Quantcast
Channel: MTAA KWA MTAA BLOG
Viewing all 39112 articles
Browse latest View live

TUNAHITAJI WAWEKEZAJI KWENYE MAZAO YA KILIMO, SAMAKI NA MIFUGO-MAJALIWA

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Tanzania inahitaji wawekezaji wakubwa kutoka China ambao watawekeza kwenye viwanda vya mazao ya kilimo, samaki na mifugo.

Aliyasema hayo jana (Jumatatu, Septemba 03 ,2018) wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Kilimo wa China, Bw. Han Changfu, jijini Beijing.

Alisema  katika kipindi hiki ambacho Tanzania imeamua kukuza uchumi wake kupitia sekta ya viwanda, China ni nchi sahihi kushirikiana nayo kwa sababu inawawekezaji wa kutosha.

“China ni rafiki yetu na pia imepiga hatua kubwa kwenye teknolojia ya viwanda, hivyo tunahitaji kuendelea kushirikiana nayo ili tuweze kupata na teknolojia sahihi ya viwanda mbalimbali.”

Waziri Mkuu alisema Serikali zote mbili ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ziko tayari wakati wowote kuwapokea wawekezaji kutoka China.

Alisema wawekezaji hao watapatiwa ardhi ya kujenga  viwanda ambavyo vitatumia mazao ya kilimo, mifugo na bahari hasa samaki  ambayo mengi yanapatikana kwa wingi nchini.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu alisema Tanzania inahitaji kupata soko la mbaazi na soya nchini China ili kuwawezesha wakulima wake kuwa na soko la uhakika la mazao hayo.

Alisema Tanzania hivi sasa inakabiliwa  na tatizo la ukosefu wa soko la mazao hayo, baada ya wakulima kuitikia wito wa Serikali  wa kuwataka walime mazao hayo kwa ajili chakula na biashara.

“Tumelazimika kutafuta masoko ya mazao hayo hapa China ili kutowakatisha tamaa wakulima wetu kwani itakuwa vigumu kwao kuendelea kulima mazao hayo kwa wingi bila ya kuwa na uhakika wa soko.”

Kwa upande wake, Waziri wa Kilimo wa China alisema nchi yake iko tayari kutoa elimu na mafunzo kwa Watanzania hasa kwa kuandaa semina zitakazowawezesha washiriki kuongeza ujuzi wao, hatua ambayo itawasaidia Maafisa Ugani wetu kufanya kazi zao vizuri zaidi.
Katika mazungumzo hayo, Tanzania na China  zimesaini hati ya makubaliano ya  ushirikiano katika maeneo ya uvuvi, ambapo Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi wa Zanzibar, Bw. Rashidi Ali Juma alitia saini kwa upanda wa Tanzania na China iliwakilishwa na Naibu Waziri wa Kilimo, Eudong  Yu .
MapemaWaziri Mkuu alikutana na kufanya mazungumzo na Naibu Gavana wa Jimbo la Jiangsu, Bw. Guo  Yuan Qiang ambaye aliahidi kuwa jimbo lake litaendelea kushirikiana na Tanzania katika sekta za elimu na afya. 
Gavana Qiang aliishukuru Tanzania kwa kuyawezesha makampuni kutoka jimbo  hilo ambayo yamejenga viwanda nchini na kufanya  shughuli zao kwa amani na usalama. 
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMANNE, SEPTEMBA 04, 2018.

UTPC:WAANDISHI SIYO MAADUI BALI NI WADAU WA MAENDELEO

$
0
0
 Rais wa Klabu za waandishi wa habari nchini Deogratius Nsokolo akizungumza katika mkutano wa UTPC unaofanyika Jijini Arusha katika ukumbu wa Lush Garden. Picha na Vero Ignatus.
 Mkurugenzi wa idara ya Maendeleo ubalozi wa Sweden Ulf Kallsting
 Mkuu wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro akizungumza na viongozi wa Klabu za waandishi wa habari kutoka mikoa tofauti hapa nchini. Picha na Vero Ignatus.
Afisa program, Mafunzo, Utafiti na Uchapishaji kutoka UTPC Victor Maleko akizungumza na viongizi wa Klabu za waandishi wa habari kwenye mkutano mkuu uliofanyika Mkoani Arusha.
 Mkurugenzi wa UTPC Abubakari Karsan akiwa na Mkuu wa idara ya Maendeleo ubalozi wa Sweden Na. Vero Ignatus. Arusha

RAIS wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania Deogratius Nsokolo ameiomba serikali kuwaangalia waandishi wa habari kwa jicho la tofauti ili kuwalinda kwa kuwa tasnia hiyo sio adui bali ni wadau muhimu wa maendeleo ya Nchi.

Amesema hayo katika ufunguzi wa mkutano mkuu wa wanachama wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania unaofanyika Jiini Arusha,ambapo amesema ndani ya miaka miwili waandishi 57 wamepata matatizo ya kupigwa,kuumizwa na kunyang'anywa vifaa vya kazi na baadhi kupote jambo ambalo linaleta woga katika utendaji kazi.

Nsokolo amesema hawawezi kutupia lawama kwa serikali kwa sababu hawajafanya uchunguzi wa kutosha,bali wanaomba kulindwa ili waweze kuchangia maendeleo kupitia kalamu zao.

''Napenda ifahamike pote kuwa waandishi wa habari sio maadui bali ni wadau muhimu wa maendeleo hivyo vema kushirikiana na sio kuonana maadui,"alisema

Aidha amemshauri Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Magufuli kuangalia aina ya viongozi anaowateua kutokana na hivi karibu kujitokeza hadharani baadhi ya kiongozi mmoja kutoa kauli tata kwa mwandishi wa habari aliyepigwa uwanja wa mpira Dar es Salaam.

"Ni wazi tukio hilo la kulaaniwa na halipaswi kufumbiwa macho tunaomba wahusika wachukuliwe hatua maana tunafahamu kabla ya kuingia uwanjani kuna kukaguliwa hivyo huwezi kuingia mtu na silaha,"alisema

Pia alisema katika mkutano huo iliohudhuriwa na wajumbe 81 toka Klabu 28 Tanzania Bara na Visiwani watatoa Tuzo ya tatu ya Daudi Mwangosi kama ishara ya kuonyesha waandishi hawako salama.

"Lakini tunaomba wafadhili wetu SIDA waangalie jinsi ya kusaidia Klabu ya Dodoma na tutapeleka andiko maalum ili wajengewe ofisi zenye hadhi kulingana na hali ilivyo sasa na kuwapatia mafunzo wanahabari ili wafahamu jinsi ya kuandika habari za viongozi mbalimbali wanaotembelea Dodoma,"alisema

Naye Mkuu wa Idara ya ushirikiano wa Balozi wa Sweden Tanzania (SIDA) Ulf Kastig alipongeza Klabu ya Arusha na Morogoro kubuni miradi kwa ajili ya kujiongezea kipato kwa ushirikiano na wadau wa mikoa yao.

Aliwakumbusha wanahabari kuhakikisha wanaandika habari za utafiti ili kuepuka kuleta shida katika nchi.

"Lakini ili Klabu zenu ziendelee kuwa na vyanzo vingi vya mapato vema mkaongeza idadi ya wanachama,"alisema

Alipongeza ushirikiano mzuri uliopo kati ya Klabu za wanahabari na UTPC na kusema jambo la kuigwa kwani linajenga Demokrasia ya kweli.

Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Jerry Muro aliwaasa wanahabari kuzingatia maadili ya kazi zao licha ya kukabiliana na changamoto nyingi ikiwemo ukosefu wa ajira.

Amesema Wilaya yake inakabiliwa na changamoto kubwa ya migogoro ya ardhi ambayo sehemu kubwa inasabishwa na ukosefu wa uelewa wa sheria ya umiliki ardhi na baadhi ya wanasiasa kuitumia kujipatia kura.

"Mimi sitakubali kabisa kuachia wanasiasa wajinufaishe na migogoro hii lazima nibadilishe badala ya ardhi kuwalaana bali iwe baraka hasa Halmashauri ya Meru, na hili nimeanza kuzungumza na viongozi wadini tusaidiane kulimaliza," Picha na Vero Ignatus.

Kutoka katikati ni Rais wa RAIS wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania Deogratius Nsokolo, kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ubalozi wa Sweden Ulf Kallsting, wakwanza kushoto ni Kaimu mwenyekiti wa wa umoja wa Klabu za waandishi wa habari nchini Jane Mihanji. Picha na Vero Ignatus.
 Wa kwanza kulia ni Mwenyekiti wa Arusha Press Klab Cloud Ngwandu,akiwa na Katibu wa Chama cha waandishi wa habari mkoa wa Arusha Mustafa Leu katika mkutano mkuu UTPC.

Na. Vero Ignatus. Arusha. 

RAIS wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania Deogratius Nsokolo ameiomba serikali  kuwaangalia waandishi wa habari kwa jicho la tofauti ili kuwalinda kwa kuwa tasnia hiyo sio adui bali ni wadau muhimu wa maendeleo ya Nchi. 

