Quantcast
Channel: MTAA KWA MTAA BLOG
Viewing all 39098 articles
Browse latest View live

KAMATI ZA BUNGE ZAISHAURI SERIKALI KUTEKELEZA MIRADI YA MAENDELEO KWA UBIA NA SEKTA BINAFSI

$
0
0
 Kamishna  wa Idara ya Ubia kati ya Sekta binafsi na  Umma, kutoka Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. John Mboya,  akizungumzia faida za miradi ya ubia kati ya Serikali na Sekta binafsi wakati wa semina kwa wajumbe wa Kamati za Kudumu za Bunge za Miundombinu, Bajeti na Kamati ya Uwekezaji Mitaji ya umma, iliyofanyika Jijini Dodoma.
 Wataalamu washauri wa masuala ya Ubia kati ya Sekta Binafsi na Sekta ya Umma (PPP) Bw. Abhijit Bhaumik (kushoto), Bw. Philip Kelly  (katikati) na Bw. Craig Sugden, wakijadiliana jambo wakati wa semina ya Kamati tatu za Bunge za Bajeti, Miundombinu na Uwekezaji Mitaji ya Umma, iliyofanyika Jijini Dodoma.
 Mkurugenzi Mkuu wa Bohari Kuu ya Dawa (MSD) Bw. Laurean Bwanakunu, akiwasilisha mada kwa wajumbe wa Kamati za Kudumu za Bunge za Miundombinu, Bajeti na Kamati ya Uwekezaji Mitaji ya Umma, ilifanyika Jijini Dodoma kuhusu hatua zilizochukuliwa na taasisi hiyo za kupanga kujenga viwanda vitatu vya dawa na vifaa tiba kwa kuishirikisha Sekta Binafsi (PPP).
 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC) Mhandisi  Kapuulya  Musomba, akiwasilisha mada kwa wajumbe wa Kamati  za Kudumu za Bunge za Miundombinu, Bajeti na Kamati ya Uwekezaji Mitaji ya Umma, Jijini Dodoma, kuhusu hatua zilizochukuliwa na Shirika hilo kutaka kuishirikisha Sekta Binafsi kutekeleza mradi mkubwa wa kuunganisha gesi majumbani katika katika mikoa ya Dar es Salaam, Lindi na Mtwara kupitia ubia kati na sekta binafsi na Umma (PPP) utakaogharimu zaidi ya shilingi bilioni 300.
 Sehemu ya wajumbe wa Kamati za Kudumu za Bunge za Miundombinu, Bajeti na ile ya Mitaji ya Umma wakifuatilia semina kuhusu dhana ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa njia ya ubia kati ya sekta binafsi na umma (PPP), Jijini Dodoma
 Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti Mhe. Mashimba Ndaki (Mb), akizungumzia matarajio ya wabunge katika utekelezaji wa miradi ya ubia kati ya Sekta ya Umma na Binafsi katika kuchochea maendeleo, wakati wa semina kwa wajumbe wa Kamati za Kudumu za Bunge za Miundombinu, Bajeti na kamati ya Uwekezaji Mitaji ya Umma, iliyofanyika Jijini Dodoma.
 Sehemu ya wajumbe wa Kamati za kudumu za Bunge za Miundombinu, Bajeti na  Uwekezaji na Mitaji ya Umma wakifuatilia semina kuhusu dhana ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa njia ya ubia kati ya sekta binafsi na umma (PPP), Jijini Dodoma.
 Mwenyekiti wa Bunge na Mbunge wa Bariadi Mhe. Andrew Chenge (kulia) na Mbunge wa Ileje Mhe. Dkt. Janeth Mbene, wakifuatilia kwa makini mada mbalimbali zilizotolewa na wataalam kutoka Benki ya Dunia kuhusu masuala ya utekelezaji wa Miradi ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi, Jijini Dodoma.

(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-WFP)

Na Benny Mwaipaja, WFM, Dodoma
WAJUMBE wa Kamati za Kudumu za Bunge za Miundombinu, Bajeti na Kamati ya Uwekezaji na Mitaji, wameishauri Serikali kutekeleza kwa vitendo miradi mikubwa na yenye tija kwa Umma kwa kutumia njia ya Ubia kati ya Umma na Sekta binafsi ili kuchochea haraka maendeleo ya nchi.

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti Mhe. Mashimba Ndaki amesema kuwa  wabunge wameridhishwa na na hatua zinazochukuliwa na Serikali katika kuhakikisha kuwa mpango wa ubia kati ya Serikali na sekta binafsi unafanikiwa na unachochea maendeleo ya wananchi.

“Kama wabunge tungependa kuona mpango unaingizwa katika mipango ya Serikali ili kuharakisha miradi ya maendeleo na pia tunapongeza hatua zilizochukuliwa na Serikali ikiwemo kumteua Kamishna anayeshughulikia miradi ya ubia kati ya sekta binafsi na ile ya umma, “ Alisisitiza Mboya

Alibainisha kuwa jukumu la Serikali ni kuhakikisha kuwa inaweka mazingira wezeshi kwa wawekezaji wote watakaojitokeza kushirikiana na Serikali katika kutekeleza miradi ya maendeleo hapa nchini.

Mwenyekiti wa Bunge ambaye pia ni Mbunge wa Bariadi Mhe. Endrew Chenge amesema kuwa nchi nyingi Duniani zimefanikiwa kuwaletea wananchi wake maendeleo kupitia utaratibu huo ambapo jambo la muhimu ni kufanywa kwa maandalizi ya kina na kuwepo kwa utashi kutasaidia kufanikiwa kwa miradi husika .

Aliongeza kuwa mwaka huu Serikali imeleta Bungeni Mswada wa Marekebisho ya Sheria ya PPP utakaojadiliwa na wabunge katika Bunge linaloanza Septemba 4 mwaka huu, pamoja na mambno mengine Muswada huo unapendekeza kuanzishwa kwa Kituo cha PPP chini ya Wizara ya Fedha na Mipango, ambacho kitakuwa na jukumu la kuishauri Serikali kuhusu masuala yanayo husu miradi mbalimbali itakayowasilishwa kwa mfumo wa Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi

Akizungumza katika Semina hiyo, Kamishna  wa Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi, Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. John Mboya amesema kuwa Dhamira ya Serikali ni kuhakikisha kuwa inaweka mazingira wezeshi katika kutekeleza miradi ya ubia na Sekta binafsi ili kuleta mageuzi katika maisha ya wananchi.

“Lengo la kuwa na miradi ya ubia kati ya Serikali na sekta binafsi ni kutekelezaIilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM), kutekeleza mpango wa maendeleo na hatimaye kutoa huduma bora kwa wananchi,” Alisisitiza Mboya

Akifafanua Mboya amesema kuwa moja ya hatua za maboresho zilizochukuliwa na Serikali ni kuhamisha Kituo cha kusimamia miradi ya ubia katika ya Umma na Sekta binafsi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu kuja Wizara ya Fedha.

Akizungumzia majukumu ya chombo cha kusimamia utekelezaji wa miradi hiyo Dkt. Mboya  amesema kuwa chombo hicho kimepewa jukumu la kufanya uchambuzi wa kina kuhusu miradi yenye sifa na kusimamia mchakato wa uteklezaji wa mpango huo kwa kufuata ngazi zote zilizopo hadi utekelezaji wa mradi husika.

Aliongeza kuwa ili kufanikisha mpango huo Serikali inasisistiza uwazi, uwajibikaji na utayari hali itakayo sababisha  kufikiwa kwa malengo ya miradi ya ubia kati ya sekta hizo mbili ambapo alitaja baadhi ya miradi itakayotekelezwa ambayo upembuzi yakinifu umekamilika kuwa ni ile ya ujenzi wa Viwanda vya dawa, usambazaji wa gesi majumbani katika Jiji la Dar es Salaam, Mtwara , Lindi na ule wa uendeshaji wa mabasi ya mwendo kasi Jijini Dar es Salaam ambao umeanza na uko katika hatua mbalimbali za uendelezwaji.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Bohari Kuu ya Dawa (MSD) Bw. Laurean Bwanakunu amesema kuwa tayari Bohari hiyo imekamilisha upembuzi yakinifu wa mradi wa ujenzi wa viwanda vya dawa na vifaa tiba vinavyotokana na malighafi zinazozalishwa hapa nchini ikiwemo pamba na kufikia machi mwakani zabuni ya mradi huo itatangazwa ili kuwapata wabia.

Katika kutekeleza mradi huo kiwanda cha kuzalisha maji ya dripu yanayotumika kwa wagonjwa mahosipitalini pia kitajengwa ambapo kwa sasa maji hayo yanaagizwa kutoka nchini Uganda na kwamba hatua hiyo itapunguza gharama za Serikali za kuagiza dawa na vifaa hivyo kutoka nje ya nchi ambapo zaidi ya shilingi trilioni 1.8  hutumika kuagiza bidhaa hizo kila mwaka.

