Quantcast
Channel: MTAA KWA MTAA BLOG
Viewing all 39168 articles
Browse latest View live

MKUU WA MKOA MJINI MAGHARIBI AMEGAWA KOMPYUTA 96 KWA WAHITIMU WA KIDATO CHA 6

$
0
0
Na Agness Francis,Glogu ya jamii
MKUU wa Mkoa wa mjini Magharibi Zanzibar Ayoub Mahmoud amekabidhi kompyuta mpakato kwa wanafunzi 96 waliohitimu kidato cha 6 ambao wana ufaulu wa  alama ya daraja la kwanza (devision 1) kwa kila mmoja.

Kompyuta hizo zimetolewa na taasisi ya Mimi na wewe foundation ili kusawasaidia wanafunzi hao kurahisisha kazi katika masomo yao ya elimu ya juu na kuleta hamasa kwa wale waliobaki mashule kufanya vizuri zaidi.

Mahmoud ameyasema hayo wakati wa ugawaji wa kupyuta hizo  kuwa kiwango cha Elimu kwa mwaka huu kimepanda kulinganisha na kipindi kilichopita.

"hali ya kiwango cha ufaulu katika mkoa wetu haikuwa ya kuridhisha kipindi cha nyuma ambapo tumechukua hatua za dharula na haraka ili kuongeza ufaulu wa wanafunzi kwa kushirikiana na wizara ya elimu,mwaka huu kumekuwa na ongezeko la ufaulu wanafunzi 96 daraja la 1"amesema mkuu wa mkoa huyo.

Katika ugawaji wa zawadi hizo walikuwepo wanamuziki wa aina ya kizazi kipya  waliamsha dude visiwani humo katika viwanja vya mapinduzi square.

Hamsha hamsha hizo zilipamba moto baada ya Mkuu wa Mkoa kumaliza kugawaji wa vifaa  mjini hapo.
 Msanii wa bongo fleva Dogo Janja alivyowapagawisha  wakazi wa visiwani Zanzibar wakati Mara baada ya zoezi la ugawaji wa kompyuta kwa wanafunzi hao katika viwanja vya Mapinduzi Square.
 Wanafunzi wa kidato cha 6 waliofaulu ambao wamehudhuria katika sherehe hizo zilizofanyika viwanjani mapinduzi square visiwani zanzibar wakati wa  kukabidhiwa zawadi zao.
 Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Ayoub Mahmoud kushoto pamoja na makamu wa  Rais wa Zanzibar balozi seif Iddy Kati kati, wakikabidhi kompyuta mpakato kwa mmoja wa wanafunzi waliofaulu kwa alama ya daraja   la kwanza (devision 1) kidato cha 6 katika viwanja vya mapinduzi square visiwani Zanzibar.
 Msanii wa kizazi kipya  Amba lulu akitoa burudani viwanjani hapo katika kuhitimisha  sherehe za ugawaji wa zawadi za  kompyuta kwa wanafunzi waliohitimu kidato cha 6  waliofaulu alama ya daraja la kwanza.
Msanii wa muziki wa dansi Papy Kocha akitoa shoo visiwani Zanzibar wakati wa hafla ya ugawaji wa zawadi kwa wanafunzi hao ambapo mkuu wa Mkoa Wa mjini magharibi Ayoub Mahmoud ndie aliyekabidhi katika viwanja vya Mapinduzi Square.

RAIS MAGUFULI AKIAGANA NA SPIKA MSTAAFU PIUS MSEKWA

$
0
0
Rais Dkt John Pombe Magufuli akiagana na wenyeji wake spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Pius Msekwa kulia,Ikulu ndogo,Nansio Ukerewe,Mkoani Mwanza. Septemba 5,2018. 
 Rais Dkt John Pombe Magufuli akiagana na wenyeji wake Mke wa Spika msaafu Pius Msekwa Mama Anna Abdallah Msekwa,Ikulu ndogo,Nansio Ukerewe,Mkoani Mwanza. Septemba 5,2018. Kushoto ni spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Pius Msekwa.
 Rais Dkt John Pombe Magufuli akiwa amewashika mikono wenyeji wake spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Pius Msekwa na Mkewe Mama Anna Abdallah Msekwa,Ikulu ndogo,Nansio Ukerewe,Mkoani Mwanza. Septemba 5,2018. 
  Rais Dkt John Pombe Magufuli akizungumza jambo na mwenyeji wake spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Pius Msekwa Ikulu ndogo,Nansio Ukerewe,Mkoani Mwanza. Septemba 5,2018. 

RAIS DKT. MAGUFULI AZUNGUMZA NA WANANCHI WA BUNDA WAKATI AKIWA NJIANI KUELEKEA MUSOMA MKOANI MARA

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Bunda mjini wakati akiwa njiani kuelekea Musoma mkoani Mara.
 Baadhi ya wananchi wa Wilaya ya Bunda wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli aliposimama kuwasalimia 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi kwa njia ya Simu kuhusu mgogoro wa ardhi uliopelekea Bibi Nyasasi Masige mwenye kilemba aliyekaa kudai  kunyang’anywa Kiwanja chake Wilayani Bunda.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi Bibi Nyasasi Masige kiasi cha Shilingi laki tano ili zimsaidie mara baada ya kusikiliza kero yake ya madai ya kunyanga’nywa kiwanja chake. Rais Dkt. Magufuli ameagiza uchunguzi ufanyike haraka ili haki ya bibi huyo iweze kupatikana. PICHA NA IKULU

DC TANGA AZINDUA KAMPENI JUMUISHI YA UPIMAJI WA MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA UKIMWI MKOANI TANGA

$
0
0
 MKUU wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa katika akizundua mpango wa Furaha Yangu uliokuwa na lengo la Pima,Jitambue,ishi ambapo kwa mkoa wa Tanga imezinduliwa leo kwenye viwanja vya Tangamano kulia ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga Dkt Asha Mahita
 MKUU wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa akizungumza wakati wa uzinduzi wa  mpango wa Furaha Yangu uliokuwa na lengo la Pima, Jitambue ambapo kwa mkoa wa Tanga imezinduliwa leo kwenye viwanja vya Tangamano kushoto ni Mganga Mkuu wa mkoa wa Tanga Dkt Asha Mahita na kulia ni Katibu Tawala wa wilaya ya Tanga Faidha Salim na Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Amref Tanzania Florance Temu 
 Mganga Mkuu wa mkoa wa Tanga Dkt Asha Mahita akizungumza katika uzinduzi huo kulia ni Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa ambaye alimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella kushoto ni Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Amref Tanzania Florance Temu
MKURUGENZI wa Mpango wa Furaha Yangu kutoka Shirika la  Benjamini Mkapa Rahel Sheiza akizungumza katika uzinduzi huo
 Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Amref Tanzania Florence Temu akizungumza katika uzinduzi huo
 Katibu Tawala wa wilaya ya Tanga Faidha Salim akizungumza katika uzinduzi huo kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa ambaye alimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella anayefuata ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga (RMO) Dkt Asha Mahita
 Mwakilishi wa JWTZ akizungumza katika uziunduzi huo
Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa ambaye alimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella   kulia akiwa na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga (RMO) Dkt Asha mahita wakifuatilia matukio mbalimbali kwenye uzinduzi huo
Sehemu ya wageni mbalimbali wakifuatilia uzinduzi huo kulia ni Suleimani Zumo Afisa Tarafa,nyuma waliokaa aliyevaa miwani ni Afisa Mradi wa Mkoa wa Tanga wa Kifua Kikuu na Ukimwi Dkt Anastazia Masanja
Mgenii rasmi kwenye uzunduzi huo Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa ambaye alimuwakilisha Mkuu wa mkoa wa Tanga Martine Shigella katikati mwenye koti la suti akikagua mabanda mara baada ya kufanya uzinduzi huo
Mgenii rasmi kwenye uzunduzi huo Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa ambaye alimuwakilisha Mkuu wa mkoa wa Tanga Martine Shigella katikati akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wengine kulia ni Katibu Tawala wa wilaya ya Tanga Faidha Salim kushoto ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga Dkt Asha Mahita
Wasanii wa kundi la Tanga Kwanza wakitumbuiza kwenye uzinduzi huo

KATIKA kuendeleza kuchangia juhudi za Serikali kuimarisha huduma za Afya ikiwemo huduma za Ukimwi,Shirika la Benjamini Mkapa kupitia Shirika lisilo la Kiserikali la Amref chini ya ufadhili wa Mfuko wa Dunia wa Kupambana na Ukimwi Kifua Kikuu na Malaria (Global Fund) inatekeleza mradi wa miaka mitatu 2018-2020 Desemba.

Mradi huo wenye kufanya upimaji Jumuishi wa Maambukizi ya Virusi vya Ukimwi katika Jamii na Kuhamasisha Jamii kubadili tabia hatarishi ili kuweza kusaidia kupunguza maambukizi hayo kwa jamii .

Hayo yalisemwa na Afisa Mradi wa Mkoa wa Tanga wa Kifua Kikuu na Ukimwi Dkt Anastazia Masanja wakati wa uzinduzi wa Kampeni hiyo iliyofanywa na Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa kwenye viwanja vya Tangamano mjini hapa na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga Dkt Asha Mahita,Katibu Tawala wa wilaya ya Tanga Faidha Salim,Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Amref Tanzania Florence Temu  na Mkurugenzi wa Mpango wa Furaha Yangu kutoka Shirika la  Benjamini Mkapa Foundation Rahel Sheiza akizungumza katika uzinduzi huo

Alisema kupitia mradi huo wa kupambana na kifua kikuu na Ukimwi ambao utekelezaji wake umeanza mwezi Juni 2018,Taasisi imepewa wilaya mbili ambazo ni Kilindi na Pangani kwa Mkoa wa Tanga .

"Kwa kipindi hiki Shirika la Benjamini Mkapa linatarajia kufikia kata zote 35 ambapo kati ya hizo 21 ni za wilaya ya Kilindi na 14 ni za wilaya ya Pangani lengo la upamaji kwa kila kati ni kuweza kupima watu 2081(Jumla 72,839 kwa kata 35).

Huduma ambazo zimekuwa zikitolewa ni pamoja na uchunguzi wa awali wa kifua kikuu ambapo watu wote 7082 waliohudhuria waliweza kuchunguzwa ambao watu 220 walikutwa na dalili za kifua kikuu na kupewa rufaa kwenda Hospitali ya wilaya kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

"Kwa upande wa shinikizo la damu ambapo jumla ya watu 5269 walipimwa kati yao 182 walikutwa na shinikizo la damu lisilokuwa la kawaida "Alisema.

Afisa Mradi huyo alisema pia huduma za uzazi wa mpango zilitolewa ikiwamo vipandikizi,sindano,vidonge ambapo jumla ya wakina mama waliopata huduma hiyo walifikia 188 na ugawaji wa kondomu ambapo jumla ya kondomu 5000 zimegawiwa.