Amesema hayo  katika ufunguzi wa mkutano mkuu wa wanachama wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania unaofanyika Jiini Arusha,ambapo amesema ndani ya miaka miwili waandishi  57 wamepata matatizo ya kupigwa,kuumizwa na kunyang'anywa vifaa vya kazi na baadhi kupote jambo ambalo linaleta woga katika utendaji kazi.

Nsokolo amesema hawawezi kutupia lawama kwa serikali kwa sababu hawajafanya uchunguzi wa kutosha,bali wanaomba kulindwa ili waweze kuchangia maendeleo kupitia kalamu zao.

''Napenda ifahamike pote kuwa waandishi wa habari sio maadui bali ni wadau muhimu wa maendeleo hivyo vema kushirikiana na sio kuonana maadui,"alisema

Aidha amemshauri Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Magufuli kuangalia aina ya viongozi anaowateua kutokana na hivi karibu kujitokeza hadharani baadhi ya kiongozi mmoja kutoa kauli tata kwa mwandishi wa habari aliyepigwa uwanja wa mpira Dar es Salaam.

"Ni wazi tukio hilo la kulaaniwa na halipaswi kufumbiwa macho tunaomba wahusika wachukuliwe hatua maana tunafahamu kabla ya kuingia uwanjani kuna kukaguliwa hivyo huwezi kuingia mtu na silaha,"alisema

Pia alisema katika mkutano huo iliohudhuriwa na wajumbe 81 toka Klabu 28  Tanzania Bara na Visiwani watatoa Tuzo ya tatu ya Daudi Mwangosi kama ishara ya kuonyesha waandishi hawako salama.

"Lakini tunaomba wafadhili wetu SIDA waangalie jinsi ya kusaidia Klabu ya Dodoma na tutapeleka andiko maalum ili wajengewe ofisi zenye hadhi kulingana na hali ilivyo sasa na kuwapatia mafunzo wanahabari ili wafahamu jinsi ya kuandika habari za viongozi mbalimbali wanaotembelea Dodoma,"alisema

Naye Mkuu wa Idara ya ushirikiano wa Balozi wa Sweden Tanzania (SIDA) Ulf Kastig alipongeza Klabu ya Arusha na Morogoro kubuni miradi kwa ajili ya kujiongezea kipato kwa ushirikiano na wadau wa mikoa yao.

Aliwakumbusha wanahabari kuhakikisha wanaandika habari za utafiti ili kuepuka kuleta shida katika nchi.

"Lakini ili Klabu zenu ziendelee kuwa na vyanzo vingi vya mapato vema mkaongeza idadi ya wanachama,"alisema
Alipongeza ushirikiano mzuri uliopo kati ya Klabu za wanahabari na UTPC na kusema jambo la kuigwa kwani linajenga Demokrasia ya kweli.

Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Jerry Muro aliwaasa wanahabari kuzingatia maadili ya kazi zao licha ya kukabiliana na changamoto nyingi ikiwemo ukosefu wa ajira.

Amesema Wilaya yake inakabiliwa na changamoto kubwa ya migogoro ya ardhi ambayo sehemu kubwa inasabishwa na ukosefu wa uelewa wa sheria ya umiliki ardhi na baadhi ya wanasiasa kuitumia kujipatia kura.

"Mimi sitakubali kabisa kuachia wanasiasa wajinufaishe na migogoro hii lazima nibadilishe badala ya ardhi kuwalaana bali iwe baraka hasa Halmashauri ya Meru, na hili nimeanza kuzungumza na viongozi wadini tusaidiane kulimaliza,"

SERIKALI YAELEZEA MBINU ZA KUKABILIANA NA UMASKINI

$
0
0
Na Benny Mwaipaja, WFM, Dodoma
Serikali imeeleza kuwa inazingatia Dira ya Taifa ya Maendeleo, Ilani ya Uchaguzi ya Chama Tawala (ccm), Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano na mwaka mmoja, pamoja na Mwongozo wa Bajeti kugawa rasilimali fedha na watu katika kukabiliana na changamoto za umaskini nchini.

Hayo yameelezwa Bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) alipokuwa akijibu maswali ya Mbunge wa Kasulu Mjini Mhe. Daniel Nicodemus Nsanzugwanko (CCM), aliyetaka kujua mbinu za Serikali katika kuhakikisha mikoa maskini nchini inapata rasilimali fedha na watu ili iweze kuondokana na hali hiyo ya umaskini.

Dkt. Kijaji alisema kuwa mgawanyo wa rasilimali fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo huenda sambamba na mgawanyo wa rasilimali watu kwa ajili ya utekelezaji, usimamizi, uperembaji na kutoa huduma kulingana na aina ya miradi.

Aidha Mhe. Nsanzugwanko alihoji hatua zilizochukuliwa na Serikali katika Mkoa wa Kigoma ili kujenga ulinganifu katika maendeleo.

Akijibu swali hilo Dkt. Kijaji alisema Serikali imebainisha  maeneo na miradi ya kimkakati kwa ajili ya utekelezaji ili kufungua fursa za kiuchumi  mkoani huo.

Alieleza kuwa miongoni mwa maeneo ya kimkakati yaliyobainishwa na kuanza kutekelezwa kwenye Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2016/17-2020/21 ni pamoja na mradi wa upanuzi na ujenzi wa Uwanja wa Ndege Kigoma.

“Miradi mingine ni mradi wa uzalishaji wa umeme wa maji katika maporomoko ya mto Malagarasi MW 44.7, kuanzisha na kuendeleza eneo huru la uwekezaji Kigoma, mradi wa gridi ya Kaskazini Magharibi kv400 na ujenzi wa Reli ya Kati kwa kiwango cha kimataifa”, alisema Dkt. Kijaji.

Katika swali jingine, Mhe. Nswanzugwanko alitaka kujua kwa nini Serikali isitenge shilingi bilioni 5 kila mwaka kwa kila mkoa ili kuondoa tishio la mikoa hiyo kuachwa nyuma kimaendeleo.

Mhe. Dkt. Kijaji alieleza kuwa kwa sasa Serikali haina sera wala mwongozo wa kutenga shilingi bilioni 5 kila mwaka kwa kila mkoa ili kukabiliana na changamoto za umasikini.

Alifafanua kuwa hoja ya kutenga shilingi bilioni 5 kwa kila mkoa kila mwaka ni lazima ifungamanishwe na Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano na Ilani ya Uchaguzi ya Chama Tawala.

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) akijibu maswali katika kikao cha Bunge leo Jijini Dodoma.

Serikali Yawasilisha Muswada wa Kulitangaza Jiji la Dodoma Makao Makuu ya Nchi

$
0
0
Na Jacquiline Mrisho - MAELEZO
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR - TAMISEMI), Mhe. Selemani Jafo leo amwewasilisha Muswada wa Sheria ya Kulitangaza Jiji la Dodoma kuwa Makao Makuu ya Nchi katika mkutano wa kumi na mbili wa kikao cha kwanza cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Waziri Jafo amesema dhumuni la muswada huo ni kupendekeza kutungwa kwa sheria ambayo italitangaza rasmi Jiji la Dodoma kuwa makao makuu ya nchi na makao makuu ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Waziri Jafo amesem chimbuko la hoja ya kutunga sheria hiyo ni kukosekana kwa sheria inayotambua na kuweka misingi ya uendelezaji wa makao makuu ya nchi, hivyo hatua ya kulitambua jiji la Dodoma kama makao makuu ya nchi itachochea ukuaji wa mji wa Dodoma na maeneo yanayozunguka moka wa Dodoma kiuchumi na kijamii.

“Kukosekana kwa sheria inayotambua Dodoma kuwa makao makuu ya nchi kulisababisha uendelezaji wa makao makuu ya nchi kutofikia malengo, hivyo msingi wa kutunga sheria hii ni kutambua kisheria jiji la Dodoma kuwa makao makuu ya nchi” alisema Waziri Jafo.

Akifafanua kuhusu muswada aliowasilisha mbele ya Spika Job Ndugai, waziri Jafo amesema muswada huo utakuwa na vifungu sita vikiwemo vya utangulizi, matumizi, tafsiri ya maneno yaliyotumika, kulitangaza Jiji la Dodoma kama makao makuu ya nchi na mwisho ni kifungu ambacho kimeweka masharti ya kubadilisha makao makuu ya nchi.

Uamuzi wa kuwasilisha muswada wa kulitanganza jiji la Dodoma kuwa makao makuu ya nchi na serikali, ni mwendelezo wa hatua za kimageuzi zinazofanywa na Serikali ya awamu ya Tano chini ya Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Selemani   Jafo akiwasilisha Bungeni maelezo ya Serikali kuhusu muswaada wa sheria ya kulitangaza Jiji la Dodoma kuwa makao makuu ya nchi wa mwaka 2018( The Dodoma Capital City ( Declaration) Bill, 2018.