Kwa upande wake. Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC) Mhandisi  Kapuulya  Musomba amesema kuwa mradi wa kusambaza gesi majumbani katika Jiji la Dar es Salaam, Mtwara na Lindi unaotarajiwa kuhgaribu zaidi ya shilingi bilioni 300, utaleta mageuzi kwa wananchi wa mikoa hiyo ambapo wananchi zaidi ya 120,000 katika Jiji la Dar es Salaam watafikiwa.

Aliongeza  kuwa katika mikoa ya Lindi na Mtwara wananchi zaidi ya 5,000 wataunganishiwa gesi majumbani mwao huku viwanda zaidi 30 katika maeneo ya mradi vitaunganishiwa huduma hiyo pamoja na vituo vya kujaza gesi kwenye magari yanayotumia nishati hiyo.

Semina kwa wabunge wa Kamati za Bajeti, Miundombinu na ile ya Uwekezaji Mitaji imefanyika Jijini Dodoma ikiwashirikisha wajumbe wa Kamati hizo ili kuwajengea uwezo wa namna dhana hiyo inavyoweza kuleta maendeleo hapa nchini.

TAA YATOA MSADA KUUNGA MKONO JUHUDI ZA WABUNGE WANAWAKE KUJENGA VYOO VYA SHULE NCHI NZIMA

$
0
0
  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) Bw. Richard Mayongela (wakwanza kulia) akiwaongoza wafanyakazi wa Mamlaka hiyo, Mkurugenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa chas Julius Nyerere (JNIA) Bw. Paul Rwegasha (watatu kulia) na Afisa Uhusiano Bi. Bahati Mollel (wapili kulia) kukabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya Shilingi Milioni 5 (5,000,000/=) kwa mgeni rasmi kwenye hafla ya bunge kuchangisha fedha kwa ajili ya ujenzi wa vyoo vya shule nchi nzima, Spika mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Anne Makinda (wapili kushoto) na Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya hafla hiyo, Mbunge wa Muleba Kusini, Profesa Anna Tibaijuka. Hafla hiyo ilifanyika usiku wa kuamkia leo Septemba 1, 2018 jijini Dar es Salaam.

  NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
MAMLAKA ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) imeunga mkono juhudi za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kupitia Umoja wa Wabunge Wanawake wa Bunge hilo, (TWPG) kukusanya fedha kwa ajili ya kujenga vyoo salama vya shule nchi nzima kwa mtoto wa Kike kwa kutoa mchango wa kiasi cha Shilingi Milioni Tano (5,000,000).
Katika hafla ya kuchangisha fedha kwa dhumuni hilo, iliyofanyika katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa TAA, Bw. Richard Mayongela, alikabidhi msaada huo wa fedha kwa mgeni rasmi, Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Anne Makinda.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa (TWPG), ambaye pia ni Mbunge wa Urambo, Mhe.Margareth S. Sitta, wazo la kutafuta fedha za ujenzi wa vyoo hivyo ni katika jitihada za kuhakikisha wanafunzi wote hususan wa kike, wanafurahia haki yao ya msingi ya kupata elimu katika mazingira rafiki na masafi bila kujali changamoto zinazosababishwa na tofauti zao za kimaumbile.
Akizungumza kwenye hafla hiyo iliyohudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Wabunge, Wakuu wa Taasisi za Umma na Binafsi, Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai, aliwapongeza Wabunge hao kwa hatua hiyo ya kuhakikisha kunakuwepo kwa  mazingira bora shuleni ili kutoa haki sawa ya kupata elimu kwa wanafunzi wote.
“Wazo hili litasaidia sana serikali katika kuhakikisha mazingira ya shule yanaboreshwa ili kutoa nafasi sawa kwa wanafunzi wote wa kike na kiume” alibainisha Spika Ndugai.
Alisema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, amefurahishwa sana na kitendo hicho na kwamba ameshindwa kuhudhuria hafla hiyo kwa vile bado yuko kwenye msiba wa dada yake huko Chato Mkoani Geita. 
Kwa upande wake, mgeni rasmi Mhe. Anne Makinda aliwapongeza wabunge hao wanawake kwa hatua hiyo ya kuunga mkono juhudi za serikali na kuwataka Wabunge wanaume kuwaunga mkono wenzao katika kufanikisha kampeni hiyo inayolenga kukusanya kiasi cha shilingi bilioni 3.5 zitakazowezesha kujenga vyoo vya shule kwenye majimbo yote 264 nchi nzima.
Taasisi mbalimbali zilichangia kwenye harambee hiyo.

 Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Job Ndugai, akizunhgumza.
 Mwenyekiti wa Kundi la Wabunge Wanawake wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Urambo, Mhe. Margareth S. Sitta, akitoa hotuba yake.
 Mgeni rasmi kwenye hafla ya bunge kuchangisha fedha kwa ajili ya ujenzi wa vyoo vya shule nchi nzima, Spika mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Anne Makinda, akitoa nasaha zake.
 Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya hafla hiyo, Mbunge wa Muleba Kusini, Profesa Anna Tibaijuka, akitoa nasaha zake.
 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) Bw. Richard Mayongela, akifuatilia kilichokuwa kikizungumzwa na viongozi.
 Mkurugenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Julius Nyerere (JNIA), Bw. Paul Rwegasha akifurahia jambo.
 Viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama wakifuatilia hafla hiyo.
 Meza ya wafanyakazi wa Idara ya Uhamiaji nchini.
 Spika Ndugai akiongoza wabunge wengine kusakata rhumba
 Mbunge wa Viti Maalum ambaye pia ni msanii wa muziki, Mhe. Martha Mlata akiimba kwenye hafla hiyo.
 Wabunge wa Viti Maalum wakisakata rhumba.
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai, akiongozana na Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson wakati wakiingia ukumbini.
Mbunge wa Chalinze, Mhe. Ridhiwani Kiwkete akiwa na Mbunge wa jimbo la Segerea, Mhe. Bonner Kalua

WATANZANIA WAISHIO NJE WATAKIWA KUSHAWISHI WAWEKEZAJI-MAJALIWA

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewatakaWatanzania waishio nje ya nchi wahakikishe wanashiriki kikamilifu kujenga uchumi wa nchi yao kwa kushawishi wawekezaji wenye mitaji mikubwa waje kuwekeza nchini na kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo Tanzania.

Amesema Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais, Dkt. John Magufuli inaamini kuwa Tanzania itapata maendeleo makubwa ya kiuchumi endapo wananchi wake watatekeleza kwa vitendo kaulimbiu ya “Hapa Kazi tu”.

Aliyasema hayo jana jioni (Jumapili, Septemba 02 ,2018) wakatiakizungumza na Watanzania waishio nchini China kwenye ofisi za Ubalozi wa Tanzani uliopo jijini Beijing. 

Alisema nchi zote zilizoendelea zilihakikisha kuwa wananchi wake wanaelewa na kutekeleza matamko yanayowahamasisha kufanya kazi, hivyo alitumia fursa hiyo kuwahamasisha Watanzania popote walipo kutekeleza kwa vitendo kaulimbiu ya ‘Hapa Kazi Tu.’

Waziri Mkuu alisema China ambayo imefanikiwa kuwa moja kati ya nchi zenye nguvu kubwa ya kiuchumi duniani, imefika hapo kutokana na mchango mkubwa uliotolewa na wananchi wake, ambao waliamua kuunga mkono juhudi za Serikali yao kwa kufanya kazi kwa bidii na weledi wakiwa ndani au nje ya nchi. 

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu aliwataka Watanzania waishio nje ya nchi wajiepushe na vitendo vya uhalifu hasa biashara ya dawa za kulevya ambayo inachafua jina na heshima ya nchi yao kimataifa. “Tanzania ni nchi nzuri na inaheshimika duniani, nawasihi wote mnaoishi nje muachane kabisa na biashara haramu ya dawa za kulevya kwa sababu inalitia doa Taifa na adhabu yake katika baadhi ya nchi ni kifo,” alisisitiza Waziri Mkuu.

Awali, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Dkt. Augustine Mahiga alisema mwelekeo wa Diplomasia ya Tanzania Kimataifa hivi sasa ni kiuchumi (economic diplomacy), hivyo Watanzania waishio nje wanapaswa kuwa wabunifu, makini katika kutafuta fursa zenye manufaa kwa nchi yao.

Alisema Diplomasia ya Uchimi si kupeleka Tanzania wawekezaji tu bali wawekezaji katika viwanda ambavyo kila vinapojengwa vinachangia kuinua uchumi wa Taifa.Kwa upande wake,Balozi wa Tanzania nchini China, Mbelwa Kairuki aliwaasa vijana kuitumia teknolojia ya mawasiliano na mitando ya jamii kutafuta habari na taarifa muhimu hasa nafasi za masomo ili kujiendeleza kielimu.