"Lakini pia tuliotoa elimu ya mfuko wa Afya ya Jamii ikiwemo ya mabadiliko ya tabia kupitia sinema na vikundi vya ngoma "Alisema

Ujumbe Kutoka MCT Wakutana na Katibu Mkuu Wizara ya Habari jijini Dodoma

$
0
0
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Suzan Mlawi  akizungumza wakati wa kikao baina yake na wajumbe wa Muungano wa Watetezi wa Haki ya kupata Taarifa (CORI) na Baraza la Habari Tanazania (MCT),  walipofika wizarani hapo kwa ajili ya kuwasilisha mapendekezo ya maboresho ya Sheria ya Huduma za Habari ya mwaka 2016 leo jijini Dodoma. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari – MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi, Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Nicolas William Mkapa na mjumbe wa bodi ya Baraza la Habari Tanazania (MCT), Wallace Maugo.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari – MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi akizungumza wakati wa kikao baina ya Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Suzan Mlawi(wapili kushoto) na wajumbe wa Muungano wa Watetezi wa Haki ya kupata Taarifa (CORI) pamoja na Baraza la Habari Tanazania (MCT),  walipofika wizarani hapo kwa ajili ya kuwasilisha mapendekezo ya maboresho ya Sheria ya Huduma za Habari ya mwaka 2016 leo jijini Dodoma. Kutoka kulia ni Kiongozi wa MCT, James Marenga, na mjumbe wa bodi ya Baraza la Habari Tanazania (MCT), Wallace Maugo na Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Nicolas William Mkapa.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bibi.Suzan Mlawi(katikati) akipokea nyaraka yenye mapendekezo ya maboresho ya Sheria ya Huduma za Habari ya Mwaka 2016 kutoka kwa Mjumbe wa Bodi ya Baraza la Habari Tanzania(MCT), Wallace Maugo(kulia) wakati wa kikao baina yake na wajumbe wa Muungano wa Watetezi wa Haki ya kupata Taarifa (CORI)na MCT  walipofika wizarani hapo kwa ajili ya kuwasilisha mapendekezo hayo leo jijini Dodoma. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi, Rodney Thadeus, Mkurugenzi wa Idara ya Habari – MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi na Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Nicolas William Mkapa (katikati).
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bibi.Suzan Mlawi(katikati) akimsikiliza kwa makini kiongozi wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), James Marenga (kulia) wakati wa kikao baina yake na wajumbe wa Muungano wa Watetezi wa Haki ya kupata Taarifa (CORI) na Baraza la Habari Tanazania (MCT),  walipofika wizarani hapo kwa ajili ya kuwasilisha mapendekezo ya maboresho ya Sheria ya Huduma za Habari ya mwaka 2016 leo jijini Dodoma. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari –MAELEZO, Bibi. Zamaradi Kawawa, Mkurugenzi Msaidizi, Rodney Thadeus, Mkurugenzi wa Idara ya Habari – MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi, Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Nicolas William Mkapa na mjumbe wa bodi ya Baraza la Habari Tanazania (MCT), Wallace Maugo.
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari – MAELEZO, Rodney Thadeus akichangia mada wakati wa kikao baina ya Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bibi.Suzan Mlawi(wanne kushoto) wakati wa kikao baina yake na wajumbe wa Jumuiya ya Watetezi wa Haki za Kupata Taarifa na Baraza la Habari Tanazania (MCT),  walipofika wizarani hapo kwa ajili ya kuwasilisha mapendekezo ya maboresho ya Sheria ya Huduma za Habari ya mwaka 2016 leo jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bibi.Suzan Mlawi(katikati) akimsikiliza kwa makini Mjumbe wa Muungano wa Watetezi wa Haki ya kupata Taarifa (CORI), Dkt. Samwilu Mwafisi (kulia) wakati wa kikao baina yake na wajumbe wa muunganiko huo na Baraza la Habari Tanazania (MCT),  walipofika wizarani hapo kwa ajili ya kuwasilisha mapendekezo ya maboresho ya Sheria ya Mkurugenzi wa Idara ya Habari – MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi, Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Nicolas William Mkapa, Mjumbe wa Bodi ya Baraza la Habari Tanazania (MCT), Wallace Maugo na Kiongozi wa MCT, James Marenga.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bibi.Suzan Mlawi(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Muungano wa Watetezi wa Haki ya kupata Taarifa (CORI) pamoja na Baraza la Habari Tanzania (MCT) mara baada ya kumaliza kikao leo Jijini Dodoma. Waliokaa kutoka kushoto ni Mjumbe wa Bodi ya MCT, Wallace Maugo, Mkurugenzi wa Idara ya Habari – MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi, Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Nicolas William Mkapa, na Mshauri wa Mradi wa Ufuatiliaji wa Wamiliki wa Vyombo vya Habari (MOM), Dkt. Samwilu Mwafisi. (Picha na: Idara ya Habari – MAELEZO).

Uchukuzi SC yajifua kwa SHIMIWI

$
0
0


Wachezaji wa timu ya wanawake na wanaume ya kuvuta Kamba ya Klabu ya Uchukuzi (USC) wakifanya mazoezi jana nyuma ya jengo la Aviation Banana ya kujiandaa na mashindano ya Shirikisho la Michezo ya Wizara, Idara za Serikali na Ofisi za Wakuu wa Mikoa (SHIMIWI), iliyopangwa kuanza Septemba 25 mkoani Dodoma.
Katibu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Bw. Vallery Chamulungu (wa kwanza kulia) akiwa ni miongoni mwa wachezaji wa klabu ya Uchukuzi walioanza mazoezi jana nyuma ya jengo la Aviation wakijiandaa na mashindano ya Shirikisho la Michezo ya Wizara, Idara za Serikali na Ofisi za Wakuu wa Mikoa (SHIMIWI), iliyopangwa kufanyika mkoani Dodoma kuanzia Septemba 25, 2018.
Katibu Mkuu wa Klabu ya Uchukuzi (USC), Bw. Mbura Tenga (katikati) jana akijumuika na wachezaji wa klabu hiyo kwenye viwanja vya nyuma ya jengo la Aviation kufanya mazoezi ya kujianda na mashindano ya Shirikisho la michezo ya Wizara, Idara za Serikali na Ofisi za Wakuu wa Mikoa (SHIMIWI), iliyopangwa kufanyika mkoani Dodoma kuanzia Septemba 25, 2018.
Bi. Sharifa Amiri (kulia) akifanya mazoezi ya mchezo wa bao na Bw. Ambakise Mwasunga jana kwenye viwanja vya nyuma ya Jengo la Aviation wakijianda na mashindano ya Shirikisho la michezo ya Wizara, Idara za Serikali na Ofisi za Wakuu wa Mikoa (SHIMIWI), iliyopangwa kuanza Septemba 25, 2018 mkoani Dodoma.
Wachezaji wa mpira wa miguu wa Klabu ya Uchukuzi (USC) jana wakijifua kwenye viwanja nyuma ya Jengo la Aviation wakijiandaa na mashindano ya Shirikisho la Michezo ya Wizara, Idara za Serikali na Ofisi za Wakuu wa Mikoa (SHIMIWI), inayotarajiwa kufanyika mkoani Dodoma kuanzia Septemba 25 hadi Oktoba 6, 2018. 

Na Mwandishi Wetu
KLABU ya michezo ya Uchukuzi (USC) imeanza kujifua kwa ajili ya kushiriki mashindano ya Shirikisho la Michezo ya Wizara, Idara za Serikali zinazojitegemea, Wakala wa Serikali na Ofisi za Wakuu wa Mikoa (SHIMIWI), itakayoanza Septemba 25 kwenye viwanja mbalimbali mkoani Dodoma.

Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa klabu hiyo, Bw. Mbura Tenga amesema wameanza kujifua kwa nguvu ili kurudi na ubingwa wa michezo mbalimbali waliyoshinda kwa mara ya mwisho michezo hiyo ilipofanyika mwaka 2014.

Bw. Tenga amesema USC watashiriki kwenye michezo tisa, ambayo imeandaliwa na SHIMIWI, ambayo ni mpira wa miguu, netiboli, kuvuta Kamba, riadha, bao, karata, draft, baiskeli na Darts.

“Tunauhakika wa kwenda kufanya vizuri kwani timu imeanza mazoezi tayari ingawa muda ni mdogo, ila ninaamini tutafanya vizuri,” amesema Bw. Tenga.

USC inatetea vikombe vinne walivyoshinda mwaka 2014, ambavyo ni Darts – wanaume(washindi wa kwanza); mpira wa miguu (washindi wa pili); na Kamba – wanaume na baiskeli - wanawake (washindi wa tatu).

Ratiba iliyotolewa na SHIMIWI inaonesha katika ufunguzi mabingwa watetezi katika mchezo wa kuvuta Kamba wanaume timu ya Ofisi ya Rais Ikulu itavutana na MSD; nao wanawake wa RAS Iringa ambao ni mabingwa watetezi watavutana na Viwanda; huku katika mpira wa miguu Wizara ya Elimu watakutana na Ukaguzi.

Michezo hiyo ambayo pamoja na kuunganisha wafanyakazi wa umma wa maeneo mbalimbali pia huleta burudani kwa wakazi wa eneo husika.

YALIYOJIRI BUNGENI LEO JIJINI DODOMA

$
0
0
Mwenyekiti wa Bunge na Mbunge wa Ilala, Mhe. Mussa Zungu (kushoto) akizungumza na Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Mhe. Dan Kazungu (kulia) alipomtembelea leo Bungeni Mjini Dodoma. Katika mazungumzo hayo Mhe. Zungu alimuwakilisha Spika wa Bunge. Balozi huyo ambae ni mpya alikuja kwa lengo la kujitambulisha kwa Mhe. Spika na kumueleza nia ya kujenga jengo lao la Ubalozi wa Kenya hapa Jijini Dodoma katika vile viwanja walivyopewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli.
Mwenyekiti wa Bunge na Mbunge wa Ilala, Mhe. Mussa Zungu (kushoto) akimsikiliza Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Mhe. Dan Kazungu (kulia) alipomtembelea leo Bungeni Mjini Dodoma. Katika mazungumzo hayo Mhe. Zungu alimuwakilisha Spika wa Bunge. Balozi huyo ambae ni mpya alikuja kwa lengo la kujitambulisha kwa Mhe. Spika na kumueleza nia ya kujenga jengo lao la Ubalozi wa Kenya hapa Jijini Dodoma katika vile viwanja walivyopewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli.
Mwenyekiti wa Bunge na Mbunge wa Ilala, Mhe. Mussa Zungu (kushoto) akisalimiana na Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Mhe. Dan Kazungu (kulia) alipomtembelea leo Bungeni Mjini Dodoma, kwa Katika mazungumzo hayo Mhe. Zungu alimuwakilisha Spika wa Bunge, Pia Balozi huyo ambae ni mpya alikuja kwa lengo la kujitambulisha kwa Mhe. Spika na kumueleza nia ya kujenga jengo lao la Ubalozi wa Kenya hapa Jijini Dodoma katika vile viwanja walivyopewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli.
Mbunge wa Muleba Kusini, Mhe. Anna Tibaijuka (kushoto) akiteta jambo na Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Mhe. Dan Kazungu alipomtembelea leo Bungeni Mjini Dodoma.
Mwenyekiti wa Bunge na Mbunge wa Ilala, Mhe. Mussa Zungu anaemuwakilisha Spika Ndugai, Wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Masuala ya Ukimwi wakimsikiliza Ofisa Mtendaji Mkuu wa Baraza la Taifa la Watu Wanaoishi na Virusi vya Ukimwi Tanzania (NACOPHA), Ndg. Deogratius Rutatwa (Kulia) wakati akiwashukuru Waheshimiwa kwa Kujitoa katika Shughuli Mbali mbali zinazohusiana na  Baraza hilo, moja wapo likiwa ni upimaji wa Virusi vya Ukimwi kwa hiari.
Mwenyekiti wa Bunge na Mbunge wa Ilala Mhe. Mussa Zungu (katikati) anaemuwakilisha Spika Ndugai akikabidhiwa cheti kutoka kwa Ofisa Mtendaji Mkuu wa Baraza la Taifa la Watu Wanaoishi na Virusi vya Ukimwi Tanzania (NACOPHA), Ndg. Deogratius Rutatwa (Kushoto) ikiwa ni Shukrani kwa Kujitoa kwao katika Shughuli Mbali mbali zilizoratibiwa na Baraza hilo, moja ya tukio likiwa ni upimaji wa Virusi vya Ukimwi kwa hiari, baada ya kikao kilichofanyika leo Bungeni Jijini Dodoma. kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Masuala ya Ukimwi, Mhe. Oscar Mukasa
Mwenyekiti wa Bunge na Mbunge wa Ilala, Mhe. Mussa Zungu (mwenye tai nyeusi mbele), anaemuwakilisha Spika Ndugai akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Masuala ya Ukimwi na Watendaji Wakuu kutoka Baraza la Taifa la Watu Wanaoishi na Virusi vya Ukimwi Tanzania (NACOPHA), baada ya kikao kilichofanyika Bungeni Jijini Dodoma. Kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Masuala ya Ukimwi, Mhe. Oscar Mukasa na kulia kwake ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Baraza la Taifa la Watu Wanaoishi na Virusi vya Ukimwi Tanzania (NACOPHA), Ndg. Deogratius Rutatwa (Kulia)


Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Masuala ya Ukimwi, Mhe. Oscar Mukasa (katikati) akizungumza na ugeni kutoka Ubalozi wa Marekani wanahusika na utekelezaji wa Miradi ya Ukimwi, Wajumbe wa kamati hiyo. Ugeni ulioongozwa na Mratibu Mkazi wa PEPFAR, Ndg. Brian Rettmann (kulia kwake) katika kikao kilichofanyika leo Bungenii Jijini Dodoma.
(PICHA NA DEONISIUS SIMBA - OFISI YA BUNGE)

KESI ZINAZOHUSU MASUALA YA FIDIA KWA WAFANYAKAZI KUSIKILIZWA MFULULIZO: DKT. ELIEZER FELESHI

$
0
0
  MHESHIMIWA Jaji Dkt. Eliezer M.Feleshi, Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, (aliyesimama) akitoa hotuba ya ufunguzi wa mafunzo kwa mahakimu wakazi wa wilaya na mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Lindi, Mtwara na Morogoro kuhusu Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi Sura  263 marejeo ya mwaka 2015 iliyoanza Septemba 5, 2018 mkoani Morogoro. Semina hiyo imeratibiwa kwa ushirikiano wa Chuo Cha Uongozi wa Mahakama Lushoto na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF). Wengine pichani ni Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, ambaye pia ni Mkuu wa Chuo hicho Dkt. Paul F. Kihwelo (kulia) na Mkurugezni Mkuu wa WCF, Bw.Masha Mshomba.


  Na K-VIS BLOG/Khalfan Said, Morogoro
MHESHIMIWA Jaji Dkt. Eliezer M.Feleshi, Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, amesema hategemei kesi zinazohusiana na masuala ya fidia kwa wafanyakazi zikichelewa pindi mashauri yake yanapofika mahakamani.
Dkt. Feleshi ameyasema hayo Mjini Morogoro Septemba 5, 2018 wakati akifungua mafunzo kwa mahakimu kutoka mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Mtwara, Lindi na Morogoro yanayoratibiwa na Chuo Cha Uongozi wa Mahakama Lushoto na kuendeshwa na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) yanayofanyika kwa siku mbili kuanzia leo.
“Sitegemei kesi za namna hii ziingie kwenye kundi la njoo kesho… njoo kesho, mashahidi wake  ni wangapi? Kesi za namna hii zikiingia zisikilizwe mfululizo, kumbukeni inamuhusu mtu aliyeumia, inagusu uhai, inahusu ulemavu wa kudumu kwa hiyo nyuma kuna wategemezi na yeye mwenyewe kwa hiyo inahusu maisha ya mtu, pia ushahidi wake uko wazi na adhabu zake ziko bayana” Alifafanua Dkt. Feleshi.
Aidha Mhe. Jaji Kiongozi alisema, kila mfanyakazi aliyeumia au kuugua kutokana na kazi anayo haki ya kupata fidia stahiki na kwa wakati kwa mujibu wa sheria na kwa yule atakayefariki katika mazingira hayo basi wategemezi wake nao wanapatiwa haki zao zilizoanishwa kisheria.
Alisema huduma ya Hifadhi ya Jamii ni haki inayotambulika na kulindwa na Katiba, ibara ya 11 (1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 pamoja na mambo mengine inatamka kwenye ibara ndogo kwamba Mamlaka ya Nchi itaweka utaratibu unaofaa kwa ajili ya kufanikisha utekelezaji wa haki ya mtu kufanya kazi, haki ya kujipatia elimu na haki ya kupata msaada kutoka kwa jamii wakati wa uzee, maradhi, au hali ya ulemavu na katika hali nyinginezo za mtu kuwa hajiwezi, na bila kuathiri haki hizo Mamlaka ya Nchi itaweka utaratibu wa kuhakikisha kwamba kila mtu anaishi kwa jasho lake.
“Hayo ni maneno ambayo yamewekwa kwenye Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa hiyo ni haki ambayo imetamkwa na inalidwa na Sheria na kwa kuzingatia matakwa hayo ya kikatiba ndio maana ilitungwa sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi iliyoanzisha Mfuko huu wa WCF.” Alifafanua Dkt. Feleshi.
Alisema Mafunzo hayo kwa Mahakimu kuhusu utekelezaji wa sheria hiyo, yana manufaa makubwa na ndio maana yameratibiwa na Chuo cha Uongozi   wa Mahakama ambacho ndio chenye jukumu la kutoa elimu kwa watumishi wa mahakama.
“Katika sheria ya sasa kwa mujibu wa vifungu vya 22 (1) 46 na 48 na majedwali ya 2,3 na 4 ulipaji wa fidia unazingatia zaidi uhalisia wa tukio, kiwango cha hasara na madhara ambavyo vinafanya fidia inayolipwa ikokotolewe kwa kufuata asilimia ya vigezo hivyo na malipo ya ujira wa mwezi au malipo ya mwisho ya mhusika.” Alibainisha Dkt. Feleshi.
“Takwimu zinaonyesha kuwa Mfuko umekwishalipa Fidia kiasi cha Shilingi bilioni 4.4 tangu ulipoanza kulipa fidia hadi Julai 31, 2018, na hii inaonyesha umuhimu wa Mfuko huu kwa jamii, taifa lakini hata sisi wenyewe kama watumishi.” Alisema.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, Bw. Masha Mshomba alisema kwa sasa Mfuko umeweka kipaumbele kwenye utoaji elimu kwa wadau mbalimbali wakiwemo Waheshimiwa Mahakimu ili na wao waelewe vizuri shughuli za Mfuko na jinsi ya kutekeleza sheria iliyoanzisha Mfuko.
Kwa sasa Mfuko umekwisha wafikia wadau wengi na kumekuwepo na mabadiliko makubwa katika uelewa wa kutekeleza sheria hii na ni wachache sana ambao bado wanakuwa wazito kutekelza sheria, alisema Bw. Mshomba.
Washiriki wa mafunzo hayo wanatarajiwa kujifunza sheria inayosimamia shughuli za Mfuko, lakini pia muundo na shighuli za Mfuko na taratibu za utoaji Fidia.

 Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba, akizungumza kwenye semina hiyo.
 Baadhi ya Wahwshimiwa Mahakimu Wakazi Wafawidhi wa Mahakama nchini.
Mheshimiwa Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya Kisarawe Mkoani Pwani, Mhe. Devota Kisoka.
 Mhe. Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mtwara, Bi.Elizabeth S. Missana, akipitia kipperushi chenye maelezo kuhusu shughuli za Mfuko.
  Baadhi ya Waheshimiwa Mahakimu Wakazi Wafawidhi wa Mahakama nchini.
 Hakimu Mfawidhi wa Mahaka ya Hakimu Mkazi Morogoro, Mheshimiwa Elizabeth Nyembele, akizungumza kwenye semina hiyo.
Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Kibaha, Mhe.Joyce J. Mkhoi, akitoa maoni yake kwenye semina hiyo.
 Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba, akishauriana jambo na Mkuu wa Huudma za Sheria wa Mfuko huo, Bw.Abraham Siyovelwa
 Bw. Mshomba (katikati), akimtambulisha Dkt. Feleshi kwa Mkurugenzi wa Uendeshaji WCF, Bw. Anselim Peter, wakati akiwasili ukumbini.
 Dkt. Feleshi akisalimiana na Bw. Siyovelwa.
  MHESHIMIWA Jaji Dkt. Eliezer M.Feleshi, Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, (kushoto), na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Bw. Masha Mshomba, wakiwa na furaha baada ya Dkt. Felishi kufungua mafunzo ya kujenga uwezo na uelewa wa sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi Kifungu namba 5 [Sura ya 263 iliyofanyiwa marejeo mwaka 2015] kwa mahakimu Wakuu Wakazi wa Mikoa na Wilaya kutoka mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Morogoro, Lindi na Mtwara. Semina hiyo iiyoandaliwa kwa ushirikiano kati ya Chuo Cha Uongozxi wa Mahakama Lushoto na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) imeanza Septemba 5, 2015 mjini Morogoro. 
 Kutoka kushoto ni Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, Mhe. Godfrey Isaya, Mhe. Dkt. Feleshi, Mhe. Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania na Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa  Mahakama Lushoto, Mhe. Dkt. Jaji Paul Kihwelo, Mkuu wa Huduma za Sheria WCF, Bw. Abraham Siyovelwa.
Mkuu wa Huduma za Sheria WCF, Bw. Abraham Siyovelwa, akitoa mada kuhusu sharia zinazosimamia Mfuko huo.
Mkurugenzi wa Uendeshaji WCF, Bw. Anselim Peter, akitoa mada
Afisa Uhusiano na Mawasiliano Mwandamizi wa WCF, Bw. Sebera Fulgence, akiongoza semina hiyo.
MHESHIMIWA Jaji Dkt. Eliezer M.Feleshi, Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, akisalimiana na Afisa Sheria wa WCF, Bw. Deo Victor.
Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, ambaye pia ni Mkuu wa Chuo Dkt. Paul F. Kihwelo, (kulia), akisindikizwa na Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro, Mhe.Elizabeth Nyembele, (kushoto) na Afisa Sheria wa WCF, Bw. Deo Victor.
Mhadhiri Msaidizi wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA), Mhe.Lamek Samson akiwa na Afisa Uhusiano na Mawasiliano Mwandamizi wa WCF, Bw. Sebera Fulgence.

TMA kupunguza athali zitokanazo mabadiliko ya hali ya hewa kwa wananchi

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Blogu ya Jamii.
MAMLAKA  ya Hali ya Hewa nchini (TMA) leo Septemba 5, 2018 imesema tathmini inaonesha kuwa kwa sasa wananchi wengi wamepata uelewa mkubwa wa hali ya hewa hali ambayo inatarajiwa kupunguza athari zitokanazo na mabadiliko ya hali ya hewa kwa wananchi kuchukua hatua stahiki katika kupunguza majanga.

Imeelezwa kuwa, tathimini zinaonyesha kuwa wananchi wamekuwa wakifatilia sana utabiri wa hali ya hewa kuliko miaka ya nyuma  kutokana na kuwepo kwa viwango sahihi. Vinavyotolea na TMA.

Akizungumza kwenye ufunguzi wa  warsha ya wanahabari kuhusu utabiri wa mvua za msimu wa vuli za Otoba mpaka Desemba 2018, jijini  Dar es salaam, Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dkt Agnes Kijazi amesema, usambazwaji wa taarifa za hali ya hewa unaofanywa na vyombo mbali mbali vya habari juu zimewezakusaidia kuongeza uelewa kwa wananchi, na mpaka sasa wengi wamekuwa wakifuatilia utabiri huo na kuutumia ipasavyo.