YALIYOJIRI LEO BUNGENI JIJINI DODOMA

$
0
0
 Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai akisisitiza jambo wakati wa kipindi cha maswali na majibu Bungeni jijini Dodoma.
 Mbunge wa Jimbo la Buyungu Mhe. Mhandisi Christopher Chiza akiapa mbele ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Job NdugaiS leo Jijini Dodoma mara baada ya kuchaguliwa kuwa mbunge wa jimbo hilo.
 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akimpongeza mbunge wa Buyungu Mhe. Mhandisi Christopher Chiza mara baada ya kula kiapo mbele ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job  Ndugai leo Bungeni Jijini Dodoma.
 Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji akijibu swali Bungeni Kuhusu hatua zinazochukuliwa na Serikali katika kuwezesha mikoa kutekeleza miradi ya kimkakati ya maendeleo ili kuinua uchumi wa mikoa hiyo.
 Naibu Waziri wa Kilimo Mhe.  Dkt. Mary Mwanjelwa akieleza mikakati ya Serikali katika kuinua sekta ya kilimo hapa nchini wakati wa kipindi cha maswali na majibu leo Bungeni Jijini Dodoma.
 Mbunge wa Kibakwe Mhe. George Simbachawene akisisitiza kuhusu faida za Dodoma kuwa makao makuu ya nchi yetu leo Bungeni  Jijini Dodoma.
 Sehemu ya wabunge wakifuatilia  mkutano wa 12 kikao cha kwanza cha Bunge leo Jijini Dodoma.(Picha zote na Frank Mvungi- MAELEZO)

MADALALI WALIA NA WAKADIRIAJI BEI YA TANZANITE

$
0
0
 Baadhi ya madalali wa madini ya Tanzanite wa Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, wakiwa kwenye kikao kilichoitishwa na viongozi wa umoja wa madalali wa mkoa huo (Magebomita). 
 Ofisa wa mamlaka ya mapato nchini TRA Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, Castory Henry akizungumza kwenye kikao na madalali wa madini ya Tanzanite. 

Ofisa madini mkazi wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, Daudi Ntalima akizungumza kwenye kikao cha madalali wa madini ya Tanzanite. 
Mwenyekiti wa Umoja wa madalali wa madini ya Tanzanite wa Mkoa wa Manyara (Magebomita) Ernest Wasonga akizungumza kwenye kikao cha wanachama wao Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro. 

MADALALI wa madini ya Tanzanite wa Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara wamewalalamikia watathmini wakadiriaji wa madini hayo kwa kukadiria bei ya juu pindi wanapopita nayo kwenye lango la ukuta unaozunguka migodi ya Tanzanite, hivyo kuwasababishia hasara.

Madalali hao walilalamikia tatizo hilo kwenye kikao cha chama cha madalali wa madini ya Tanzanite mkoa wa Manyara, (Magebomita) kilichofanyika ukumbi wa Songambele mji mdogo wa Mirerani. 

Mmoja kati ya madalali hao Vincent Peter alisema serikali inapaswa kuweka umakini kwenye hilo kwani madalali wengi wamepata hasara kwa kukadiriwa bei kubwa tofauti na thamani halisi ya madini aliyonayo. 

Peter alisema wakadiriaji wanapaswa kukadiria bei halali ili madalali walipe kodi halali ya serikali kwa kuthaminishiwa bei ambayo inapaswa kulipwa tofauti na ilivyo sasa kwani uthaminishaji unafanywa tofauti na bei halisi. 

"Hawa wathaminishaji wa madini ya Tanzanite wanakosea mno kwani jiwe lenye thamani ya sh800,000 wanakadiria kwa sh4 milioni,  mmewatoa Mbeya kwenye ndizi ndiyo wakaja Mirerani kukadiria madini ya Tanzanite," alihoji Peter. 

Makamu Mwenyekiti wa Magebomita, Sammy Chacha Opong alisema madini ya Tanzanite yanataka utaalamu pindi yakikadiriwa kwani yapo tofauti na madini mengine ya vito hivyo wakadiriaji wanatakiwa kuwa na weledi juu ya hilo. 

Opong alisema madalali wengi wamewalalamikia ukadiriaji unaofanywa hivi sasa kwenye lango la kuingia ndani ya ukuta hivyo ni jukumu la serikali kusimamia hilo ili wadau wasizidi kuumia kwa kupata hasara. 

"Pamoja na hayo kuna changamoto ya ucheleweshaji wa kutolewa kwa leseni za madalali ambazo zimechukua muda mrefu kupata pindi wanapolipia kwani hulipia mwezi Julai lakini husubiri mno," alisema. 

Hata hivyo, ofisa madini mkazi wa Mirerani, Daudi Ntalima alisema wakadiriaji hao ni wataalamu waliobobea na hupanga bei halisi pindi wanapofanya tathimini ya madini ya Tanzanite ili muuzaji asiende kupata bei ndogo hivyo kupunjwa. 

Ntalima alisema endapo dalali akibaini tathimini anayofanyiwa kwenye madini yake ni tofauti na thamani halisi ana haki ya kupinga kwa kuandika barua ili uthaminishaji ufanyike upya. 

Ofisa wa mamlaka ya mapato nchini (TRA) wa mji mdogo wa Mirerani, Castory Henry alisema madalali wa madini ya Tanzanite walipo kwenye vikundi vyao wakati wa kufanya biashara hiyo wanaweza kupatiwa leseni. 

YANGA KUCHEZA MECHI YA KIRAFIKI DHIDI YA AFRICAN LYON JUMAPILI

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

KAIMU Katibu Mkuu wa Yanga Omar Kaaya amesema kuwa kwa sasa timu inaendelea na mazoezi kwa ajili ya kujiandaa na mechi za ligi kuu Tanzania bara kulingana na proramu za mwalimu na huu ni mwendelezo wa ushindi baada ya kuanza kwa Mtibwa.

Kaaya amesema timu imemaliza mechi za kimataifa na wachezaji wakapewa mapumziko tayari wameshaanza mazoezi ikiwa  chini ya Kocha Noel Mwandila kuangalia mapungufu yaliyojitokeza kwenye mechi zilizopita ikiwemo kucheza mchezo mwinG\gine wa kirafiki hapa Jijini Dar es Salaam.

Amesema kuwa  baada ya kushindwa kwenda kucheza mchezo wao kirafiki dhidi ya Singida United uliotakiwa kufanyika Mkoani Kigoma hiyo inatokana na ratiba ya ligi kubadilika na awali walitakiwa wacheze na Mwadui Mkoani Shinyanga.

Amesema kuwa, kwa sasa watacheza mechi ya kirafiki siku ya Jumapili dhidi ya African Lyon ili kuiangalia timu kabla ya kuendelea na ligi kwenye mchezo wao ujao watakaocheza na Stand United katika Uwanja wa Taifa.

Kaaya amewaomba mashabiki wa kanda ya Ziwa kuwa na subira na timu yao kutokana na kushindwa kwenda kucheza ila watakapopata muda wakati nwingine.

Kwa upande wa Meneja wa timu ya Yanga Nadir Haroub ' Canavaro' amesema kuwa kwa sasa hali ya wachezaji ni nzuri wanaendelea na mazoezi kwa wale ambao hawakuitwa katika timu ya taifa wakiwa wanania ya kuuchukua ubingwa wa mwaka huu baada ya kuupoteza msimu uliopita.

Canavaro amesema amekuwa anakaa na wachezaji wake akiwa anawamasihsha kujena umoja ndani ya timu kwa ajili ya kuuchukua ubingwa wa mwaka huu pamoja na hamasa ingawa kumekuwa na changamoto mbalimbali ndani ya timu.

" wachezaji wamekuwa na umoja na wakicheza kwa kujituma, wameweka matatizo ya klabu pembeni kwani hizo ni changamoto ila watahakikisha wanafanya vizuri kwenye michezo ya ligi kuu inayofuata,'amesema Canavaro.

Kwa sasa Yanga wanajiandaa mchezo wao ujao dhidi ya Stand United ambapo kwa sasa Yana wamecheza mchezo mmoja na Mtibwa kufanikiwa kupata ushindi wa goli 2-1.

DKT MENGI ATEULIWA KUWA MLEZI WA SERENGETI BOYS

$
0
0
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania(TFF)leo Jumanne Septemba 4,2018 limemtangaza Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP Dkt Reginald Mengi kuwa mlezi wa timu ya Taifa ya Vijana U17 "Serengeti Boys"

Dkt Mengi amekuwa akiifuatilia kwa karibu timu hiyo na amekuwa mmoja wa wadau wakubwa wa soka la Vijana.  Akiwa ni mpenda maendeleo ya mpira wa Miguu hususani soka la Vijana na amekuwa shabiki mkubwa wa Serengeti Boys.

TFF tunaamini tutashirikiana vizuri na Dkt  Mengi katika maendeleo na ustawi wa soka la Vijana na ni mwanamichezo ambaye hakika amekuwa mstari wa mbele katika kukuza na kuendeleza soka la Vijana. 

Mara kadhaa amekuwa akiwasiliana na TFF kufuatilia maendeleo ya timu ya Taifa ya U17 kwenye mashindano mbalimbali. 

TFF wamefarijika kwa Dkt Mengi kukubali kuwa mlezi wa timu hii ya Serengeti Boys na wanaamini kwa pamoja wataifanya timu hii kuwa msingi mzuri katika maendeleo ya ustawi wa soka la Vijana. 

Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP Ndugu Reginald Mengi 

Innocent Sammy Bingwa “88 Pool Commpetitions 2018”.