LUGHA YA KISWAHILI CHANGAMOTO YA UTABIBU WILAYANI KYERWA MKOANI KAGERA

$
0
0
 Mganga Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa, Dkt. Diocles Ngaiza, akizungumza na waandishi wa habari kuhusu upatikaji wa dawa kutoka Bohari ya Dawa (MSD), mkoani humo mwishoni mwa wiki. Kulia ni Mfamasia wa wilaya hiyo,  Dominic Malabeja. 
 Wauguzi wa Zahanati ya Kaisho iliyopo wilayani Kyerwa mkoani Kagera, wakisaidia kubeba maboksi yenye  dawa baada ya kupelekewa na Bohari ya Dawa (MSD) wilayani humo mwishoni mwa wiki. Kutoka kulia ni Devotha Maganga, Editha Nyaruzi na Yolanda Joseph.

 Jengo la Zahanati ya Kata ya Kaisho.
 Taswira ya moja ya Jengo la Kituo cha Afya cha Murongo wilayani Kyerwa.
 Afisa Huduma kwa Wateja wa Bohari ya Dawa (MSD), Cornelia Mwillawi (kushoto), akimuonesha fomu maalumu ya kujaza baada ya kukabidhiwa dawa Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya cha Murongo, Dkt.Rashid Eid (kulia), baada ya kukabidhiwa dawa mwishoni mwa wiki. Katikati ni Tabibu wa kituo hicho, Denis Rugemalira.
Tabibu wa kituo hicho, Denis Rugemalira (kulia), akijadiliana jambo na Afisa Huduma kwa Wateja wa Bohari ya Dawa (MSD), Cornelia Mwillawi baada ya kukabidhi dawa katika kituo hicho.

Na Dotto Mwaibale, Kyerwa Kagera

KUTOKUFAHAMU Lugha ya Kiswahili imekuwa ni changamoto kubwa ya upatikanaji wa matibabu katika Kituo cha Afya cha Murongo kilichopo mpakani mwa Tanzania na Uganda wilayani Kyerwa mkoani Kagera.

Hayo yalielezwa na Mganga Mfawidhi wa kituo hicho, Dkt. Rashid Eid, mwishoni mwa wiki wakati akizungumza na waandishi wa habari ambao walikuwepo mkoani Kagera kuangalia taratibu za usambazaji dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara kwenye vituo vya kutolea huduma za afya mkoani Kagera zinazofanywa na Bohari ya Dawa (MSD)

"Changamoto kubwa tuliyonayo ni wagonjwa wetu tunaowapatia matibabu katika hiki kituo chetu cha afya cha Murongo kutojua lugha ya kiswahili hivyo ulazimika kutumia lugha ya alama kuweza kuelewana kama vile kama mgonjwa anaumwa kichwa basi atashika kichwa na kama tumbo vilevile atashika tumbo" alisema Dkt. Eid.

Alisema katika eneo hilo kunamuingiliano mkubwa wa watu kutokana na kuoleana kwani kuna Waganda waliooa Tanzania na Watanzania waliooa Uganda na kuwa kwa pande zote hizo mbili wananchi wake hawajui kuzungumza kiswahili zaidi ya makabila yao ya Kiganda, Kinyankole, Kihaya na Kinyambo.

Aliongeza kuwa kutokana na hali hiyo kuna wakati hulazimika kuwaita wafanyakazi wa kituo hicho wanao elewa kiswahili kutafsiri lugha wakati wanapozungumza na mgonjwa  ambaye hajui kiswahili ili kubaini ugonjwa wake.

Akizungumzia upatikanaji wa dawa kutoka MSD alisema zinapatikana kwa wakati na kuwa pamoja na kituo hicho kuwepo na muingiliano huo wa watu kutoka nchi jirani ya Uganda hawana ubaguzi wa kutoa huduma kwao.

"Kituo chetu kinatoa huduma kwa watu wote bila ya ubaguzi na hatujawahi kupungukiwa dawa kwa vile tunapo agiza dawa tunakuwa na idadi ya pande zote mbili na kuongeza za ziada jambo ambalo limsaidia tusiwe tunapungukiwa kwa dawa zote muhimu" alisema Dkt.Eid.

Alisema katika kituo hicho cha afya kwenye mwezi wa sita wagonjwa wanaotibiwa ni kati ya 50 hadi 80 kwa siku lakini kwa hivi sasa ni wagonjwa kuanzia 20 hadi 40 ingawa hakufafanua kwanini idadi hiyo inapungua katika kipindi hicho.

Mganga Mkuu wa wilaya hiyo, Dkt. Diocles Ngaiza alisema upatikana wa dawa katika wilaya hiyo kutoka MSD ni mzuri ukilinganisha na miaka 2015 ambapo walikuwa wakipata asilimia 30 lakini sasa hivi ni zaidi ya 70.

Katika ziara hiyo wilayani Kyerwa MSD ilikabidhi dawa katika Kituo cha Afya cha Murongo na Zahanati ya Kaisho.

MTENDAJI MKUU TFS ATOA NENO KWA WASHIRIKI MISS TANZANIA 2018

$
0
0
*Awataka wawe mabalozi kuhimiza uhifadhi wa misitu,utalii wa ndani
 Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
WAREMBO wa Shindano la Miss Tanzania 2018 wametajwa kuwa mabalozi wazuri wa Vivutio vya Utalii nchini ikiwemo Rasilimali za Misitu na Nyuki pamoja na Maporoko.

Akizungumza na Warembo hao jijini Dar es Salaam wakati anawaaga wakielekea katika hifadhi ya Amani mkoani Tanga, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu nchini (TFS), Profesa Dos Santos Silayo amewataka walimbwende hao kutumia weledi, uwezo Kitaaluma na nafasi katika jamii kusaidia uhifadhi wa misitu.

Prof. Silayo amewataka warembo hao kutangaza Misitu hiyo mazuri yake ili iweze kutumika kutoa huduma za kiutalii na kuonesha thamani yake iliyosimama.

Amesema uhifadhi wa misitu unaifaida nyingi na moja ya faida misitu ni cha chanzo uhifadhi wa maji na kuongeza pamoja na hewa safi.

Amesema kuwa TFS itatumia sehemu ya washiriki hao wa Miss Tanzania mwaka huu kwa ajili ya kuwa malozi ambao watashiriki kikamilifu kuhimiza uhifadhi misitu.

Amefafanua watawajengea uwezo katika kuhakikisha wanaifanya kazi hiyo kwa weledi mkubwa na zaidi kuna maeneo mengi ya misitu ambayo imehifadhiwa ambayo inahitaji mabalozi wa kutangazwa.

"TFS pamoja na wadau wengine wakiwamo wa utalii nchini ambao wapo Wizara ya Maliasili na Utalii tumeamua kushirikiana na  ya Miss Tanzania kuhakikisha washiriki watano wa Miss Tanzania tunawatumia kuutangaza vivutio vya utalii na uhifadhi misitu,"amefafanua Profesa Silayo.

Amesema katika kuhakikisha wanakuwa mabalozi wazuri warembo hao watatembelea baadhi ua misitu iliyohifadhiwa ukiwamo hiyo hifadhi ya msitu Amani.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Kampuni ya The Look, Basilla Mwanukuzi amesema kuwa lengo la ushiriki wa taasisi za utalii katika Shindano hilo la Ulimbwende ni kukuza utalii wa ndani.

Mwanukuzi ameeleza kuwa taasisi za utalii zimeunga mkono kuhakikisha Utalii unatangazwa na hivyo washiriki watano kati ya 20 waliopo kwenye shindano hilo watapata fursa ya kuwa mabalozi wa utalii na uhifadhi wa misitu.


Mwanukuzi amesema kutakuwa na mabalozi watano katika Shindano hilo la Miss Tanzania 2018 wamegawanyika katika sehemu tano.

Ametaja kutakuwa na Miss Domestic Tourism, Miss Ruaha, Balozi TANAPA), Miss Ngorongoro, Miss Seleu(Tanzania World Life Authority) na  Miss Equal Tourism chini ya Forest Services.

Kuhusu shindano la Miss Tanzania ,Mwanakuzi amesema wameshusha bei ya kiingilio ili kutoa fursa ya watanzania wengi kushuhudia.

Ametaja viingilio hivyo ni kwamba  VVIP 70,000, VIP 50,000 na kawaida 30,000.