Taarifa ya hali ya hewa taarifa ya hewa ni muhimu sana kwa jamii katika kila sekta mbali mbali ka vule ya Kilimo, afya, miundombinu na zinginezo hasa katika wakati huu wa kuelekea kuwa na uchumi wa viwanda.

"Taarifa za hali ya hewa ni muhimu sana kwa Jamii katika kila sekta, ukizungumzia uchumi wa viwanda lazima utahitaji taarifa za hali ya hewa na hata katika katika sekta zingine zote kama vile, Kilimo,Afya,Mifugo,Nishati,Usafiri wa anga,usafiri wa kwenye maji usafiri wa nchi kavu ,Utalii na Maliasili, elimu na sekta nyingine nyingi."amesema Dkt Kijazi.

Alisema utabiri unaotolewa unasaidia wananchi kuchukua hatua stahiki ili kupunguza athari zinazotarajiwa ikiwemo mafuliko na kusaidia wakulima katika kufanya shughuli zao za kilimo.

Dkt Kijazi alisema Wananchi wengi kwa sasa  wanafahamu na kufatilia utabiri wa hali ya hewa kwa sababu unawasaidia katika shughuli zao.
Dkt Kijazi amesema utabiri wa msimu wa mvua za vuli, Oktoba-Desemba 2018 utatolewa kesho.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini, (TMA), Dkt Agnes Kijazi (katikati) akizungumza wakati wa ufunguzi wa warsha ya wanahabari kuhusu utabiri wa mvua za msimu za Vuli, Oktoba hadi  Desemba 2018 iliyofanyika leo katika Ofisa za mamlaka hiyo jijini Dar es Salaam, kulia kwake ni Kaimu Mkurugenzi wa Utabiri wa TMA Samwel Mbuya na  kushoto kwake ni Hellena Msemo, Meneja utendaji.
Wanahabari wakifuatilia kwa makini mada juu ya utabiri wa hali ya hewa kwa msimu wa mvua za Vuli za Oktoba hadi Desemba 2018.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini, (TMA), Dkt Agnes Kijazi akiwa kwenye picha ya pamoja na waandishi wa habari leo kwenye ufunguzi wa  warsha ya wanahabari kuhusu utabiri wa mvua za msimu wa vuli za Otoba mpaka Desemba 2018, jijini  Dar es Salaam.

CHAMA CHA WAAJIRI WAANZA MAFUNZO KUNDI LA TATU LA PROGRAMU YA MWANAMKE WA WAKATI UJAO

$
0
0

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.


CHAMA cha waajiri Tanzania (ATE) wameanza kutoa mafunzo ya kundi la tatu kwa wafanyakazi wa kike ikiwa ni programu ya mwanamke wa wakati ujao (Female Future) wakishirikiana na Shirikisho la Vyama vya Waajiri Nchini Norway (Confederation Of Norway Enterpise NHO) kwa ajili ya kuboresha ufanisi kwa wafanyakazi wa kike mahali pa kazi nchini Tanzania.

Mafunzo hayo yatakayokuwa katika kozi tatu yanalenga zaidi katika kuwapa mwongozo bora wafanyakazi wa kike ili waweze kumudu nafasi zao za uongozi katika makampuni na bodi za wakurugenzi.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi wa ATE Dkt Aggrey Mlimuka amesema kuwa wameshasajili wafanyakazi wa kike 24 kutoka makampuni 11 ambayo yamefadhili mafunzo hayo na kundi hili ni la tatu toka waazne kutoa mafunzo hayo na tayari wanawake 60 wameweza kupata programu hiyo.

Dkt Mlimuka amesema mafunzo haya yatachochea mazingira bora ya kujifunza na kuendeleza viongozi kwa maendeleo ya kampuni na yatawapa ujasiri wanawake kuomba nafasi za uongozi sehemu mbalmbali ikiwemo bodi ya wakurugenzi..

Amesema kuwa mafunzo hayo yatatolewa juu ya uongozi, ufanisi katika bodi, ufanisi katika mawasiliano na katika maisha yao kwa kushirikiana na Taasisi ya Usimamizi wa Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika (
ESAMI) kwa muda wa siku 14 muda wa darasani kwa kozi zote tatu ndani ya miezi tisa na yatafanyika kwa mfumo wa kuunganishwa na shughuli za kila za muhusika mahali pake pa kazi.

" Tumewasajili wahitimu wote kama wafanisi wa bodi za wakurugenzi na uongozi, ujuzi hui utaendelezwa katika kizazi cha baadae lengo likiwa ni kuongeza ufanisi na mazingira bora ya kazi," amesema.

Dkt Mlimuka aliongeza kuwa ATE inatambua ushiriki kutoka makampuni hayo kama chachu ya kuendeleza mipango mikakati katika usawa, elimu bora na mazingira bora ya kazi katika kuinua uchumi wa nchi.

Mbali na hilo amesema kuwa wanatarajia kufanya mkutano wa pamoja kwa wanawake wote waliofanikiwa kupata mafunzo hayo kuona wamefikia wapi kabla na baada ya kupata programu ya mwanamke wa wakati ujao pia hafla hiyo itatoa mwongozo wa mwendelezo wa kila mwaka kuwa na makongano hayo. 

Programu huu ya mwanamke wa wakati ujao (Female Future) ilizinduliwa na Makamu wa Rais Samia Hassan Suluhu mwaka 2016 ambapo ililenga zaidi kuongeza ufanisi kwa waajiri wa kike mahali pa kazi pamoja na mambo mengine ilibanishiwa kuwa wahusika wataunda mtandao wa kubadilishana uzoefu katika fani mbalimbali.

Makampuni yaliyoshirikiana na ATE ni Barclays Bank Tanzania, Commercial Bank of Africa, Equinor Tanzania AS, Global Health Program- Tanzania (HJFMRI), Grumeti Reserves, Kilimanjaro Airports Developments Co. (KADCO), Legal and Human Rights Centre (LHRC), National Housing Corporation (NHC), Social Action Trust Fund (SATF), Standard Chattered Bank na TOL Gases Ltd.
Mkurugenzi wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) Dkt Aggrey Mlimuka akizungumza na wanawake walioko katika mafunzo ya proramu ya mwanamke wa wakati ujao (Female in future) yenye malengo ya kumpa fursa mwanamke 
juu ya uongozi, ufanisi katika bodi, ufanisi katika mawasiliano 
wakati akizindua leo Jijini Dar es Salaam. Chini akizungumza na wanahabari.




Mhadhiri mwandamizi wa




Taasisi ya Usimamizi wa Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika (ESAMI) Prof Apollonia Kerenge akizungumza na wanawake waliokatika mafunzo ya mwanamke wa wakati ujao (female in future) iliyoandaliwa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) iliyozinduliwa leo Jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) Dkt Aggrey Mlimuka akiwa katika picha ya pamoja na wanawake walioko katika mafunzo ya proramu ya wanawake wa wakati ujao (female in future) iliyozinduliwa leo Jijini Dar es Salaam .

RAIS DKT. MAGUFULI AZUNGUMZA NA MAMIA YA WANANCHI WA MUSOMA MKOANI MARA BAADA YA KUZINDUA MIRADI YA MAENDELEO MKOANI HUMO

$
0
0


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia wananchi wa Musoma waliokusanyika katika viwanja vya Mukendo vilivyopo Musoma mjini kwa ajili ya kumsikiliza mara baada ya kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo mkoani Mara.
Sehemu ya wananchi waliohudhuria mkutano huo uliofanyika Musoma mjini katika viwanja vya Mukendo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia dawati ambalo alikuwa akilitumia kujisomea Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere katika Shule ya Msingi Mwisenge Musoma. Hayati Mwalimu Nyerere alisoma shule hapo elimu ya Msingi tarehe 20/4/ 1934 hadi 1/10/1936.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Maji Profesa Makame Mbarawa, mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Ufaransa AFD Stephanie Mouen wakanza kulia mwenye wakivuta utepe kuashiria ufunguzi wa mradi wa maji safi na usafi wa mazingira katika manispaa ya Musoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Waziri wa Maji Profesa Makame Mbarawa wakisikiliza maelezo ya mradi wa wa maji safi na usafi wa mazingira katika manispaa ya Musoma mjini Mkoani Mara kabla ya kuuzindua.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Stephanie Mouen mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Ufaransa AFD Agence Francaise De Development waliosaidia katika mradi huo wa maji Musoma mkoani Mara.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akivuta utepe pamoja na Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isaack Kamwelwe wakivuta utepe kuashiria ufunguzi wa barabara ya kutoka Mpakani mwa Simiyu/Mara na Musoma km 85.5.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isaack Kamwelwe mara baada ya kufungua barabara ya kutoka Mpakani mwa Simiyu/Mara na Musoma km 85.5.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Musoma mjini (hawaonekani pichani) katika viwanja vya Mukendo Musoma mkoani Mara. Picha namba 16. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoka katika bweni alilokuwa akilala Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere katika Shule ya Msingi Mwisenge Musoma. Hayati Mwalimu Nyerere alisoma shule hapo elimu ya Msingi kuanzia tarehe 20/4/ 1934 hadi 1/10/193. PICHA NA IKULU


BODI YA USAJIRI YAWAHANDISI WASHEREKEA MIAKA 50 YA KUANZISHWA KWAKE

$
0
0
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi akizungumza na wahandisi na wakandarasi wakati wa hafla ya kusheherekea miaka 50 ya Bodi ya Usajili ya Wahandisi (ERB) tangu ianzishwe mwaka 1968.
Kaimu Msajili wa Bodi ya Usajili ya Wahandisi (ERB), Mhandisi Patrick Barozi (kulia), akitoa utambulisho kwa wahandisi na wageni waalikwa wakati wa hafla ya kusheherekea miaka 50 ya Bodi hiyo tangu ianzishwe mwaka 1968.
Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili ya Wahandisi (ERB), Profesa Ninatubu Lema (kulia) akitoa neon la utangulizi kwa mgeni rasmi wakati wa hafla ya kusheherekea miaka 50 ya Bodi hiyo tangu ianzishwe mwaka 1968.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Elias Kwandikwa akimkaribisha mgeni rasmi, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi kuzungumza na wahandisi na wakandarasi wakati wa hafla ya kusheherekea miaka 50 ya Bodi ya Usajili ya Wahandisi (ERB) tangu ianzishwe mwaka 1968.
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi akimkabidhi tuzo ya heshima Naibu Balozi wa Norway Tanzania Trygve Bendiksby wakati wa hafla ya kusheherekea miaka 50 ya Bodi ya Usajili ya Wahandisi (ERB) tangu ianzishwe mwaka 1968.
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi (kulia) akiteta jambo na Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Elias Kwandikwa wakati wa hafla ya kusheherekea miaka 50 ya Bodi ya Usajili ya Wahandisi (ERB) tangu ianzishwe mwaka 1968.
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi akimkabidhi tuzo ya heshima Mhandisi Milton Nyerere kwa niaba ya familia ya Hayati Baba wa Taifa Mwl. Julius Nyerere kwa kutambua mchango Baba wa Taifa katika kuanzishwa kwa Bodi ya Usajili ya Wahandisi (ERB) wakati wa hafla ya kusheherekea miaka 50 ya Bodi hiyo tangu ianzishwe mwaka 1968.
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi (kushoto) akipokea saa toka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili ya Wahandisi (ERB), Profesa Ninatubu Lema (kulia) kwa niaba ya Rais John Magufuli wakati wa hafla ya kusheherekea miaka 50 ya Bodi hiyo tangu ianzishwe mwaka 1968.
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi (kulia) akimkabidhi tuzo ya heshima moja ya mjumbe wa kwanza wa Bodi ya Usajili Wahandisi, Mhandisi Anase Shayo wakati wa hafla ya kusheherekea miaka 50 ya Bodi hiyo tangu ianzishwe mwaka 1968.
Baadhi ya Wahandisi wakimsikiliza Mgeni Rasmi Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi (hayupo pichani) wakati wa hafla ya kusheherekea miaka 50 ya Bodi ya Usajili ya Wahandisi (ERB) tangu ianzishwe mwaka 1968.
Picha na MAELEZO