$
0
0

Meneja Rasilimali watu (HR) WA Kampuni ya kutengeneza meza za Pool ya KENICE, Fionce Halelwa(kushoto) akimkabidhi Kikombe na Meza ya mchezo wa Pool yenye thamani ya Shilingi milioni mbili, Innocent Sammy mara baada ya kuibuka bingwa kwenye mashindano ya Pool ya mchezaji mmoja mmoja (Singles) yaliyojukana kwa “88 Kenice Pool Competitations 2018” yaliyofanyika katika Ukumbi wa Meeda Sinza jijini Dar es Salaam. 

Meneja Rasilimali watu (HR) WA Kampuni ya kutengeneza meza za Pool ya KENICE, Fionce Halelwa(kushoto) akimkabidhi fimbo maalumu za kuchezea mchezo wa Pool na Meza ya mchezo wa Pool yenye thamani ya Shilingi milioni mbili, Innocent Sammy mara baada ya kuibuka bingwa kwenye mashindano ya Pool ya mchezaji mmoja mmoja (Singles) yaliyojukana kwa “88 Kenice Pool Competitations 2018” yaliyofanyika katika Ukumbi wa Meeda Sinza jijini Dar es Salaam.
Meneja Rasilimali watu (HR) WA Kampuni ya kutengeneza meza za Pool ya KENICE, Fionce Halelwa(kushoto) akimkabidhi pesa taslimu Shilingi laki moja, Patrick Nyangusi mara baada ya kuibuka shindig wa pili kwenye mashindano ya Pool ya mchezaji mmoja mmoja (Singles) yaliyojukana kwa “88 Kenice Pool Competitations 2018” yaliyofanyika katika Ukumbi wa Meeda Sinza jijini Dar es Salaam.

Na Mwandishi Wetu.
KAMPUNI ya Kenice Tanzania imemkabidhi rasmi Bingwa wa mashindano ya Pool ya siku kuu ya nane nane Kikombe na meza ya Pool yenye thamani ya Shilingi milioni mbili, Innocent Sammy yajulikanayo kama “88 Kenice Pool Competitions 2018” yaliyomalizika hivi karibuni jijini Dar es Salaam katika Ukumbi wa Meeda jijini Dar es Salaam.

Akikabidhi zawadi Meneja Rasilimali Watu(HR) wa Kampuni ya Kutengeneza Meza za Pool ya Kenice, Fionce Halelwa, alimpongeza bingwa na kumuomba akaitumie vyema meza hiyo kwanza kama kitega uchumi lakini pia kama kiwanja maalumu cha mazoezi kwake cha kufanya kipaji chake cha kucheza pool kukua zaidi.

Alisema Fionce, tunatambua unakabiliawa na mechi kubwa ya Kimataifa na mchezaji kutoka Afrika Kusini, basi meza hii ikakusaidie kujiandaa vyema na shindano hilo ili ushinde na kuipa sifa Nchi yako ya Tanzania

Fionce alisema Kampuni ya Kenice itaendelea kusapoti mchezo wa Pool Tanzania kwa kadri watakavyojaliwa lakini zaidi pale wachezaji watakapokuwa wanafanya vizuri zaidi kwa ni hiyo ni hamasa pekee ya wao kuendelea kusaidia kwenye mchezo wa Pool.

Nae mratibu wa wa mashindano ya Pool, Michael machella alisema mashindano ya mwaka huu yalikuwa na hamasa ya pekee kwani yalishirikisha Wilaya tano za Mkoa wa Dar es Salaam kwa kipengele cha mchezaji mmoja mmoja(Singles) mpaka kumpata Bingwa wa mwaka huu 2018, Innocent Sammy

Machellah alisema ni mwaka wan ne sasa mfululizo akiandaa mashndano hayo na kila mwaka kampuni ya Kenice wamekuwa wakitoa ufadhili hivyo aliwashukuru sana kwa moyo wao huo na kuwaomba wasichoke kuisaidia Pool kwani mchango wao unatambulika kwa wachezaji na jamii ya Watanzani kwa ujumla.

Mwisho aliwapongeza washindi akianzia na Bingwa wa 2018, Innocent Sammy na mshindi wa pili Patrick Nyangusi ambao aliwataka wajiandae vyema na mashindano ya Kimataifa.

MAMA AMMWAGIA MWANAYE MAFUTA YA TAA NA KUMCHOMA MOTO

$
0
0
Mtoto wa Kike mwenye umiri wa miaka  13, (Jina limehifadhiwa) ameunguzwa baada ya kumwagiwa mafuta ya taa na  kisha kuwashwa na kiberiti na mama yake mzazi.

Binti huyo amelazwa katika hosptali ya St, Joseph Mbweni katika wodi ya watoto akiwa hawezi hata kutoa maelezo  vizuri.

Akizungumza jinsi mtoto huyo alivyofikishwa hospitalini hapo, Dkt,  Valentino Francis Bangi amesema, mtoto alifikishwa hospitalini hapo alfajiri ya Agosti 31 kuamkia Septemba Mosi mwaka huu akiwa katika hali mbaya, alikuwa ameunguzwa na moto sehemu ya mbele ya  kifua na usoni.

Dkt, Bangi amesema, mtoto huyo alipofikishwa hospitalini hapo alikuwa hawezi kupumua wala kuongea, lakini walimpatia huduma ya kumuweka katika hali nzuri na kuanza kurudi katika hali ya ubinadamu .

Dkt. Bangi amesema moja ya huduma waliyoifanya ni kumuoongezea maji pamoja na kumpatia huduma nyingine ya kumfanya apumue.

‘kwa sasa hali ya mgonjwa, anaendelea vizuri tofauti na alivyokuwa kwa sababu alikuwa hawezi hata kuongea, lakini sasa hivi anazungumza ambapo amelazwa wodi ya watoto hospitalini hapa.

Kwa upande wake, Ofisa Ustawi wa Jamii, wa Hospitali hiyo,  Angela Isingo ambaye anashughulikia masuala ya watoto, amesema tukio hilo linasikitisha , kwani wamemuhoji  binti huyo amesema aliyemfanyia kitendo hicho ni mama yake mzazi.

Isingo amesema mtoto huyo ameeleza chanzo cha tukio hilo kwamba, “binti alirudi usiku kutoka shule, mama yake akamuuliza kibubu cha pesa kiko wapi?, kwa sababu ndani kulikuwa na vibubu viwili havionekani kwa hiyo akaenda moja kwa moja kwa huyo mtoto na kumuuliza, anasema mtoto alimjibu kuwa hafahamu kibubu kilipo, mama yake akaendelea kumuhoji tena kuwa akitafute hadi akipate, akasema akazunguka akapata kibubu kimoja, na pale  ndani haishi peke yake ana baba yake na  ndugu zake wawili na dada yake mkubwa mmoja.

Akasema licha ya kumjibu mama yake kuwa hafahamu kibubu hicho kilipo, mama yake akaendelea kumuhoji kuwa, lazima aseme kibubu kilipokwenda ndiyo mama yake akachukua mafuta ya taa akamwagia na  kisha  akachukua kiberiti kumuwasha.

Amesema, baada ya kumuwasha ndiyo alihisi maumivu.

Hata hivyo, Isingo amesema, hali ya binti huyo ni nzuri kwa sasa tofauti na mwanzo alivyofikishwa hospitalini hapo alikuwa amevimba kwani kwa sasa maumivu ya ndani yamepungua. 

"Kitendo alichofanyiwa mtoto huyu cha kinyama na cha kikatili sana, nina amini vyombo vya dola vitafanya kazi yake kama nilivyosikia mama yake yupo polisi.

"Ninaamini sheria itashika mkondo wake na mimi nitasimamia kesi hii hadi inafika mahakamani, kwa sababu kesi nyingi za watoto huwa zinaishia njiani wanasema familia ikakae ielewane," amesema Isingo 

Ofisa huyo alisema lazima wasimame kidete kuhakikisha jambo hilo linakomoshwa na anaweza huyu akawa mfano kwa wamama wengine ambao wanawafanyia watoto wao au watoto wa kuwalea.tuwe walinzi wa watoto na si wa kuwafanyia vitendo vya kikatili.

Blogu ya jamii imefanikiwa kufika nyumbani kwa binti huyo na kufanikiwa kuzungumza na mdogo wa binti aliyechomwa moto (jina limehifadhiwa), anayesoma darasa la tatu hapa jijini, 

Akisimulia mtoto huyo ambaye ndiye aliyekuwa ameachiwa nyumba bada ya dada yake mkumbwa kwenda kupeleka chakuila Hospitali amesema, 
“Mama ndiyo alinituma nikanunue mafuta ya taa ya sh 300 pale dukani, (akionyeshea kwa kidole duka hilo), amesema, hakujua mama yake alitaka kufanyia nini mafuta yale, kwa usiku huo.

Alipoulizwa na Diwani wa kata ya bunju  mahali alipo mama yake, amesema, “mama yupo polisi na dada Angel ameenda hospitali kumpelekwa mgonjwa chakula (dada yake).