Amesema lengo la mashindano hayo si kupata faida bali kuhakikisha jukwaa hilo linatoa fursa kwa watoto wa kike kuwa daraja katika kutimiza ndoto zao kwani anaamini baada ya mashindano hayo watashiriki kufanya kazi za kijamii kwa uaminifu na uadilifu mkubwa.
 Washiriki wa Miss Tanzania mwaka 2018 wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza safari ya kuelekea Msitu Amani mkoani Tanga.
 Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS) Profesa Dos Santos Silayo(wa pili kulia)akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa Miss Tanzania mwaka 2018 baada ya kuzungumza nao kuhusu umuhimu wa warembo hao kuutangaza uhifadhi wa misitu na utalii nchini
 Muandaji wa Mashindano ya Miss Tanzania mwaka 2018 Basila ambaye pia amewahi kuwa Miss Tanzania mwaka 1998 akiwa na Mtendaji Mkuu wa TFS Profesa Dos Sontos Silayo wakati wakizungumza na washiriki wa mashindano hayo jijini Dar es Salaam
 Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS) Profesa Dos Santos Silayo(wa pili kushoto)akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mashindano ya Miss Tanzania mwaka 2018 kutoka Kanda ya Ziwa ambao pia ni mabalozi wa kuyatangaza  maporomoko ya Karambo
 Washiriki wa Miss Tanzania mwaka 2018 wakiwaaga viongozi kutoka taasisi mbalimbali za utalii pamoja na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS) kabla ya kuanza kwasafari ya kuelekea katika Hifadhi ya Amani mkoani Tanga.

TANZANIA YAPATA MWAKILISHI WA HESHIMA HONG KONG NA MACAO

$
0
0
Balozi wa Tanzania nchini China, Mhe. Mbelwa Kairuki kwa pamoja na Bibi Annie Suk-Ching Wu wakisaini Mkataba kumwezesha Bibi Wu kuwa Mwakilishi wa Heshima wa Tanzania huko Hong Kong na Macao. Tukio hilo lilifanyika kwenye Ubalozi wa Tanzania jijini Beijing, China na kushuhudiwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Adolf Mkenda pamoja viongozi wengine ambao wapo nchini China kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya Afrika na China (FOCAC).
Balozi Mbelwa na Bibi Wu wakibadilishana mkataba mara baada ya kuusaini
Mhe. Waziri Mahiga akitoa hotuba kumpongeza Bibi Wu kwa kukubali kuiwakilisha Tanzania kwenye maeneo hayo na kumtaka kuiwakilisha vema nchi
Mhe. Waziri na viongozi wengine wakisubiri kuanza kwa ratiba
Mhe. Waziri Mahiga akiwa katika picha ya pamoja na Mhe. Balozi Mbelwa na Bibi Wu mara baada ya kushuhudia uwekwaji saini wa mkataba wa kumwezesha Bibi Wu kuiwakilisha Tanzania Hong Kong na Macao
Picha ya pamoja na viongozi na wageni mbalimbali waliohudhuria hafla hiyo
Katibu Mkuu, Prof. Mkenda akiteta jambo na Mhe. Balozi Mbelwa
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia, Bibi Justa Nyange akiwa na Maafisa ambao walikuwepo kushuhudia uwekwaji saini wa mkataba wa kumwezesha Bibi Wu kuwa Mwakilishi wa Heshima kwenye majimbo ya Hong Kong na Macao ya nchini China

TAWLA yaanzisha kampeni ya kuandika wosia kwa wamasai na wameru

$
0
0
 Wananchi wa kata ya Olmotonyi wakiwasikiliz Mafisa sheria wa chama cha wanawasheria wanawake (Tawla), Neema Ahmed, na Aika Palangyo katika kampeni kuhusu suala la uandishi wa wosia.
 Wananchi wa kata ya Olmotonyi wakimsikiliz afisa sheria wa chama cha wanawasheria wanawake (Tawla), Neema Ahmed ( hayupo pichani), akiwahamasisha kuhusu suala la uandishi wa wosia.
Mwanasheria wa Tawla Aika Palangyo aliwaeleza wakazi wa kata ya Olmotonyi namna wosia unavyoandikwa.

Seif Mangwangi, Arusha
CHAMA cha wanasheria wanawake (Tawla), kimeanza kampeni ya kuhamasisha Jamii ya kabila la  maasai na wameru kuandika wosia kabla ya kufariki dunia kufuatia kuwepo kwa matukio mengi ya unyanyasaji baada ya mmoja katika familia kufariki.

Akizungumza jana katika kampeni hiyo iliyofanyika kwa wananchi wa vijiji vya ngaramtoni, emaoi na olmotonyi katika kata ya olmotonyi wilayani Arumeru, Afisa sheria kutoka Tawla, Neema Ahmed alisema ofisi yao imekuwa ikipokea matukio mengi ya wanawake kunyanyaswa baada ya waume zao kufariki.

Alisema wajane katika familia nyingi za jamii ya kimaasai na kimeru wamekuwa mafukara kutokana na kunyang’anywa mali na mashemeji mara baada ya waume zao kufariki dunia bila kuacha maandishi yanaayoonyesha urithi wa mali.

“Lakini cha kushangaza hizi mali zinazogombewa unakuta ulizitafuta na mme wako lakini inapotokea ukafariki dunia wanaibuka mashemeji na hata wakati mwingine wakwe wanawanyang’anya, sasa kama kutakuwa na wosia hakuna atakaeweza kuingilia mali za marehemu, “ alisema.

Neema alisema mila nyingi za jamii hizo zimekuwa zikikandamiza haki za wanawake lakini suluhisho la mila hizo ni wosia ambao hueleza warithi halali wa mali za marehemu baada ya kufariki na kuepusha migogoro.

Hata hivyo aliwaeleza wakazi hao kuwa ni muhimu kuwashirikisha wanasheria wakati wa kuandika wosia kwa kuwa wosia ni siri ya mtu  ili kuwa shahidi wakati kifo kinapotokea na kuepusha migogoro isiyokuwa ya lazima.

Kwa upande wake Afisa mtendaji wa kata ya Olmotonyi, Judica Elisha Lukumay alisema mafunzo kuhusiana na uandishi wa wosia ni muhimu sana kwa jamii hiyo kwa kuwaa wanawake wamekuwa wakinyanyasika sana.
Alisema jamii ya kimaasai na wameru wamekuwa na uelewa mdogo kuhusiana na uandishi wa wosia jambo ambalo limekuwa likisababisha wanawake na watoto kunyanyasika baada ya Baba kufariki katika familia.

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini afanya mabadiliko kwa baadhi ya makamanda wa Polisi.


WAZIRI MKUU MAJALIWA ASHIRIKI MKUTANO WA JUKWAA LA USHIRIKIANO KATI YA CHINA NA AFRIKA ULIOANZA JIJINI BEIJING

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Xi Jinping katika Mkutano wa Jukwaa la Ushirikiano Kati ya China na Afrika uliofunguliwa na Rais huyo kwenye ukumbi wa Great Hall of the People uliopo Beijing, Septemba 3, 2018. Mheshimwa Majaliwa amemwakilisha Rais, Dkt. John Pombe Magufuli katika mkutano huo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Wakuu wa Afrika na China baada ya Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Xi Jinping kufungua Mkutano wa Jukwaa la Ushirikiano Kati ya Tanzania na China Kwenye ukumbi wa Mikutano wa Great Hall of the People uliopo Beijing, Septemba 3, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

MAADHIMISHO YA WAHANDISI TANZANIA KUFANYIKA AGOSTI 5-7, UKUMBI WA DIAMOND JUBILEE

$
0
0
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Maadhimisho ya Siku ya Wahandisi Tanzania, Mhandisi Ngwisa Mpembe akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusiana naMaadhimisho ya Siku ya Wahandisi hapa nchini Bodi ya Usajili Wahandisi nchini.
 Kaimu Msajili toka Bodi ya Usajili Wahandisi (ERB), Mhandisi Patrick Barozi (kulia) akionesha kwa waandishi wa habari picha za wahandisi waliokuwepo kipindi cha uongozi wa Mwalimu Julius Nyerere mwaka 1968 wakati akizungumza na waandishi wa habari jiji Dar es Salaam leo.
  Kaimu Msajili toka Bodi ya Usajili Wahandisi (ERB), Mhandisi Patrick Barozi (kulia) akionesha kwa waandishi wa habari hati iliyosainiwa na Baba wa Taifa, Mwl. Julius Nyerere mwaka 1968 ili kuanzishwa kwa bodi hiyo, kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Maadhimisho ya Siku ya Wahandisi Tanzania, Mhandisi Ngwisa Mpembe.
Msajili Msaidizi wa Bodi ya usajili wa Wahandisi (Kushoto) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.
Picha na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.

BODI ya usajili ya wahandisi kuadhimisha miaka 50 tangu kuanzishwa kwake pia wahandisi wataalam watakula kiapo cha utii, Maadhimisho hayo  yatafanyika katika ukumbi wa DiamonJubilee jijini Dar es Salaam kuanzia Agosti 5 hadi 7.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Mhandisi Ngwisa Mpembe amesema kuwa Jumuiya ya wahandisi nchini, taasisi na mashirika ya kihandisi, jamii ya wafanyabiashara pamoja na jamii kwa ujumla kuwa siku ya wahandisi Tanzania itaadhimishwa Agosti 5-7.


