sehemu ya barabara kutoka Sanzate hadi Nata na ile ya Mugumu hadi Serengeti pindi watakapokamilisha mradi huo.

Waziri Kamwelwe ameongeza kuwa pamoja na mradi wa barabara hiyo kuwa na maeneo korofi na mawe hadi sasa mradi umefikia asilimia 69 na KM 10 tayari zimeshawekwa lami.

Naye Mkandarasi wa Kampuni hiyo Mhandisi Andrew Nantori ameishukuru Serikali kwa kuwaamini makandarasi wazawa na amemuahidi Waziri Kamwelwe kuwa hatowaangusha.

Mradi wa ujenzi wa barabara ya Bulamba-Kisorya yenye urefu wa KM 51 na barabara ya Makutano-Sanzate yenye urefu wa KM 50 inafadhiliwa na Serikali kwa asilimia 100.
Muonekano wa sehemu ya barabara ya Bulamba-Kisorya yenye urefu wa KM 51 inayojengwa kwa kiwango cha lami, wilayani Bunda, mkoani Mara.
Muonekano wa sehemu ya barabara ya Makutano-Sanzate yenye urefu wa KM 50 inayojengwa kwa kiwango cha lami ambapo ujenzi wake umefikia asilimia 69. Barabara hiyo inajengwa na makandarasi wazawa M/S Mbutu JV.

Matumizi ya ARV hupunguza maambukizi kwa mtu mwingine

$
0
0
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy Mwalimu  akiendelea na matembezi katika moja ya banda lililokuwa katika viwanja vya maji maji Songea mkoa wa Ruvuma wakati wa ufunguzi wa kampeni ya Furaha yangu Mkoa wa Ruvuma.

Na WAMJW-SONGEA,RUVUMA

Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imesema kuwa mtu akitumia ARV kwa usahihi na kikamilifu anapunguza ewezekano wa kuambukiza VVU kwa mtu mwingine  kwa takribani Asilimia 60.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, jinsia, Wazee na watoto Mhe. Ummy Mwalimu leo wakati akizindua Kampeni ya FURAHA YANGU, PIMA, JITAMBUE, ISHI katika  viwanja vya Majimaji Songea Mkoa wa Ruvuma. 

“Kwa mujibu wa Wataalamu wa Afya ikiwemo Wanasayansi imedhihirika kwamba mtu akianza mapema kutumia Dawa anapunguza uwezekano wa kupata magonjwa nyemelezi, pia anaongeza muda wa kuishi na anapunguza uwezekano wa kuwaambukiza watu wengine”  alisema Waziri Ummy Mwalimu.
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy Mwalimu aliselebuka na kikundi cha Bendi cha JKT Mlale wakati wa ufunguzi wa kampeni ya Furaha Yangu mkoa wa Ruvuma katika viwanja vya maji maji Songea.

Waziri Ummy aliendelea kusema kuwa mtu akigundulika kuwa na maambukizi ya VVU na UKIMWI ataanzishiwa dawa za kupunguza makali ya Ukimwi mara moja badala ya kusubiri hali yake kuwa mbaya zaidi. 

Waziri Ummy alisema kuwa wakati Takwimu za Kitaifa zikionesha maambukizi ya VVU yamepungua kutoka Asilimia 5.7 hadi Asilimia 4.7, bado maambukizi mapya yameendelea kuwepo, takribani vijana wenye umri kati ya miaka 15 hadi 24 sawa na Asilimia 40 wanaambukizwa VVU.

Aidha, Waziri Ummy alisema kuwa Asilimia 52 ya watu wanaoishi na maambukizi ya VVU wanajifahamu kuwa wana VVU,  katika kila watu 100 Watu 48 wenye maambukizi ya VVU hawajui kuwa wana VVU jambo ambalo ni hatari kwenye kaya zao na Taifa kwa ujumla .