Amesema,mgonjwa aliunguzwa na mama,sababu alikuwa anachukua hela za mama ndani anaenda kuzila. Amesema wakati dada yake anachomwa yeye na mdogo wake walikuwa humo humo ndani lakini dada yao mkubwa Angel alikuwa nje, 

“Mama  alimuunguzia ndani sisi tukiwa humo humo tulipiga kelele. Nikamshuhudia dada anawaka moto kifuani, wakati huo baba hakuwepo,,baba alipokuja alimkuta Dada yupo ndani hajapelekwa hospitali, baba akauliza mama yake huko kuna nini, hapo sasa sijui mama alimjibuje baba. Tupo watoto wa nne dada Mary ni wa pili.

Amesema,baadae mama yao alimmwagia maji dada yake na kumzima moto ule sisi hatujafurahishwa na kitendo alichokifanya mama.Mama” amesimulia mtoto huyo.

Kwa upande wake, Alex John, Mjumbe na Katibu wa Shina namba tatu, kata ya bunju, ameelezea  tukio hilo la kusikitisha 

Amesema, aliamshwa majira ya saa tano kasoro usiku na dada mmoja ambaye ni jirani yake, aliyemtaja kwa jina la Maria Clement, amesema alimueleza kuwa jirani yangu kamuunguza mtoto na wanapiga makelele 

Nilipopata hiyo taarifa tukaongozana hadi nyumbani kwa mtoto huyo, bahati nzuri tukamkuta mama yake yupo, mume wake na watu wengine nikamuuliza kulikoni? Nipewa taarifa na jirani yenu kuwa mtoto wenu ameungua moto na nyinyi ndio mmemuunguza, wakaniambia kuwa yule ni mwizi.

Ameongeza, Nikawaambia hata kama ni mwizi yuko wapi? Sasa wakati wanataka kunipa maelezo ya kina akaja jirani yangu ambaye ni Abiti Njau akasema kuna nini mbona yule mtoto ameungua namna ile, nikamuuliza yuko wapi? akasema yupo kule kwangu Yale mazungumzo yakaishia pale, kwa hiyo sikupewa maelezo ya kina 

Ikabidi kuongozana na yule jirani yangu ili tuweze kumuona huyo mtoto kuona jinsi gani ambayo tunaweza kumsaidia, tulipofika tukaambiwa tena amekwenda bondeni kwa sababu alikuwa anapiga makelele huku analalamika, yaani alikuwa kama vile ukimchinja kuku halafu ukamuachia si anaweza akakimbia basi ndiyo kitu ambacho kilimtokea huyo mtoto

Wakati tunarudi tena eneo la tukio tukakuta wamemkata. “Kwa kweli nilivyomuona nilihisi kuumia sana, mtoto alikuwa ameungua kupita kiasi. Ili tukio kwa mujibu niliyopewa na dada Maria aliniambia mama mtu ndiye aliyehusika, muda huo sikujua baba mtu yuko wapi. Tulifanya utaratibu na kumpeleka mtoto hospitali baada ya kupata Fomu namba Tatu ya Polisi (PF3) kutoka polisi Mbweni.

Nilipowaeleza watoto kuhusiana na tukio hilo wakataharuki baada ya kumuona mtoto alivyounguzwa ,wakaniuliza nani alifanya hivyo, nikamwambia kwa taarifa ambazo ninazo Mimi hadi sasa mama yake ndiyo alimfanyia kitendo hiki, askari wakamchukua huyo mama wakamuweka chini ya ulinzi wakamuingia ndani.

Akizungumzia suala la baba wa mtoto huyo kuwa ana undugu na mkubwa mmoja wa Jeshi la Polisi kutaka kumaliza suala hilo mezani, Ofisa Mtendaji wa Kata ya Bunju, Ibrahimu Mabeo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya usalama amesema wamesikia kuwa baba wa mtoto yupo uraiani, wataenda polisi yeye pamoja na Diwani kuhakikisha na baba mtu naye anachukuliwa hatua kwa sababu kama na baba naye anatetea jambo hilo la kinyama basi kama viongozi wa kata hatuwezi kulifumbia macho. 

Nae Diwani wa kata hiyo, Elly Nassoro ameeleza kusikitishwa kwake na tukio hilo, kwani kitendo kilichofanywa na  wazazi wa binti huyo ni cha aibu na kibaya. 

“Binti ameungua sana hali yake hatujui itakuwaje tunaomba Mwenyezi Mungu amsaidie ili apone. Kitendo ni cha kinyama kama tulivyomuhoji mtoto akasema mama ndiyo alimtuma kununua mafuta, halafu akachukua kiberiti akamuwasha”.

"Tumefikia hivi Watanzania kweli, kwa kweli inasikitisha sana wito wangu tuzidi kukemea maovu haya ambayo ya anaendelea kutokea kama vile mzazi mwenyewe anaweza kufanya hivi ni jambo la kutisha, tubadilishe," alisema Msingi 

Kamanda wa Polisi mkoa wa Kinondoni , Murilo Jumanne Murilo amedhibitisha kutokea tukio hilo ambapo mama wa mtoto huyo wanamshikilia na wakati wowote watampandisha mahakamani.
“Taarifa hii ni ya kwali na mhusika tumeshamkamata na tumemuweka mahabusu na wakati wowote atapandishwa mahakamani kwa tuhuma hizo”amesema Murilo  
 Mtoto wa Kike mwenye umiri wa miaka  13, (Jina limehifadhiwa )ameunguzwa baada ya kumwagiwa mafuta ya taa na  kisha kuwashwa na kiberiti na mama yake mzazi.

RAIS MAGUFULI AWEKA JIWE LA MSINGI MRADI WA BARABARA YA NYAMUSWA-BUNDA-KISORYA-NANSIO , AHUTUBIA WANANCHI WA NANSIO UKEREWE

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akivuta utepe pamoja na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Isaack Kamwelwe kuashiria uzinduzi wa Barabara ya Nyamuswa-Bunda-Kisorya-Nansio km 121 katika sehemu ya Barabara ya Bulamba Kisorya km 51 katika sherehe zilizofanyika Kisorya Bunda mkoani Mara.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa ameshika mkasi na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Isaack Kamwelwe wakikata utepe kuashiria uzinduzi wa Mitambo itakayotumika katika ujenzi wa barabara Barabara ya Nyamuswa-Bunda-Kisorya-Nansio km 121 katika sehemu ya Barabara ya Bulamba Kisorya km 51 katika sherehe zilizofanyika Kisorya Bunda mkoani Mara.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Kisorya kabla ya kuweka jiwe la msingi Ujenzi wa Barabara ya Nyamuswa-Bunda-Kisorya-Nansio km 121 katika sehemu ya Barabara ya Bulamba Kisorya km 51 katika sherehe zilizofanyika Kisorya Bunda mkoani Mara.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akivuta utepe pamoja na Waziri wa Elimu Profesa Joyce Ndalichako ili kuweka jiwe la msingi ujenzi wa Chuo cha Ualimu Murutunguru kilichopo Nasio Ukerewe mkoani Mwanza.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipiga makofi pamoja na Waziri wa Maji Profesa Makame Mbarawa wakati akipokuwa akisikiliza maelezo ya mradi wa maji wa Nansio Ukerewe mkoani Mwanza.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Ukerewe mara baada ya kuwasili akitokea Kisorya mkoani Mara.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Mkuu wa Mkoa wa Mara Adam Malima kabla ya kuweka jiwe la msingi ujenzi wa barabara Barabara ya Nyamuswa-Bunda-Kisorya-Nansio km 121 katika sehemu ya Barabara ya Bulamba Kisorya km 51 katika sherehe zilizofanyika Kisorya Bunda mkoani Mara.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Waziri wa Maji Profesa Makame Mbarawa wakati akitoka kukagua pampu za kusukuma maji katika mradi wa maji uliopo Nansio Ukerewe mkoani Mwanza.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Nansio hawaonekani pichani katika eneo la chuo cha Ualimu cha Murutunguru kilichopo Nasio Ukerewe mkoani Mwanza.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Magu mara baada ya kufungua viwanda vya Lakairo Industries Ltd vilivyopo Magu mkoani Mwanza.
Sehemu ya Wananchi wa Nansio Ukerewe waliohudhuria katika mkutano wa hadhara leo.
Sehemu ya barabara ya ya Bulamba Kisorya km 51 iliyoanza kujengwa kwa kiwango cha lami. PICHA NA IKULU

KOCHA WA RIADHA AAHIDI MEDALI MASHINDANO YA TAIFA

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

KOCHA wa timu ya Taifa ya Riadha Iddi Muhunzi 'kipepe' amesema vijana aliokuwa nao katika mazoezi yake kwa sasa wana uhakika wa kuleta medali kwenye mashindano ya Taifa yatakayoanyika baadae mwaka huu.

Akizungumzia maadalizi ya mashindano mbalimbali yanayotarajiwa kufanyika hapo baadae, Muhunzi amesema wataanza na kutafuta ya mkoa wa Dar es salaam na kutakuwa na mashindano ya wazi siku ya Jumamosi yatakayofanyika Uwanja wa Taifa ili kuwapata vijana watakaowakilisha mkoa.

Muhunzi amesema baada ya hapo watajiandaa na mashindano ya Namtumbo ya Half Marathon yatakayoshirikisha vijana mbalimbali na mpaka sasa vijana wana ari ya hali ya juu kuweza kufanya vijana vizuri.