KURASA ZA MBELE ZA MAGAZETI YA LEO

Wafanyabiashara wahimiza kuwekeza India

$
0
0
Mwenyekiti mstaafu wa TPSF ambaye pia ni Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP Ltd, Dk Reginald Mengi akibadilishana mawazo na Balozi wa India nchini Mh. Sandeep Arya mara baada ya kuwasili kwenye mkutano mkubwa wa wafanyabiashara kutoka Jimbo la Gujarat nchini India waliopo nchini kwa ajili ya kuangalia maeneo ya uwekezaji ikiwa ni sehemu ya jukwaa la biashara ndani ya Mkutano Mkubwa wa Biashara wa Gujarat uliofanyika katika hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti mstaafu wa TPSF ambaye pia ni Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP Ltd, Dk Reginald Mengi akisalimiana na Kaimu Mwenyekiti wa Chemba ya Wafanyabiashara wenye Viwanda na Kilimo – TCCIA Bw.Octavian Mshiu (aliyeipa kisogo kamera) wakati wa mkutano mkubwa wa wafanyabiashara kutoka Jimbo la Gujarat nchini India waliopo nchini kwa ajili ya kuangalia maeneo ya uwekezaji ikiwa ni sehemu ya jukwaa la biashara ndani ya Mkutano Mkubwa wa Biashara wa Gujarat uliofanyika katika hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya ONGC Petro additions Limited ya nchini India, Avinash Joshi.
Katibu Mkuu (idara ya usambazaji maji) na Mwenyekiti wa GWSSB wa Serikali ya Gujarat nchini India, J.P. Gupta akieleza fursa zilizopo katika maeneo mbalimbali jimbo la Gujarat nchini India wakati wa mkutano mkubwa wa wafanyabiashara kutoka Jimbo la Gujarat nchini India waliopo nchini kwa ajili ya kuangalia maeneo ya uwekezaji ikiwa ni sehemu ya jukwaa la biashara ndani ya Mkutano Mkubwa wa Biashara wa Gujarat uliofanyika katika hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti mstaafu wa TPSF ambaye pia ni Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP Ltd, Dk Reginald Mengi akizungumza na wafanyabiashara wa jimbo la Gujarat na Tanzania wakati wa mkutano mkubwa wa wafanyabiashara kutoka Jimbo la Gujarat nchini India waliopo nchini kwa ajili ya kuangalia maeneo ya uwekezaji ikiwa ni sehemu ya jukwaa la biashara ndani ya Mkutano Mkubwa wa Biashara wa Gujarat uliofanyika katika hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Shirikisho la wenye viwanda nchini CTI Bw. Shubhash Patel akizungumza na wageni waalikwa wakati wa mkutano mkubwa wa wafanyabiashara kutoka Jimbo la Gujarat nchini India waliopo nchini kwa ajili ya kuangalia maeneo ya uwekezaji ikiwa ni sehemu ya jukwaa la biashara ndani ya Mkutano Mkubwa wa Biashara wa Gujarat uliofanyika katika hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.
Kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya ONGC Petro additions Limited ya nchini India, Avinash Joshi, Mwenyekiti mstaafu wa TPSF ambaye pia ni Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP Ltd, Dk Reginald Mengi, Balozi wa India nchini Mh. Sandeep Arya pamoja na Katibu Mkuu (idara ya usambazaji maji) na Mwenyekiti wa GWSSB wa Serikali ya Gujarat nchini India, J.P. Gupta wakifurahi jambo wakati wa risala ya Mwenyekiti wa Shirikisho la wenye viwanda nchini CTI Bw. Shubhash Patel (hayupo pichani) katika mkutano mkubwa wa wafanyabiashara kutoka Jimbo la Gujarat nchini India waliopo nchini kwa ajili ya kuangalia maeneo ya uwekezaji ikiwa ni sehemu ya jukwaa la biashara ndani ya Mkutano Mkubwa wa Biashara wa Gujarat uliofanyika katika hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mwenyekiti wa Chemba ya Wafanyabiashara wenye Viwanda na Kilimo (TCCIA) Bw.Octavian Mshiu akihitimisha wakati wa semina maalum kwa wafanyabiashara wa Tanzania walipokutana na wafanyabiashara kutoka Jimbo la Gujarat nchini India waliopo nchini kwa ajili ya kuangalia maeneo ya uwekezaji ikiwa ni sehemu ya jukwaa la biashara ndani ya Mkutano Mkubwa wa Biashara wa Gujarat iliofanyika katika hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.




Pichani juu na chini ni sehemu ya Wafanyabishara kutoka Tanzania walioshiriki mkutano mkubwa wa wafanyabiashara kutoka Jimbo la Gujarat nchini India waliopo nchini kwa ajili ya kuangalia maeneo ya uwekezaji ikiwa ni sehemu ya jukwaa la biashara ndani ya Mkutano Mkubwa wa Biashara wa Gujarat uliofanyika katika hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti mstaafu wa TPSF ambaye pia ni Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP Ltd, Dk Reginald Mengi akisalamiana Mtalaam Mshauri wa Mambo ya Biashara, Bw. Victor Tesha (kulia) wakati wa mkutano mkubwa wa wafanyabiashara kutoka Jimbo la Gujarat nchini India waliopo nchini kwa ajili ya kuangalia maeneo ya uwekezaji ikiwa ni sehemu ya jukwaa la biashara ndani ya Mkutano Mkubwa wa Biashara wa Gujarat uliofanyika katika hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mwenyekiti wa Jukwaa la Wafanyabiashara wa India nchini, Bw. Gagan Gupta.
Mwenyekiti mstaafu wa TPSF ambaye pia ni Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP Ltd, Dk Reginald Mengi akibadilishana ‘contact’ na wafanyabiashara wa jimbo la Gujarat mara baada ya kumalizika kwa mkutano mkubwa wa wafanyabiashara kutoka Jimbo la Gujarat nchini India waliopo nchini kwa ajili ya kuangalia maeneo ya uwekezaji ikiwa ni sehemu ya jukwaa la biashara ndani ya Mkutano Mkubwa wa Biashara wa Gujarat uliofanyika katika hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mwenyekiti wa Jukwaa la Wafanyabiashara wa India nchini, Bw. Gagan Gupta.
Mwenyekiti mstaafu wa TPSF ambaye pia ni Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP Ltd, Dk Reginald Mengi akipiga picha za ukumbusho na baadhi ya wafanyabiashara wa Tanzania katika sekta mbalimbali waliohudhuria mkutano mkubwa wa wafanyabiashara kutoka Jimbo la Gujarat nchini India waliopo nchini kwa ajili ya kuangalia maeneo ya uwekezaji ikiwa ni sehemu ya jukwaa la biashara ndani ya Mkutano Mkubwa wa Biashara wa Gujarat uliofanyika katika hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.
Sektretarieti iliyoandaa mkutano huo kutoka jimbo la Gujarat katika picha ya pamoja na meza kuu mara baada ya kumalizika kwa mkutano mkubwa wa wafanyabiashara kutoka Jimbo la Gujarat nchini India waliopo nchini kwa ajili ya kuangalia maeneo ya uwekezaji ikiwa ni sehemu ya jukwaa la biashara ndani ya Mkutano Mkubwa wa Biashara wa Gujarat 2019 uliofanyika katika hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.

Meza kuu katika picha Kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya ONGC Petro additions Limited ya nchini India, Avinash Joshi, Mwenyekiti mstaafu wa TPSF ambaye pia ni Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP Ltd, Dk Reginald Mengi, Balozi wa India nchini Mh. Sandeep Arya pamoja na Katibu Mkuu (idara ya usambazaji maji) na Mwenyekiti wa GWSSB wa Serikali ya Gujarat nchini India, J.P. Gupta, Mwenyekiti wa Shirikisho la wenye viwanda nchini CTI Bw. Shubhash Patel, Kaimu Mwenyekiti wa Chemba ya Wafanyabiashara wenye Viwanda na Kilimo (TCCIA) Bw.Octavian Mshiu pamoja na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wafanyabiashara wa India nchini, Bw. Gagan Gupta.


Wafanyabiashara wa Tanzania wamehamasishwa kushiriki maonyesho ya Kimataifa ya Biashara katika Jimbo la Gujarat nchini India ili kupata fursa ya kufanya biashara na uwekezaji.
Hayo yamezungumzwa katika mkutano mkubwa wa wafanyabiashara kutoka jimbo hilo waliopo nchini kwa ajili ya kuangalia maeneo ya uwekezaji ikiwa ni sehemu ya jukwaa la biashara ndani ya Mkutano Mkubwa wa Biashara wa Gujarat 2019.
Jimbo la Gujarat lina pato la ndani la dola za Marekani bilioni 15 na linachangia asilimia 17 ya pato la viwanda nchini India na ni jimbo lenye viwanda vikubwa duniani.
Jimbo hilo pia linatoa mchango wa mauzo ya nje kwa asilimia 22 na asilimia 40 ya mizigo inayosafirishwa nchini india.
Akielezea Fursa za Uwekezaji zilizopo Gujarat katika semina maalum kwa wafanyabiashara wa Tanzania jijini Dar es salaam, Balozi wa India nchini Bw. Sandeep Arya amesema Watanzania wana fursa kubwa ya kushiriki uchumi wa Gujarat kwa kuona maeneo ya kushrikiana kiuchumi katika pande hizo mbili.
Akizungumza katika  mkutano huo Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Dk Reginald Mengi, ambaye ni   Mwenyekiti mstaafu wa TPSF, aliwataka wawekezaji wa India kuja nchini kuwekeza kwa ubia na Watanzania, hususan katika maeneo ya utafiti,  ubunifu na  uongezaji thamani kwa mazao ya kilimo.
Aidha Mwenyekiti wa Shirikisho la wenye viwanda nchini CTI Bw. Shubhash Patel, Kaimu Mwenyekiti wa Chemba ya Wafanyabiashara wenye Viwanda na Kilimo – TCCIA Bw.Octovian Mshiu walisema mkutano huo ni muhimu katika kuendeleza ushirikiano wa kibiashara baina ya Tanzania na India wenye historia ndefu.
Naye Katibu Mtendaji wa Chama cha watengeneza vitambaa vya nguo na  mavazi (TEGAMAT), Adam Zuku amesema kuwa semina hiyo  ina maana kubwa kwa watanzania  hasa viwanda vya nguo.
Alisema Tanzania inahitaji kufufua viwanda vyake vya nguo ili viweze kutoa ajira na pia kuwa na matumizi ya pamba yetu.
Alisema kuna changamoto kubwa katika viwanda vya nguo nchini, tatizo la soko linalotokana na nguo zinazotoka nje zinazosababisha tatizo kwenye ushindani sokoni.
Alisema nguo zinazozalishwa nchini zinakuwa ghali kulingana na zinazotoka nje na hivyo kuyumbuisha viwanda vya nguo nchini.
Alisema teknolojia si tatizo, tatizo ni wananchi kuwa wazalendo na kununua bidhaa zao ili kuwezesha viwanda kuendelea kuwapo.
Katika mkutano huo alisema wakati umefika kwa Wafanyabiashara na wadau mbalimbali nchini kushiriki katika fursa za uwekezaji kwenye nguo.