Mbali ya yote Waziri Ummy aliwaagiza watoa huduma  kupitia Kampeni hiyo kwamba  watu wote wanaotumia dawa za kupunguza makali ya VVU vizuri kwa kuzingatia masharti wapewe dawa za miezi mitatu badala ya mwezi mmoja kama inavyofanywa sasa.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy Mwalimu (wapili Kushoto) akiendelea na matembezi katika viwanja vya maji maji wakati wa ufunguzi wa kampeni ya Furaha yangu mkoa wa Ruvuma.Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Bi Christina Mndeme.

“Watu wote wanaotumia Dawa vizuri kwa kuzingatia masharti, wapewe dawa za miezi mitatu badala ya kila mwezi kwenda kuchukua dawa katika vituo vya kutoa huduma za afya, tunaamini kwamba hatua hii itachochea watu wengi zaidi kwenda kupima na kujiandikisha kupata huduma za dawa” alisema Waziri Ummy.

Pia, Waziri Ummy  amewaagiza Waganga Wakuu wa mikoa nchini kuhakikisha kwamba  vituo vya Afya vyote nchi ambavyo vimesajiliwa na kutambulika na Wizara ya Afya  kutoa huduma za kupima VVU, kutoa ushauri nasaa na kutoa dawa

“Maelekezo ambayo tumetoa Serikali, hatuoni ni kwanini katika kila kituo cha Afya kisitoe huduma za kupima VVU, zakutoa Ushaurinasaa na kutoa huduma za dawa kama ameambukizwa” alisema Waziri Ummy Mwalimu.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy Mwalimu akisisitiza jambo mbele ya wananchi waliojitokeza katika viwanja vya maji maji katika kampeni ya Furaha yangu mkoa wa Ruvuma

Sambamba na hayo Waziri Ummy alisema kuwa  katika kila watoto 100 wanaozaliwa nchini Tanzania ,Watoto 11 walikuwa wanazaliwa na maambukizi ya VVU,  ndani ya mika miwili maambukizi ya VVU yamepungua kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto hadi kuwa chini ya Asilimia 5 kutoka Asilimia 11.

Aliendelea kusema kuwa  katika kila watoto 11 wanaozaliwa na VVU ni takribani watoto 5 ndio wanazaliwa na maambukizi ya VVU, inawezekana kabisa kuwa na mtoto  asilimia 0 ambae anazaliwa na maambukizi ya VVU.

Nae Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Bi. Christina Mndeme alisema kuwa kwa upande wa 909090 hali ya hali ya Mkoa wa Ruvuma takwimu zinaonesha kuwa 90 ya kwanza imefikia Asilimia 71.3 sawa na watu 41,789 wanaokadiliwa kuishi na maambukizi ya VVU imefikiwa kati ya watu wanaokadiliwa 58,534 wanaishi na VVU katika MKoa wa Ruvuma, huku 90 ya pili Asilimia 78 ambayo ni sawa na watu 41,141 ya watu waliotambuliwa hali zao za maambukizi ya VVU na tayari wamekwisha anzishiwa dawa.

Aidha, Bi. Mndeme aliendelea kusema kuwa vituo vya kutolea huduma za upimaji wa VVU vimeongezeka mkoani Ruvuma kutoka vituo 240 kwa mwaka 2016 hadi kufikia vituo 293 kufikia mwezi juni 2018, Mkoa wa Ruvuma Tayari una vituo 303, huku vituo 293 vikiwa Tayari vimekwishafikiwa.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy Mwalimu akipata huduma ya kupima maambukizi ya VVU wakati wa ufunguzi wa kampeni ya Furaha yangu katika viwanja vya maji maji Songea mkoa wa Ruvuma.
 Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Bi Christina Mndeme akipata huduma ya kupima maambukizi ya VVU wakati wa ufunguzi wa kampeni ya Furaha yangu katika viwanja vya maji maji Songea mkoa wa Ruvuma.
Picha ya pamoja ikiongonzwa na Waziri wa Afya, Mhe Ummy Mwalimu na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Bi. Christina Mndeme wakati wa ufunguzi wa kampeni ya Furaha yangu mkoa wa Ruvuma katika viwanja vya maji maji Songea.
Viewing all 39044 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>