Ameeleza kuwa, mashindano ya Taifa  anataka kuhakikisha vijana wake wanabakisha medali kutokana na morali kubwa waliyonayo na kutaka kufanya vizuri kwenye mashindano hayo wakianza katika mazoezi ya kila siku yanayoendelea.

Muhunzi amesema, amekuwa na hamasa kubwa sana kwa vijana hao na wengi wameonesha wana vipaji vikubwa vya kuja kuipatia medali taifa siku zijazo.

'Programu ninazowapatia ni za kufa mtu na wengi wameonesha moyo wa kujituma na kufanya mazoezi kwa nguvu zote na hilo limeonesha kuwa vijana wamedhamiria kuleta medali,'amesema Muhunzi.

"Kwa hamasa hii ya vijana inaonesha natumia vyeti vyangu vizuri sio kusomea halafu kujaza makaratasi ndani na hili litakuja kusaidia kupata vijana wenye vipaji vikubwa sana
'

Timu ya taifa ya riadha wanaendelea na mazoezi kwa sasa wakiwa wanajiandaa na mashindano mbalimbali yanayokuja hapo baadae na maandalizi yao yanaanzia siku ya Jumamosi kwa kuanza mashindano ya wazi ya kupata timu itakayowakilisha mkoa wa Dar es salaam na kisha mashindano ya Namtumbo kabla ya  kuanza kwa mashindano ya taifa.

ZAIDI YA WANAFUNZI 6000 KUFANYA MTIHANI WA KUHITIMU DARASA LA SABA MKURANGA

$
0
0

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mkuranga,Mhadisi Mshamu Munde akizungumza na Michuzi Blog leo kuhusu wasimamizi wa mitihani ya darasa la saba unaoanza kesho Jumatano 5-6 Septemba wasimamiee kwa weledi na wanafuzi wafanye kwa waminifu.

Mitihani ya taifa ya darasa la saba inatarajiwa kuanza kesho nchini kote hivyo walimu wameombwa kusimamia mitihani hiyo vizuri na wale watakaokiuka sheria za usimamizi wa mitihani hatua Kali zitachukuliwa dhidi yao huku zaidi wanafunzi 6000 watafanya mtihani huo.

Akizungumza Wilayani Mkuranga Mkoani Pwani Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Juma Abeid amesema kesho wanafunzi wa darasa la saba nchi  nzima wanafanya mtihani wao wa mwisho kwahiyo amewaomba walimu wanaosimamia mitihani hii wafanye kazi yao kwa uadilifu na kufuata sheria muache udanganyifu.

Aidha amewataka wanafunzi kuwa watulivu katika pindi chote cha mitihani ili waweze kufanya vizuri katika mitihani yao hiyo nakuiletea sifa wilaya ya Mkuranga."Mwaka Jana Mkuranga tulishika nafasi ya kwanza katika mkoa wa Pwani naamini tunaweza pia kuwa wa kwanza kitaifa kama wanafunza watatumia nafasi ya kesho kufanya mitihani vizuri"alisema Abeid

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mkuranga Mhandisi Mshamu Munde amesema kuwa halmashauri hiyo imejiandaa vizuri kwani mpaka sasa vifaa vyote vinavyohusiana na mitihani vimeshakamilika."mandalizi ya mitihani yanahusisha vifaa vya mitihani,na mafunzo kwa wasimamizi wote wa mitihani vyote vimakailika ikiwemo masurufu,usambazaji wa mitihani na magari"alisema

Alisema kuwa zoezi hilo ni la kitaifa na serikali imewekeza fedha nyigi kwahiyo anawasihi wasimamizi wawe waadilifu wasijihusishe na vitendo vya udanganyifu wataitia serikali hasara kwa sababu imetumia pesa nyingi na kutoa rai kwao wafanye kazi kwa weledi.

Aidha alitoa wito kwa wanafunzi kufanya mitihani yao kwa uaminifu mkubwa wadifanye udanganyifu wa aina yeyote ile kwani utawaletea hasara kubwa

Hata hivyo zaidi ya wanafunzi 6000 wilayani mkuranga wanatarajiwa kuanzà mitihani wao wa mwisho wa kumaliza Elimu ya msingi hapo kesho

KURASA ZA MBELE ZA MAGAZETI LEO

RC ALLY HAPI:MAJENGO YA UWANJA WA NDEGE WA NDULI YANAHARIBU TASWIRA YA KUIJENGA IRINGA MPYA

$
0
0
Mkuu wa mkoa wa Iringa Ally Hapi akiwa ameongozana na mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela pamoja na meneja wa uwanja wa nduli Anna Kibopile alipofanya ziara katika uwanja wa ndege wa Nduli kwa kufahamu maendeleo ya ukarabati mdogo wa uwanja huo na kubaini baadahi ya changamoto zinaukabili uwanja huo hasa katika swala la majengo kuto kidhi mahitaji ya wasafiri 
Mkuu wa mkoa wa Iringa Ally Hapi akiwa ameongozana na mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela pamoja na meneja wa uwanja wa nduli Anna Kibopile wakiwa kwenye eneo ambalo linafanyiwa ukarabati mdogo 
Mkuu wa mkoa wa Iringa Ally Hapi akiwa ameongozana na mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela wakipata maelezo kutoka kwa meneja wa uwanja wa nduli Anna Kibopile juu ya ukarabati wa uwanja unaoendelea.
Mkuu wa mkoa wa Iringa Ally Hapi akiwa ameongozana na mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela pamoja na kamanda wa police mkoa wa Iringa Juma Bwire wakiangalia jengo la wasafiri katika uwanja wa nduli mkoani Iringa.
Mkuu wa mkoa wa Iringa Ally Hapi akiwa ameongozana na mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela pamoja na meneja wa uwanja wa nduli Anna Kibopile wakiwa ndani katika sehemu ya abiri ambao wanasubiri kusafiri. 
Mkuu wa mkoa wa Iringa Ally Hapi akiongea na waandishi wa habari wakati wa ziara katika uwanja wa nduli na kubaini mapungufu mengi ikiwapo gari hilo ambalo linaonekana la zimamoto ambalo toka lifike hapo halijawi kufanya kazi kutokana na kuwa bovu na spea zake kutopatikana.

NA FREDY MGUNDA,IRINGA.
MKUU wa mkoa wa Iringa Ally Hapi hajaridhishwa na hali halisi ya uwanja wa ndege wa nduli uliopo kata ya nduli kuelekea kuijenga Iringa mpya kwa maendeleo ya wanairinga.

Akizungumza wakati wa ziara ya kukagua ukarabati mdogo unaoendelea katika uwanja huo,hapi alisema kuwa uwanja huo wa ndege unahitaji ukarabati wa maana ili kukidhi mahitaji ya watumiaji na kukuza maendeleo ya wananchi wa mkoa wa Iringa.

“Nimetembea kwenye maeneo mengi ya uwanja huu hayaridhi wala hayavutii kwa wawekezaji kuja mkoani hapa kwa kuwa saizi wawekezaji wengi wanapenda kutumia usafiri wa anga hivyo ni lazima kuwa na kiwanja cha ndege ambacho kitakidhi na kuvutia watalii na wawekezaji wanapokuja mkoani hapa” alisema Hapi

Hapi alisema kuwa jengo la wageni la uwanja huo ni dogo,halina ubora unaotakiwa na halikidhi kuwa katika uwanja huo ambao hivi karibuni utaanza kupokea wageni wengi kutoka maeneo mbalimbali ya ndani ya nje ya nchi.

“Sehemu hii ya kupumzikia wageni hakuna,sehemu ya wasafiri wanapoongokea bado ni ndogo na haina vigezo vya kuwa eneo la kupuzikia wasafiri,vyoo havifai eneo lenyewe bado halina miundombinu ya kisasa ambayo itawavutia watu wengi kuja mkoani Iringa hivyo tunahitaji kujenga jengo jipya na la kisasa kabisa” alisema Hapi.

Haiwezekani uwanja wa ndegehuu ukawa unamajengo na vifaa vingi ambavyo vimechoka na havikizi mahitaji ya kuijenga Iringa mpya hivyo ni lazima kuwekeza kwenye uwanja ili kuvutia wawekezaji na watalii ambao watakuja mkoani hapa.

Hapi aliongeza kuwa uwanja wa ndege wa Nduli hauna hapa gari la fire ambalo litasaidia kuongoa majanga yoyote yatakayotokea kwenye uwanja huu,hivyo ni lazima tserikali ijue kuwa tunahitaji kuwa na gari la fire hapa kwa kuwa Iringa ni kitovu cha utali nyanda za juu kusini.

“Nimejionea hapa mwenyewe kuwa hakuna gari la fire linalofanya kazi kwa kuwa lililopo ni bovu na haliwezi kutengenezeka kwa kuwa liltengenezwa kwenye viwanda vya miaka mingi iliyopita na spea zake hazipatika hata nje ya nchi kwa mjibu wa wataalamu ambao wamenieleza hapa” alisema Hapi.

Hapi alisema kuwa gari ambalo lipo katika uwanja wa ndege wa Nduli halijawahi kufanya kazi toka liletwe na inasadikiaka kuwa litengenezwa miaka ya themanini huko hivyo hakuna gari la zimamoto katika eneo hili hivyo ni hatari kwa watumiaji wa uwanja huu.