VETA KUJENGA CHUO CHA UFUNDI STADI MKOANI RUKWA

$
0
0

Picha mbalimbali katika hafla ya makabidhiano ya Ujenzi wa Chuo cha VETA Rukwa.
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Dkt Halfan Haule akizungumza katika Hafla ya kukabidhiana eneo la ujenzi wa Chuo cha VETA mkoani Rukwa.
Mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu naMafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) Adelina Macha akitoa taarifa za kuhusiana na mipango ya ujenzi ya Chuo cha VETA mkoani Rukwa.
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Dkt Halfan Haule akiwa katika picha ya pamoja na watendaji wa VETA Kanda VETA Makao Makuu na Viongozi mbalimbali wa Mkoa.
Kaimu Mkurugenzi wa Soko la Ajira VETA, Hildergardis Bitegera akikabidhi mchoro wa ramani ya Jengo la Chuo VETA Rukwa kwa Mkandarasi atakayejenga Chuo hicho.

Na David Edward, VETA.
KAIMU Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Dkt Halfan Haule amesema kuwa Mkoa wa Rukwa ulikuwa na uhitaji wa Chuo cha mafunzo ya Ufundi Stadi ili kuwazesha wanannchi wa mkoa huo kupata ujuzi wa ufundi kwa maendeleo ya mkoa na Taifa kwa ujumla.

Dkt Halfan Haule aliyasema wakati wa makabidhiano ya eneo la ujenzi wa Chuo cha VETA mkoani Rukwa katika hafla ya makabidhiano uliofanyika wilayani Sumbawanga mkoani Rukwa, amesema vijana wa Mkoa wa Rukwa ni fursa kupata mafunzo ya ujuzi na kuweza kujiajiri au kujiariwa.

Amesema wanaishukuru serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dk.John Pombe Magufuli kutatua tatizo upatikaji wa chuo cha mafunzo ya Ufundi Stadi mkoani humo.

Amesema vijana watapata ujuzi wa kusindika mazao mbalimbali na maendeleo yatapatikana kupitia usindikaji ambao utaogeza thamani ya mazao.

Nae Mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu naMafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) Adelina Macha amesema VETA imedhamiria kujenga vyuo vya ufundi stadi kila mkoa ili kwendana na malengo ya serikali ya Tanzania ya viwanda ambavyo vitahitaji watalaam wenye ujunzi wakitokea VETA.

Amesema kuwa ujenzi wa chuo hicho kinatakiwa kukamilika ndani ya mwaka mmoja na kuanza udahili wa wanafunzi katika kukimbizana na ujenzi wa viwanda mkoani Rukwa ambapo ujenzi huo utagharimu zaidi ya sh.bilioni10.

Macha amesema mpango wa serikali unaolenga kuwezesha upatinakaji wa ujuzi wa ufundi stadi kwa vijana nchini ili kuwawezesha kujiajiri au kuajiriwa katika kutekeleza mpango huo nchi nzima.

Macha amesema VETA inatarajia kujenga vyuo vinne vyenye hadhi ya mkoa vitakavyojengwa katika mikoa ya Njombe,Geita,Simiyu pamoja na Rukwa.

Amesema ujenzi wa vyuo hivyo ni ishara ya kuweza kufikia malengo ya uchumi wa viwanda nchini kutokana na mkoa wa Rukwa kufanya vizuri katika Kilimo,Ufugaji pamoja na Uvuvi.

Aidha amesema kuwa ili kufikia uchumi wa kati mwaka 2025 VETA kuwawezesha wananchi kupata nguvu kazi yenye ujunzi wa kuweza kutumika katika sekta mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuhimiri ushindani wa soko la ajira.

Aliongeza kuwa matarajio ya serikali kuwa uwepo chuo hicho kutahamasisha maendeleo kuongeza kipato kwa wanacnhi katika mkoa wa Rukwa ambapo watafanya usindikaji wa chakula pamoja na uhifadhi wa mazao.

Amesema utafiti ulibaini kuwa shughuli kubwa za kiuchumi kwa wananchi wa mkoa wa Rukwa ni kilimo, ufugaji na uvuvi. hivyo, ujenzi wa chuo cha ufundi stadi unalenga kuwezesha na kupanua uwigo wa ajira wa kuweza kujiajiri au kuajiriwa.

Nae Kaimu Mkurugenzi wa Soko la Ajira VETA, Hildergardis Bitegera amesema Chuo cha Mkoa wa Rukwa kitakapokamilika kitakuwa na uwezo wa kudahili wanafunzi 600 kwa ngazi ya kwanza hadi ya tatu katika mafunzo ya muda mrefu kwa mwaka na wanafunzi wasiopungua 900 kwa mafunzo ya muda mfupi.

Amesema kuwa katika ujenzi huo utahusisha ujenzi wa karakana zitakazofundishia mafunzo kwa vitendo katika kozi za ufundi magari,uchomeleaji na uungaji vyuma, uhudumiaji na uuzaji wa vinywaji. ufundi umeme,uandaaji na utayarishaji wa chakula, mafunzo ya ukatibu muhtasi,ubunifu wa mavazi na ushonaji wa nguo ,ufundi useremala , ufundi uashi ukarimu na utengenezaji wa chakula.

TFS IMESABABISHA MACHO YA WASHIRIKI SHINDANO LA MISS TANZANIA 2018 KUYAONA AMBAYO HAWAJAWAHI KUYAONA

$
0
0
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
MOJA ya kauli ambayo nimeisikia zaidi ya mara moja ikitamkwa na washiriki wa Shindano la Miss Tanzania mwaka 2018 ni ile inayoonesha kutoa shukrani zao za dhati kwa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS).

Warembo hao waliombwa na Molla wao wakaumbika hawakuwa na shaka hata kidogo kupaza sauti zao kwa madaha na madoido wakisema Tanzania yetu, Misitu yetu, Fahari yetu, Utembo oyeee na kisha wanamalizia kwa kusema TFS oyeee... Unajua kwanini?Iko hivi TFS ambayo ipo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii iliamua kuwapeleka warembo hao kwenye Hifadhi ya Mazingira ya Msitu Asili wa Amani iliyopo mkoani Tanga.

Hifadhi hiyo ipo katika Wilaya ya Muheza .Ipo umbali wa kilometa 35 kutoka Muheza Mjini.Hivyo ni hifadhi ambayo haiko mbali saaana lakini kwa vivutio vilivyopo kwenye hifadhi hiyo hata ingekuwa mbali kiasi gani ningekushauri ufike ujioonee mwenyewe. Nzuri na hivi TFS wanavyojua kutunza hifadhi zetu hadi raha.Nenda Mtanzania mwenzangu ukaone vilivyomo.

Kwa kukumbusha tu ukubwa wa hifadhi hiyo ni hekta 8380 .Ni eneo kubwa na ukweli ni kwamba TFS wameonesha kufanya kazi nzuri ya kuhakikisha hifadhi hiyo inatunzwa kama ambavyo wamekuwa wakifanya kwenye hifadhi nyingi za misiti ambayo wamepewa jukumu la kuhakikisha iko salama.

Safari ya warembo hao kwenda katika hifadhi hiyo ilianza katika Hoteli ya Serene jijini Dar es Salaam.Kama kumbukumbu zangu ziko sawa safari ilianzaa saa 10 alfajiri.Kwa picha ya haraka haraka ni kwamba warembo hao walianza maandalizi ya safari hiyo usiku wa manane.Haikuwa tatizo kwao kuhusu muda wa kuondoka.

Wakiwa kwenye basi kubwa lenye hadhi ya kubeba warembo ambapo miongoni mwao ndimo atapatikana Miss Tanzania mwaka 2018 ifikapo Septemba 8 mwaka huu safari ilianza kwa mwendo ambao hata askari wa Usalama Barabarani akiuona anasema kweli dereva anafuata sheria za ulama barabarani.Hakuna sababu ya trafiki kumulika tochi.

Naomba nieleze kidogo kabla ya kuendelea zaidi. Sababu ya kuandaliwa kwa safari hiyo ni kwamba mkakati wa TFS ni kuhakikisha warembo mbali ya kwenda katika hifadhi hiyo pia wanapata nafasi ya kushuhudia vivutio vya utalii ambavyo watakutana navyo wakati wanaelekea huko.

Naishukuru TFS kwa kutambua nafasi ya warembo hao katika kuutangaza hifadhi zilizopo nchini pamoja na utalii uliopo kwwnye hifadhi hizo na ule ambao upo nje ya hifadhi.Pia naishukuru TFS kwasababu iliona haja ya kuwa na waandishi ambao nao watashuhudia hifadhi hiyo na utalii uliopo na kisha kwa kutumia kalamu zao ili kuandika maandishi ambayo yatafikisha ujumbe mmoja tu wenye lengo la kuhamasisha watalii wa ndani na nje ya nchi yetu kutembelea vivutio vilivyopo.

Ahsante Mtendaji Mkuu wa TFS Profesa Dos Santos Silayo. Baada ya kutoa shukrani zangu kwa Profesa Silayo basi acha niendelee kuelezea.Safari ikawa inaendelea na basi lilipofika Mto Wami tukasimama kidogo na warembo kushuka na kisha kwenda katika eneo la mto huo.

Wakapiga picha kama kawaida na kisha safari ikaendelea mdogo mdogo. Kwa kuwa dhamira ni kuangalia utalii kabla kuingia Hifadhi ya Msitu wa Amani warembo hao wakapata nafasi ya kwenda hoteli ya Tanga Beach.Wakapumzika kwa muda na kisha kuelekea mapango ya Amboni.

Naomba niseme jambo unapozungumzia mapango ya Amboni maana yake unazungumzia mapango ambayo yamejaa historia ya aina yake.Usijidanganye kwa kusema Tanga hakuna utalii, utachekwa.

Kuna maeneo mengi ya utalii.Ukitaka kujua waulize warembo hao.Wameona kila aina ya vivutio. Hivyo warembo hao wakiwa katika mapango ya Amboni wakapata nafasi ya kuelezwa mambo mengi.Hakika utabaini eneo hilo limejaa historia kubwa na yenye mvuto ambayo kimsingi inakwenda sambamba na michoro inayoonekana kwa macho.

Mchoro wa Simba ambao upo kwenye mlango wa mapango hayo uliwafanya warembo hao kuonesha mshango.Ujue ukingalia mchoro ule ambao upo kwenye mapango hayo unaona kabisa kichwa cha Simba kinatazama ndani.

Inaelezwa hivi miaka ya zamani.Tena zamani sana eneo hilo lilikuwa ni la bahari na baadae maji yaliposogea kwenye kina kirefu cha bahari ikaacha mapango hayo ambayo ndio imejaa michoro.

Yaani unaambiwa kuna mapango moja linaitwa Osare Otanga na lingine linaitwa Paul Hamisi na pango dogo kabisa lililopo hapo linajulikana kana pango la jinsia.Ndani ya mapango hayo kwa mujibu wa watoa maelezo wanasema ukiingia ndani kuna njia.

Ukipita njia ya kulia unaenda Mombasa nchini Kenya na ukipita kushoto unaenda kutokea Stendi ya Mabasi ya Kange huko huko mkoani Tanga. Pia kuna michoro ambayo ukiangali inaonesha jengo la Msikiti na Kanisa.Ndani ya mapango hayo kuna michoro ya inayoonesha Biblia na Koraani.