"Siku ya wahandisi ni siku pekee kwa wahandisi wa Tanzania kuweza kuonyesha yale wanayoweza kufanya kwa maendeleo ya taifa". Amesema Mhandisi Mpembe.

Amesema kuwa  maadhimisho hayo shughuli mbalimbali zitafanyika kama majadiliano ya kitaaluma, kiapo cha wahandisinwatalaam, maonyesho mbalimbali ya kiufundi na biashara, kutoa tuzo kwa wahandisi na waliosaidia uhandisi ndani ya miaka 50, kutambua na kuzawadia na kuwatambua wahitimu waliofanya vizuri zaidi katika mitihani yao ya mwaka wa mwisho wa masomo 2017/2018.

Maadhimisho ya siku ya wahandisi Tanzania 2018 inafanyika kila mwaka na mwaka huu ni mwaka wa sita tangu kuanzishwa kwake.

Kamati ya Bunge yawataka wananchi kuacha kukwamisha miradi ya maendeleo

$
0
0
 Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani akiongoza mkutano wa Wadau wanaohusika katika  utekelezaji wa mradi wa kuzalisha umeme katika maporomoko ya maji ya Bonde la Mto Rufiji,uliofanyika mkoani Njombe.
 Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Ussi Pondeza ( katikati), Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu( kushoto) na Kaimu Kamishna wa Umeme na Nishati Mbadala, Mhandisi Innocent Luoga (kulia) wakifuatilia mada wakati wa mkutano wa wadau wanaohusika na  utekelezaji wa mradi wa kuzalisha umeme katika maporomoko ya maji bonde la mto Rufiji, uliofanyika mkoani Njombe.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (wa nne kulia) na Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu ( katikati mbele) wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Wizara, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini na viongozi mbalimbali kutoka mkoa wa Njombe walioshiriki mkutano wa wadau wa utekelezaji mradi wa kuzalisha umeme katika maporomoko ya maji ya bonde la mto Rufiji, uliofanyika mkoani Njombe.Kamati ya Bunge yawataka wananchi kuacha kukwamisha miradi ya maendeleo 
Na Zuena Msuya Njombe,

KAMPUNI ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, imewataka wananchi kuwa wazalendo na kujali maslahi ya nchi na taifa katika kutekeleza miradi ya mikubwa ya maendeleo ukiwemo mradi kuzalisha umeme wa maji wa megawati 2100 katika maporomoko ya bonde la Mto Rufiji. 

Kauli hiyo imetolewa na Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Ussi Pondeza, mkoani Njombe wakati wa mkutano wa Wadau wa mradi wa kuzalisha umeme wa maji katika maporomoko ya bonde la mto Rufiji.

Pondeza alisema kuwa,  Watanzania wengi wamekuwa na tabia ya kupenda kuangalia maslahi yao binafsi kwa kutaka malipo makubwa ama fidia zinazoweza kuepukwa  pindi Serikali inapoanzisha miradi mikubwa ya maendeleo bila kujali kuwa miradi hiyo ni kwa manufaa ya Watanzania wote.

Alitoa angalizo kuwa,  tabia hiyo imekuwa ikichelewesha utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo  na hata wakati mwingine kukwamisha utekelezaji wake. 

"Baadhi yetu sisi watanzania sijui tuna tabia gani, tunaletewa mradi kwa maendeleo yetu wenyewe lakini kwa vile ni wabinafsi tunaanza kukwamisha kwa kutaka fidia ili mradi mtu upate fedha! unasahau kuwa hizo ni juhudi za Serikali katika kutuletea maendeleo sisi wenyewe,” alisema Pondeza.

Aliongeza kuwa,  kuna baadhi ya watu wakikosa huduma fulani huilalamikia Serikali kuwa haijafanya kitu hali ya kuwa wao ndio walikuwa wakizuia utekelezaji hivyo aliwataka wabadilike.

Kwa upande wake,  Waziri wa Nishati,  Dkt. Medard Kalemani alisema katika kuelekea uchumi wa viwanda nchi inahitaji umeme mwingi, wa uhakika, gharama nafuu na unaotabirika.

Aliongeza, kuwa kwa sasa nchi ina umeme wa kutosha lakini hauwezi kutosheleza mahitaji ya miaka ijayo katika kujenga uchumi wa viwanda. 

Alifafanua kuwa,  ili kutimiza adhma  ya Serikali ya uchumi wa Viwanda, sasa ni wakati muafaka wa kutekeleza miradi mikubwa ya nishati ya umeme ukiwemo wa kuzalisha umeme wa maji kwa  maporomoko ya mto Rufiji (Rufiji Hydropower Project).

Aliweka wazi kuwa,  umeme unaozalishwa kwa kutumia nguvu za maji huwa ni wa gharama nafuu na hudumu kwa miaka mingi.

Aidha, Dkt. Kalemani aliongeza kuwa,  Tanzania ina maji ambayo yanaweza kuzalisha umeme wa  zaidi ya MW 4700 ambayo bado hayajaanza kutumika.
Vilevile alisema kuwa, Serikali itaendelea kuzalisha umeme kupitia vyanzo vingine ikiwemo Makaa ya Mawe, Gesi asilia, Joto ardhi, Upepo na Jua. 

Kwa upande wake,  Mbunge wa Tunduma, Frank Mwakajoka alisema kuwa Wabunge watashirikiana na Serikali katika  kutoa elimu sahihi kwa wananchi ili waweze kuuelewa vyema  mradi huo kwa lengo la kuharakisha utekelezaji wake. 

Vile vile alitoa wito kuwa, Serikali iangalie utaratibu wa kuunda vikundi maalum vitakavyokuwa na jukumu la kulinda vyanzo maji ili kudhibiti uharibifu unaofanywa na baadhi ya watu katika vyanzo hivyo.                          

Wanahabari wafundwa juu ya mlipuko wa ugonjwa wa Ebola Nchini

$
0
0
Waandishi wa Habari wametakiwa kushirikiana na Serikali katika kuihabarisha jamii ili kuepukana na janga hatari la ugonjwa wa Ebola.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu  ameyabainisha hayo wakati wa kufungua mafunzo maalum kwa waandishi wa namna ya kutoa taarifa za ugonjwa huo wa Ebola.
Jamii imetakiwa kujua dalili za ugonjwa huo wa Ebola kwa kina kwani kupitia Wanahabari,mafunzo hayo yatasaidia sana kutoa elimu na itaenea maeneo mengi.

“Ugonjwa huu wa Ebola kiukweli ni ugonjwa hatari. Na tokea kutokea katika nchi za wenzetu umesababisha madhara makubwa sana ikiwemo Uchumi ikiwemo masuala ya biashara na uwekezaji.

Imebainishwa kuwa madhara ya kiuchumi juu ya Ebola yangeuwa watu wengi zaidi kuliko ugonjwa wenyewe. Sisi tulikuwa na wasiwasi sana ndio maana tulienda wenyewe huko kufuatilia..mimi nilienda mipakani Rusumo na Mganga Mkuu yeye alienda mipaka ya Ngala na maeneo mengine.” Amesema Waziri Ummy Mwalimu.

Na kuongeza kuwa, tatizo kubwa ni suala la wasafiri wanaopita njia za panya kwani zimekuwa zikiwapa changamoto na wameomba Kamati za Ulinzi na Usalama kuhakikisha wanalinda maeneo hayo.

Lakini nataka kukiri kwa kweli baadhi ya mipaka hali sio nzuri. wameweka tenti pekee bila mahitaji mengine ikiwemo sehemu za Choo. kiukweli tumejiandaa ila kuna maeneo tunahitaji kuyaboresha” alifafanua Waziri Ummy Mwalimu.

Hata Waziri amebainisha kuwa, wamejipanga na wanaendelea kuona njia bora zaidi mara kwa mara ambapo wameomba Wanahabari kushirikiana na Wizara kupata taarifa na uelewa zaidi.

“Ndugu wanahabari kupitia semina hii itaongeza uelewa wa ugonjwa wa Ebola. Nimefurahi sana Wanahabari na wachora vibonzo wameanza kutoa taarifa na kuchora vibonzo juu ya ebola.

Nimalizie kwa kusema tena ..Hadi saa hakuna mgonjwa yeyote aliyehisiwa au kuthibitishwa kuwa na Virusi 
vya Ebola hapa Nchini. Hata hivyo kutokana na ukweli kwamba kuna mwingiliano mkubwa wa wananchi kati ya nchi hizi mbili na ugonjwa huu kugunduliwa kwenye jimbo la Kivu Kaskazini ambalo linapakana na nchi ya 
Uganda ni ukweli unaotuweka kwenye hali ya wasiwasi mkubwa” Alimalizia Waziri Ummy Mwalimu.