Aidha hapa alisema kuwa uwanja wa ndege wa Nduli unaumuhimu mkubwa wa kukuza uchumi wa mkoa wa Iringa kwa kuwa watalii na wawekezaji wengi watautumia uwanja huu wa ndege kufanya kazi kwa muda muafaka na kurudi walikotoka kwa kutumia usafiri wa anga.

“Ukiwa na uwanja wa ndege ambao unakidhi vigezo vinavyotakiwa utasaidia kuongeza utalii wa kusini kama ambavyo unajua kuwa Iringa ndio kitovu cha utalii na kuvutia wawekezaji wengi ambao mara nyingi wamekuwa wakitumia usafiri wa anga tofautia wachache ambao wamekuwa wakitumia usafiri wa barabara za chini” alisema Hapi

Naye meneja wa uwanja wa ndege wa Nduli Anna Kibopile alisema kuwa jengo la abiria halikidhi mahitaji kupokea abiri wengi ambao pia watakuwa wakitumia ndege ya serikali aina ya Bombardie ambayo itaanza safari mkoani Iringa hapo baadae.

“Unajua kuwa ndege yetu ya Bombardie ataanza safari ya kuja hapa mkoani hiyo itakuwa inachukua abiria wengi sana hivyo jengo letu la abiria halitoshi kuwahudumia wasafiri ambao watakuwa wakiutumia unjwa huo kufanya safari zao” alisema Kibopile 

Kibopile alisema kuwa ndege ya Bombardie inabeba abira zaidi ya sabini hivyo ni lazima kuhakikisha tunataua au tunajenga jengo kubwa la abira ambalo mkuu wa mkoa wa iringa ameshauri kuwa jengo hilo halikidhi mahitaji ya abiria ambao watakaokuwa wanakuja mkoani Iringa.

RAIS DKT. SHEIN AZINDUA VITUO VYA MFUMO WA KIELEKTRONI WA KUSAJILI WAKAAZI WA ZANZIBAR (E-ID CARD)

$
0
0
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein, akikata utepe kuashiria Uzinduzi wa Vituo vya Usajili wa Vitambulisho vya Mzanzibar na Uzinduzi wa Uimarishaji Mfumo wa Usajili kielektroniki, (kushoto_ Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara Maalum za SMZ Mhe. Haji Omar Kheri, na (kushoto) Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi, wakishuhudia hafla hiyo iliofanyika katika viwanja vya Ofisi hiyo Dunga Wilaya ya Kati Unguja. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akifungua pazia kuzindua jengo la Ofisi mpya za Wilaya -Dunga pamoja na uzinduzi wa Uimarishaji wa mfumo wa matukio ya kijamii uliofanyika katika Wilaya kati Mkoa wa Kusini Unguja.  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akipata maelezo ya kifundi kutoka kwa Mkurugenzi wa Mtendaji wa Wakala wa Usajili wa Matukio ya Kijamii Zanzibar Dkt. Hussein Khamis Shaaban mara baada ya uzinduzi wa Uimarishaji wa mfumo wa matukio ya kijamii na Jengo la Ofisi mpya ya Wilaya Dunga uliofanyika leo katika Wilaya ya Kati, Mkoa wa Kusini Unguja, (kulia) Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein.     RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akihutubia wakati wa hafla hiyo ya Uzinduzi wa Ofisi za Wilaya za Usajili wa Vitambulisho vya Mzanzibar, katika viwanja vya Dunga Wilaya ya Kati Unguja.   WANANCHI wa Mkoa wa Kusini Unguja wakifuatilia hafla ya Uzinduzi wa Mfumo wa Usajili wa Kieletroniki na Ofisi za Usajili wa Vitambulisho Wilaya ya Dunga wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein, akihutubia hafla hiyo.   RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, wakiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa SMZ na Wafanyakazi wa Wakala wa Usajili, baada ya hafla ya uzinduzi huo, uliofanyika Dunga Wilaya ya Kati Unguja

DC PANGANI AWATAKA WASHIRIKI SHINDANO MISS TANZANIA KUUTANGAZA UTALII, UKIWEMO WA HIFADHI YA MSITU WA AMANI,SADANI

$
0
0
Washiriki wa Miss Tanzania 2018.

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
MKUU wa Wilaya ya Pangani Zainab Abdallah amewataka washiriki wa mashindano ya urembo ya Miss Tanzania mwaka 2018 kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo nchini.

Amesema lengo ni  kusaidia kuongeza idadi ya watalii nchini huku akiwahakikishia warembo hao Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dk.John Magufuli imeamua kutoa kipaumbele kwa vijana kutimiza ndoto zao.

Abdallah  ambaye ndio Mkuu wa Wilaya mwenye umri mdogo kwa wakuu wa wilaya nchini amesema hayo wilayani Muheza mkoani Tanga  baada ya kuwapokea warembo 20 wanaoshiriki shindano hilo.

Ambapo walifika mkoani Tanga kwa ajili ya kutembelea vituo vya utalii vinavyosimamiwa na Wakala wa Huduma za Misitu nchini(TFS) ambapo amewahakikishia kwenye hifadhi hiyo kuna utalii ambao haupo mahali kokote duniani zaidi ya Misitu ya Amani.

Hivyo amesema ujio wa warembo huo ni muhimu na kuwataka wawe mabalozi wazuri wa kuutangaza utalii

"Tanzania  ina vivutio vingi sana,mfano kwa  wilaya ya Pangani tuna mbuga  Sadan ambayo ndio mbuga ambayo imepakana na bahari barani Afrika.

" Pia tuna majengo ya kale kwa kifupi Pangani haitofautiani na Zanzibar.Tujitahidi kuutangaza utalii wa ndani ili tusaidie kuleta pato la Taifa,"amefafanua.

Ameongeza kupitia utalii wa ndani warembo hao watajipambanua kwakutumka fursa zilizopo ili kujipatia fursa za ajira.

Wakati huo huo Meneja Masoko na Uwekezaji wa TFS Mariam Kobelo  ameeleza kwamba malengo ya kuwapeleka  warembo hao katika vivutio hivyo ili waone vivutio na kisha kuvitangaza vivutio.

"TFS itatumia warembo hao kama chombo cha kutangaza utalii wandani kwa upande wa mazingira,kwa kufanya hivyo watasaidia kuongeza pato kwa sbabu tutawatumia kama chombo cha kutangaza utalii wa mazingira,mito inayoteteresha maji,misitu na vinginevyo.

Warembo hao kwa wakiwa katika hifadhi ya msitu asili wa Amani wamepata nafasi ya kuelezwa vivutio vinavyopatikana na hasa vinyonga wa pembe tatu ambao wanapatikani katika hifadhi hiyo.

Kwa upande wa warembo hao wamefurahishwa kutembelea hifadhi hiyo kwani wamepata nafasi ya kushuhudia vivutio mbalimbali vya utali

Kwa kukumbusha mashindano ya Miss Tanzania yanatarajia kufanyika Septemba 8 mwaka huu jijini Dar es Salaam.

SERIKALI KUUNDA KIKOSI KAZI KUPAMBANA NA MIMEA VAMIZI

$
0
0
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira January Makamba akifungua mkutano wa wadau wa Mazingira  Jijini Arusha. Mkutano huo umeshirikisha wadau mbalimbali kutoka Taasisi za Serikali na zile zisizo za kiserikali kwa lengo la kujadili changamoto ya mimea vamizi yenye athari hapa nchini.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira January Makamba akifuatilia mawasilisho ya mimea vamizi kutoka kwa Mtaalamu wa COSTECH (hayupo pichani). Kulia ni Mhe. Nape Nnauye Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ardhi na Maliasili.
Sehemu ya Washiriki wa Mkutano wa wadau wa kujadili changamoto za mimea vamizi. Mkutano umefanyika katika ukumbi wa AICC jijini Arusha. Mstari wa mbele katika picha ni waheshimiwa wabunge waliohudhuria.

KATIKA jitahada za kupambana na mimea vamizi nchini ambayo kwa kiasi kikubwa ina athari kwa uchumi wa Nchi yetu, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba hii leo amewakutanisha wadau kutoka sekta mbalimbali, asasi za kiserikali na zisizo za kiserikali, Wenyeviti wa Kamati za Bunge za Ardhi na Maliasili, Kamati ya Viwanda, Biashara na Mazingira na Kamati ya Kilimo, Mifugo na Maji ili kwa pamoja waweza kujadili namna bora ya kupambana na mimea vamizi ambayo imetapakaa kwa kasi katika maeneo mbalimbali hapa nchi.

“Pamoja na kwamba viumbe vamizi wageni ni janga kwa makazi asilia ya viumbe, lakini hatujalishughulikia kikamilifu, kuweka mikakati madhubuti ya kuzuia na kukabiliana na viumbe hivi. Kwa muktadha huo, leo tumepata fursa adimu na adhimu kutafakari kuhusu hali ilivyo kwa sasa, changamoto zilizopo na kujadili mikakati madhubuti ya kukabiliana na tatizo la viumbe vamizi wageni hapa nchini” Makamba alisisitiza.