Wakati maelezo hayo yanatolewa warembo hao walikuwa makini kuhakikisha wanailewa vema. Kilichoawaacha midomo wazi warembo hao ni maelezo kwamba ndani ya mapango kuna eneo la mzimu ambapo watu mbalimbali wanakwenda kufanya maombi na hasa wanaoamini katika kuomba mzimu.

Kwa kuwa lengo la ziara hiyo ni kujifunza zaidi, hivyo walipata nafasi ya kuuliza maswali kwa waliokuwa wanatoa maelezo kuhusu mapango hayo..Wakajibiwa vizuri.Baada ya kujionea utalii wa ndani katika mapango ya Amboni hatua iliyoafuata kwa warembo hao wakaanza kupiga picha za kumbukumbu kuwa nao wamewahi kufika hapo.

Hata hivyo kwa kuwa ratiba ilikuwa ni kwenda Hifadhi ya Amani warembo hao wakaanza safari ya kwenda kwenye hifadhi hiyo.Waliingia hifadhini saa tatu usiku.Walipofika moja kwa moja wakaenda kuangalia vinyonga wenye pembe tatu.

Tena unaambiwa kuna aina saba ya vinyonga ndani ya hifadhi hiyo.Usiku wanaonekana vizuri kuliko mchana.Mbona maajabu mwenzangu! Nashukuru binafsi nimewaona vinyinga na ikitokea nafasi nitakwenda kwa mara nyingine.Wala haichoshi kuwaangalia.TFS basi twendeni tena.

Unajua bwana vinyonga hao tunaelezwa kuwa wanapatikana tu kwenye hifadhi hiyo na si mahali kwingine kokote duniani.Watalii kutoka mataifa mbalimbali duniani wanafunga safari kwenda kuangalia vinyonga.

Utalii ambao warembo hao wameushuhudia ujumbe wao kwa Watanzania ni kwamba wawe na utamaduni wa kutembelea hifadhi ya Amani yenye utalii wa kila aina.Mbali ya kushuhudia vinyonga hao siku iliyofuata ilipofika saa 12 asubuhi walipata nafasi ya kwenda eneo ambalo ni maalum kwa kuangalia jua linavyochomoza.

Ukiwa katika eneo hilo utapata nafasi ya kuona vizuri namna jua linavyochomoza(Sun Rise).Kwa kuwa TFS ilihakikisha imejipanga vema kwa kuwapa nafasi ya warembo hao kushuhudia utalii uliopo ndani ya hifadhi hiyo waliamua kuwapeleka eneo ambalo lipo juu ya hifadhi na ni maalumu kwa ajili ya kilimo cha Chai. Safari ya kufika kwenye shamba hilo nayo ilikuwa ni utalii tosha kabisa.Warembo walipanda kwenye magari ya wazi.Pia kama unavyojua unapanda mlima katika barabara ambayo haina lami zaidi ya udongo wenye tope. Nitoe rai kwa Mtanzania mwenzangu tena muda kisha tembelea katika hifadhi hiyo.

TFS wanajitahidi kutunza misitu ya asili na kubwa zaidi wanatambua umuhimu wa misitu katika maisha binadamu.Ukiwamo wewe na mimi.Hivyo wanaitunza kwa kiwango cha hali ya juu. Ukiwa Amani utapelekwa na eneo ambalo kuna ndege ambao wanapatikana tu ndani ya hifadhi hiyo.

Akizungumza na warembo Mhifadhi wa Msitu wa Mazingira Asili wa Aman Mwanaid Kijazi amefafanua kwa kina kuhusu utalii unaopatikana ndani ya hifadhi hiyo ambayo inatunzwa na TFS.

Akatumia nafasi hiyo kuwaomba warembo hao kuwa mabalozi wa kuutungaza hifadhi hiyo na nyingine zilizopo nchini pamoja na utalii wa kila aina tulio nao nchini kwetu. Pamoja na mambo mengine warembo hao walipata nafasi ya kulala katika eneo hilo la hifadhi .

Nyumba zilizopo zilijengwa miaka ya zamani na Wajeruman.Hivyo nyumba zilizopo ndani ya hifadhi hiyo nazo zinahistoria yake. Kabla ya kujengwa eneo la hifadhi Wajeruman baada ya kuingia nchini waliamua kwenda Muheza na kutaka kujenga nyuma karibu na makazi ya watu.

Hata hivyo inaelezwa wenyeji walikubali kwa shingo upande.Hali hiyo Wajeruman waliona si sehemu salama na kisha kuamua kwenda kujenga ndani ya msitu huo.Hivyo waliona wako eneo lenye Amani na ndio kisa cha msitu huo kujulikana kwa jina hilo. Kwa upande wa TFS unawahimiza warembo hayo kuchukua jukumu la kuutangaza hifadhi zilizopo nchini pamoja vivutio vya utalii.Inatosha kwa leo.

KATIBU MKUU WA WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO AFUNGUA SEMINA YA UBIA KATI YA SEKTA BINAFSI NA UMMA

$
0
0






Na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.
KATIBU Mkuu wa wizara ya fedha na mipango, Dotto James amefungua semina ya ubia kati ya sekta ya umma na sekta binafsi (PPP) cha makatibu wakuu wa taasisi na wakuu wa idara wa wizara ya fedha na mipango inayofanyika ukumbi wa benki kuu ya Tanzania jijini Dar es Salaam leo.

Amesema kuwa semina hiyo itawajengea uwezo maafisa hao kutoka wizara na taasisi wanazooongoza ili waweze kutekeleza miradi ya PPP-(Public service Private partnership) yenye sifa.

James ametoa wito kwa washiriki wa semina wawe na utayari,uzalendo wad hat katika kuchangia, kuchambua kikamilifu miradi yenye sifa ili kuongeza ufanisi na wigo wa kutoa huduma za kiuchumi na kijamii.

“Matumaini yangu kuwa kila mmoja atashiriki kikamilifu katika semina hii muhimu na kupata uelewa wa mambo mhimu yatakayowezesha kuongeza jitihada za maandalizi ya mradi wa PPP.”Amesema James.

Nae Kaimu Mkurugezi wa mkondo wa chini wa shirika la mafuta na gesi (PTDC), Emmanuel Gilbert mradi wa PPP unatambulishwa kwa makatibu wakuu ili serikali na sekta binafsi waweze kushirikiana kikamilifu katika mradi huo.

Amesema kuwa katika uwekezaji katika usambazaji wa mafuta na gesi hapa nchini utasaidia kwa haraka wananchi kuweza kutumia gesi ya hapa nchini.

Amesema kuwa katika mradi huo wa kusambaza gesi utashirikisha waombaji watakao kidhi vigezo kwaajili ya usambazaji wa gesi hiyo ambapo kwa jiji la Dar es Salaam kutakuwa na vituo vitatu ambapo kitakuwa Ilala, Temeke na Kinondoni.
 Katibu Mkuu wizara ya Fedha na Mipango,Dotto James akizungumza  wakati wa kufungua semina ya ubia kati ya sekta ya umma na sekta binafsi (PPP) cha makatibu wakuu wa taasisi na wakuu wa idara wa wizara ya fedha na mipango inayofanyika ukumbi wa benki kuu ya Tanzania jijini Dar es Salaam leo Agosti 6, 2018.
 Mtaalamu wa masuala ya ubia kati ya sekta za umma na sekta binafsi, Philip Kelly  akifafanua jinsi Mradi wa sekta Binafsi na sekta za umma wakati wa semina ya ubia kati ya sekta ya umma na sekta binafsi (PPP) iliyofanyika ukumbi wa benki kuu ya Tanzania jijini Dar es Salaam leo Agosti 6, 2018.
Mtaalamu wa masuala ya ubia kati ya sekta za umma na sekta binafsi, Craig Sugden wakati wa semina ya ubia kati ya sekta ya umma na wakuu wa sekta binafsi (PPP) iliyofanyika ukumbi wa benki kuu ya Tanzania jijini Dar es Salaam leo Agosti 6, 2018.
Makatibu wakuu wa taasisi na wakuu wa idara wa wizara ya fedha na mipango wakiwa kwenye semina ya ubia kati ya sekta ya umma na sekta binafsi (PPP) iliyofanyika ukumbi wa benki kuu ya Tanzania jijini Dar es Salaam leo Agosti 6, 2018.

 Makatibu wakuu wa taasisi na wakuu wa idara wa wizara ya fedha na mipango wakiwa kwenye semina ya ubia kati ya sekta ya umma na sekta binafsi (PPP) iliyofanyika ukumbi wa benki kuu ya Tanzania jijini Dar es Salaam leo Agosti 6, 2018 wakimsikiliza Katibu Mkuuwa Wizara ya Fedha, Dotto James(Mbele).




 Makatibu wakuu wa taasisi na wakuu wa idara wa wizara ya fedha na mipango wakifatilia semina ya ubia kati ya sekta ya umma na sekta binafsi (PPP) iliyofanyika ukumbi wa benki kuu ya Tanzania jijini Dar es Salaam leo Agosti 6, 2018.
Kaimu Mkurugezi wa mkondo wa chini wa shirika la mafuta na gesi (PTDC), Emmanuel Gilbert akizungumza na waandishi wa hanbari jijini Dar es Salaam leo mara baada ya semina ya ubia kati ya sekta ya umma na sekta binafsi (PPP) iliyofanyika ukumbi wa benki kuu ya Tanzania jijini Dar es Salaam leo Agosti 6, 2018.
Picha ya Pamoja ya Makatibu wakuu wa taasisi na wakuu wa idara wa wizara ya fedha na mipango mara baada ya semina ya ubia kati ya sekta ya umma na sekta binafsi (PPP) iliyofanyika ukumbi wa benki kuu ya Tanzania jijini Dar es Salaam leo Agosti 6, 2018.

RC HAPI: MARUFUKU KUWANYANYASA MACHINGA KATIKA MAENEO WANAYOFANYIA YA KAZI ZAO

$
0
0
Mkuu wa mkoa wa Iringa Ally Hapi akiongea na wafanyabiashara wadogo wadogo maarufu kama machinga wa manispaa ya Iringa kwa lengo la kusikiliza kero na changamoto ambazo wanakabiliana katika kuleta maendeleo ya mkoa wa Iringa na kuhakikisha wanaijenga Iringa mpya ambayo inatakiwa na wanairinga 
Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akiongea wakati wa kikao cha wafanyabiashara wadogo wadogo maarufu kama machinga na mkuu wa mkoa wa Iringa
Baadhi ya wafanyabiashara wadogo wadogo maarufu kama machinga walijitokeza kumsikiliza mkuu wa mkoa wa Iringa Ally Hapi na kama ambavyo unawaona walivyokuwa makini kumsikiliza hapo

 NA FREDY MGUNDA,IRINGA
MKUU wa mkoa wa Iringa amepiga marufuku wafanyabiashara wadogo wadogo kunyanyaswa katika mahali ambazo wanafanyia biashara kwa kuwa wanatoa kodi ambayo inachochea kuleta maendeleo ya watanzania hususani mkoani iringa tukielekea kuijenga Iringa mpya.

Akizungumza kwenye mkutano na wafanyabiasha wadogodogo wa manispaa ya Iringa mkuu wa mkoa Ally Hapi alisema kuwa wafanyabiasha wadogo wadogo maarufu kama machinga wanatakiwa kufanya biashara zao kwa kufuta taratibu na sheria za nchi huku viongozi wakiancha kuwanyanyasa kwa kuwa nao ni wafanyabiashara.