Waziri pia aliwashukuru Shirika la Afya (WHO) kwa kuweza kuisaidia mapambano dhidi ya Ebola kwa kuwezesha fedha za manunuzi ya madawa na kutoa elimu.

Kwa upande wake Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Dkt. Adiele Onyeze amebainisha kuwa wataendelea kushirikiana na Tanzania katika kuzuia milipuko ya magonjwa mbalimbali ikiwemo  ugonjwa huo wa Ebola ambao umekuwa ukiripotiwa mara kwa mara katika nchi za Afrika.

“Dunia kwa sasa ipo katika mapambano ya kuzuia milipuko ya magonjwa. Sisi WHO tumejipanga kusaidia juhudi za Mataifa yote yenye hatari hivyo tutasaidia kutoa elimu na uwelewa kwa Wananchi wote” alieleza Dkt. Adiele Onyeze.
 Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,Mhe. Ummy Mwalimu akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar as Salaam wakati wa Semina jinsi  ya kurepot Kuhusu ugonjwa wa Ebola na namna ya kuzuia usiingie nchini.(Picha na Emmanuel Massaka Globu ya jamii)

 Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Dkt. Adiele Onyeze Akizungumza na waandishi wa habari kuhusukushirikiana na Tanzania katika kuzuia milipuko ya magonjwa mbalimbali ikiwemo  ugonjwa huo wa Ebola ambao umekuwa ukiripotiwa mara kwa mara katika nchi za Afrika leo katika mkutano uliofanyika jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya waandishi wa habari Washiriki wakifuatilia semina hiyo juu ya uelewa wa ugonjwa Ebola

Picha ya pamoja

RAIS DKT. MAGUFULI ASHUHUDIA UTIAJI SAINI MIKATABA YA UJENZI WA MELI MPYA, CHELEZO, UKARABATI WA MELI YA MV VICTORIA NA MV BUTIAMA RAIS DKT. MAGUFULI ASHUHUDIA UTIAJI SAINI MIKATABA YA UJENZI WA MELI MPYA, CHELEZO, UKARABATI WA MELI YA MV VICTORIA NA MV BUTIAMA

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akishuhudia zoezi la utiaji saini Mikataba mbalimbali ikiwemo Ujenzi wa Meli mpya ya abiria na mizigo, Chelezo, ukarabati wa Meli za Mv Victoria na Mv Butiama, Mikataba ambayo ilisainiwa kati ya Kampuni ya Huduma za Meli Tanzania Marine Services Company (MSCL) na Kampuni tatu za Korea Kusini ambazo ni M/S STX engine Co ltd, Saekyung Construction ltd na KTMI Co ltd.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi katika Bandari ya Mwanza Kusini mara baada ya kushudia utiaji saini wa Mikataba mbalimbali ikiwemo Ujenzi wa Meli mpya ya abiria na mizigo, Chelezo, ukarabati wa Meli za Mv Victoria na Mv Butiama, Mikataba ambayo ilisainiwa kati ya Kampuni ya Huduma za Meli Tanzania Marine Services Company (MSCL) na Kampuni tatu za Korea Kusini ambazo ni M/S STX engine Co ltd, Saekyung Construction ltd na KTMI Co ltd.
 Mfano wa Meli mpya itakayojengwa ambayo Mkataba wake umesainiwa. Meli hiyo itakuwa na Urefu wa Mita 90, Kimo mita 10, uwezo wa kubeba abiria 1200 magari madogo 20, mizigo tani 400 na itakuwa ikisafiri kwa muda wa masaa sita tu kutoka Mwanza mpaka mkoa wa Kagera.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Balozi wa Korea Kusini hapa nchini Song Geum Yong watatu kutoka kushoto waliokaa,Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella wakwanza kulia waliokaa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Isaack Kamwelwe watatu kutoka kulia pamoja na wabunge mbalimbali wa mikoa ya Kanda ya ziwa.

MANONGA QUEENS YAILAZA SINGIDA WORRIER MECHI YA KIRAFIKI

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Blogu ya Jamii
TIMU ya Wanawake ya Mkoani Tabora katika jimbo la Manonga maarufu kama Manonga Queens wameichapa timu ya Singida Worrier bao 2-0 kwenye mechi ya kirafiki iliyochezwa kwenye uwanja Namfua Mkoani Singida.

Manonga Queens walianza kuchungulia nyavu za Singida Worrier mnamo dakika ya 32 na waliandika bao la kwanza kupitia Ashura Shaabani.

Katika kipindi cha pili Singida Worrier walipata pigo la pili baada ya Ashura Shaban kwa mara nyingine kuifungia timu yake bao la pili mnamo dakika ya 85, na matokeo hayo yalidumu hadi dakika 90 zilipokamilika na Manonga Queens kutoa kifua mbele dhidi ya wwnyeji wao Singida Worrier.

Akizungumza baada ya mtanange huo kocha wa Manonga Queens Khamis Abihud amesema kuwa licha ya mchezo huo kuwa mgumu wachezaji walijituma na kuibuka na ushindi huo mnono ukiwa ugenini na ameeleza kuwa wamejizatiti katika kufuzu ligi kuu daraja la kwanza.

Ashura Shaban ambaye aliipatia timu yake mabao 2 ameeleza kuwa mazoezi, maagizo ya mwalimu na ushirikiano kutoka kwa wadau hasa Mbunge wa Manonga Seif Gulamali unazidi kuwapa ari na kasi zaidi ya kujituma katika soka.
Mbunge wa Manonga Seif Gulamali(katikati) akikabidhi mipira kwa viongozi na wachezaji wa Manonga Queens timu ya jimboni hapo ambayo inashiriki mpira ligi daraja la kwanza kwa wanawake.

NIPE FAGIO NA WADAU WA MAZINGIRA WAFANYA USAFI COCO BEACH IKIWA MAANDALIZI YA SIKU YA MAZINGIRA DUNIANI SEPT 15, 2018

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Nipe Fagio, Bi, Ana Rocha (Kushoto) akimkabidhi fagio Meya wa Jiji la Dar es salaam Mh. Isaya Mwita (Kulia) katika tukio lililofanyika ufukwe wa Coco Dar es salaam ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Siku ya Usafi Duniani itakayofanyika tarehe 15 Septemba 2018 kupitia kampeni ya Let’s Do It Tanzania. Picha na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.
Meya wa Jiji la Dar es salaam Mh. Isaya Mwita  akiongea na wakazi wa jiji la Dar es Salaam waliojitokeza katika usafi wa mazingira katika ufukwe wa Coco Dar es salaam ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Siku ya Usafi Duniani itakayofanyika tarehe 15 Septemba 2018 kupitia kampeni ya Let’s Do It Tanzania. Pembeni ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Nipe Fagio, Bi, Ana Rocha (Kushoto)
Wakazi wa jiji la Dar es Salaam waliojitokeza katika usafi wa mazingira katika ufukwe wa Coco Dar es salaam ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Siku ya Usafi Duniani itakayofanyika tarehe 15 Septemba 2018 kupitia kampeni ya Let’s Do It Tanzania.
Meya wa Jiji la Dar es salaam Mh. Isaya Mwita (Kushoto), Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Nipe Fagio, Bi, Ana Rocha na Naibu Balozi wa Sweden ambae pia Mkuu wa ushirikiano na maendeleo Mh. Ulf Kallstig wakifanya usafi katika tukio lililofanyika ufukwe wa Coco Dar es salaam ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Siku ya Usafi Duniani itakayofanyika tarehe 15 Septemba 2018 kupitia kampeni ya Let’s Do It Tanzania.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Nipe Fagio, Bi, Ana Rocha akiongea na waandishi wa habari.
Takataka zilizokusanywa na wadau mbalimbali wa Mazingira katika tukio lililofanyika ufukwe wa Coco Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Siku ya Usafi Duniani itakayofanyika tarehe 15 Septemba 2018 kupitia kampeni ya Let’s Do It Tanzania.
Moja ya nyuma iliyojengwa kwa machupa ya plastiki ambayo ni kituo cha mazingira kilichopo Coco Beach jijini Dar es Salaam.