Wadau waliohudhuria mkutano huo wameitaka Serikali kuongeza nguvu katika kupambana na tatizo hilo kwa kuibua miradi mbalimbali kote nchini ili kwa pamoja kuwa na mkakati wa kitaifa wa kupambana na hali hiyo ambayo ina athari kubwa kiutalii.

Mhe. Innocent Bashungwa Makamu mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira amesema kuwa suala kubwa ni kuuongeza bajeti kila mwaka katika sekta ya usimamizi wa mazingira pamoja na kuanzishwa kwa Mfuko wa Mazingira.

Nae Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira Mhe. Murad Sadick amesema kuwa Ofisi ya Makamu wa Rais iunde kikosi kazi cha kusimamia jambo husika na kulipa kipaumbele kama hatua za haraka, ikiwa ni pamoja na kuitaka Serikali kutenga fedha nyingi katika suala la utafiti ambao utasaidia kuja na suluhu katika changamoto hiyo.

Wakati huo huo, Mwenyekiti wa Kamati ya Kilimo, Mifugo na Maji Mhe. Mahmoud Mgimwa amesema kuwa kwa uwakilishi wao wa Kamati hizo tatu, jumla ya wabunge 75 kutoka Kamati wanazo ziongoza wameshafahamu tatizo hilo. “Sisi tuko tayari kuunga mkono upatikanaji wa fedha ili kuendesha tafiti mbalimbali, kama hatua za dharura na kuhakikisha Sheria iliyounda Mamlaka ya Ngorongoro inapitiwa upya ikiwa ni pamoja na kutokujenga majengo ya kudumu ili kutoathiri ikolojia ya eneo hilo.”

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Maliasili na Utalii Mhe. Nape Nnauye amesema Kamati yake ya Maliasili na Utalii na Bunge kwa ujumla watachukua hatua kama janga la Kitaifa, “Tunazungumzia uhai wetu sisi, athari za mimea na wanyama zinaathiri binadamu, hivyo lazima tupambane kwa nguvu zote kutokomeza hili jambo, madhara yake ni makubwa kwetu sisi binadamu”.

Mhe. Nnauye amewataka watafiti kutumia uzoefu kutoka nchi nyingine kuleta uhalisia katika nchi yetu na kuondoa dhana potofu ya kuamini kuwa kila tatizo jibu lake ni siasa. “Nyinyi wasomi, wataalamu andaeni majibu ya matatizo, nashauri kiundwe kikosi kazi na kuandaa majibu kwa makundi, sera, sheria, kanuni, bajeti, hamasa na usimamizi” Mhe. Nape alifafanua.

Waziri Makamba amesema kuwa pamoja na kwamba zipo Sera na Sheria mbalimbali zinazo simamia udhibiti wa viumbe vamizi wageni nchini ikiwemo sekta za Kilimo, Misitu, Uvuvi, Wanyamapori, Mifugo na Mazingira na Kanuni za Udhibiti wa Magugu Maji (2001), lakini suala hili halijapata utatuzi mahiri, hivyo msukumo zaidi na ushirikiano wa pamoja wa sekta zote katika kutafuta ufumbuzi wa changamoto hii unahitajika.

Mhe. Makamba amesema kuwa yeye kama Waziri mwenye dhamana ya Mazingira anayo mamlaka kupitia sheria ya mazingira kifungu cha 66 3 (a) “Waziri kwa kushauriana na Wizara ya sekta husika anaweza kutunga kanuni zinazo agiza kutengeneza mikakati. Programu na mipango ya kitaifa ya hifadhi na matumizi endelevu ya bioanuai”. Aidha, kifungu cha 67 2 (f) “Waziri kwa kushauriana na Wizara ya sekta anaweza kuandaa kanuni zinazoweza kubainisha ukarabati na urejeshaji mifumo ikolojia iliyoharibiwa na kuendeleza urejeshwaji wa sipishi zilizoko hatarini, pamoja na mengineyo, kwa kuendeleza na kutekeleza mipango, mikakati mingine ya usimamizi” .

Mwenyekiti wa Kikao hicho Waziri Makamba amesema mkutano huo ni mwanzo wa suluhisho la kudumu la kupata majawabu katika kuratibu utokomezaji wa mimea vamizi. “Nitaunda kikosi kazi cha kitaifa ndani ya wiki moja ijayo ili kiweze kushughulikia jambo hili na kuleta mapendekezo yatakayoleta andiko la kuchukua kama hatua za haraka, kwa mwezi mmoja” Makamba alisisitiza.

Changamoto ya viumbe vamizi wageni inagusa sekta muhimu kwa uchumi wetu ikiwemo kilimo, misitu, uvuvi, mifugo, wanyamapori, utalii na hata shughuli za uchukuzi majini.

UMOJA WA VILABU VYA WAANDISHI WA HABARI WAMPA TUZO AZORY GWANDA

$
0
0
Jopo la majaji wa Tuzo ya Daudi Mwangosi mwaka 2018 limemtangaza Mwandishi wa habari I wa gazeti la Mwananchi Azory Gwanda kuwa mshindi wa tuzo hiyo mwaka 2018.
Tuzo hiyo imetangazwa leo Jumanne Septemba 4,2018 wakati wa mkutano mkuu wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa habari Tanzania UTPC unaofanyika katika ukumbi wa Lush Garden Hotel jijini Arusha.
Kushoto ni Absalom Kibanda Mhariri mkuu kutoka gazeti la. Mtanzania akikabidhi tuzo ya Daudi Mwangosi 2018 kwa mke wa Azory Gwanda.Katikati ni rais wa UTPC,Deogratius Nsokolo
Kushoto ni Absalom Kibanda akikabidhi cheti cha utambuzi kwa mke wa Azory Gwanda
Mwenyekiti wa Jopo la Majaji wa Tuzo ya Mwangosi Mwaka 2018, Ndimara Tegambwage akitangaza mshindi wa tuzo ya Mwangosi 2018.
Mbali na kukabidhiwa tuzo hiyo,pia amekabidhiwa cheti cha utambuzi pamoja na shilingi milioni 10.
Jopo la Majaji wa Tuzo ya Mwangosi Mwaka 2018, wakwanza kulia ni mwenyekiti wa jopo hiloNdimara Tegambwage, Katikati ni mama Edda Sanga, na wengine wawili. 

Na Seif Mangwangi,Arusha
UMOJA wa vilabu vya waandishi wa habari nchini (UTPC), imemtangaza Mwandishi Azory Gwanda ambaye amepotea katika mazingira ya kutatanisha Novemba mwaka jana kuwa mshindi wa tuzo ya Daudi Mwangosi kwa mwaka 2018.

Gwanda aliyekuwa mfanyakazi wa kampuni ya mwananchi communication akiandikia gazeti la Mwananchi alipotea katika mazingira ya kutatanisha akiwa katika kazi zake za kihabari katika maeneo ya Kibiti na Rufiji.

Tuzo hiyo ya Daudi Mwangosi sambamba na kiasi cha shilingi milioni kumi (10), alikabidhiwa mke wa Gwanda, katika mkutano mkuu wa mwaka wa UTPC.

Mgeni rasmi katika utoaji wa tuzo hiyo, Absolom Kibanda aliiomba Serikali kutofumbia macho matukio ya utekaji wa waandishi wa habari kwa kuwa yanatoa ishara mbaya kwa jamii na kuminya uhuru wa habari.

Alisema Rais Dkt John Magufuli amekuwa rafiki mkubwa wa vyombo vya habari hivyo alimtaka kutoishia kuwa rafiki na badala yake achukue hatua dhidi ya matukio ya utekwaji na kuteswa kwa waandishi wa habari.

WAZIRI MKUU MAJALIWA AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA MEYA WA SHENZHEN, ATEMBELEA OFISI KUU YA KAMPUNI YA HUAWEI TECHNOLOGIES ILIYOPO SHENZHEN NCHINI CHINA

$
0
0

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Meya wa Manispaa ya Shenzhen, Bw. Wang Wanzhong kwenye ukumbi wa Hoteli ya Wuzhou nchini China, Septemba 5, 2018.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Meya wa Manispaa ya Shenzhen kwenye hoteli ya Wuzhou nchini China, Septemba 5, 2018.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akionyeshwa piano ya Kichina na msan , Xing Man baada ya mazungumzo kati yake na Meya wa Manispaa ya Shenzhen nchini China. Bw. Wang Wanzhong, Septemba 5, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea maua wakati alipowasili kwenye makao mkuu ya kampuni ya Huawei Technologies yaliyopo Shenzhen nchini China, Septemba 5, 2018. Kulia ni Makamu wa Rais wa Kampuni hiyo duniani, Li Da Feng. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama vifaa vya elektroniki wakati alipotembelea makao makuu ya kampuni ya Huawei Technologiies yaliyopo, Shenzhen nchini China, Septemba 5, 2018. Kulia ni Makamu wa Rais wa Kampuni hiyo Duniani, Li Da Feng . Kulia kwake ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Augustine Mahiga.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitoka ndani ya jengo la Makao Makuu ya Kampuni ya Huawei Techinologies yaliyopo Shenzhen nchini China baada ya kutembelea Ofisi hizo na kuzungumza na viongozi wa Kampuni hiyo, Septemba 5, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Viewing all 39112 articles
Browse latest View live