“Toka nikiwa mkuu wa wilaya najua umuhimu wafanyabiasha wadogo wadogo kwa kuchangia katika kukuza uchumi wa eneo husika hivyo natangaza rasmi ni marufuku kuwanyanyasa wafanyabiasha wadogo wadogo wa mkoa wa Iringa” alisema Hapi

Hapi aliwataka polisi wanasimamia eneo lastand kuu kuacha mara moja kunyanyasa wafanyabiasha wadogo wadogo wanaofanyia biashara katika eneo hilo.

Kauli hiyo imekuja mara baada ya katibu na mwenyekiti wa chama cha wafanyabiasha wadogo wadogo (machinga) kutoa kilio hicho mbele ya mkuu ya mkoa kwa kusema wamekuwa wakinyanyaswa na askari ambao wanafanya kazi katika stand kuu.

Katibu wa wafanyabiasha wadogo wadogo manispaa ya Iringa Joseph Kilyenyi alisema kuwa baadhi ya viongozi wa halimashauri ya manispaa ya Iringa pamoja na baadhi ya polisi wamekuwa kikwazo cha kufanya biasha kwa uhuru na kuongeza pato la manispaa ya Iringa.

“wafanyabiasha wadogo wadogo tupo zaidi ya elfu moja tukiwekewa mfumo sahihi kwa wakati sahihi tunaweza kutoa kodi zaidi ya shilingi milioni tisa  ambapo hapo tunatoa shilingi mia tatu  na ikiwa shilingi mia tano halmashauri itaingiza mapato mengi ambayo yatachangia maendeeleo ya manispaa” alisema Kilyenyi

Kilyenyi alisema kuwa wafanyabiasha wadogo wadogo wa manispaa ya Iringa wapo tayari kulipa kodi kama ambavyo Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuleta maendeleo na kuwapa nafasi wafanyabiasha wadogo wadogo kufanya kazi kwa uhuru na kuchochoe maendeleo.

“Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania DR John Pombe Magufuli amekuwa akitupelea na kuthamini hivyo hata sisi tunawajibu wa kuhakikisha tunalipa ushuru na kodi pale inapotakiwa ili kukuza juhudi za kuleta maendeleo ya nchi yetu” alisema Kilyenyi

Kilyenyi alimpongeza mkuu wa wilaya ya Iringa Richard kasesela pamoja na MNEC wa mkoa wa Iringa Salim Asas kwa kuwasaidia kutatua migogoro mbalimbali ambayo imekuwa ikiwakabili wafanyabiasha wadogo wadogo

“Baada ya kupokea kero za wafanyabiasha wadogo wadogo mkuu wa mkoa wa Iringa Hapi alimtaka Mkurugenzi wa halmashauri ya Iringa ndani ya mwezi mmoja kuhakikisha wanatengeza mfumo rafiki ambao utakuwa utasidia kukusanya kodi kwa wafanyabiasha hao.

Nimetoa siku thelathini kwa viongozi wa halmashauri kuhakikisha wanatengeza mfumo rafiki ambao hausababisha wafanyabiasha wadogo wadogo kulipa kodi katika maeneo wanayofanyia kazi ili kuwaondolea usumbufu wa kuwafuta mliko” alisema Hapi

Aidha hapi alisema kuwa hatawavumia viongozi wowote wale ambao watakwamisha kuijenga Iringa mya ambayo inatakiwa kuwa kama kituvu cha utalii nyanda za juu kusini

Naye afisa biashara wa manispaa ya Iringa kassim majariwa alisema kuwa ameyapogea maagizo yote ambayo mkuu wa mkoa ameagiza kuhakikisha kunakuwa na ongezeko la ukusanyaji wa kodi katika halmashauri ya Iringa.

RAIS MAGUFULI AWEKA JIWE LA MSINGI MRADI WA UJENZI WA BARABARA YA MAKUTANO-NYAMUSWA-SANZATE –NATA-IKOMA GATE KM 135 SEHEMU YA MAKUTANO-SANZATE 50KM, BUTIAMA MKOANI MARA

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akivuta utepe pamoja na Mama Maria Nyerere mke wa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ili kuweka jiwe la msingi mradi wa ujenzi wa Barabara ya Makutano-Nyamuswa- Sanzate-Nata-Ikoma gate km 135 katika sehemu ya Makutano-Sanzate km 50 katika sherehe zilizofanyika Butiama mkoani Mara.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Mama Maria Nyerere mke wa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere mara bada ya kuweka jiwe la msingi mradi wa ujenzi wa Barabara ya Makutano-Nyamuswa- Sanzate-Nata-Ikoma gate km 135 katika sehemu ya Makutano-Sanzate km 50 katika sherehe zilizofanyika Butiama mkoani Mara.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiimba na kucheza pamoja na vijana wa Kambi ya  JKT Rwamkoma iliyopo mkoani Mara mara baada ya kuweka jiwe la msingi mradi wa ujenzi wa Barabara ya Makutano-Nyamuswa- Sanzate-Nata-Ikoma gate km 135 katika sehemu ya Makutano-Sanzate km 50 katika sherehe zilizofanyika Butiama mkoani Mara.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Butiama(hawaonekani pichani) kabla ya kuweka jiwe la msingi mradi wa ujenzi wa Barabara ya Makutano-Nyamuswa- Sanzate-Nata-Ikoma gate km 135 katika sehemu ya Makutano-Sanzate km 50 katika sherehe zilizofanyika Butiama mkoani Mara.
Mzee Joseph Butiku akiwa amekaa na Mwanasiasa mklongwe Stephen Wassira pamoja na viogozi wengine wakifatilia kwa makini hotuba ya Rais Dkt. Magufuli katika sherehe hizo za uwekaji wa jiwe la msingi Butiama mkoani Mara. 
 Kikundi cha ngoma za asili cha Engubha cha kabila la wakabwa wenyeji wa Butiama mkoani Mara kikitumbuzia katika sherehe hizo. PICHA NA IKULU

DKT. JANABI:VYAKULA VISIVYO NA AFYA HUSABABISHA MAGONJWA YA MOYO

$
0
0
Na Salome Majaliwa - JKCI
ULAJI wa vyakula visivyokuwa na afya ni moja ya sababu zinazosababisha watu kupata magonjwa  yasiyo ya kuambukiza ukiwemo ugonjwa wa moyo.
Hayo yamesemwa jana na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi wakati akitoa mada kuhusu afya na mazoezi   kwenye  mkutano wa wahandisi unaofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.

Katika mada hiyo ya afya na mazoezi Prof. Janabi alifundisha kuhusu ugonjwa wa shambulio la moyo na kiharusi, tezi dume, saratani, kukoma kwa hedhi na huduma zinazotolewa na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete.
Prof. Janabi ambaye pia ni Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo alisema hivi sasa  watu wanapenda kula vyakula ambavyo ni hatari kwa afya zao zikiwemo chips na bagger badala ya kula kwa wingi matunda na mboga za majani.

“Dhibitini vyakula mnavyokula hii ikiwa ni pamoja na kutokula vyakula vyenye mafuta mengi ambavyo vinapelekea mishipa ya moyo kuziba kutokana na mafuta na kusababisha tatizo la kiharusi pia  fanyeni mazoezi ya mara kwa mara”, alisisitiza Prof. Janabi.

Alisema ugonjwa wa moyo ni moja ya magonjwa yanayoua watu wengi wakiwemo watoto ambao wasipopata chanjo za muhimu zinazotolewa chini ya umri wa miaka mitano pia mama mjamzito asipopata chanjo   kuna uwezekano mkubwa kwa watoto kuzaliwa na kupata magonjwa ya moyo.

Kwa upande wa  ugonjwa wa shambilio la moyo  alizitaja dalili zake kuwa ni maumivu kwenye kifua ambayo yanakwenda kwenye mgongo upande wa kulia na kushoto na kuwasihi wanapoona dalili kama hiyo wawahi  mapema kwa daktari. 

Alizitaja aina  za ugonjwa wa  kiharusi kuwa ni mshipa unaopeleka damu kwenye ubongo kuziba  na kushindwa kusambaza damu (ischemic) na mshipa wa  damu kupasuka na kumwaga damu katika ubongo (hemorrhagic) ukipata aina hii ya kiharusi ni ngumu  kupona.

Kuhusu ugonjwa wa tezi dume Prof. Janabi alisema wanaume wenye umri wa kuanzia miaka 50 kwenda juu wako katika hatari ya kupata ugonjwa huo  na kuzitaja baadhi ya  dalili kuwa ni kwenda  haja ndogo mara kwa mara hasa nyakati za  usiku na ukipata haja ndogo haitoki yote. 

Akielezea kuhusu kitendo cha mwanamke kukoma hedhi alisema mwanamke aliyekuwa katika hali hiyo ni yule ambaye   hawezi kuzaa tena na wengi wao huwa ni wenye umri wa kuanzia miaka 50 na kuendelea.

Alizitaja dalili za kukoma kwa hedhi kuwa ni pamoja na kupoteza hamu ya kufanya tendo la ndoa, mama kuwa mkali na mwenye hasira, joto la mwili kuwa kali. Ili kukabiliana na kipindi hicho aliwashauri wanawake kufanya  mazoezi na kuvaa nguo nyepesi ili kulikabili joto na kuepuka kula vyakula vyenye viungo vikali kama pilipili.

Prof. Janabi alimalizia kwa kuzitaja baadhi ya sababu zinazosababisha ugonjwa wa saratani kuwa ni kutokwenda haja kubwa kwa wakati, kutokupata muda wa kutosha wa kulala, kutokula  chakula kwa wakati , msongo wa mawazo na kutokunywa  maji ya kutosha.  
 Daktari wa  Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Salehe Mrutu akimpa dawa ya moyo  mhandisi aliyetembelea banda la Taasisi hiyo  kwa ajili ya kupima afya  wakati wa mkutano wa 16 wa Wahandisi uliofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dar es Salaam. Wahandisi waliopima magonjwa ya moyo na kukutwa na matatizo walipewa dawa bila malipo.
 Wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)  wakitoa huduma ya upimaji wa magonjwa ya moyo  kwa wahandisi wakati wa Mkutano wa 16 wa Wahandisi unaofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dar es Salaam.

 Pix 3 & 4: Baadhi ya Wahandisi wakiwa katika foleni ya kufanya upimaji wa magonjwa ya moyo katika  banda la Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakati wa Mkutano wa 16 wa Wahandisi ulifanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dar es Salaam. Taasisi hiyo ilishiriki kutoa huduma ya upimaji wa magonjwa ya  moyo kwa wahandisi hao.
Afisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Adela Martine akitoa ushauri kwa mhandisi aliyepata huduma za upimaji wa magonjwa ya moyo katika banda la Taasisi hiyo wakati wa mkutano wa 16 wa Wahandisi unaofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akitoa elimu ya Afya na mazoezi kwa wahandisi wakati wa Mkutano wa 16 wa Wahandisi uliofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee jana Jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya wanafunzi kutoka shule mbalimbali za Sekondari za Jijini Dar es Salaam wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)  Prof. Mohamed Janabi (hayupo pichani) alipokuwa akitoa mada ya Afya na mazoezi kwa wahandisi wakati wa Mkutano wa 16 wa Wahandisi unaofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dar es Salaam.
 Beatrice Nchimbi ambaye ni Mwanafunzi wa shule ya Sekondari Kisutu akiuliza swali baada ya kupata elimu ya afya na mazoezi kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)  Prof. Mohamed Janabi (hayopo pichani) wakati wa Mkutano wa 16 wa Wahandisi unaofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dar es Salaam.

Wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakitoa elimu ya lishe bora pamoja na umuhimu wa kufanya mazoezi kwa wahandisi waliotembea banda la Taasisi hiyo wakati wa Mkutano wa 16 wa Wahandisi unaofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dar es Salaam.
Picha na JKCI
Viewing all 39168 articles
Browse latest View live