MAKONGORO NYERERE AWATAKA WAKAZI WA ZAVARA KUMCHAGUA WAITARA

$
0
0
 Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Makongoro Nyerere akizungumza wakati w akumuombea kura na kumnadio mgombea ubungo wa jimbo la Ukonga kupitia CCM Mwita Waitara katika kata ya Buyuni Viwanja vya Zavara

Mgombea Ubunge wa Jimbo la Ukonga Kupitia Chama Cha Mapinduzi Mwita Waitara akizungumza na wakazi wa kata ya Buyuni wakati wa Mkutano wake kampeni wa kuomba kura kwa wakazi wa Mtaa wa Zavara.
 Kada Mpya wa Chama Cha Mapinduz na aliyekuw akatibu wa Chadema Moshi Vijijini ,Emmanuel Mlaki akieleza kilichomtoa Chadema na kurudi CCM
 Aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi wa Chama Cha Wananchi CUF , Julius Mtatiro akiwaomba wakazi wa Zavara kumchagua Waitara kwani ndio mtu sahii kwa ajili ya kutatua kero zao
 Mbunge Viti Maalum Kutoka Zanzibara Angelina Malembeka akipiga magoti kumuombea kura Mwita Waitara kura kwa wakazi wa kata ya Buyuni Mtaa wa Zavara.
 Wabunge wa Bunge Jamhuri la Muungano kwa Tiketi ya CCM Wakicheza kwa furaha wakati wa mkutano wa kampeni


Wakazi wa Mtaa wa zavara waliojitokeza katika Mkutano wa kampeni kumsikiliza Mwita Waitara

MAKAMU WA RAIS ZANZIABAR AWAASA UONGOZI WA KARAKANA YA SERIKALI KUANDAA MAPENDEKEZO

$
0
0
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Kushoto akiangalia baadhi ya vitengo vya Karakana Kuu ya Serikali iliyopo Chumbuni alipofanya ziara ya ghafla kwenye Taasisi hiyo ya Uhandisi.
 Balozi Seif akionyesha mshangao wake kutokana na  baadhi ya Mashine  nzima kutofanya kazi kutokana na ukosefu wa Wahandisi wa kuziendesha kwa sababu za kustaafu na wengine kufariki Dunia.
 Kaimu Mkuu wa Karakana ya Serikali Ndugu Yussuf  Kulia Masururu akimkaguza sehemu mbali mbali balozi Seif kujionea hali halisi ya Mazingira ya Karakana hiyo. Wa kwanza kutoka Kushoto ni Naibu Waziri Wizara ya Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mheshimiwa Mihayo Juma N’hunga.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Kushoto akiangalia baadhi ya vitengo vya Karakana Kuu ya Serikali iliyopo Chumbuni alipofanya ziara ya ghafla kwenye Taasisi hiyo ya Uhandisi.Aliyepo Kulia ni Kaimu Mkuu wa Karakana ya Serikali Ndugu Yussuf  Masururu na nyuma ya Balozi Seif ni Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji Mh. Mohamed Ahmed Salum.

MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ameukumbusha Uongozi wa Karakana Kuu ya Serikali kuandaa mapendekezo yatakayotoa mwanga wa kuifufua Karakana hiyo ili itoe huduma imara zilizokusudiwa kutokana na uwepo wa azma ya kujengwa kwake.

Alisema mapendekezo hayo ambayo tayari alikwisha yaagiza kwa Uongozi huo kufuatia ziara yake aliyoifanya kwenye Karakana hiyo karibu Miaka Mitano iliyopita ni vyema yakaainisha vyema mpango Mkuu wa muda mfupi wa kati na mrefu.

Balozi Seif Ali Iddi alitoa kumbusho hilo wakati alipofanya ziara ya ghafla katika Karakana hiyo iliyopo Chumbuni kuangalia uhalisia  wa mazingira halisi ya uwajibikaji wa Watendaji wake na changamoto zinazowakabili katika utendaji wao wa kazi wa kila siku.

Alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar iliamua kwa makusudi kuanzisha mradi huo wa Karakana ya Serikali ili kujaribu kusimamia huduma za matengenezo kwa Vyombo vya Moto kama Gari na Ringi Mbili vya Taasisi za Umma na hata zile binafsi.

Balozi Seif alieleza kwamba hatua hiyo ilikuwa na azma ya kuokoa fedha nyingi za Serikali zinazopotea kutokana na mfumo wa utengenezaji wa vyombo vyake kufanywa na Mkampuni au Watu Binafsi Mitaani.

Alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar  itafikiria kuchukua hatua stahiki za kuona Karaka hiyo inaendelea kutoa huduma kama kawaida baada ya kupata ufafanuzi wa kutosha wa ripoti au mapendekezo yatakayotolewa na Wahandisi hao.

“ Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar iliamua kuifufua Karakana  yake  ili Taasisi za Serikali ziache tabia ya vyombo vyao vya Moto kutengenezwa Vichochoroni mfumo unaoigharimu fedha nyingi Serikali Kuu”. Alisema Balozi Seif.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwapongeza Wafanyakazi na Uongozi wa Karakana Kuu ya Serikali kwa jitihada zao za kufanya kazi katika mazingira magumu ya ukosefu wa baadhi ya zana muhimu za Kisasa za kutendea kazi.

Alisema Dunia ya sasa inaendelea kushuhudia Maendeleo makubwa ya Teknolojia Ulimwenguni yanayopaswa kwenda sambamba na uwajibikaji wa Watendaji wa Karakana hiyo.

Mapema  Balozi Seif  akikaguzwa sehemu mbali mbali za Karakana hiyo ambapo Kaimu Mkuu wa Karakana ya Serikali  Ndugu Yussuf  Masururu ameishauri Serikali wakati inapoagiza vyombo vya Moto kama Magari kuushauri Uongozi wa Karakana hiyo ili utoe baraka kwa vyombo vinavyostahiki kununuliwa kwa mujibu wa zana za matengenezo zilizopo.

Nd. Yussuf alisema zipo changamoto zinazowakuta Wahandisi wa Karakana hiyo hasa pale wanapopokea baadhi ya Magari ya Serikali ambayo vipuri vyake  kwa mujibu wa muundo wa Gari hizo huwa havipatikani Nchini jambo ambalo chombo hicho hubaki kuchakaa au matengenzo yake kuchuukuwa gharama kubwa endapo kifaa kinachohitajika italazimika kukiagiza nje ya nchi.

Kaimu Mkuu wa Karakana hiyo ya Serikali alimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba utoaji wao wa huduma hivi sasa unategemea Wahandisi wa Karakana kuwasiliana na  muhusika wa Gari lililopelekekwa kufanyiwa matengenezo kulazimika kununua kwa Kampuni na Taasisi binafsi nje ya Karakana hiyo.

Hata hivyo ndugu Yussuf  alifahamisha kwamba zipo baadhi ya Mashine zinashindwa kufanya kazi kwa vile Wataalamu waliokuwa wakizihudumia kumaliza muda wao wa Utumishi nawengine  kufariki Dunia.

Akitoa shukrani zake Naibu Waziri Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji Zanzibar Mh. Mohamed Ahmed Salum  alisema Wizara hiyo hivi sasa iko katika hatua za mwisho za kufanya upembuzi wa mapendekezo ya uimarishaji wa Karakana ya Serikali.

Mh. Mohamed alisema Wizara hiyo imekusudia kuweka mikakati itakayoweka misingi imara ya kuimarisha Karakana hiyo  ili gari zote za Serikali zirejee kupatiwa huduma za matengenezo kama kawaida.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
03/09/2018. 

PROF.MKUMBO AWATAKA WANASHERIA KUSIMAMIA SHERIA WANAZOZIWEKA

$
0
0
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Profesa Kitila Mkumbo akizungumza na wanasheria wa Sekta ya Maji (hawamo pichani), Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Sheria wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Simon Nkanyemka (kulia) na Mwenyekiti wa kikao hicho, Bernadetha Mkandya kutoka DAWASA.
 Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Sheria wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Simon Nkanyemka akizungumza, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Profesa Kitila Mkumbo (katikati) na Mwenyekiti wa Kikao hicho, Bernadetha Mkandya kutoka DAWASA.
 Baadhi ya washiriki wa mkutano wa wanasheria wa Sekta ya Maji.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Profesa Kitila Mkumbo akiwa pamoja na washiriki wote wa mkutano wa wanasheria wa Sekta ya Maji.

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Profesa Kitila Mkumbo amewataka wanasheria wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji pamoja na taasisi zake kuhakikisha wanasimamia sheria wanazoziweka, ili kuepusha migogoro ambayo inaweza kuisababishia Serikali hasara na kukwamisha maendeleo ya Sekta ya Maji.

Profesa Mkumbo amezungumza hayo katika mkutano uliowakutanisha wanasheria 36 kati ya 41 kutoka taasisi mbalimbali zilizo chini ya Wizara ya Maji na Umwagiliaji, pamoja na wanasheria wa wizara hiyo uliofanyika jijini Dodoma; lengo la mkutano huo likiwa ni kuboresha utendaji wa wanasheria katika Sekta ya Maji katika Ukumbi wa Chuo cha Mipango, jijini Dodoma.

Amesema kama washauri na wasimamizi wa sheria katika Sekta ya Maji waendelee kusimamia vyema sheria, taratibu na miongozo inayotolewa na Serikali na kutekeleza majukumu yao kwa weledi, uadilifu na ufanisi; kuzingatia kanuni za maadili na utendaji kazi wa wanasheria. 

Wakihakikisha kuwa wanaifahamu vizuri sekta na vipaumbele vyake na kuvitekeleza; wakitoa ushauri pasipo woga pamoja na kuongeza ujuzi katika utendaji wao wa kazi.

 ‘‘Nichukue fursa hii kuwapongeza kwa kazi nzuri mnayoifanya katika sekta yetu, mmekuwa mkitatua migogoro mingi ya kisheria na kuisaidia Serikali katika mambo mengi ya msingi’’, alisema Profesa Mkumbo.

‘‘Jambo la msingi ni kuhakikisha mnasimamia misingi ya sheria mnazoziweka ili kuisaidia Serikali kuepukana na hasara na migogoro ambayo itakwamisha maendeleo ya Sekta ya Maji, huku mkifanya kazi yenu kwa weledi na uadilifu’’, alisisitiza Profesa Mkumbo.

Awali, Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Sheria wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Simon Nkanyemka akizungumza kwenye mkutano huo, amesema lengo lake ni kufahamiana; kujifunza; kubadilishana uzoefu; changamoto wanazokumbana nazo na mbinu za kuzitatua, na kujenga ushirikiano ili kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yao kiutendaji.

Nkanyemka alisema kuna haja ya wanasheria kupata mafunzo ya ziada mbali na taaluma yao ya sheria; ikiwemo mafunzo ya ununuzi na utumishi ili kuwa na weledi zaidi wa kutatua migogoro ya kisheria inayohusisha maeneo hayo katika utendaji wao wa kazi, ambapo mara nyingi wanahusishwa mara baada ya matatizo kutokea.

Aidha, mkutano huo umefanikiwa kukusanya maoni yatakayosaidia kuboresha mapendekezo ya kutungwa kwa Sheria Mpya ya Huduma za Maji na Usafi wa Mazingira ya mwaka 2018, ambayo inalenga kuboresha mfumo wa kitaasisi wa usimamizi wa utoaji wa huduma za maji na usafi wa mazingira ili kuongeza kasi na ufanisi katika utoaji wa huduma za maji nchini.

Lengo la sheria hiyo itayotekelezeka ni kukidhi mahitaji, ambayo itakuwa ni kichocheo cha kuhakikisha kwamba jamii inapata huduma bora ya maji na endelevu kwa vizazi vya sasa na vijavyo na kuimarisha utawala bora wa maji.

KONDO ATUHUMIWA KUMUUA MKEWE KISA KUCHAT NA SIMU-RPC WANKYO

$
0
0
NA MWAMVUA MWINYI,PWANI
JESHI la polisi Mkoani Pwani ,limefanikiwa kumkamata Salum Mzee Kondo (38),fundi ujenzi mkazi waKidongoChekundu ,Bagamoyo aliyehusika na tukio la mauaji ya mkewe Mwajuma Omary (27) kisha kutoroka baada ya kutenda kosa hilo.

Mtuhumiwa huyo amekamatwa septemba 2 mwaka huu ,Yombo Buza jijini Dar es salaam ambako alikimbilia baada ya kufanya kitendo hicho Agosti 31 2018, saa 9 alasiri huko Kidongochekundu.

Akiweka bayana kuhusiana na tukio hilo kwa waandishi wa habari ,kamanda wa polisi mkoani Pwani (ACP) Wankyo Nyigesa alisema, mtuhumiwa alipokamatwa alikiri kutenda kosa hilo ,na kudai alichukua hatua hiyo kutokana na wivu wa kimapenzi .

Alieleza kwamba , mkewe alikuwa akichat na simu huku akiwa anacheka mwenyewe ndipo alipoamua kumnyang'anya simu na kukuta message alizokuwa akichat na mwanaume mwingine .

"Jambo hilo lilisababisha mgogoro kati yao ,ambao ulisuluhishwa na mwenyekiti wa kitongoji cha Magomeni B, lakini marehemu alishikilia kuchoshwa kuishi na mumewe huyo na kuomba kupewa talaka na mumewe aligoma kutoa talaka " alifafanua Nyigesa .

Pamoja na hilo ,Nyigesa alisema wawili hao walikuwa na mgogoro mwingine, uliotokana na mtuhumiwa kuchukua ATM Card ya marehemu mkewe na kwenda kutoa sh.50,000 bila ridhaa yake.

Alibainisha ,jambo hilo lilimsababisha marehemu mkewe kuondoka nyumbani wanakoishi na kwenda kuishi kwa baba yake mdogo.

Kamanda huyo alieleza ,ilipofika tarehe 31 agost mwaka huu alimpigia simu mumewe kuhitaji fedha zake hizo ambapo mumewe alimwambia aende nyumbani kwao akachukue na mkewe huyo (marehemu)aliendelea kushikilia kutaka fedha zake na talaka ndipo mtuhumiwa kwa hasira alimkaba na kumsababisha kifo .

Baada ya kutenda kosa hilo mtuhumiwa alimfunika marehemu kwa shuka ndani ya chumba walichokuwa wakiishi na kuacha ujumbe kuwa ameua kutokana na wivu wa kimapenzi .

Kwa mujibu wa Nyigesa ,Ujumbe huo uliendelea kueleza ,mtuhumiwa nae anaenda kujiua hivyo mali zote walizoacha ni za watoto wawili waliozaa na marehemu .

Mradi wa umeme wa Makambako - Songea wakamilika

$
0
0
 Zaidi ya shilingi bilioni 9.1 za mafuta mazito kuokolewa.
Na Zuena Msuya, Njombe
Waziri wa Nishati,  Dkt. Medard Kalemani, amesema kuwa mradi wa njia ya kusafirisha umeme ya kV220  kutoka Mji mdogo wa Makambako mkoani Njombe hadi Songea mkoani Ruvuma umekamilika na utazinduliwa muda wowote kuanzia sasa.

Dkt. Kalemani alisema hayo wakati alipofanya ziara ya kukagua mradi huo katika Mji Mdogo wa Makambako mkoani Njombe, ambapo aliambatana na Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt Hamisi Mwinyimvua na watendaji wengine kutoka Wizara ya Nishati na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO). 

Dkt. Kalemani alisema kuwa, kukamilika kwa mradi huo kutaokoa zaidi ya shilingi bilioni 9.1 zilizokuwa zikitumika kila mwaka kwa kununua mafuta mazito yaliyokuwa yakitumika kuzalisha umeme katika Mikoa ya Njombe, Ruvuma na Wilaya 8 zilizokuwa hazina umeme wa Gridi ya Taifa.

“ Kukamilika kwa mradi huu ambao ulianza mwaka 2016, kutaondoa adha na gharama ya kutumia mafuta mazito katika kuzalisha umeme kwa maeneo yaliyokosa umeme wa gridi ya taifa kwa miaka mingi ukiwemo Mkoa wa Ruvuma,”  alisema Dkt. Kalemani.

Alisema kuwa, mashine tano zilizokuwa zikitumia mafuta mazito kuzalisha umeme zitazimwa, ili maeneo yaliyokuwa yakitegemea umeme huo wa mafuta mazito yaunganishwe katika gridi ya taifa.
Alitaja maeneo yatakayounganishwa na gridi ya taifa kuwa ni pamoja na Mbinga, Madaba, Namtumbo, Njombe, Songea pamoja na Ludewa.

Dkt. Kalemani aliwataka wakandarasi wanaosambaza umeme katika maeneo yaliyopitiwa na mradi huo, kuharakisha uunganishaji wa wateja kwani tayari kuna umeme wa kutosha baada ya mradi huo kukamilika.

Aliwataka wakandarasi hao kuunganisha walau Vijiji vitatu kwa wiki ili kuendana na adhma ya Serikali ya kuunganisha vijiji vyote na huduma ya umeme ifikapo 2021.

Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, pamoja na kupongeza utekelezaji wa mradi huo, alimtaka Mkandarasi anayesambaza umeme katika Vijiji 122 katika mradi huo ambaye ni kampuni ya Isolux, kuhakikisha kuwa naye anakamilisha kazi aliyopewa ndani ya wakati aliopewa.

Kwa upande wake, Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Ally Kasinge ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Wanging’ombe, aliahidi kuwa viongozi wa Mkoa huo watasimamia ipasavyo utekelezaji wa mradi huo ili kuhakikisha kuwa wananchi wanapata huduma ya umeme kwa haraka.
 Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (katikati), akizungumza na mkandarasi anayejenga miundombinu ya kusambaza umeme  kwa wananchi kupitia mradi wa Makambako hadi Songea, (kushoto) ni Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu.
 Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (katikati) akikagua mradi wa njia ya kusambaza umeme kutoka Makambako hadi Songea.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani( katikati) akipata maelezo kutoka kwa Mkandarasi anayetekeleza mradi wa njia  ya kusambaza umeme kutoka Makambako hadi Songea, wakati akikagua utekelezaji wa mradi huo ambao tayari umekamilika.
Viewing all 39098 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>